WEBVTT 00:00:01.054 --> 00:00:06.534 Miezi kadhaa iliyopita, nilitembelea jiji moja lililopo Afrika Mashariki, 00:00:06.558 --> 00:00:09.547 na tulikuwa tumekwama kwenye msongamano wa magari. 00:00:09.571 --> 00:00:12.613 Na mchuuzi mmoja alikuja ghafla kwenye dirisha langu 00:00:12.637 --> 00:00:15.180 na karatasi ya alfabeti iliyofunguka nusu. 00:00:16.505 --> 00:00:19.324 Niliangalia kwa haraka ile karatasi ya alfabeti, 00:00:19.348 --> 00:00:20.783 na nikamuwaza binti yangu, 00:00:20.807 --> 00:00:23.369 ni namna gani ingekuwa vyema kuitandaza kwenye sakafu 00:00:23.393 --> 00:00:25.233 na kucheza juu yake nikiwa nae 00:00:25.257 --> 00:00:27.446 wakati nikiwa ninamfundisha alfabeti. 00:00:27.470 --> 00:00:30.765 Msongamano ukasogea kidogo, na nikanunua ile nakala haraka, 00:00:30.789 --> 00:00:32.788 na tukaendelea na safari. NOTE Paragraph 00:00:34.165 --> 00:00:37.266 Nilipopata muda wa kuifungua ile karatasi ya alfabeti 00:00:37.290 --> 00:00:39.619 na kuiangalia kwa makini, 00:00:39.643 --> 00:00:42.666 Nilitambua ya kwamba sitaitumia kumfundishia binti yangu. 00:00:43.267 --> 00:00:44.784 Nilijutia ununuzi wangu. 00:00:46.331 --> 00:00:47.673 Kwanini? 00:00:48.338 --> 00:00:51.124 Kutazama karatasi ya alfabeti kunanikumbusha ukweli kwamba 00:00:51.148 --> 00:00:53.524 mambo mengi hayajabadilika 00:00:53.548 --> 00:00:55.971 katika mtaala wa elimu barani Afrika. 00:00:56.729 --> 00:01:00.449 Miongo kadhaa iliyopita, nilifundishwa kutoka katika karatasi hiyohiyo. 00:01:01.312 --> 00:01:03.569 Na kwa sababu ya hilo, nilitaabika kwa miaka. 00:01:04.464 --> 00:01:08.960 Nilitaabika kuweza kukubali uhalisia wangu kutokana na elimu niliyokuwa nikipokea 00:01:08.984 --> 00:01:11.131 shuleni, katika shule nilizosoma. 00:01:12.592 --> 00:01:14.602 Nilikuwa na janga la utambulisho. 00:01:14.626 --> 00:01:17.535 Nikitazama kuangalia uhalisia wangu. 00:01:17.559 --> 00:01:21.805 Niliangalia mababu zangu, nilitazama kizazi changu bila heshima. 00:01:22.205 --> 00:01:27.258 Nilikuwa na subira kidogo kwa yale ambayo maisha yangeweza kunipa kutoka katika mazingira yangu. NOTE Paragraph 00:01:29.045 --> 00:01:30.444 Kwanini? 00:01:31.496 --> 00:01:32.915 "A ni kwa ajili ya Apple." 00:01:34.421 --> 00:01:35.845 "A ni kwa ajili ya Apple." 00:01:37.528 --> 00:01:42.216 "A ni kwa ajili ya Apple" ni kwa ajili ya mtoto katika pande ya dunia 00:01:42.240 --> 00:01:43.972 ambayo wanalima Apple; 00:01:44.751 --> 00:01:46.727 nani aliye na Apple katika mfuko wake wa chakula cha mchana; 00:01:48.235 --> 00:01:51.637 nani ambaye huenda dukani na mama yake na kuona apple jekundu, 00:01:51.661 --> 00:01:55.314 kijani, njano katika kila umbo na rangi na ukubwa. 