Je, mnaona mahali ambapo nimeketi? Tunakuletea hili kwenye kipindi hiki cha R&D Africa kwenye AAU TV. Tunamwangazia kwa kijana Lawrence Adjei, ambaye ameweza kutengeneza pikipiki hii ya umeme kwa kutumia betri za vipakatalishi vilivyoharibika. Tegea. Tutakuonyesha zaidi. Katika enzi ambapo ulinzi wa mazingira, siha na usafiri unaotunza mazingira unathaminiwa na kufanywa kwa sana na watu, kinachokujia akilini wakati usafiri unaokuruhusu, kuepuka msongamano wa trafiki, usiochafua hewa na unaotunza mazingira unatajwa. Baiskeli zinazotumia umeme zina vifaa vya kielektroniki vilivyowekwa kusaidia au kuchukua nafasi ya kuendesha mwenyewe. Zina manufaa kadhaa. Hazitumii mafuta mengi, zina mwendo wa kasi, hupunguza msongamano wa trafiki na hazichafui mazingira. Kwa sana wavumbuzi wanategemea betri kama vile lithium-ion, nickel-cadmium, betri za lithium-cobalt lead acid, nickel-metal hydrate, lithium-manganese na betri za lithium-ion polymer kama vifuasi. Cha kushangaza, kijana mchanga wa Ghana, Lawrence Adjei amechagia kwenye uvumbuzi katika sekta ya baiskeli za umeme. Anatumia betri za vipakatalishi, ambazo ananunua kutoka kwa maduka ya takataka kompyuta huko Accra ili kutengeneza baiskeli zake. Anajulikana kuwa raia wa kwanza wa Ghana kutengeneza baiskeli za umeme kutoka kwa betri za vipakatalishi na amejifunza. Naishi karibu na Lawrence na mimi ni msaidizi wake. Hii si mara yangu ya kwanza kuendesha. Nimekuwa nikiendesha pikipiki kwa miaka miwili sasa. Hali ya uendeshaji ni tofauti. Tofauti. Siwezi hata kulinganisha kwa sababu kuendesha baiskeli ya kawaida... kuna uchungu mwingi. Na kisha unaweza kupenda idadi ya kilomita unazohitaji kwenda. Kwa hivyo hii ni tofauti kabisa ikilinganishwa na nilizowahi kutumia. Hii ina gia tatu na hizo nyingine hazina. Ina breki ambayo inachaji betri wakati unaitumia, baiskeli nyingine hazina. Ina lango la USB ambalo linaweza kuchaji simu yako au kutumia mwangaza wa USB. Vitu ambavyo havipo kwa nyingine. Na pia ina kengele, nyingine hazikuwa na kengele. Na kisha unaweza kusimama mara moja ukitumia breko. Zinasimama mara moja. Inayofuata. Tukiangazia betri, ina kiwango cha juu unachoweza kutumia, kuweka mwanga kwa nyumba. Hapa ndipo Bw Lawrence AJ hufanya uvumbuzi wote. Hapa ndipo utengenezaji wa baiskeli za umeme kutokana na betri za vipakatalishi vilivyoharibika hufanyika na Kwa sasa nipo hapa na Bw Lawrence. Tuonyeshe mchakato unaohusika katika matumizi ya betri hizi ili kutengeneza baiskeli ya umeme. Kwa hivyo kuna betri hapa. Kwa hivyo, unazipasua hivi. Wakati mwingine unakunja au... unatumia koleo. Sawa Unaona kuwa hatutumii seli zote. Hii iko hapa, imechomoza. -Sawa -Huwezi kutumia hii, kwa hivyo Unatafuta tofauti. Jaribu nyingine. Inayofanana. Hii iko sawa. Kwa hivyo unachukua mathabodi - ya betri. Kwa hivyo... - Sawa Kwa hivyo kuziondoa [Haisikiki] Kisha ondoa seli zake hivi. Sawa Kwa hivyo kwa jumla, unahitaji seli hizi ngapi? Nahitaji nyingi, lakini Nina betri 6 pekee hapa. Sawa Kisha unapima kwa kutumia votimita ili uone iwapo kuna kiwango cha volti ndani. Unahitaji wastani wa volti ngapi katika betri? Nafikiri kama volti 2.5. Volti 2.5 ni sawa. - Sawa - Hii ni nzuri - Sawa - Kisha tunakuja hapa na kupima kupitia mashine hii hapa. Hii inaitwa Opus. Hii hufanya vipimo vya kiwango. - Sawa - Kwa hivyo unaweka seli ndani hivi. Unaweza kuona kuwa inachaji, kwa hivyo... Itachaji betri kwa takribani saa mbili - Sawa - Saa mbili pekee Baada ya hilo, mashine itaondoa umeme kwenye betri na kukuonyesha kiwango, -Sawa -Kisha tunaiondoa. Kisha tunaandika kiwango juu yake. Kulinganisha vitu vingine pia Ina kifaa cha Bluetooth ndani yake, unachoweza kutumia kusanidi simu yako. Kwa hivyo fikiri naenda kwa kasi ya juu, haupunguzi kasi kwenye simu yako na kisha itapungua kiotomatiki. Haijalishi mchapuko. Kwa baiskeli nyingine, hazina gia ya nyuma. Unahitaji tu kuzikuma nyuma hivi. Lakini hii ina gia ya nyuma. Kwa hivyo hamna haja. Wakati umewasha ufunguo, bonyeza tu kitufe na kisha unaanza kwenda. Haichapuki kama unapokua kwenye kasi ya juu lakini ina nguvu na inapunguza kasi taratibu. Bila kujali kizuizi, itapunguza kasi taratibu. Nafikiri haya ni yote kuihusu. Kwa baiskeli nyingine, hatuna shokomzoba za mbele. Na kisha, shokomzoba za mbele, tukizungumzia hili, limejazwa hewa. Ni tofauti na hilo lingine. Hiyo nyingine ina hewa kidogo na mafuta mengi. Lakini hii ina hewa, kwa hivyo unasimama mara moja. Na unaona kuna ya nyuma pia. Pia ni tofauti upande wa nyuma. Kwa kweli, baiskeli nyingine, unapoendesha na upitie kwenye shimo, unahisi uchungu kwenye kiuno. Lakini kwa hii, huhisi uchungu. Unapitia tu shimoni na unakuwa sawa. Kwa hivyo wakati wowote unapoendesha baiskeli hii, inakufanya utamani kwenda zaidi na zaidi. Ni vyema zaidi kuwa na mojawapo ya baiskeli hizi. Jina langu ni AJ Lawarence. Naishi Kaswa katika eneo la kati la Ghana. Akiwa na miaka 11, wakati Lawrence aligundua talanta yake, alijifunza kucheza na vifaa vya kielektroniki kama vile kompyuta. Mwaka mmoja baada ya mvuto wake kukua katika nyanya hiyo, alichukua kasi ya kurekebisha baiskeli. Hadi leo, bado anarekebisha baiskeli kadhaa. Kufikia sasa, Lawrence ametengeneza na kuuza baiskeli nne za umeme mwenyewe. Baiskeli ya sasa ina vitu vilivyoboreshwa ikilinganishwa na alizotengeneza zamani. Profesa Jaya anatazamia kuwasiliana na vyuo kwa ajili ya ushirikiano ili kuboresha mawazo yake ya ubunifu. Ana ndoto ya kutumia sola kuendesha baiskeli zake baadaye, lakini anahitaji ushirikiano na vyumo na taasisi za kiufundi ili kuboresha utengenzaji kutoka sampuli hadi kuwa biashara. Katika ushirikiano huo, anatafuta kuwafunza wanafunzi wa kiufundi kuboresha ufahamu wao kuhusu elektroniki. Nina swali. Kwa hivyo jaribio hili hufanikiwa tu wakati unatumia betri za kuunganishwa au za vipakatilishi vibovu au unaweza kutumia betri mpya. Kwa hakika unaweza kutumia mpya. Sawa Sawa. Sasa kuhusu kuchaji baiskeli, inafanywa vipi? Inachajiwa kwa kutumia chaja hii hapa. Hii ni chaja maalum niliyobuni. Si kama chaja ya kawaida. Huenda ikachukua saa 12, saa 6 ili kuchaji. Sawa Hii huchaji kwa takribani saa 3. Sawa. Na, uliitengeneza mwenyewe? Ndiyo. Nilinunua sehemu. Sawa. Kwa sehemu ulizotumia, unaweza kuangazia kwa kifupi mchakato, ulivyofikia hitimisho hilo? Kwa hii, ni chanzo cha nishati cha seva. Sawa. Inatumika katika huduma ya mwanga. Unajua, huduma ya mwanga, zina kompyuta nyingi ndani. Kwa hivyo zina prosesa nzuri sana. Na hii hapa inaitwa konvata ya kuongeza nishati Sawa Kwa hivyo ukiweka volti 3 Inaibadilisha kuwa volti 84 Sawa Sasa kuhusu vipengele vya baiskeli yako Baiskeli yako ina vipengele vipi ambavyo havipo kwenye baiskeli zilizo sokoni> Kila kitu kimesanidiwa kwenye hii. Unaweza kuchagua programu inayofanya kazi kwenye simu yako. Sawa, sawa. Pia ina sehemu ya kuchaji simu zako. Pia ina breki za Evergine. Hiyo inamaanisha unapofunga breki, inachaji baiskeli Hivyo, hujaribu kutumia Venoma Veperseto unapofunga breki Inafanya mara moja unapofunga breki Unashughulikia vipi usaidizi wa mrai huu? Umekuwa ukiifanya vipi? Kujiamini. Sawa, kwa hivyo changamoto nilipokuwa nikitengeneza baiskeli zilikuwa, mwanzo sikuwa na mashine ya kushikanisha vyuma na mashine ya rangi. Kwa hivyo napeleka kwa waunganisha vyuma na wapaka rangi. Lakini wanachukua pesa na hawafanyi kazi nzuri. Niliamua kunua mashine hizo. Kisha nikaanza kujifuza kuchomelea na kupaka rangi mwenyewe. Ilinichukua takribani wiki moja au mbili kujifunza zote. Wakati mwingine marafiki zangu hunishusha moyo kuwa haitafanikiwa na kila mara unapoteza wakati kwa jambo hili, nenda ukatafute kazi na upate pesa. Changamoto zangu kuhusu fedha ni kama wakati mwingine Sipati pesa kwa wingi za kununua sehemu. Kwa hivyo nitanunua moja mwezi huu, mwezi unaofuata ninunue nyingine na zote husafirishwa, ambayo ni gharama kubwa. Kwa hivyo nikipata fedha ya kuzinunua kwa wingi, nafikiri itasaidia mchakato. Lawrence anatazamia kujenga eneo la kazi ili kubuni ajira kwa wavumbuzi wanaovutiwa na kusaidia jamii. Lawrence Adjei haweki tu Bara la Afrika kwenye ramani, pia ameonekana kuwa mmoja wa watu wengi afrika wenye akili za uvumbuzi ambao wanaweza kunawiri wakisaidiwa kiasi. Huu ndio mwisho wa kipindi cha kufana, kinachofichua na cha mafunzo cha R&D Africa kwenye AAU TV. Usisahau kuwa huenda wakati mwingine ni wewe utakayeangaziwa. Kwa hivyo iwapo una uvumbuzi wowote, wasiliana na AAU TV na tutakufikia. Tufuatilie kwenye YouTube, Facebook na kwenye mifumo yetu yote ya mtandao jamii ili upate maudhui zaidi. Jina langu - Maame Ekua Otuakoa Nyame. Hadi wakati mwingine, tumemaliza! [Muziki].