Ninataka kuzungumza namna kusoma
kunavyoweza kubadilisha maisha yetu
na kuhusu mipaka ya mabadiliko hayo
Ninataka kuzungumza na wewe namna kusoma
kunavyoweza kutupa ulimwengu wa ushirika
wa muunganiko wenye nguvu wa kibinadamu
pia namna ambavyo muunganiko huo
ni sehemu tu mara zote
Kusoma mwisho wa siku ni kitendo cha
upweke na kisicho cha kawaida.
Muandishi aliyebadilisha maisha yangu
Ni mmarekani mweusi na mwandishi
wa riwaya James Baldwin
Wakati ninakuwa katika eneo la
Magharibi mwa Michigan miaka ya 1980,
hakukuwa na wamarekani wenye asili ya asia
wengi wanaoandika kuhusu mabadiliko ya kijamii
Na ndio maana nilimgeukia James Baldwin
kama namna ya kuliziba hili ombwe,
kama namna ya kuwamakini na rangi
lakini haswa kwa sababu nilifahamu
mimi sikuwa mmarekani mweusi,
Pia nilisikia kupata changamoto na
kuthibitishwa na maneno yake.
Hasusani maneno haya:
"Ni watu huria walio na mitazamo sahihi,
lakini hawana misimamo halisi.
pale ambapo vipande vipo chini
na unawategemea kuleta matokeo,
na huenda hawako hapo kwa namna fulani".
Hawako hapo kwa namna fulani.
Nikayachukua hayo maneno nikitafakari.
Nijiweke wapi?
Nilikwenda kwenye delta ya Mississippi,
mojawapo ya maeneo masikini sana ya
Marekani.
Hii ni sehemu ambayo imejengwa
na historia yenye nguvu.
Katika mwaka wa 1960, Wamarekani weusi
walijitoa maisha yao kupigania Elimu,
kupigania haki ya kupiga kura.
Nilitaka kuwa sehemu ya badiliko hilo,
kuwasaidia vijana wadogo wamalize shule
na kujiunga na vyuo.
Nilipoenda kwenye Delta ya Mississipi,
Palikuwa ni mahali duni bado,
bado pametengwa,
Bado panahitaji mabadiliko ya kasi.
Shule yangu, pale nilipokuwa nasoma,
haikuwa na maktaba, hakuna mshauri,
lakini ilikuwa na afisa wa polisi.
Nusu ya walimu walikuwa ni mbadala
na wanafunzi walipoingia kwenye ugomvi,
Shule iliwapeleka kwenye jela ya
mahali hapo.
Hii ndiyo shule nilipokutana na Patrick.
Alikuwa na miaka 15 na alikamatwa mara
mbili, alikuwa darasa la nane.
Alikuwa ni mkimya na mndani,
ni kama kila wakati alikuwa mwenye mawazo.
Na alichukia kuona wengine wakipigana.
Nilimuona mara moja akiruka kati ya
mabinti wawili walipokuwa wakipigana
Na akajikuta akidondoka na kuanguka chini.
Patrick alikuwa na tatizo moja.
Hakuwa akifika shuleni.
Alisema kuwa shule wakati mwingine humfanya kuwa na msongo
Sababu wanafunzi hupigana mara zote na
walimu wanaondoka.
Lakini pia, mama yake anafanya kazi mbili
na huwa anachoka kuweza kumfanya aje shule.
Hivyo nikafanya iwe kazi yangu
kumfanya awe anakuja shule.
Na sababu nilikuwa na wazimu na miaka 22
na mwenye bidii ya matumaini
Njia yangu ilikuwa ni
kwenda nyumbani kwao
na kusema "Eti, kwanini hauji
shuleni?"
Na njia hii ilifanya kazi,
akaanza kuja shuleni kila siku.
Na akaanza kufanikiwa katika darasa langu.
Aliandika mashairi,
alisoma vitabu.
Alikuja shuleni kila siku.
takriban muda ule ule
Nilipogundua namna ya kushirikiana
na Patrick,
Nilikwenda shule ya sheria Harvard.
Nilikutana tena na swali hili,
nijiweke wapi,
niuweke wapi mwili wangu?
Na nikawaza mwenyewe
Kuwa Mississipi Delta
ni mahali ambapo watu wenye fedha,
watu wenye fursa,
watu hao huondoka.
Na watu wanaobakia
ni watu ambao hawana fursa ya kuondoka.
Sikutaka kuwa mtu anayeondoka.
Nilitaka kuwa mtu anayebakia.
Kwa upande mwingine, nilikuwa mpweke
na mchovu.
Na hivyo nilijishawishi mwenyewe
kuwa ninaweza kufanya mabadiliko
Kwa kiasi kikubwa kama ningekuwa
na shahada yenye heshima ya sheria.
Hivyo nikaondoka.
