-
Nipo hapa na Jesse ambae ni Mwalimu wa hesabu
-
kwenye chuo cha Khan
-
na una maswali mazuri au mawazo.
-
Swali ambalo wanafunzi wamekuwa wanauliza wanapojifunza algebra
-
ni kwa nini tunatumia herufi, kwa nini tuisitumie namba kwenye kila kitu?
-
Kwa nini tunatumia herufi?kwa nini tuna hizi
-
X, Y na Z na ABC tunapoanza kufanya algebra?
-
sawa.
-
Inafurahisha, tunawaacha mtafakari kwa mda kidogo.
-
Hivyo Sal, utajibuje hili swali?
-
Kwa nini tunahitaji herufi kwenye Algebra?
-
Kuna sababu naweza kuzieleza.
-
Moja ni ukiwa huna kitu.
-
Hivyo kama nikiandika X jumlisha tatu in sawa na kumi.
-
tunafanya hivi kwa sababu hatujui X ni nini
-
ni kitu kisichojulikana.
-
Hivyo tunaanza kuitafuta kwa njia tofauti.
-
Ila haitakiwi kuwa X.
-
Tunaweza kuweka nafasi wazi jumlisha tatu ni sawa na kumi.
-
Au tunaweza kuweka alama ya ulizo jumlisha tatu ni sawa na kumi.
-
Hivyo sio lazima iwe herufi, ila kinachohitajika ni alama tu.
-
Inaweza kuwekwa hata uso jumlisha tatu ni sawa na kumi.
-
Ila mpaka ufahamu, unahitaji alama kuwakilisha hiyo namba tusiyoijua.
-
Sasa tunafanya hili swali na kisha tujue hiyo alama inawakilisha nini.
-
Kama tulijua kabla ya muda, isingekuwa ni kitu tusichokifahamu.
-
Isingekuwa ni kitu tusichokifahamu.
-
Hivyo hiyo ni moja ya sababu ya kutumia herufi
-
na sehemu ambayo namba zenyewe haziwezi kusaidia.
-
Nyingine ni wakati unatazama mahusiano ya namba.
-
Hivyo nitafanya kitu kama- ninaweza kusema
-
ukinipa tatu, nitakupa nne.
-
Na naweza kusema, kama ukinipa tano, nitakupa sita.
-
Ninaweza kuendelea mpaka mwisho.
-
Ukinipa 7.1, nitakupa 8.1.
-
Ninaweza kuendelea kuainisha mpaka mwisho.
-
Unaweza kunipa namba yeyote na nitakuambia nitakupa ngapi.
-
Ila nitaishiwa na sehemu na muda kama nikiziorodhesha zote.
-
Tutafanya vizuri kama tutatumia herufi kutambua namba.
-
Pengine ulichonipa tunakiita X na ninachokupa tunakiita Y.
-
Ninaweza kuisema chochote unachonipa nitajumlisha na moja.
-
Na ndicho nitakacho kurudishia.
-
Sasa, huu ni mlinganyo mrahisi hapa
-
unaweza kugundua namba inayowakilisha mahusiano baina ya X
-
na Y.
-
Sasa inajulikana X yeyote utakayonipa
-
umenipa tatu, nina jumlisha moja na nitakupa nne.
-
Ukinipa 7.1, nitajumlisha moja na nitakupa 8.1.
-
Hakuna njia ya kuwakilisha zaidi ya kutumia alama.
-
Kwahiyo, sihitaji kutumia X na Y.
-
Hizi zimezoeleka kutumika tangu zamani
-
Ninaweza kusema ulichonipa ni nyota
-
na nilichokupa ni sura
-
na hii pia inaweza kuwa njia sahihi ya kuwakilisha.
-
Hivyo herufi ni alama tu,
Hakuna cha ziada.