0:00:01.054,0:00:06.534 Miezi kadhaa iliyopita, nilitembelea jiji moja lililopo Afrika Mashariki, 0:00:06.558,0:00:09.547 na tulikuwa tumekwama kwenye msongamano wa magari. 0:00:09.571,0:00:12.613 Na mchuuzi mmoja alikuja ghafla kwenye dirisha langu 0:00:12.637,0:00:15.180 na karatasi ya alfabeti iliyofunguka nusu. 0:00:16.505,0:00:19.324 Niliangalia kwa haraka ile karatasi ya alfabeti, 0:00:19.348,0:00:20.783 na nikamuwaza binti yangu, 0:00:20.807,0:00:23.369 ni namna gani ingekuwa vyema kuitandaza kwenye sakafu 0:00:23.393,0:00:25.233 na kucheza juu yake nikiwa nae 0:00:25.257,0:00:27.446 wakati nikiwa ninamfundisha alfabeti. 0:00:27.470,0:00:30.765 Msongamano ukasogea kidogo, na nikanunua ile nakala haraka, 0:00:30.789,0:00:32.788 na tukaendelea na safari. 0:00:34.165,0:00:37.266 Nilipopata muda wa kuifungua ile karatasi ya alfabeti 0:00:37.290,0:00:39.619 na kuiangalia kwa makini, 0:00:39.643,0:00:42.666 Nilitambua ya kwamba sitaitumia kumfundishia binti yangu. 0:00:43.267,0:00:44.784 Nilijutia ununuzi wangu. 0:00:46.331,0:00:47.673 Kwanini? 0:00:48.338,0:00:51.124 Kutazama karatasi ya alfabeti kunanikumbusha ukweli kwamba 0:00:51.148,0:00:53.524 mambo mengi hayajabadilika 0:00:53.548,0:00:55.971 katika mtaala wa elimu barani Afrika. 0:00:56.729,0:01:00.449 Miongo kadhaa iliyopita, nilifundishwa kutoka katika karatasi hiyohiyo. 0:01:01.312,0:01:03.569 Na kwa sababu ya hilo, nilitaabika kwa miaka. 0:01:04.464,0:01:08.960 Nilitaabika kuweza kukubali uhalisia wangu kutokana na elimu niliyokuwa nikipokea 0:01:08.984,0:01:11.131 shuleni, katika shule nilizosoma. 0:01:12.592,0:01:14.602 Nilikuwa na janga la utambulisho. 0:01:14.626,0:01:17.535 Nikitazama kuangalia uhalisia wangu. 0:01:17.559,0:01:21.805 Niliangalia mababu zangu, nilitazama kizazi changu bila heshima. 0:01:22.205,0:01:27.258 Nilikuwa na subira kidogo kwa yale ambayo maisha yangeweza kunipa kutoka katika mazingira yangu. 0:01:29.045,0:01:30.444 Kwanini? 0:01:31.496,0:01:32.915 "A ni kwa ajili ya Apple." 0:01:34.421,0:01:35.845 "A ni kwa ajili ya Apple." 0:01:37.528,0:01:42.216 "A ni kwa ajili ya Apple" ni kwa ajili ya mtoto katika pande ya dunia 0:01:42.240,0:01:43.972 ambayo wanalima Apple; 0:01:44.751,0:01:46.727 nani aliye na Apple katika mfuko wake wa chakula cha mchana; 0:01:48.235,0:01:51.637 nani ambaye huenda dukani na mama yake na kuona apple jekundu, 0:01:51.661,0:01:55.314 kijani, njano katika kila umbo na rangi na ukubwa. 0:01:56.049,0:01:58.938 Kwa hiyo, kumpa elimu mtoto huyu 0:01:58.962,0:02:01.084 ukitumia karatasi ya alfabeti kama hii 0:02:02.090,0:02:05.131 inatimiza moja ya kazi kuu katika elimu, 0:02:05.155,0:02:08.317 ambayo ni kumkutanisha msomaji 0:02:08.341,0:02:11.714 kuridhika na mazingira ya msomaji 0:02:11.738,0:02:16.380 na udadisi wa kuweza kutafuta zaidi ili kuweza kuongeza thamani. 