0:00:00.896,0:00:03.437 Mwaka 2014 ulikua ,mkubwa kwangu. 0:00:03.461,0:00:04.627 Ulishawahi kuwa na hio, 0:00:04.651,0:00:06.896 kama tu mwaka mkubwa, kama mwaka bango? 0:00:07.198,0:00:08.635 Kwangu, ulienda hivi: 0:00:08.659,0:00:11.958 Oktoba 3, nilipoteza ujauzito wangu wa[br]pili. 0:00:11.982,0:00:15.077 Halfu Oktoba 3, baba yangu alifariki kwa[br]saratani. 0:00:15.101,0:00:17.871 Halafu tena Novemba 25,[br]mme wangu Aaron alifariki 0:00:17.895,0:00:20.673 baada ya miaka mitatu[br]ya hatua ya nne ya glioblastoma, 0:00:20.697,0:00:23.132 ambalo ni neno la mbwembwe[br]la saratani ya ubongo. 0:00:24.822,0:00:25.972 Hivyo, nina vichekesho. 0:00:26.639,0:00:28.012 (Kicheko) 0:00:28.036,0:00:31.877 Watu wanapenda kunialika sehemu kila mara. 0:00:31.901,0:00:33.307 Maingiano kibao. 0:00:33.331,0:00:36.395 Kawaida, ninapoongelea[br]hiki kipindi cha maisha yangu, 0:00:36.419,0:00:39.633 majibu ninayopata kimsingi ni: 0:00:39.657,0:00:41.592 (Mhemo) 0:00:41.616,0:00:43.476 "Siwezi -- siwezi kufikiria." 0:00:45.061,0:00:46.595 Lakini ninafikiri unaweza. 0:00:47.696,0:00:48.847 Ninafikiri unaweza. 0:00:48.871,0:00:50.238 Na ninafikiri kua unatakiwa 0:00:50.262,0:00:52.879 kwa sababu, siku moja,[br]itakutokea wewe. 0:00:52.903,0:00:57.561 Labda sio hizi hasara kabisa[br]kwenye namna hii maalum au kwa kazi hii, 0:00:57.585,0:00:58.975 ila nimesema, nina vichekesho 0:00:58.999,0:01:02.696 na utafiti nilioona[br]utakushangaza: 0:01:02.720,0:01:06.330 kila mtu unaempenda ana[br]nafasi asilimia 100 ya kufa. 0:01:06.354,0:01:08.950 (Kicheko) 0:01:08.974,0:01:10.545 Na ndio maana ukaja TED. 0:01:10.569,0:01:12.631 (Kicheko) 0:01:12.655,0:01:15.967 (Makofi) 0:01:16.292,0:01:18.022 Tangu hasara yote ilivyonitokea, 0:01:18.046,0:01:22.339 nimefanya kazi kuongelea kuhusu kifo na[br]hasara, 0:01:22.363,0:01:24.783 sio yangu tu,[br]kwa sababu ni rahisi kukumbuka, 0:01:24.807,0:01:28.853 lakini hasara na mikasa[br]ambayo watu wengine wamepitia. 0:01:28.877,0:01:31.216 Ni sehemu, naweza kusema. 0:01:31.240,0:01:32.981 (Kicheko) 0:01:33.005,0:01:36.104 Ni sehemu ndogo, na natamani[br]ningekua na hela nyingi, lakini ... 0:01:36.128,0:01:37.458 (Kicheko) 0:01:37.482,0:01:40.593 Nimeandika vitabu vya kuinua kweli, 0:01:40.617,0:01:44.310 nikaendesha podikasti ya kuinua sana,[br]nikaanzaisha shirika lisilo la serikali. 0:01:44.334,0:01:45.934 Ninajaribu tu kufanya ninachoweza 0:01:45.958,0:01:49.482 kufanya watu wengi zaidi wafarijike[br]kwenye hali zilizo ngumu, 0:01:49.506,0:01:51.640 na majonzi ni magumu sana. 0:01:52.014,0:01:55.831 Ni magumu sana, haswa[br]kama ni majonzi ya mtu mwingine. 