Nguvu inayoponya katika kusoma
-
0:01 - 0:06Ninataka kuzungumza namna kusoma
kunavyoweza kubadilisha maisha yetu -
0:06 - 0:09na kuhusu mipaka ya mabadiliko hayo
-
0:10 - 0:14Ninataka kuzungumza na wewe namna kusoma
kunavyoweza kutupa ulimwengu wa ushirika -
0:14 - 0:17wa muunganiko wenye nguvu wa kibinadamu
-
0:18 - 0:21pia namna ambavyo muunganiko huo
ni sehemu tu mara zote -
0:21 - 0:26Kusoma mwisho wa siku ni kitendo cha
upweke na kisicho cha kawaida. -
0:28 - 0:30Muandishi aliyebadilisha maisha yangu
-
0:30 - 0:35Ni mmarekani mweusi na mwandishi
wa riwaya James Baldwin -
0:35 - 0:38Wakati ninakuwa katika eneo la
Magharibi mwa Michigan miaka ya 1980, -
0:38 - 0:42hakukuwa na wamarekani wenye asili ya asia
wengi wanaoandika kuhusu mabadiliko ya kijamii -
0:43 - 0:47Na ndio maana nilimgeukia James Baldwin
-
0:47 - 0:51kama namna ya kuliziba hili ombwe,
kama namna ya kuwamakini na rangi -
0:52 - 0:56lakini haswa kwa sababu nilifahamu
mimi sikuwa mmarekani mweusi, -
0:56 - 1:00Pia nilisikia kupata changamoto na
kuthibitishwa na maneno yake. -
1:00 - 1:03Hasusani maneno haya:
-
1:03 - 1:07"Ni watu huria walio na mitazamo sahihi,
-
1:07 - 1:09lakini hawana misimamo halisi.
-
1:10 - 1:14pale ambapo vipande vipo chini
na unawategemea kuleta matokeo, -
1:14 - 1:17na huenda hawako hapo kwa namna fulani".
-
1:17 - 1:19Hawako hapo kwa namna fulani.
-
1:19 - 1:22Nikayachukua hayo maneno nikitafakari.
-
1:22 - 1:23Nijiweke wapi?
-
1:24 - 1:27Nilikwenda kwenye delta ya Mississippi,
-
1:27 - 1:30mojawapo ya maeneo masikini sana ya
Marekani. -
1:30 - 1:33Hii ni sehemu ambayo imejengwa
na historia yenye nguvu. -
1:33 - 1:38Katika mwaka wa 1960, Wamarekani weusi
walijitoa maisha yao kupigania Elimu, -
1:38 - 1:40kupigania haki ya kupiga kura.
-
1:41 - 1:43Nilitaka kuwa sehemu ya badiliko hilo,
-
1:43 - 1:47kuwasaidia vijana wadogo wamalize shule
na kujiunga na vyuo. -
1:48 - 1:51Nilipoenda kwenye Delta ya Mississipi,
-
1:51 - 1:53Palikuwa ni mahali duni bado,
-
1:53 - 1:55bado pametengwa,
-
1:55 - 1:58Bado panahitaji mabadiliko ya kasi.
-
1:59 - 2:02Shule yangu, pale nilipokuwa nasoma,
-
2:02 - 2:07haikuwa na maktaba, hakuna mshauri,
-
2:07 - 2:10lakini ilikuwa na afisa wa polisi.
-
2:10 - 2:12Nusu ya walimu walikuwa ni mbadala
-
2:12 - 2:14na wanafunzi walipoingia kwenye ugomvi,
-
2:14 - 2:18Shule iliwapeleka kwenye jela ya
mahali hapo. -
2:20 - 2:23Hii ndiyo shule nilipokutana na Patrick.
-
2:23 - 2:28Alikuwa na miaka 15 na alikamatwa mara
mbili, alikuwa darasa la nane. -
2:28 - 2:31Alikuwa ni mkimya na mndani,
-
2:31 - 2:34ni kama kila wakati alikuwa mwenye mawazo.
