Return to Video

Namna Afrika inavyoweza kutumia maarifa ya kitamaduni kupiga hatua

  • 0:01 - 0:07
    Miezi kadhaa iliyopita, nilitembelea jiji moja lililopo Afrika Mashariki,
  • 0:07 - 0:10
    na tulikuwa tumekwama kwenye msongamano wa magari.
  • 0:10 - 0:13
    Na mchuuzi mmoja alikuja ghafla kwenye dirisha langu
  • 0:13 - 0:15
    na karatasi ya alfabeti iliyofunguka nusu.
  • 0:17 - 0:19
    Niliangalia kwa haraka ile karatasi ya alfabeti,
  • 0:19 - 0:21
    na nikamuwaza binti yangu,
  • 0:21 - 0:23
    ni namna gani ingekuwa vyema kuitandaza kwenye sakafu
  • 0:23 - 0:25
    na kucheza juu yake nikiwa nae
  • 0:25 - 0:27
    wakati nikiwa ninamfundisha alfabeti.
  • 0:27 - 0:31
    Msongamano ukasogea kidogo, na nikanunua ile nakala haraka,
  • 0:31 - 0:33
    na tukaendelea na safari.
  • 0:34 - 0:37
    Nilipopata muda wa kuifungua ile karatasi ya alfabeti
  • 0:37 - 0:40
    na kuiangalia kwa makini,
  • 0:40 - 0:43
    Nilitambua ya kwamba sitaitumia kumfundishia binti yangu.
  • 0:43 - 0:45
    Nilijutia ununuzi wangu.
  • 0:46 - 0:48
    Kwanini?
  • 0:48 - 0:51
    Kutazama karatasi ya alfabeti kunanikumbusha ukweli kwamba
  • 0:51 - 0:54
    mambo mengi hayajabadilika
  • 0:54 - 0:56
    katika mtaala wa elimu barani Afrika.
  • 0:57 - 1:00
    Miongo kadhaa iliyopita, nilifundishwa kutoka katika karatasi hiyohiyo.
  • 1:01 - 1:04
    Na kwa sababu ya hilo, nilitaabika kwa miaka.
  • 1:04 - 1:09
    Nilitaabika kuweza kukubali uhalisia wangu kutokana na elimu niliyokuwa nikipokea
  • 1:09 - 1:11
    shuleni, katika shule nilizosoma.
  • 1:13 - 1:15
    Nilikuwa na janga la utambulisho.
  • 1:15 - 1:18
    Nikitazama kuangalia uhalisia wangu.
  • 1:18 - 1:22
    Niliangalia mababu zangu, nilitazama kizazi changu bila heshima.
  • 1:22 - 1:27
    Nilikuwa na subira kidogo kwa yale ambayo maisha yangeweza kunipa kutoka katika mazingira yangu.
  • 1:29 - 1:30
    Kwanini?
  • 1:31 - 1:33
    "A ni kwa ajili ya Apple."
  • 1:34 - 1:36
    "A ni kwa ajili ya Apple."
  • 1:38 - 1:42
    "A ni kwa ajili ya Apple" ni kwa ajili ya mtoto katika pande ya dunia
  • 1:42 - 1:44
    ambayo wanalima Apple;
  • 1:45 - 1:47
    nani aliye na Apple katika mfuko wake wa chakula cha mchana;
  • 1:48 - 1:52
    nani ambaye huenda dukani na mama yake na kuona apple jekundu,
  • 1:52 - 1:55
    kijani, njano katika kila umbo na rangi na ukubwa.
  • 1:56 - 1:59
    Kwa hiyo, kumpa elimu mtoto huyu
  • 1:59 - 2:01
    ukitumia karatasi ya alfabeti kama hii
  • 2:02 - 2:05
    inatimiza moja ya kazi kuu katika elimu,
  • 2:05 - 2:08
    ambayo ni kumkutanisha msomaji
  • 2:08 - 2:12
    kuridhika na mazingira ya msomaji
  • 2:12 - 2:16
    na udadisi wa kuweza kutafuta zaidi ili kuweza kuongeza thamani.
  • 2:18 - 2:19
    Nikijiangalia mimi,
  • 2:20 - 2:22
    wakati na mahali nilipokulia Afrika,
  • 2:24 - 2:25
    apple ni tunda hadimu.