0:01:57.323,0:02:01.545 Basi sehemu ya hio kazi ni hili kundi[br]nililoanzisha na rafiki yangu Moe, 0:02:01.569,0:02:02.791 ambae pia ni mjane; 0:02:02.815,0:02:05.350 tunaliita Chama cha Wajane Wadogo Wakali. 0:02:05.374,0:02:06.748 (Kicheko) 0:02:06.772,0:02:09.247 Na ni ukweli, tuna kadi za uwanachama 0:02:09.271,0:02:10.644 na tisheti. 0:02:11.272,0:02:14.952 Na pale mtu wako akifariki,[br]mmeo, mke, mchumba, 0:02:14.976,0:02:16.967 hatujali kabisa kama ulikua kwenye ndoa, 0:02:16.991,0:02:19.742 marafiki zako na familia yako[br]watakua tu wanaangalia 0:02:19.766,0:02:22.122 kwa marafiki wa marafiki[br]wa marafiki wa marafiki 0:02:22.146,0:02:25.010 mpaka wapate mtu[br]ambae amepitia hali inayofanana, 0:02:25.034,0:02:27.395 halafu watawasukuma[br]mje pamoja 0:02:27.419,0:02:31.786 ili muongee miongoni mwenu na msiwe[br]na masikitiko kwa watu wengine. 0:02:31.810,0:02:33.969 (Kicheko) 0:02:33.993,0:02:35.394 Basi ndicho tunachofanya. 0:02:35.418,0:02:38.910 Ni mfululizo tu wa makundi madogo, 0:02:38.934,0:02:42.483 ambapo wanaume, wanawake, mashoga, wa[br]kawaida, wanandoa, wenye wenza, 0:02:42.507,0:02:46.776 wanaweza kuongelea kuhusu mtu wao[br]aliyekufa, 0:02:46.800,0:02:48.046 na kusema vile vitu 0:02:48.070,0:02:51.789 ambavyo mtu mwingine kwenye maisha yao[br]hayuko tayari kuvisikia bado. 0:02:51.813,0:02:54.291 Eneo kubwa la mazungumzo. 0:02:54.315,0:02:56.103 Kama, "Mme wangu alikufa wiki mbili[br]zilizopita, 0:02:56.127,0:02:58.445 siwezi kuacha kufikiria kuhusu[br]ngono, ni kawaida?" 0:02:58.469,0:02:59.623 Ndio. 0:02:59.647,0:03:01.696 "Je kama ni mmoja wa[br]Property Brothers?" 0:03:01.720,0:03:03.266 Kawaida kidogo, ila nitaikubali. 0:03:03.290,0:03:06.424 (Kicheko) 0:03:06.910,0:03:10.751 Vitu kama, "Ona, nikiwa hadharani na[br]nikaona wazee wanashikana mikono, 0:03:10.775,0:03:13.361 wenzi ambao ni wazi wamekua[br]pamoja kwa miongo, 0:03:13.385,0:03:15.712 halafu ninawaangalia na kuwaza 0:03:15.736,0:03:17.982 vitu vyote ambavyo wamepitia[br]pamoja, 0:03:18.006,0:03:19.545 vitu vizuri na vitu vibaya, 0:03:19.569,0:03:22.640 ugomvi waliokuanao[br]kuhusu nani wa kutoa taka ... 0:03:22.664,0:03:25.696 nakuta tu moyo umejawa na hasira." 0:03:25.720,0:03:26.721 (Kicheko) 0:03:26.745,0:03:28.552 Na huo mfano ni wa pekee kwangu. 0:03:30.077,0:03:33.228 Mazungumzo mengi ambayo[br]tunakuwa nayo kwenye kundi 0:03:33.252,0:03:35.229 yanaweza na yanakaa miongoni mwetu, 0:03:35.253,0:03:37.172 lakini kuna vitu tunavyoviongelea 0:03:37.196,0:03:40.379 ambavyo duniani --[br]dunia ambayo iko karibu na majonzi 0:03:40.403,0:03:41.917 ila bado haijapigwa na majonzi 0:03:41.941,0:03:43.847 inaweza kweli kunufaika kusikia. 