0:02:17.581,0:02:18.992 Nikijiangalia mimi, 0:02:20.014,0:02:22.326 wakati na mahali nilipokulia Afrika, 0:02:23.613,0:02:25.443 apple ni tunda hadimu. 0:02:26.719,0:02:28.104 Mara mbili au tatu kwa mwaka, 0:02:28.128,0:02:33.495 Nilikuwa napata apple za rangi ya njano zilizo na alama ndogo ndogo za rangi ya kahawia, unajua, 0:02:33.519,0:02:37.416 ikiashiria maelfu ya maili yaliposafiri -- ghalani, katika upangaji 0:02:37.440,0:02:38.614 kunifikia mimi. 0:02:39.575,0:02:41.486 Nilikulia katika jiji 0:02:41.510,0:02:44.510 kwa wazazi ambao wanajiweza kiuchumi, 0:02:44.534,0:02:46.476 kwa hiyo ulikuwa ni uhalisia wangu wa kuheshimika, 0:02:46.500,0:02:48.811 kama vile vile 0:02:48.835,0:02:52.997 mihogo au ugali kwa kawaida hautakuwepo 0:02:53.021,0:02:55.922 katika mlo wa Kimarekani, Kichina au Kihindi, 0:02:56.851,0:02:59.280 apple hazikuwa katika uhalisia wa maisha yangu. 0:03:00.208,0:03:03.256 Kwa hiyo hii ilinifanya nini mimi, 0:03:03.280,0:03:06.964 kunipa elimu kwangu ya "A ni kwa ajili ya apple," 0:03:06.988,0:03:09.447 imefanya elimu kuwa ngumu mno kuelewa. 0:03:09.914,0:03:11.783 Imefanya kitu ambacho kipo na upeo wangu -- 0:03:12.665,0:03:14.571 kitu cha nchi za nje, 0:03:14.595,0:03:18.401 jambo ambalo ningekuwa nikilitafuta mara zote 0:03:18.425,0:03:20.236 uthibitisho wa yale yanayohusiana 0:03:20.260,0:03:23.200 kwa ajili yangu ili kupiga hatua ndani yake na pamoja yake. 0:03:24.109,0:03:27.015 Hiyo ilikuwa ngumu kwa mtoto; 0:03:28.042,0:03:30.765 Nilipokuwa kiumri na kuelimika, 0:03:30.789,0:03:35.853 uhalisia wangu uligawanyika zaidi na elimu yangu. 0:03:36.739,0:03:38.485 Katika historia, nilifundishwa 0:03:38.509,0:03:42.760 kwamba mtalii aliyeitwa Mungo Park aligundua mto wa Niger. 0:03:43.631,0:03:45.424 Na hili lilinikwaza. 0:03:45.448,0:03:47.463 Mababu wa mababu zangu walikulia 0:03:47.487,0:03:49.490 karibu na kingo za mto wa Niger. 0:03:49.514,0:03:51.933 (Kicheko) 0:03:51.957,0:03:58.434 Na ilichukua mtu mwingine kusafiri maelfu ya maili kutoka Ulaya 0:03:58.458,0:04:00.905 kuja kugundua mto ambao upo karibu nao kabisa? 0:04:00.929,0:04:03.370 (Kicheko) 0:04:03.394,0:04:04.551 Hapana! 0:04:04.575,0:04:09.994 (Makofi na shangilio) 0:04:10.018,0:04:11.947 Walitumia vipi muda wao? 0:04:11.971,0:04:13.868 (Kicheko) 0:04:13.892,0:04:16.723 Kucheza bao, kukaanga magimbi, 0:04:16.747,0:04:18.127 kupigana vita vya ukabila? 0:04:18.557,0:04:23.417 Namaanisha, nilijua ya kwamba elimu yangu ilikuwa ikiniandaa kwenda sehemu nyingine 0:04:23.441,0:04:27.208 na kuitumia na katika mazingira mengine ambayo inahusiana nayo. 0:04:27.232,0:04:30.415 Haikuwa kwa ajili ya mazingira yangu, mahali na muda nilipokua. 0:04:31.029,0:04:32.188 Na hali hii iliendelea. 0:04:32.212,0:04:34.105 Na hii philosophia iliimarisha masomo yangu 0:04:34.129,0:04:36.594 muda wote nilipokuwa nikisoma barani Afrika. 0:04:36.618,0:04:40.452 Ilihitaji uzoefu mwingi na baadhi ya mafunzo 0:04:40.476,0:04:43.628 kwa mimi kuanza pata mabadiliko ya mtazamo wangu. 