< Return to Video

MAOMBI YENYE UPAKO ili KUFUNGUA MALANGO YA MAFURIKO YA MBINGUNI KATIKA MAISHA YAKO!

  • 0:00 - 0:13
    Ninazungumza na hiyo nguvu ya kipepo inayosumbua hisia zako. Toka nje sasa hivi!
  • 0:13 - 0:25
    Roho hiyo nyuma ya wasiwasi, woga, huzuni - toka nje, kwa jina la Yesu Kristo!
  • 0:27 - 0:41
    Watu wa Mungu, ni hali ipi inayowazunguka leo?
  • 0:41 - 0:49
    Moyo wako umeumizwa au umevunjika
  • 0:49 - 1:00
    kwa sababu ya maswala ambayo maisha yamekukabili au yaliyosababishwa na chaguzi zisizo sahihi?
  • 1:00 - 1:05
    Niko hapa leo kukuambia ukweli huu.
  • 1:05 - 1:16
    Kuna uponyaji na utimilifu unaopatikana kwa ajili yako katika Yesu Kristo.
  • 1:16 - 1:26
    Labda sijui ni nini kinasumbua roho yako kwa wakati huu
  • 1:26 - 1:31
    unapoungana na na huduma hii, lakini jambo moja najua -
  • 1:31 - 1:39
    kuna pumziko katika Kristo Yesu kwa ajili yako.
  • 1:39 - 1:44
    Lakini zingatia hili.
  • 1:44 - 1:50
    Ni Mmiliki wa nafsi yako pekee ndiye anayeweza kutatua masuala ya nafsi yako.
  • 1:50 - 1:59
    Ni Muumba wa moyo wako pekee ndiye anayeweza kurekebisha masuala ya moyo wako.
  • 1:59 - 2:12
    Kutafuta misaada katika mwili, kwa juu tu katika uso, kutasababisha tu shida zaidi.
  • 2:12 - 2:16
    Kutakuacha ukiwa na sonona zaidi.
  • 2:16 - 2:23
    Ni Mmiliki wa nafsi yako pekee ndiye anayewez akutatua masuala ya nafsi yako.
  • 2:23 - 2:27
    Na ndio maana nakuambia leo hongera
  • 2:27 - 2:30
    kwa sababu umefanya chaguo sahihi.
  • 2:30 - 2:36
    Umechagua kutafuta uhusikaji wa Mungu.
  • 2:36 - 2:42
    Ndiyo maana uko hapa kwa wakati huu, umeunganishwa kwenye huduma hii.
  • 2:42 - 2:47
    Kwa hivyo swali sasa hivi ni hili.
  • 2:47 - 2:56
    Je, hali ya moyo wako ikoje tunapokaribia kuomba pamoja?
  • 2:56 - 3:01
    Je, moyo wako uko wazi kwa ajili ya Roho Mtakatifu?
  • 3:01 - 3:05
    Je, roho yako iko huru?
  • 3:05 - 3:10
    Au roho yako bado imefungwa?
  • 3:10 - 3:21
    Umefungwa kwa maumivu ya siku za nyuma, uchungu, kutosamehe au chuki?
  • 3:21 - 3:30
    Kwa sababu kinachofunga roho yako kinaweza kuwa kinazuia baraka zako.
  • 3:30 - 3:40
    Ni wakati sasa wa wewe kuachana na maumivu yote ya zamani.
  • 3:40 - 3:43
    Achana na huko kutosamehe.
  • 3:43 - 3:53
    Acha uchungu huo na umkaribishe Roho Mtakatifu aingie moyoni mwako sasa hivi.
  • 3:53 - 3:57
    Mkaribishe Roho Mtakatifu ndani ya moyo wako.
  • 3:57 - 4:01
    Mkaribishe Roho Mtakatifu katikati yako.
  • 4:01 - 4:04
    Mkaribishe Roho Mtakatifu nyumbani kwako.
  • 4:04 - 4:07
    Mkaribishe sasa hivi.
  • 4:07 - 4:19
    Ee Roho Mtakatifu, tunaomba utufungulie malango ya Mbinguni leo.
  • 4:19 - 4:28
    Tunapofungua mioyo yetu Kwako, fungua milango ya mafuriko kwetu katika jina la Yesu Kristo.
