Namna Afrika inavyoweza kutumia maarifa ya kitamaduni kupiga hatua
-
0:01 - 0:07Miezi kadhaa iliyopita, nilitembelea jiji moja lililopo Afrika Mashariki,
-
0:07 - 0:10na tulikuwa tumekwama kwenye msongamano wa magari.
-
0:10 - 0:13Na mchuuzi mmoja alikuja ghafla kwenye dirisha langu
-
0:13 - 0:15na karatasi ya alfabeti iliyofunguka nusu.
-
0:17 - 0:19Niliangalia kwa haraka ile karatasi ya alfabeti,
-
0:19 - 0:21na nikamuwaza binti yangu,
-
0:21 - 0:23ni namna gani ingekuwa vyema kuitandaza kwenye sakafu
-
0:23 - 0:25na kucheza juu yake nikiwa nae
-
0:25 - 0:27wakati nikiwa ninamfundisha alfabeti.
-
0:27 - 0:31Msongamano ukasogea kidogo, na nikanunua ile nakala haraka,
-
0:31 - 0:33na tukaendelea na safari.
-
0:34 - 0:37Nilipopata muda wa kuifungua ile karatasi ya alfabeti
-
0:37 - 0:40na kuiangalia kwa makini,
-
0:40 - 0:43Nilitambua ya kwamba sitaitumia kumfundishia binti yangu.
-
0:43 - 0:45Nilijutia ununuzi wangu.
-
0:46 - 0:48Kwanini?
-
0:48 - 0:51Kutazama karatasi ya alfabeti kunanikumbusha ukweli kwamba
-
0:51 - 0:54mambo mengi hayajabadilika
-
0:54 - 0:56katika mtaala wa elimu barani Afrika.
-
0:57 - 1:00Miongo kadhaa iliyopita, nilifundishwa kutoka katika karatasi hiyohiyo.
-
1:01 - 1:04Na kwa sababu ya hilo, nilitaabika kwa miaka.
-
1:04 - 1:09Nilitaabika kuweza kukubali uhalisia wangu kutokana na elimu niliyokuwa nikipokea
-
1:09 - 1:11shuleni, katika shule nilizosoma.
-
1:13 - 1:15Nilikuwa na janga la utambulisho.
-
1:15 - 1:18Nikitazama kuangalia uhalisia wangu.
-
1:18 - 1:22Niliangalia mababu zangu, nilitazama kizazi changu bila heshima.
-
1:22 - 1:27Nilikuwa na subira kidogo kwa yale ambayo maisha yangeweza kunipa kutoka katika mazingira yangu.
-
1:29 - 1:30Kwanini?
-
1:31 - 1:33"A ni kwa ajili ya Apple."
-
1:34 - 1:36"A ni kwa ajili ya Apple."
-
1:38 - 1:42"A ni kwa ajili ya Apple" ni kwa ajili ya mtoto katika pande ya dunia
-
1:42 - 1:44ambayo wanalima Apple;
-
1:45 - 1:47nani aliye na Apple katika mfuko wake wa chakula cha mchana;
-
1:48 - 1:52nani ambaye huenda dukani na mama yake na kuona apple jekundu,
-
1:52 - 1:55kijani, njano katika kila umbo na rangi na ukubwa.
-
1:56 - 1:59Kwa hiyo, kumpa elimu mtoto huyu
-
1:59 - 2:01ukitumia karatasi ya alfabeti kama hii
-
2:02 - 2:05inatimiza moja ya kazi kuu katika elimu,
-
2:05 - 2:08ambayo ni kumkutanisha msomaji
-
2:08 - 2:12kuridhika na mazingira ya msomaji
-
2:12 - 2:16na udadisi wa kuweza kutafuta zaidi ili kuweza kuongeza thamani.
-
2:18 - 2:19Nikijiangalia mimi,
-
2:20 - 2:22wakati na mahali nilipokulia Afrika,
-
2:24 - 2:25apple ni tunda hadimu.
