-
Mambo ambayo yanaweza kusababisha migongano,kutokuelewana na matatizo
-
katika mahusiano ya kibinadamu, huwa hayakosekani,
-
Lakini kadiri unavyotegemea mwitiko wako kwenye matendo ya mtu mwingine,
-
kamwe hautapatia.
-
Namaanisha nini?
-
'Hey, alinikasirisha. Ndiyo maana nina hasira.'
-
'Aliniambia hivi. Ndiyo maana nilimfokea tena.'
-
Kadiri unavyoegemeza mwitikio wako kwenye kitendo cha mtu huyo, umekosea
-
kwa sababu unafanya kazi chini ya kiwango kilichoundwa na mwanadamu, si kiwango cha Mungu.
-
Mtu anaweza kukuchokoza.
-
Angalia, simtetei mtu kama huyo. Ni vibaya kumkasirisha mtu.
-
Lakini majibu yangu ya hasira sio jukumu la mtu huyo, ni langu.
-
Jibu langu la hasira linaonyesha mahali ambapo moyo wangu hauko vizuri na Mungu,
-
si kile ambacho mtu huyo amekifanya ili kunikasirisha.