Miaka mitatu baadaye,
Nilipokaribia kuhitimu
shule ya sheria,
rafiki yangu alinipigia simu
na kuniambia kuwa Patrick
amepigana na kuua mtu.
Nilitaharuki.
Sehemu ya mimi haikuamini,
na sehemu ya mimi pia iliamini kuwa
ni kweli.
Nilisafiri kwenda kumuona Patrick.
Nilimtembelea gerezani.
Na aliniambia kuwa ilikuwa kweli.
Ya kwamba ameua mtu.
Na asingependa kuzungumzia suala hilo.
Nilimuuliza nini kiliendelea kuhusu shule
na akasema aliacha shule mwaka mooja
baada ya mimi kuondoka.
Na alitaka kuniambia kuhusu kitu kingine
Alitazama chini akasema
ya kwamba amepata mtoto wa kike
ambaye ndiye kwanza amezaliwa.
Na anahisi kuwa amemuangusha binti yake.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mazungumzo yetu
yalikuwa ya haraka na mabaya.
Nilipotoka nje ya gereza,
sauti ndani yangu iliniambia,
"Rudi.
Usiporudi sasa, hutarudi kamwe".
Hivyo nikahitimu shule ya sheria na
nikarudi.
Nikarudi kumuona Patrick,
Nikarudi kuona kama ninaweza kumsaidia
na kesi yake ya sheria.
Muda huu,
nilipomuona kwa mara ya pili,
Nilidhani nina hili wazo zuri,
nikamwambia,
"Hey, Patrick, kwanini usiandike barua
kwa binti yako,
ili uweze kumuweka katika
fikra zako?"
Nikampatia kalamu na
kipande cha karatasi,
na akaanza kuandika.
Lakini nilipoiona karatasi aliyonipatia,
Nilipigwa na butwaa.
Sikuutambua mwandiko wake,
alikuwa amefanya makosa
machache ya matamshi.
na nikawaza mwenyewe kama mwalimu,
Ninafahamu ya kuwa mwanafunzi
anaweza kufanya vizuri kwa kasi
Kwa muda mfupi sana,
lakini sikuwahi kuwaza kuwa mwanafunzi
anaweza kurudi nyuma kwa kasi.
kilichoniumiza zaidi,
ni kuona kile alichokiandika
kwa binti yake.
aliandika,
"Ninasikitika kwa makosa yangu,
ninasikitika kutokuwa pamoja nawe."
Na hiki ndicho alichojisikia
anataka kusema naye.
Nikajiuliza ni namna gani ninaweza
kumshawishi kuwa anaweza kumwambia zaidi,
ile sehemu yake ambayo
hahitaji kuomba radhi kwayo.
Nilitaka yeye ajisikie
kuwa anakitu cha thamani
kumshirikisha binti yake.
Kwa kila siku kwa miezi saba iliyofuatia,
Nilimtembelea na kumpelekea vitabu.
Mkoba wangu uligeuka kuwa maktaba ndogo.
Nilimpelekea James Baldwin,
Nilipeleka Walt Whitman, C.S.Lewis.
Nilileta vitabu vya mwongozo wa miti,
wa ndege,
na kitabu alichotokea kukipenda zaidi,
kamusi.
Kwa baadhi ya siku,
tulikaa kimya kwa masaa,
wote wawili tukisoma.
Na siku nyingine,
tulisoma pamoja,
tulisoma mashairi.
tulianza kwa kusoma haikus,
mamia ya haikus,
ni kito rahisi na danganyifu.
Na ningemuuliza,
"Nishirikishe haiku zako unazozipenda".
Na baadhi yake ni za kufurahisha sana.
Kuna hii ya Issa:
"Usijali, buibui,
ninaweka nyumba kikawaida."
Na hii: "Nimelala nusu ya siku,
na hakuna aliyeniadhibu!"
Na hii nyingine ya kuvutia, inayohusu
siku ya kwanza barafu ilipodondoka,
"Kulungu wakilamba baridi ya kwanza
kutoka kwenye koti la kila mmoja wao."
Kuna kitu cha ajabu na cha kuvutia
kuhusu namna shairi linavyoonekana.
Nafasi ya shairi ni muhimu
kama maneno yenyewe.
Tunasoma shairi hili lililoandikwa na
W.S.Merwin,
ambalo aliliandika baada ya kumuona
mkewe akifanya kazi kwenye bustani
na akakumbuka kuwa wataishi maisha
yao yote yaliyobaki wakiwa pamoja.
"Wacha nifikiri kuwa tutakuja tena
tutakapotaka na itakuwa wakati wa masika
hatutakuwa na umri mkubwa
kuliko tulivyowahi kuwa
na majonzi yatakuwa mepesi kama
mawingu ya mapema
ambayo kwayo asubuhi
huja yenyewe taratibu"
Nikamuuliza Patrick mstari alioupenda
zaidi ni upi, na akasema
"Hatutakuwa na umri mkubwa
kuliko tulivyokuwa."
