< Return to Video

Algebra: Linear equations 4 | Linear equations | Algebra I | Khan Academy

  • 0:00 - 0:01
  • 0:01 - 0:04
    Karibu kwenye kipindi cha milinganyo hatua ya nne.
  • 0:04 - 0:07
    Hebu tufanye baadhi ya maswali.
  • 0:07 - 0:07
    Hivyo.
  • 0:07 - 0:10
    Tuchukulie nina-- ngoja nikupe baadhi ya
  • 0:10 - 0:20
    maswali-- kama nikisema 3 juu ya x ni sawa na 5.
  • 0:20 - 0:23
    Hivyo, tunachotaka kufanya--hili swali ni tofauti na
  • 0:23 - 0:24
    yale tulioyaona.
  • 0:24 - 0:27
    Kwa sababu hapa, badala ya kuwa na x kwenye kiasi, tuna
  • 0:27 - 0:28
    x kwenye asili.
  • 0:28 - 0:31
    Hivyo, sihitaji kuwa na x kwenye asili,
  • 0:31 - 0:34
    tunahitaji kuitoa kwenye asili na kuwa kwenye
  • 0:34 - 0:36
    kiasi na sio kwenye asili
  • 0:36 - 0:37
    kama ifuatavyo.
  • 0:37 - 0:41
    Hivyo, njia mojawapo ya kuondoa namba kwenye asili ni hivi, kama
  • 0:41 - 0:46
    tunazidisha pande zote za huu mlinganyo kwa x, unaona
  • 0:46 - 0:47
    kwenye huu upande wa kushoto wa mlinganyo hizi
  • 0:47 - 0:49
    x mbili zitaisha.
  • 0:49 - 0:52
    Na upande wa kulia, utapata 5 mara x.
  • 0:52 - 0:57
    Hivyo hii ni sawa na -- x mbili zinaisha.
  • 0:57 - 1:01
    na unapata 3 ni sawa na 5x.
  • 1:01 - 1:05
    Tunaweza kuiandika hivi, 5x ni sawa na 3.
  • 1:05 - 1:08
    Kisha tunachagua njia ya kufanya kati ya hizi mbili.
  • 1:08 - 1:12
    Tunaweza kuzidisha pande zote kwa 1/5, au unaweza
  • 1:12 - 1:14
    kugawanya kwa 5.
  • 1:14 - 1:16
    Kama ukizidisha pande zote kwa 1/5.
  • 1:16 - 1:19
    Upande wa kushoto unabakia na x.
  • 1:19 - 1:24
    Na upande wa kulia ni, 3 mara 1/5, ni sawa na 3/5.
  • 1:24 - 1:25
    Nini tulichokifanya hapa?
  • 1:25 - 1:27
    Hii inaturudisha kwenye swali la hatua
  • 1:27 - 1:29
    ya pili, au swali la hatua ya kwanza,
  • 1:29 - 1:29
    napitia kwa haraka.
  • 1:29 - 1:32
    Tulichokifanya nikuzidisha pande zote za huu
  • 1:32 - 1:33
    mlinganyo kwa x.
  • 1:33 - 1:35
    Na tukaitoa x kwenye asili.
  • 1:35 - 1:36
    Hebu tufanye swali lingine.
  • 1:36 - 1:41
  • 1:41 - 1:54
    Tuchukulie tuna, x jumlisha 2 juu ya x jumlisha 1 ni
  • 1:54 - 1:59
    sawa na 7.
  • 1:59 - 2:01
    Hapa, badala ya kuwa na x kwenye asili,
  • 2:01 - 2:03
    tuna x jumlisha 1 kwenye asili.
  • 2:03 - 2:05
    Lakini tutafanya kwa njia ileile.
  • 2:05 - 2:09
    Ili kuondoa x jumlisha 1 kwenye asili, tunazidisha pande
  • 2:09 - 2:15
    zote za huu mlinganyo mara x jumlisha 1 juu ya 1 mara huu upande.
  • 2:15 - 2:17
    Kwa kuwa tumefanya hivyo upande wa kushoto pia tuna
  • 2:17 - 2:20
    fanya hivyo upande wa kulia, na hii ni 7/1,
  • 2:20 - 2:24
    mara x jumlisha 1 juu ya 1.
  • 2:24 - 2:28
    Kwenye upande wa kushoto, x jumlisha 1 zinaisha.
  • 2:28 - 2:31
    Na unabakiwa na x jumlisha 2.
