Mtandao wa utambuzi wa virusi katika kuzuia mlipuko mwingine wa magonjwa.
-
0:01 - 0:02[Mnamo Januari ya mwaka 2020,
-
0:02 - 0:05Christian Happi na Pardis Sabeti waliwasilisha wazo lenye uthubutu]
-
0:07 - 0:11[Sentinel: Mfumo wa ilani ya mapema katika kutambua na kufuatilia mlipuko wa gonjwa lijalo]
-
0:13 - 0:15[Hivi ni namna utavyofanya kazi ...]
-
0:16 - 0:23Christian Happi: Kiashiria ni mfumo wa ilani ya mapema iliyo amilifu katika kukinzana na magonjwa yanayoenea sana.
-
0:23 - 0:26Inajengwa na misingi mikuu mitatu.
-
0:26 - 0:28Pardis Sabeti: Msingi wa kwanza ni Utambuzi.
-
0:28 - 0:31Mimi na Christian tumekuwa tukitafiti pamoja magonjwa ya kuambukizwa
-
0:31 - 0:33duniani kote kwa miongo miwili.
-
0:33 - 0:35Tumekuwa tukitumia mfululizo wa jenomu.
-
0:35 - 0:38Tukizisoma taarifa timilifu za vinasaba vya vijidudu,
-
0:38 - 0:42inatusaidia kutambua virusi, hata vile ambavyo hatujawahi kuviona kabla,
-
0:42 - 0:44kuvifuatilia pale vinaposambaa
-
0:44 - 0:45na kuangazia mabadiliko yake mapya.
-
0:45 - 0:49Na sasa tukiwa na teknolojia yenye uwezo mkubwa wa kuziboresha chembe za urithi(jeni) iitwayo CRISPR,
-
0:49 - 0:51tunaweza kutumia taarifa hizi za kinasaba
-
0:51 - 0:56kutengeneza vipimo vya utambuzi vilivyo sahihi kwa vijidudu aina zote.
-
0:57 - 0:59CH: Moja ya nyenzo hizi zinafahamika kama SHERLOCK.
-
0:59 - 1:04Inaweza kutumika kutambua virusi vinavyotambulika katika vijikaratasi.
-
1:05 - 1:07Ni nafuu mno,
-
1:07 - 1:10na wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele wanaweza tumia SHERLOCK
-
1:10 - 1:14Kutambua virusi vinavyojulikana au vile ambavyo ni tishio
-
1:14 - 1:16ndani ya saa moja.
-
1:16 - 1:18PS: Nyenzo nyingine ni CARMEN.
-
1:18 - 1:22Inahitaji maabara, lakini inaweza kupima mamia ya virusi kwa wakati mmoja.
-
1:22 - 1:25Hivyo wafanyakazi wa maabara wanaweza pima sampuli za wagonjwa
-
1:25 - 1:26kutambua aina nyingi za virusi
-
1:26 - 1:28ndani ya siku moja.
-
1:28 - 1:31Msingi wetu wa pili ni Ungana.
-
1:31 - 1:33Kumuunganisha kila mmoja na kushirikishana taarifa
-
1:33 - 1:35kote katika jamii ya afya ya umma.
-
1:36 - 1:37Katika magonjwa mengi ya mlipuko,
-
1:37 - 1:42wafanyakazi wa hospitali hushirikishana taarifa kupitia nyaraka za karatasi.
-
1:42 - 1:45Hii hufanya ufatiliaji wa taarifa katika nafasi na nyakati
-
1:45 - 1:46na upatikanaji wa huduma
-
1:46 - 1:47kuwa mgumu sana.
-
1:48 - 1:51Hivyo tunatengeneza mfumo wa kimtandao na programu za simu
-
1:51 - 1:53ambazo zinawaunganisha wafanyakazi wa afya,
-
1:53 - 1:56waliopo zahanati, timu za afya umma -- kila mmoja --
-
1:56 - 1:58na kuwawezesha kuingiza taarifa,
-
1:58 - 2:01kufanya tathmini, kushirikishana vidokezo
-
2:01 - 2:03na kutengeneza mpango wa kuweza kuchukua hatua
-
2:03 - 2:05katika wakati sahihi.