0:03:43.871,0:03:45.149 Na kama huwezi kusema, 0:03:45.173,0:03:49.553 ninavutiwa/uwezo tu wa[br]masomo yabbsiyo ya kisayansi, 0:03:49.577,0:03:51.951 nilienda kwenye[br]Chama cha Wajane Wadogo Wakali 0:03:51.975,0:03:56.585 na kusema, "Habari, marafiki, unakumbuka[br]mtu wako alivyokufa?" Walikumbuka. 0:03:56.609,0:03:59.094 "Unakumbuka vitu vyote watu[br]walikuambia?" 0:03:59.118,0:04:00.289 "Ah, ndio." 0:04:00.313,0:04:02.076 "Ni vipi ulivyovichukia zaidi?" 0:04:02.100,0:04:05.307 Nilipata maoni mengi, majibu mengi,[br]watu wanasema vitu vingi, 0:04:05.331,0:04:07.931 lakini viwili vilisimama juu haraka sana. 0:04:08.990,0:04:10.140 "Kusonga mbele." 0:04:11.561,0:04:14.171 Sasa, tangu 2014, 0:04:14.195,0:04:18.243 nitakuambia nilifunga ndoa tena na[br]mwanaume mzuri kweli aitwae Matthew, 0:04:18.267,0:04:21.370 tuna watoto wanne[br]kwenye familia yetu iliyochanganyika, 0:04:21.394,0:04:24.887 tuniashi kwenye viunga[br]vya Minneapolis, Minnesota, Marekani. 0:04:24.911,0:04:26.331 Tuna mbwa aliyeokolewa. 0:04:26.355,0:04:27.662 (Kicheko) 0:04:27.686,0:04:29.098 ninaendesha gari la familia, 0:04:29.122,0:04:31.938 kama la aina ambayo milango inafunguka[br]bila hata kuigusa. 0:04:31.962,0:04:33.146 (Kicheko) 0:04:33.170,0:04:36.363 Kama, "mezhure" yoyte, maisha ni mazuri. 0:04:36.387,0:04:39.459 Sijawahi pia kusema "mezhure,"[br]sijawahi hata mara moja kuisema hivyo. 0:04:39.483,0:04:44.762 (Kicheko) 0:04:44.786,0:04:46.437 Sijui hata imetokea wapi. 0:04:46.461,0:04:48.222 (Kicheko) 0:04:48.246,0:04:50.521 Sijawahi kusikia mtu yeyote[br]akiisema hivyo. 0:04:50.545,0:04:52.522 Inaonekana kama inapaswa kusemwa hivyo, 0:04:52.546,0:04:55.103 na ndio sababu lugha ya Kiingereza[br]ni mbovu, basi ... 0:04:55.127,0:04:56.181 (Kicheko) 0:04:56.205,0:04:58.331 Ninavutiwa sana na mtu[br]ambae anaiongea 0:04:58.355,0:05:01.228 kuongezea kwenye lugha[br]inayoeleweka -- kazi nzuri. 0:05:01.252,0:05:03.244 (Kicheko) 0:05:03.268,0:05:04.704 Lakini, kwa vyovote vile ... 0:05:04.728,0:05:06.228 (Kicheko) 0:05:06.252,0:05:11.402 Kwa vyovyote vile, maisha ni mazuri[br]sana sana, lakini "sijasonga mbele." 0:05:12.085,0:05:15.109 Sijasonga mbele,[br]na siupendi kabisa huo msemo, 0:05:15.133,0:05:16.924 na ninaelewa kwanini wengine hawaupendi. 0:05:16.948,0:05:18.098 Kwa sababu unachosema 0:05:18.122,0:05:22.710 ni kua maisha na kifo cha Aaron[br]na upendo ni wakati tu 0:05:22.734,0:05:26.537 ambao nauweza kuuacha nyuma yangu --[br]na kua napaswa kufanya hivyo. 0:05:26.561,0:05:30.791 Na ninapoongelea kuhusu Aaron,[br]ninaingia kirahisi kwenye hali halisi, 0:05:30.815,0:05:33.371 na nimewaza kweli kua hio inanifanya[br]wa ajabu. 0:05:33.395,0:05:35.819 Halafu nikagundua kua kila mtu anafanya[br]hivyo. 