-
Tunapitia mambo mengi moja kwa moja.
Tunajua kilichojiri kwa sababu tulikuwepo.
-
Kwa sababu haiwezekani kujionea kila kitu,
lazima tutegemee ripoti za wengine.
-
Kwa mashirika ya kitaalamu ya habari kazi
ya kubuni ripoti hizi hufanyika kupitia
-
mchakato wa uandishi wa habari. Uanahabari
ni desturi ya kukusanya, kutathmini,
-
na kuonyesha habari na maelezo kwa
ajili ya gazeti, matangazo au mtandao.
-
Kazi ya mwanahabari ni kufanya
utafiti, kuhakikisha ukweli,
-
na kuonyesha ripoti sahihi
zinazofafanua masuala na matukio.
-
Uanahabari unaweza kukabili mada yoyote
kuanzia spoti, burudani, afya na siasa.
-
Uanahabari unaotolewa na mashirika ya
habari ni muhimu zaidi kwa demokrasia.
-
Kama raia tunategemea wanahabari
kutoa maelezo tunayohitaji
-
ili kufanya uamuzi bora zaidi kuhusu
maisha, jumuiya na serikali zetu.
-
Kuna majukumu kadhaa muhimu
ambayo uandishi wa habari hutimiza.
-
Uandishi wa habari husaidia kuwaarifu
watu kuhusu matukio na masuala
-
ambayo ni muhimu kwa jamii kwa jumla.
-
Inachangia maarifa ya jumla
-
na husaidia kubadili maoni kuhusu
kinachoendelea duniani.
-
Uanahabari unaweza pia kutoa taswira
tofauti ya masuala na baraza la mijadala.
-
Wanahabari hutenda kama wanaohakikisha
walio katika mamlaka wanawajibika.
-
Wanahimiza ukweli na uwazi kwa maafisa
wa serikali na wengine walio mamlakani
-
kwa kuuliza maswali kuhusu matendo na
maamuzi yao na kwa kufichua ukweli.
-
Uanahabari unaweza kuwakilisha wanyonge
katika jamii kwa kushiriki hadithi za
-
wanaokumbana na changamoto tofauti.
-
Wanahabari wanaweza kusaidia kubuni uwezo
wa kuhisi maoni ya wengine katika umma.
-
Uandishi wa habari ni muhimu kwa
demokrasia kwa sababu unaangazia maeneo
-
ambayo yamefichika na huwasaidia
watu kupata taarifa kuhusu masuala muhimu.