Alisema inamkumbusha
mahali ambapo muda husimama,
pale ambapo muda haumaanishi
kitu chochote.
Na nikamuuliza kama amewahi kuwa
na mahali pa jinsi hiyo.
pale ambapo muda hudumu milele.
Na akasema, "Mama yangu".
Na pale unaposoma shairi
pamoja na mtu mwingine,
shairi hubadilika katika maana.
Kwa sababu huwa la kibinafsi kwa mtu huyo,
huwa la kibinafsi kwako.
Halafu tulisoma vitabu,
tulisoma vitabu vingi sana,
tulisoma kumbukumbu za Frederick Douglass,
Mtumwa wa Marekani aliyejifunza mwenyewe
kusoma na kuandika
na aliyetoroka na kuwa huru
sababu ya kuelimika kwake.
Nimekua nikimfikiria Frederick Douglass
kama shujaa
na niliiona hii simulizi kama
iliyojaa matumaini na yenye kuinua
Lakini kitabu hiki kilimuweka Patrick
katika hofu.
Alibakia katika simulizi aliyoielezea
Douglass jinsi ambavyo, katika Christmas,
Mabwana waliwapa watumwa jini(pombe kali)
kama namna ya kuwaaminisha kuwa
hawawezi kuumudu uhuru.
Kwa sababu watumwa waliweweseka
katika mashamba.
Patrick alisema anajifananisha na hili.
Alisema kuwa kuna watu gerezani ambao,
kama watumwa,
hawataki kuwaza juu ya hali zao,
kwa sababu inawaumiza sana.
Inaumiza sana kuwaza mambo ya nyuma,
inaumiza sana kuwaza
kuhusu umbali gani tunapaswa kwenda.
Mstari alioupenda sana ulikuwa huu:
"Chochote kile, bila kujali chochote,
kujiondoa katika kuwaza!
Ilikuwa ni huku kuwaza kusiko koma kuhusu
hali yangu ndiko kunako kipa mateso."
Patrick alisema Douglass alikuwa jasiri
kuandika, ili aendelee kuwaza.
Lakini Patrick hakufahamu kuwa alionekana
kufanana sana na Douglass kwangu.
Namna alivyoendelea kusoma,
ijapokuwa ilimuweka katika hofu.
Alimaliza kitabu kabla yangu,
akisoma katika ngazi za
zege zisizo na taa.
Halafu tukaendelea kusoma mojawapo
ya vitabu ninavyovipenda,
Cha Marilynne Robinson's "Gilead,"
ambayo ni barua endelevu kutoka
kwa baba kwenda kwa mwanae.
Alipenda mstari huu:
"Ninaandika hii kwa sehemu kukuambia
ya kwamba kama umewahi kujiuliza
kile umekifanya katika maisha yako...
umekuwa neema ya Mungu kwangu,
muujiza, kitu ambacho ni zaidi
ya muujiza."
Kitu kimoja kuhusu hii lugha,
upendo wake, subira yake, sauti yake,
iliamsha shauku ya Patrick katika kuandika.
Na alijaza daftari kwa daftari
na barua kwenda kwa binti yake.
katika barua hizi nzuri na imara,
alijiwazia yeye na binti yake
wakipanda mtumbwi katika mto Mississipi
Alijiwazia yeye na binti yake
wakipata vijito vya milimani
vikiwa na maji masafi bila kasoro.
Nilipomtazama Patrick akiandika,
Nilijiwazia mwenyewe,
na sasa ninawaulizeni nyote,
ni wangapi wenu mmewahi kuandika barua
kwa mtu unayehisi umemwangusha?
Ni rahisi sana
kuwaweka hao watu nje ya fikra zako.
Lakini Patrick alijitokeza kila siku,
akimkabili binti yake,
akijiwajibisha kwake,
neno kwa neno kwa umakini wa hali ya juu.
Ningependa katika maisha yangu binafsi
kujiweka katika hatari kwa namna hiyo.
Kwa sababu hatari hiyo inadhihirisha
nguvu za moyo wa mtu.
Ngoja nirudi hatua moja nyuma na niulize
swali ambalo linaleta wasiwasi.
Mimi ni nani kusimulia simulizi hii,
hii simulizi ya Patrick?
Patrick ndiye aliyeishi kwenye
maumivu haya
na mimi sijawahi kukaa na njaa hata
kwa siku moja kwenye maisha yangu
Ninawaza sana kuhusu swali hili,
lakini ninachotaka kusema ni kuwa hii
simulizi sio tu kuhusu Patrick.
Inatuhusu sisi,
ni kuhusu tofauti kati yetu.
