[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:00.00,0:00:04.00,Default,,0000,0000,0000,,Takriban miaka 10 iliyopita, nilianza kazi ya kufundisha maendeleo ya ulimwengu Dialogue: 0,0:00:04.00,0:00:08.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa wanafunzi wa Kiswidishi wa shahada ya kwanza. Hii ilikuwa baada ya Dialogue: 0,0:00:08.00,0:00:12.00,Default,,0000,0000,0000,,takriban miaka 20 ya kufanya kazi pamoja na taasisi mbalimbali za Afrika nikitafiti kuhusu njaa Dialogue: 0,0:00:12.00,0:00:16.00,Default,,0000,0000,0000,,katika Afrika, kwa hiyo nilikuwa natarajiwa niwe najua zaidi kuhusu dunia. Dialogue: 0,0:00:16.00,0:00:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Na nilianzia kwenye chuo chetu cha utabibu, Taasisi ya Karolinska, Dialogue: 0,0:00:21.00,0:00:25.00,Default,,0000,0000,0000,,kozi ya shahada ya kwanza iliyoitwa Afya ya Ulimwengu. Lakini ukipata Dialogue: 0,0:00:25.00,0:00:28.00,Default,,0000,0000,0000,,fursa hiyo, unapata mshawasha kidogo. Nilifikiri wanafunzi hawa Dialogue: 0,0:00:28.00,0:00:31.00,Default,,0000,0000,0000,,kuja kwetu ni lazima wana maksi za juu unazoweza kupata Dialogue: 0,0:00:31.00,0:00:34.00,Default,,0000,0000,0000,,kwenye mfumo wa vyuo vya Sweden -- kwahiyo labda wanajua kila kitu Dialogue: 0,0:00:34.00,0:00:38.00,Default,,0000,0000,0000,,kuhusu nitakachowafundisha. Kwa hiyo niliwapa mtihani mara tu walipokuja. Dialogue: 0,0:00:38.00,0:00:41.00,Default,,0000,0000,0000,,Na moja wapo kati ya maswali ambayo nilijifunza mengi ni hili hapa: Dialogue: 0,0:00:41.00,0:00:45.00,Default,,0000,0000,0000,,"Ni nchi gani kati ya hizi tano ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto kati ya jozi hizi tano?" Dialogue: 0,0:00:45.00,0:00:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Na niliziweka pamoja, ili katika kila kundi la nchi, Dialogue: 0,0:00:49.00,0:00:54.00,Default,,0000,0000,0000,,moja ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto zaidi ya nyingine. Na hii inamaanisha kwamba Dialogue: 0,0:00:54.00,0:00:59.00,Default,,0000,0000,0000,,kuna tofauti kubwa sana kuliko uhakika wa takwimu. Dialogue: 0,0:00:59.00,0:01:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Sitawapa mtihani hapa, lakini ni Uturuki, Dialogue: 0,0:01:01.00,0:01:06.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ina kiwango kikubwa pale, Poland, Urusi, Pakistani na Afrika Kusini. Dialogue: 0,0:01:06.00,0:01:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Na haya ndiyo majibu ya wanafunzi wa Kiswidishi. Nilifanya hivyo na nilipata Dialogue: 0,0:01:09.00,0:01:12.00,Default,,0000,0000,0000,,kiwango cha imani, ambacho kilikuwa kidogo, na nilifurahi, Dialogue: 0,0:01:12.00,0:01:16.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa hakika: 1.8 ya jibu sahihi kati ya matano inawezekana. Hii ina maana kwamba Dialogue: 0,0:01:16.00,0:01:19.00,Default,,0000,0000,0000,,kulikuwa kuna nafasi ya Profesa wa afya ya ulimwengu -- Dialogue: 0,0:01:19.00,0:01:21.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) na kwa kozi yangu. Dialogue: 0,0:01:21.00,0:01:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini usiku mmoja, wakati nilipokuwa natayarisha ripoti Dialogue: 0,0:01:25.00,0:01:29.00,Default,,0000,0000,0000,,Niligundua uvumbuzi wangu. Nimeonyesha Dialogue: 0,0:01:29.00,0:01:34.00,Default,,0000,0000,0000,,kuwa wanafunzi Waswidishi wenye alama za juu wanajua kidogo sana kuhusu takwimu Dialogue: 0,0:01:34.00,0:01:36.00,Default,,0000,0000,0000,,za ulimwengu kuliko hata sokwe. Dialogue: 0,0:01:36.00,0:01:38.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:01:38.00,0:01:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwasababu sokwe wangepata nusu iwapo ningewapa Dialogue: 0,0:01:42.00,0:01:45.00,Default,,0000,0000,0000,,ndizi mbili zenye Sri Lanka na Uturuki. Wangekuwa sahihi kwa nusu yake. Dialogue: 0,0:01:45.00,0:01:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini wanafunzi hawapo huko. Tatizo langu halikuwa kutokujua kwao: Dialogue: 0,0:01:49.00,0:01:52.00,Default,,0000,0000,0000,,ilikuwa ni mawazo waliyojijengea. Dialogue: 0,0:01:52.00,0:01:56.00,Default,,0000,0000,0000,,Pia nilifanya utafiti kinyume na maadili kwa maprofesa wa taasisi ya Karolinska Dialogue: 0,0:01:56.00,0:01:57.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:01:57.00,0:01:59.00,Default,,0000,0000,0000,,-- ambao wanatoa tuzo ya Nobel katika utabibu, Dialogue: 0,0:01:59.00,0:02:01.00,Default,,0000,0000,0000,,na wao wako sawa tu na sokwe. Dialogue: 0,0:02:01.00,0:02:04.