-
2:27 - 2:28Mara mbili au tatu kwa mwaka,
-
2:28 - 2:33Nilikuwa napata apple za rangi ya njano zilizo na alama ndogo ndogo za rangi ya kahawia, unajua,
-
2:34 - 2:37ikiashiria maelfu ya maili yaliposafiri -- ghalani, katika upangaji
-
2:37 - 2:39kunifikia mimi.
-
2:40 - 2:41Nilikulia katika jiji
-
2:42 - 2:45kwa wazazi ambao wanajiweza kiuchumi,
-
2:45 - 2:46kwa hiyo ulikuwa ni uhalisia wangu wa kuheshimika,
-
2:46 - 2:49kama vile vile
-
2:49 - 2:53mihogo au ugali kwa kawaida hautakuwepo
-
2:53 - 2:56katika mlo wa Kimarekani, Kichina au Kihindi,
-
2:57 - 2:59apple hazikuwa katika uhalisia wa maisha yangu.
-
3:00 - 3:03Kwa hiyo hii ilinifanya nini mimi,
-
3:03 - 3:07kunipa elimu kwangu ya "A ni kwa ajili ya apple,"
-
3:07 - 3:09imefanya elimu kuwa ngumu mno kuelewa.
-
3:10 - 3:12Imefanya kitu ambacho kipo na upeo wangu --
-
3:13 - 3:15kitu cha nchi za nje,
-
3:15 - 3:18jambo ambalo ningekuwa nikilitafuta mara zote
-
3:18 - 3:20uthibitisho wa yale yanayohusiana
-
3:20 - 3:23kwa ajili yangu ili kupiga hatua ndani yake na pamoja yake.
-
3:24 - 3:27Hiyo ilikuwa ngumu kwa mtoto;
-
3:28 - 3:31Nilipokuwa kiumri na kuelimika,
-
3:31 - 3:36uhalisia wangu uligawanyika zaidi na elimu yangu.
-
3:37 - 3:38Katika historia, nilifundishwa
-
3:39 - 3:43kwamba mtalii aliyeitwa Mungo Park aligundua mto wa Niger.
-
3:44 - 3:45Na hili lilinikwaza.
-
3:45 - 3:47Mababu wa mababu zangu walikulia
-
3:47 - 3:49karibu na kingo za mto wa Niger.
-
3:50 - 3:52(Kicheko)
-
3:52 - 3:58Na ilichukua mtu mwingine kusafiri maelfu ya maili kutoka Ulaya
-
3:58 - 4:01kuja kugundua mto ambao upo karibu nao kabisa?
-
4:01 - 4:03(Kicheko)
-
4:03 - 4:05Hapana!
-
4:05 - 4:10(Makofi na shangilio)
-
4:10 - 4:12Walitumia vipi muda wao?
-
4:12 - 4:14(Kicheko)
-
4:14 - 4:17Kucheza bao, kukaanga magimbi,
-
4:17 - 4:18kupigana vita vya ukabila?
-
4:19 - 4:23Namaanisha, nilijua ya kwamba elimu yangu ilikuwa ikiniandaa kwenda sehemu nyingine
-
4:23 - 4:27na kuitumia na katika mazingira mengine ambayo inahusiana nayo.
-
4:27 - 4:30Haikuwa kwa ajili ya mazingira yangu, mahali na muda nilipokua.
-
4:31 - 4:32Na hali hii iliendelea.
-
4:32 - 4:34Na hii philosophia iliimarisha masomo yangu
-
4:34 - 4:37muda wote nilipokuwa nikisoma barani Afrika.
-
4:37 - 4:40Ilihitaji uzoefu mwingi na baadhi ya mafunzo
-
4:40 - 4:44kwa mimi kuanza pata mabadiliko ya mtazamo wangu.
-
4:44 - 4:47Nitawaambia baadhi ya mambo makubwa mazuri.
