< Return to Video

Hans Rosling aonyesha takwimu bora kuliko zote ulizoziona

  • 0:00 - 0:04
    Takriban miaka 10 iliyopita, nilianza kazi ya kufundisha maendeleo ya ulimwengu
  • 0:04 - 0:08
    kwa wanafunzi wa Kiswidishi wa shahada ya kwanza. Hii ilikuwa baada ya
  • 0:08 - 0:12
    takriban miaka 20 ya kufanya kazi pamoja na taasisi mbalimbali za Afrika nikitafiti kuhusu njaa
  • 0:12 - 0:16
    katika Afrika, kwa hiyo nilikuwa natarajiwa niwe najua zaidi kuhusu dunia.
  • 0:16 - 0:21
    Na nilianzia kwenye chuo chetu cha utabibu, Taasisi ya Karolinska,
  • 0:21 - 0:25
    kozi ya shahada ya kwanza iliyoitwa Afya ya Ulimwengu. Lakini ukipata
  • 0:25 - 0:28
    fursa hiyo, unapata mshawasha kidogo. Nilifikiri wanafunzi hawa
  • 0:28 - 0:31
    kuja kwetu ni lazima wana maksi za juu unazoweza kupata
  • 0:31 - 0:34
    kwenye mfumo wa vyuo vya Sweden -- kwahiyo labda wanajua kila kitu
  • 0:34 - 0:38
    kuhusu nitakachowafundisha. Kwa hiyo niliwapa mtihani mara tu walipokuja.
  • 0:38 - 0:41
    Na moja wapo kati ya maswali ambayo nilijifunza mengi ni hili hapa:
  • 0:41 - 0:45
    "Ni nchi gani kati ya hizi tano ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto kati ya jozi hizi tano?"
  • 0:45 - 0:49
    Na niliziweka pamoja, ili katika kila kundi la nchi,
  • 0:49 - 0:54
    moja ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto zaidi ya nyingine. Na hii inamaanisha kwamba
  • 0:54 - 0:59
    kuna tofauti kubwa sana kuliko uhakika wa takwimu.
  • 0:59 - 1:01
    Sitawapa mtihani hapa, lakini ni Uturuki,
  • 1:01 - 1:06
    ambayo ina kiwango kikubwa pale, Poland, Urusi, Pakistani na Afrika Kusini.
  • 1:06 - 1:09
    Na haya ndiyo majibu ya wanafunzi wa Kiswidishi. Nilifanya hivyo na nilipata
  • 1:09 - 1:12
    kiwango cha imani, ambacho kilikuwa kidogo, na nilifurahi,
  • 1:12 - 1:16
    kwa hakika: 1.8 ya jibu sahihi kati ya matano inawezekana. Hii ina maana kwamba
  • 1:16 - 1:19
    kulikuwa kuna nafasi ya Profesa wa afya ya ulimwengu --
  • 1:19 - 1:21
    (Kicheko) na kwa kozi yangu.
  • 1:21 - 1:25
    Lakini usiku mmoja, wakati nilipokuwa natayarisha ripoti
  • 1:25 - 1:29
    Niligundua uvumbuzi wangu. Nimeonyesha
  • 1:29 - 1:34
    kuwa wanafunzi Waswidishi wenye alama za juu wanajua kidogo sana kuhusu takwimu
  • 1:34 - 1:36
    za ulimwengu kuliko hata sokwe.
  • 1:36 - 1:38
    (Kicheko)
  • 1:38 - 1:42
    Kwasababu sokwe wangepata nusu iwapo ningewapa
  • 1:42 - 1:45
    ndizi mbili zenye Sri Lanka na Uturuki. Wangekuwa sahihi kwa nusu yake.
  • 1:45 - 1:49
    Lakini wanafunzi hawapo huko. Tatizo langu halikuwa kutokujua kwao:
  • 1:49 - 1:52
    ilikuwa ni mawazo waliyojijengea.
  • 1:52 - 1:56
    Pia nilifanya utafiti kinyume na maadili kwa maprofesa wa taasisi ya Karolinska
  • 1:56 - 1:57
    (Kicheko)
  • 1:57 - 1:59
    -- ambao wanatoa tuzo ya Nobel katika utabibu,
  • 1:59 - 2:01
    na wao wako sawa tu na sokwe.