00:01:56.049 --> 00:01:58.938 Kwa hiyo, kumpa elimu mtoto huyu 00:01:58.962 --> 00:02:01.084 ukitumia karatasi ya alfabeti kama hii 00:02:02.090 --> 00:02:05.131 inatimiza moja ya kazi kuu katika elimu, 00:02:05.155 --> 00:02:08.317 ambayo ni kumkutanisha msomaji 00:02:08.341 --> 00:02:11.714 kuridhika na mazingira ya msomaji 00:02:11.738 --> 00:02:16.380 na udadisi wa kuweza kutafuta zaidi ili kuweza kuongeza thamani. NOTE Paragraph 00:02:17.581 --> 00:02:18.992 Nikijiangalia mimi, 00:02:20.014 --> 00:02:22.326 wakati na mahali nilipokulia Afrika, 00:02:23.613 --> 00:02:25.443 apple ni tunda hadimu. 00:02:26.719 --> 00:02:28.104 Mara mbili au tatu kwa mwaka, 00:02:28.128 --> 00:02:33.495 Nilikuwa napata apple za rangi ya njano zilizo na alama ndogo ndogo za rangi ya kahawia, unajua, 00:02:33.519 --> 00:02:37.416 ikiashiria maelfu ya maili yaliposafiri -- ghalani, katika upangaji 00:02:37.440 --> 00:02:38.614 kunifikia mimi. 00:02:39.575 --> 00:02:41.486 Nilikulia katika jiji 00:02:41.510 --> 00:02:44.510 kwa wazazi ambao wanajiweza kiuchumi, 00:02:44.534 --> 00:02:46.476 kwa hiyo ulikuwa ni uhalisia wangu wa kuheshimika, 00:02:46.500 --> 00:02:48.811 kama vile vile 00:02:48.835 --> 00:02:52.997 mihogo au ugali kwa kawaida hautakuwepo 00:02:53.021 --> 00:02:55.922 katika mlo wa Kimarekani, Kichina au Kihindi, 00:02:56.851 --> 00:02:59.280 apple hazikuwa katika uhalisia wa maisha yangu. 00:03:00.208 --> 00:03:03.256 Kwa hiyo hii ilinifanya nini mimi, 00:03:03.280 --> 00:03:06.964 kunipa elimu kwangu ya "A ni kwa ajili ya apple," 00:03:06.988 --> 00:03:09.447 imefanya elimu kuwa ngumu mno kuelewa. 00:03:09.914 --> 00:03:11.783 Imefanya kitu ambacho kipo na upeo wangu -- 00:03:12.665 --> 00:03:14.571 kitu cha nchi za nje, 00:03:14.595 --> 00:03:18.401 jambo ambalo ningekuwa nikilitafuta mara zote 00:03:18.425 --> 00:03:20.236 uthibitisho wa yale yanayohusiana 00:03:20.260 --> 00:03:23.200 kwa ajili yangu ili kupiga hatua ndani yake na pamoja yake. 00:03:24.109 --> 00:03:27.015 Hiyo ilikuwa ngumu kwa mtoto; NOTE Paragraph 00:03:28.042 --> 00:03:30.765 Nilipokuwa kiumri na kuelimika, 00:03:30.789 --> 00:03:35.853 uhalisia wangu uligawanyika zaidi na elimu yangu. 00:03:36.739 --> 00:03:38.485 Katika historia, nilifundishwa 00:03:38.509 --> 00:03:42.760 kwamba mtalii aliyeitwa Mungo Park aligundua mto wa Niger. 00:03:43.631 --> 00:03:45.424 Na hili lilinikwaza. 00:03:45.448 --> 00:03:47.463 Mababu wa mababu zangu walikulia 00:03:47.487 --> 00:03:49.490 karibu na kingo za mto wa Niger. NOTE Paragraph 00:03:49.514 --> 00:03:51.933 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:03:51.957 --> 00:03:58.434 Na ilichukua mtu mwingine kusafiri maelfu ya maili kutoka Ulaya 00:03:58.458 --> 00:04:00.905 kuja kugundua mto ambao upo karibu nao kabisa? NOTE Paragraph 00:04:00.929 --> 00:04:03.370 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:03.394 --> 00:04:04.551 Hapana! NOTE Paragraph 00:04:04.575 --> 00:04:09.994 (Makofi na shangilio) NOTE Paragraph 00:04:10.018 --> 00:04:11.947 Walitumia vipi muda wao? NOTE Paragraph 00:04:11.971 --> 00:04:13.868 (Kicheko) NOTE Paragraph 00:04:13.892 --> 00:04:16.723 Kucheza bao, kukaanga magimbi, 00:04:16.747 --> 00:04:18.127 kupigana vita vya ukabila? 