Jack Andraka: Kipimo kinachotia matumaini cha kansa ya kongosho kutoka kwa kijana mdogo.
-
0:01 - 0:04Je umeshawahi kukutana na wakati maishani
-
0:04 - 0:08ambao ulikuwa ni wa huzuni sana
-
0:08 - 0:10kiasi kitu pekee ulichotaka
-
0:10 - 0:14kufanya ni kujifunza zaidi na zaidi ili kuelewa hali hiyo?
-
0:14 - 0:17Nilipokuwa na miaka 13, rafiki wa karibu wa familia
-
0:17 - 0:18ambaye alikuwa kama mjomba kwangu
-
0:18 - 0:21alifariki kwa kansa ya kongosho.
-
0:21 - 0:24Wakati ugonjwa ulipokumba karibu sana na nyumbani,
-
0:24 - 0:26Nilitambua nahitaji kujifunza zaidi,
-
0:26 - 0:28nikaingia mtandaoni kutafuta majibu.
-
0:28 - 0:32kwa kutumia mtandao, nikapata takwimu mbalimbali
-
0:32 - 0:33kuhusu kansa ya kongosho,
-
0:33 - 0:36na kilichonishtusha.
-
0:36 - 0:40zaidi ya asilimia 85 ya kansa zote za kongosho
-
0:40 - 0:41zinagundulika kwa kuchelewa sana,
-
0:41 - 0:46wakati mtu ana chini ya asilimia ya kuishi.
-
0:46 - 0:50kwa nini hatufanyi vizuri kugundua kansa ya kongosho?
-
0:50 - 0:53Sababu?mfumo wetu wa utabibu na dawa
-
0:53 - 0:55una umri wa miaka karibu 60 sasa.
-
0:55 - 0:58Umri huo ni mkubwa kuliko wa baba yangu
-
0:58 - 1:01(vicheko)
-
1:01 - 1:04lakini pia, ni wa gharama kubwa sana,
-
1:04 - 1:07unagharimu dola za kimarekani 800 kwa kipimo,
-
1:07 - 1:10lakini pia vipimo havina uhakika,
-
1:10 - 1:13na kushindwa kugundua asilimia 30 ya kansa zote za kongosho
-
1:13 - 1:16Daktari wako itabidi awe ni mdadisi wa ajabu sana
-
1:16 - 1:20kuamua kukuandikia kipimo hiki.
-
1:20 - 1:23nilipojua hili, nikajua lazima iwepo njia bora zaidi.
-
1:23 - 1:26kwa nikaweka kigezo
-
1:26 - 1:28cha kipimo kinavyotakiwa kuwa
-
1:28 - 1:31ili kugundua vizuri kansa ya kongosho.
-
1:31 - 1:35Kipimo kinahitajika kuwa cha gharama nafuu, haraka,
-
1:35 - 1:39rahisi,kinachogundua haraka,
-
1:39 - 1:42na kisichohitaji kuingia kwa sehemu kubwa mwilini.
-
1:42 - 1:44Kuna sababu kwa nini kipimo hiki hakijabadilishwa
-
1:44 - 1:47kwa karibia miaka sitini,
-
1:47 - 1:50kwa sababu,tunapoangalia kansa ya kongosho,
-
1:50 - 1:52tunaangalia mzunguko wako wa damu
-
1:52 - 1:57ambao tayari umejaa tani nyingi za protini,
-
1:57 - 1:59na unatafuta chembe tofauti ndogo sana
-
1:59 - 2:01katika protini ndogo sana,
-
2:01 - 2:02protini hii moja tu.
-
2:02 - 2:04jambo hili ni gumu sana
-
2:04 - 2:07lakini, bila kukatishwa tamaa kutokana na shauku ya ujana
-
2:07 - 2:13(makofi)
-
2:13 - 2:17nikaenda mtandaoni kwa marafiki wawili sana wa kijana
-
2:17 - 2:19Google na Wikipedia
-
2:19 - 2:23Nilipata kila kitu kutoka vyanzo hivyo viwili,
-
2:23 - 2:25nilichokipata ilikuwa ni chapisho
-
2:25 - 2:29ambalo lilionyesha taarifa za protini 8000 tofauti
-
2:29 - 2:32ambazo zinaonekana ukiwa na kansa ya kongosho.
-
2:32 - 2:35kwa hiyo nikaamua hii iwe kazi yangu mpya
-
2:35 - 2:38kupitia protini zote hizi na kuona zipi
-
2:38 - 2:41zinaweza kuwa kitambulishi cha kansa ya kongosho.
-
2:41 - 2:43na kunirahisishia mambo,
-
2:43 - 2:47nikachagua kigezo, na ni hiki.