-
2:34 - 2:36Na alichukia kuona wengine wakipigana.
-
2:38 - 2:41Nilimuona mara moja akiruka kati ya
mabinti wawili walipokuwa wakipigana -
2:41 - 2:44Na akajikuta akidondoka na kuanguka chini.
-
2:45 - 2:48Patrick alikuwa na tatizo moja.
-
2:48 - 2:50Hakuwa akifika shuleni.
-
2:51 - 2:54Alisema kuwa shule wakati mwingine humfanya kuwa na msongo
-
2:54 - 2:57Sababu wanafunzi hupigana mara zote na
walimu wanaondoka. -
2:58 - 3:04Lakini pia, mama yake anafanya kazi mbili
na huwa anachoka kuweza kumfanya aje shule. -
3:04 - 3:07Hivyo nikafanya iwe kazi yangu
kumfanya awe anakuja shule. -
3:07 - 3:11Na sababu nilikuwa na wazimu na miaka 22
na mwenye bidii ya matumaini -
3:11 - 3:13Njia yangu ilikuwa ni
kwenda nyumbani kwao -
3:13 - 3:16na kusema "Eti, kwanini hauji
shuleni?" -
3:17 - 3:18Na njia hii ilifanya kazi,
-
3:18 - 3:21akaanza kuja shuleni kila siku.
-
3:21 - 3:23Na akaanza kufanikiwa katika darasa langu.
-
3:23 - 3:26Aliandika mashairi,
alisoma vitabu. -
3:27 - 3:29Alikuja shuleni kila siku.
-
3:31 - 3:33takriban muda ule ule
-
3:33 - 3:35Nilipogundua namna ya kushirikiana
na Patrick, -
3:35 - 3:37Nilikwenda shule ya sheria Harvard.
-
3:40 - 3:43Nilikutana tena na swali hili,
nijiweke wapi, -
3:43 - 3:45niuweke wapi mwili wangu?
-
3:45 - 3:48Na nikawaza mwenyewe
-
3:48 - 3:52Kuwa Mississipi Delta
ni mahali ambapo watu wenye fedha, -
3:52 - 3:54watu wenye fursa,
-
3:54 - 3:55watu hao huondoka.
-
3:56 - 3:57Na watu wanaobakia
-
3:57 - 4:00ni watu ambao hawana fursa ya kuondoka.
-
4:01 - 4:03Sikutaka kuwa mtu anayeondoka.
-
4:03 - 4:05Nilitaka kuwa mtu anayebakia.
-
4:06 - 4:09Kwa upande mwingine, nilikuwa mpweke
na mchovu. -
4:09 - 4:13Na hivyo nilijishawishi mwenyewe
kuwa ninaweza kufanya mabadiliko -
4:14 - 4:18Kwa kiasi kikubwa kama ningekuwa
na shahada yenye heshima ya sheria. -
4:20 - 4:21Hivyo nikaondoka.
-
4:23 - 4:24Miaka mitatu baadaye,
-
4:24 - 4:27Nilipokaribia kuhitimu
shule ya sheria, -
4:27 - 4:29rafiki yangu alinipigia simu
-
4:29 - 4:33na kuniambia kuwa Patrick
amepigana na kuua mtu. -
4:35 - 4:37Nilitaharuki.
-
4:37 - 4:40Sehemu ya mimi haikuamini,
-
4:40 - 4:43na sehemu ya mimi pia iliamini kuwa
ni kweli. -
4:44 - 4:46Nilisafiri kwenda kumuona Patrick.
-
4:47 - 4:49Nilimtembelea gerezani.
-
4:51 - 4:54Na aliniambia kuwa ilikuwa kweli.
-
4:54 - 4:57Ya kwamba ameua mtu.
-
4:57 - 4:59Na asingependa kuzungumzia suala hilo.
-
5:00 - 5:02Nilimuuliza nini kiliendelea kuhusu shule
-
5:02 - 5:06na akasema aliacha shule mwaka mooja
baada ya mimi kuondoka. -
5:06 - 5:09Na alitaka kuniambia kuhusu kitu kingine
-
5:09 - 5:12Alitazama chini akasema
ya kwamba amepata mtoto wa kike -
5:12 - 5:14ambaye ndiye kwanza amezaliwa.