00:04:18.557 --> 00:04:23.417 Namaanisha, nilijua ya kwamba elimu yangu ilikuwa ikiniandaa kwenda sehemu nyingine 00:04:23.441 --> 00:04:27.208 na kuitumia na katika mazingira mengine ambayo inahusiana nayo. 00:04:27.232 --> 00:04:30.415 Haikuwa kwa ajili ya mazingira yangu, mahali na muda nilipokua. NOTE Paragraph 00:04:31.029 --> 00:04:32.188 Na hali hii iliendelea. 00:04:32.212 --> 00:04:34.105 Na hii philosophia iliimarisha masomo yangu 00:04:34.129 --> 00:04:36.594 muda wote nilipokuwa nikisoma barani Afrika. 00:04:36.618 --> 00:04:40.452 Ilihitaji uzoefu mwingi na baadhi ya mafunzo 00:04:40.476 --> 00:04:43.628 kwa mimi kuanza pata mabadiliko ya mtazamo wangu. 00:04:43.652 --> 00:04:46.616 Nitawaambia baadhi ya mambo makubwa mazuri. NOTE Paragraph 00:04:47.735 --> 00:04:50.090 Nilikuwa nchini Marekani katika jimbo la Washington, DC 00:04:50.114 --> 00:04:52.156 kusomea masomo yangu ya shahada ya uzamivu, 00:04:52.180 --> 00:04:56.057 nilipata nafasi ya kuwa mshauri katika Benki ya Dunia ukanda wa Afrika, 00:04:56.735 --> 00:04:59.491 Kwa hiyo nakumbuka siku moja, 00:04:59.515 --> 00:05:04.163 mkuu wangu wa kazi -- tulikuwa tukiongelea kuhusu mradi fulani, 00:05:04.187 --> 00:05:07.228 na alitaja mradi unaohusiana na Benki ya Dunia, 00:05:07.252 --> 00:05:12.224 mradi mkubwa wa umwagiliaji unaogharimu mamilioni ya dola 00:05:12.248 --> 00:05:13.579 katika Jamhuri ya Niger 00:05:13.603 --> 00:05:16.877 uliokuwa unasuasua uendelezaji wake. 00:05:16.901 --> 00:05:19.244 Alisema mradi huu haupo imara, 00:05:19.268 --> 00:05:23.491 na unawakera wale ambao waliupa mamlaka. 00:05:24.035 --> 00:05:26.824 Lakini aliutaja mradi fulani, 00:05:27.517 --> 00:05:32.434 namna ya umwagiliaji wa kitamaduni ambao ulikuwa na mafanikio makubwa sana 00:05:32.458 --> 00:05:36.155 katika nchi hiyo hiyo ya Jamhuri ya Niger ambapo mradi wa Benki ya Dunia ulikuwa ukifeli. 00:05:36.930 --> 00:05:38.426 Na ikanifanya kuwaza. 00:05:39.281 --> 00:05:41.024 Kwa hiyo nikafanya utafiti zaidi, 00:05:41.984 --> 00:05:44.369 na nikagundua kuhusu Tassa. NOTE Paragraph 00:05:45.775 --> 00:05:49.545 Tassa ni namna ya umwagiliaji wa kienyeji 00:05:49.569 --> 00:05:55.762 ambapo mashimo yenye upana wa kati ya sentimenta 20 hadi 30 na kina cha sentimeta 20 hadi 30 00:05:55.786 --> 00:05:58.660 huchimbwa katika shamba ambalo linaelekea kulimwa. 