-
4:48 - 4:50Nilikuwa nchini Marekani katika jimbo la Washington, DC
-
4:50 - 4:52kusomea masomo yangu ya shahada ya uzamivu,
-
4:52 - 4:56nilipata nafasi ya kuwa mshauri katika Benki ya Dunia ukanda wa Afrika,
-
4:57 - 4:59Kwa hiyo nakumbuka siku moja,
-
5:00 - 5:04mkuu wangu wa kazi -- tulikuwa tukiongelea kuhusu mradi fulani,
-
5:04 - 5:07na alitaja mradi unaohusiana na Benki ya Dunia,
-
5:07 - 5:12mradi mkubwa wa umwagiliaji unaogharimu mamilioni ya dola
-
5:12 - 5:14katika Jamhuri ya Niger
-
5:14 - 5:17uliokuwa unasuasua uendelezaji wake.
-
5:17 - 5:19Alisema mradi huu haupo imara,
-
5:19 - 5:23na unawakera wale ambao waliupa mamlaka.
-
5:24 - 5:27Lakini aliutaja mradi fulani,
-
5:28 - 5:32namna ya umwagiliaji wa kitamaduni ambao ulikuwa na mafanikio makubwa sana
-
5:32 - 5:36katika nchi hiyo hiyo ya Jamhuri ya Niger ambapo mradi wa Benki ya Dunia ulikuwa ukifeli.
-
5:37 - 5:38Na ikanifanya kuwaza.
-
5:39 - 5:41Kwa hiyo nikafanya utafiti zaidi,
-
5:42 - 5:44na nikagundua kuhusu Tassa.
-
5:46 - 5:50Tassa ni namna ya umwagiliaji wa kienyeji
-
5:50 - 5:56ambapo mashimo yenye upana wa kati ya sentimenta 20 hadi 30 na kina cha sentimeta 20 hadi 30
-
5:56 - 5:59huchimbwa katika shamba ambalo linaelekea kulimwa.
-
5:59 - 6:03Kisha, bwawa dogo hujengwa kuzunguka shamba
-
6:04 - 6:08na mazao hupandwa ardhini.
-
6:08 - 6:11Kinachotokea ni kwamba mvua itaponyesha,
-
6:11 - 6:14mashimo huwa na uwezo wa kutunza maji
-
6:14 - 6:18na kupelekea kiasi kwamba mmea kuhitaji maji.
-
6:18 - 6:21Mmea unaweza pata maji mengi unavyohitaji
-
6:21 - 6:23mpaka muda wa mavuno.
-
6:25 - 6:28Niger ni asilimia 75 jangwa,
-
6:28 - 6:31na hii kitu cha maisha au kifo,
-
6:31 - 6:33na imekuwa ikitumika kwa karne.
-
6:33 - 6:35Katika utafiti ambao ulifanyika,
-
6:36 - 6:42mashamba mawili yanayofanana yalitumika katika utafiti,
-
6:42 - 6:44na shamba moja
-
6:44 - 6:46halikutumia njia ya Tassa.
-
6:46 - 6:47Mashamba yanayofanana.
-
6:47 - 6:51Lingine lilitumia njia ya Tassa.
-
6:51 - 6:55Kisha mbegu sawa za mtama zilipandwa katika mashamba yote mawili.
-
6:56 - 6:58Wakati wa mavuno,
-
6:58 - 7:01Shamba ambalo halikutumia njia ya Tassa
-
7:01 - 7:06lilizalisha kilogramu 11 za mtama kwa hektari.
-
7:07 - 7:09Shamba lililotumia njia ya Tassa
-
7:09 - 7:15lilizalisha kilogramu 553 za mtama kwa hektari.
-
7:16 - 7:18(Makofi)
-
7:18 - 7:22Niliangalia ule utafiti na nikajitazama.
