0:00:00.000,0:00:04.000 Takriban miaka 10 iliyopita, nilianza kazi ya kufundisha maendeleo ya ulimwengu 0:00:04.000,0:00:08.000 kwa wanafunzi wa Kiswidishi wa shahada ya kwanza. Hii ilikuwa baada ya 0:00:08.000,0:00:12.000 takriban miaka 20 ya kufanya kazi pamoja na taasisi mbalimbali za Afrika nikitafiti kuhusu njaa 0:00:12.000,0:00:16.000 katika Afrika, kwa hiyo nilikuwa natarajiwa niwe najua zaidi kuhusu dunia. 0:00:16.000,0:00:21.000 Na nilianzia kwenye chuo chetu cha utabibu, Taasisi ya Karolinska, 0:00:21.000,0:00:25.000 kozi ya shahada ya kwanza iliyoitwa Afya ya Ulimwengu. Lakini ukipata 0:00:25.000,0:00:28.000 fursa hiyo, unapata mshawasha kidogo. Nilifikiri wanafunzi hawa 0:00:28.000,0:00:31.000 kuja kwetu ni lazima wana maksi za juu unazoweza kupata 0:00:31.000,0:00:34.000 kwenye mfumo wa vyuo vya Sweden -- kwahiyo labda wanajua kila kitu 0:00:34.000,0:00:38.000 kuhusu nitakachowafundisha. Kwa hiyo niliwapa mtihani mara tu walipokuja. 0:00:38.000,0:00:41.000 Na moja wapo kati ya maswali ambayo nilijifunza mengi ni hili hapa: 0:00:41.000,0:00:45.000 "Ni nchi gani kati ya hizi tano ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto kati ya jozi hizi tano?" 0:00:45.000,0:00:49.000 Na niliziweka pamoja, ili katika kila kundi la nchi, 0:00:49.000,0:00:54.000 moja ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto zaidi ya nyingine. Na hii inamaanisha kwamba 0:00:54.000,0:00:59.000 kuna tofauti kubwa sana kuliko uhakika wa takwimu. 0:00:59.000,0:01:01.000 Sitawapa mtihani hapa, lakini ni Uturuki, 0:01:01.000,0:01:06.000 ambayo ina kiwango kikubwa pale, Poland, Urusi, Pakistani na Afrika Kusini. 0:01:06.000,0:01:09.000 Na haya ndiyo majibu ya wanafunzi wa Kiswidishi. Nilifanya hivyo na nilipata 0:01:09.000,0:01:12.000 kiwango cha imani, ambacho kilikuwa kidogo, na nilifurahi, 0:01:12.000,0:01:16.000 kwa hakika: 1.8 ya jibu sahihi kati ya matano inawezekana. Hii ina maana kwamba 0:01:16.000,0:01:19.000 kulikuwa kuna nafasi ya Profesa wa afya ya ulimwengu -- 0:01:19.000,0:01:21.000 (Kicheko) na kwa kozi yangu. 0:01:21.000,0:01:25.000 Lakini usiku mmoja, wakati nilipokuwa natayarisha ripoti 0:01:25.000,0:01:29.000 Niligundua uvumbuzi wangu. Nimeonyesha 0:01:29.000,0:01:34.000 kuwa wanafunzi Waswidishi wenye alama za juu wanajua kidogo sana kuhusu takwimu 0:01:34.000,0:01:36.000 za ulimwengu kuliko hata sokwe. 0:01:36.000,0:01:38.000 (Kicheko) 0:01:38.000,0:01:42.000 Kwasababu sokwe wangepata nusu iwapo ningewapa 0:01:42.000,0:01:45.000 ndizi mbili zenye Sri Lanka na Uturuki. Wangekuwa sahihi kwa nusu yake. 0:01:45.000,0:01:49.000 Lakini wanafunzi hawapo huko. Tatizo langu halikuwa kutokujua kwao: 0:01:49.000,0:01:52.000 ilikuwa ni mawazo waliyojijengea. 0:01:52.000,0:01:56.000 Pia nilifanya utafiti kinyume na maadili kwa maprofesa wa taasisi ya Karolinska 0:01:56.000,0:01:57.000 (Kicheko) 0:01:57.000,0:01:59.000 -- ambao wanatoa tuzo ya Nobel katika utabibu, 0:01:59.000,0:02:01.000 na wao wako sawa tu na sokwe. 