00:05:59.220 --> 00:06:03.333 Kisha, bwawa dogo hujengwa kuzunguka shamba 00:06:04.296 --> 00:06:07.922 na mazao hupandwa ardhini. 00:06:07.946 --> 00:06:11.250 Kinachotokea ni kwamba mvua itaponyesha, 00:06:11.274 --> 00:06:14.258 mashimo huwa na uwezo wa kutunza maji 00:06:14.282 --> 00:06:18.100 na kupelekea kiasi kwamba mmea kuhitaji maji. 00:06:18.124 --> 00:06:21.390 Mmea unaweza pata maji mengi unavyohitaji 00:06:21.414 --> 00:06:22.984 mpaka muda wa mavuno. 00:06:24.582 --> 00:06:28.275 Niger ni asilimia 75 jangwa, 00:06:28.299 --> 00:06:30.992 na hii kitu cha maisha au kifo, 00:06:31.016 --> 00:06:32.824 na imekuwa ikitumika kwa karne. 00:06:33.384 --> 00:06:35.486 Katika utafiti ambao ulifanyika, 00:06:36.233 --> 00:06:41.646 mashamba mawili yanayofanana yalitumika katika utafiti, 00:06:41.670 --> 00:06:44.301 na shamba moja 00:06:44.325 --> 00:06:46.267 halikutumia njia ya Tassa. 00:06:46.291 --> 00:06:47.458 Mashamba yanayofanana. 00:06:47.482 --> 00:06:50.640 Lingine lilitumia njia ya Tassa. 00:06:51.332 --> 00:06:55.087 Kisha mbegu sawa za mtama zilipandwa katika mashamba yote mawili. 00:06:56.045 --> 00:06:58.252 Wakati wa mavuno, 00:06:58.276 --> 00:07:01.428 Shamba ambalo halikutumia njia ya Tassa 00:07:01.452 --> 00:07:05.623 lilizalisha kilogramu 11 za mtama kwa hektari. 00:07:06.737 --> 00:07:09.032 Shamba lililotumia njia ya Tassa 00:07:09.056 --> 00:07:14.909 lilizalisha kilogramu 553 za mtama kwa hektari. NOTE Paragraph 00:07:15.660 --> 00:07:18.245 (Makofi) NOTE Paragraph 00:07:18.269 --> 00:07:22.182 Niliangalia ule utafiti na nikajitazama. 00:07:22.206 --> 00:07:25.458 Nilisema, "Nimesomea kilimo kwa miaka 12, 00:07:25.482 --> 00:07:28.892 kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato cha sita, kama tuitavyo kwa Afrika Mashariki, 00:07:28.916 --> 00:07:31.262 SS3 kwa Afrika Magharibi au darasa la 12. 00:07:31.286 --> 00:07:32.943 Hakuna aliyewahi kunifundisha 00:07:32.967 --> 00:07:36.773 namna yoyote ya maarifa ya Kiafrika katika ukulima -- 00:07:36.797 --> 00:07:38.591 katika mavuno, katika chochote -- 00:07:38.615 --> 00:07:42.443 ambayo itafanya kazi katika nyakati za kisasa na hakika kufanikiwa, 00:07:42.467 --> 00:07:47.068 pale ambapo jambo fulani lillotolewa nchi za Magharibi limehangaika kufanikiwa. 00:07:47.775 --> 00:07:50.888 Hapo ndipo nilitambua changamoto, 00:07:50.912 --> 00:07:53.491 changamoto ya mtaala wa Kiafrika, 00:07:53.649 --> 00:07:58.447 Na kisha nikaanza lengo langu la kujitolea maisha yangu, kujali maisha yangu ya kazi, 00:07:58.471 --> 00:08:02.763 katika kusoma, kufanya tafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika 00:08:02.787 --> 00:08:05.787 na kuweza kuyawakilisha katika njia kuu 00:08:05.811 --> 00:08:08.658 katika elimu, katika tafiti, sera 00:08:08.682 --> 00:08:10.737 katika sekta na viwanda. NOTE Paragraph 00:08:11.445 --> 00:08:15.289 Maongezi mengine na uzoefu niliopata nikiwa Benki ya Dunia 00:08:15.313 --> 00:08:20.063 Nahisi umenifanya nichukue uamuzi wa mwisho wa wapi nitaelekea, 00:08:20.087 --> 00:08:24.111 ingawa haikuwa tafiti yenye matunda makubwa ya kuielekea, 00:08:24.135 --> 00:08:26.452 lakini ilikuwa kuhusu jambo ambalo nililiamini. 