-
2:47 - 2:50Kwanza, protini lazima ionekane
-
2:50 - 2:53katika kansa zote za kongosho kwa kiasi kikubwa,katika damu
-
2:53 - 2:57katika hatua za mwanzoni.
-
2:57 - 3:00Kwa hiyo nikawa nafanya majaribio katika kazi hii ngumu,
-
3:00 - 3:04na mwishowe, katika jaribio la 4000,
-
3:04 - 3:05wakati nakaribia kuwa kichaa,
-
3:05 - 3:07nikaipata hiyo protini.
-
3:07 - 3:10jina la protini niliyoiona
-
3:10 - 3:11linaitwa mesothelin,
-
3:11 - 3:14na ni protini ya kawaida tu,
-
3:14 - 3:16ikiwa tu hauna kansa ya kongosho
-
3:16 - 3:18ya kizazi au ya mapafu,
-
3:18 - 3:21ikiwa unazo,protini hii inakua nyingi sana katika damu
-
3:21 - 3:22lakini pia muhimu ni
-
3:22 - 3:25kwamba inapatikana katika hatua za mwanzo kabisa za ugonjwa,
-
3:25 - 3:28wakati mtu ana nafasi ya asilimia 100
-
3:28 - 3:29ya kupona kabisa.
-
3:29 - 3:32baada ya kupata protini ya uhakika,kuigundua
-
3:32 - 3:35nikabadilisha mwelekeo kwenda katika kuigundua sasa,
-
3:35 - 3:38na hivyo, kugundua pia kansa ya kongosho.
-
3:38 - 3:41mafanikio yangu yalipatina mahali pasipotarajiwa kabisa,
-
3:41 - 3:44labda sehemu isiyotegemewa kwa uvumbuzi kabisa:
-
3:44 - 3:46katika darasa langu la biolojia la sekondari,
-
3:46 - 3:48mahali ambapo ubunifu unazuiwa kabisa.
-
3:48 - 3:53(vicheko)(makofi)
-
3:53 - 3:57na nilifanikiwa kuliona andiko kuhusu vitu vinaitwa
-
3:57 - 4:00tyubu ndogo sana za kaboni.
-
4:00 - 4:01ambazo upana wake ni kama wa atom
-
4:01 - 4:04na kipenyo chake moja ya hamsini ya kipenyo cha nywele yako.
-
4:04 - 4:06pamoja na udogo huu
-
4:06 - 4:08zina tabia za ajabu sana.
-
4:08 - 4:11ni kama mashujaa wa sayansi ya maada.
-
4:11 - 4:13wakati nasoma chapisho
-
4:13 - 4:15chini ya dawati katika darasa la elimu ya viumbe,
-
4:15 - 4:17tulitakiwa tuwe makini
-
4:17 - 4:21katika molekyuli ziitwazo antibodi
-
4:21 - 4:23na hizi zimetulia sana kwa kuwa zinaweza ungana tu
-
4:23 - 4:24na protini moja,
-
4:24 - 4:27lakini sio za kupendeza kama tyubu ndogo za kaboni
-
4:27 - 4:30kwa hiyo nilikuwa darasani,
-
4:30 - 4:33na ghafla nikatambua:
-
4:33 - 4:35Kwamba naweza kuunganisha nilichokuwa nasoma,
-
4:35 - 4:37tyubu ndogo za kaboni,
-
4:37 - 4:40na kile nilichotakiwa kuwaza, antibodi.
-
4:40 - 4:42naweza nikazungusha antibodi hizi
-
4:42 - 4:44katika mkusanyiko wa tyubu ndogo za kaboni
-
4:44 - 4:46kiasi kwamba unakuwa na mkusanyiko
-
4:46 - 4:48ambao unaungana na protini moja
-
4:48 - 4:52lakini,pia kutokana na tabia za tyubu ndogo za kaboni,
-
4:52 - 4:54itabadilisha tabia zake za kiumeme
-
4:54 - 4:56kulingana na kiasi cha protini kilichopo
-
4:56 - 4:58lakini kuna jambo la kuzingatia.
-
4:58 - 5:02muunganiko huu wa tybu ndogo za kaboni ni laini sana
-
5:02 - 5:05kwa kuwa ni laini sana,zinahitaji kutegemezwa
-
5:05 - 5:07ndio maana nikachagua karatasi.
-
5:07 - 5:10Kutengeneza kipimo cha kansa kwa karatasi
-
5:10 - 5:12ni rahisi kama kutengeneza biskuti za chokleti
-
5:12 - 5:15ambazo nazipenda
-
5:15 - 5:19unaanza na maji,unamimina nanotubes,
-
5:19 - 5:21ongeza antibodies, changanya,
-
5:21 - 5:24chukua karatasi,chovya,ikaushe,
-
5:24 - 5:27na unaweza ukagundua kansa.