  • 2:01 - 2:04
    (Kicheko)
  • 2:04 - 2:08
    Hapa ndipo nilipogundua kwamba kuna haja ya kuwasiliana,
  • 2:08 - 2:11
    kwasababu ya takwimu za kinachotokea duniani
  • 2:11 - 2:14
    na afya ya mtoto katika kila nchi inajulikana.
  • 2:14 - 2:19
    Tulitengeneza hii programu ya kompyuta ambayo inayoonyesha kama hivi: kila kiputo hapa ni nchi.
  • 2:19 - 2:25
    Hii nchi hapa ni China. Hii ni India.
  • 2:25 - 2:31
    Ukubwa wa kiputo ni idadi ya watu, na katika mhimili huu nimeweka kiwango cha uzazi.
  • 2:31 - 2:34
    Kwasababu wanafunzi wangu, walichosema
  • 2:34 - 2:36
    wakati walipoangalia dunia, na nilipowauliza,
  • 2:36 - 2:38
    "Nini mnafikiri kuhusu dunia?"
  • 2:38 - 2:42
    Naam, kwanza niligundua kuwa kitabu cha kiada kilikuwa Tintin, angalau.
  • 2:42 - 2:43
    (Kicheko)
  • 2:43 - 2:46
    Na walisema, "Dunia bado ni 'sisi' na 'wao.'
  • 2:46 - 2:49
    Na sisi ni dunia ya Magharibi na wao ni Dunia ya Tatu."
  • 2:49 - 2:52
    "Na una maana gani kwa kusema dunia ya magharibi?" Niliuliza.
  • 2:52 - 2:57
    "Naam, haya ni maisha marefu na familia ndogo, na dunia ya tatu ni maisha mafupi na familia kubwa."
  • 2:57 - 3:03
    Kwa hiyo hii ndio ninayoweza kuonyesha hapa. Niliweka kiwango cha uzazi hapa: idadi ya watoto kwa mwanamke,
  • 3:03 - 3:07
    moja, mbili, tatu, nne, mpaka watoto nane kwa mwanamke mmoja.
  • 3:07 - 3:13
    Tuna takwimu nzuri sana toka mwaka 1962 -- 1960 kuhusu -- ukubwa wa familia katika nchi zote.
  • 3:13 - 3:16
    Kiwango cha makosa ni kidogo sana. Hapa naweka umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa,
  • 3:16 - 3:20
    kuanzia miaka 30 katika nchi nyingine mpaka karibu miaka 70.
  • 3:20 - 3:23
    Na mwaka 1962 kulikuwa na kundi kubwa la nchi hapa,
  • 3:23 - 3:28
    ambazo zilikuwa nchi zenye viwanda, na walikuwa na familia ndogo na maisha marefu.
  • 3:28 - 3:30
    Na hizi zilikuwa nchi zinazoendelea:
  • 3:30 - 3:33
    walikuwa na familia kubwa na walikuwa na maisha mafupi.
  • 3:33 - 3:37
    Sasa nini kimetokea toka mwaka 1962? Tunataka kuona mabadiliko.
  • 3:37 - 3:40
    Je wanafunzi wako sahihi? Bado ni aina mbili za nchi?
  • 3:41 - 3:44
    Au hizi nchi zilizoendelea zina familia ndogo na wanaishi hapa?
  • 3:44 - 3:46
    Au wana maisha marefu na wanaishi hapo juu?
  • 3:46 - 3:49
    Hebu tuone. Tulisimamisha dunia wakati ule. Hizi zote ni takwimu za Umoja wa Mataifa
  • 3:49 - 3:52
    ambazo zinapatikana. Hebu tuone. Unaweza kuona kule?
  • 3:52 - 3:55
    Ni China kule, ikiendelea dhidi ya afya bora hapa, inaboreka kule.
  • 3:55 - 3:58
    Nchi zote za kijani za Amerika ya Kusini zimeanza kuelekea kuwa na familia ndogo.
  • 3:58 - 4:01
    Hizi za njano hapa ni nchi za Kiarabu,
  • 4:01 - 4:05
    na wana familia kubwa, lakini wao -- hawana maisha marefu, lakini si familia kubwa.
  • 4:05 - 4:08
    Waafrika ni kijani hapa chini. Bado wamebaki hapa.
  • 4:08 - 4:11
    Hii ni India. Indonesia inaenda kwa kasi sana.