-
5:14 - 5:16Na anahisi kuwa amemuangusha binti yake.
-
5:19 - 5:22Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mazungumzo yetu
yalikuwa ya haraka na mabaya. -
5:23 - 5:28Nilipotoka nje ya gereza,
sauti ndani yangu iliniambia, -
5:28 - 5:30"Rudi.
-
5:30 - 5:33Usiporudi sasa, hutarudi kamwe".
-
5:36 - 5:40Hivyo nikahitimu shule ya sheria na
nikarudi. -
5:41 - 5:43Nikarudi kumuona Patrick,
-
5:43 - 5:46Nikarudi kuona kama ninaweza kumsaidia
na kesi yake ya sheria. -
5:47 - 5:50Muda huu,
nilipomuona kwa mara ya pili, -
5:50 - 5:53Nilidhani nina hili wazo zuri,
nikamwambia, -
5:53 - 5:56"Hey, Patrick, kwanini usiandike barua
kwa binti yako, -
5:56 - 6:00ili uweze kumuweka katika
fikra zako?" -
6:00 - 6:04Nikampatia kalamu na
kipande cha karatasi, -
6:04 - 6:05na akaanza kuandika.
-
6:07 - 6:09Lakini nilipoiona karatasi aliyonipatia,
-
6:09 - 6:11Nilipigwa na butwaa.
-
6:13 - 6:15Sikuutambua mwandiko wake,
-
6:15 - 6:18alikuwa amefanya makosa
machache ya matamshi. -
6:19 - 6:22na nikawaza mwenyewe kama mwalimu,
-
6:22 - 6:25Ninafahamu ya kuwa mwanafunzi
anaweza kufanya vizuri kwa kasi -
6:25 - 6:28Kwa muda mfupi sana,
-
6:28 - 6:32lakini sikuwahi kuwaza kuwa mwanafunzi
anaweza kurudi nyuma kwa kasi. -
6:34 - 6:36kilichoniumiza zaidi,
-
6:36 - 6:39ni kuona kile alichokiandika
kwa binti yake. -
6:40 - 6:41aliandika,
-
6:41 - 6:45"Ninasikitika kwa makosa yangu,
ninasikitika kutokuwa pamoja nawe." -
6:46 - 6:49Na hiki ndicho alichojisikia
anataka kusema naye. -
6:50 - 6:55Nikajiuliza ni namna gani ninaweza
kumshawishi kuwa anaweza kumwambia zaidi, -
6:55 - 6:58ile sehemu yake ambayo
hahitaji kuomba radhi kwayo. -
6:59 - 7:00Nilitaka yeye ajisikie
-
7:00 - 7:04kuwa anakitu cha thamani
kumshirikisha binti yake. -
7:06 - 7:09Kwa kila siku kwa miezi saba iliyofuatia,
-
7:09 - 7:12Nilimtembelea na kumpelekea vitabu.
-
7:12 - 7:16Mkoba wangu uligeuka kuwa maktaba ndogo.
-
7:16 - 7:18Nilimpelekea James Baldwin,
-
7:18 - 7:23Nilipeleka Walt Whitman, C.S.Lewis.
-
7:23 - 7:28Nilileta vitabu vya mwongozo wa miti,
wa ndege, -
7:28 - 7:31na kitabu alichotokea kukipenda zaidi,
kamusi. -
7:32 - 7:33Kwa baadhi ya siku,
-
7:33 - 7:37tulikaa kimya kwa masaa,
wote wawili tukisoma. -
7:38 - 7:40Na siku nyingine,
-
7:40 - 7:43tulisoma pamoja,
tulisoma mashairi. -
7:44 - 7:47tulianza kwa kusoma haikus,
mamia ya haikus, -
7:47 - 7:50ni kito rahisi na danganyifu.
-
7:50 - 7:53Na ningemuuliza,
"Nishirikishe haiku zako unazozipenda". -
7:53 - 7:56Na baadhi yake ni za kufurahisha sana.