  • 4:52 - 5:02
    Hivi sasa, mbegu yoyote ya uchungu ambayo imetia mizizi moyoni mwako -
  • 5:02 - 5:08
    Nasema, ng'olewa kwa jina kuu la Yesu Kristo!
  • 5:24 - 5:34
    Unapoachilia msamaha, pokea msamaha!
  • 5:34 - 5:40
    Unapoachilia msamaha, wekwa kando ka ajili ya uangalifu wa Mungu!
  • 5:40 - 5:47
    UtengwE kwa ajili ya huruma ya Mungu! Wekwa kando kando kwa upendeleo wa Mungu leo!
  • 6:06 - 6:12
    Kila doa la dhambi - lioshwe!
  • 6:12 - 6:18
    Uoshwe kwa Damu ya Yesu Kristo!
  • 6:32 - 6:40
    Roho Mtakatifu, ruhusu malango yako ya ukombozi yafunguke sasa hivi.
  • 6:40 - 6:50
    Acha nguvu Yako ya ukombozi ishuke sasa hivi!
  • 6:50 - 6:55
    Pokea ukombozi wako!
  • 6:55 - 6:58
    Pokea, katika jina la Yesu Kristo!
  • 7:21 - 7:28
    Kila silaha ya giza inayosababisha dhiki katika nafsi yako,
  • 7:28 - 7:33
    Ninasema hivi sasa - toweshwa!
  • 7:33 - 7:37
    Utoweshwe, katika jina la Yesu Kristo!
  • 7:37 - 7:41
    Uvunjwe sasa hivi!
  • 8:00 - 8:13
    Ninazungumza na hiyo nguvu ya kipepo inayosumbua hisia zako. Toka nje sasa hivi!
  • 8:13 - 8:26
    Roho hiyo nyuma ya wasiwasi, mashaka, huzuni - toka nje, kwa jina la Yesu Kristo!
  • 8:55 - 9:06
    Wewe pepo mchafu uletaye madhara na chuki - sikia Neno la Mungu. Toka nje sasa hivi!
  • 9:06 - 9:09
    Tupwa nje!
  • 9:09 - 9:13
    Tupwa nje, kwa jina kuu la Yesu!
  • 9:26 - 9:37
    Kila roho chafu iliyo nyuma ya tabia hizo mbaya, ambayo inasababisha tabia yako mbaya -
  • 9:37 - 9:38
    inatosha!
  • 9:38 - 9:45
    Ninakuamuru wewe pepo mchafu utoke sasa hivi!
  • 9:45 - 9:54
    Roho hiyo iliyo nyuma ya uasherati -toka kwa jina kuu la Yesu!
  • 10:22 - 10:26
    Watu wa Mungu, ukombozi unafanyika.
  • 10:26 - 10:33
    Nguvu za Roho Mtakatifu zinakutenganisha na nguvu zozote za giza.
  • 10:33 - 10:35
    Ikiwa uko pamoja na wanafamilia,
  • 10:35 - 10:40
    Ninataka kuombea familia sasa hivi kwa ajili ya ukombozi kutoka kwenye laana za vizazi.
  • 10:40 - 10:45
    Shikilia wanafamilia yako sasa hivi. Tuombe pamoja.
  • 10:45 - 10:55
    Kila roho ya umaskini inayoshikilia familia yako mateka - inatosha!
  • 10:55 - 10:58
    Kwa mamlaka katika jina la Yesu Kristo,
  • 10:58 - 11:03
    Ninakuamuru utoke katika gereza hilo la umaskini!
  • 11:03 - 11:06
    Toka katika gereza hilo la umaskini!
  • 11:06 - 11:10
    Toka katika gereza hilo katika familia yako!
  • 11:39 - 11:44
    Sasa hivi, toka kwenye ngome hiyo katika familia yako!
  • 11:44 - 11:52
    Ngome hiyo ya kizuizi, vilio, kurudi nyuma - ufukuwe kutoka kwenye ngome hiyo!
  • 11:52 - 11:57
    Ukombolewe kutoka kwenye ngome hiyo!