-
7:22 - 7:25Nilisema, "Nimesomea kilimo kwa miaka 12,
-
7:25 - 7:29kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato cha sita, kama tuitavyo kwa Afrika Mashariki,
-
7:29 - 7:31SS3 kwa Afrika Magharibi au darasa la 12.
-
7:31 - 7:33Hakuna aliyewahi kunifundisha
-
7:33 - 7:37namna yoyote ya maarifa ya Kiafrika katika ukulima --
-
7:37 - 7:39katika mavuno, katika chochote --
-
7:39 - 7:42ambayo itafanya kazi katika nyakati za kisasa na hakika kufanikiwa,
-
7:42 - 7:47pale ambapo jambo fulani lillotolewa nchi za Magharibi limehangaika kufanikiwa.
-
7:48 - 7:51Hapo ndipo nilitambua changamoto,
-
7:51 - 7:53changamoto ya mtaala wa Kiafrika,
-
7:54 - 7:58Na kisha nikaanza lengo langu la kujitolea maisha yangu, kujali maisha yangu ya kazi,
-
7:58 - 8:03katika kusoma, kufanya tafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika
-
8:03 - 8:06na kuweza kuyawakilisha katika njia kuu
-
8:06 - 8:09katika elimu, katika tafiti, sera
-
8:09 - 8:11katika sekta na viwanda.
-
8:11 - 8:15Maongezi mengine na uzoefu niliopata nikiwa Benki ya Dunia
-
8:15 - 8:20Nahisi umenifanya nichukue uamuzi wa mwisho wa wapi nitaelekea,
-
8:20 - 8:24ingawa haikuwa tafiti yenye matunda makubwa ya kuielekea,
-
8:24 - 8:26lakini ilikuwa kuhusu jambo ambalo nililiamini.
-
8:27 - 8:32Kwa hiyo siku moja, mkuu wangu wa kazi alisema kwamba angependelea kwenda Afrika
-
8:32 - 8:36kwa ajili ya kujadiliana kuhusu mikopo ya Benki ya Dunia na kufanyia kazi miradi ya Benki hiyo.
-
8:37 - 8:39Na nilihamasika, nikamuuliza kwanini.
-
8:39 - 8:41Alisema, "Oh, nitapoenda Afrika,
-
8:41 - 8:43ni rahisi.
-
8:43 - 8:48Ninaandika tu nyaraka za mkopo na dhumuni la mkopo nikiwa Washington, DC,
-
8:48 - 8:51Ninakwenda Afrika, na kisha nyaraka zote zinasainiwa.
-
8:51 - 8:54Ninapata mpango mzuri kabisa, na kisha narudi ofisini.
-
8:54 - 8:57Wakuu wangu wa kazi watanifurahia."
-
8:57 - 9:01Lakini kisha akasema, "sipendi kwenda Asia au ..."
-
9:01 - 9:04na alitaja nchi fulani, bara la Asia na nchi baadhi.
-
9:04 - 9:08"Huwa wananifanya nikae kwa muda mrefu, wakijaribu kutafuta mipango bora kwa nchi zao.
-
9:08 - 9:09Huwa wanapata mipango bora.
-
9:09 - 9:12Wananiambia, 'Oh, hicho kipengele hakitatufaa
-
9:12 - 9:14katika mazingira yetu.
-
9:14 - 9:17Si uhalisia wetu. Kimekaa katika mfumo wa Magharibi sana.'
-
9:17 - 9:20Na wananiambia, 'Oh, tuna wataalamu wa kutosha
-
9:20 - 9:21kwa ajili ya kushughulikia hili.
-
9:21 - 9:23Huna wataalamu wa kutosha.
-
9:23 - 9:24Tunafahamu lengo letu.'
-
9:24 - 9:27Na wanaendelea kupitia haya mambo yote.
-
9:27 - 9:29Ikifika muda wa kumaliza, ndiyo, wanapata mpango bora,
-
9:29 - 9:32lakini nakuwa nimechoka na sipati mpango mzuri kwa ajili ya benki,
-
9:32 - 9:33na sisi tupo katika biashara."
-
9:34 - 9:35"Kweli?" Niliwaza akilini, "Sawa."
-
9:35 - 9:40Nilipata kipaumbele cha kupata nafasi ya kuwepo katika kikao cha kujadili kuhusu mkopo
-
9:40 - 9:41katika nchi ya Kiafrika.
-
9:41 - 9:44Kwa hivyo ningefanya kazi ya ushauri wakati wa kiangazi,
-
9:44 - 9:47unajua, ukizingatia mimi ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu.
-
9:47 - 9:51Na nilisafiri na timu, na timu ya Benki ya Dunia,
-
9:51 - 9:56kama mtu ambaye ningesaidia katika masuala ya upangaji wa majadiliano.
-
9:56 - 9:59Lakini nilipokuwa wakati wa majadiliano.
-
10:00 - 10:05Niliokuwa nao wengi ni toka Ulaya na Marekani, unajua, wakiwa na mimi kutoka Washington, DC.
-
10:05 - 10:10Na nilitazama katika meza nikiwaangalia kaka na dada zangu wa Kiafrika.
-
10:10 - 10:12Niliona uoga katika nyuso zao.
-
10:13 - 10:15Hawakuamini kama walikuwa na chochote cha kuwapa
-
10:15 - 10:17vilembwe wa Mungo Park --
-
10:17 - 10:20wamiliki wa "apple" katika "A is for Apple."
-
10:20 - 10:23Walikaa na kutazama:"Oh, mtupatie, tuweze tia saini.
-
10:23 - 10:25Mnayo maarifa, mnafahamu yote.
-
10:25 - 10:27Wapi tunatakiwa kutia saini?Tuonyeshe, tutie saini."
-
10:27 - 10:30Hawakuwa na sauti. Hawakujiamini.
-
10:35 - 10:36Mniwie radhi.
-
10:37 - 10:38Na kwa hiyo,
-
10:39 - 10:42Nimekuwa nikifanya hivi kwa muongo.
-
10:42 - 10:45Nimekuwa nikifanyia utafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika,
-
10:45 - 10:47asilia, halisi, maarifa ya Kiafrika.
-
10:47 - 10:50Katika mambo machache ambapo hili suala limehusishwa,
-
10:51 - 10:53kumekuwa na mafanikio makubwa ya kusisimua yaliyorekodiwa.
-
10:53 - 10:55Nawaza kuhusu Gacaca.
-
10:55 - 11:00Gacaca ni mfumo wa kitamaduni wa korti wa nchini Rwanda
-
11:00 - 11:02ambao ulitumika baada ya mauaji ya kimbari.
-
11:02 - 11:05Mnamo 1994, mauaji yalipoisha,
-
11:06 - 11:09Mfumo wa mahakama wa taifa la Rwanda ulikuwa hafifu katika utendaji:
-
11:09 - 11:14hakuna majaji, hakuna mawakili kuweza fanyia kazi mamia ya maelfu ya kesi za mauaji ya kimbari.
-
11:14 - 11:18Kwa hiyo serikali ya Rwanda ilipata wazo hili
-
11:18 - 11:21kufufua mfumo wa jadi wa korti unaofahamika kama Gacaca.
-
11:22 - 11:25Gacaca ni mfumo wa jamii wa mahakama,
-
11:25 - 11:28ambapo wanajamii hukutana pamoja
-
11:28 - 11:32kuchagua waume kwa wake walio na uadilifu
-
11:32 - 11:36kusimamia kesi ya jinai zilizofanyika katika jamii yao.
-
11:37 - 11:43Kwa wakati Gacaca ilipomaliza kutoa hukumu ya kesi za mauaji ya kimbari mnamo mwaka 2012,
-
11:44 - 11:51mahakama 12,000 za kijamii ziliweza simamia kesi takribani milioni 1.2.