0:02:01.000,0:02:04.000 (Kicheko) 0:02:04.000,0:02:08.000 Hapa ndipo nilipogundua kwamba kuna haja ya kuwasiliana, 0:02:08.000,0:02:11.000 kwasababu ya takwimu za kinachotokea duniani 0:02:11.000,0:02:14.000 na afya ya mtoto katika kila nchi inajulikana. 0:02:14.000,0:02:19.000 Tulitengeneza hii programu ya kompyuta ambayo inayoonyesha kama hivi: kila kiputo hapa ni nchi. 0:02:19.000,0:02:25.000 Hii nchi hapa ni China. Hii ni India. 0:02:25.000,0:02:31.000 Ukubwa wa kiputo ni idadi ya watu, na katika mhimili huu nimeweka kiwango cha uzazi. 0:02:31.000,0:02:34.000 Kwasababu wanafunzi wangu, walichosema 0:02:34.000,0:02:36.000 wakati walipoangalia dunia, na nilipowauliza, 0:02:36.000,0:02:38.000 "Nini mnafikiri kuhusu dunia?" 0:02:38.000,0:02:42.000 Naam, kwanza niligundua kuwa kitabu cha kiada kilikuwa Tintin, angalau. 0:02:42.000,0:02:43.000 (Kicheko) 0:02:43.000,0:02:46.000 Na walisema, "Dunia bado ni 'sisi' na 'wao.' 0:02:46.000,0:02:49.000 Na sisi ni dunia ya Magharibi na wao ni Dunia ya Tatu." 0:02:49.000,0:02:52.000 "Na una maana gani kwa kusema dunia ya magharibi?" Niliuliza. 0:02:52.000,0:02:57.000 "Naam, haya ni maisha marefu na familia ndogo, na dunia ya tatu ni maisha mafupi na familia kubwa." 0:02:57.000,0:03:03.000 Kwa hiyo hii ndio ninayoweza kuonyesha hapa. Niliweka kiwango cha uzazi hapa: idadi ya watoto kwa mwanamke, 0:03:03.000,0:03:07.000 moja, mbili, tatu, nne, mpaka watoto nane kwa mwanamke mmoja. 0:03:07.000,0:03:13.000 Tuna takwimu nzuri sana toka mwaka 1962 -- 1960 kuhusu -- ukubwa wa familia katika nchi zote. 0:03:13.000,0:03:16.000 Kiwango cha makosa ni kidogo sana. Hapa naweka umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa, 0:03:16.000,0:03:20.000 kuanzia miaka 30 katika nchi nyingine mpaka karibu miaka 70. 0:03:20.000,0:03:23.000 Na mwaka 1962 kulikuwa na kundi kubwa la nchi hapa, 0:03:23.000,0:03:28.000 ambazo zilikuwa nchi zenye viwanda, na walikuwa na familia ndogo na maisha marefu. 0:03:28.000,0:03:30.000 Na hizi zilikuwa nchi zinazoendelea: 0:03:30.000,0:03:33.000 walikuwa na familia kubwa na walikuwa na maisha mafupi. 0:03:33.000,0:03:37.000 Sasa nini kimetokea toka mwaka 1962? Tunataka kuona mabadiliko. 0:03:37.000,0:03:40.000 Je wanafunzi wako sahihi? Bado ni aina mbili za nchi? 0:03:41.000,0:03:44.000 Au hizi nchi zilizoendelea zina familia ndogo na wanaishi hapa? 0:03:44.000,0:03:46.000 Au wana maisha marefu na wanaishi hapo juu? 0:03:46.000,0:03:49.000 Hebu tuone. Tulisimamisha dunia wakati ule. Hizi zote ni takwimu za Umoja wa Mataifa 0:03:49.000,0:03:52.000 ambazo zinapatikana. Hebu tuone. Unaweza kuona kule? 0:03:52.000,0:03:55.000 Ni China kule, ikiendelea dhidi ya afya bora hapa, inaboreka kule. 0:03:55.000,0:03:58.000 Nchi zote za kijani za Amerika ya Kusini zimeanza kuelekea kuwa na familia ndogo. 0:03:58.000,0:04:01.000 Hizi za njano hapa ni nchi za Kiarabu, 0:04:01.000,0:04:05.000 na wana familia kubwa, lakini wao -- hawana maisha marefu, lakini si familia kubwa. 