Ulimwengu wa vingi
ambao Patrick na wazazi wake
na mababu zake
hawajawahi kuuona.
Katika simulizi hii, mimi ninawakilisha
huo ulimwengu wa vingi.
Na katika kueleza simulizi hii
sikutaka kujificha mwenyewe.
Kuficha nguvu ambazo ninazo.
Katika kueleza simulizi hii,
ninataka kuifichua nguvu hiyo
halafu kuuliza,
tunawezaje kuipunguza
umbali kati yetu?
Kusoma ni njia mojawapo ya kuipunguza
hiyo nafasi.
Kunatuma ulimwengu wa ukimya
ambao tunaweza kuushiriki pamoja,
ambao tunaweza kuushiriki kwa usawa.
Inawezekana unajiuliza sasa kuwa
ni nini kilitokea kwa Patrick.
Je kusoma kuliokoa maisha yake?
Kuliyaokoa na hakukuyaokoa.
Patrick alipotoka gerezani,
safari yake ilikuwa ya maumivu.
Waajiri hawakumkubali kwa sababu
ya historia yake,
rafiki yake mpenzi, mama yake,
alifariki katika umri wa miaka 43
kwa ugonjwa wa moyo na kisukari.
Alikuwa hana pa kuishi,
amekuwa hana chakula.
Kwa hiyo watu wanasema mengi kuhusu kusoma
ambayo kwangu ninahisi wanazidisha chumvi.
Uwezo wa kusoma haukumzuia yeye
asitengwe na jamii.
Hakukumzuia mama yake asifariki.
Kwa hiyo kusoma kunaweza kufanya nini?
Nina majibu machache ninapomalizia leo.
Kusoma kulibadili utu wake wa ndani
kwa mambo yaliyofichika na uwezo wa
kuwaza kwa picha.
kwa uzuri.
Kusoma kulimpa taswira zilizompa furaha:
milima, bahari, kulungu, theluji.
Maneno yenye ladha ya ulimwengu huru
na halisi.
Kusoma kulimpa lugha kwa yale aliyopoteza.
Ni jinsi gani yalivyo mazuri haya maneno
kutoka kwa mshairi Derek Walcott?
Patrick alilikariri hili shairi.
"Siku ambazo nilizishikilia,
siku ambazo nilizipoteza,
siku ambazo zinakuwa kupitiliza,
kama mabinti,
mikono yangu inayoshikilia."
Kusoma kulimfundisha ujasiri wake
mwenyewe.
Kumbuka kwamba aliendelea kusoma
Frederick Douglass,
ijapokuwa ilikuwa ya kuumiza.
Aliendelea kuwa makini,
ijapokuwa kuwa makini kunauma.
Kusoma ni aina ya kutafakari,
ndio maana ni vigumu sana kusoma
kwa sababu tunataka kutafakari.
Na Patrick alichagua kutafakari,
badala ya kutokutafakari.
Na mwishoni, kusoma kulimpa lugha
ya kuongea na binti yake.
Kusoma kulimpa shauku ya kutaka kuandika.
Muunganiko kati ya kusoma na
kuandika ni wenye nguvu sana.
Tunapoanza kusoma,
tunaanza kupata maneno.
Na alipata maneno ya kutafakari
wao wawili wakiwa pamoja.
Alipata maneno
ya kumwelezea ni namna gani anampenda.
Kusoma pia kulibadilisha
mahusiano baina yetu.
Kunatupa nyakati za kuwa karibu,
kuweza kuona zaidi ya mitazamo yetu.
Na kusoma kulichukua mahusiano ya
kutokuwa sawa
na kulitupa usawa wa muda mfupi.
Ukikutana na mtu kama msomaji,
unakutana naye kwa mara ya kwanza,
kwa upya kabisa.
Hakuna namna unaweza kufahamu mstari
anaoupenda sana ni upi.
Ni kumbukumbu zipi na huzuni zipi za
siri alizonazo.
Na unakutana na sitara ya hali ya juu
ya utu wake wa ndani.
Na halafu unaanza kushangaa,
"Eti,utu wangu wa ndani umejengwa na nini?
Ni kitu gani nilichonacho cha thamani
cha kumshirikisha mwingine?"
Ninataka kufunga
kwa mistari yangu ninayoipenda
kutoka kwa barua za Patrick kwa bintiye.
"Mto una kivuli kwenye baadhi ya maeneo
lakini mwanga unaangaza
kupitia mianya ya miti...
Kwenye baadhi ya matawi
muliberi nyingi zimening'inia.
Unanyoosha mkono wako
ili uweze kuyachukua baadhi".
Na barua hii ya upendo, anapoandika,
"Fumba macho yako na usikilize
sauti ya maneno.
Ninafahamu shairi hili kwa moyo
na ningependa pia wewe ulifahamu."
Ninawashukuruni nyote.
(Makofi)