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:02:04.00,0:02:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Hapa ndipo nilipogundua kwamba kuna haja ya kuwasiliana, Dialogue: 0,0:02:08.00,0:02:11.00,Default,,0000,0000,0000,,kwasababu ya takwimu za kinachotokea duniani Dialogue: 0,0:02:11.00,0:02:14.00,Default,,0000,0000,0000,,na afya ya mtoto katika kila nchi inajulikana. Dialogue: 0,0:02:14.00,0:02:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Tulitengeneza hii programu ya kompyuta ambayo inayoonyesha kama hivi: kila kiputo hapa ni nchi. Dialogue: 0,0:02:19.00,0:02:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii nchi hapa ni China. Hii ni India. Dialogue: 0,0:02:25.00,0:02:31.00,Default,,0000,0000,0000,,Ukubwa wa kiputo ni idadi ya watu, na katika mhimili huu nimeweka kiwango cha uzazi. Dialogue: 0,0:02:31.00,0:02:34.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwasababu wanafunzi wangu, walichosema Dialogue: 0,0:02:34.00,0:02:36.00,Default,,0000,0000,0000,,wakati walipoangalia dunia, na nilipowauliza, Dialogue: 0,0:02:36.00,0:02:38.00,Default,,0000,0000,0000,,"Nini mnafikiri kuhusu dunia?" Dialogue: 0,0:02:38.00,0:02:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Naam, kwanza niligundua kuwa kitabu cha kiada kilikuwa Tintin, angalau. Dialogue: 0,0:02:42.00,0:02:43.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:02:43.00,0:02:46.00,Default,,0000,0000,0000,,Na walisema, "Dunia bado ni 'sisi' na 'wao.' Dialogue: 0,0:02:46.00,0:02:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Na sisi ni dunia ya Magharibi na wao ni Dunia ya Tatu." Dialogue: 0,0:02:49.00,0:02:52.00,Default,,0000,0000,0000,,"Na una maana gani kwa kusema dunia ya magharibi?" Niliuliza. Dialogue: 0,0:02:52.00,0:02:57.00,Default,,0000,0000,0000,,"Naam, haya ni maisha marefu na familia ndogo, na dunia ya tatu ni maisha mafupi na familia kubwa." Dialogue: 0,0:02:57.00,0:03:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo hii ndio ninayoweza kuonyesha hapa. Niliweka kiwango cha uzazi hapa: idadi ya watoto kwa mwanamke, Dialogue: 0,0:03:03.00,0:03:07.00,Default,,0000,0000,0000,,moja, mbili, tatu, nne, mpaka watoto nane kwa mwanamke mmoja. Dialogue: 0,0:03:07.00,0:03:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Tuna takwimu nzuri sana toka mwaka 1962 -- 1960 kuhusu -- ukubwa wa familia katika nchi zote. Dialogue: 0,0:03:13.00,0:03:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Kiwango cha makosa ni kidogo sana. Hapa naweka umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa, Dialogue: 0,0:03:16.00,0:03:20.00,Default,,0000,0000,0000,,kuanzia miaka 30 katika nchi nyingine mpaka karibu miaka 70. Dialogue: 0,0:03:20.00,0:03:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Na mwaka 1962 kulikuwa na kundi kubwa la nchi hapa, Dialogue: 0,0:03:23.00,0:03:28.00,Default,,0000,0000,0000,,ambazo zilikuwa nchi zenye viwanda, na walikuwa na familia ndogo na maisha marefu. Dialogue: 0,0:03:28.00,0:03:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hizi zilikuwa nchi zinazoendelea: Dialogue: 0,0:03:30.00,0:03:33.00,Default,,0000,0000,0000,,walikuwa na familia kubwa na walikuwa na maisha mafupi. Dialogue: 0,0:03:33.00,0:03:37.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa nini kimetokea toka mwaka 1962? Tunataka kuona mabadiliko. Dialogue: 0,0:03:37.00,0:03:40.00,Default,,0000,0000,0000,,Je wanafunzi wako sahihi? Bado ni aina mbili za nchi? Dialogue: 0,0:03:41.00,0:03:44.00,Default,,0000,0000,0000,,Au hizi nchi zilizoendelea zina familia ndogo na wanaishi hapa? Dialogue: 0,0:03:44.00,0:03:46.00,Default,,0000,0000,0000,,Au wana maisha marefu na wanaishi hapo juu? Dialogue: 0,0:03:46.00,0:03:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Hebu tuone. Tulisimamisha dunia wakati ule. Hizi zote ni takwimu za Umoja wa Mataifa Dialogue: 0,0:03:49.00,0:03:52.00,Default,,0000,0000,0000,,ambazo zinapatikana. Hebu tuone. Unaweza kuona kule? Dialogue: 0,0:03:52.00,0:03:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Ni China kule, ikiendelea dhidi ya afya bora hapa, inaboreka kule. Dialogue: 0,0:03:55.00,0:03:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Nchi zote za kijani za Amerika ya Kusini zimeanza kuelekea kuwa na familia ndogo. Dialogue: 0,0:03:58.00,0:04:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Hizi za njano hapa ni nchi za Kiarabu, Dialogue: 0,0:04:01.00,0:04:05.00,Default,,0000,0000,0000,,na wana familia kubwa, lakini wao -- hawana maisha marefu, lakini si familia kubwa. Dialogue: 0,0:04:05.00,0:04:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Waafrika ni kijani hapa chini. Bado wamebaki hapa. Dialogue: 0,0:04:08.00,0:04:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni India. Indonesia inaenda kwa kasi sana. Dialogue: 0,0:04:11.00,0:04:12.