0:04:05.000,0:04:08.000 Waafrika ni kijani hapa chini. Bado wamebaki hapa. 0:04:08.000,0:04:11.000 Hii ni India. Indonesia inaenda kwa kasi sana. 0:04:11.000,0:04:12.000 (Kicheko) 0:04:12.000,0:04:15.000 Na miaka ya 80 hapa, kuna Bangladesh bado iko miongoni mwa nchi za Afrika kule. 0:04:15.000,0:04:18.000 Lakini sasa, Bangladesh -- ni miujiza iliyotokea miaka ya 80: 0:04:18.000,0:04:21.000 Maimamu walianza kuhamasisha uzazi wa mpango. 0:04:21.000,0:04:26.000 Walisogea juu kwenye ile kona. Na katika miaka ya 90, tulikuwa na janga la Ukimwi 0:04:26.000,0:04:29.000 ambalo lilishusha umri wa kuishi wa nchi za Afrika 0:04:29.000,0:04:33.000 na nyingine zote zilipanda kwenye ile kona, 0:04:33.000,0:04:37.000 ambako tuna maisha marefu na familia ndogo, na tuna ulimwengu mpya kabisa. 0:04:37.000,0:04:50.000 (Makofi) 0:04:50.000,0:04:55.000 Ngoja nifananishe kati ya Marekani na Vietnam. 0:04:55.000,0:05:00.000 1964: Marekani ilikuwa na familia ndogo na maisha marefu; 0:05:00.000,0:05:04.000 Vietnam ilikuwa na familia kubwa na maisha mafupi. Na hiki ndicho kilichotokea: 0:05:04.000,0:05:10.000 takwimu wakati wa vita zilionyesha kuwa pamoja na vifo vyote, 0:05:10.000,0:05:13.000 kulikuwa kuna mabadiliko katika umri wa kuishi. Mwisho wa mwaka, 0:05:13.000,0:05:16.000 uzazi wa mpango ulianza Vietnam na waliamua kuwa na familia ndogo. 0:05:16.000,0:05:19.000 Na Marekani pale juu wanakuwa na maisha marefu, 0:05:19.000,0:05:22.000 wanabaki na ukubwa wa familia. Na miaka ya 80 sasa, 0:05:22.000,0:05:25.000 waliacha mpango wa kikomunisti na wakaingia kwenye uchumi wa soko huria, 0:05:25.000,0:05:29.000 na inaenda haraka hata zaidi ya maisha ya jamii. Na leo, 0:05:29.000,0:05:34.000 Vietnam ina umri wa kuishi na ukubwa wa familia sawa 0:05:34.000,0:05:41.000 hapa Vietnam, 2003, kama ilivyokuwa Marekani, 1974, mwishoni mwa vita. 0:05:41.000,0:05:45.000 Nafikiri sote -- kama hatutaangalia vielelezo -- 0:05:45.000,0:05:49.000 tutapuuza mabadiliko makubwa huko Asia, ambayo yalikuwa 0:05:49.000,0:05:53.000 mabadiliko ya kijamii kabla hatujaona mabadiliko ya kiuchumi. 0:05:53.000,0:05:58.000 Hebu tuendelee kwingine hapa ambako tunaweza kuonyesha 0:05:58.000,0:06:05.000 mgawanyo wa kipato duniani. Hii ni mgao wa kipato cha watu. 0:06:05.000,0:06:10.000 Dola moja, dola 10 au dola 100 kwa siku. 0:06:10.000,0:06:14.000 Hakuna pengo tena kati ya matajiri na maskini. Hii ni hali ya kufikirika 0:06:14.000,0:06:18.000 Kuna kituta kidogo hapa. Lakini kuna watu kila sehemu. 0:06:19.000,0:06:23.000 Na tukiangalia kipato kinapoishia -- kipato hicho -- 0:06:23.000,0:06:29.000 hii ni asilimia 100 ya kipato cha dunia kwa mwaka. Na asilimia 20 ya matajiri wakubwa kabisa, 0:06:29.000,0:06:36.000 wanachukua karibu asilimia 74. Na asilimia 20 ya masikini zaidi, 0:06:36.000,0:06:41.000 wanachukua karibu asilimia mbili. Na hii inaonyesha kwamba dhana 0:06:41.000,0:06:45.000 ya nchi zinazoendelea ni ya mashaka. Tunafikiria kuhusu misaada, kama 0:06:45.000,0:06:50.000 watu hawa wanatoa misaada kwa watu wale pale. Lakini katikati, 0:06:50.000,0:06:54.000 tuna idadi kubwa ya watu duniani, wenye asilimia 24 ya kipato. 0:06:54.000,0:06:58.000 Tuliyasikia haya kwa namna nyingine. Na hawa ni akina nani? 0:06:58.000,0:07:02.000 Nchi mbalimbali ziko wapi? Naweza kukuonyesha Afrika. 