0:04:43.652,0:04:46.616 Nitawaambia baadhi ya mambo makubwa mazuri. 0:04:47.735,0:04:50.090 Nilikuwa nchini Marekani katika jimbo la Washington, DC 0:04:50.114,0:04:52.156 kusomea masomo yangu ya shahada ya uzamivu, 0:04:52.180,0:04:56.057 nilipata nafasi ya kuwa mshauri katika Benki ya Dunia ukanda wa Afrika, 0:04:56.735,0:04:59.491 Kwa hiyo nakumbuka siku moja, 0:04:59.515,0:05:04.163 mkuu wangu wa kazi -- tulikuwa tukiongelea kuhusu mradi fulani, 0:05:04.187,0:05:07.228 na alitaja mradi unaohusiana na Benki ya Dunia, 0:05:07.252,0:05:12.224 mradi mkubwa wa umwagiliaji unaogharimu mamilioni ya dola 0:05:12.248,0:05:13.579 katika Jamhuri ya Niger 0:05:13.603,0:05:16.877 uliokuwa unasuasua uendelezaji wake. 0:05:16.901,0:05:19.244 Alisema mradi huu haupo imara, 0:05:19.268,0:05:23.491 na unawakera wale ambao waliupa mamlaka. 0:05:24.035,0:05:26.824 Lakini aliutaja mradi fulani, 0:05:27.517,0:05:32.434 namna ya umwagiliaji wa kitamaduni ambao ulikuwa na mafanikio makubwa sana 0:05:32.458,0:05:36.155 katika nchi hiyo hiyo ya Jamhuri ya Niger ambapo mradi wa Benki ya Dunia ulikuwa ukifeli. 0:05:36.930,0:05:38.426 Na ikanifanya kuwaza. 0:05:39.281,0:05:41.024 Kwa hiyo nikafanya utafiti zaidi, 0:05:41.984,0:05:44.369 na nikagundua kuhusu Tassa. 0:05:45.775,0:05:49.545 Tassa ni namna ya umwagiliaji wa kienyeji 0:05:49.569,0:05:55.762 ambapo mashimo yenye upana wa kati ya sentimenta 20 hadi 30 na kina cha sentimeta 20 hadi 30 0:05:55.786,0:05:58.660 huchimbwa katika shamba ambalo linaelekea kulimwa. 0:05:59.220,0:06:03.333 Kisha, bwawa dogo hujengwa kuzunguka shamba 0:06:04.296,0:06:07.922 na mazao hupandwa ardhini. 0:06:07.946,0:06:11.250 Kinachotokea ni kwamba mvua itaponyesha, 0:06:11.274,0:06:14.258 mashimo huwa na uwezo wa kutunza maji 0:06:14.282,0:06:18.100 na kupelekea kiasi kwamba mmea kuhitaji maji. 0:06:18.124,0:06:21.390 Mmea unaweza pata maji mengi unavyohitaji 0:06:21.414,0:06:22.984 mpaka muda wa mavuno. 0:06:24.582,0:06:28.275 Niger ni asilimia 75 jangwa, 0:06:28.299,0:06:30.992 na hii kitu cha maisha au kifo, 0:06:31.016,0:06:32.824 na imekuwa ikitumika kwa karne. 0:06:33.384,0:06:35.486 Katika utafiti ambao ulifanyika, 0:06:36.233,0:06:41.646 mashamba mawili yanayofanana yalitumika katika utafiti, 0:06:41.670,0:06:44.301 na shamba moja 0:06:44.325,0:06:46.267 halikutumia njia ya Tassa. 0:06:46.291,0:06:47.458 Mashamba yanayofanana. 0:06:47.482,0:06:50.640 Lingine lilitumia njia ya Tassa. 0:06:51.332,0:06:55.087 Kisha mbegu sawa za mtama zilipandwa katika mashamba yote mawili. 0:06:56.045,0:06:58.252 Wakati wa mavuno, 0:06:58.276,0:07:01.428 Shamba ambalo halikutumia njia ya Tassa 0:07:01.452,0:07:05.623 lilizalisha kilogramu 11 za mtama kwa hektari. 0:07:06.737,0:07:09.032 Shamba lililotumia njia ya Tassa 0:07:09.056,0:07:14.909 lilizalisha kilogramu 553 za mtama kwa hektari. 