-
7:56 - 7:58Kuna hii ya Issa:
-
7:58 - 8:02"Usijali, buibui,
ninaweka nyumba kikawaida." -
8:03 - 8:07Na hii: "Nimelala nusu ya siku,
na hakuna aliyeniadhibu!" -
8:09 - 8:13Na hii nyingine ya kuvutia, inayohusu
siku ya kwanza barafu ilipodondoka, -
8:13 - 8:18"Kulungu wakilamba baridi ya kwanza
kutoka kwenye koti la kila mmoja wao." -
8:19 - 8:22Kuna kitu cha ajabu na cha kuvutia
-
8:22 - 8:25kuhusu namna shairi linavyoonekana.
-
8:25 - 8:30Nafasi ya shairi ni muhimu
kama maneno yenyewe. -
8:31 - 8:34Tunasoma shairi hili lililoandikwa na
W.S.Merwin, -
8:34 - 8:38ambalo aliliandika baada ya kumuona
mkewe akifanya kazi kwenye bustani -
8:38 - 8:42na akakumbuka kuwa wataishi maisha
yao yote yaliyobaki wakiwa pamoja. -
8:43 - 8:46"Wacha nifikiri kuwa tutakuja tena
-
8:46 - 8:49tutakapotaka na itakuwa wakati wa masika
-
8:49 - 8:52hatutakuwa na umri mkubwa
kuliko tulivyowahi kuwa -
8:52 - 8:56na majonzi yatakuwa mepesi kama
mawingu ya mapema -
8:56 - 9:00ambayo kwayo asubuhi
huja yenyewe taratibu" -
9:00 - 9:03Nikamuuliza Patrick mstari alioupenda
zaidi ni upi, na akasema -
9:03 - 9:07"Hatutakuwa na umri mkubwa
kuliko tulivyokuwa." -
9:08 - 9:13Alisema inamkumbusha
mahali ambapo muda husimama, -
9:13 - 9:16pale ambapo muda haumaanishi
kitu chochote. -
9:16 - 9:18Na nikamuuliza kama amewahi kuwa
na mahali pa jinsi hiyo. -
9:18 - 9:20pale ambapo muda hudumu milele.
-
9:20 - 9:22Na akasema, "Mama yangu".
-
9:24 - 9:28Na pale unaposoma shairi
pamoja na mtu mwingine, -
9:28 - 9:30shairi hubadilika katika maana.
-
9:31 - 9:36Kwa sababu huwa la kibinafsi kwa mtu huyo,
huwa la kibinafsi kwako. -
9:38 - 9:40Halafu tulisoma vitabu,
tulisoma vitabu vingi sana, -
9:40 - 9:43tulisoma kumbukumbu za Frederick Douglass,
-
9:43 - 9:47Mtumwa wa Marekani aliyejifunza mwenyewe
kusoma na kuandika -
9:47 - 9:50na aliyetoroka na kuwa huru
sababu ya kuelimika kwake. -
9:52 - 9:55Nimekua nikimfikiria Frederick Douglass
kama shujaa -
9:55 - 9:58na niliiona hii simulizi kama
iliyojaa matumaini na yenye kuinua -
9:59 - 10:02Lakini kitabu hiki kilimuweka Patrick
katika hofu. -
10:03 - 10:08Alibakia katika simulizi aliyoielezea
Douglass jinsi ambavyo, katika Christmas, -
10:08 - 10:11Mabwana waliwapa watumwa jini(pombe kali)
-
10:11 - 10:15kama namna ya kuwaaminisha kuwa
hawawezi kuumudu uhuru. -
10:15 - 10:17Kwa sababu watumwa waliweweseka
katika mashamba. -
10:20 - 10:22Patrick alisema anajifananisha na hili.
-
10:22 - 10:26Alisema kuwa kuna watu gerezani ambao,
kama watumwa, -
10:26 - 10:28hawataki kuwaza juu ya hali zao,
-
10:28 - 10:30kwa sababu inawaumiza sana.