0:07:02.000,0:07:07.000 Hii ni Afrika. Asilimia 10 ya idadi ya watu duniani, wengi wao wako kwenye umaskini. 0:07:07.000,0:07:12.000 Hii ni OECD. Nchi tajiri. Nchi za kundi la Umoja wa Mataifa. 0:07:12.000,0:07:17.000 Na wapo huku upande huu. Kuna mwingiliano kati ya Afrika na OECD 0:07:17.000,0:07:20.000 Hii hapa ni Amerika Kusini. Ni kila kitu katika dunia hii, 0:07:20.000,0:07:23.000 kuanzia maskini zaidi mpaka matajiri, huko Amerika Kusini. 0:07:23.000,0:07:28.000 Zaidi ya hayo, tunaweza kuiweka Ulaya Mashariki, Asia Mashariki, 0:07:28.000,0:07:33.000 na Asia Kusini. Na ingekuwaje iwapo tungerejea nyuma, 0:07:33.000,0:07:38.000 mpaka mwaka 1970? Wakati huo kulikuwa na nundu kubwa zaidi. 0:07:38.000,0:07:42.000 Na waliokuwa kwenye umaskini mkubwa zaidi ni Waasia. 0:07:42.000,0:07:49.000 Tatizo la dunia lilikuwa umaskini huko Asia. Na sasa kama nitaicha dunia isogee mbele, 0:07:49.000,0:07:52.000 utaona kwamba wakati idadi ya watu inaongezeka, kuna 0:07:52.000,0:07:55.000 mamia ya milioni huko Asia wanajikwamua kutoka umaskini na wengine 0:07:55.000,0:07:58.000 wanaingia katika umaskini, na hii ndiyo hali tuliyonayo leo hii. 0:07:58.000,0:08:02.000 Na makadirio mazuri kutoka Benki ya Dunia, ni kwamba haya yatatokea, 0:08:02.000,0:08:06.000 na hatutakuwa na dunia iliyogawanyika. Tutakuwa na watu wengi katikati. 0:08:06.000,0:08:08.000 Naam, hiki ni kipimo cha logarithm, 0:08:08.000,0:08:13.000 lakini dhana yetu ya uchumi ni kukua kwa asilimia. Tunaiangalia 0:08:13.000,0:08:19.000 kama ni uwezekano wa kuongezeka kwa asilimia. Kama nitabadili hii, na kuchukua 0:08:19.000,0:08:23.000 GDP kwa taifa badala ya kipato cha familia, na ninabadili hivi 0:08:23.000,0:08:29.000 takwimu moja moja kwenye takwimu za kanda za GDP, 0:08:29.000,0:08:33.000 na ninazileta kanda hapa chini, ukubwa wa kiputo bado ni idadi ya watu. 0:08:33.000,0:08:36.000 Na una OECD pale, na una Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara hapo, 0:08:36.000,0:08:39.000 na tunatoa nchi za Kiarabu pale, 0:08:39.000,0:08:43.000 zinatoka Afrika na Asia, na tunaziweka tofauti, 0:08:43.000,0:08:48.000 na tunaweza kuukuza muhimili huu, na ninaipa vipimo vipya hapa, 0:08:48.000,0:08:51.000 kwa kuongeza thamani ya ustawi wa jamii pale, uwezekano wa kusalimika mtoto. 0:08:51.000,0:08:56.000 Sasa nimeweka pesa pale kwenye mhimili, na nina uwezekano wa watoto kusalimika pale. 0:08:56.000,0:09:00.000 Katika baadhi ya nchi, asilimia 99.7 ya watoto wanaishi mpaka miaka mitano; 0:09:00.000,0:09:04.000 wengine, mika 70 tu. Na hapa inaonekana kuna pengo 0:09:04.000,0:09:08.000 kati ya OECD, Amerika Kusini, Ulaya Mashariki, Asia Mashariki, 0:09:08.000,0:09:12.000 Nchi za kiarabu, Asia Kusini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. 0:09:12.000,0:09:17.000 Uwiano baina ya maisha ya watoto na pesa ni wa karibu sana. 0:09:17.000,0:09:25.000 Lakini hebu niigawanye Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Afya iko hapa na afya bora iko kule. 0:09:25.000,0:09:30.000 Ninaweza kwenda hapa na kuigawa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara katika nchi tofauti. 