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:04:12.00,0:04:15.00,Default,,0000,0000,0000,,Na miaka ya 80 hapa, kuna Bangladesh bado iko miongoni mwa nchi za Afrika kule. Dialogue: 0,0:04:15.00,0:04:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini sasa, Bangladesh -- ni miujiza iliyotokea miaka ya 80: Dialogue: 0,0:04:18.00,0:04:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Maimamu walianza kuhamasisha uzazi wa mpango. Dialogue: 0,0:04:21.00,0:04:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Walisogea juu kwenye ile kona. Na katika miaka ya 90, tulikuwa na janga la Ukimwi Dialogue: 0,0:04:26.00,0:04:29.00,Default,,0000,0000,0000,,ambalo lilishusha umri wa kuishi wa nchi za Afrika Dialogue: 0,0:04:29.00,0:04:33.00,Default,,0000,0000,0000,,na nyingine zote zilipanda kwenye ile kona, Dialogue: 0,0:04:33.00,0:04:37.00,Default,,0000,0000,0000,,ambako tuna maisha marefu na familia ndogo, na tuna ulimwengu mpya kabisa. Dialogue: 0,0:04:37.00,0:04:50.00,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi) Dialogue: 0,0:04:50.00,0:04:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Ngoja nifananishe kati ya Marekani na Vietnam. Dialogue: 0,0:04:55.00,0:05:00.00,Default,,0000,0000,0000,,1964: Marekani ilikuwa na familia ndogo na maisha marefu; Dialogue: 0,0:05:00.00,0:05:04.00,Default,,0000,0000,0000,,Vietnam ilikuwa na familia kubwa na maisha mafupi. Na hiki ndicho kilichotokea: Dialogue: 0,0:05:04.00,0:05:10.00,Default,,0000,0000,0000,,takwimu wakati wa vita zilionyesha kuwa pamoja na vifo vyote, Dialogue: 0,0:05:10.00,0:05:13.00,Default,,0000,0000,0000,,kulikuwa kuna mabadiliko katika umri wa kuishi. Mwisho wa mwaka, Dialogue: 0,0:05:13.00,0:05:16.00,Default,,0000,0000,0000,,uzazi wa mpango ulianza Vietnam na waliamua kuwa na familia ndogo. Dialogue: 0,0:05:16.00,0:05:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Na Marekani pale juu wanakuwa na maisha marefu, Dialogue: 0,0:05:19.00,0:05:22.00,Default,,0000,0000,0000,,wanabaki na ukubwa wa familia. Na miaka ya 80 sasa, Dialogue: 0,0:05:22.00,0:05:25.00,Default,,0000,0000,0000,,waliacha mpango wa kikomunisti na wakaingia kwenye uchumi wa soko huria, Dialogue: 0,0:05:25.00,0:05:29.00,Default,,0000,0000,0000,,na inaenda haraka hata zaidi ya maisha ya jamii. Na leo, Dialogue: 0,0:05:29.00,0:05:34.00,Default,,0000,0000,0000,,Vietnam ina umri wa kuishi na ukubwa wa familia sawa Dialogue: 0,0:05:34.00,0:05:41.00,Default,,0000,0000,0000,,hapa Vietnam, 2003, kama ilivyokuwa Marekani, 1974, mwishoni mwa vita. Dialogue: 0,0:05:41.00,0:05:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Nafikiri sote -- kama hatutaangalia vielelezo -- Dialogue: 0,0:05:45.00,0:05:49.00,Default,,0000,0000,0000,,tutapuuza mabadiliko makubwa huko Asia, ambayo yalikuwa Dialogue: 0,0:05:49.00,0:05:53.00,Default,,0000,0000,0000,,mabadiliko ya kijamii kabla hatujaona mabadiliko ya kiuchumi. Dialogue: 0,0:05:53.00,0:05:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Hebu tuendelee kwingine hapa ambako tunaweza kuonyesha Dialogue: 0,0:05:58.00,0:06:05.00,Default,,0000,0000,0000,,mgawanyo wa kipato duniani. Hii ni mgao wa kipato cha watu. Dialogue: 0,0:06:05.00,0:06:10.00,Default,,0000,0000,0000,,Dola moja, dola 10 au dola 100 kwa siku. Dialogue: 0,0:06:10.00,0:06:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Hakuna pengo tena kati ya matajiri na maskini. Hii ni hali ya kufikirika Dialogue: 0,0:06:14.00,0:06:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Kuna kituta kidogo hapa. Lakini kuna watu kila sehemu. Dialogue: 0,0:06:19.00,0:06:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Na tukiangalia kipato kinapoishia -- kipato hicho -- Dialogue: 0,0:06:23.00,0:06:29.00,Default,,0000,0000,0000,,hii ni asilimia 100 ya kipato cha dunia kwa mwaka. Na asilimia 20 ya matajiri wakubwa kabisa, Dialogue: 0,0:06:29.00,0:06:36.00,Default,,0000,0000,0000,,wanachukua karibu asilimia 74. Na asilimia 20 ya masikini zaidi, Dialogue: 0,0:06:36.00,0:06:41.00,Default,,0000,0000,0000,,wanachukua karibu asilimia mbili. Na hii inaonyesha kwamba dhana Dialogue: 0,0:06:41.00,0:06:45.00,Default,,0000,0000,0000,,ya nchi zinazoendelea ni ya mashaka. Tunafikiria kuhusu misaada, kama Dialogue: 0,0:06:45.00,0:06:50.00,Default,,0000,0000,0000,,watu hawa wanatoa misaada kwa watu wale pale. Lakini katikati, Dialogue: 0,0:06:50.00,0:06:54.00,Default,,0000,0000,0000,,tuna idadi kubwa ya watu duniani, wenye asilimia 24 ya kipato. Dialogue: 0,0:06:54.00,0:06:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Tuliyasikia haya kwa namna nyingine. Na hawa ni akina nani? Dialogue: 0,0:06:58.00,0:07:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Nchi mbalimbali ziko wapi? Naweza kukuonyesha Afrika. Dialogue: 0,0:07:02.00,0:07:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni Afrika. Asilimia 10 ya idadi ya watu duniani, wengi wao wako kwenye umaskini. Dialogue: 0,0:07:07.00,0:07:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni OECD. Nchi tajiri. Nchi za kundi la Umoja wa Mataifa. Dialogue: 0,0:07:12.00,0:07:17.00,Default,,0000,0000,0000,,Na wapo huku upande huu. Kuna mwingiliano kati ya Afrika na OECD Dialogue: 0,0:07:17.00,0:07:20.