  • 2:27 - 2:28
    Mara mbili au tatu kwa mwaka,
  • 2:28 - 2:33
    Nilikuwa napata apple za rangi ya njano zilizo na alama ndogo ndogo za rangi ya kahawia, unajua,
  • 2:34 - 2:37
    ikiashiria maelfu ya maili yaliposafiri -- ghalani, katika upangaji
  • 2:37 - 2:39
    kunifikia mimi.
  • 2:40 - 2:41
    Nilikulia katika jiji
  • 2:42 - 2:45
    kwa wazazi ambao wanajiweza kiuchumi,
  • 2:45 - 2:46
    kwa hiyo ulikuwa ni uhalisia wangu wa kuheshimika,
  • 2:46 - 2:49
    kama vile vile
  • 2:49 - 2:53
    mihogo au ugali kwa kawaida hautakuwepo
  • 2:53 - 2:56
    katika mlo wa Kimarekani, Kichina au Kihindi,
  • 2:57 - 2:59
    apple hazikuwa katika uhalisia wa maisha yangu.
  • 3:00 - 3:03
    Kwa hiyo hii ilinifanya nini mimi,
  • 3:03 - 3:07
    kunipa elimu kwangu ya "A ni kwa ajili ya apple,"
  • 3:07 - 3:09
    imefanya elimu kuwa ngumu mno kuelewa.
  • 3:10 - 3:12
    Imefanya kitu ambacho kipo na upeo wangu --
  • 3:13 - 3:15
    kitu cha nchi za nje,
  • 3:15 - 3:18
    jambo ambalo ningekuwa nikilitafuta mara zote
  • 3:18 - 3:20
    uthibitisho wa yale yanayohusiana
  • 3:20 - 3:23
    kwa ajili yangu ili kupiga hatua ndani yake na pamoja yake.
  • 3:24 - 3:27
    Hiyo ilikuwa ngumu kwa mtoto;
  • 3:28 - 3:31
    Nilipokuwa kiumri na kuelimika,
  • 3:31 - 3:36
    uhalisia wangu uligawanyika zaidi na elimu yangu.
  • 3:37 - 3:38
    Katika historia, nilifundishwa
  • 3:39 - 3:43
    kwamba mtalii aliyeitwa Mungo Park aligundua mto wa Niger.
  • 3:44 - 3:45
    Na hili lilinikwaza.
  • 3:45 - 3:47
    Mababu wa mababu zangu walikulia
  • 3:47 - 3:49
    karibu na kingo za mto wa Niger.
  • 3:50 - 3:52
    (Kicheko)
  • 3:52 - 3:58
    Na ilichukua mtu mwingine kusafiri maelfu ya maili kutoka Ulaya
  • 3:58 - 4:01
    kuja kugundua mto ambao upo karibu nao kabisa?
  • 4:01 - 4:03
    (Kicheko)
  • 4:03 - 4:05
    Hapana!
  • 4:05 - 4:10
    (Makofi na shangilio)
  • 4:10 - 4:12
    Walitumia vipi muda wao?
  • 4:12 - 4:14
    (Kicheko)
  • 4:14 - 4:17
    Kucheza bao, kukaanga magimbi,
  • 4:17 - 4:18
    kupigana vita vya ukabila?
  • 4:19 - 4:23
    Namaanisha, nilijua ya kwamba elimu yangu ilikuwa ikiniandaa kwenda sehemu nyingine
  • 4:23 - 4:27
    na kuitumia na katika mazingira mengine ambayo inahusiana nayo.
  • 4:27 - 4:30
    Haikuwa kwa ajili ya mazingira yangu, mahali na muda nilipokua.
  • 4:31 - 4:32
    Na hali hii iliendelea.
  • 4:32 - 4:34
    Na hii philosophia iliimarisha masomo yangu
  • 4:34 - 4:37
    muda wote nilipokuwa nikisoma barani Afrika.
  • 4:37 - 4:40
    Ilihitaji uzoefu mwingi na baadhi ya mafunzo
  • 4:40 - 4:44
    kwa mimi kuanza pata mabadiliko ya mtazamo wangu.