  • 4:11 - 4:12
    (Kicheko)
  • 4:12 - 4:15
    Na miaka ya 80 hapa, kuna Bangladesh bado iko miongoni mwa nchi za Afrika kule.
  • 4:15 - 4:18
    Lakini sasa, Bangladesh -- ni miujiza iliyotokea miaka ya 80:
  • 4:18 - 4:21
    Maimamu walianza kuhamasisha uzazi wa mpango.
  • 4:21 - 4:26
    Walisogea juu kwenye ile kona. Na katika miaka ya 90, tulikuwa na janga la Ukimwi
  • 4:26 - 4:29
    ambalo lilishusha umri wa kuishi wa nchi za Afrika
  • 4:29 - 4:33
    na nyingine zote zilipanda kwenye ile kona,
  • 4:33 - 4:37
    ambako tuna maisha marefu na familia ndogo, na tuna ulimwengu mpya kabisa.
  • 4:37 - 4:50
    (Makofi)
  • 4:50 - 4:55
    Ngoja nifananishe kati ya Marekani na Vietnam.
  • 4:55 - 5:00
    1964: Marekani ilikuwa na familia ndogo na maisha marefu;
  • 5:00 - 5:04
    Vietnam ilikuwa na familia kubwa na maisha mafupi. Na hiki ndicho kilichotokea:
  • 5:04 - 5:10
    takwimu wakati wa vita zilionyesha kuwa pamoja na vifo vyote,
  • 5:10 - 5:13
    kulikuwa kuna mabadiliko katika umri wa kuishi. Mwisho wa mwaka,
  • 5:13 - 5:16
    uzazi wa mpango ulianza Vietnam na waliamua kuwa na familia ndogo.
  • 5:16 - 5:19
    Na Marekani pale juu wanakuwa na maisha marefu,
  • 5:19 - 5:22
    wanabaki na ukubwa wa familia. Na miaka ya 80 sasa,
  • 5:22 - 5:25
    waliacha mpango wa kikomunisti na wakaingia kwenye uchumi wa soko huria,
  • 5:25 - 5:29
    na inaenda haraka hata zaidi ya maisha ya jamii. Na leo,
  • 5:29 - 5:34
    Vietnam ina umri wa kuishi na ukubwa wa familia sawa
  • 5:34 - 5:41
    hapa Vietnam, 2003, kama ilivyokuwa Marekani, 1974, mwishoni mwa vita.
  • 5:41 - 5:45
    Nafikiri sote -- kama hatutaangalia vielelezo --
  • 5:45 - 5:49
    tutapuuza mabadiliko makubwa huko Asia, ambayo yalikuwa
  • 5:49 - 5:53
    mabadiliko ya kijamii kabla hatujaona mabadiliko ya kiuchumi.
  • 5:53 - 5:58
    Hebu tuendelee kwingine hapa ambako tunaweza kuonyesha
  • 5:58 - 6:05
    mgawanyo wa kipato duniani. Hii ni mgao wa kipato cha watu.
  • 6:05 - 6:10
    Dola moja, dola 10 au dola 100 kwa siku.
  • 6:10 - 6:14
    Hakuna pengo tena kati ya matajiri na maskini. Hii ni hali ya kufikirika
  • 6:14 - 6:18
    Kuna kituta kidogo hapa. Lakini kuna watu kila sehemu.
  • 6:19 - 6:23
    Na tukiangalia kipato kinapoishia -- kipato hicho --
  • 6:23 - 6:29
    hii ni asilimia 100 ya kipato cha dunia kwa mwaka. Na asilimia 20 ya matajiri wakubwa kabisa,
  • 6:29 - 6:36
    wanachukua karibu asilimia 74. Na asilimia 20 ya masikini zaidi,
  • 6:36 - 6:41
    wanachukua karibu asilimia mbili. Na hii inaonyesha kwamba dhana
  • 6:41 - 6:45
    ya nchi zinazoendelea ni ya mashaka. Tunafikiria kuhusu misaada, kama
  • 6:45 - 6:50
    watu hawa wanatoa misaada kwa watu wale pale. Lakini katikati,
  • 6:50 - 6:54
    tuna idadi kubwa ya watu duniani, wenye asilimia 24 ya kipato.
  • 6:54 - 6:58
    Tuliyasikia haya kwa namna nyingine. Na hawa ni akina nani?
  • 6:58 - 7:02
    Nchi mbalimbali ziko wapi? Naweza kukuonyesha Afrika.