-
5:27 - 5:33(makofi)
-
5:33 - 5:37ghafla, wazo likanijia,
-
5:37 - 5:41lililoweka doa katika mpango wangu wa ajabu.
-
5:41 - 5:43siwezi nikafanya utafiti wa kansa
-
5:43 - 5:44katika jiko langu.
-
5:44 - 5:46mama yangu hatapenda kitu hicho.
-
5:46 - 5:50kwa hiyo, nikaamua kwenda maabara.
-
5:50 - 5:52nikaandika bajeti, orodha ya vifaa,
-
5:52 - 5:54ratiba na taratibu zitakazotumika,
-
5:54 - 5:57nikatuma kama barua pepe kwa maprofesa 200 tofauti
-
5:57 - 5:58katika chuo cha Johns Hopkins
-
5:58 - 6:00na katika taasisi ya afya ya taifa,
-
6:00 - 6:03kimsingi yoyote ambaye alikuwa na chochote kuhusu kansa ya kongosho.
-
6:03 - 6:06nikakaa nikisubiri majibu mazuri kuingia,
-
6:06 - 6:08yakisema, "wewe una kipaji cha ajabu!
-
6:08 - 6:09unaenda kutusaidia sisi wote!"
-
6:09 - 6:14na - (vicheko)
-
6:14 - 6:15baadae ukweli ukaanza kuonekana,
-
6:15 - 6:17na ndani ya mwezi mmoja,
-
6:17 - 6:22nikapata majibu ya kukataa 199 kati ya barua pepe zile 200.
-
6:22 - 6:24profesa mmoja akapitia mpango wangu wote
-
6:24 - 6:27sijui alipata wapi muda wote huu --
-
6:27 - 6:31na akaanza kusema kwa nini kila hatua
-
6:31 - 6:34ni kosa kubwa sana.
-
6:34 - 6:37wazi wazi kabisa kila profesa hakuwa na maono makubwa
-
6:37 - 6:40kuhusu kazi yangu kama nilivyokuwa mimi.
-
6:40 - 6:42lakini, kulikuwa bado na tumaini.
-
6:42 - 6:45profesa mmoja, "labda naweza kukusaidia kijana."
-
6:45 - 6:48kwa hiyo nikaenda katika mwelekeo huo.
-
6:48 - 6:52(vicheko)
-
6:52 - 6:54kwa kuwa hauwezi kumkatalia mtoto.
-
6:54 - 6:57kwa hiyo miezi mitatu baadae,
-
6:57 - 7:00nilifanikiwa kupanga kukutana na mtu huyu,
-
7:00 - 7:01nikaingia katika maabara yake,
-
7:01 - 7:03nikawa na shauku kubwa, halafu nikakaa chini
-
7:03 - 7:05nikaanza kuongea,
-
7:05 - 7:08sekunde tano baadaye akamwita Daktari wa fasafa
-
7:08 - 7:11madaktari wa falsafa wakajaa katika chumba hiki kidogo,
-
7:11 - 7:14wakawa wananiuliza maswali,
-
7:14 - 7:16na mwishowe,nikahisi kama nilikuwa katika gari lililojaa watu wengi mno
-
7:16 - 7:18Kulikuwa na madaktari wa falsafa 20, mimi na huyu Profesa
-
7:18 - 7:20tumejazana katika ofisi ndogo
-
7:20 - 7:23wakinirushia maswali ya haraka haraka
-
7:23 - 7:26wakijaribu kuzamisha mpango wangu.
-
7:26 - 7:28Jinsi gani jambo hili lilivyokuwa gumu?
-
7:28 - 7:32(vicheko)
-
7:32 - 7:35bila kujali kuhojiwa kote kule,
-
7:35 - 7:37nilijibu maswali yao yote,
-
7:37 - 7:39nilibahatisha katika baadhi ya maswali lakini nilikuwa sahihi,
-
7:39 - 7:43mwishowe nikafanikiwa kupata nafasi ya maabara niliyoihitaji.
-
7:43 - 7:46muda mfupi baadae ndipo nikagundua
-
7:46 - 7:48mpango wango mahiri
-
7:48 - 7:50kuwa na makosa karibia milioni moja,
-
7:50 - 7:51na ndani ya miezi saba,
-
7:51 - 7:55nikaanza kazi nzito ya kusahihisha makosa haya yote moja baada ya jingine.
-
7:55 - 7:58Matokeo yake? kipimo cha karatasi
-
7:58 - 8:01kikigharimu senti tatu za dola kikichukua dakika tano.