0:09:30.000,0:09:35.000 Na ikipasuka, ukubwa wa puto la nchi ni sawa na idadi ya watu. 0:09:35.000,0:09:39.000 Hapa chini ni Siera Leone. Mauritus iko pale juu. Mauritius ilikuwa nchi ya kwanza 0:09:39.000,0:09:42.000 kuondokana na vikwazo vya biashara, na waliweza kuuza sukari yao. 0:09:43.000,0:09:48.000 Waliweza kuuza nguo kwa taratibu sawa na watu wa Ulaya na Amerika Kaskazini. 0:09:48.000,0:09:52.000 Kuna tofauti kubwa sana ndani ya Afrika. Na Ghana iko hapa katikati. 0:09:52.000,0:09:55.000 Huko Siera Leone, misaada ya kibinadamu. 0:09:55.000,0:10:00.000 Hapa Uganda, misaada ya maendeleo. Hapa, muda wa kuwekeza, kule, 0:10:00.000,0:10:03.000 unaweza kwenda kwa mapumziko. Ni tofauti kubwa sana 0:10:03.000,0:10:08.000 katika Afrika ambayo mara nyingi tunaitambua -- kuwa iko sawa kwa kila kitu. 0:10:08.000,0:10:12.000 Naweza kuigawa Asia Kusini hapa. India ni kiputo kikubwa cha katikati. 0:10:12.000,0:10:16.000 Lakini kuna tofauti kubwa kati ya Afghanistani na Sri Lanka. 0:10:16.000,0:10:20.000 Naweza kugawa nchi za Kiarabu. Wakoje? Hali ya hewa sawa, utamaduni sawa, 0:10:20.000,0:10:24.000 dini sawa. Tofauti kubwa. Hata kati ya majirani. 0:10:24.000,0:10:29.000 Yemen, vita vya wao kwa wao. Umoja wa Falme za Kiarabu, pesa ya kutosha ni sawa na ikatumiwa vizuri. 0:10:29.000,0:10:36.000 Sio kama tunavyofikiria. Na hii inajumuisha watoto wa raia wa kigeni ambao wapo nchini. 0:10:36.000,0:10:40.000 Takwimu ni bora zaidi ya unavyofikiria. Watu wengi wanasema takwimu ni mbaya. 0:10:41.000,0:10:43.000 Kuna nafasi ya mashaka, lakini tunaweza kuona tofauti hapa: 0:10:43.000,0:10:46.000 Cambodia, Singapore. Tofauti ni kubwa 0:10:46.000,0:10:49.000 zaidi ya udhaifu wa takwimu. Ulaya Mashariki: 0:10:49.000,0:10:55.000 Uchumi wa Kisovieti muda mrefu, lakini waliweza kujikwamua baada ya miaka kumi 0:10:55.000,0:10:58.000 kwa utofauti sana. Na kuna Amerika Kusini. 0:10:58.000,0:11:02.000 Leo, hatuna haja ya kwenda Cuba kutafuta nchi yenye afya bora Amerika Kusini. 0:11:02.000,0:11:07.000 Chile itakuwa na idadi ndogo ya vifo vya watoto zaidi ya Cuba miaka michache ijayo kuanzia sasa. 0:11:07.000,0:11:10.000 Na hapa tuna nchi zenye kipato kikubwa katika OECD. 0:11:10.000,0:11:14.000 Na hapa tunapata mwelekeo wote wa ulimwengu, 0:11:14.000,0:11:19.000 ambao ni karibu ni sawa na hali hii. Na tukiiangalia, 0:11:19.000,0:11:25.000 inavyoonekana -- dunia, mwaka 1960, inaanza kusogea. 1960. 0:11:25.000,0:11:28.000 Huyu ni Mao Tse-tung. Alileta afya China. Halafu akafariki. 0:11:28.000,0:11:33.000 Halafu akaja Deng Xiaoping na akaleta pesa kwa China, na kuwapandisha chati tena. 0:11:33.000,0:11:37.000 Na tumeona jinsi nchi zinavyosogea katika mwenendo tofauti kama hivi, 0:11:37.000,0:11:41.000 kwa hiyo inakuwa vigumu kupata 0:11:41.000,0:11:46.000 mfano wa nchi ambayo inaonyesha mwelekeo wa ulimwengu. 0:11:46.000,0:11:52.000 Ningependa kuwarudisha nyuma mpaka karibu na mwaka 1960. 