  • 7:02 - 7:07
    Hii ni Afrika. Asilimia 10 ya idadi ya watu duniani, wengi wao wako kwenye umaskini.
  • 7:07 - 7:12
    Hii ni OECD. Nchi tajiri. Nchi za kundi la Umoja wa Mataifa.
  • 7:12 - 7:17
    Na wapo huku upande huu. Kuna mwingiliano kati ya Afrika na OECD
  • 7:17 - 7:20
    Hii hapa ni Amerika Kusini. Ni kila kitu katika dunia hii,
  • 7:20 - 7:23
    kuanzia maskini zaidi mpaka matajiri, huko Amerika Kusini.
  • 7:23 - 7:28
    Zaidi ya hayo, tunaweza kuiweka Ulaya Mashariki, Asia Mashariki,
  • 7:28 - 7:33
    na Asia Kusini. Na ingekuwaje iwapo tungerejea nyuma,
  • 7:33 - 7:38
    mpaka mwaka 1970? Wakati huo kulikuwa na nundu kubwa zaidi.
  • 7:38 - 7:42
    Na waliokuwa kwenye umaskini mkubwa zaidi ni Waasia.
  • 7:42 - 7:49
    Tatizo la dunia lilikuwa umaskini huko Asia. Na sasa kama nitaicha dunia isogee mbele,
  • 7:49 - 7:52
    utaona kwamba wakati idadi ya watu inaongezeka, kuna
  • 7:52 - 7:55
    mamia ya milioni huko Asia wanajikwamua kutoka umaskini na wengine
  • 7:55 - 7:58
    wanaingia katika umaskini, na hii ndiyo hali tuliyonayo leo hii.
  • 7:58 - 8:02
    Na makadirio mazuri kutoka Benki ya Dunia, ni kwamba haya yatatokea,
  • 8:02 - 8:06
    na hatutakuwa na dunia iliyogawanyika. Tutakuwa na watu wengi katikati.
  • 8:06 - 8:08
    Naam, hiki ni kipimo cha logarithm,
  • 8:08 - 8:13
    lakini dhana yetu ya uchumi ni kukua kwa asilimia. Tunaiangalia
  • 8:13 - 8:19
    kama ni uwezekano wa kuongezeka kwa asilimia. Kama nitabadili hii, na kuchukua
  • 8:19 - 8:23
    GDP kwa taifa badala ya kipato cha familia, na ninabadili hivi
  • 8:23 - 8:29
    takwimu moja moja kwenye takwimu za kanda za GDP,
  • 8:29 - 8:33
    na ninazileta kanda hapa chini, ukubwa wa kiputo bado ni idadi ya watu.
  • 8:33 - 8:36
    Na una OECD pale, na una Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara hapo,
  • 8:36 - 8:39
    na tunatoa nchi za Kiarabu pale,
  • 8:39 - 8:43
    zinatoka Afrika na Asia, na tunaziweka tofauti,
  • 8:43 - 8:48
    na tunaweza kuukuza muhimili huu, na ninaipa vipimo vipya hapa,
  • 8:48 - 8:51
    kwa kuongeza thamani ya ustawi wa jamii pale, uwezekano wa kusalimika mtoto.
  • 8:51 - 8:56
    Sasa nimeweka pesa pale kwenye mhimili, na nina uwezekano wa watoto kusalimika pale.
  • 8:56 - 9:00
    Katika baadhi ya nchi, asilimia 99.7 ya watoto wanaishi mpaka miaka mitano;
  • 9:00 - 9:04
    wengine, mika 70 tu. Na hapa inaonekana kuna pengo
  • 9:04 - 9:08
    kati ya OECD, Amerika Kusini, Ulaya Mashariki, Asia Mashariki,
  • 9:08 - 9:12
    Nchi za kiarabu, Asia Kusini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.
  • 9:12 - 9:17
    Uwiano baina ya maisha ya watoto na pesa ni wa karibu sana.
  • 9:17 - 9:25
    Lakini hebu niigawanye Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Afya iko hapa na afya bora iko kule.
  • 9:25 - 9:30
    Ninaweza kwenda hapa na kuigawa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara katika nchi tofauti.
  • 9:30 - 9:35
    Na ikipasuka, ukubwa wa puto la nchi ni sawa na idadi ya watu.