  • 12:18 - 12:22
    Ikiwa wanafamilia wako hawako nawe kimwili lakini una picha yao,
  • 12:22 - 12:23
    unaweza kuishikilia kwa imani.
  • 12:23 - 12:25
    Unaweza kuzishikilia picha zao kwa imani.
  • 12:25 - 12:27
    Roho wa Mungu anatenda kazi.
  • 12:27 - 12:32
    Sasa hivi, vunja laana hiyo katika familia yako!
  • 12:32 - 12:35
    Jiepushe na laana hiyo!
  • 13:05 - 13:17
    Laana hiyo ya kizazi cha ugumu katika familia yako - ivunjwe sasa hivi!
  • 13:17 - 13:24
    Laana hiyo ya kizazi ya magonjwa, maradhi, maumivu katika familia yako -
  • 13:24 - 13:30
    vunjwa, katika jina la Yesu Kristo!
  • 14:00 - 14:06
    Katika mazingira haya ya imani, weka mkono wako popote pale unapopata maumivu.
  • 14:06 - 14:12
    Roho Mtakatifu sasa hivi anaachilia nguvu zake za uponyaji.
  • 14:12 - 14:14
    Weka mkono wako hapo sasa hivi.
  • 14:14 - 14:22
    Malango ya Mbinguni yanafunguka na kuachilia uponyaji katika maisha yako leo.
  • 14:22 - 14:35
    Ninazungumza moja kwa moja na huyo pepo mchafu anayekuletea maumivu, magonjwa, maradhi.
  • 14:35 - 14:41
    Sikia Neno la Mungu. Toka nje sasa hivi!
  • 14:41 - 14:46
    Uponywe, katika jina la Yesu!
  • 14:46 - 14:51
    Uponywe, katikajina kuu la Yesu Kristo!
  • 15:20 - 15:29
    Kila chanzo cha ugonjwa katika mfumo wako - ufurumishwe leo!
  • 15:29 - 15:32
    Ufurumishwe sasa hivi!
  • 15:32 - 15:35
    Kitapike sasa hivi, katika jina la Yesu Kristo!
  • 15:35 - 15:39
    Popote ambapo ugonjwa huo umejificha,p opote ugonjwa huo unanyemelea -
  • 15:39 - 15:44
    toka kwenye mfumo wako!Kutoka kwa viungo vyako!
  • 15:44 - 15:46
    Kutolewa sasa hivi!
  • 16:13 - 16:22
    Kila kitu kigeni katika mwili wako -uoshwe nje sasa hivi!
  • 16:22 - 16:26
    Usafishwe kwa Damu ya Yesu Kristo!
  • 16:40 - 16:47
    Ninazungumza na ugonjwa huo wa ajabu katika damu yako, katika misuli yako, katika mifupa yako.
  • 16:47 - 16:52
    Maambukizi hayo, sasa hivi -toka kwenye mfumo wao!
  • 16:52 - 16:55
    Usafishwe kwa jina la Yesu!
  • 16:55 - 16:58
    Katika damu yako - takaswa sasa hivi!
  • 16:58 - 17:02
    Katika mifupa yako - takaswa hivi sasa!
  • 17:02 - 17:06
    Katika uwezo wako -takaswa!
  • 17:31 - 17:42
    Kizuizi hicho kinachoathiri kupumua kwako, kinachoathiri moyo wako, kinachoathiri mapafu yako,
  • 17:42 - 17:52
    Ninakiambia kizuizi hicho -kiondolewe sasa hivi!
  • 17:52 - 18:04
    Pokea maisha mapya katika mapafu yako, moyo, uwezo, damu, mifupa!
  • 18:04 - 18:06
    Pokea kwa jina la Yesu!
  • 18:43 - 18:47
    Roho hiyo ya ajabu inasumbua usingizi wako,
  • 18:47 - 18:53
    kusababisha kukosa utulivu usiku, kuathiri uwezo wako wa kulala,
  • 18:53 - 18:58
    Ninaiambia roho hiyo - toka leo!
  • 18:58 - 19:02
    Ondoka, kwa jina la Yesu Kristo!
  • 19:02 - 19:09
    Pokea hilo pumziko katika roho,nafsi na mwili wako sasa hivi!