  • 4:44 - 4:47
    Nitawaambia baadhi ya mambo makubwa mazuri.
  • 4:48 - 4:50
    Nilikuwa nchini Marekani katika jimbo la Washington, DC
  • 4:50 - 4:52
    kusomea masomo yangu ya shahada ya uzamivu,
  • 4:52 - 4:56
    nilipata nafasi ya kuwa mshauri katika Benki ya Dunia ukanda wa Afrika,
  • 4:57 - 4:59
    Kwa hiyo nakumbuka siku moja,
  • 5:00 - 5:04
    mkuu wangu wa kazi -- tulikuwa tukiongelea kuhusu mradi fulani,
  • 5:04 - 5:07
    na alitaja mradi unaohusiana na Benki ya Dunia,
  • 5:07 - 5:12
    mradi mkubwa wa umwagiliaji unaogharimu mamilioni ya dola
  • 5:12 - 5:14
    katika Jamhuri ya Niger
  • 5:14 - 5:17
    uliokuwa unasuasua uendelezaji wake.
  • 5:17 - 5:19
    Alisema mradi huu haupo imara,
  • 5:19 - 5:23
    na unawakera wale ambao waliupa mamlaka.
  • 5:24 - 5:27
    Lakini aliutaja mradi fulani,
  • 5:28 - 5:32
    namna ya umwagiliaji wa kitamaduni ambao ulikuwa na mafanikio makubwa sana
  • 5:32 - 5:36
    katika nchi hiyo hiyo ya Jamhuri ya Niger ambapo mradi wa Benki ya Dunia ulikuwa ukifeli.
  • 5:37 - 5:38
    Na ikanifanya kuwaza.
  • 5:39 - 5:41
    Kwa hiyo nikafanya utafiti zaidi,
  • 5:42 - 5:44
    na nikagundua kuhusu Tassa.
  • 5:46 - 5:50
    Tassa ni namna ya umwagiliaji wa kienyeji
  • 5:50 - 5:56
    ambapo mashimo yenye upana wa kati ya sentimenta 20 hadi 30 na kina cha sentimeta 20 hadi 30
  • 5:56 - 5:59
    huchimbwa katika shamba ambalo linaelekea kulimwa.
  • 5:59 - 6:03
    Kisha, bwawa dogo hujengwa kuzunguka shamba
  • 6:04 - 6:08
    na mazao hupandwa ardhini.
  • 6:08 - 6:11
    Kinachotokea ni kwamba mvua itaponyesha,
  • 6:11 - 6:14
    mashimo huwa na uwezo wa kutunza maji
  • 6:14 - 6:18
    na kupelekea kiasi kwamba mmea kuhitaji maji.
  • 6:18 - 6:21
    Mmea unaweza pata maji mengi unavyohitaji
  • 6:21 - 6:23
    mpaka muda wa mavuno.
  • 6:25 - 6:28
    Niger ni asilimia 75 jangwa,
  • 6:28 - 6:31
    na hii kitu cha maisha au kifo,
  • 6:31 - 6:33
    na imekuwa ikitumika kwa karne.
  • 6:33 - 6:35
    Katika utafiti ambao ulifanyika,
  • 6:36 - 6:42
    mashamba mawili yanayofanana yalitumika katika utafiti,
  • 6:42 - 6:44
    na shamba moja
  • 6:44 - 6:46
    halikutumia njia ya Tassa.
  • 6:46 - 6:47
    Mashamba yanayofanana.
  • 6:47 - 6:51
    Lingine lilitumia njia ya Tassa.
  • 6:51 - 6:55
    Kisha mbegu sawa za mtama zilipandwa katika mashamba yote mawili.
  • 6:56 - 6:58
    Wakati wa mavuno,
  • 6:58 - 7:01
    Shamba ambalo halikutumia njia ya Tassa
  • 7:01 - 7:06
    lilizalisha kilogramu 11 za mtama kwa hektari.
  • 7:07 - 7:09
    Shamba lililotumia njia ya Tassa
  • 7:09 - 7:15
    lilizalisha kilogramu 553 za mtama kwa hektari.
  • 7:16 - 7:18
    (Makofi)
  • 7:18 - 7:22
    Niliangalia ule utafiti na nikajitazama.