  • 2:31 - 2:33
    Juu ya 1, lakini tunaiacha 1.
  • 2:33 - 2:39
    Hii ni sawa na 7 mara x jumlisha 1.
  • 2:39 - 2:42
    Hiyo ni sawa na x jumlisha 2.
  • 2:42 - 2:46
    Kumbuka, 7 mara kitu kizima, x jumlisha 1.
  • 2:46 - 2:48
    Hivyo tunatakiwa tufungua mabano.
  • 2:48 - 2:54
    Na hii ni sawa na 7x jumlisha 7.
  • 2:54 - 2:57
    Hii inaturudisha kwenye mlinganyo
  • 2:57 - 2:59
    hatua ya tatu.
  • 2:59 - 3:02
    Tunachokifanya sasa, tunaweka x zote
  • 3:02 - 3:03
    upande mmoja wa mlinganyo.
  • 3:03 - 3:06
    Kisha tunaweka namba kamili, ambazo ni 2 na 7, kwenye
  • 3:06 - 3:07
    upande mwingine wa mlinganyo
  • 3:07 - 3:09
    Hivyo naamua kuweka x upande wa kushoto.
  • 3:09 - 3:11
    Hivyo tunaileta 7x kwenye upande wa kushoto.
  • 3:11 - 3:14
    Na tunafanya hivyo kwa kutoa 7x pande zote.
  • 3:14 - 3:19
    Toa 7x, toa 7x.
  • 3:19 - 3:23
    Upande wa kulia, hizi 7x mbili zinaisha.
  • 3:23 - 3:26
    Na upande wa kushoto tuna hasi 7x jumlisha x.
  • 3:26 - 3:33
    Vizuri, hii ni hasi 6x jumlisha 2 ni sawa na,
  • 3:33 - 3:35
    kulia tumebakiwa na 7.
  • 3:35 - 3:36
    Hivyo tunataka kuondoa hii 2.
  • 3:36 - 3:41
    Na tunfanya hivyo kwa kutoa 2 pande zote.
  • 3:41 - 3:48
    Na tutabakiwa na hasi 6x ni sawa na 5.
  • 3:48 - 3:49
    Hili ni swali la kwenye hatua ya kwanza.
  • 3:49 - 3:52
    Tunatakiwa tuzidishe pande zote mara kinyume katika kuzidisha
  • 3:52 - 3:54
    kizidishi upande wa kushoto.
  • 3:54 - 3:56
    Na kizidishi ni hasi 6.
  • 3:56 - 4:00
    Hivyo tunazidisha pande zote za mlinganyo kwa hasi 1/6.
  • 4:00 - 4:03
  • 4:03 - 4:06
    Hasi 1/6.
  • 4:06 - 4:09
    Upande wa kushoto, hasi 1 juu ya 6 mara hasi 6.
  • 4:09 - 4:10
    Ni sawa na 1,
  • 4:10 - 4:16
    Tumepata x ni sawa na 5 mara hasi 1/6.
  • 4:16 - 4:19
    Hii ni hasi 5/6.
  • 4:19 - 4:22
  • 4:22 - 4:23
    Na tumemaliza.
  • 4:23 - 4:26
    Na kama unataka kuhakikisha, utachukua hii x
  • 4:26 - 4:29
    sawa na hasi 5/6 na kuiweka kwenye swali letu la awali
  • 4:29 - 4:31
    kuthibitisha jibu.
  • 4:31 - 4:31
    Tufanye swali lingine.
  • 4:31 - 4:35
  • 4:35 - 4:38
    Naandika kwa hapa juu.
  • 4:38 - 4:40
    Tuchukulie.
  • 4:40 - 4:51
    3 mara x jumlisha 5 ni sawa na 8 mara x jumlisha 2.
  • 4:51 - 4:53
    Tunafanya kitu kilekile hapa.
  • 4:53 - 4:56
    Ingawa tuna milinganyo miwili, tunayohitaji kuiondoa
  • 4:56 - 4:57
    kwenye asili.
  • 4:57 - 4:59
    Tunataka kuondoa x jumlisha 5 pia tunataka kuondoa
  • 4:59 - 5:00
    x jumlisha 2.
  • 5:00 - 5:02
    Tuondoe x jumlisha 5 kwanza.
  • 5:02 - 5:04
    Vizuri, kama tulivyofanya awali, tunazidisha pande zote
  • 5:04 - 5:06
    za huu mlinganyo kwa x jumlisha 5.