-
10:30 - 10:32Inaumiza sana kuwaza mambo ya nyuma,
-
10:32 - 10:35inaumiza sana kuwaza
kuhusu umbali gani tunapaswa kwenda. -
10:37 - 10:40Mstari alioupenda sana ulikuwa huu:
-
10:40 - 10:43"Chochote kile, bila kujali chochote,
kujiondoa katika kuwaza! -
10:44 - 10:49Ilikuwa ni huku kuwaza kusiko koma kuhusu
hali yangu ndiko kunako kipa mateso." -
10:50 - 10:54Patrick alisema Douglass alikuwa jasiri
kuandika, ili aendelee kuwaza. -
10:55 - 11:01Lakini Patrick hakufahamu kuwa alionekana
kufanana sana na Douglass kwangu. -
11:01 - 11:04Namna alivyoendelea kusoma,
ijapokuwa ilimuweka katika hofu. -
11:05 - 11:08Alimaliza kitabu kabla yangu,
-
11:08 - 11:12akisoma katika ngazi za
zege zisizo na taa. -
11:14 - 11:16Halafu tukaendelea kusoma mojawapo
ya vitabu ninavyovipenda, -
11:16 - 11:19Cha Marilynne Robinson's "Gilead,"
-
11:19 - 11:23ambayo ni barua endelevu kutoka
kwa baba kwenda kwa mwanae. -
11:23 - 11:25Alipenda mstari huu:
-
11:25 - 11:27"Ninaandika hii kwa sehemu kukuambia
-
11:27 - 11:31ya kwamba kama umewahi kujiuliza
kile umekifanya katika maisha yako... -
11:31 - 11:33umekuwa neema ya Mungu kwangu,
-
11:33 - 11:36muujiza, kitu ambacho ni zaidi
ya muujiza." -
11:37 - 11:43Kitu kimoja kuhusu hii lugha,
upendo wake, subira yake, sauti yake, -
11:43 - 11:46iliamsha shauku ya Patrick katika kuandika.
-
11:46 - 11:49Na alijaza daftari kwa daftari
-
11:49 - 11:53na barua kwenda kwa binti yake.
-
11:53 - 11:56katika barua hizi nzuri na imara,
-
11:56 - 12:02alijiwazia yeye na binti yake
wakipanda mtumbwi katika mto Mississipi -
12:02 - 12:05Alijiwazia yeye na binti yake
wakipata vijito vya milimani -
12:05 - 12:07vikiwa na maji masafi bila kasoro.
-
12:08 - 12:10Nilipomtazama Patrick akiandika,
-
12:11 - 12:13Nilijiwazia mwenyewe,
-
12:13 - 12:15na sasa ninawaulizeni nyote,
-
12:16 - 12:21ni wangapi wenu mmewahi kuandika barua
kwa mtu unayehisi umemwangusha? -
12:22 - 12:27Ni rahisi sana
kuwaweka hao watu nje ya fikra zako. -
12:28 - 12:33Lakini Patrick alijitokeza kila siku,
akimkabili binti yake, -
12:33 - 12:36akijiwajibisha kwake,
-
12:36 - 12:39neno kwa neno kwa umakini wa hali ya juu.
-
12:42 - 12:45Ningependa katika maisha yangu binafsi
-
12:46 - 12:49kujiweka katika hatari kwa namna hiyo.
-
12:49 - 12:53Kwa sababu hatari hiyo inadhihirisha
nguvu za moyo wa mtu. -
12:57 - 13:01Ngoja nirudi hatua moja nyuma na niulize
swali ambalo linaleta wasiwasi. -
13:01 - 13:04Mimi ni nani kusimulia simulizi hii,
hii simulizi ya Patrick? -
13:06 - 13:09Patrick ndiye aliyeishi kwenye
maumivu haya -
13:09 - 13:13na mimi sijawahi kukaa na njaa hata
kwa siku moja kwenye maisha yangu -
13:15 - 13:17Ninawaza sana kuhusu swali hili,
-
13:17 - 13:21lakini ninachotaka kusema ni kuwa hii
simulizi sio tu kuhusu Patrick. -
13:21 - 13:22Inatuhusu sisi,
-
13:22 - 13:25ni kuhusu tofauti kati yetu.