  • 19:32 - 19:39
    Jeraha hilo la ndani - liponywe sasa hivi!
  • 19:39 - 19:46
    Jeraha hilo la ndani - upone sasa hivi!
  • 19:46 - 19:50
    Uwe mzima, katika jina la Yesu Kristo.
  • 20:08 - 20:14
    Hivi sasa, chochote ambacho shetani amekiingilia katika kazi yako
  • 20:14 - 20:23
    ambacho imesababisha kuchelewa, kizuizi, vilio - leo ni siku yako ya urejesho.
  • 20:23 - 20:26
    Urejeshwe sasa hivi!
  • 20:26 - 20:29
    Urejeshwe katika kazi yako!
  • 20:29 - 20:31
    Urejeshwe katika fedha zako!
  • 20:31 - 20:34
    Urejeshwe katika biashara yako!
  • 20:34 - 20:37
    Urejeshwe!
  • 21:05 - 21:14
    Ni kipi kinachosababisha 'uchhovu kupindukia' katika kazi yako?
  • 21:14 - 21:25
    Je, unateseka chini ya uzito wa shinikizo na mvutano mahali pa kazi yako?
  • 21:25 - 21:30
    Ni wakati wa kuchukua tena udhibiti wa moyo wako
  • 21:30 - 21:36
    na kuteka tena eneo lililochukuliwa na adui, lililoibiwa na adui.
  • 21:36 - 21:41
    Uchukue tena sasa hivi na upokee nguvu!
  • 21:41 - 21:48
    Pokea nguvu ya kuendelea kujitahidi -kupambana kufanya vizuri,
  • 21:48 - 21:54
    kupambania ukuu, kupambania mafanikio. Pokea nguvu hizo!
  • 22:29 - 22:34
    Pokea nguvu hizo katikati ya mapambano yako!
  • 22:34 - 22:39
    Ninakuambia kwa imani - mapambano yakoyatakufanya uwe na nguvu zaidi!
  • 22:39 - 22:42
    Mapambano yako yatakufanya uwe na nguvu!
  • 22:42 - 22:45
    Mapambano yako yatafanya biashara yako kuwa imara.
  • 22:45 - 22:48
    Mapambano yako yataimarisha ndoa yako.
  • 22:48 - 22:51
    Mapambano yako yatafanya fedha zako kuwa na nguvu zaidi.
  • 22:51 - 22:56
    Mapambano yako yatakufanya uwe na nguvu zaidi. Pokea leo!
  • 23:31 - 23:38
    Shida tuliyonayo wengi siku hizi tunajikuta tunachanganyikiwa kirahisi,
  • 23:38 - 23:43
    na kuchanganyikiwa kumetushawishi kuchukua maamuzi ya kizembe
  • 23:43 - 23:46
    ambayo hufanya hali zetu kuwa mbaya zaidi.
  • 23:46 - 23:54
    Ninaamuru roho hiyo ya kuchanganyikiwa ikuache leo!
  • 23:54 - 23:56
    Iachie biashara yako leo!
  • 23:56 - 23:58
    Iachie fedha zako leo!
  • 23:58 - 24:04
    Iachie familia yako leo ,katika jina la Yesu Kristo!
  • 24:46 - 24:49
    Najua kuna wengi wetu tunaungana sasa hivi
  • 24:49 - 24:56
    ambao wanatafuta kazi, wanatafuta kazi.
  • 24:56 - 25:03
    Nakuambia, leo ni siku yako!
  • 25:03 - 25:07
    Kwa mamlaka katika jina kuu la Yesu Kristo,
  • 25:07 - 25:15
    acha maombi yako ya kazi yapate kibali cha Mungu!
  • 25:15 - 25:24
    Acha CV yako ivutie kibali cha kimungu, katika jina la Yesu Kristo!
  • 25:46 - 25:49
    Baada ya Ibada hii Shirikishi ya Maombi,
  • 25:49 - 25:59
    tuma ombi lako la kazi n aupokee kazi uliyokusudiwa!
  • 25:59 - 26:04
    Pokea kupandishwa cheo kwako, kwa jina la Yesu Kristo!
  • 26:27 - 26:30
    Watu wa Mungu, nataka mzingatie jambo fulani.