0:05:36.595,0:05:40.762 Na sio kwa sababu tuna kana[br]au kwa sababu tunasahau, 0:05:40.786,0:05:43.047 ni kwa sababu watu[br]tunaowapenda, tuliowapoteza, 0:05:43.071,0:05:45.229 bado ni halisi kwetu sisi. 0:05:46.800,0:05:49.400 Basi, ninaposema, "Oh, Aaron ni ..." 0:05:50.276,0:05:52.521 Ni kwa sababu Aaron bado yupo. 0:05:53.831,0:05:55.871 Na sio kwa namna[br]alivyokua kabla. 0:05:55.895,0:05:57.078 iliyokua bora zaidi, 0:05:57.102,0:06:00.744 na sio namna ambayo watu wa kanisani[br]wanavyojaribu kuniambia anavyokua. 0:06:00.768,0:06:04.447 ni kua tu amezimika, 0:06:05.411,0:06:08.047 na hivyo yupo sasa kwangu. 0:06:08.610,0:06:09.760 Hapa, 0:06:09.784,0:06:12.043 yupo hapa kwenye kazi ninayofanya, 0:06:12.067,0:06:14.675 kwenye mtoto tulionae pamoja, 0:06:14.699,0:06:16.754 kwenye hawa watoto wengine watatu[br]ninaolea, 0:06:16.778,0:06:19.564 ambao hawajawahi kunuona,[br]ambao hawana DNA yake, 0:06:19.588,0:06:23.453 lakini wapo kwenye maisha yangu tu[br]kwa sababu nilikuwa na Aaron 0:06:23.477,0:06:25.143 na kwa sababu nilimpoteza Aaron. 0:06:26.302,0:06:28.653 Yupo nami kwenye ndoa yangu na Matthew, 0:06:28.677,0:06:31.882 kwa sababu maisha na upendo na kifo cha[br]Aaron 0:06:31.906,0:06:34.572 vimenifanya kua mtu ambae[br]Matthew angetaka kuoa. 0:06:34.596,0:06:38.829 Hivyo sijasonga mbele kutoka kwa Aaron, 0:06:38.853,0:06:41.694 nimesonga mbele na yeye. 0:06:44.925,0:06:50.574 (Makofi) 0:06:50.995,0:06:55.662 Tulisambaza majivu ya Aaron[br]kwenye mto aupendao huko Minnesota, 0:06:55.686,0:06:57.193 na pale begi lilipokua tupu -- 0:06:57.217,0:07:01.938 kwa sababu ukiwa umechomwa,[br]unatoshea kwenye mfuko wa plastiki -- 0:07:01.962,0:07:04.882 kulikua na majibu bado[br]yamebaki kwenye vidole vyangu. 0:07:04.906,0:07:07.993 Na ningeingiza tu mikono yangu kwenye[br]maji na kuisuuza, 0:07:08.017,0:07:10.823 lakini badala lake, nililamba mikono[br]yangu, 0:07:11.617,0:07:15.339 kwa sababu niliogopa kupoteza zaidi[br]ya nilichopoteza zaidi, 0:07:15.363,0:07:19.426 na nilitamani sana kuhakikisha kua[br]atakua ni sehemu yangu daima. 0:07:20.371,0:07:22.104 Lakini bila shaka atakua. 0:07:22.878,0:07:27.339 Kwa sababu unapomuona mtu wako[br]akijijaza na sumu kwa miaka mitatu, 0:07:27.363,0:07:30.023 ili tu aweze kuishi[br]zaidi kidogo na wewe, 0:07:30.047,0:07:31.791 hilo linakaa na wewe. 0:07:33.196,0:07:37.846 Unapomuangalia akififia kutoka kwenye[br]mtu mwenye afya siku mliokutana 0:07:37.870,0:07:39.453 kuwa sifuri, hiyo inakaa na wewe. 0:07:39.477,0:07:42.314 Unapomuangalia mwanao,[br]amba hata bado hana miaka miwili, 0:07:42.338,0:07:45.029 akienda kitandani kwa baba yake[br]siku ya mwisho ya maisha yake, 0:07:45.053,0:07:47.323 kama vile anajua kinachofuata[br]masaa machache, 0:07:47.347,0:07:52.363 na kusema, "Nakupenda. Nimemaliza.