-
8:01 - 8:04hii inakifanya kiwe mara 168 haraka zaidi,
-
8:04 - 8:07kikiwa na gharama ya chini ya mara 26,000
-
8:07 - 8:10na kikiwa cha uhakika kwa zaidi ya mara 400
-
8:10 - 8:13kushinda kipimo cha sasa cha kansa ya kongosho
-
8:13 - 8:22(makofi)
-
8:22 - 8:25moja kati ya vitu muhimu kuhusu kipimo hiki,
-
8:25 - 8:27ni kuwa kinatoa majibu sahihi kwa karibia asilimia 100,
-
8:27 - 8:30na kinagundua kansa katika hatua za mwanzo kabisa
-
8:30 - 8:33wakati mtu ana nafasi ya asilimia 100 ya kupona.
-
8:33 - 8:35kwa hiyo ndani ya miaka miwili mpaka mitano ijayo,
-
8:35 - 8:39kipimo hiki kinaweza kikaongeza watu kupona kansa ya kongosho
-
8:39 - 8:41kutoka asilimia 5.5
-
8:41 - 8:43mpaka karibu na asilimia 100,
-
8:43 - 8:46na pia itafanya hivyo hivyo kwa kansa ya kizazi na ya mapafu.
-
8:46 - 8:48lakini haitaishia hapo tu.
-
8:48 - 8:50Kwa kuifunga hiyo antibodi,
-
8:50 - 8:52unaweza ukaangalia protini mbalimbali,
-
8:52 - 8:53kwa hiyo pia magonjwa mbalimbali,
-
8:53 - 8:57lakini uwezo huu ni kwa ugonjwa wowote duniani
-
8:57 - 8:59kutoka ugonjwa wa moyo
-
8:59 - 9:01mpaka Malaria,HIV,AIDS,
-
9:01 - 9:04pia ni aina nyingine za kansa-- ugonjwa wowote ule.
-
9:04 - 9:06Kwa hiyo, tumaini ni kuwa siku moja
-
9:06 - 9:09wote tunaweza tukawa na yule mjomba wa ziada,
-
9:09 - 9:12yule mama,yule kaka,dada,
-
9:12 - 9:15tunaweza kuwa na ndugu wa kumpenda,
-
9:15 - 9:20na mioyo yetu itapunguziwa mzigo wa ugonjwa mmoja
-
9:20 - 9:23utokanao na kansa ya kongosho,kizazi na mapafu,
-
9:23 - 9:25au ugonjwa wowote mwingine,
-
9:25 - 9:27na kupitia mtandao mengi yanawezekana.
-
9:27 - 9:29tunaweza kushirikishana nadharia,
-
9:29 - 9:30na sio lazima uwe profesa
-
9:30 - 9:33na shahada nyingi ili mawazo yako yathaminike.
-
9:33 - 9:34ni eneo lililo wazi kwa mtu yeyote
-
9:34 - 9:37ambapo mwonekano,umri wako au jinsia,
-
9:37 - 9:38haijalishi.
-
9:38 - 9:41ni mawazo yako tu ndiyo yanayojalisha.
-
9:41 - 9:44Kwangu mimi,ni suala la kuangalia mtandao wa intaneti
-
9:44 - 9:46kwa mtazamo mpya kabisa
-
9:46 - 9:48ili kujua kuna mengi sana ndani yake
-
9:48 - 9:53badala ya kuweka picha zako tu mtandaoni.
-
9:53 - 9:56unaweza ukaibadilisha dunia.
-
9:56 - 9:58kwa hiyo kama kijana wa miaka 15
-
9:58 - 10:01ambaye alikuwa hajui hata kongosho ni nini
-
10:01 - 10:05anaweza akavumbua njia mpya ya kugundua kansa ya kongosho.
-
10:05 - 10:07jaribu kufikiri unaweza ukafanya mangapi.
-
10:07 - 10:09Asante sana
-
10:09 - 10:14(makofi)
- Title:
- Jack Andraka: Kipimo kinachotia matumaini cha kansa ya kongosho kutoka kwa kijana mdogo.
- Speaker:
- Jack Andraka
- Description:
-
Zaidi ya asilimia 85 ya kansa zote za kongosho zinagundulika kwa kuchelewa sana wakati nafasi ya kupona iko chini ya asilimia 2. Kwa nini iko hivi? Jack Andraka anaongelea jinsi alivyovumbua kipimo kinachotia matumaini cha kugundua kansa ya kongosho ambacho ni rahisi mno,kinafanya kazi kwa usahihi na hakihitaji kuingia katika mwili -- yote hayo kabla hata ya kutimiza miaka 16 ya kuzaliwa.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 10:49
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager | |
![]() |
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for A promising test for pancreatic cancer ... from a teenager |