-
13:26 - 13:27Ulimwengu wa vingi
-
13:28 - 13:32ambao Patrick na wazazi wake
na mababu zake -
13:32 - 13:34hawajawahi kuuona.
-
13:34 - 13:37Katika simulizi hii, mimi ninawakilisha
huo ulimwengu wa vingi. -
13:38 - 13:42Na katika kueleza simulizi hii
sikutaka kujificha mwenyewe. -
13:42 - 13:44Kuficha nguvu ambazo ninazo.
-
13:45 - 13:49Katika kueleza simulizi hii,
ninataka kuifichua nguvu hiyo -
13:49 - 13:51halafu kuuliza,
-
13:51 - 13:54tunawezaje kuipunguza
umbali kati yetu? -
13:56 - 14:00Kusoma ni njia mojawapo ya kuipunguza
hiyo nafasi. -
14:00 - 14:04Kunatuma ulimwengu wa ukimya
ambao tunaweza kuushiriki pamoja, -
14:04 - 14:07ambao tunaweza kuushiriki kwa usawa.
-
14:08 - 14:12Inawezekana unajiuliza sasa kuwa
ni nini kilitokea kwa Patrick. -
14:12 - 14:13Je kusoma kuliokoa maisha yake?
-
14:15 - 14:17Kuliyaokoa na hakukuyaokoa.
-
14:18 - 14:21Patrick alipotoka gerezani,
-
14:21 - 14:23safari yake ilikuwa ya maumivu.
-
14:24 - 14:28Waajiri hawakumkubali kwa sababu
ya historia yake, -
14:28 - 14:31rafiki yake mpenzi, mama yake,
alifariki katika umri wa miaka 43 -
14:31 - 14:33kwa ugonjwa wa moyo na kisukari.
-
14:33 - 14:36Alikuwa hana pa kuishi,
amekuwa hana chakula. -
14:38 - 14:43Kwa hiyo watu wanasema mengi kuhusu kusoma
ambayo kwangu ninahisi wanazidisha chumvi. -
14:44 - 14:48Uwezo wa kusoma haukumzuia yeye
asitengwe na jamii. -
14:48 - 14:50Hakukumzuia mama yake asifariki.
-
14:52 - 14:54Kwa hiyo kusoma kunaweza kufanya nini?
-
14:55 - 14:59Nina majibu machache ninapomalizia leo.
-
15:01 - 15:03Kusoma kulibadili utu wake wa ndani
-
15:05 - 15:08kwa mambo yaliyofichika na uwezo wa
kuwaza kwa picha. -
15:08 - 15:09kwa uzuri.
-
15:10 - 15:15Kusoma kulimpa taswira zilizompa furaha:
-
15:15 - 15:21milima, bahari, kulungu, theluji.
-
15:21 - 15:25Maneno yenye ladha ya ulimwengu huru
na halisi. -
15:28 - 15:31Kusoma kulimpa lugha kwa yale aliyopoteza.
-
15:31 - 15:36Ni jinsi gani yalivyo mazuri haya maneno
kutoka kwa mshairi Derek Walcott? -
15:36 - 15:38Patrick alilikariri hili shairi.
-
15:38 - 15:40"Siku ambazo nilizishikilia,
-
15:40 - 15:42siku ambazo nilizipoteza,
-
15:42 - 15:46siku ambazo zinakuwa kupitiliza,
kama mabinti, -
15:46 - 15:48mikono yangu inayoshikilia."
-
15:49 - 15:52Kusoma kulimfundisha ujasiri wake
mwenyewe. -
15:52 - 15:55Kumbuka kwamba aliendelea kusoma
Frederick Douglass, -
15:55 - 15:57ijapokuwa ilikuwa ya kuumiza.