[br]Kwaheri." 0:07:53.776,0:07:55.751 Hiyo inakaa na wewe. 0:07:57.347,0:08:02.037 Kama tu unapopenda,[br]hatimae, unapopenda kweli 0:08:02.061,0:08:04.403 mtu anaekuelewa na kukuona 0:08:04.427,0:08:07.524 na unaona pia, "Mungu wangu,[br]nimekua nikikosea mda wote huu. 0:08:07.548,0:08:12.332 Upendo sio mashindano au[br]kipindi cha televisheni -- ni ukimya sana, 0:08:12.356,0:08:16.045 ni huu uzi usioonekana wa utulivu[br]unatuunganisha wawili 0:08:16.069,0:08:17.837 hata kama kila kitu kina vurugu, 0:08:17.861,0:08:20.787 vitu vinapoenda vibaya,[br]hata kama akiondoka." 0:08:22.474,0:08:24.743 Hio inakaa na wewe. 0:08:26.958,0:08:28.329 Tulikua tunafanya hivi -- 0:08:28.353,0:08:30.988 mikono yangu ilikua na[br]baridi na yeye ana joto, 0:08:31.012,0:08:34.424 nilichukua mikono yangu ya barafu[br]na kuisukuma ndani ya shati lake ... 0:08:34.886,0:08:36.895 kuikandamiza kwenye mwili wake mkali. 0:08:36.919,0:08:38.982 (Kicheko) 0:08:39.405,0:08:41.920 Na alikua hapendi kabisa, 0:08:41.944,0:08:42.965 (Kicheko) 0:08:42.989,0:08:44.347 lakini alinipenda, 0:08:44.371,0:08:49.228 na alivyokufa,[br]nililala kitandani na Aaron 0:08:49.252,0:08:51.656 na nikaweka mikono yangu chini yake 0:08:53.355,0:08:55.845 na nikahisi joto lake. 0:08:58.374,0:09:01.881 Na sikuweza hata kusema kama[br]mikono yangu ilikua na baridi, 0:09:01.905,0:09:03.461 lakini ninaweza kuwaambia 0:09:03.485,0:09:06.413 kua nilijua ilikua mara ya mwisho[br]ningeweza kufanya hivyo. 0:09:08.209,0:09:11.409 Na hio kumbukumbu[br]itakua ya kusikitisha daima. 0:09:11.733,0:09:13.666 Hio kumbukumbu itauma daima. 0:09:14.051,0:09:16.895 Hata kama nikiwa na miaka 600[br]na ni hologramu tu. 0:09:16.919,0:09:19.196 (Kicheko) 0:09:20.204,0:09:25.897 Kama tu kumbukumbu ya kukutana nae[br]itanifanya nicheke daima. 0:09:27.860,0:09:29.654 Maombolezo hayatokei kwenye huu[br]utupu, 0:09:29.678,0:09:36.146 yanatokea pamoja na na ikichanganyika[br]na hisia zote hizi nyingine. 0:09:38.024,0:09:42.572 Hivyo, nikakutana na Matthew, mme wangu wa[br]sasa -- 0:09:42.596,0:09:44.468 ambae hapendi hicho cheo, 0:09:44.492,0:09:48.270 (Kicheko) 0:09:48.713,0:09:50.189 lakini ni sawa kabisa. 0:09:50.213,0:09:52.823 (Kicheko) 0:09:53.935,0:09:56.283 Nilikutana na Matthew, na ... 0:09:57.577,0:10:00.908 kulikua na hii pumzi ya wazi ya faraja[br]kati ya watu wanaonipenda, 0:10:00.932,0:10:03.354 kama, "Imekwisha! 0:10:04.680,0:10:05.830 Ameweza. 0:10:07.069,0:10:09.537 Amepata mwisho mzuri,[br]tunaweza kurudi nyumbani sasa. 0:10:09.561,0:10:11.562 Na tumefanya vizuri." 