0:11:52.000,0:12:02.000 Ningependa kulinganisha Korea Kusini ambayo ni hii hapa, na Brazil, 0:12:02.000,0:12:07.000 ambayo ni hii hapa. Kibandiko kimetoka hapa. Na ningependa kufananisha Uganda, 0:12:07.000,0:12:12.000 ambayo iko kule. Na ninaweza kuileta mbele, kama hivi. 0:12:12.000,0:12:21.000 Na unaweza kuona jinsi Korea Kusini wanavyosonga mbele kwa kasi sana, 0:12:21.000,0:12:24.000 wakati Brazil inakwenda polepole. 0:12:24.000,0:12:30.000 Na kama tukirudi nyuma tena, hapa, na tukiweka alama juu yao, kama hivi, 0:12:30.000,0:12:34.000 unaweza kuona tena kuwa kasi ya maendeleo 0:12:34.000,0:12:40.000 ni tofauti sana, na nchi zinasogea sana au kidogo 0:12:40.000,0:12:44.000 katika kiwango sawa na kukua kwa pesa na afya, lakini inaonekana unaweza kusogea 0:12:44.000,0:12:48.000 haraka sana iwapo una afya kwanza kuliko ukiwa na pesa kwanza. 0:12:49.000,0:12:53.000 na kuonyesha hii, unaweza kuweka Umoja wa Falme za Kiarabu. 0:12:53.000,0:12:56.000 Walitokea hapa, nchi ya madini. Walivuna mafuta yote, 0:12:56.000,0:13:00.000 walipata pesa zote, lakini afya haiwezi kununuliwa dukani. 0:13:00.000,0:13:04.000 Inabidi uwekeze kwenye afya. Inabidi uwapeleke watoto shule. 0:13:04.000,0:13:07.000 Inabidi kuwafunza wafanyakazi wa afya. Inabidi kuwaelimisha watu. 0:13:07.000,0:13:10.000 Na Sheikh Sayed alifanya hivyo kwa namna nzuri. 0:13:10.000,0:13:14.000 Pamoja na kuanguka kwa bei ya mafuta, aliipandisha nchi yake hapa juu. 0:13:14.000,0:13:18.000 Kwa hiyo tumepata muelekeo wa ulimwengu, 0:13:18.000,0:13:20.000 ambapo nchi zote zinatabia ya kutumia pesa zao 0:13:20.000,0:13:25.000 vizuri zaidi ya walivyokuwa wakitumia huko nyuma. Naam, hivi ndivyo, zaidi au pungufu kidogo, 0:13:25.000,0:13:32.000 ukiangalia wastani wa takwimu za nchi. Ziko kama hivi. 0:13:32.000,0:13:37.000 Sasa hii ni hatari, kutumia wastani wa takwimu, kwasababu kuna 0:13:37.000,0:13:43.000 tofauti kubwa kati ya nchi. Kwa hiyo nikienda kuangalia hapa, tunaona 0:13:43.000,0:13:49.000 kuwa Uganda ya leo ni mahali ambapo Korea ya Kusnini ilikuwa mwaka 1960. Na kama nikiigawa Uganda, 0:13:49.000,0:13:54.000 kuna tofauti ndani ya Uganda. Hii ni moja ya tano ya takwimu ndani ya Uganda. 0:13:54.000,0:13:57.000 Asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Uganda wako pale. 0:13:57.000,0:14:01.000 Masikini zaidi wako hapa chini. Iwapo nikiigawa Afrika Kusini, iko kama hivi. 0:14:01.000,0:14:06.000 Na iwapo nikiangalia Niger, ambako kulikuwa na ukame mbaya sana, 0:14:06.000,0:14:11.000 mwishoni, iko kama hivi. Asilimia 20 ya masikini zaidi huko Niger wako hapa, 0:14:11.000,0:14:14.000 na asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Afrika Kusini wako kule, 0:14:14.000,0:14:19.000 na bado tunatabia ya kuzungumzia kuhusu utatuzi upi unafaa kwa matatizo ya Afrika. 0:14:19.000,0:14:22.000 Kila kitu kilichopo hapa duniani kinapatikana Afrika. Na hamuwezi 0:14:22.000,0:14:26.000 kuongelea upatikanaji wa dawa za VVU [madawa] kwa moja ya tano hapa juu 0:14:26.000,0:14:30.000 kwa mkakati sawa kama hapa chini. Maendeleo ya ulimwengu 0:14:30.000,0:14:35.000 ni lazima yawekwe kwa makundi tofauti, na si lazima kuwa nayo 0:14:35.000,0:14:38.000 katika ngazi ya kanda. Ni lazima tuingie ndani zaidi. 