-
2:05 - 2:08CH: Msingi wetu wa tatu ni Uwezeshaji.
-
2:08 - 2:11Mfumo wa uangalizi wa magonjwa ya mlipuko unaweza fanikiwa
-
2:11 - 2:15kama tutawawezesha wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele
-
2:15 - 2:17kuhudumia jamii.
-
2:17 - 2:19Inahitaji mafunzo mengi sana.
-
2:19 - 2:22Mimi na Pardis tunalitambua hilo.
-
2:22 - 2:23Tumetumia miaka kumi
-
2:23 - 2:27tukiwafunza mamia ya wanasayansi wadogo na wafanyakazi wa zanahati barani Afrika.
-
2:27 - 2:32Katika miaka mitano ijayo, tutaweza kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya wengine takribani 1,000
-
2:32 - 2:34katika kutumia mfumo wa Kiashiria
-
2:34 - 2:37na kuwawezesha pia kufundisha wafanyakazi wenzao.
-
2:37 - 2:40Namna hii, tutaweza kuboresha mfumo halisi wa afya
-
2:40 - 2:45na kuweza tumia uangalizi wa kina katika masuala ya kitabibu.
-
2:45 - 2:49[Tangu kuwakilisha mpango wao wa Uthubutu katika TED, ulimwengu umebadilika ...]
-
2:51 - 2:53Briar Goldberg: Tupo hapa, tunarekodi hili tukio.
-
2:53 - 2:56Ni tarehe 7 mwezi Aprili, 2020,
-
2:56 - 3:01na kwa uhakika, tupo katika tabu ya hili gonjwa ambalo ni janga la ulimwengu
-
3:01 - 3:03linalosababishwa na virusi vipya vya corona.
-
3:03 - 3:06Nyinyi wawili mmekuwa mkifanya kazi pamoja siku zote,
-
3:06 - 3:08na mlikuwa pamoja kwa juhudi
-
3:08 - 3:11katika janga la Ebola mwaka 2014.
-
3:11 - 3:14Mnalitazamaje hili jambo?
-
3:14 - 3:17CH: Miaka sita baada ya mlipuko wa Ebola,
-
3:17 - 3:19tumekumbana na janga lingine,
-
3:19 - 3:25na tupo katika wakati, ambao kwamba, hatujajifunza mengi kuhusu janga lililopita.
-
3:25 - 3:27Na hivyo, kiukweli, kwangu mimi, inanivunja moyo.
-
3:27 - 3:34PS: Ninadhani janga hili limetuonyesha ni namna gani hatukujiandaa
-
3:34 - 3:35duniani kote.
-
3:35 - 3:40Christian na washirika wetu pamoja tulikuwa na vikagua magonjwa katika hospitali zetu
-
3:40 - 3:43nchini Nigeria, Sierra Leone na Senegal mapema mwezi Februari.
-
3:43 - 3:49Majimbo mengi nchini Marekani hayakuwa navyo mpaka baadaye.
-
3:49 - 3:52Inatueleza kwamba wote tupo pamoja katika hili,
-
3:52 - 3:54na wote tupo nyuma .
-
3:54 - 3:58BG: Hivyo, huu mfumo wa Kiashiria ni mzuri,
-
3:58 - 4:01lakini nafahamu swali ambalo lipo akilini mwa kila mtu:
-
4:01 - 4:03Namna gani huu mfumo unasaidia sasa hivi?
-
4:03 - 4:06PS: Unajua, tumeelezea Kiashiria kama mfumo wa kuondokana na magonjwa yanayoenea sana,
-
4:06 - 4:08na hapa tupo katika moja ya magonjwa hayo.
-
4:08 - 4:10Lakini kilicho kikubwa ni kwamba, nyenzo zilezile unazohitaji
-
4:10 - 4:12kuondokana na gonjwa linaloenea
-
4:12 - 4:14ni zilezile unazohitaji kuondokana nalo.