0:10:11.586,0:10:14.609 Na hio hadithi inafaa hata[br]hata kwangu, 0:10:14.633,0:10:18.475 na nikawaza labda nimeipata[br]hio pia, lakini haikua hivyo. 0:10:18.499,0:10:21.037 Nilipata sura nyingine. 0:10:21.061,0:10:25.006 Na ni sura nzuri sana --[br]nakupenda, mpenzi -- 0:10:25.030,0:10:26.775 ni sura nzuri sana. 0:10:27.419,0:10:31.280 Tena haswahaswa mwanzoni,[br]ilikua kama ulimwengu mbadala, 0:10:31.304,0:10:34.462 au moja ya vile vitabu ya zamani vya[br]"chagua shani yako" vya miaka ya 80 0:10:34.486,0:10:36.414 ambapo kuna mistari miwili sambamba. 0:10:36.438,0:10:38.032 Nikafungua moyo wangu kwa[br]Matthew, 0:10:38.056,0:10:41.820 na ubongo wangu ukawa,[br]"Ungependa kumfikiria Aaron? 0:10:42.409,0:10:46.409 Kama zamani, sasa, mbeleni,[br]ingia tu huko," na nilifanya hivyo. 0:10:47.052,0:10:50.141 Na ghafla,[br]hiyo mistari miwili ilifunguka kwa pamoja, 0:10:50.165,0:10:53.752 na kupendana na Matthew kumenisaidia[br]sana kugundua ukubwa 0:10:53.776,0:10:55.842 wa nilichopoteza Aaron alivyofariki. 0:10:57.680,0:10:58.843 Na ilivyo muhimu, 0:10:58.867,0:11:02.617 ilinisaidia kugundua kua upendo wangu[br]kwa Aaron 0:11:02.641,0:11:04.752 na maombolezo yangu kwa Aaron, 0:11:04.776,0:11:09.307 na upendo wangu kwa Matthew,[br]sio nguvu za kupishana. 0:11:10.680,0:11:13.480 Ni sehemu tu za uzi mmoja 0:11:14.111,0:11:15.644 Ni vitu sawa sawa. 0:11:18.000,0:11:21.246 Wazazi wangu wangesemaje? 0:11:21.270,0:11:22.809 Mimi sio wa pekee. 0:11:23.645,0:11:24.660 (Kicheko) 0:11:24.684,0:11:27.220 Walikua na watoto wanne,[br]walikua kama ... wa kweli. 0:11:27.244,0:11:29.029 (Kicheko) 0:11:29.053,0:11:30.821 Lakini mimi sio, mimi sio wa pekee. 0:11:30.845,0:11:32.903 Ninajua hilo, ninajua vizuri 0:11:32.927,0:11:35.434 kua siku nzima, kila siku[br]duniani kote, 0:11:35.458,0:11:37.236 vitu vibaya vinatokea. 0:11:37.260,0:11:38.411 Kila mara. 0:11:38.435,0:11:40.180 Kama nilivyosema, mtu mcheshi. 0:11:40.204,0:11:42.690 Lakini vitu vibaya vinatokea, 0:11:42.714,0:11:49.108 watu wanapata hasara za kina na mbaya[br]kila siku. 0:11:49.132,0:11:51.720 Na kama sehemu ya kazi yangu, 0:11:51.744,0:11:53.426 hii podikasti ya ajabu niliyonayo, 0:11:53.450,0:11:54.698 kuna mda ninaongea na watu 0:11:54.722,0:11:57.706 kuhusu kitu kibaya[br]kilichowahi kuwatokea. 0:11:57.730,0:12:00.761 Na saa nyingine, hio ni[br]kupotelewa na mpendwa, 0:12:00.785,0:12:05.475 mara nyingine siku, wiki miaka[br]au miongo iliyopita. 0:12:06.373,0:12:08.903 Na hawa watu ninaowahoji, 0:12:08.927,0:12:11.235 hawajajifungia wenyewe[br]kwenye hii hasara 0:12:11.259,0:12:13.609 na kuifanya sehemu kuu ya maisha yao. 0:12:13.911,0:12:18.212 Wameishi, dunia zao[br]zimeendelea kuzunguka. 