0:14:38.000,0:14:42.000 Tumetambua kuwa wanafunzi wanapatwa na mshawasha wakiweza kutumia hii. 0:14:42.000,0:14:47.000 Na wapanga sera na sekta binafsi zingependa kuona 0:14:47.000,0:14:51.000 namna gani dunia inabadilika. Sasa, kwanini hii haitokei? 0:14:51.000,0:14:55.000 Kwanini hatutumii takwimu tulizonazo? Tuna takwimu katika Umoja wa Mataifa, 0:14:55.000,0:14:57.000 na katika taasisi za takwimu za nchi 0:14:57.000,0:15:01.000 na katika vyuo vikuu na mashirika yasiyo ya kiserikali. 0:15:01.000,0:15:03.000 Kwasababu takwimu zimefichwa kwenye masijala. 0:15:03.000,0:15:08.000 Na umma uko pale, na mtandao wa Intaneti uko, lakini bado hatujautumia ipasavyo. 0:15:08.000,0:15:11.000 Taarifa zote tunazoziona zikibadilika duniani 0:15:11.000,0:15:15.000 hazihusishi takwimu zinazogharimiwa na umma. Kuna baadhi ya kurasa za tovuti 0:15:15.000,0:15:21.000 mfano hii, kama ujuavyo, lakini zinachukua kutoka kwenye masijala ya takwimu, 0:15:21.000,0:15:26.000 lakini watu wanaziwekea bei, funguo za siri na takwimu za kuchosha. 0:15:26.000,0:15:29.000 (Kicheko). (Makofi). 0:15:29.000,0:15:33.000 Na hii haitatusaidia. Sasa nini kinatakiwa? Tuna masijala za takwimu. 0:15:33.000,0:15:37.000 Si masijala mpya ya takwimu unayoihitaji. Tuna vifaa vizuri vya ubunifu, 0:15:37.000,0:15:40.000 na vingi vinaongezewa hapa. Kwa hiyo tulianzisha 0:15:40.000,0:15:45.000 shirika lisilo la kibiashara ambalo tukaliita -- kuunganisha takwimu kwa ubunifu -- 0:15:45.000,0:15:48.000 tunaiita Gapminder, kutoka London chini ya ardhi, ambako wanakuonya, 0:15:48.000,0:15:51.000 "angalia upenyo" Kwa hiyo tulifikiri Gapminder ilikuwa ni sahihi. 0:15:51.000,0:15:55.000 Na tulianza kuandika programu ya kompyuta ambayo ingeweza kuunganisha takwimu kama hivi. 0:15:55.000,0:16:01.000 Na haikuwa vigumu sana. Iliwachukua watu wengine miaka kadhaa, na tumetengeneza vielelezo. 0:16:01.000,0:16:03.000 Unaweza kuchukua seti ya takwimu na kuiweka hapa. 0:16:03.000,0:16:08.000 Tunakomboa takwimu za Umoja wa Mataifa, mashirika machache ya Umoja wa Mataifa. 0:16:08.000,0:16:12.000 Nchi nyingine zinakubali takwimu zao ziwe wazi duniani, 0:16:12.000,0:16:15.000 lakini tunachohitaji zaidi ni, kwa hakika, namna ya kuzichambua. 0:16:15.000,0:16:20.000 Programu ya kutafuta ambayo itakuwezesha kunakili takwimu katika muundo wa kutafutika 0:16:20.000,0:16:23.000 na kuiweka wazi duniani. Na nini tunasikia tuzungukapo? 0:16:23.000,0:16:27.000 Nimefanya anthopolojia katika sehemu kubwa za takwimu. Kila mtu anasema, 0:16:28.000,0:16:32.000 "Haiwezekani. Hii haiwezi kufanyika. Taarifa zetu ni za ovyoovyo 0:16:32.000,0:16:35.000 kwa ndani, na kwahiyo haziwezi kupangiliwa zitafutike kama nyingine zinavyoweza kutafutwa. 0:16:35.000,0:16:40.000 Hatuwezi kutoa takwimu bure kwa wanafunzi, bure kwa wajasiliamali wa dunia." 0:16:40.000,0:16:43.000 Lakini hivi ndivyo tungependa tuone, au sio? 0:16:43.000,0:16:46.000 Takwimu zilizogharimiwa na umma zipo hapa chini. 0:16:46.000,0:16:49.000 Na tungependa maua yaote nje kwenye mtandao. 