  • 7:22 - 7:25
    Nilisema, "Nimesomea kilimo kwa miaka 12,
  • 7:25 - 7:29
    kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato cha sita, kama tuitavyo kwa Afrika Mashariki,
  • 7:29 - 7:31
    SS3 kwa Afrika Magharibi au darasa la 12.
  • 7:31 - 7:33
    Hakuna aliyewahi kunifundisha
  • 7:33 - 7:37
    namna yoyote ya maarifa ya Kiafrika katika ukulima --
  • 7:37 - 7:39
    katika mavuno, katika chochote --
  • 7:39 - 7:42
    ambayo itafanya kazi katika nyakati za kisasa na hakika kufanikiwa,
  • 7:42 - 7:47
    pale ambapo jambo fulani lillotolewa nchi za Magharibi limehangaika kufanikiwa.
  • 7:48 - 7:51
    Hapo ndipo nilitambua changamoto,
  • 7:51 - 7:53
    changamoto ya mtaala wa Kiafrika,
  • 7:54 - 7:58
    Na kisha nikaanza lengo langu la kujitolea maisha yangu, kujali maisha yangu ya kazi,
  • 7:58 - 8:03
    katika kusoma, kufanya tafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika
  • 8:03 - 8:06
    na kuweza kuyawakilisha katika njia kuu
  • 8:06 - 8:09
    katika elimu, katika tafiti, sera
  • 8:09 - 8:11
    katika sekta na viwanda.
  • 8:11 - 8:15
    Maongezi mengine na uzoefu niliopata nikiwa Benki ya Dunia
  • 8:15 - 8:20
    Nahisi umenifanya nichukue uamuzi wa mwisho wa wapi nitaelekea,
  • 8:20 - 8:24
    ingawa haikuwa tafiti yenye matunda makubwa ya kuielekea,
  • 8:24 - 8:26
    lakini ilikuwa kuhusu jambo ambalo nililiamini.
  • 8:27 - 8:32
    Kwa hiyo siku moja, mkuu wangu wa kazi alisema kwamba angependelea kwenda Afrika
  • 8:32 - 8:36
    kwa ajili ya kujadiliana kuhusu mikopo ya Benki ya Dunia na kufanyia kazi miradi ya Benki hiyo.
  • 8:37 - 8:39
    Na nilihamasika, nikamuuliza kwanini.
  • 8:39 - 8:41
    Alisema, "Oh, nitapoenda Afrika,
  • 8:41 - 8:43
    ni rahisi.
  • 8:43 - 8:48
    Ninaandika tu nyaraka za mkopo na dhumuni la mkopo nikiwa Washington, DC,
  • 8:48 - 8:51
    Ninakwenda Afrika, na kisha nyaraka zote zinasainiwa.
  • 8:51 - 8:54
    Ninapata mpango mzuri kabisa, na kisha narudi ofisini.
  • 8:54 - 8:57
    Wakuu wangu wa kazi watanifurahia."
  • 8:57 - 9:01
    Lakini kisha akasema, "sipendi kwenda Asia au ..."
  • 9:01 - 9:04
    na alitaja nchi fulani, bara la Asia na nchi baadhi.
  • 9:04 - 9:08
    "Huwa wananifanya nikae kwa muda mrefu, wakijaribu kutafuta mipango bora kwa nchi zao.
  • 9:08 - 9:09
    Huwa wanapata mipango bora.
  • 9:09 - 9:12
    Wananiambia, 'Oh, hicho kipengele hakitatufaa
  • 9:12 - 9:14
    katika mazingira yetu.
  • 9:14 - 9:17
    Si uhalisia wetu. Kimekaa katika mfumo wa Magharibi sana.'
  • 9:17 - 9:20
    Na wananiambia, 'Oh, tuna wataalamu wa kutosha
  • 9:20 - 9:21
    kwa ajili ya kushughulikia hili.
  • 9:21 - 9:23
    Huna wataalamu wa kutosha.
  • 9:23 - 9:24
    Tunafahamu lengo letu.'
  • 9:24 - 9:27
    Na wanaendelea kupitia haya mambo yote.
  • 9:27 - 9:29
    Ikifika muda wa kumaliza, ndiyo, wanapata mpango bora,
  • 9:29 - 9:32
    lakini nakuwa nimechoka na sipati mpango mzuri kwa ajili ya benki,
  • 9:32 - 9:33
    na sisi tupo katika biashara."