0:07:15.660,0:07:18.245 (Makofi) 0:07:18.269,0:07:22.182 Niliangalia ule utafiti na nikajitazama. 0:07:22.206,0:07:25.458 Nilisema, "Nimesomea kilimo kwa miaka 12, 0:07:25.482,0:07:28.892 kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato cha sita, kama tuitavyo kwa Afrika Mashariki, 0:07:28.916,0:07:31.262 SS3 kwa Afrika Magharibi au darasa la 12. 0:07:31.286,0:07:32.943 Hakuna aliyewahi kunifundisha 0:07:32.967,0:07:36.773 namna yoyote ya maarifa ya Kiafrika katika ukulima -- 0:07:36.797,0:07:38.591 katika mavuno, katika chochote -- 0:07:38.615,0:07:42.443 ambayo itafanya kazi katika nyakati za kisasa na hakika kufanikiwa, 0:07:42.467,0:07:47.068 pale ambapo jambo fulani lillotolewa nchi za Magharibi limehangaika kufanikiwa. 0:07:47.775,0:07:50.888 Hapo ndipo nilitambua changamoto, 0:07:50.912,0:07:53.491 changamoto ya mtaala wa Kiafrika, 0:07:53.649,0:07:58.447 Na kisha nikaanza lengo langu la kujitolea maisha yangu, kujali maisha yangu ya kazi, 0:07:58.471,0:08:02.763 katika kusoma, kufanya tafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika 0:08:02.787,0:08:05.787 na kuweza kuyawakilisha katika njia kuu 0:08:05.811,0:08:08.658 katika elimu, katika tafiti, sera 0:08:08.682,0:08:10.737 katika sekta na viwanda. 0:08:11.445,0:08:15.289 Maongezi mengine na uzoefu niliopata nikiwa Benki ya Dunia 0:08:15.313,0:08:20.063 Nahisi umenifanya nichukue uamuzi wa mwisho wa wapi nitaelekea, 0:08:20.087,0:08:24.111 ingawa haikuwa tafiti yenye matunda makubwa ya kuielekea, 0:08:24.135,0:08:26.452 lakini ilikuwa kuhusu jambo ambalo nililiamini. 0:08:26.937,0:08:31.563 Kwa hiyo siku moja, mkuu wangu wa kazi alisema kwamba angependelea kwenda Afrika 0:08:31.587,0:08:36.123 kwa ajili ya kujadiliana kuhusu mikopo ya Benki ya Dunia na kufanyia kazi miradi ya Benki hiyo. 0:08:36.614,0:08:38.563 Na nilihamasika, nikamuuliza kwanini. 0:08:38.587,0:08:41.033 Alisema, "Oh, nitapoenda Afrika, 0:08:41.057,0:08:42.766 ni rahisi. 0:08:43.255,0:08:47.913 Ninaandika tu nyaraka za mkopo na dhumuni la mkopo nikiwa Washington, DC, 0:08:47.937,0:08:50.890 Ninakwenda Afrika, na kisha nyaraka zote zinasainiwa. 0:08:50.914,0:08:54.302 Ninapata mpango mzuri kabisa, na kisha narudi ofisini. 0:08:54.326,0:08:56.533 Wakuu wangu wa kazi watanifurahia." 0:08:56.933,0:09:00.620 Lakini kisha akasema, "sipendi kwenda Asia au ..." 0:09:00.644,0:09:04.087 na alitaja nchi fulani, bara la Asia na nchi baadhi. 0:09:04.111,0:09:08.134 "Huwa wananifanya nikae kwa muda mrefu, wakijaribu kutafuta mipango bora kwa nchi zao. 0:09:08.158,0:09:09.334 Huwa wanapata mipango bora. 0:09:09.358,0:09:12.266 Wananiambia, 'Oh, hicho kipengele hakitatufaa 0:09:12.290,0:09:13.897 katika mazingira yetu. 0:09:13.921,0:09:16.894 Si uhalisia wetu. Kimekaa katika mfumo wa Magharibi sana.' 0:09:16.918,0:09:20.029 Na wananiambia, 'Oh, tuna wataalamu wa kutosha 0:09:20.053,0:09:21.256 kwa ajili ya kushughulikia hili. 0:09:21.280,0:09:22.901 Huna wataalamu wa kutosha. 