0:16:49.000,0:16:54.000 Na jambo la muhimu zaidi ni kuzipangilia ili ziweze kutafutika, na watu waweze kuzitumia 0:16:54.000,0:16:56.000 vifaa tofauti vya ubunifu kueleleza pale. 0:16:56.000,0:17:01.000 Nina habari nzuri kwenu. Nina habari nzuri kwamba, 0:17:01.000,0:17:05.000 Mkuu wa Kitengo cha Takwimu cha Umoja wa Mataifa, hasemi haiwezekani. 0:17:05.000,0:17:07.000 Anasema, "Hatuwezi kufanya." 0:17:07.000,0:17:11.000 (Kicheko) 0:17:11.000,0:17:13.000 Huyu ni mtu mwenye akili, eeeh? 0:17:13.000,0:17:15.000 (Kicheko) 0:17:15.000,0:17:19.000 Kwa hiyo tunaona mambo mengi yakitokea kwenye takwimu katika miaka ijayo. 0:17:19.000,0:17:23.000 Tutaweza kuangalia mgawanyo wa kipato katika namna mpya kabisa. 0:17:23.000,0:17:28.000 Huu ni mgao wa kipato huko China, 1970, 0:17:29.000,0:17:34.000 mgao wa kipato wa Marekani, 1970. 0:17:34.000,0:17:38.000 Karibu hakuna mwingiliano, karibu hakuna mwingiliano. Na nini kimetokea? 0:17:38.000,0:17:43.000 Kilichotokea ni hiki: China inakua, haiko sawa tena, 0:17:43.000,0:17:47.000 na inatokea hapa, ikiingalia Marekani. 0:17:47.000,0:17:49.000 Kama vile mzuka, au sio, eeeh? 0:17:49.000,0:17:51.000 (Kicheko) 0:17:51.000,0:18:01.000 Inatisha. Lakini nadhani ni muhimu sana kuwa na taarifa hizi. 0:18:01.000,0:18:07.000 Tunahitaji sana kuziona. Badala ya kuangalia hii, 0:18:07.000,0:18:12.000 ningependa kumalizia kwa kuwaonyesha watumiaji wa mtandao kwa kila 1,000. 0:18:12.000,0:18:17.000 Katika programu hii ya kompyuta, tunaweza kupata karibu alama 500 kutoka katika nchi zote kwa urahisi. 0:18:17.000,0:18:21.000 Inachukua muda kubadilika kwa hii, 0:18:21.000,0:18:26.000 lakini katika mihimili, unaweza kupata alama yeyote utakayopenda kupata. 0:18:26.000,0:18:31.000 Na kitu kizuri itakuwa ni kuziweka masijala za takwimu bure, 0:18:31.000,0:18:34.000 kuweza kuzifanya ziweze kutafutika, na kuzipata kwa kubonyeza kwa nukta moja 0:18:34.000,0:18:39.000 kwenye mfumo wa michoro majira ya nukta, ambapo utazielewa kwa urahisi. 0:18:39.000,0:18:42.000 Naam, wanatakwimu hawazipendi, kwasababu wanasema kuwa hii 0:18:42.000,0:18:51.000 haitaonyesha hali halisi; inabidi tuwe na mbinu za kuchambua takwimu. 0:18:51.000,0:18:54.000 Lakini hii inajenga nadharia. 0:18:54.000,0:18:58.000 Ninamalizia sasa na dunia. Pale, mtandao wa intaneti unakuja. 0:18:58.000,0:19:02.000 Idadi ya wanaotumia mtandao inaongezeka kama hivi. Hii ni GDP per capita 0:19:02.000,0:19:07.000 Na ni teknolojia mpya inayokuja, lakini cha kushangaza, ni namna ambavyo 0:19:07.000,0:19:12.000 inashabihiana na hali ya uchumi wa nchi. Ndio maana 0:19:12.000,0:19:15.000 kompyuta ya dola 100 itakuwa ya muhimu sana. Lakini ni muelekeo mzuri. 0:19:15.000,0:19:18.000 Ni kama vile dunia inakuwa bapa. Au sio? Nchi hizi 0:19:18.000,0:19:21.000 zinanyanyuka zaidi ya uchumi na itakuwa ni ya kufurahisha 0:19:21.000,0:19:25.000 kufuatilia hii kwa miaka ijayo, na kama ambavyo ningependa muweze kufanya 0:19:25.000,0:19:27.000 kwa kutumia takwimu zilizogharamiwa na umma. Asanteni sana. 0:19:28.000,0:19:31.000 (Makofi)