  • 9:35 - 9:39
    Hapa chini ni Siera Leone. Mauritus iko pale juu. Mauritius ilikuwa nchi ya kwanza
  • 9:39 - 9:42
    kuondokana na vikwazo vya biashara, na waliweza kuuza sukari yao.
  • 9:43 - 9:48
    Waliweza kuuza nguo kwa taratibu sawa na watu wa Ulaya na Amerika Kaskazini.
  • 9:48 - 9:52
    Kuna tofauti kubwa sana ndani ya Afrika. Na Ghana iko hapa katikati.
  • 9:52 - 9:55
    Huko Siera Leone, misaada ya kibinadamu.
  • 9:55 - 10:00
    Hapa Uganda, misaada ya maendeleo. Hapa, muda wa kuwekeza, kule,
  • 10:00 - 10:03
    unaweza kwenda kwa mapumziko. Ni tofauti kubwa sana
  • 10:03 - 10:08
    katika Afrika ambayo mara nyingi tunaitambua -- kuwa iko sawa kwa kila kitu.
  • 10:08 - 10:12
    Naweza kuigawa Asia Kusini hapa. India ni kiputo kikubwa cha katikati.
  • 10:12 - 10:16
    Lakini kuna tofauti kubwa kati ya Afghanistani na Sri Lanka.
  • 10:16 - 10:20
    Naweza kugawa nchi za Kiarabu. Wakoje? Hali ya hewa sawa, utamaduni sawa,
  • 10:20 - 10:24
    dini sawa. Tofauti kubwa. Hata kati ya majirani.
  • 10:24 - 10:29
    Yemen, vita vya wao kwa wao. Umoja wa Falme za Kiarabu, pesa ya kutosha ni sawa na ikatumiwa vizuri.
  • 10:29 - 10:36
    Sio kama tunavyofikiria. Na hii inajumuisha watoto wa raia wa kigeni ambao wapo nchini.
  • 10:36 - 10:40
    Takwimu ni bora zaidi ya unavyofikiria. Watu wengi wanasema takwimu ni mbaya.
  • 10:41 - 10:43
    Kuna nafasi ya mashaka, lakini tunaweza kuona tofauti hapa:
  • 10:43 - 10:46
    Cambodia, Singapore. Tofauti ni kubwa
  • 10:46 - 10:49
    zaidi ya udhaifu wa takwimu. Ulaya Mashariki:
  • 10:49 - 10:55
    Uchumi wa Kisovieti muda mrefu, lakini waliweza kujikwamua baada ya miaka kumi
  • 10:55 - 10:58
    kwa utofauti sana. Na kuna Amerika Kusini.
  • 10:58 - 11:02
    Leo, hatuna haja ya kwenda Cuba kutafuta nchi yenye afya bora Amerika Kusini.
  • 11:02 - 11:07
    Chile itakuwa na idadi ndogo ya vifo vya watoto zaidi ya Cuba miaka michache ijayo kuanzia sasa.
  • 11:07 - 11:10
    Na hapa tuna nchi zenye kipato kikubwa katika OECD.
  • 11:10 - 11:14
    Na hapa tunapata mwelekeo wote wa ulimwengu,
  • 11:14 - 11:19
    ambao ni karibu ni sawa na hali hii. Na tukiiangalia,
  • 11:19 - 11:25
    inavyoonekana -- dunia, mwaka 1960, inaanza kusogea. 1960.
  • 11:25 - 11:28
    Huyu ni Mao Tse-tung. Alileta afya China. Halafu akafariki.
  • 11:28 - 11:33
    Halafu akaja Deng Xiaoping na akaleta pesa kwa China, na kuwapandisha chati tena.
  • 11:33 - 11:37
    Na tumeona jinsi nchi zinavyosogea katika mwenendo tofauti kama hivi,
  • 11:37 - 11:41
    kwa hiyo inakuwa vigumu kupata
  • 11:41 - 11:46
    mfano wa nchi ambayo inaonyesha mwelekeo wa ulimwengu.
  • 11:46 - 11:52
    Ningependa kuwarudisha nyuma mpaka karibu na mwaka 1960.
  • 11:52 - 12:02
    Ningependa kulinganisha Korea Kusini ambayo ni hii hapa, na Brazil,
  • 12:02 - 12:07
    ambayo ni hii hapa. Kibandiko kimetoka hapa. Na ningependa kufananisha Uganda,
  • 12:07 - 12:12
    ambayo iko kule. Na ninaweza kuileta mbele, kama hivi.
