Google Tafsiri ni zana ya bure ambayo hukuwezesha kutafsiri sentensi, nyaraka na hata pia tovuti nzima papo hapo. Lakini inafanya kazi aje? Ijapokuwa huenda ikaonekana tuna chumba kilichojaa vijini vya lugha mbalimbali vinavyotufanyia kazi, kwa hakika tafsiri zetu zote zimetoka kwenye kompyuta. Kompyuta hizi hutumia mchakato unaoitwa "utafsiri wa mashine ya takwimu"-- ambayo ni njia maridadi ya kusema ya kamba kompyuta zetu huzalisha tafsiri zinazotegemea ruwaza zinazopatikana katika viwango vikubwa vya matini. Lakini wacha turudi nyuma. Kama unataka kumfundisha mtu lugha mpya unaweza kuanza kwa kumfunza maneno ya msamiati na kanuni za sarufi ambazo hufafanua jinsi ya kubuni sentensi. Kompyuta inaweza kujifunza lugha geni kwa njia hiyo moja - kwa kurejelea msamiati na kanuni. Lakini lugha ni changamani na, kama vile mwanafunzi yeyote wa lugha anavyoweza kukuambia, kuna buraa za takriban kila kanuni. Wakati unapojaribu kunasa buraa hizi zote, na buraa hadi buraa, katika programu ya kompyuta, ubora wa utafsiri huanza kuainishwa. Google Tafsiri huchukua mbinu tofauti. Badala ya kujaribu kufunza kompyuta zetu kanuni zote za lugha, sisi huruhusu kompyuta zetu kutambua kanuni kivyao. Zinafanya hivi kwa kuchunguza mamilioni na mamiliano ya nyaraka ambazo zimetafsiriwa tayari na watafsiri wanadamu. Matini haya yaliyotafsiriwa hutoka kwenye vitabu, mashirika kama vile UN na tovuti kutoka ulimwenguni kote. Kompyuta zetu huskani matini haya kwa kutafuta ruwaza muhimu ya tarakimu--hiyo ni kusema, ruwaza kati ya utafsiri na matini halisi ambayo hayawezi kutokea kibahati. Punde tu kompyuta inapopata ruwaza, inaweza kutumia ruwaza hii ili kutafsiri matini yanayofanana baadaye. Wakati unaporudia mchakato huu mabilioni ya muda unapata mabilioni ya ruwaza na programu moja maizi sana ya kompyuta. Walakini kwa lugha zingine tuna nyaraka chache zilizotafsiriwa zinazopatikana na kwa hivyo ruwaza chache ambazo programu yetu imetambua. Hii ndiyo maana ubora wa utafsiri wetu hutofautiana kilugha na kwa jozi ya lugha. Tunajua tafsiri zetu sio kamili kila wakati lakini kwa kutoa matini mapya yaliyotafsiriwa mara kwa mara tunaweza kufanya kompyuta zetu kuwa maizi zaidi na tafsiri zetu kuwa nzuri zaidi. Kwa hivyo wakati mwingine unapotafsiri sentensi au ukurasa wa wavuti na Google Tafsiri, fikiria kuhusu mamilioni ya nyaraka na mabilioni ya ruwaza ambazo zinatoa utafsiri wako - na na hayo yote hufanyika unapopepesa jicho. Nzuri sana, sivyo? Jaribu kwenye translate.google.com.