00:08:26.937 --> 00:08:31.563 Kwa hiyo siku moja, mkuu wangu wa kazi alisema kwamba angependelea kwenda Afrika 00:08:31.587 --> 00:08:36.123 kwa ajili ya kujadiliana kuhusu mikopo ya Benki ya Dunia na kufanyia kazi miradi ya Benki hiyo. 00:08:36.614 --> 00:08:38.563 Na nilihamasika, nikamuuliza kwanini. 00:08:38.587 --> 00:08:41.033 Alisema, "Oh, nitapoenda Afrika, 00:08:41.057 --> 00:08:42.766 ni rahisi. 00:08:43.255 --> 00:08:47.913 Ninaandika tu nyaraka za mkopo na dhumuni la mkopo nikiwa Washington, DC, 00:08:47.937 --> 00:08:50.890 Ninakwenda Afrika, na kisha nyaraka zote zinasainiwa. 00:08:50.914 --> 00:08:54.302 Ninapata mpango mzuri kabisa, na kisha narudi ofisini. 00:08:54.326 --> 00:08:56.533 Wakuu wangu wa kazi watanifurahia." NOTE Paragraph 00:08:56.933 --> 00:09:00.620 Lakini kisha akasema, "sipendi kwenda Asia au ..." 00:09:00.644 --> 00:09:04.087 na alitaja nchi fulani, bara la Asia na nchi baadhi. 00:09:04.111 --> 00:09:08.134 "Huwa wananifanya nikae kwa muda mrefu, wakijaribu kutafuta mipango bora kwa nchi zao. 00:09:08.158 --> 00:09:09.334 Huwa wanapata mipango bora. 00:09:09.358 --> 00:09:12.266 Wananiambia, 'Oh, hicho kipengele hakitatufaa 00:09:12.290 --> 00:09:13.897 katika mazingira yetu. 00:09:13.921 --> 00:09:16.894 Si uhalisia wetu. Kimekaa katika mfumo wa Magharibi sana.' 00:09:16.918 --> 00:09:20.029 Na wananiambia, 'Oh, tuna wataalamu wa kutosha 00:09:20.053 --> 00:09:21.256 kwa ajili ya kushughulikia hili. 00:09:21.280 --> 00:09:22.901 Huna wataalamu wa kutosha. 00:09:22.925 --> 00:09:24.078 Tunafahamu lengo letu.' 00:09:24.102 --> 00:09:26.547 Na wanaendelea kupitia haya mambo yote. 00:09:26.571 --> 00:09:29.091 Ikifika muda wa kumaliza, ndiyo, wanapata mpango bora, 00:09:29.115 --> 00:09:32.280 lakini nakuwa nimechoka na sipati mpango mzuri kwa ajili ya benki, 00:09:32.304 --> 00:09:33.483 na sisi tupo katika biashara." 00:09:33.507 --> 00:09:35.302 "Kweli?" Niliwaza akilini, "Sawa." NOTE Paragraph 00:09:35.326 --> 00:09:39.606 Nilipata kipaumbele cha kupata nafasi ya kuwepo katika kikao cha kujadili kuhusu mkopo 00:09:39.630 --> 00:09:41.295 katika nchi ya Kiafrika. 00:09:41.319 --> 00:09:44.139 Kwa hivyo ningefanya kazi ya ushauri wakati wa kiangazi, 00:09:44.163 --> 00:09:46.847 unajua, ukizingatia mimi ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu. 00:09:46.871 --> 00:09:51.203 Na nilisafiri na timu, na timu ya Benki ya Dunia, 00:09:51.227 --> 00:09:55.543 kama mtu ambaye ningesaidia katika masuala ya upangaji wa majadiliano. 