-
4:14 - 4:17Na hivyo teknolojia ambazo tumeziainisha --
-
4:17 - 4:19Vipimo vyote vya awali vya uchaguzi,
-
4:19 - 4:23utambuzi na ufatiliaji wa virusi vinavyobadilika,
-
4:23 - 4:26na utumiaji wa programu za simu --
-
4:26 - 4:27ni muhimu mno.
-
4:27 - 4:30CH: Kwetu sisi, ni vita.
-
4:30 - 4:33Kimsingi tumejidhatiti katika ratiba ya masaa 24
-
4:33 - 4:35ili kuweza kutoa majibu,
-
4:35 - 4:39na inatuhitaji sisi kufanya kazi bila kupoteza muda.
-
4:39 - 4:41Hivyo ni nyakati yenye changamoto sana.
-
4:41 - 4:43Tupo mbali na familia.
-
4:43 - 4:45Angalau nina wasaha wa kuiona familia yangu leo,
-
4:45 - 4:48na kisha nina uhakika kesho ninarudi tena kwenye kazi.
-
4:48 - 4:51Katika maabara yangu, tumetengeneza mfululizo wa kwanza wa jenomu ya COVID-19
-
4:51 - 4:52katika bara la Afrika,
-
4:52 - 4:54na hilo lilifanyika ndani ya masaaa 48.
-
4:54 - 4:58Haya ni mapinduzi yanayotokea Afrika
-
4:58 - 5:01na kisha kufanya taarifa hizi kupatikana katika jamii ya masuala ya afya ulimwenguni
-
5:01 - 5:03ili kuona virusi vya Afrika vinaonekana katika namna gani.
-
5:03 - 5:06Ninaamini kwa kutumia teknolojia na maarifa
-
5:06 - 5:08na kisha kushirikisha taarifa,
-
5:08 - 5:10tunaweza fanya vizuri na kuweza kulishinda gonjwa.
-
5:10 - 5:13PS: Wazo zima la Sentinel
-
5:13 - 5:15ni katika kusimama wote kwa pamoja kulindana.
-
5:15 - 5:16Wote tunatazama.
-
5:16 - 5:17Kila mmoja wetu ni mlinzi.
-
5:17 - 5:21Kila mmoja wetu, anaweza tambua kipi kinachofanya sisi kuumwa,
-
5:21 - 5:24na kuweza kushirikisha jamii nzima taarifa hizo.
-
5:24 - 5:27Na nadhani hichi ndicho kitu ninachohitaji kiukweli,
-
5:27 - 5:29ni kwa wote kusimama kulindana
-
5:29 - 5:31na kutazamiana pamoja.
-
5:31 - 5:34[Dr. Pardis Sabeti na Dr. Christian Happi]
-
5:35 - 5:36[Wanasayansi wenye ustadi.
-
5:36 - 5:38Washirika wenye moyo.
-
5:38 - 5:40Mashujaa wa ulimwengu.]
- Title:
- Mtandao wa utambuzi wa virusi katika kuzuia mlipuko mwingine wa magonjwa.
- Speaker:
- Pardis Sabeti, Christian Happi
- Description:
-
Tunaweza vipi kuzuia mlipuko mwingine wa magonjwa kabla haujaanza? Watafiti wa magonjwa Pardis Sabeti na Christian Happi wameunda mfumo wa Sentinel, mfumo wa mapema ambao unatambua na kufatilia maambukizi yanayotokana na virusi katika muda mfupi -- na kuweza kuzuia kusambaa. Jifunze zaidi kuhusu teknolojia hii madhubuti inayosaidia mfumo na namna gani timu ya Sentinel inasaidia wanasayansi na wahudumu wa afya wakati wa janga la ugonjwa wa coronavirus.(Mpango huu wenye uthubutu ni moja ya miradi ya Audacious, ukisimamiwa na TED katika kuhamasisha mabadiliko ya kiulimwengu.)
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 05:54
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for A virus detection network to stop the next pandemic | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for A virus detection network to stop the next pandemic | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A virus detection network to stop the next pandemic | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for A virus detection network to stop the next pandemic | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for A virus detection network to stop the next pandemic | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for A virus detection network to stop the next pandemic |