-
Tunapitia mambo mengi moja kwa moja.
Tunajua kilichojiri kwa sababu tulikuwepo.
-
Kwa sababu haiwezekani kujionea kila kitu,
lazima tutegemee ripoti za wengine.
-
Kwa mashirika ya kitaalamu ya habari kazi
ya kubuni ripoti hizi hufanyika kupitia
-
mchakato wa uandishi wa habari. Uanahabari
ni desturi ya kukusanya, kutathmini,
-
na kuonyesha habari na maelezo kwa
ajili ya gazeti, matangazo au mtandao.
-
Kazi ya mwanahabari ni kufanya
utafiti, kuhakikisha ukweli,
-
na kuonyesha ripoti sahihi
zinazofafanua masuala na matukio.
-
Uanahabari unaweza kukabili mada yoyote
kuanzia spoti, burudani, afya na siasa.
-
Uanahabari unaotolewa na mashirika ya
habari ni muhimu zaidi kwa demokrasia.
-
Kama raia tunategemea wanahabari
kutoa maelezo tunayohitaji
-
ili kufanya uamuzi bora zaidi kuhusu
maisha, jumuiya na serikali zetu.
-
Kuna majukumu kadhaa muhimu
ambayo uandishi wa habari hutimiza.
-
Uandishi wa habari husaidia kuwaarifu watu
kuhusu matukio na masuala
-
ambayo ni muhimu kwa jamii kwa jumla.
-
Inachangia katika maarifa ya jumla
-
na husaidia kubadili maoni kuhusu kinachoendelea kote duniani.
-
Uandishi wa habari unaweza pia kuonyesha mitazamo tofauti kuhusu masuala na kutoa mjadala wa umma.
-
Wanahabari hutenda kama wanaohakikisha walio katika mamlaka wanawajibika.
-
Wanahimiza ukweli na uwazi kutoka kwa maafisa wa serikali na wengine walio mamlakani
-
kwa kuhoji matendo na maamuzi yao na kwa kufichua ukweli.
-
Mwishowe, uandishi wa habari unaweza kuwapa watu ambao hawana mamlaka katika jamii sauti kwa kushiriki hadithi za wale
-
wanaokumbana na changamoto tofauti.
-
Uandishi wa habari unaweza kusaidia kubuni huruma katika umma.
-
Uandishi wa habari ni muhimu kwa demokrasia kwa sababu inaangazia maeneo
-
ambayo huenda hayajulikani na huwasaida watu kupata taarifa kuhusu masuala yanayofaa.