  • 12:12 - 12:21
    Na unaweza kuona jinsi Korea Kusini wanavyosonga mbele kwa kasi sana,
  • 12:21 - 12:24
    wakati Brazil inakwenda polepole.
  • 12:24 - 12:30
    Na kama tukirudi nyuma tena, hapa, na tukiweka alama juu yao, kama hivi,
  • 12:30 - 12:34
    unaweza kuona tena kuwa kasi ya maendeleo
  • 12:34 - 12:40
    ni tofauti sana, na nchi zinasogea sana au kidogo
  • 12:40 - 12:44
    katika kiwango sawa na kukua kwa pesa na afya, lakini inaonekana unaweza kusogea
  • 12:44 - 12:48
    haraka sana iwapo una afya kwanza kuliko ukiwa na pesa kwanza.
  • 12:49 - 12:53
    na kuonyesha hii, unaweza kuweka Umoja wa Falme za Kiarabu.
  • 12:53 - 12:56
    Walitokea hapa, nchi ya madini. Walivuna mafuta yote,
  • 12:56 - 13:00
    walipata pesa zote, lakini afya haiwezi kununuliwa dukani.
  • 13:00 - 13:04
    Inabidi uwekeze kwenye afya. Inabidi uwapeleke watoto shule.
  • 13:04 - 13:07
    Inabidi kuwafunza wafanyakazi wa afya. Inabidi kuwaelimisha watu.
  • 13:07 - 13:10
    Na Sheikh Sayed alifanya hivyo kwa namna nzuri.
  • 13:10 - 13:14
    Pamoja na kuanguka kwa bei ya mafuta, aliipandisha nchi yake hapa juu.
  • 13:14 - 13:18
    Kwa hiyo tumepata muelekeo wa ulimwengu,
  • 13:18 - 13:20
    ambapo nchi zote zinatabia ya kutumia pesa zao
  • 13:20 - 13:25
    vizuri zaidi ya walivyokuwa wakitumia huko nyuma. Naam, hivi ndivyo, zaidi au pungufu kidogo,
  • 13:25 - 13:32
    ukiangalia wastani wa takwimu za nchi. Ziko kama hivi.
  • 13:32 - 13:37
    Sasa hii ni hatari, kutumia wastani wa takwimu, kwasababu kuna
  • 13:37 - 13:43
    tofauti kubwa kati ya nchi. Kwa hiyo nikienda kuangalia hapa, tunaona
  • 13:43 - 13:49
    kuwa Uganda ya leo ni mahali ambapo Korea ya Kusnini ilikuwa mwaka 1960. Na kama nikiigawa Uganda,
  • 13:49 - 13:54
    kuna tofauti ndani ya Uganda. Hii ni moja ya tano ya takwimu ndani ya Uganda.
  • 13:54 - 13:57
    Asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Uganda wako pale.
  • 13:57 - 14:01
    Masikini zaidi wako hapa chini. Iwapo nikiigawa Afrika Kusini, iko kama hivi.
  • 14:01 - 14:06
    Na iwapo nikiangalia Niger, ambako kulikuwa na ukame mbaya sana,
  • 14:06 - 14:11
    mwishoni, iko kama hivi. Asilimia 20 ya masikini zaidi huko Niger wako hapa,
  • 14:11 - 14:14
    na asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Afrika Kusini wako kule,
  • 14:14 - 14:19
    na bado tunatabia ya kuzungumzia kuhusu utatuzi upi unafaa kwa matatizo ya Afrika.
  • 14:19 - 14:22
    Kila kitu kilichopo hapa duniani kinapatikana Afrika. Na hamuwezi
  • 14:22 - 14:26
    kuongelea upatikanaji wa dawa za VVU [madawa] kwa moja ya tano hapa juu
  • 14:26 - 14:30
    kwa mkakati sawa kama hapa chini. Maendeleo ya ulimwengu
  • 14:30 - 14:35
    ni lazima yawekwe kwa makundi tofauti, na si lazima kuwa nayo
  • 14:35 - 14:38
    katika ngazi ya kanda. Ni lazima tuingie ndani zaidi.
  • 14:38 - 14:42
    Tumetambua kuwa wanafunzi wanapatwa na mshawasha wakiweza kutumia hii.
  • 14:42 - 14:47
    Na wapanga sera na sekta binafsi zingependa kuona
  • 14:47 - 14:51
    namna gani dunia inabadilika. Sasa, kwanini hii haitokei?