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii hapa ni Amerika Kusini. Ni kila kitu katika dunia hii, Dialogue: 0,0:07:20.00,0:07:23.00,Default,,0000,0000,0000,,kuanzia maskini zaidi mpaka matajiri, huko Amerika Kusini. Dialogue: 0,0:07:23.00,0:07:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Zaidi ya hayo, tunaweza kuiweka Ulaya Mashariki, Asia Mashariki, Dialogue: 0,0:07:28.00,0:07:33.00,Default,,0000,0000,0000,,na Asia Kusini. Na ingekuwaje iwapo tungerejea nyuma, Dialogue: 0,0:07:33.00,0:07:38.00,Default,,0000,0000,0000,,mpaka mwaka 1970? Wakati huo kulikuwa na nundu kubwa zaidi. Dialogue: 0,0:07:38.00,0:07:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Na waliokuwa kwenye umaskini mkubwa zaidi ni Waasia. Dialogue: 0,0:07:42.00,0:07:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Tatizo la dunia lilikuwa umaskini huko Asia. Na sasa kama nitaicha dunia isogee mbele, Dialogue: 0,0:07:49.00,0:07:52.00,Default,,0000,0000,0000,,utaona kwamba wakati idadi ya watu inaongezeka, kuna Dialogue: 0,0:07:52.00,0:07:55.00,Default,,0000,0000,0000,,mamia ya milioni huko Asia wanajikwamua kutoka umaskini na wengine Dialogue: 0,0:07:55.00,0:07:58.00,Default,,0000,0000,0000,,wanaingia katika umaskini, na hii ndiyo hali tuliyonayo leo hii. Dialogue: 0,0:07:58.00,0:08:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Na makadirio mazuri kutoka Benki ya Dunia, ni kwamba haya yatatokea, Dialogue: 0,0:08:02.00,0:08:06.00,Default,,0000,0000,0000,,na hatutakuwa na dunia iliyogawanyika. Tutakuwa na watu wengi katikati. Dialogue: 0,0:08:06.00,0:08:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Naam, hiki ni kipimo cha logarithm, Dialogue: 0,0:08:08.00,0:08:13.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini dhana yetu ya uchumi ni kukua kwa asilimia. Tunaiangalia Dialogue: 0,0:08:13.00,0:08:19.00,Default,,0000,0000,0000,,kama ni uwezekano wa kuongezeka kwa asilimia. Kama nitabadili hii, na kuchukua Dialogue: 0,0:08:19.00,0:08:23.00,Default,,0000,0000,0000,,GDP kwa taifa badala ya kipato cha familia, na ninabadili hivi Dialogue: 0,0:08:23.00,0:08:29.00,Default,,0000,0000,0000,,takwimu moja moja kwenye takwimu za kanda za GDP, Dialogue: 0,0:08:29.00,0:08:33.00,Default,,0000,0000,0000,,na ninazileta kanda hapa chini, ukubwa wa kiputo bado ni idadi ya watu. Dialogue: 0,0:08:33.00,0:08:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Na una OECD pale, na una Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara hapo, Dialogue: 0,0:08:36.00,0:08:39.00,Default,,0000,0000,0000,,na tunatoa nchi za Kiarabu pale, Dialogue: 0,0:08:39.00,0:08:43.00,Default,,0000,0000,0000,,zinatoka Afrika na Asia, na tunaziweka tofauti, Dialogue: 0,0:08:43.00,0:08:48.00,Default,,0000,0000,0000,,na tunaweza kuukuza muhimili huu, na ninaipa vipimo vipya hapa, Dialogue: 0,0:08:48.00,0:08:51.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa kuongeza thamani ya ustawi wa jamii pale, uwezekano wa kusalimika mtoto. Dialogue: 0,0:08:51.00,0:08:56.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa nimeweka pesa pale kwenye mhimili, na nina uwezekano wa watoto kusalimika pale. Dialogue: 0,0:08:56.00,0:09:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika baadhi ya nchi, asilimia 99.7 ya watoto wanaishi mpaka miaka mitano; Dialogue: 0,0:09:00.00,0:09:04.00,Default,,0000,0000,0000,,wengine, mika 70 tu. Na hapa inaonekana kuna pengo Dialogue: 0,0:09:04.00,0:09:08.00,Default,,0000,0000,0000,,kati ya OECD, Amerika Kusini, Ulaya Mashariki, Asia Mashariki, Dialogue: 0,0:09:08.00,0:09:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Nchi za kiarabu, Asia Kusini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Dialogue: 0,0:09:12.00,0:09:17.00,Default,,0000,0000,0000,,Uwiano baina ya maisha ya watoto na pesa ni wa karibu sana. Dialogue: 0,0:09:17.00,0:09:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini hebu niigawanye Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Afya iko hapa na afya bora iko kule. Dialogue: 0,0:09:25.00,0:09:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninaweza kwenda hapa na kuigawa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara katika nchi tofauti. Dialogue: 0,0:09:30.00,0:09:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Na ikipasuka, ukubwa wa puto la nchi ni sawa na idadi ya watu. Dialogue: 0,0:09:35.00,0:09:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Hapa chini ni Siera Leone. Mauritus iko pale juu. Mauritius ilikuwa nchi ya kwanza Dialogue: 0,0:09:39.00,0:09:42.00,Default,,0000,0000,0000,,kuondokana na vikwazo vya biashara, na waliweza kuuza sukari yao. Dialogue: 0,0:09:43.00,0:09:48.00,Default,,0000,0000,0000,,Waliweza kuuza nguo kwa taratibu sawa na watu wa Ulaya na Amerika Kaskazini. Dialogue: 0,0:09:48.00,0:09:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Kuna tofauti kubwa sana ndani ya Afrika. Na Ghana iko hapa katikati. Dialogue: 0,0:09:52.00,0:09:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Huko Siera Leone, misaada ya kibinadamu. Dialogue: 0,0:09:55.00,0:10:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Hapa Uganda, misaada ya maendeleo. Hapa, muda wa kuwekeza, kule, Dialogue: 0,0:10:00.00,0:10:03.00,Default,,0000,0000,0000,,unaweza kwenda kwa mapumziko. Ni tofauti kubwa sana Dialogue: 0,0:10:03.00,0:10:08.00,Default,,0000,0000,0000,,katika Afrika ambayo mara nyingi tunaitambua -- kuwa iko sawa kwa kila kitu. Dialogue: 0,0:10:08.00,0:10:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Naweza kuigawa Asia Kusini hapa. India ni kiputo kikubwa cha katikati. Dialogue: 0,0:10:12.00,0:10:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kuna tofauti kubwa kati ya Afghanistani na Sri Lanka. Dialogue: 0,0:10:16.00,0:10:20.00,Default,,0000,0000,0000,,Naweza kugawa nchi za Kiarabu. Wakoje? Hali ya hewa sawa, utamaduni sawa, Dialogue: 0,0:10:20.00,0:10:24.00,Default,,0000,0000,0000,,dini sawa. Tofauti kubwa. Hata kati ya majirani. Dialogue: 0,0:10:24.00,0:10:29.00,Default,,0000,0000,0000,,Yemen, vita vya wao kwa wao. Umoja wa Falme za Kiarabu, pesa ya kutosha ni sawa na ikatumiwa vizuri. Dialogue: 0,0:10:29.00,0:10:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Sio kama tunavyofikiria. Na hii inajumuisha watoto wa raia wa kigeni ambao wapo nchini. Dialogue: 0,0:10:36.00,0:10:40.00,Default,,0000,0000,0000,,Takwimu ni bora zaidi ya unavyofikiria. Watu wengi wanasema takwimu ni mbaya. Dialogue: 0,0:10:41.00,0:10:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Kuna nafasi ya mashaka, lakini tunaweza kuona tofauti hapa: Dialogue: 0,0:10:43.00,0:10:46.00,Default,,0000,0000,0000,,Cambodia, Singapore. Tofauti ni kubwa Dialogue: 0,0:10:46.00,0:10:49.00,Default,,0000,0000,0000,,zaidi ya udhaifu wa takwimu. Ulaya Mashariki: Dialogue: 0,0:10:49.00,0:10:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Uchumi wa Kisovieti muda mrefu, lakini waliweza kujikwamua baada ya miaka kumi Dialogue: 0,0:10:55.00,0:10:58.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa utofauti sana. Na kuna Amerika Kusini. Dialogue: 0,0:10:58.00,0:11:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Leo, hatuna haja ya kwenda Cuba kutafuta nchi yenye afya bora Amerika Kusini. Dialogue: 0,0:11:02.00,0:11:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Chile itakuwa na idadi ndogo ya vifo vya watoto zaidi ya Cuba miaka michache ijayo kuanzia sasa. Dialogue: 0,0:11:07.00,0:11:10.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hapa tuna nchi zenye kipato kikubwa katika OECD. Dialogue: 0,0:11:10.00,0:11:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hapa tunapata mwelekeo wote wa ulimwengu, Dialogue: 0,0:11:14.00,0:11:19.00,Default,,0000,0000,0000,,ambao ni karibu ni sawa na hali hii. Na tukiiangalia, Dialogue: 0,0:11:19.00,0:11:25.00,Default,,0000,0000,0000,,inavyoonekana -- dunia, mwaka 1960, inaanza kusogea. 1960. Dialogue: 0,0:11:25.00,0:11:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Huyu ni Mao Tse-tung. Alileta afya China. Halafu akafariki. Dialogue: 0,0:11:28.00,0:11:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Halafu akaja Deng Xiaoping na akaleta pesa kwa China, na kuwapandisha chati tena. Dialogue: 0,0:11:33.00,0:11:37.00,Default,,0000,0000,0000,,Na tumeona jinsi nchi zinavyosogea katika mwenendo tofauti kama hivi, Dialogue: 0,0:11:37.00,0:11:41.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa hiyo inakuwa vigumu kupata Dialogue: 0,0:11:41.00,0:11:46.00,Default,,0000,0000,0000,,mfano wa nchi ambayo inaonyesha mwelekeo wa ulimwengu. Dialogue: 0,0:11:46.00,0:11:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Ningependa kuwarudisha nyuma mpaka karibu na mwaka 1960. Dialogue: 0,0:11:52.00,0:12:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Ningependa kulinganisha Korea Kusini ambayo ni hii hapa, na Brazil, Dialogue: 0,0:12:02.00,0:12:07.