WEBVTT 00:00:00.602 --> 00:00:01.753 [Mnamo Januari ya mwaka 2020, 00:00:01.777 --> 00:00:04.809 Christian Happi na Pardis Sabeti waliwasilisha wazo lenye uthubutu] NOTE Paragraph 00:00:06.934 --> 00:00:11.242 [Sentinel: Mfumo wa ilani ya mapema katika kutambua na kufuatilia mlipuko wa gonjwa lijalo] NOTE Paragraph 00:00:13.223 --> 00:00:14.984 [Hivi ni namna utavyofanya kazi ...] NOTE Paragraph 00:00:16.455 --> 00:00:23.080 Christian Happi: Kiashiria ni mfumo wa ilani ya mapema iliyo amilifu katika kukinzana na magonjwa yanayoenea sana. 00:00:23.104 --> 00:00:25.500 Inajengwa na misingi mikuu mitatu. NOTE Paragraph 00:00:25.524 --> 00:00:27.552 Pardis Sabeti: Msingi wa kwanza ni Utambuzi. 00:00:27.576 --> 00:00:30.557 Mimi na Christian tumekuwa tukitafiti pamoja magonjwa ya kuambukizwa 00:00:30.581 --> 00:00:32.545 duniani kote kwa miongo miwili. 00:00:32.569 --> 00:00:34.773 Tumekuwa tukitumia mfululizo wa jenomu. 00:00:34.797 --> 00:00:37.734 Tukizisoma taarifa timilifu za vinasaba vya vijidudu, 00:00:37.758 --> 00:00:42.095 inatusaidia kutambua virusi, hata vile ambavyo hatujawahi kuviona kabla, 00:00:42.119 --> 00:00:43.520 kuvifuatilia pale vinaposambaa 00:00:43.544 --> 00:00:45.428 na kuangazia mabadiliko yake mapya. 00:00:45.452 --> 00:00:48.749 Na sasa tukiwa na teknolojia yenye uwezo mkubwa wa kuziboresha chembe za urithi(jeni) iitwayo CRISPR, 00:00:48.773 --> 00:00:50.943 tunaweza kutumia taarifa hizi za kinasaba 00:00:50.967 --> 00:00:56.093 kutengeneza vipimo vya utambuzi vilivyo sahihi kwa vijidudu aina zote. NOTE Paragraph 00:00:56.557 --> 00:00:59.076 CH: Moja ya nyenzo hizi zinafahamika kama SHERLOCK. 00:00:59.100 --> 00:01:04.467 Inaweza kutumika kutambua virusi vinavyotambulika katika vijikaratasi. 00:01:04.885 --> 00:01:06.596 Ni nafuu mno, 00:01:06.620 --> 00:01:09.634 na wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele wanaweza tumia SHERLOCK 00:01:09.658 --> 00:01:14.227 Kutambua virusi vinavyojulikana au vile ambavyo ni tishio 00:01:14.251 --> 00:01:15.641 ndani ya saa moja. NOTE Paragraph 00:01:16.109 --> 00:01:17.689 PS: Nyenzo nyingine ni CARMEN. 00:01:17.713 --> 00:01:22.045 Inahitaji maabara, lakini inaweza kupima mamia ya virusi kwa wakati mmoja. 00:01:22.069 --> 00:01:24.777 Hivyo wafanyakazi wa maabara wanaweza pima sampuli za wagonjwa 00:01:24.801 --> 00:01:26.303 kutambua aina nyingi za virusi 00:01:26.327 --> 00:01:27.841 ndani ya siku moja. NOTE Paragraph 00:01:27.865 --> 00:01:30.556 Msingi wetu wa pili ni Ungana. 00:01:30.580 --> 00:01:33.016 Kumuunganisha kila mmoja na kushirikishana taarifa 00:01:33.040 --> 00:01:34.974 kote katika jamii ya afya ya umma. 00:01:35.752 --> 00:01:37.093 Katika magonjwa mengi ya mlipuko, 00:01:37.117 --> 00:01:41.560 wafanyakazi wa hospitali hushirikishana taarifa kupitia nyaraka za karatasi. 