  • 14:51 - 14:55
    Kwanini hatutumii takwimu tulizonazo? Tuna takwimu katika Umoja wa Mataifa,
  • 14:55 - 14:57
    na katika taasisi za takwimu za nchi
  • 14:57 - 15:01
    na katika vyuo vikuu na mashirika yasiyo ya kiserikali.
  • 15:01 - 15:03
    Kwasababu takwimu zimefichwa kwenye masijala.
  • 15:03 - 15:08
    Na umma uko pale, na mtandao wa Intaneti uko, lakini bado hatujautumia ipasavyo.
  • 15:08 - 15:11
    Taarifa zote tunazoziona zikibadilika duniani
  • 15:11 - 15:15
    hazihusishi takwimu zinazogharimiwa na umma. Kuna baadhi ya kurasa za tovuti
  • 15:15 - 15:21
    mfano hii, kama ujuavyo, lakini zinachukua kutoka kwenye masijala ya takwimu,
  • 15:21 - 15:26
    lakini watu wanaziwekea bei, funguo za siri na takwimu za kuchosha.
  • 15:26 - 15:29
    (Kicheko). (Makofi).
  • 15:29 - 15:33
    Na hii haitatusaidia. Sasa nini kinatakiwa? Tuna masijala za takwimu.
  • 15:33 - 15:37
    Si masijala mpya ya takwimu unayoihitaji. Tuna vifaa vizuri vya ubunifu,
  • 15:37 - 15:40
    na vingi vinaongezewa hapa. Kwa hiyo tulianzisha
  • 15:40 - 15:45
    shirika lisilo la kibiashara ambalo tukaliita -- kuunganisha takwimu kwa ubunifu --
  • 15:45 - 15:48
    tunaiita Gapminder, kutoka London chini ya ardhi, ambako wanakuonya,
  • 15:48 - 15:51
    "angalia upenyo" Kwa hiyo tulifikiri Gapminder ilikuwa ni sahihi.
  • 15:51 - 15:55
    Na tulianza kuandika programu ya kompyuta ambayo ingeweza kuunganisha takwimu kama hivi.
  • 15:55 - 16:01
    Na haikuwa vigumu sana. Iliwachukua watu wengine miaka kadhaa, na tumetengeneza vielelezo.
  • 16:01 - 16:03
    Unaweza kuchukua seti ya takwimu na kuiweka hapa.
  • 16:03 - 16:08
    Tunakomboa takwimu za Umoja wa Mataifa, mashirika machache ya Umoja wa Mataifa.
  • 16:08 - 16:12
    Nchi nyingine zinakubali takwimu zao ziwe wazi duniani,
  • 16:12 - 16:15
    lakini tunachohitaji zaidi ni, kwa hakika, namna ya kuzichambua.
  • 16:15 - 16:20
    Programu ya kutafuta ambayo itakuwezesha kunakili takwimu katika muundo wa kutafutika
  • 16:20 - 16:23
    na kuiweka wazi duniani. Na nini tunasikia tuzungukapo?
  • 16:23 - 16:27
    Nimefanya anthopolojia katika sehemu kubwa za takwimu. Kila mtu anasema,
  • 16:28 - 16:32
    "Haiwezekani. Hii haiwezi kufanyika. Taarifa zetu ni za ovyoovyo
  • 16:32 - 16:35
    kwa ndani, na kwahiyo haziwezi kupangiliwa zitafutike kama nyingine zinavyoweza kutafutwa.
  • 16:35 - 16:40
    Hatuwezi kutoa takwimu bure kwa wanafunzi, bure kwa wajasiliamali wa dunia."
  • 16:40 - 16:43
    Lakini hivi ndivyo tungependa tuone, au sio?
  • 16:43 - 16:46
    Takwimu zilizogharimiwa na umma zipo hapa chini.
  • 16:46 - 16:49
    Na tungependa maua yaote nje kwenye mtandao.
  • 16:49 - 16:54
    Na jambo la muhimu zaidi ni kuzipangilia ili ziweze kutafutika, na watu waweze kuzitumia
  • 16:54 - 16:56
    vifaa tofauti vya ubunifu kueleleza pale.
  • 16:56 - 17:01
    Nina habari nzuri kwenu. Nina habari nzuri kwamba,
  • 17:01 - 17:05
    Mkuu wa Kitengo cha Takwimu cha Umoja wa Mataifa, hasemi haiwezekani.