00:09:55.567 --> 00:09:58.834 Lakini nilipokuwa wakati wa majadiliano. 00:09:59.730 --> 00:10:04.662 Niliokuwa nao wengi ni toka Ulaya na Marekani, unajua, wakiwa na mimi kutoka Washington, DC. 00:10:04.686 --> 00:10:09.536 Na nilitazama katika meza nikiwaangalia kaka na dada zangu wa Kiafrika. 00:10:09.993 --> 00:10:12.327 Niliona uoga katika nyuso zao. 00:10:12.771 --> 00:10:15.034 Hawakuamini kama walikuwa na chochote cha kuwapa 00:10:15.058 --> 00:10:17.346 vilembwe wa Mungo Park -- 00:10:17.370 --> 00:10:19.987 wamiliki wa "apple" katika "A is for Apple." 00:10:20.011 --> 00:10:22.787 Walikaa na kutazama:"Oh, mtupatie, tuweze tia saini. 00:10:22.811 --> 00:10:24.724 Mnayo maarifa, mnafahamu yote. 00:10:24.748 --> 00:10:26.957 Wapi tunatakiwa kutia saini?Tuonyeshe, tutie saini." 00:10:26.981 --> 00:10:30.017 Hawakuwa na sauti. Hawakujiamini. NOTE Paragraph 00:10:34.544 --> 00:10:35.727 Mniwie radhi. NOTE Paragraph 00:10:36.587 --> 00:10:37.759 Na kwa hiyo, 00:10:39.212 --> 00:10:41.538 Nimekuwa nikifanya hivi kwa muongo. 00:10:41.562 --> 00:10:45.006 Nimekuwa nikifanyia utafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika, 00:10:45.030 --> 00:10:47.274 asilia, halisi, maarifa ya Kiafrika. 00:10:47.298 --> 00:10:50.495 Katika mambo machache ambapo hili suala limehusishwa, 00:10:50.519 --> 00:10:53.003 kumekuwa na mafanikio makubwa ya kusisimua yaliyorekodiwa. NOTE Paragraph 00:10:53.027 --> 00:10:54.564 Nawaza kuhusu Gacaca. 00:10:55.256 --> 00:10:59.988 Gacaca ni mfumo wa kitamaduni wa korti wa nchini Rwanda 00:11:00.012 --> 00:11:02.106 ambao ulitumika baada ya mauaji ya kimbari. 00:11:02.130 --> 00:11:04.561 Mnamo 1994, mauaji yalipoisha, 00:11:06.100 --> 00:11:08.662 Mfumo wa mahakama wa taifa la Rwanda ulikuwa hafifu katika utendaji: 00:11:08.686 --> 00:11:14.212 hakuna majaji, hakuna mawakili kuweza fanyia kazi mamia ya maelfu ya kesi za mauaji ya kimbari. 00:11:14.236 --> 00:11:17.744 Kwa hiyo serikali ya Rwanda ilipata wazo hili 00:11:17.768 --> 00:11:21.163 kufufua mfumo wa jadi wa korti unaofahamika kama Gacaca. 00:11:21.625 --> 00:11:25.072 Gacaca ni mfumo wa jamii wa mahakama, 00:11:25.096 --> 00:11:28.033 ambapo wanajamii hukutana pamoja 00:11:28.057 --> 00:11:31.806 kuchagua waume kwa wake walio na uadilifu 00:11:31.830 --> 00:11:36.340 kusimamia kesi ya jinai zilizofanyika katika jamii yao. 00:11:37.255 --> 00:11:42.732 Kwa wakati Gacaca ilipomaliza kutoa hukumu ya kesi za mauaji ya kimbari mnamo mwaka 2012, 00:11:43.619 --> 00:11:50.594 mahakama 12,000 za kijamii ziliweza simamia kesi takribani milioni 1.2. 