  • 26:30 - 26:40
    Sio kila kushindwa, kukokufanikiwa katika biashara yako, fedha ni kutokana na mashambulizi ya kiroho.
  • 26:40 - 26:47
    Hapana! Mara nyingi, sisi ndio wabunifu wa anguko letu wenyewe
  • 26:47 - 26:53
    kwa sababu ya jinsi tunavyotumia vibaya rasilimali zetu.
  • 26:53 - 26:55
    Leo, nakuombea.
  • 26:55 - 27:00
    Pokea hekima yausimamizi wa fedha.
  • 27:00 - 27:04
    Pokea hekima yausimamizi wa biashara.
  • 27:04 - 27:11
    Pokea hekima ya usimamizi wa watu, katika jina la Yesu Kristo!
  • 27:38 - 27:45
    Sasa hivi, watu wa Mungu, nataka muombee mataifa ya ulimwengu.
  • 27:45 - 27:51
    Ikiwa una bendera ya taifa lako, ishikilie kama mahali pa kuwasiliana.
  • 27:51 - 27:56
    Tumeunganishwa kwa huduma hii kutoka kote ulimwenguni hivi sasa.
  • 27:56 - 27:58
    Sisi hatuko hapa kwa ajili yetu wenyewe tu.
  • 27:58 - 28:02
    Tuko hapa kusimama kwenye pengo kwa ajili ya mataifa.
  • 28:02 - 28:06
    Kumbuka sasa hivi mataifa hayoyanayoshughulika
  • 28:06 - 28:11
    na athari za majanga ya asili.
  • 28:11 - 28:19
    Kumbuka mataifa hayo na uombe Mungu aingilie kati sasa hivi.
  • 28:19 - 28:22
    Omba uingiliaji kati wa Mungu.
  • 28:45 - 28:53
    Kumbuka mataifa ambayo yanashughulika na migogoro na machafuko inayoendelea.
  • 28:53 - 28:55
    Kumbuka mataifa hayo.
  • 28:55 - 29:00
    Omba uingiliaji kati wa Mungu.
  • 29:00 - 29:03
    Omba Mungu aingilie kati leo.
  • 29:24 - 29:28
    Kumbuka taifa lako mwenyewe katika maombi sasa hivi.
  • 29:28 - 29:30
    Taja jina la taifa lako.
  • 29:30 - 29:36
    Likabidhi taifa lako, wakabidhi viongozi wako mikononi mwa Mungu
  • 29:36 - 29:45
    na uombe uingiliaji wa kimungu katika mambo ya taifa lako.
  • 30:09 - 30:14
    Kila pazia linalotia giza moyo wako,
  • 30:14 - 30:20
    ukizuia moyo wako kupokea ufunuo kutoka juu,
  • 30:20 - 30:27
    Ninasema kwa pazia hilo - vunjwa leo!
  • 30:27 - 30:36
    Macho ya imani yako na yafumbuke, kwa jina kuu la Yesu.
  • 31:15 - 31:23
    Macho ya imani yako - yafumbuliwe sasa hivi, katika jina la Yesu Kristo!
  • 31:23 - 31:26
    Anza kuona maisha dhahiri.
  • 31:26 - 31:28
    Jionee dhahiri.
  • 31:28 - 31:30
    Tazama wengine kwa uwazi.
  • 31:30 - 31:34
    Jitambue.
  • 31:34 - 31:41
    Pata maoni ya Mungu juu yako mwenyewe na wengine, katika jina la Yesu Kristo!
  • 32:11 - 32:17
    Katika jina kuu la Yesu Kristo tunaomba.
  • 32:25 - 32:33
    Watu wa Mungu, Maandiko yanasema katika kitabu cha Zaburi 142:7
  • 32:33 - 32:43
    ili Mungu azifungue roho zetu kutoka gerezani ili tulisifu jina lake takatifu.
  • 32:43 - 32:51
    Ninasema sasa hivi, leo, kwa mamlakakatika jina la Yesu Kristo,
  • 32:51 - 32:56
    nafsi yako imefunguliwa kutoka katika gereza hilo la utumwa.
  • 32:56 - 33:01
    Familia yako imeachiliwa kutoka katika gereza la laana za vizazi.