0:12:19.478,0:12:22.620 Lakini wanaongea na mimi,[br]mgeni kabisa, 0:12:22.644,0:12:24.579 kuhusu mtu wanaempenda aliyekufa, 0:12:24.603,0:12:27.743 kwa sababu hivi ndivyo vitu tunavyopitia 0:12:27.767,0:12:32.854 vinavyotuonyesha na kutufanya[br]kama tu wale wenye furaha. 0:12:33.355,0:12:35.212 Na kama ilivyo ya kudumu. 0:12:36.895,0:12:39.466 Baadae baada ya kupata kadi yako[br]ya mwisho ya huruma 0:12:39.490,0:12:40.957 au pishi la moto la mwisho. 0:12:41.546,0:12:43.577 Kama, hatuangalii watu[br]wanaotuzunguka 0:12:43.601,0:12:48.100 wakipitia furaha na maajabu ya maisha[br]na kuwaambia "wasonge mbele", ndio? 0:12:48.124,0:12:51.680 Hatutumi kadi ambazo zinasema[br]"Hongera kwa mtoto mzuri," 0:12:51.704,0:12:55.395 halafu, miaka mitano baadae, tunawaza, [br]"Sherehe nyingine ya kuzaliwa? Acha hizo." 0:12:55.419,0:12:57.085 (Kicheko) 0:12:57.109,0:12:58.768 Ndio, tunaelewa, ana miaka mitano. 0:12:58.792,0:13:00.220 (Kicheko) 0:13:00.244,0:13:01.418 Wow. 0:13:01.442,0:13:02.592 (Kicheko) 0:13:04.148,0:13:06.164 Lakini maombolezo ni moja ya vile vitu, 0:13:06.188,0:13:09.967 kama kupenda au kuwa na mtoto[br]au kuangalia "The Wire" kwenye HBO, 0:13:09.991,0:13:14.073 ambapo hauelewi[br]mpaka upate, mpaka ufanye. 0:13:15.219,0:13:20.522 Na punde unavyofanya,[br]punde ni mpenzi wako au mtoto wako, 0:13:20.546,0:13:25.736 punde ni maombolezo yako[br]na uko mstari wa mbele kwenye msiba, 0:13:25.760,0:13:26.910 unaelewa. 0:13:27.315,0:13:31.451 Unaelewa unachopitia sio[br]sehemu ya mda, 0:13:31.475,0:13:33.417 sio mfupa kua utajirudi, 0:13:33.441,0:13:36.307 lakini kua umeguswa na kitu kikali. 0:13:36.919,0:13:38.117 Kitu kisichotibika. 0:13:38.141,0:13:40.997 Hakiui, lakini saa nyingine[br]yanakua kama yanaweza. 0:13:43.269,0:13:46.848 Na kama hatuwezi kuzuia miongoni mwetu, 0:13:46.872,0:13:48.189 nini tunaweza kufanya? 0:13:50.554,0:13:54.874 Nini tunaweza kufanya zaidi ya[br]kukumbushiana 0:13:54.898,0:13:57.604 kua vitu vingine havirekebishiki, 0:13:58.136,0:14:01.318 na sio kila kidonda kinapaswa kupona. 0:14:02.493,0:14:05.684 Tunahitajiana kukumbuka, 0:14:05.708,0:14:07.470 kusaidiana kukumbuka, 0:14:07.494,0:14:10.263 kua maombolezo ni hisia ya mambo mengi. 0:14:10.287,0:14:16.084 Kua unaweza na utakua na huzuni, na[br]furaha; utaomboleza na kupenda 0:14:16.108,0:14:19.347 kwenye mwaka au wiki au pumzi hio hio. 0:14:20.982,0:14:26.704 Tunahitaji kukumbuka kua mtu anaeomboleza[br]ataenda kucheka na kutabasamu tena. 0:14:27.498,0:14:30.698 Wakibahatika,[br]wanaweza hata kupenda tena. 0:14:31.697,0:14:35.163 Lakini ndio, hakika[br]wataenda kusonga mbele. 0:14:36.071,0:14:39.071 Lakini hiyo haimaanishi kua[br]wameendelea mbele. 0:14:40.253,0:14:41.412 Asanteni. 0:14:41.436,0:14:48.078 (Makofi)