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ni hii hapa. Kibandiko kimetoka hapa. Na ningependa kufananisha Uganda, Dialogue: 0,0:12:07.00,0:12:12.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo iko kule. Na ninaweza kuileta mbele, kama hivi. Dialogue: 0,0:12:12.00,0:12:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Na unaweza kuona jinsi Korea Kusini wanavyosonga mbele kwa kasi sana, Dialogue: 0,0:12:21.00,0:12:24.00,Default,,0000,0000,0000,,wakati Brazil inakwenda polepole. Dialogue: 0,0:12:24.00,0:12:30.00,Default,,0000,0000,0000,,Na kama tukirudi nyuma tena, hapa, na tukiweka alama juu yao, kama hivi, Dialogue: 0,0:12:30.00,0:12:34.00,Default,,0000,0000,0000,,unaweza kuona tena kuwa kasi ya maendeleo Dialogue: 0,0:12:34.00,0:12:40.00,Default,,0000,0000,0000,,ni tofauti sana, na nchi zinasogea sana au kidogo Dialogue: 0,0:12:40.00,0:12:44.00,Default,,0000,0000,0000,,katika kiwango sawa na kukua kwa pesa na afya, lakini inaonekana unaweza kusogea Dialogue: 0,0:12:44.00,0:12:48.00,Default,,0000,0000,0000,,haraka sana iwapo una afya kwanza kuliko ukiwa na pesa kwanza. Dialogue: 0,0:12:49.00,0:12:53.00,Default,,0000,0000,0000,,na kuonyesha hii, unaweza kuweka Umoja wa Falme za Kiarabu. Dialogue: 0,0:12:53.00,0:12:56.00,Default,,0000,0000,0000,,Walitokea hapa, nchi ya madini. Walivuna mafuta yote, Dialogue: 0,0:12:56.00,0:13:00.00,Default,,0000,0000,0000,,walipata pesa zote, lakini afya haiwezi kununuliwa dukani. Dialogue: 0,0:13:00.00,0:13:04.00,Default,,0000,0000,0000,,Inabidi uwekeze kwenye afya. Inabidi uwapeleke watoto shule. Dialogue: 0,0:13:04.00,0:13:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Inabidi kuwafunza wafanyakazi wa afya. Inabidi kuwaelimisha watu. Dialogue: 0,0:13:07.00,0:13:10.00,Default,,0000,0000,0000,,Na Sheikh Sayed alifanya hivyo kwa namna nzuri. Dialogue: 0,0:13:10.00,0:13:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Pamoja na kuanguka kwa bei ya mafuta, aliipandisha nchi yake hapa juu. Dialogue: 0,0:13:14.00,0:13:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo tumepata muelekeo wa ulimwengu, Dialogue: 0,0:13:18.00,0:13:20.00,Default,,0000,0000,0000,,ambapo nchi zote zinatabia ya kutumia pesa zao Dialogue: 0,0:13:20.00,0:13:25.00,Default,,0000,0000,0000,,vizuri zaidi ya walivyokuwa wakitumia huko nyuma. Naam, hivi ndivyo, zaidi au pungufu kidogo, Dialogue: 0,0:13:25.00,0:13:32.00,Default,,0000,0000,0000,,ukiangalia wastani wa takwimu za nchi. Ziko kama hivi. Dialogue: 0,0:13:32.00,0:13:37.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa hii ni hatari, kutumia wastani wa takwimu, kwasababu kuna Dialogue: 0,0:13:37.00,0:13:43.00,Default,,0000,0000,0000,,tofauti kubwa kati ya nchi. Kwa hiyo nikienda kuangalia hapa, tunaona Dialogue: 0,0:13:43.00,0:13:49.00,Default,,0000,0000,0000,,kuwa Uganda ya leo ni mahali ambapo Korea ya Kusnini ilikuwa mwaka 1960. Na kama nikiigawa Uganda, Dialogue: 0,0:13:49.00,0:13:54.00,Default,,0000,0000,0000,,kuna tofauti ndani ya Uganda. Hii ni moja ya tano ya takwimu ndani ya Uganda. Dialogue: 0,0:13:54.00,0:13:57.00,Default,,0000,0000,0000,,Asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Uganda wako pale. Dialogue: 0,0:13:57.00,0:14:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Masikini zaidi wako hapa chini. Iwapo nikiigawa Afrika Kusini, iko kama hivi. Dialogue: 0,0:14:01.00,0:14:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Na iwapo nikiangalia Niger, ambako kulikuwa na ukame mbaya sana, Dialogue: 0,0:14:06.00,0:14:11.00,Default,,0000,0000,0000,,mwishoni, iko kama hivi. Asilimia 20 ya masikini zaidi huko Niger wako hapa, Dialogue: 0,0:14:11.00,0:14:14.00,Default,,0000,0000,0000,,na asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Afrika Kusini wako kule, Dialogue: 0,0:14:14.00,0:14:19.00,Default,,0000,0000,0000,,na bado tunatabia ya kuzungumzia kuhusu utatuzi upi unafaa kwa matatizo ya Afrika. Dialogue: 0,0:14:19.00,0:14:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Kila kitu kilichopo hapa duniani kinapatikana Afrika. Na hamuwezi Dialogue: 0,0:14:22.00,0:14:26.00,Default,,0000,0000,0000,,kuongelea upatikanaji wa dawa za VVU [madawa] kwa moja ya tano hapa juu Dialogue: 0,0:14:26.00,0:14:30.