  • 33:01 - 33:06
    Biashara yako imeachiliwa kutoka kwenye gereza la vilio.
  • 33:06 - 33:11
    Afya yako imetolewa kutoka katika gereza la mateso.
  • 33:11 - 33:14
    Maisha yako yamekombolewa leo.
  • 33:14 - 33:18
    Furahia kukombolewa kwako!
  • 33:18 - 33:24
    Ndiyo, furahia kuachiliwa kwako na ulisifu jina lake kwa uponyaji wako.
  • 33:24 - 33:27
    Lisifuni jina lake kwa ukombozi wako.
  • 33:27 - 33:29
    Lisifuni jina lake kwa uhuru wako.
  • 33:29 - 33:32
    Lisifuni jina lake kwa kazi hiyo mpya.
  • 33:32 - 33:34
    Lisifiwe jina lake kwa kupandiswa cheo.
  • 33:34 - 33:37
    Lisifuni jina lake kwa ongezeko hilo.
  • 33:37 - 33:40
    Lisifuni jina lake kwa upatanisho huo.
  • 33:40 - 33:43
    Lisifuni jina lake!
  • 33:43 - 33:50
    Kila mwenye pumzina amsifu Bwana!
  • 33:50 - 34:01
    Na zingatia haya - unapomtafuta Mungu katikati ya hali yako.
  • 34:01 - 34:07
    utamwona Mungu katikati ya hali yako.
  • 34:07 - 34:13
    Lakini hamu yako ya kupokea kutoka kwa Yesu Kristo
  • 34:13 - 34:23
    lazima iambatane na kujitolea kumfuata Yesu Kristo.
  • 34:23 - 34:31
    Je, kuna eneo lolote la maisha yako ,maisha yako ya kila siku,
  • 34:31 - 34:40
    kwamba unajua unahitaji kulirekebisha ili kudumisha uhusiano wako pamoja na Mungu?
  • 34:40 - 34:47
    Ukweli wa utayari wako wa kumfuata Yesu
  • 34:47 - 34:54
    unaonyeshwa na uzito ambao unajibu swali hili -
  • 34:54 - 35:01
    si kwa midomo tu bali kwa maisha yako.
  • 35:01 - 35:03
    Kumbuka, watu wa Mungu.
  • 35:03 - 35:07
    Bila shaka, kila mtu hufanya makosa.
  • 35:07 - 35:12
    Na ndio, sote tunapambana na udhaifu wetu.
  • 35:12 - 35:23
    Lakini la msingi ni wewe kumkimbilia Mungu kwa ajili ya toba.
  • 35:23 - 35:30
    Unapomkimbilia Mungu kwa toba, utapata nguvu ya kushinda
  • 35:30 - 35:34
    na neema ya kuendelea.
Title:
MAOMBI YENYE UPAKO ili KUFUNGUA MALANGO YA MAFURIKO YA MBINGUNI KATIKA MAISHA YAKO!
Description:

Shuhudia nguvu za Roho Mtakatifu zikishuka na kuleta ukombozi, uponyaji na uhuru wakati huo huo kwa maelfu ya waliounganishwa ulimwenguni kote kupitia Zoom katika Ibada hii iliyotiwa mafuta ya Maombi Shirikishi na Ndugu Chris. Unapofungua moyo wako kwa Roho Mtakatifu, Yeye atafungua milango ya Mbingu katika maisha yako!

Je, ungependa kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Kaka Chris kupitia Zoom? Tuma ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

"Roho Mtakatifu, ruhusu malango yako ya ukombozi yafunguke sasa hivi. Acha nguvu yako ya ukombozi ishuke sasa hivi! Pokea ukombozi wako! Upokee, kwa jina la Yesu Kristo! Kila silaha ya giza inayosababisha dhiki katika nafsi yako, nasema. sasa hivi - uondolewe, kwa jina la Yesu Kristo!" - Ndugu Chris

➡️ Pata kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Saidia TV ya Moyo wa Mungu kifedha - https://godsheart.tv/financial/
➡️ Taarifa kuhusu Maombi Shirikishi - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
36:24

Swahili subtitles

Incomplete

Revisions Compare revisions