00:01:42.115 --> 00:01:44.683 Hii hufanya ufatiliaji wa taarifa katika nafasi na nyakati 00:01:44.707 --> 00:01:46.037 na upatikanaji wa huduma 00:01:46.061 --> 00:01:47.496 kuwa mgumu sana. 00:01:47.877 --> 00:01:50.982 Hivyo tunatengeneza mfumo wa kimtandao na programu za simu 00:01:51.006 --> 00:01:52.985 ambazo zinawaunganisha wafanyakazi wa afya, 00:01:53.009 --> 00:01:56.253 waliopo zahanati, timu za afya umma -- kila mmoja -- 00:01:56.277 --> 00:01:58.455 na kuwawezesha kuingiza taarifa, 00:01:58.479 --> 00:02:01.215 kufanya tathmini, kushirikishana vidokezo 00:02:01.239 --> 00:02:03.318 na kutengeneza mpango wa kuweza kuchukua hatua 00:02:03.342 --> 00:02:04.840 katika wakati sahihi. NOTE Paragraph 00:02:04.864 --> 00:02:07.887 CH: Msingi wetu wa tatu ni Uwezeshaji. 00:02:08.462 --> 00:02:11.074 Mfumo wa uangalizi wa magonjwa ya mlipuko unaweza fanikiwa 00:02:11.098 --> 00:02:15.119 kama tutawawezesha wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele 00:02:15.143 --> 00:02:16.833 kuhudumia jamii. 00:02:16.857 --> 00:02:19.037 Inahitaji mafunzo mengi sana. 00:02:19.061 --> 00:02:21.531 Mimi na Pardis tunalitambua hilo. 00:02:21.555 --> 00:02:23.422 Tumetumia miaka kumi 00:02:23.446 --> 00:02:27.413 tukiwafunza mamia ya wanasayansi wadogo na wafanyakazi wa zanahati barani Afrika. 00:02:27.437 --> 00:02:31.547 Katika miaka mitano ijayo, tutaweza kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya wengine takribani 1,000 00:02:31.571 --> 00:02:33.897 katika kutumia mfumo wa Kiashiria 00:02:33.921 --> 00:02:36.794 na kuwawezesha pia kufundisha wafanyakazi wenzao. 00:02:36.818 --> 00:02:40.332 Namna hii, tutaweza kuboresha mfumo halisi wa afya 00:02:40.356 --> 00:02:44.538 na kuweza tumia uangalizi wa kina katika masuala ya kitabibu. NOTE Paragraph 00:02:45.488 --> 00:02:49.368 [Tangu kuwakilisha mpango wao wa Uthubutu katika TED, ulimwengu umebadilika ...] NOTE Paragraph 00:02:50.773 --> 00:02:53.292 Briar Goldberg: Tupo hapa, tunarekodi hili tukio. 00:02:53.316 --> 00:02:55.760 Ni tarehe 7 mwezi Aprili, 2020, 00:02:55.784 --> 00:03:00.867 na kwa uhakika, tupo katika tabu ya hili gonjwa ambalo ni janga la ulimwengu 00:03:00.891 --> 00:03:02.653 linalosababishwa na virusi vipya vya corona. 00:03:02.677 --> 00:03:05.611 Nyinyi wawili mmekuwa mkifanya kazi pamoja siku zote, 00:03:05.635 --> 00:03:08.454 na mlikuwa pamoja kwa juhudi 00:03:08.478 --> 00:03:11.353 katika janga la Ebola mwaka 2014. 00:03:11.377 --> 00:03:13.573 Mnalitazamaje hili jambo? NOTE Paragraph 00:03:13.597 --> 00:03:16.964 CH: Miaka sita baada ya mlipuko wa Ebola, 00:03:16.988 --> 00:03:19.076 tumekumbana na janga lingine, 00:03:19.100 --> 00:03:25.028 na tupo katika wakati, ambao kwamba, hatujajifunza mengi kuhusu janga lililopita. 00:03:25.052 --> 00:03:27.413 Na hivyo, kiukweli, kwangu mimi, inanivunja moyo. NOTE Paragraph 00:03:27.437 --> 00:03:34.035 PS: Ninadhani janga hili limetuonyesha ni namna gani hatukujiandaa 00:03:34.059 --> 00:03:35.227 duniani kote. 00:03:35.251 --> 00:03:39.984 Christian na washirika wetu pamoja tulikuwa na vikagua magonjwa katika hospitali zetu 00:03:40.008 --> 00:03:43.245 nchini Nigeria, Sierra Leone na Senegal mapema mwezi Februari. 00:03:43.269 --> 00:03:48.789 Majimbo mengi nchini Marekani hayakuwa navyo mpaka baadaye. 00:03:48.813 --> 00:03:51.792 Inatueleza kwamba wote tupo pamoja katika hili, 00:03:51.816 --> 00:03:53.942 na wote tupo nyuma . NOTE Paragraph 00:03:53.966 --> 00:03:57.874 BG: Hivyo, huu mfumo wa Kiashiria ni mzuri, 00:03:57.898 --> 00:04:00.715 lakini nafahamu swali ambalo lipo akilini mwa kila mtu: 00:04:00.739 --> 00:04:02.767 Namna gani huu mfumo unasaidia sasa hivi? NOTE Paragraph 00:04:02.791 --> 00:04:06.050 PS: Unajua, tumeelezea Kiashiria kama mfumo wa kuondokana na magonjwa yanayoenea sana, 00:04:06.074 --> 00:04:07.520 na hapa tupo katika moja ya magonjwa hayo. 00:04:07.544 --> 00:04:10.328 Lakini kilicho kikubwa ni kwamba, nyenzo zilezile unazohitaji 00:04:10.352 --> 00:04:11.506 kuondokana na gonjwa linaloenea 00:04:11.530 --> 00:04:13.639 ni zilezile unazohitaji kuondokana nalo. 00:04:13.663 --> 00:04:16.728 Na hivyo teknolojia ambazo tumeziainisha -- 00:04:16.752 --> 00:04:19.377 Vipimo vyote vya awali vya uchaguzi, 00:04:19.401 --> 00:04:22.811 utambuzi na ufatiliaji wa virusi vinavyobadilika, 00:04:22.835 --> 00:04:26.235 na utumiaji wa programu za simu -- 00:04:26.259 --> 00:04:27.418 ni muhimu mno. NOTE Paragraph 00:04:27.442 --> 00:04:29.574 CH: Kwetu sisi, ni vita. 00:04:29.598 --> 00:04:32.939 Kimsingi tumejidhatiti katika ratiba ya masaa 24 00:04:32.963 --> 00:04:34.908 ili kuweza kutoa majibu, 00:04:34.932 --> 00:04:39.119 na inatuhitaji sisi kufanya kazi bila kupoteza muda. 00:04:39.143 --> 00:04:41.352 Hivyo ni nyakati yenye changamoto sana. 00:04:41.376 --> 00:04:42.550 Tupo mbali na familia. 00:04:42.574 --> 00:04:44.950 Angalau nina wasaha wa kuiona familia yangu leo, 00:04:44.974 --> 00:04:47.934 na kisha nina uhakika kesho ninarudi tena kwenye kazi. 00:04:47.958 --> 00:04:51.122 Katika maabara yangu, tumetengeneza mfululizo wa kwanza wa jenomu ya COVID-19 00:04:51.146 --> 00:04:52.385 katika bara la Afrika, 00:04:52.409 --> 00:04:54.440 na hilo lilifanyika ndani ya masaaa 48. 00:04:54.464 --> 00:04:57.531 Haya ni mapinduzi yanayotokea Afrika 00:04:57.555 --> 00:05:01.110 na kisha kufanya taarifa hizi kupatikana katika jamii ya masuala ya afya ulimwenguni 00:05:01.134 --> 00:05:03.372 ili kuona virusi vya Afrika vinaonekana katika namna gani. 00:05:03.396 --> 00:05:06.052 Ninaamini kwa kutumia teknolojia na maarifa 00:05:06.076 --> 00:05:08.185 na kisha kushirikisha taarifa, 00:05:08.209 --> 00:05:10.377 tunaweza fanya vizuri na kuweza kulishinda gonjwa. NOTE Paragraph 00:05:10.401 --> 00:05:12.523 PS: Wazo zima la Sentinel 00:05:12.547 --> 00:05:14.695 ni katika kusimama wote kwa pamoja kulindana. 00:05:14.719 --> 00:05:15.875 Wote tunatazama. 00:05:15.899 --> 00:05:17.359 Kila mmoja wetu ni mlinzi. 00:05:17.383 --> 00:05:21.292 Kila mmoja wetu, anaweza tambua kipi kinachofanya sisi kuumwa, 00:05:21.316 --> 00:05:23.917 na kuweza kushirikisha jamii nzima taarifa hizo. 00:05:23.941 --> 00:05:26.966 Na nadhani hichi ndicho kitu ninachohitaji kiukweli, 00:05:26.990 --> 00:05:29.295 ni kwa wote kusimama kulindana 00:05:29.319 --> 00:05:30.855 na kutazamiana pamoja. NOTE Paragraph 00:05:31.269 --> 00:05:33.606 [Dr. Pardis Sabeti na Dr. Christian Happi] NOTE Paragraph 00:05:34.998 --> 00:05:36.153 [Wanasayansi wenye ustadi. 00:05:36.177 --> 00:05:37.933 Washirika wenye moyo. 00:05:37.957 --> 00:05:39.650 Mashujaa wa ulimwengu.]