WEBVTT 00:00:00.917 --> 00:00:06.393 Ninataka kuzungumza namna kusoma kunavyoweza kubadilisha maisha yetu 00:00:06.417 --> 00:00:08.792 na kuhusu mipaka ya mabadiliko hayo 00:00:09.750 --> 00:00:14.018 Ninataka kuzungumza na wewe namna kusoma kunavyoweza kutupa ulimwengu wa ushirika 00:00:14.042 --> 00:00:16.750 wa muunganiko wenye nguvu wa kibinadamu 00:00:17.833 --> 00:00:21.393 pia namna ambavyo muunganiko huo ni sehemu tu mara zote 00:00:21.417 --> 00:00:26.500 Kusoma mwisho wa siku ni kitendo cha upweke na kisicho cha kawaida. NOTE Paragraph 00:00:27.625 --> 00:00:30.476 Muandishi aliyebadilisha maisha yangu 00:00:30.500 --> 00:00:34.934 Ni mmarekani mweusi na mwandishi wa riwaya James Baldwin 00:00:34.958 --> 00:00:38.226 Wakati ninakuwa katika eneo la Magharibi mwa Michigan miaka ya 1980, 00:00:38.250 --> 00:00:42.167 hakukuwa na wamarekani wenye asili ya asia wengi wanaoandika kuhusu mabadiliko ya kijamii 00:00:43.292 --> 00:00:46.518 Na ndio maana nilimgeukia James Baldwin 00:00:46.542 --> 00:00:50.583 kama namna ya kuliziba hili ombwe, kama namna ya kuwamakini na rangi 00:00:51.958 --> 00:00:55.934 lakini haswa kwa sababu nilifahamu mimi sikuwa mmarekani mweusi, 00:00:55.958 --> 00:01:00.476 Pia nilisikia kupata changamoto na kuthibitishwa na maneno yake. 00:01:00.500 --> 00:01:02.625 Hasusani maneno haya: 00:01:03.458 --> 00:01:07.059 "Ni watu huria walio na mitazamo sahihi, 00:01:07.083 --> 00:01:09.042 lakini hawana misimamo halisi. 00:01:10.083 --> 00:01:14.018 pale ambapo vipande vipo chini na unawategemea kuleta matokeo, 00:01:14.042 --> 00:01:16.518 na huenda hawako hapo kwa namna fulani". 00:01:16.542 --> 00:01:19.351 Hawako hapo kwa namna fulani. 00:01:19.375 --> 00:01:21.726 Nikayachukua hayo maneno nikitafakari. 00:01:21.750 --> 00:01:23.458 Nijiweke wapi? NOTE Paragraph 00:01:24.500 --> 00:01:26.518 Nilikwenda kwenye delta ya Mississippi, 00:01:26.542 --> 00:01:29.684 mojawapo ya maeneo masikini sana ya Marekani. 00:01:29.708 --> 00:01:32.601 Hii ni sehemu ambayo imejengwa na historia yenye nguvu. 00:01:32.625 --> 00:01:37.768 Katika mwaka wa 1960, Wamarekani weusi walijitoa maisha yao kupigania Elimu, 00:01:37.792 --> 00:01:39.500 kupigania haki ya kupiga kura. 00:01:40.625 --> 00:01:43.059 Nilitaka kuwa sehemu ya badiliko hilo, 00:01:43.083 --> 00:01:46.792 kuwasaidia vijana wadogo wamalize shule na kujiunga na vyuo. 00:01:48.250 --> 00:01:50.976 Nilipoenda kwenye Delta ya Mississipi, 00:01:51.000 --> 00:01:53.434 Palikuwa ni mahali duni bado, 00:01:53.458 --> 00:01:55.184 bado pametengwa, 00:01:55.208 --> 00:01:57.750 Bado panahitaji mabadiliko ya kasi. NOTE Paragraph 00:01:58.958 --> 00:02:02.393 Shule yangu, pale nilipokuwa nasoma, 00:02:02.417 --> 00:02:06.726 haikuwa na maktaba, hakuna mshauri, 00:02:06.750 --> 00:02:09.726 lakini ilikuwa na afisa wa polisi. 00:02:09.750 --> 00:02:12.309 Nusu ya walimu walikuwa ni mbadala 00:02:12.333 --> 00:02:14.309 na wanafunzi walipoingia kwenye ugomvi, 00:02:14.333 --> 00:02:18.208 Shule iliwapeleka kwenye jela ya mahali hapo. NOTE Paragraph 00:02:20.250 --> 00:02:23.226 Hii ndiyo shule nilipokutana na Patrick. 00:02:23.250 --> 00:02:28.184 Alikuwa na miaka 15 na alikamatwa mara mbili, alikuwa darasa la nane. 00:02:28.208 --> 00:02:30.684 Alikuwa ni mkimya na mndani, 00:02:30.708 --> 00:02:33.518 ni kama kila wakati alikuwa mwenye mawazo. 00:02:33.542 --> 00:02:36.333 Na alichukia kuona wengine wakipigana. 00:02:37.500 --> 00:02:41.309 Nilimuona mara moja akiruka kati ya mabinti wawili walipokuwa wakipigana 00:02:41.333 --> 00:02:44.042 Na akajikuta akidondoka na kuanguka chini. 00:02:45.375 --> 00:02:47.893 Patrick alikuwa na tatizo moja. 00:02:47.917 --> 00:02:49.708 Hakuwa akifika shuleni. 00:02:51.249 --> 00:02:53.726 Alisema kuwa shule wakati mwingine humfanya kuwa na msongo 00:02:53.750 --> 00:02:56.792 Sababu wanafunzi hupigana mara zote na walimu wanaondoka. 00:02:58.042 --> 00:03:03.500 Lakini pia, mama yake anafanya kazi mbili na huwa anachoka kuweza kumfanya aje shule. 00:03:04.417 --> 00:03:07.184 Hivyo nikafanya iwe kazi yangu kumfanya awe anakuja shule. 00:03:07.208 --> 00:03:11.268 Na sababu nilikuwa na wazimu na miaka 22 na mwenye bidii ya matumaini 00:03:11.292 --> 00:03:13.434 Njia yangu ilikuwa ni kwenda nyumbani kwao 00:03:13.458 --> 00:03:15.583 na kusema "Eti, kwanini hauji shuleni?" 00:03:16.542 --> 00:03:18.184 Na njia hii ilifanya kazi, 00:03:18.208 --> 00:03:20.643 akaanza kuja shuleni kila siku. 00:03:20.667 --> 00:03:23.059 Na akaanza kufanikiwa katika darasa langu. 00:03:23.083 --> 00:03:26.000 Aliandika mashairi, alisoma vitabu. 00:03:26.917 --> 00:03:29.208 Alikuja shuleni kila siku. NOTE Paragraph 00:03:31.042 --> 00:03:32.518 takriban muda ule ule 00:03:32.542 --> 00:03:35.226 Nilipogundua namna ya kushirikiana na Patrick, 00:03:35.250 --> 00:03:37.458 Nilikwenda shule ya sheria Harvard. 00:03:39.583 --> 00:03:42.934 Nilikutana tena na swali hili, nijiweke wapi, 00:03:42.958 --> 00:03:44.667 niuweke wapi mwili wangu? 00:03:45.458 --> 00:03:48.101 Na nikawaza mwenyewe 00:03:48.125 --> 00:03:51.643 Kuwa Mississipi Delta ni mahali ambapo watu wenye fedha, 00:03:51.667 --> 00:03:53.559 watu wenye fursa, 00:03:53.583 --> 00:03:54.833 watu hao huondoka. 00:03:55.875 --> 00:03:57.309 Na watu wanaobakia 00:03:57.333 --> 00:03:59.833 ni watu ambao hawana fursa ya kuondoka. 00:04:00.833 --> 00:04:03.101 Sikutaka kuwa mtu anayeondoka. 00:04:03.125 --> 00:04:05.167 Nilitaka kuwa mtu anayebakia. 00:04:06.333 --> 00:04:09.268 Kwa upande mwingine, nilikuwa mpweke na mchovu. 00:04:09.292 --> 00:04:12.750 Na hivyo nilijishawishi mwenyewe kuwa ninaweza kufanya mabadiliko 00:04:14.125 --> 00:04:17.708 Kwa kiasi kikubwa kama ningekuwa na shahada yenye heshima ya sheria. 00:04:19.541 --> 00:04:20.791 Hivyo nikaondoka. NOTE Paragraph 00:04:22.750 --> 00:04:24.351 Miaka mitatu baadaye, 00:04:24.375 --> 00:04:26.768 Nilipokaribia kuhitimu shule ya sheria, 00:04:26.792 --> 00:04:28.518 rafiki yangu alinipigia simu 00:04:28.542 --> 00:04:33.458 na kuniambia kuwa Patrick amepigana na kuua mtu. 00:04:35.333 --> 00:04:37.393 Nilitaharuki. 00:04:37.417 --> 00:04:39.851 Sehemu ya mimi haikuamini, 00:04:39.875 --> 00:04:42.542 na sehemu ya mimi pia iliamini kuwa ni kweli. 00:04:43.583 --> 00:04:45.583 Nilisafiri kwenda kumuona Patrick. 00:04:46.750 --> 00:04:49.458 Nilimtembelea gerezani. 00:04:50.542 --> 00:04:54.184 Na aliniambia kuwa ilikuwa kweli. 00:04:54.208 --> 00:04:56.601 Ya kwamba ameua mtu. 00:04:56.625 --> 00:04:58.875 Na asingependa kuzungumzia suala hilo. 00:04:59.833 --> 00:05:01.851 Nilimuuliza nini kiliendelea kuhusu shule 00:05:01.875 --> 00:05:06.018 na akasema aliacha shule mwaka mooja baada ya mimi kuondoka. 00:05:06.042 --> 00:05:08.684 Na alitaka kuniambia kuhusu kitu kingine 00:05:08.708 --> 00:05:11.976 Alitazama chini akasema ya kwamba amepata mtoto wa kike 00:05:12.000 --> 00:05:13.768 ambaye ndiye kwanza amezaliwa. 00:05:13.792 --> 00:05:16.375 Na anahisi kuwa amemuangusha binti yake. 00:05:18.625 --> 00:05:22.000 Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mazungumzo yetu yalikuwa ya haraka na mabaya. NOTE Paragraph 00:05:23.417 --> 00:05:28.476 Nilipotoka nje ya gereza, sauti ndani yangu iliniambia, 00:05:28.500 --> 00:05:29.768 "Rudi. 00:05:29.792 --> 00:05:33.083 Usiporudi sasa, hutarudi kamwe". 00:05:36.292 --> 00:05:39.875 Hivyo nikahitimu shule ya sheria na nikarudi. 00:05:40.833 --> 00:05:42.518 Nikarudi kumuona Patrick, 00:05:42.542 --> 00:05:45.500 Nikarudi kuona kama ninaweza kumsaidia na kesi yake ya sheria. 00:05:46.917 --> 00:05:50.268 Muda huu, nilipomuona kwa mara ya pili, 00:05:50.292 --> 00:05:52.559 Nilidhani nina hili wazo zuri, nikamwambia, 00:05:52.583 --> 00:05:56.184 "Hey, Patrick, kwanini usiandike barua kwa binti yako, 00:05:56.208 --> 00:05:59.976 ili uweze kumuweka katika fikra zako?" 00:06:00.000 --> 00:06:03.684 Nikampatia kalamu na kipande cha karatasi, 00:06:03.708 --> 00:06:05.333 na akaanza kuandika. NOTE Paragraph 00:06:06.542 --> 00:06:09.351 Lakini nilipoiona karatasi aliyonipatia, 00:06:09.375 --> 00:06:10.708 Nilipigwa na butwaa. 00:06:13.000 --> 00:06:15.101 Sikuutambua mwandiko wake, 00:06:15.125 --> 00:06:17.958 alikuwa amefanya makosa machache ya matamshi. 00:06:19.167 --> 00:06:21.851 na nikawaza mwenyewe kama mwalimu, 00:06:21.875 --> 00:06:25.351 Ninafahamu ya kuwa mwanafunzi anaweza kufanya vizuri kwa kasi 00:06:25.375 --> 00:06:28.434 Kwa muda mfupi sana, 00:06:28.458 --> 00:06:32.125 lakini sikuwahi kuwaza kuwa mwanafunzi anaweza kurudi nyuma kwa kasi. 00:06:34.375 --> 00:06:36.268 kilichoniumiza zaidi, 00:06:36.292 --> 00:06:39.476 ni kuona kile alichokiandika kwa binti yake. 00:06:39.500 --> 00:06:40.893 aliandika, 00:06:40.917 --> 00:06:45.208 "Ninasikitika kwa makosa yangu, ninasikitika kutokuwa pamoja nawe." 00:06:46.458 --> 00:06:49.292 Na hiki ndicho alichojisikia anataka kusema naye. 00:06:50.250 --> 00:06:54.559 Nikajiuliza ni namna gani ninaweza kumshawishi kuwa anaweza kumwambia zaidi, 00:06:54.583 --> 00:06:58.000 ile sehemu yake ambayo hahitaji kuomba radhi kwayo. 00:06:58.958 --> 00:07:00.226 Nilitaka yeye ajisikie 00:07:00.250 --> 00:07:04.208 kuwa anakitu cha thamani kumshirikisha binti yake. NOTE Paragraph 00:07:05.917 --> 00:07:09.101 Kwa kila siku kwa miezi saba iliyofuatia, 00:07:09.125 --> 00:07:11.809 Nilimtembelea na kumpelekea vitabu. 00:07:11.833 --> 00:07:15.684 Mkoba wangu uligeuka kuwa maktaba ndogo. 00:07:15.708 --> 00:07:17.768 Nilimpelekea James Baldwin, 00:07:17.792 --> 00:07:22.684 Nilipeleka Walt Whitman, C.S.Lewis. 00:07:22.708 --> 00:07:27.518 Nilileta vitabu vya mwongozo wa miti, wa ndege, 00:07:27.542 --> 00:07:30.750 na kitabu alichotokea kukipenda zaidi, kamusi. 00:07:31.667 --> 00:07:33.351 Kwa baadhi ya siku, 00:07:33.375 --> 00:07:37.167 tulikaa kimya kwa masaa, wote wawili tukisoma. 00:07:38.083 --> 00:07:39.934 Na siku nyingine, 00:07:39.958 --> 00:07:43.476 tulisoma pamoja, tulisoma mashairi. NOTE Paragraph 00:07:43.500 --> 00:07:47.393 tulianza kwa kusoma haikus, mamia ya haikus, 00:07:47.417 --> 00:07:50.309 ni kito rahisi na danganyifu. 00:07:50.333 --> 00:07:53.143 Na ningemuuliza, "Nishirikishe haiku zako unazozipenda". 00:07:53.167 --> 00:07:56.226 Na baadhi yake ni za kufurahisha sana. 00:07:56.250 --> 00:07:58.101 Kuna hii ya Issa: 00:07:58.125 --> 00:08:01.833 "Usijali, buibui, ninaweka nyumba kikawaida." 00:08:02.750 --> 00:08:07.292 Na hii: "Nimelala nusu ya siku, na hakuna aliyeniadhibu!" 00:08:08.667 --> 00:08:13.101 Na hii nyingine ya kuvutia, inayohusu siku ya kwanza barafu ilipodondoka, 00:08:13.125 --> 00:08:17.583 "Kulungu wakilamba baridi ya kwanza kutoka kwenye koti la kila mmoja wao." 00:08:19.250 --> 00:08:22.268 Kuna kitu cha ajabu na cha kuvutia 00:08:22.292 --> 00:08:24.934 kuhusu namna shairi linavyoonekana. 00:08:24.958 --> 00:08:29.583 Nafasi ya shairi ni muhimu kama maneno yenyewe. NOTE Paragraph 00:08:31.375 --> 00:08:33.893 Tunasoma shairi hili lililoandikwa na W.S.Merwin, 00:08:33.917 --> 00:08:38.143 ambalo aliliandika baada ya kumuona mkewe akifanya kazi kwenye bustani 00:08:38.167 --> 00:08:42.042 na akakumbuka kuwa wataishi maisha yao yote yaliyobaki wakiwa pamoja. 00:08:43.167 --> 00:08:45.518 "Wacha nifikiri kuwa tutakuja tena 00:08:45.542 --> 00:08:48.934 tutakapotaka na itakuwa wakati wa masika 00:08:48.958 --> 00:08:52.143 hatutakuwa na umri mkubwa kuliko tulivyowahi kuwa 00:08:52.167 --> 00:08:56.101 na majonzi yatakuwa mepesi kama mawingu ya mapema 00:08:56.125 --> 00:08:59.893 ambayo kwayo asubuhi huja yenyewe taratibu" 00:08:59.917 --> 00:09:03.309 Nikamuuliza Patrick mstari alioupenda zaidi ni upi, na akasema 00:09:03.333 --> 00:09:06.875 "Hatutakuwa na umri mkubwa kuliko tulivyokuwa." 00:09:08.375 --> 00:09:12.809 Alisema inamkumbusha mahali ambapo muda husimama, 00:09:12.833 --> 00:09:15.768 pale ambapo muda haumaanishi kitu chochote. 00:09:15.792 --> 00:09:17.851 Na nikamuuliza kama amewahi kuwa na mahali pa jinsi hiyo. 00:09:17.875 --> 00:09:20.268 pale ambapo muda hudumu milele. 00:09:20.292 --> 00:09:21.958 Na akasema, "Mama yangu". 00:09:23.875 --> 00:09:28.184 Na pale unaposoma shairi pamoja na mtu mwingine, 00:09:28.208 --> 00:09:30.083 shairi hubadilika katika maana. 00:09:31.333 --> 00:09:36.000 Kwa sababu huwa la kibinafsi kwa mtu huyo, huwa la kibinafsi kwako. NOTE Paragraph 00:09:37.500 --> 00:09:40.184 Halafu tulisoma vitabu, tulisoma vitabu vingi sana, 00:09:40.208 --> 00:09:43.351 tulisoma kumbukumbu za Frederick Douglass, 00:09:43.375 --> 00:09:46.976 Mtumwa wa Marekani aliyejifunza mwenyewe kusoma na kuandika 00:09:47.000 --> 00:09:50.333 na aliyetoroka na kuwa huru sababu ya kuelimika kwake. 00:09:51.875 --> 00:09:54.518 Nimekua nikimfikiria Frederick Douglass kama shujaa 00:09:54.542 --> 00:09:57.750 na niliiona hii simulizi kama iliyojaa matumaini na yenye kuinua 00:09:58.917 --> 00:10:01.750 Lakini kitabu hiki kilimuweka Patrick katika hofu. 00:10:02.875 --> 00:10:07.934 Alibakia katika simulizi aliyoielezea Douglass jinsi ambavyo, katika Christmas, 00:10:07.958 --> 00:10:11.059 Mabwana waliwapa watumwa jini(pombe kali) 00:10:11.083 --> 00:10:14.559 kama namna ya kuwaaminisha kuwa hawawezi kuumudu uhuru. 00:10:14.583 --> 00:10:17.375 Kwa sababu watumwa waliweweseka katika mashamba. 00:10:19.500 --> 00:10:21.500 Patrick alisema anajifananisha na hili. 00:10:22.333 --> 00:10:25.809 Alisema kuwa kuna watu gerezani ambao, kama watumwa, 00:10:25.833 --> 00:10:28.059 hawataki kuwaza juu ya hali zao, 00:10:28.083 --> 00:10:29.893 kwa sababu inawaumiza sana. 00:10:29.917 --> 00:10:32.101 Inaumiza sana kuwaza mambo ya nyuma, 00:10:32.125 --> 00:10:35.458 inaumiza sana kuwaza kuhusu umbali gani tunapaswa kwenda. NOTE Paragraph 00:10:36.958 --> 00:10:39.851 Mstari alioupenda sana ulikuwa huu: 00:10:39.875 --> 00:10:43.476 "Chochote kile, bila kujali chochote, kujiondoa katika kuwaza! 00:10:43.500 --> 00:10:48.542 Ilikuwa ni huku kuwaza kusiko koma kuhusu hali yangu ndiko kunako kipa mateso." 00:10:49.958 --> 00:10:53.917 Patrick alisema Douglass alikuwa jasiri kuandika, ili aendelee kuwaza. 00:10:55.083 --> 00:11:00.643 Lakini Patrick hakufahamu kuwa alionekana kufanana sana na Douglass kwangu. 00:11:00.667 --> 00:11:04.417 Namna alivyoendelea kusoma, ijapokuwa ilimuweka katika hofu. 00:11:05.250 --> 00:11:08.309 Alimaliza kitabu kabla yangu, 00:11:08.333 --> 00:11:12.042 akisoma katika ngazi za zege zisizo na taa. NOTE Paragraph 00:11:13.583 --> 00:11:16.309 Halafu tukaendelea kusoma mojawapo ya vitabu ninavyovipenda, 00:11:16.333 --> 00:11:18.518 Cha Marilynne Robinson's "Gilead," 00:11:18.542 --> 00:11:22.684 ambayo ni barua endelevu kutoka kwa baba kwenda kwa mwanae. 00:11:22.708 --> 00:11:25.059 Alipenda mstari huu: 00:11:25.083 --> 00:11:27.268 "Ninaandika hii kwa sehemu kukuambia 00:11:27.292 --> 00:11:30.601 ya kwamba kama umewahi kujiuliza kile umekifanya katika maisha yako... 00:11:30.625 --> 00:11:32.643 umekuwa neema ya Mungu kwangu, 00:11:32.667 --> 00:11:35.833 muujiza, kitu ambacho ni zaidi ya muujiza." NOTE Paragraph 00:11:37.375 --> 00:11:43.018 Kitu kimoja kuhusu hii lugha, upendo wake, subira yake, sauti yake, 00:11:43.042 --> 00:11:45.500 iliamsha shauku ya Patrick katika kuandika. 00:11:46.292 --> 00:11:49.393 Na alijaza daftari kwa daftari 00:11:49.417 --> 00:11:52.726 na barua kwenda kwa binti yake. 00:11:52.750 --> 00:11:55.684 katika barua hizi nzuri na imara, 00:11:55.708 --> 00:12:01.684 alijiwazia yeye na binti yake wakipanda mtumbwi katika mto Mississipi 00:12:01.708 --> 00:12:04.518 Alijiwazia yeye na binti yake wakipata vijito vya milimani 00:12:04.542 --> 00:12:06.708 vikiwa na maji masafi bila kasoro. 00:12:08.042 --> 00:12:10.083 Nilipomtazama Patrick akiandika, 00:12:11.250 --> 00:12:13.393 Nilijiwazia mwenyewe, 00:12:13.417 --> 00:12:15.476 na sasa ninawaulizeni nyote, 00:12:15.500 --> 00:12:20.792 ni wangapi wenu mmewahi kuandika barua kwa mtu unayehisi umemwangusha? 00:12:22.042 --> 00:12:27.125 Ni rahisi sana kuwaweka hao watu nje ya fikra zako. 00:12:28.083 --> 00:12:32.726 Lakini Patrick alijitokeza kila siku, akimkabili binti yake, 00:12:32.750 --> 00:12:35.684 akijiwajibisha kwake, 00:12:35.708 --> 00:12:39.417 neno kwa neno kwa umakini wa hali ya juu. NOTE Paragraph 00:12:42.417 --> 00:12:44.958 Ningependa katika maisha yangu binafsi 00:12:46.042 --> 00:12:49.101 kujiweka katika hatari kwa namna hiyo. 00:12:49.125 --> 00:12:52.750 Kwa sababu hatari hiyo inadhihirisha nguvu za moyo wa mtu. 00:12:56.625 --> 00:13:00.684 Ngoja nirudi hatua moja nyuma na niulize swali ambalo linaleta wasiwasi. 00:13:00.708 --> 00:13:04.417 Mimi ni nani kusimulia simulizi hii, hii simulizi ya Patrick? 00:13:06.042 --> 00:13:09.018 Patrick ndiye aliyeishi kwenye maumivu haya 00:13:09.042 --> 00:13:13.208 na mimi sijawahi kukaa na njaa hata kwa siku moja kwenye maisha yangu 00:13:15.250 --> 00:13:17.018 Ninawaza sana kuhusu swali hili, 00:13:17.042 --> 00:13:20.768 lakini ninachotaka kusema ni kuwa hii simulizi sio tu kuhusu Patrick. 00:13:20.792 --> 00:13:22.309 Inatuhusu sisi, 00:13:22.333 --> 00:13:24.833 ni kuhusu tofauti kati yetu. 00:13:25.667 --> 00:13:27.083 Ulimwengu wa vingi 00:13:28.375 --> 00:13:32.018 ambao Patrick na wazazi wake na mababu zake 00:13:32.042 --> 00:13:33.851 hawajawahi kuuona. 00:13:33.875 --> 00:13:36.958 Katika simulizi hii, mimi ninawakilisha huo ulimwengu wa vingi. 00:13:37.792 --> 00:13:41.601 Na katika kueleza simulizi hii sikutaka kujificha mwenyewe. 00:13:41.625 --> 00:13:44.292 Kuficha nguvu ambazo ninazo. NOTE Paragraph 00:13:45.333 --> 00:13:48.893 Katika kueleza simulizi hii, ninataka kuifichua nguvu hiyo 00:13:48.917 --> 00:13:51.309 halafu kuuliza, 00:13:51.333 --> 00:13:54.250 tunawezaje kuipunguza umbali kati yetu? 00:13:56.250 --> 00:13:59.851 Kusoma ni njia mojawapo ya kuipunguza hiyo nafasi. 00:13:59.875 --> 00:14:04.309 Kunatuma ulimwengu wa ukimya ambao tunaweza kuushiriki pamoja, 00:14:04.333 --> 00:14:06.583 ambao tunaweza kuushiriki kwa usawa. NOTE Paragraph 00:14:08.500 --> 00:14:11.601 Inawezekana unajiuliza sasa kuwa ni nini kilitokea kwa Patrick. 00:14:11.625 --> 00:14:13.333 Je kusoma kuliokoa maisha yake? 00:14:14.583 --> 00:14:16.708 Kuliyaokoa na hakukuyaokoa. 00:14:17.875 --> 00:14:20.768 Patrick alipotoka gerezani, 00:14:20.792 --> 00:14:23.125 safari yake ilikuwa ya maumivu. 00:14:24.292 --> 00:14:27.768 Waajiri hawakumkubali kwa sababu ya historia yake, 00:14:27.792 --> 00:14:30.934 rafiki yake mpenzi, mama yake, alifariki katika umri wa miaka 43 00:14:30.958 --> 00:14:33.434 kwa ugonjwa wa moyo na kisukari. 00:14:33.458 --> 00:14:36.167 Alikuwa hana pa kuishi, amekuwa hana chakula. NOTE Paragraph 00:14:38.250 --> 00:14:42.792 Kwa hiyo watu wanasema mengi kuhusu kusoma ambayo kwangu ninahisi wanazidisha chumvi. 00:14:43.792 --> 00:14:47.768 Uwezo wa kusoma haukumzuia yeye asitengwe na jamii. 00:14:47.792 --> 00:14:50.417 Hakukumzuia mama yake asifariki. 00:14:51.708 --> 00:14:54.083 Kwa hiyo kusoma kunaweza kufanya nini? 00:14:55.375 --> 00:14:59.333 Nina majibu machache ninapomalizia leo. NOTE Paragraph 00:15:00.667 --> 00:15:03.417 Kusoma kulibadili utu wake wa ndani 00:15:05.083 --> 00:15:08.143 kwa mambo yaliyofichika na uwezo wa kuwaza kwa picha. 00:15:08.167 --> 00:15:09.417 kwa uzuri. 00:15:10.292 --> 00:15:14.625 Kusoma kulimpa taswira zilizompa furaha: 00:15:15.417 --> 00:15:20.976 milima, bahari, kulungu, theluji. 00:15:21.000 --> 00:15:25.125 Maneno yenye ladha ya ulimwengu huru na halisi. 00:15:27.625 --> 00:15:31.143 Kusoma kulimpa lugha kwa yale aliyopoteza. 00:15:31.167 --> 00:15:35.809 Ni jinsi gani yalivyo mazuri haya maneno kutoka kwa mshairi Derek Walcott? 00:15:35.833 --> 00:15:38.059 Patrick alilikariri hili shairi. 00:15:38.083 --> 00:15:40.184 "Siku ambazo nilizishikilia, 00:15:40.208 --> 00:15:42.476 siku ambazo nilizipoteza, 00:15:42.500 --> 00:15:45.726 siku ambazo zinakuwa kupitiliza, kama mabinti, 00:15:45.750 --> 00:15:47.583 mikono yangu inayoshikilia." NOTE Paragraph 00:15:48.667 --> 00:15:51.643 Kusoma kulimfundisha ujasiri wake mwenyewe. 