0:09:22.925,0:09:24.078 Tunafahamu lengo letu.' 0:09:24.102,0:09:26.547 Na wanaendelea kupitia haya mambo yote. 0:09:26.571,0:09:29.091 Ikifika muda wa kumaliza, ndiyo, wanapata mpango bora, 0:09:29.115,0:09:32.280 lakini nakuwa nimechoka na sipati mpango mzuri kwa ajili ya benki, 0:09:32.304,0:09:33.483 na sisi tupo katika biashara." 0:09:33.507,0:09:35.302 "Kweli?" Niliwaza akilini, "Sawa." 0:09:35.326,0:09:39.606 Nilipata kipaumbele cha kupata nafasi ya kuwepo katika kikao cha kujadili kuhusu mkopo 0:09:39.630,0:09:41.295 katika nchi ya Kiafrika. 0:09:41.319,0:09:44.139 Kwa hivyo ningefanya kazi ya ushauri wakati wa kiangazi, 0:09:44.163,0:09:46.847 unajua, ukizingatia mimi ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu. 0:09:46.871,0:09:51.203 Na nilisafiri na timu, na timu ya Benki ya Dunia, 0:09:51.227,0:09:55.543 kama mtu ambaye ningesaidia katika masuala ya upangaji wa majadiliano. 0:09:55.567,0:09:58.834 Lakini nilipokuwa wakati wa majadiliano. 0:09:59.730,0:10:04.662 Niliokuwa nao wengi ni toka Ulaya na Marekani, unajua, wakiwa na mimi kutoka Washington, DC. 0:10:04.686,0:10:09.536 Na nilitazama katika meza nikiwaangalia kaka na dada zangu wa Kiafrika. 0:10:09.993,0:10:12.327 Niliona uoga katika nyuso zao. 0:10:12.771,0:10:15.034 Hawakuamini kama walikuwa na chochote cha kuwapa 0:10:15.058,0:10:17.346 vilembwe wa Mungo Park -- 0:10:17.370,0:10:19.987 wamiliki wa "apple" katika "A is for Apple." 0:10:20.011,0:10:22.787 Walikaa na kutazama:"Oh, mtupatie, tuweze tia saini. 0:10:22.811,0:10:24.724 Mnayo maarifa, mnafahamu yote. 0:10:24.748,0:10:26.957 Wapi tunatakiwa kutia saini?Tuonyeshe, tutie saini." 0:10:26.981,0:10:30.017 Hawakuwa na sauti. Hawakujiamini. 0:10:34.544,0:10:35.727 Mniwie radhi. 0:10:36.587,0:10:37.759 Na kwa hiyo, 0:10:39.212,0:10:41.538 Nimekuwa nikifanya hivi kwa muongo. 0:10:41.562,0:10:45.006 Nimekuwa nikifanyia utafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika, 0:10:45.030,0:10:47.274 asilia, halisi, maarifa ya Kiafrika. 0:10:47.298,0:10:50.495 Katika mambo machache ambapo hili suala limehusishwa, 0:10:50.519,0:10:53.003 kumekuwa na mafanikio makubwa ya kusisimua yaliyorekodiwa. 0:10:53.027,0:10:54.564 Nawaza kuhusu Gacaca. 0:10:55.256,0:10:59.988 Gacaca ni mfumo wa kitamaduni wa korti wa nchini Rwanda 0:11:00.012,0:11:02.106 ambao ulitumika baada ya mauaji ya kimbari. 0:11:02.130,0:11:04.561 Mnamo 1994, mauaji yalipoisha, 0:11:06.100,0:11:08.662 Mfumo wa mahakama wa taifa la Rwanda ulikuwa hafifu katika utendaji: 0:11:08.686,0:11:14.212 hakuna majaji, hakuna mawakili kuweza fanyia kazi mamia ya maelfu ya kesi za mauaji ya kimbari. 0:11:14.236,0:11:17.744 Kwa hiyo serikali ya Rwanda ilipata wazo hili 0:11:17.768,0:11:21.163 kufufua mfumo wa jadi wa korti unaofahamika kama Gacaca. 