Return to Video

RnD-Africa: Super Electric Bikes made in Ghana

  • 0:00 - 0:02
    Je, mnaona mahali ambapo nimeketi?
  • 0:02 - 0:07
    Tunakuletea hili kwenye kipindi hiki cha
    R&D Africa kwenye AAU TV.
  • 0:07 - 0:12
    Tunamwangazia kwa kijana Lawrence Adjei,
    ambaye ameweza kutengeneza
  • 0:12 - 0:16
    pikipiki hii ya umeme kwa kutumia
    betri za vipakatalishi vilivyoharibika.
  • 0:16 - 0:18
    Tegea.
    Tutakuonyesha zaidi.
  • 0:26 - 0:31
    Katika enzi ambapo ulinzi wa mazingira,
    siha na usafiri unaotunza mazingira
  • 0:31 - 0:34
    unathaminiwa na kufanywa kwa sana na watu,
  • 0:34 - 0:37
    kinachokujia akilini wakati
    usafiri unaokuruhusu,
  • 0:37 - 0:39
    kuepuka msongamano wa trafiki,
  • 0:40 - 0:42
    usiochafua hewa na unaotunza mazingira unatajwa.
  • 0:46 - 0:50
    Baiskeli zinazotumia umeme
    zina vifaa vya kielektroniki
  • 0:50 - 0:53
    vilivyowekwa kusaidia au kuchukua
    nafasi ya kuendesha mwenyewe.
  • 0:53 - 0:55
    Zina manufaa kadhaa.
  • 0:55 - 1:00
    Hazitumii mafuta mengi, zina mwendo
    wa kasi, hupunguza msongamano wa trafiki
  • 1:00 - 1:02
    na hazichafui mazingira.
  • 1:04 - 1:07
    Kwa sana wavumbuzi wanategemea
    betri kama vile lithium-ion,
  • 1:08 - 1:09
    nickel-cadmium,
  • 1:09 - 1:11
    betri za lithium-cobalt
  • 1:11 - 1:12
    lead acid,
  • 1:12 - 1:14
    nickel-metal hydrate,
  • 1:14 - 1:15
    lithium-manganese
  • 1:15 - 1:18
    na betri za lithium-ion polymer
    kama vifuasi.
  • 1:19 - 1:22
    Cha kushangaza, kijana mchanga wa Ghana,
    Lawrence Adjei
  • 1:22 - 1:26
    amechagia kwenye uvumbuzi katika
    sekta ya baiskeli za umeme.
  • 1:26 - 1:29
    Anatumia betri za vipakatalishi, ambazo ananunua
  • 1:29 - 1:34
    kutoka kwa maduka ya takataka kompyuta
    huko Accra ili kutengeneza baiskeli zake.
  • 1:35 - 1:38
    Anajulikana kuwa raia wa kwanza wa
    Ghana kutengeneza baiskeli za umeme
  • 1:38 - 1:42
    kutoka kwa betri za vipakatalishi
    na amejifunza.
  • 1:45 - 1:50
    Naishi karibu na Lawrence na
    mimi ni msaidizi wake.
  • 1:50 - 1:52
    Hii si mara yangu ya kwanza kuendesha.
  • 1:52 - 1:54
    Nimekuwa nikiendesha pikipiki
    kwa miaka miwili sasa.
  • 1:54 - 1:56
    Hali ya uendeshaji ni tofauti.
  • 1:57 - 2:00
    Tofauti. Siwezi hata kulinganisha kwa
    sababu kuendesha baiskeli ya kawaida...
  • 2:00 - 2:01
    kuna uchungu mwingi.
  • 2:01 - 2:06
    Na kisha unaweza kupenda idadi
    ya kilomita unazohitaji kwenda.
  • 2:06 - 2:10
    Kwa hivyo hii ni tofauti kabisa
    ikilinganishwa na nilizowahi kutumia.
  • 2:10 - 2:14
    Hii ina gia tatu
    na hizo nyingine hazina.
  • 2:14 - 2:21
    Ina breki ambayo inachaji betri wakati
    unaitumia, baiskeli nyingine hazina.
  • 2:21 - 2:25
    Ina lango la USB ambalo linaweza
    kuchaji simu yako
  • 2:25 - 2:26
    au kutumia mwangaza wa USB.
  • 2:27 - 2:28
    Vitu ambavyo havipo kwa nyingine.
  • 2:29 - 2:32
    Na pia ina kengele, nyingine
    hazikuwa na kengele.
  • 2:33 - 2:37
    Na kisha unaweza kusimama
    mara moja ukitumia breko.
  • 2:37 - 2:38
    Zinasimama mara moja.
  • 2:38 - 2:41
    Inayofuata. Tukiangazia betri,
  • 2:41 - 2:43
    ina kiwango cha juu unachoweza kutumia,
  • 2:43 - 2:46
    kuweka mwanga kwa nyumba.
  • 2:49 - 2:53
    Hapa ndipo Bw Lawrence AJ
    hufanya uvumbuzi wote.
  • 2:53 - 2:56
    Hapa ndipo utengenezaji
    wa baiskeli za umeme
  • 2:56 - 2:59
    kutokana na betri za vipakatalishi
    vilivyoharibika hufanyika na
  • 2:59 - 3:01
    Kwa sasa nipo hapa na Bw Lawrence.
  • 3:02 - 3:04
    Tuonyeshe
    mchakato unaohusika katika
  • 3:04 - 3:07
    matumizi ya betri hizi ili
    kutengeneza baiskeli ya umeme.
  • 3:07 - 3:10
    Kwa hivyo kuna betri hapa.
  • 3:10 - 3:12
    Kwa hivyo, unazipasua hivi.
  • 3:13 - 3:15
    Wakati mwingine unakunja au...
  • 3:16 - 3:17
    unatumia koleo.
  • 3:17 - 3:18
    Sawa
  • 3:22 - 3:24
    Unaona kuwa hatutumii seli zote.
  • 3:25 - 3:26
    Hii iko hapa, imechomoza.
  • 3:27 - 3:29
    -Sawa
    -Huwezi kutumia hii, kwa hivyo
  • 3:29 - 3:30
    Unatafuta tofauti.
  • 3:31 - 3:32
    Jaribu nyingine.
  • 3:39 - 3:40
    Inayofanana.
  • 3:40 - 3:43
    Hii iko sawa. Kwa hivyo unachukua
    mathabodi
  • 3:43 - 3:44
    - ya betri. Kwa hivyo...
    - Sawa
  • 3:44 - 3:45
    Kwa hivyo kuziondoa
  • 3:46 - 3:49
    [Haisikiki]
  • 3:55 - 3:57
    Kisha ondoa seli zake hivi.
  • 3:57 - 3:59
    Sawa
  • 4:00 - 4:03
    Kwa hivyo kwa jumla,
    unahitaji seli hizi ngapi?
  • 4:03 - 4:04
    Nahitaji nyingi, lakini
  • 4:04 - 4:06
    Nina betri 6 pekee hapa.
  • 4:06 - 4:07
    Sawa
  • 4:07 - 4:12
    Kisha unapima kwa kutumia votimita ili
    uone iwapo kuna kiwango cha volti ndani.
  • 4:12 - 4:15
    Unahitaji wastani wa
    volti ngapi katika betri?
  • 4:15 - 4:18
    Nafikiri kama volti 2.5.
    Volti 2.5 ni sawa.
  • 4:18 - 4:19
    - Sawa
    - Hii ni nzuri
  • 4:19 - 4:21
    - Sawa
    - Kisha tunakuja hapa
  • 4:21 - 4:23
    na kupima kupitia mashine hii hapa.
  • 4:23 - 4:25
    Hii inaitwa Opus.
  • 4:25 - 4:27
    Hii hufanya vipimo vya kiwango.
  • 4:27 - 4:30
    - Sawa
    - Kwa hivyo unaweka seli ndani hivi.
  • 4:30 - 4:32
    Unaweza kuona kuwa inachaji, kwa hivyo...
  • 4:32 - 4:35
    Itachaji betri kwa
    takribani saa mbili
  • 4:35 - 4:36
    - Sawa
    - Saa mbili pekee
  • 4:36 - 4:43
    Baada ya hilo, mashine itaondoa umeme
    kwenye betri na kukuonyesha kiwango,
  • 4:43 - 4:45
    -Sawa
    -Kisha tunaiondoa.
  • 4:45 - 4:48
    Kisha tunaandika kiwango juu yake.
  • 4:52 - 4:54
    Kulinganisha vitu vingine pia
  • 4:54 - 4:58
    Ina kifaa cha Bluetooth ndani yake,
    unachoweza kutumia kusanidi simu yako.
  • 4:58 - 5:02
    Kwa hivyo fikiri naenda kwa kasi ya juu,
    haupunguzi kasi
  • 5:02 - 5:05
    kwenye simu yako na
    kisha itapungua kiotomatiki.
  • 5:05 - 5:07
    Haijalishi mchapuko.
  • 5:07 - 5:10
    Kwa baiskeli nyingine,
    hazina gia ya nyuma.
  • 5:10 - 5:12
    Unahitaji tu kuzikuma nyuma hivi.
  • 5:12 - 5:14
    Lakini hii ina gia ya nyuma.
  • 5:14 - 5:15
    Kwa hivyo hamna haja.
  • 5:15 - 5:19
    Wakati umewasha ufunguo, bonyeza tu
    kitufe na kisha unaanza kwenda.
  • 5:19 - 5:22
    Haichapuki kama unapokua
    kwenye kasi ya juu
  • 5:22 - 5:27
    lakini ina nguvu na
    inapunguza kasi taratibu.
  • 5:27 - 5:31
    Bila kujali kizuizi,
    itapunguza kasi taratibu.
  • 5:31 - 5:34
    Nafikiri haya ni yote kuihusu.
  • 5:34 - 5:37
    Kwa baiskeli nyingine,
    hatuna shokomzoba za mbele.
  • 5:37 - 5:42
    Na kisha, shokomzoba za mbele,
    tukizungumzia hili, limejazwa hewa.
  • 5:42 - 5:44
    Ni tofauti na hilo lingine.
  • 5:44 - 5:47
    Hiyo nyingine ina hewa kidogo
    na mafuta mengi.
  • 5:47 - 5:51
    Lakini hii ina hewa, kwa hivyo
    unasimama mara moja.
  • 5:51 - 5:53
    Na unaona kuna ya nyuma pia.
  • 5:53 - 5:55
    Pia ni tofauti upande wa nyuma.
  • 5:55 - 5:57
    Kwa kweli, baiskeli nyingine, unapoendesha
  • 5:57 - 6:01
    na upitie kwenye shimo,
    unahisi uchungu kwenye kiuno.
  • 6:01 - 6:02
    Lakini kwa hii, huhisi uchungu.
  • 6:02 - 6:05
    Unapitia tu shimoni na unakuwa sawa.
  • 6:05 - 6:08
    Kwa hivyo wakati wowote unapoendesha
    baiskeli hii, inakufanya
  • 6:08 - 6:11
    utamani kwenda zaidi na zaidi.
  • 6:11 - 6:15
    Ni vyema zaidi kuwa na
    mojawapo ya baiskeli hizi.
  • 6:19 - 6:21
    Jina langu ni AJ Lawarence.
  • 6:21 - 6:23
    Naishi Kaswa katika eneo la kati la Ghana.
  • 6:23 - 6:26
    Akiwa na miaka 11, wakati
    Lawrence aligundua talanta yake,
  • 6:26 - 6:31
    alijifunza kucheza na vifaa vya
    kielektroniki kama vile kompyuta.
  • 6:31 - 6:34
    Mwaka mmoja baada ya mvuto
    wake kukua katika nyanya hiyo,
  • 6:34 - 6:37
    alichukua kasi ya
    kurekebisha baiskeli.
  • 6:37 - 6:40
    Hadi leo, bado
    anarekebisha baiskeli kadhaa.
  • 6:40 - 6:44
    Kufikia sasa, Lawrence ametengeneza na
    kuuza baiskeli nne za umeme mwenyewe.
  • 6:44 - 6:50
    Baiskeli ya sasa ina vitu vilivyoboreshwa
    ikilinganishwa na alizotengeneza zamani.
  • 6:50 - 6:52
    Profesa Jaya anatazamia
    kuwasiliana na
  • 6:52 - 6:54
    vyuo kwa ajili
    ya ushirikiano
  • 6:54 - 6:59
    ili kuboresha mawazo
    yake ya ubunifu.
  • 6:59 - 7:04
    Ana ndoto ya kutumia sola kuendesha
    baiskeli zake baadaye, lakini anahitaji
  • 7:04 - 7:07
    ushirikiano na vyumo na taasisi za
  • 7:07 - 7:10
    kiufundi ili kuboresha
    utengenzaji kutoka sampuli
  • 7:10 - 7:12
    hadi kuwa biashara.
  • 7:12 - 7:15
    Katika ushirikiano huo,
    anatafuta kuwafunza
  • 7:15 - 7:18
    wanafunzi wa kiufundi kuboresha
    ufahamu wao kuhusu elektroniki.
  • 7:21 - 7:23
    Nina swali.
  • 7:23 - 7:26
    Kwa hivyo jaribio hili hufanikiwa
    tu wakati unatumia betri
  • 7:26 - 7:30
    za kuunganishwa au za vipakatilishi vibovu
    au unaweza kutumia betri mpya.
  • 7:30 - 7:31
    Kwa hakika unaweza kutumia mpya.
  • 7:31 - 7:32
    Sawa
  • 7:32 - 7:33
    Sawa.
  • 7:33 - 7:36
    Sasa kuhusu kuchaji
    baiskeli, inafanywa vipi?
  • 7:36 - 7:39
    Inachajiwa kwa kutumia chaja hii hapa.
  • 7:39 - 7:41
    Hii ni chaja maalum niliyobuni.
  • 7:41 - 7:43
    Si kama chaja ya kawaida.
  • 7:43 - 7:45
    Huenda ikachukua
    saa 12, saa 6 ili kuchaji.
  • 7:45 - 7:46
    Sawa
  • 7:46 - 7:48
    Hii huchaji kwa takribani saa 3.
  • 7:48 - 7:49
    Sawa.
  • 7:51 - 7:52
    Na, uliitengeneza mwenyewe?
  • 7:52 - 7:53
    Ndiyo.
  • 7:53 - 7:55
    Nilinunua sehemu.
  • 7:55 - 7:56
    Sawa.
  • 7:56 - 8:00
    Kwa sehemu ulizotumia,
    unaweza kuangazia kwa kifupi
  • 8:00 - 8:02
    mchakato, ulivyofikia hitimisho hilo?
  • 8:02 - 8:05
    Kwa hii, ni chanzo cha nishati cha seva.
  • 8:05 - 8:06
    Sawa.
  • 8:06 - 8:08
    Inatumika katika huduma ya mwanga.
  • 8:08 - 8:11
    Unajua, huduma ya mwanga,
    zina kompyuta nyingi ndani.
  • 8:11 - 8:13
    Kwa hivyo zina prosesa nzuri sana.
  • 8:14 - 8:18
    Na hii hapa inaitwa
    konvata ya kuongeza nishati
  • 8:18 - 8:20
    Sawa
  • 8:20 - 8:22
    Kwa hivyo ukiweka volti 3
  • 8:22 - 8:25
    Inaibadilisha kuwa volti 84
  • 8:25 - 8:27
    Sawa
  • 8:27 - 8:30
    Sasa kuhusu vipengele vya baiskeli yako
  • 8:30 - 8:36
    Baiskeli yako ina vipengele vipi ambavyo
    havipo kwenye baiskeli zilizo sokoni>
  • 8:36 - 8:38
    Kila kitu kimesanidiwa kwenye hii.
  • 8:38 - 8:42
    Unaweza kuchagua programu
    inayofanya kazi kwenye simu yako.
  • 8:42 - 8:44
    Sawa, sawa.
  • 8:45 - 8:48
    Pia ina sehemu ya kuchaji simu zako.
  • 8:49 - 8:52
    Pia ina breki za Evergine.
  • 8:52 - 8:56
    Hiyo inamaanisha unapofunga
    breki, inachaji baiskeli
  • 8:56 - 9:02
    Hivyo, hujaribu kutumia
    Venoma Veperseto unapofunga breki
  • 9:02 - 9:05
    Inafanya mara moja unapofunga breki
  • 9:07 - 9:10
    Unashughulikia vipi usaidizi wa mrai huu?
  • 9:10 - 9:12
    Umekuwa ukiifanya vipi?
  • 9:12 - 9:13
    Kujiamini.
  • 9:17 - 9:20
    Sawa, kwa hivyo changamoto
    nilipokuwa nikitengeneza baiskeli
  • 9:20 - 9:23
    zilikuwa, mwanzo sikuwa na mashine ya
    kushikanisha vyuma na mashine ya rangi.
  • 9:23 - 9:26
    Kwa hivyo napeleka kwa waunganisha
    vyuma na wapaka rangi.
  • 9:26 - 9:28
    Lakini wanachukua
    pesa na hawafanyi kazi nzuri.
  • 9:28 - 9:32
    Niliamua kunua
    mashine hizo.
  • 9:32 - 9:35
    Kisha nikaanza kujifuza kuchomelea
    na kupaka rangi mwenyewe.
  • 9:35 - 9:39
    Ilinichukua takribani wiki
    moja au mbili kujifunza zote.
  • 9:39 - 9:42
    Wakati mwingine marafiki
    zangu hunishusha moyo
  • 9:42 - 9:44
    kuwa haitafanikiwa na
    kila mara unapoteza wakati
  • 9:44 - 9:47
    kwa jambo hili,
    nenda ukatafute kazi na upate pesa.
  • 9:47 - 9:50
    Changamoto zangu kuhusu fedha
    ni kama wakati mwingine
  • 9:50 - 9:53
    Sipati pesa kwa wingi za kununua sehemu.
  • 9:53 - 9:55
    Kwa hivyo nitanunua moja mwezi huu,
  • 9:55 - 9:57
    mwezi unaofuata ninunue nyingine na zote
  • 9:57 - 10:00
    husafirishwa, ambayo ni gharama kubwa.
  • 10:00 - 10:05
    Kwa hivyo nikipata fedha ya kuzinunua
    kwa wingi, nafikiri itasaidia mchakato.
  • 10:09 - 10:12
    Lawrence anatazamia kujenga eneo la kazi
  • 10:12 - 10:15
    ili kubuni ajira kwa
  • 10:15 - 10:19
    wavumbuzi wanaovutiwa na kusaidia jamii.
  • 10:19 - 10:22
    Lawrence Adjei haweki tu Bara la
  • 10:22 - 10:25
    Afrika kwenye ramani, pia ameonekana kuwa
  • 10:25 - 10:28
    mmoja wa watu wengi afrika wenye
    akili za uvumbuzi
  • 10:28 - 10:32
    ambao wanaweza kunawiri wakisaidiwa kiasi.
  • 10:32 - 10:36
    Huu ndio mwisho wa kipindi
    cha kufana, kinachofichua
  • 10:36 - 10:39
    na cha mafunzo cha R&D Africa
    kwenye AAU TV.
  • 10:39 - 10:42
    Usisahau kuwa huenda wakati
    mwingine ni wewe utakayeangaziwa.
  • 10:42 - 10:45
    Kwa hivyo iwapo una uvumbuzi wowote,
  • 10:45 - 10:49
    wasiliana na AAU TV na tutakufikia.
  • 10:49 - 10:52
    Tufuatilie kwenye
    YouTube, Facebook na kwenye
  • 10:52 - 10:55
    mifumo yetu yote ya mtandao
    jamii ili upate maudhui zaidi.
  • 10:55 - 10:57
    Jina langu - Maame Ekua Otuakoa Nyame.
  • 10:57 - 10:59
    Hadi wakati mwingine, tumemaliza!
  • 10:59 - 11:14
    [Muziki].
Title:
RnD-Africa: Super Electric Bikes made in Ghana
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
Amplifying Voices
Project:
AAU
Duration:
11:14

Swahili subtitles

Incomplete

Revisions Compare revisions