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa mkakati sawa kama hapa chini. Maendeleo ya ulimwengu Dialogue: 0,0:14:30.00,0:14:35.00,Default,,0000,0000,0000,,ni lazima yawekwe kwa makundi tofauti, na si lazima kuwa nayo Dialogue: 0,0:14:35.00,0:14:38.00,Default,,0000,0000,0000,,katika ngazi ya kanda. Ni lazima tuingie ndani zaidi. Dialogue: 0,0:14:38.00,0:14:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Tumetambua kuwa wanafunzi wanapatwa na mshawasha wakiweza kutumia hii. Dialogue: 0,0:14:42.00,0:14:47.00,Default,,0000,0000,0000,,Na wapanga sera na sekta binafsi zingependa kuona Dialogue: 0,0:14:47.00,0:14:51.00,Default,,0000,0000,0000,,namna gani dunia inabadilika. Sasa, kwanini hii haitokei? Dialogue: 0,0:14:51.00,0:14:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwanini hatutumii takwimu tulizonazo? Tuna takwimu katika Umoja wa Mataifa, Dialogue: 0,0:14:55.00,0:14:57.00,Default,,0000,0000,0000,,na katika taasisi za takwimu za nchi Dialogue: 0,0:14:57.00,0:15:01.00,Default,,0000,0000,0000,,na katika vyuo vikuu na mashirika yasiyo ya kiserikali. Dialogue: 0,0:15:01.00,0:15:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwasababu takwimu zimefichwa kwenye masijala. Dialogue: 0,0:15:03.00,0:15:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Na umma uko pale, na mtandao wa Intaneti uko, lakini bado hatujautumia ipasavyo. Dialogue: 0,0:15:08.00,0:15:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Taarifa zote tunazoziona zikibadilika duniani Dialogue: 0,0:15:11.00,0:15:15.00,Default,,0000,0000,0000,,hazihusishi takwimu zinazogharimiwa na umma. Kuna baadhi ya kurasa za tovuti Dialogue: 0,0:15:15.00,0:15:21.00,Default,,0000,0000,0000,,mfano hii, kama ujuavyo, lakini zinachukua kutoka kwenye masijala ya takwimu, Dialogue: 0,0:15:21.00,0:15:26.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini watu wanaziwekea bei, funguo za siri na takwimu za kuchosha. Dialogue: 0,0:15:26.00,0:15:29.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko). (Makofi). Dialogue: 0,0:15:29.00,0:15:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hii haitatusaidia. Sasa nini kinatakiwa? Tuna masijala za takwimu. Dialogue: 0,0:15:33.00,0:15:37.00,Default,,0000,0000,0000,,Si masijala mpya ya takwimu unayoihitaji. Tuna vifaa vizuri vya ubunifu, Dialogue: 0,0:15:37.00,0:15:40.00,Default,,0000,0000,0000,,na vingi vinaongezewa hapa. Kwa hiyo tulianzisha Dialogue: 0,0:15:40.00,0:15:45.00,Default,,0000,0000,0000,,shirika lisilo la kibiashara ambalo tukaliita -- kuunganisha takwimu kwa ubunifu -- Dialogue: 0,0:15:45.00,0:15:48.00,Default,,0000,0000,0000,,tunaiita Gapminder, kutoka London chini ya ardhi, ambako wanakuonya, Dialogue: 0,0:15:48.00,0:15:51.00,Default,,0000,0000,0000,,"angalia upenyo" Kwa hiyo tulifikiri Gapminder ilikuwa ni sahihi. Dialogue: 0,0:15:51.00,0:15:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Na tulianza kuandika programu ya kompyuta ambayo ingeweza kuunganisha takwimu kama hivi. Dialogue: 0,0:15:55.00,0:16:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Na haikuwa vigumu sana. Iliwachukua watu wengine miaka kadhaa, na tumetengeneza vielelezo. Dialogue: 0,0:16:01.00,0:16:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Unaweza kuchukua seti ya takwimu na kuiweka hapa. Dialogue: 0,0:16:03.00,0:16:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunakomboa takwimu za Umoja wa Mataifa, mashirika machache ya Umoja wa Mataifa. Dialogue: 0,0:16:08.00,0:16:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Nchi nyingine zinakubali takwimu zao ziwe wazi duniani, Dialogue: 0,0:16:12.00,0:16:15.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini tunachohitaji zaidi ni, kwa hakika, namna ya kuzichambua. Dialogue: 0,0:16:15.00,0:16:20.00,Default,,0000,0000,0000,,Programu ya kutafuta ambayo itakuwezesha kunakili takwimu katika muundo wa kutafutika Dialogue: 0,0:16:20.00,0:16:23.00,Default,,0000,0000,0000,,na kuiweka wazi duniani. Na nini tunasikia tuzungukapo? Dialogue: 0,0:16:23.00,0:16:27.00,Default,,0000,0000,0000,,Nimefanya anthopolojia katika sehemu kubwa za takwimu. Kila mtu anasema, Dialogue: 0,0:16:28.00,0:16:32.00,Default,,0000,0000,0000,,"Haiwezekani. Hii haiwezi kufanyika. Taarifa zetu ni za ovyoovyo Dialogue: 0,0:16:32.00,0:16:35.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa ndani, na kwahiyo haziwezi kupangiliwa zitafutike kama nyingine zinavyoweza kutafutwa. Dialogue: 0,0:16:35.00,0:16:40.00,Default,,0000,0000,0000,,Hatuwezi kutoa takwimu bure kwa wanafunzi, bure kwa wajasiliamali wa dunia." Dialogue: 0,0:16:40.00,0:16:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini hivi ndivyo tungependa tuone, au sio? Dialogue: 0,0:16:43.00,0:16:46.00,Default,,0000,0000,0000,,Takwimu zilizogharimiwa na umma zipo hapa chini. Dialogue: 0,0:16:46.00,0:16:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Na tungependa maua yaote nje kwenye mtandao. Dialogue: 0,0:16:49.00,0:16:54.00,Default,,0000,0000,0000,,Na jambo la muhimu zaidi ni kuzipangilia ili ziweze kutafutika, na watu waweze kuzitumia Dialogue: 0,0:16:54.00,0:16:56.00,Default,,0000,0000,0000,,vifaa tofauti vya ubunifu kueleleza pale. Dialogue: 0,0:16:56.00,0:17:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Nina habari nzuri kwenu. Nina habari nzuri kwamba, Dialogue: 0,0:17:01.00,0:17:05.00,Default,,0000,0000,0000,,Mkuu wa Kitengo cha Takwimu cha Umoja wa Mataifa, hasemi haiwezekani. Dialogue: 0,0:17:05.00,0:17:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Anasema, "Hatuwezi kufanya." Dialogue: 0,0:17:07.00,0:17:11.