00:15:51.667 --> 00:15:54.976 Kumbuka kwamba aliendelea kusoma Frederick Douglass, 00:15:55.000 --> 00:15:57.143 ijapokuwa ilikuwa ya kuumiza. 00:15:57.167 --> 00:16:00.875 Aliendelea kuwa makini, ijapokuwa kuwa makini kunauma. 00:16:02.208 --> 00:16:04.768 Kusoma ni aina ya kutafakari, 00:16:04.792 --> 00:16:08.851 ndio maana ni vigumu sana kusoma kwa sababu tunataka kutafakari. 00:16:08.875 --> 00:16:13.125 Na Patrick alichagua kutafakari, badala ya kutokutafakari. 00:16:16.000 --> 00:16:19.958 Na mwishoni, kusoma kulimpa lugha ya kuongea na binti yake. 00:16:21.375 --> 00:16:24.601 Kusoma kulimpa shauku ya kutaka kuandika. 00:16:24.625 --> 00:16:28.768 Muunganiko kati ya kusoma na kuandika ni wenye nguvu sana. 00:16:28.792 --> 00:16:30.851 Tunapoanza kusoma, 00:16:30.875 --> 00:16:32.958 tunaanza kupata maneno. 00:16:33.958 --> 00:16:38.601 Na alipata maneno ya kutafakari wao wawili wakiwa pamoja. 00:16:38.625 --> 00:16:40.333 Alipata maneno 00:16:41.958 --> 00:16:44.208 ya kumwelezea ni namna gani anampenda. NOTE Paragraph 00:16:46.042 --> 00:16:49.976 Kusoma pia kulibadilisha mahusiano baina yetu. 00:16:50.000 --> 00:16:52.059 Kunatupa nyakati za kuwa karibu, 00:16:52.083 --> 00:16:54.976 kuweza kuona zaidi ya mitazamo yetu. 00:16:55.000 --> 00:16:57.684 Na kusoma kulichukua mahusiano ya kutokuwa sawa 00:16:57.708 --> 00:17:00.375 na kulitupa usawa wa muda mfupi. 00:17:02.125 --> 00:17:05.059 Ukikutana na mtu kama msomaji, 00:17:05.083 --> 00:17:07.059 unakutana naye kwa mara ya kwanza, 00:17:07.083 --> 00:17:08.791 kwa upya kabisa. 00:17:09.875 --> 00:17:13.083 Hakuna namna unaweza kufahamu mstari anaoupenda sana ni upi. 00:17:14.458 --> 00:17:17.666 Ni kumbukumbu zipi na huzuni zipi za siri alizonazo. 00:17:18.833 --> 00:17:22.833 Na unakutana na sitara ya hali ya juu ya utu wake wa ndani. 00:17:23.666 --> 00:17:27.101 Na halafu unaanza kushangaa, "Eti,utu wangu wa ndani umejengwa na nini? 00:17:27.125 --> 00:17:30.375 Ni kitu gani nilichonacho cha thamani cha kumshirikisha mwingine?" NOTE Paragraph 00:17:33.000 --> 00:17:34.333 Ninataka kufunga 00:17:36.208 --> 00:17:40.500 kwa mistari yangu ninayoipenda kutoka kwa barua za Patrick kwa bintiye. 00:17:41.333 --> 00:17:44.101 "Mto una kivuli kwenye baadhi ya maeneo 00:17:44.125 --> 00:17:47.393 lakini mwanga unaangaza kupitia mianya ya miti... 00:17:47.417 --> 00:17:50.976 Kwenye baadhi ya matawi muliberi nyingi zimening'inia. 00:17:51.000 --> 00:17:54.458 Unanyoosha mkono wako ili uweze kuyachukua baadhi". 00:17:56.042 --> 00:17:58.476 Na barua hii ya upendo, anapoandika, 00:17:58.500 --> 00:18:02.851 "Fumba macho yako na usikilize sauti ya maneno. 00:18:02.875 --> 00:18:05.059 Ninafahamu shairi hili kwa moyo 00:18:05.083 --> 00:18:07.917 na ningependa pia wewe ulifahamu." NOTE Paragraph 00:18:09.375 --> 00:18:11.184 Ninawashukuruni nyote. NOTE Paragraph 00:18:11.208 --> 00:18:14.500 (Makofi)