  • 5:06 - 5:08
    Unaweza kusema x jumlisha 5 juu ya 1.
  • 5:08 - 5:13
    Mara x jumlisha 5 juu ya 1.
  • 5:13 - 5:15
    Upande wa kushoto, zinaisha.
  • 5:15 - 5:24
    Hivyo tunabakiwa na 3 ni sawa na 8 mara x jumlisha tano.
  • 5:24 - 5:29
    juu ya x jumlisha 2.
  • 5:29 - 5:32
    Sasa, tunarahisisha, kwa mara nyingine
  • 5:32 - 5:34
    tunazidisha 8 mara mlinganyo wote.
  • 5:34 - 5:42
    Hivyo ni 8x jumlisha 40 juu ya x jumlisha 2.
  • 5:42 - 5:44
    Sasa, tunataka kuondoa x jumlisha 2.
  • 5:44 - 5:45
    Hivyo tutafanya njia ileile.
  • 5:45 - 5:47
    Tunazidisha pande zote za mlinganyo kwa
  • 5:47 - 5:51
    x jumlisha 2 juu ya 1.
  • 5:51 - 5:53
    x jumlisha 2.
  • 5:53 - 5:54
    Tunaweza kusema tunazidisha
  • 5:54 - 5:54
    pande zote kwa x jumlisha 2.
  • 5:54 - 5:57
    Hii 1 ni sio ya lazima.
  • 5:57 - 6:03
    Hivyo upande wa kushoto unakuwa 3x jumlisha 6.
  • 6:03 - 6:05
    Kumbuka kuzidisha mara 3 kote, kwa sababu
  • 6:05 - 6:07
    unaizidisha kwa mlinganyo wote.
  • 6:07 - 6:09
    x jumlisha 2.
  • 6:09 - 6:10
    Kwenye upande wa kulia.
  • 6:10 - 6:14
    Hii x jumlisha 2 na hii x jumlisha 2 zinaisha.
  • 6:14 - 6:16
    Tunabakiwa na 8x jumlisha 40.
  • 6:16 - 6:19
    Na hii ni swali la hatua ya tatu.
  • 6:19 - 6:25
    Kama tunatoa 8x pande zote, hasi 8x, jumlisha
  • 6:25 - 6:27
    nafikiri nimemaliza nafasi.
  • 6:27 - 6:28
    Toa 8x.
  • 6:28 - 6:31
    Kwenye upande wa kulia 8x zinaisha.
  • 6:31 - 6:39
    Kwenye upande wa kushoto tuna hasi 5x jumlisha 6 ni sawa
  • 6:39 - 6:42
    na, kwenye upande wa kulia tumebakiwa na 40.
  • 6:42 - 6:45
    Sasa tunatoa 6 kwenye pande zote za mlinganyo.
  • 6:45 - 6:46
    Naandika hapa.
  • 6:46 - 6:50
    Toa 6 jumlisha toa 6.
  • 6:50 - 6:51
    Natumaini mmenielewa
  • 6:51 - 6:53
    mpaka hapa.
  • 6:53 - 6:56
  • 6:56 - 6:58
    Tukitoa kwa hasi 6 pande zote, upande wa kushoto
  • 6:58 - 7:05
    tumebakiwa na hasi 5x sawa na kwenye
  • 7:05 - 7:09
    upande wa kulia tuna 34.
  • 7:09 - 7:10
    Hili ni swali la kwenye hatua ya kwanza.
  • 7:10 - 7:13
    Tunazidisha pande zote mara hasi 1/5.
  • 7:13 - 7:17
  • 7:17 - 7:18
    Hasi 1/5.
  • 7:18 - 7:21
    Kwenye upande wa kushoto tuna x.
  • 7:21 - 7:27
    Na kwenye upande wa kulia tuna hasi 34/5.
  • 7:27 - 7:30
    Huenda kuna makosa madogomadogo, lakini natumai nipo sahihi.
  • 7:30 - 7:33
    Natumai kama umeelewa tulichofanya hapa, basi
  • 7:33 - 7:37
    upo tayari kufanya maswali ya milinganyo ya hatua ya nne.
  • 7:37 - 7:38
    Uwe na furaha.
  • 7:38 - 7:39
Title:
Algebra: Linear equations 4 | Linear equations | Algebra I | Khan Academy
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
Khan Academy
Duration:
07:39

Swahili subtitles

Revisions