-
15:57 - 16:01Aliendelea kuwa makini,
ijapokuwa kuwa makini kunauma. -
16:02 - 16:05Kusoma ni aina ya kutafakari,
-
16:05 - 16:09ndio maana ni vigumu sana kusoma
kwa sababu tunataka kutafakari. -
16:09 - 16:13Na Patrick alichagua kutafakari,
badala ya kutokutafakari. -
16:16 - 16:20Na mwishoni, kusoma kulimpa lugha
ya kuongea na binti yake. -
16:21 - 16:25Kusoma kulimpa shauku ya kutaka kuandika.
-
16:25 - 16:29Muunganiko kati ya kusoma na
kuandika ni wenye nguvu sana. -
16:29 - 16:31Tunapoanza kusoma,
-
16:31 - 16:33tunaanza kupata maneno.
-
16:34 - 16:39Na alipata maneno ya kutafakari
wao wawili wakiwa pamoja. -
16:39 - 16:40Alipata maneno
-
16:42 - 16:44ya kumwelezea ni namna gani anampenda.
-
16:46 - 16:50Kusoma pia kulibadilisha
mahusiano baina yetu. -
16:50 - 16:52Kunatupa nyakati za kuwa karibu,
-
16:52 - 16:55kuweza kuona zaidi ya mitazamo yetu.
-
16:55 - 16:58Na kusoma kulichukua mahusiano ya
kutokuwa sawa -
16:58 - 17:00na kulitupa usawa wa muda mfupi.
-
17:02 - 17:05Ukikutana na mtu kama msomaji,
-
17:05 - 17:07unakutana naye kwa mara ya kwanza,
-
17:07 - 17:09kwa upya kabisa.
-
17:10 - 17:13Hakuna namna unaweza kufahamu mstari
anaoupenda sana ni upi. -
17:14 - 17:18Ni kumbukumbu zipi na huzuni zipi za
siri alizonazo. -
17:19 - 17:23Na unakutana na sitara ya hali ya juu
ya utu wake wa ndani. -
17:24 - 17:27Na halafu unaanza kushangaa,
"Eti,utu wangu wa ndani umejengwa na nini? -
17:27 - 17:30Ni kitu gani nilichonacho cha thamani
cha kumshirikisha mwingine?" -
17:33 - 17:34Ninataka kufunga
-
17:36 - 17:40kwa mistari yangu ninayoipenda
kutoka kwa barua za Patrick kwa bintiye. -
17:41 - 17:44"Mto una kivuli kwenye baadhi ya maeneo
-
17:44 - 17:47lakini mwanga unaangaza
kupitia mianya ya miti... -
17:47 - 17:51Kwenye baadhi ya matawi
muliberi nyingi zimening'inia. -
17:51 - 17:54Unanyoosha mkono wako
ili uweze kuyachukua baadhi". -
17:56 - 17:58Na barua hii ya upendo, anapoandika,
-
17:58 - 18:03"Fumba macho yako na usikilize
sauti ya maneno. -
18:03 - 18:05Ninafahamu shairi hili kwa moyo
-
18:05 - 18:08na ningependa pia wewe ulifahamu."
-
18:09 - 18:11Ninawashukuruni nyote.
-
18:11 - 18:14(Makofi)
- Title:
- Nguvu inayoponya katika kusoma
- Speaker:
- Michelle Kuo
- Description:
-
Kusoma na kuandika vinaweza kuwa vitendo vya ujasiri vinavyotuleta karibu na watu wengine na karibu na nafsi zetu pia. Mwandishi Michelle Kuo anashirikisha namna ambavyo kufundisha stadi za kusoma kwa wanafunzi wake kule Mississippi Delta kulivyofunua nguvu ya daraja la maneno yaliyoandikwa-- pamoja na mipaka ya nguvu hiyo.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 18:27
![]() |
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for The healing power of reading | |
![]() |
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for The healing power of reading | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The healing power of reading | |
![]() |
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The healing power of reading | |
![]() |
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The healing power of reading | |
![]() |
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The healing power of reading | |
![]() |
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The healing power of reading | |
![]() |
Miriam Loivotoki Elisha edited Swahili subtitles for The healing power of reading |