-
11:51 - 11:53Hicho ni kiasi kikubwa.
-
11:53 - 11:58(Makofi)
-
11:58 - 12:04Muhimu ni kwamba Gacaca ilihimiza philosophia ya kitamaduni ya Rwanda
-
12:04 - 12:07na majadiliano ya amani na kuungana pamoja tena,
-
12:07 - 12:11kupingana na mawazo ya mateso na adhabu
-
12:11 - 12:15ambayo yanatumika katika mifumo ya nchi za Magharibi hadi siku hizi.
-
12:15 - 12:19Na sio kwa kulinganisha, lakini kwa kusema tu kwamba ilihamasisha sana
-
12:19 - 12:23Mfumo wa jadi wa philosophia ya Rwanda.
-
12:23 - 12:26Na kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Julius Nyerere,
-
12:26 - 12:28raisi wa kwanza wa nchi ya Tanzania --
-
12:28 - 12:29(Makofi)
-
12:29 - 12:32nani amesema huwezi kuwaendeleza watu.
-
12:33 - 12:36Watu watatakiwa kujiendeleza wenyewe.
-
12:37 - 12:38Nakubaliana na Mwalimu.
-
12:38 - 12:40Nimekubaliana
-
12:40 - 12:44kwamba mabadiliko zaidi ya Afrika, maendeleo ya Afrika,
-
12:44 - 12:48yapo katika utambuzi, uhalalishaji na kuweza njia kuu
-
12:48 - 12:53tamaduni zetu wenyewe, uhalisi, asili ya maarifa
-
12:53 - 12:58katika elimu, katika tafiti, katika utengenezaji sera katika sekta.
-
12:59 - 13:01Hii haiwezi kuwa rahisi kwa Afrika.
-
13:01 - 13:05Si rahisi kwa watu waliozoea kuambiwa namna ya kufikiri,
-
13:05 - 13:07nini cha kufanya, jinsi ya kukifanya,
-
13:07 - 13:10watu ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa katika muongozo wa maarifa
-
13:10 - 13:12na dira za wengine,
-
13:12 - 13:14wawe wakoloni,
-
13:14 - 13:17mashirika ya misaada au vyombo vya habari vya kimataifa.
-
13:17 - 13:20Lakini ni jambo tunalotakiwa kufanya ili kupiga hatua.
-
13:20 - 13:23Ninaimarishwa na maneno ya Joseph Shabalala,
-
13:23 - 13:27muanzilishi wa kundi la kwaya la Afrika Kusini liitwalo Ladysmith Black Mambazo.
-
13:27 - 13:32Alisema kwamba kazi iliyopo mbele yetu haiwezi kamwe, kuwa kubwa
-
13:32 - 13:34kuliko nguvu iliyopo ndani yetu.
-
13:34 - 13:36Tunaweza kufanya.
-
13:36 - 13:38Tunaweza kuacha kujidharau.
-
13:38 - 13:42Tunaweza kujifunza kuweka thamani katika uhalisia wetu na maarifa yetu.
-
13:42 - 13:44Asante.
-
13:44 - 13:45Asante sana.
-
13:45 - 13:47(Makofi)
-
13:47 - 13:49Asante. Asante
- Title:
- Namna Afrika inavyoweza kutumia maarifa ya kitamaduni kupiga hatua
- Speaker:
- Chika Ezeanya-Esiobu
- Description:
-
Chika Ezeanya-Esiobu anataka kuona Waafrika wakitumia ubunifu na uvumbuzi wao uliokandamizwa kwa kutambua umuhimu wa tamaduni zao, na maarifa yaliyo halisi. Katika hotuba hii yenye nguvu, anaelezea mifano inayohusu maarifa ya Kiafrika katika kilimo na utungaji sera, akiwaasa Waafrika kupiga hatua kwa kukubali na kuheshimu uhalisia wao.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 14:27
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How Africa can use its traditional knowledge to make progress |