00:11:51.334 --> 00:11:52.686 Hicho ni kiasi kikubwa. NOTE Paragraph 00:11:53.169 --> 00:11:58.150 (Makofi) NOTE Paragraph 00:11:58.438 --> 00:12:04.038 Muhimu ni kwamba Gacaca ilihimiza philosophia ya kitamaduni ya Rwanda 00:12:04.062 --> 00:12:07.155 na majadiliano ya amani na kuungana pamoja tena, 00:12:07.179 --> 00:12:11.057 kupingana na mawazo ya mateso na adhabu 00:12:11.081 --> 00:12:14.803 ambayo yanatumika katika mifumo ya nchi za Magharibi hadi siku hizi. 00:12:15.481 --> 00:12:19.376 Na sio kwa kulinganisha, lakini kwa kusema tu kwamba ilihamasisha sana 00:12:19.400 --> 00:12:22.754 Mfumo wa jadi wa philosophia ya Rwanda. NOTE Paragraph 00:12:23.269 --> 00:12:25.866 Na kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Julius Nyerere, 00:12:25.890 --> 00:12:27.631 raisi wa kwanza wa nchi ya Tanzania -- NOTE Paragraph 00:12:27.655 --> 00:12:29.131 (Makofi) NOTE Paragraph 00:12:29.155 --> 00:12:32.331 nani amesema huwezi kuwaendeleza watu. 00:12:32.916 --> 00:12:35.974 Watu watatakiwa kujiendeleza wenyewe. 00:12:36.563 --> 00:12:37.948 Nakubaliana na Mwalimu. 00:12:38.487 --> 00:12:39.875 Nimekubaliana 00:12:39.899 --> 00:12:43.522 kwamba mabadiliko zaidi ya Afrika, maendeleo ya Afrika, 00:12:43.546 --> 00:12:48.325 yapo katika utambuzi, uhalalishaji na kuweza njia kuu 00:12:48.349 --> 00:12:53.338 tamaduni zetu wenyewe, uhalisi, asili ya maarifa 00:12:53.362 --> 00:12:58.233 katika elimu, katika tafiti, katika utengenezaji sera katika sekta. 00:12:58.816 --> 00:13:01.333 Hii haiwezi kuwa rahisi kwa Afrika. 00:13:01.357 --> 00:13:04.821 Si rahisi kwa watu waliozoea kuambiwa namna ya kufikiri, 00:13:04.845 --> 00:13:07.210 nini cha kufanya, jinsi ya kukifanya, 00:13:07.234 --> 00:13:10.388 watu ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa katika muongozo wa maarifa 00:13:10.412 --> 00:13:12.154 na dira za wengine, 00:13:12.178 --> 00:13:13.845 wawe wakoloni, 00:13:13.869 --> 00:13:16.841 mashirika ya misaada au vyombo vya habari vya kimataifa. 00:13:16.865 --> 00:13:20.099 Lakini ni jambo tunalotakiwa kufanya ili kupiga hatua. NOTE Paragraph 00:13:20.123 --> 00:13:23.023 Ninaimarishwa na maneno ya Joseph Shabalala, 00:13:23.047 --> 00:13:26.521 muanzilishi wa kundi la kwaya la Afrika Kusini liitwalo Ladysmith Black Mambazo. 00:13:26.545 --> 00:13:32.232 Alisema kwamba kazi iliyopo mbele yetu haiwezi kamwe, kuwa kubwa 00:13:32.256 --> 00:13:34.409 kuliko nguvu iliyopo ndani yetu. 00:13:34.433 --> 00:13:35.591 Tunaweza kufanya. 00:13:35.615 --> 00:13:38.175 Tunaweza kuacha kujidharau. 00:13:38.199 --> 00:13:42.394 Tunaweza kujifunza kuweka thamani katika uhalisia wetu na maarifa yetu. NOTE Paragraph 00:13:42.418 --> 00:13:43.573 Asante. NOTE Paragraph 00:13:43.597 --> 00:13:45.068 Asante sana. NOTE Paragraph 00:13:45.092 --> 00:13:46.615 (Makofi) NOTE Paragraph 00:13:46.639 --> 00:13:48.841 Asante. Asante