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:17:11.00,0:17:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Huyu ni mtu mwenye akili, eeeh? Dialogue: 0,0:17:13.00,0:17:15.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:17:15.00,0:17:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo tunaona mambo mengi yakitokea kwenye takwimu katika miaka ijayo. Dialogue: 0,0:17:19.00,0:17:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Tutaweza kuangalia mgawanyo wa kipato katika namna mpya kabisa. Dialogue: 0,0:17:23.00,0:17:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Huu ni mgao wa kipato huko China, 1970, Dialogue: 0,0:17:29.00,0:17:34.00,Default,,0000,0000,0000,,mgao wa kipato wa Marekani, 1970. Dialogue: 0,0:17:34.00,0:17:38.00,Default,,0000,0000,0000,,Karibu hakuna mwingiliano, karibu hakuna mwingiliano. Na nini kimetokea? Dialogue: 0,0:17:38.00,0:17:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Kilichotokea ni hiki: China inakua, haiko sawa tena, Dialogue: 0,0:17:43.00,0:17:47.00,Default,,0000,0000,0000,,na inatokea hapa, ikiingalia Marekani. Dialogue: 0,0:17:47.00,0:17:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Kama vile mzuka, au sio, eeeh? Dialogue: 0,0:17:49.00,0:17:51.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:17:51.00,0:18:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Inatisha. Lakini nadhani ni muhimu sana kuwa na taarifa hizi. Dialogue: 0,0:18:01.00,0:18:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunahitaji sana kuziona. Badala ya kuangalia hii, Dialogue: 0,0:18:07.00,0:18:12.00,Default,,0000,0000,0000,,ningependa kumalizia kwa kuwaonyesha watumiaji wa mtandao kwa kila 1,000. Dialogue: 0,0:18:12.00,0:18:17.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika programu hii ya kompyuta, tunaweza kupata karibu alama 500 kutoka katika nchi zote kwa urahisi. Dialogue: 0,0:18:17.00,0:18:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Inachukua muda kubadilika kwa hii, Dialogue: 0,0:18:21.00,0:18:26.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini katika mihimili, unaweza kupata alama yeyote utakayopenda kupata. Dialogue: 0,0:18:26.00,0:18:31.00,Default,,0000,0000,0000,,Na kitu kizuri itakuwa ni kuziweka masijala za takwimu bure, Dialogue: 0,0:18:31.00,0:18:34.00,Default,,0000,0000,0000,,kuweza kuzifanya ziweze kutafutika, na kuzipata kwa kubonyeza kwa nukta moja Dialogue: 0,0:18:34.00,0:18:39.00,Default,,0000,0000,0000,,kwenye mfumo wa michoro majira ya nukta, ambapo utazielewa kwa urahisi. Dialogue: 0,0:18:39.00,0:18:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Naam, wanatakwimu hawazipendi, kwasababu wanasema kuwa hii Dialogue: 0,0:18:42.00,0:18:51.00,Default,,0000,0000,0000,,haitaonyesha hali halisi; inabidi tuwe na mbinu za kuchambua takwimu. Dialogue: 0,0:18:51.00,0:18:54.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini hii inajenga nadharia. Dialogue: 0,0:18:54.00,0:18:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninamalizia sasa na dunia. Pale, mtandao wa intaneti unakuja. Dialogue: 0,0:18:58.00,0:19:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Idadi ya wanaotumia mtandao inaongezeka kama hivi. Hii ni GDP per capita Dialogue: 0,0:19:02.00,0:19:07.00,Default,,0000,0000,0000,,Na ni teknolojia mpya inayokuja, lakini cha kushangaza, ni namna ambavyo Dialogue: 0,0:19:07.00,0:19:12.00,Default,,0000,0000,0000,,inashabihiana na hali ya uchumi wa nchi. Ndio maana Dialogue: 0,0:19:12.00,0:19:15.00,Default,,0000,0000,0000,,kompyuta ya dola 100 itakuwa ya muhimu sana. Lakini ni muelekeo mzuri. Dialogue: 0,0:19:15.00,0:19:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Ni kama vile dunia inakuwa bapa. Au sio? Nchi hizi Dialogue: 0,0:19:18.00,0:19:21.00,Default,,0000,0000,0000,,zinanyanyuka zaidi ya uchumi na itakuwa ni ya kufurahisha Dialogue: 0,0:19:21.00,0:19:25.00,Default,,0000,0000,0000,,kufuatilia hii kwa miaka ijayo, na kama ambavyo ningependa muweze kufanya Dialogue: 0,0:19:25.00,0:19:27.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa kutumia takwimu zilizogharamiwa na umma. Asanteni sana. Dialogue: 0,0:19:28.00,0:19:31.00,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi)