-
Google Tafsiri ni zana ya bure ambayo hukuwezesha kutafsiri sentensi, nyaraka na hata pia
-
tovuti nzima papo hapo.
-
Lakini inafanya kazi aje? Ijapokuwa huenda ikaonekana tuna chumba kilichojaa vijini vya lugha
-
mbalimbali vinavyotufanyia kazi, kwa hakika tafsiri zetu zote zimetoka kwenye kompyuta. Kompyuta hizi
-
hutumia mchakato unaoitwa "utafsiri wa mashine ya takwimu"-- ambayo ni njia maridadi ya kusema ya kamba
-
kompyuta zetu huzalisha tafsiri zinazotegemea ruwaza zinazopatikana katika viwango vikubwa vya matini.
-
Lakini wacha turudi nyuma. Kama unataka kumfundisha mtu lugha mpya unaweza kuanza kwa kumfunza maneno ya
-
msamiati na kanuni za sarufi ambazo hufafanua jinsi ya kubuni sentensi. Kompyuta inaweza kujifunza lugha
-
geni kwa njia hiyo moja - kwa kurejelea msamiati na kanuni.
-
Lakini lugha ni changamani na, kama vile mwanafunzi yeyote wa lugha anavyoweza kukuambia, kuna buraa
-
za takriban kila kanuni. Wakati unapojaribu kunasa buraa hizi zote, na buraa hadi buraa, katika
-
programu ya kompyuta, ubora wa utafsiri huanza kuainishwa.
-
Google Tafsiri huchukua mbinu tofauti. Badala ya kujaribu kufunza kompyuta zetu kanuni zote za lugha,
-
sisi huruhusu kompyuta zetu kutambua kanuni kivyao. Zinafanya hivi kwa kuchunguza mamilioni na
-
mamiliano ya nyaraka ambazo zimetafsiriwa tayari na watafsiri wanadamu. Matini haya
-
yaliyotafsiriwa hutoka kwenye vitabu, mashirika kama vile UN na tovuti
-
kutoka ulimwenguni kote.
-
Kompyuta zetu huskani matini haya kwa kutafuta ruwaza muhimu ya tarakimu--hiyo ni kusema,
-
ruwaza kati ya utafsiri na matini halisi ambayo hayawezi kutokea kibahati. Punde tu kompyuta
-
inapopata ruwaza, inaweza kutumia ruwaza hii ili kutafsiri matini yanayofanana baadaye.
-
Wakati unaporudia mchakato huu mabilioni ya muda unapata mabilioni ya ruwaza na
-
programu moja maizi sana ya kompyuta.
-
Walakini kwa lugha zingine tuna nyaraka chache zilizotafsiriwa zinazopatikana na kwa hivyo
-
ruwaza chache ambazo programu yetu imetambua. Hii ndiyo maana ubora wa utafsiri wetu hutofautiana
-
kilugha na kwa jozi ya lugha. Tunajua tafsiri zetu sio kamili kila wakati lakini kwa kutoa matini mapya
-
yaliyotafsiriwa mara kwa mara tunaweza kufanya kompyuta zetu kuwa maizi zaidi na tafsiri
-
zetu kuwa nzuri zaidi.
-
Kwa hivyo wakati mwingine unapotafsiri sentensi au ukurasa wa wavuti na Google Tafsiri, fikiria
-
kuhusu mamilioni ya nyaraka na mabilioni ya ruwaza ambazo zinatoa utafsiri wako - na na
-
hayo yote hufanyika unapopepesa jicho.
-
Nzuri sana, sivyo?
-
Jaribu kwenye translate.google.com.