  • 9:34 - 9:35
    "Kweli?" Niliwaza akilini, "Sawa."
  • 9:35 - 9:40
    Nilipata kipaumbele cha kupata nafasi ya kuwepo katika kikao cha kujadili kuhusu mkopo
  • 9:40 - 9:41
    katika nchi ya Kiafrika.
  • 9:41 - 9:44
    Kwa hivyo ningefanya kazi ya ushauri wakati wa kiangazi,
  • 9:44 - 9:47
    unajua, ukizingatia mimi ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu.
  • 9:47 - 9:51
    Na nilisafiri na timu, na timu ya Benki ya Dunia,
  • 9:51 - 9:56
    kama mtu ambaye ningesaidia katika masuala ya upangaji wa majadiliano.
  • 9:56 - 9:59
    Lakini nilipokuwa wakati wa majadiliano.
  • 10:00 - 10:05
    Niliokuwa nao wengi ni toka Ulaya na Marekani, unajua, wakiwa na mimi kutoka Washington, DC.
  • 10:05 - 10:10
    Na nilitazama katika meza nikiwaangalia kaka na dada zangu wa Kiafrika.
  • 10:10 - 10:12
    Niliona uoga katika nyuso zao.
  • 10:13 - 10:15
    Hawakuamini kama walikuwa na chochote cha kuwapa
  • 10:15 - 10:17
    vilembwe wa Mungo Park --
  • 10:17 - 10:20
    wamiliki wa "apple" katika "A is for Apple."
  • 10:20 - 10:23
    Walikaa na kutazama:"Oh, mtupatie, tuweze tia saini.
  • 10:23 - 10:25
    Mnayo maarifa, mnafahamu yote.
  • 10:25 - 10:27
    Wapi tunatakiwa kutia saini?Tuonyeshe, tutie saini."
  • 10:27 - 10:30
    Hawakuwa na sauti. Hawakujiamini.
  • 10:35 - 10:36
    Mniwie radhi.
  • 10:37 - 10:38
    Na kwa hiyo,
  • 10:39 - 10:42
    Nimekuwa nikifanya hivi kwa muongo.
  • 10:42 - 10:45
    Nimekuwa nikifanyia utafiti kuhusu mfumo wa maarifa ya Kiafrika,
  • 10:45 - 10:47
    asilia, halisi, maarifa ya Kiafrika.
  • 10:47 - 10:50
    Katika mambo machache ambapo hili suala limehusishwa,
  • 10:51 - 10:53
    kumekuwa na mafanikio makubwa ya kusisimua yaliyorekodiwa.
  • 10:53 - 10:55
    Nawaza kuhusu Gacaca.
  • 10:55 - 11:00
    Gacaca ni mfumo wa kitamaduni wa korti wa nchini Rwanda
  • 11:00 - 11:02
    ambao ulitumika baada ya mauaji ya kimbari.
  • 11:02 - 11:05
    Mnamo 1994, mauaji yalipoisha,
  • 11:06 - 11:09
    Mfumo wa mahakama wa taifa la Rwanda ulikuwa hafifu katika utendaji:
  • 11:09 - 11:14
    hakuna majaji, hakuna mawakili kuweza fanyia kazi mamia ya maelfu ya kesi za mauaji ya kimbari.
  • 11:14 - 11:18
    Kwa hiyo serikali ya Rwanda ilipata wazo hili
  • 11:18 - 11:21
    kufufua mfumo wa jadi wa korti unaofahamika kama Gacaca.
  • 11:22 - 11:25
    Gacaca ni mfumo wa jamii wa mahakama,
  • 11:25 - 11:28
    ambapo wanajamii hukutana pamoja
  • 11:28 - 11:32
    kuchagua waume kwa wake walio na uadilifu
  • 11:32 - 11:36
    kusimamia kesi ya jinai zilizofanyika katika jamii yao.
  • 11:37 - 11:43
    Kwa wakati Gacaca ilipomaliza kutoa hukumu ya kesi za mauaji ya kimbari mnamo mwaka 2012,
  • 11:44 - 11:51
    mahakama 12,000 za kijamii ziliweza simamia kesi takribani milioni 1.2.