  • 17:05 - 17:07
    Anasema, "Hatuwezi kufanya."
  • 17:07 - 17:11
    (Kicheko)
  • 17:11 - 17:13
    Huyu ni mtu mwenye akili, eeeh?
  • 17:13 - 17:15
    (Kicheko)
  • 17:15 - 17:19
    Kwa hiyo tunaona mambo mengi yakitokea kwenye takwimu katika miaka ijayo.
  • 17:19 - 17:23
    Tutaweza kuangalia mgawanyo wa kipato katika namna mpya kabisa.
  • 17:23 - 17:28
    Huu ni mgao wa kipato huko China, 1970,
  • 17:29 - 17:34
    mgao wa kipato wa Marekani, 1970.
  • 17:34 - 17:38
    Karibu hakuna mwingiliano, karibu hakuna mwingiliano. Na nini kimetokea?
  • 17:38 - 17:43
    Kilichotokea ni hiki: China inakua, haiko sawa tena,
  • 17:43 - 17:47
    na inatokea hapa, ikiingalia Marekani.
  • 17:47 - 17:49
    Kama vile mzuka, au sio, eeeh?
  • 17:49 - 17:51
    (Kicheko)
  • 17:51 - 18:01
    Inatisha. Lakini nadhani ni muhimu sana kuwa na taarifa hizi.
  • 18:01 - 18:07
    Tunahitaji sana kuziona. Badala ya kuangalia hii,
  • 18:07 - 18:12
    ningependa kumalizia kwa kuwaonyesha watumiaji wa mtandao kwa kila 1,000.
  • 18:12 - 18:17
    Katika programu hii ya kompyuta, tunaweza kupata karibu alama 500 kutoka katika nchi zote kwa urahisi.
  • 18:17 - 18:21
    Inachukua muda kubadilika kwa hii,
  • 18:21 - 18:26
    lakini katika mihimili, unaweza kupata alama yeyote utakayopenda kupata.
  • 18:26 - 18:31
    Na kitu kizuri itakuwa ni kuziweka masijala za takwimu bure,
  • 18:31 - 18:34
    kuweza kuzifanya ziweze kutafutika, na kuzipata kwa kubonyeza kwa nukta moja
  • 18:34 - 18:39
    kwenye mfumo wa michoro majira ya nukta, ambapo utazielewa kwa urahisi.
  • 18:39 - 18:42
    Naam, wanatakwimu hawazipendi, kwasababu wanasema kuwa hii
  • 18:42 - 18:51
    haitaonyesha hali halisi; inabidi tuwe na mbinu za kuchambua takwimu.
  • 18:51 - 18:54
    Lakini hii inajenga nadharia.
  • 18:54 - 18:58
    Ninamalizia sasa na dunia. Pale, mtandao wa intaneti unakuja.
  • 18:58 - 19:02
    Idadi ya wanaotumia mtandao inaongezeka kama hivi. Hii ni GDP per capita
  • 19:02 - 19:07
    Na ni teknolojia mpya inayokuja, lakini cha kushangaza, ni namna ambavyo
  • 19:07 - 19:12
    inashabihiana na hali ya uchumi wa nchi. Ndio maana
  • 19:12 - 19:15
    kompyuta ya dola 100 itakuwa ya muhimu sana. Lakini ni muelekeo mzuri.
  • 19:15 - 19:18
    Ni kama vile dunia inakuwa bapa. Au sio? Nchi hizi
  • 19:18 - 19:21
    zinanyanyuka zaidi ya uchumi na itakuwa ni ya kufurahisha
  • 19:21 - 19:25
    kufuatilia hii kwa miaka ijayo, na kama ambavyo ningependa muweze kufanya
  • 19:25 - 19:27
    kwa kutumia takwimu zilizogharamiwa na umma. Asanteni sana.
  • 19:28 - 19:31
    (Makofi)
Title:
Hans Rosling aonyesha takwimu bora kuliko zote ulizoziona
Speaker:
Hans Rosling
Description:

Hujapata kuona takwimu zikielelezwa namna hii. Kwa ufundi na umahiri wa kuhadhiri, gwiji wa takwimu Hans Rosling anachambua mtazamo potofu uitwao "nchi zinazoendelea."

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
19:33
TED added a translation

Swahili subtitles

Revisions