0:11:21.625,0:11:25.072 Gacaca ni mfumo wa jamii wa mahakama, 0:11:25.096,0:11:28.033 ambapo wanajamii hukutana pamoja 0:11:28.057,0:11:31.806 kuchagua waume kwa wake walio na uadilifu 0:11:31.830,0:11:36.340 kusimamia kesi ya jinai zilizofanyika katika jamii yao. 0:11:37.255,0:11:42.732 Kwa wakati Gacaca ilipomaliza kutoa hukumu ya kesi za mauaji ya kimbari mnamo mwaka 2012, 0:11:43.619,0:11:50.594 mahakama 12,000 za kijamii ziliweza simamia kesi takribani milioni 1.2. 0:11:51.334,0:11:52.686 Hicho ni kiasi kikubwa. 0:11:53.169,0:11:58.150 (Makofi) 0:11:58.438,0:12:04.038 Muhimu ni kwamba Gacaca ilihimiza philosophia ya kitamaduni ya Rwanda 0:12:04.062,0:12:07.155 na majadiliano ya amani na kuungana pamoja tena, 0:12:07.179,0:12:11.057 kupingana na mawazo ya mateso na adhabu 0:12:11.081,0:12:14.803 ambayo yanatumika katika mifumo ya nchi za Magharibi hadi siku hizi. 0:12:15.481,0:12:19.376 Na sio kwa kulinganisha, lakini kwa kusema tu kwamba ilihamasisha sana 0:12:19.400,0:12:22.754 Mfumo wa jadi wa philosophia ya Rwanda. 0:12:23.269,0:12:25.866 Na kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Julius Nyerere, 0:12:25.890,0:12:27.631 raisi wa kwanza wa nchi ya Tanzania -- 0:12:27.655,0:12:29.131 (Makofi) 0:12:29.155,0:12:32.331 nani amesema huwezi kuwaendeleza watu. 0:12:32.916,0:12:35.974 Watu watatakiwa kujiendeleza wenyewe. 0:12:36.563,0:12:37.948 Nakubaliana na Mwalimu. 0:12:38.487,0:12:39.875 Nimekubaliana 0:12:39.899,0:12:43.522 kwamba mabadiliko zaidi ya Afrika, maendeleo ya Afrika, 0:12:43.546,0:12:48.325 yapo katika utambuzi, uhalalishaji na kuweza njia kuu 0:12:48.349,0:12:53.338 tamaduni zetu wenyewe, uhalisi, asili ya maarifa 0:12:53.362,0:12:58.233 katika elimu, katika tafiti, katika utengenezaji sera katika sekta. 0:12:58.816,0:13:01.333 Hii haiwezi kuwa rahisi kwa Afrika. 0:13:01.357,0:13:04.821 Si rahisi kwa watu waliozoea kuambiwa namna ya kufikiri, 0:13:04.845,0:13:07.210 nini cha kufanya, jinsi ya kukifanya, 0:13:07.234,0:13:10.388 watu ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa katika muongozo wa maarifa 0:13:10.412,0:13:12.154 na dira za wengine, 0:13:12.178,0:13:13.845 wawe wakoloni, 0:13:13.869,0:13:16.841 mashirika ya misaada au vyombo vya habari vya kimataifa. 0:13:16.865,0:13:20.099 Lakini ni jambo tunalotakiwa kufanya ili kupiga hatua. 0:13:20.123,0:13:23.023 Ninaimarishwa na maneno ya Joseph Shabalala, 0:13:23.047,0:13:26.521 muanzilishi wa kundi la kwaya la Afrika Kusini liitwalo Ladysmith Black Mambazo. 0:13:26.545,0:13:32.232 Alisema kwamba kazi iliyopo mbele yetu haiwezi kamwe, kuwa kubwa 0:13:32.256,0:13:34.409 kuliko nguvu iliyopo ndani yetu. 0:13:34.433,0:13:35.591 Tunaweza kufanya. 0:13:35.615,0:13:38.175 Tunaweza kuacha kujidharau. 0:13:38.199,0:13:42.394 Tunaweza kujifunza kuweka thamani katika uhalisia wetu na maarifa yetu. 0:13:42.418,0:13:43.573 Asante. 0:13:43.597,0:13:45.068 Asante sana. 0:13:45.092,0:13:46.615 (Makofi) 0:13:46.639,0:13:48.841 Asante. Asante