  • 11:51 - 11:53
    Hicho ni kiasi kikubwa.
  • 11:53 - 11:58
    (Makofi)
  • 11:58 - 12:04
    Muhimu ni kwamba Gacaca ilihimiza philosophia ya kitamaduni ya Rwanda
  • 12:04 - 12:07
    na majadiliano ya amani na kuungana pamoja tena,
  • 12:07 - 12:11
    kupingana na mawazo ya mateso na adhabu
  • 12:11 - 12:15
    ambayo yanatumika katika mifumo ya nchi za Magharibi hadi siku hizi.
  • 12:15 - 12:19
    Na sio kwa kulinganisha, lakini kwa kusema tu kwamba ilihamasisha sana
  • 12:19 - 12:23
    Mfumo wa jadi wa philosophia ya Rwanda.
  • 12:23 - 12:26
    Na kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Julius Nyerere,
  • 12:26 - 12:28
    raisi wa kwanza wa nchi ya Tanzania --
  • 12:28 - 12:29
    (Makofi)
  • 12:29 - 12:32
    nani amesema huwezi kuwaendeleza watu.
  • 12:33 - 12:36
    Watu watatakiwa kujiendeleza wenyewe.
  • 12:37 - 12:38
    Nakubaliana na Mwalimu.
  • 12:38 - 12:40
    Nimekubaliana
  • 12:40 - 12:44
    kwamba mabadiliko zaidi ya Afrika, maendeleo ya Afrika,
  • 12:44 - 12:48
    yapo katika utambuzi, uhalalishaji na kuweza njia kuu
  • 12:48 - 12:53
    tamaduni zetu wenyewe, uhalisi, asili ya maarifa
  • 12:53 - 12:58
    katika elimu, katika tafiti, katika utengenezaji sera katika sekta.
  • 12:59 - 13:01
    Hii haiwezi kuwa rahisi kwa Afrika.
  • 13:01 - 13:05
    Si rahisi kwa watu waliozoea kuambiwa namna ya kufikiri,
  • 13:05 - 13:07
    nini cha kufanya, jinsi ya kukifanya,
  • 13:07 - 13:10
    watu ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa katika muongozo wa maarifa
  • 13:10 - 13:12
    na dira za wengine,
  • 13:12 - 13:14
    wawe wakoloni,
  • 13:14 - 13:17
    mashirika ya misaada au vyombo vya habari vya kimataifa.
  • 13:17 - 13:20
    Lakini ni jambo tunalotakiwa kufanya ili kupiga hatua.
  • 13:20 - 13:23
    Ninaimarishwa na maneno ya Joseph Shabalala,
  • 13:23 - 13:27
    muanzilishi wa kundi la kwaya la Afrika Kusini liitwalo Ladysmith Black Mambazo.
  • 13:27 - 13:32
    Alisema kwamba kazi iliyopo mbele yetu haiwezi kamwe, kuwa kubwa
  • 13:32 - 13:34
    kuliko nguvu iliyopo ndani yetu.
  • 13:34 - 13:36
    Tunaweza kufanya.
  • 13:36 - 13:38
    Tunaweza kuacha kujidharau.
  • 13:38 - 13:42
    Tunaweza kujifunza kuweka thamani katika uhalisia wetu na maarifa yetu.
  • 13:42 - 13:44
    Asante.
  • 13:44 - 13:45
    Asante sana.
  • 13:45 - 13:47
    (Makofi)
  • 13:47 - 13:49
    Asante. Asante
Title:
Namna Afrika inavyoweza kutumia maarifa ya kitamaduni kupiga hatua
Speaker:
Chika Ezeanya-Esiobu
Description:

Chika Ezeanya-Esiobu anataka kuona Waafrika wakitumia ubunifu na uvumbuzi wao uliokandamizwa kwa kutambua umuhimu wa tamaduni zao, na maarifa yaliyo halisi. Katika hotuba hii yenye nguvu, anaelezea mifano inayohusu maarifa ya Kiafrika katika kilimo na utungaji sera, akiwaasa Waafrika kupiga hatua kwa kukubali na kuheshimu uhalisia wao.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
14:27

Swahili subtitles

Revisions