Swahili subtitles

← Kutambua magonjwa mapema, tuongee lugha ya siri ya bakteria

Get Embed Code
28 Languages

Showing Revision 6 created 04/09/2019 by Julieth Mbeyella.

 1. Hauwajui.
 2. Hauwaoni.
 3. Lakini daima wapo wanazunguka,
 4. wananong'oneza,
 5. wakitengeneza mipango ya siri,
 6. wakijenga jeshi la mamilioni ya wanajeshi.
 7. Na wanapoamua kushambulia,
 8. wanashambulia kwa wakati mmoja.
 9. Ninaongelea kuhusu bakteria.
 10. (Kicheko)

 11. Mlidhani ninaongelea kuhusu nani?

 12. Bakteria wanaishi kwenye jamii
  kama tu binadamu.

 13. Wana familia,
 14. wanaongea,
 15. na wanapanga shughuli zao.
 16. Na kama tu binadamu, wanahila, waongo,
 17. na wengine hata wanadanganyana wenyewe.
 18. Je kama nikikuambia kua tunaweza
  kusikiliza mazungumzo ya bakteria
 19. na kutafsiri taarifa zao za siri
  kuwa lugha ya binadamu?
 20. Na kama je nikiwaambia kuwa kutafsiri
  mazungumzo ya bakteria kutaokoa maisha?
 21. Nina PhD ya nanofizikia,
 22. na nimetumia teknolojia ya nano kuunda
  chombo cha kutafsiri cha muda halisi
 23. kinachoweza kupeleleza kwenye jamii
  za bakteria
 24. na kutupa rekodi za nini
  bakteria wanafanya.
 25. Bakteria wanaishi kila sehemu.

 26. Wako kwenye udongo, kwenye samani zetu
 27. na ndani ya miili yetu.
 28. Ki ukweli, asilimia 90 ya seli zote hai
  kwenye huu ukumbi ni bakteria.
 29. Baadhi ya bakteria ni wazuri
  kwetu;
 30. wanatusaidia kumeng'enya chakula
  au kutengeneza dawa.
 31. Na baadhi ya bakteria na wabaya kwetu:
 32. wanasababisha magonjwa na kifo.
 33. Kushirikisha kazi zote bakteria
  walizonazo,
 34. wanatakiwa wawe na uwezo wa
  kupanga,
 35. na wanafanya hivyo kama tu sisi
  binadamu --
 36. kwa mawasiliano.
 37. Lakini badala ya kutumia
  maneno,
 38. wanatumia molekuli za ishara
  kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe.
 39. Bakteria wanapokuwa wachche,
 40. molekuli za ishara zinatiririka nje,
 41. kama kelele za mtu peke yake
  jangwani.
 42. Lakini kukiwa na bakteria wengi,
  molekuli za ishara zinajikusanya,
 43. na bakteria wanaanza kuhisi kuwa
  hawapo peke yao.
 44. Wanasikilizana wenyewe.
 45. Kwa njia hii, wanapima
  wako wangapi
 46. na wanapokuwa wengi wa kutosha
  kuanzisha hatua mpya.
 47. Na pale molekuli za ishara zinafika
  kizingiti flani,
 48. bakteria wote wanahisi kwa mara moja
  kua wanahitaji kutenda
 49. kwa tendo hilo hilo.
 50. Hivyo mazungumzo ya bakteria yanakuwa
  na mwanzo na jibu,

 51. uzalishaji wa molekuli
  na majibu yake.
 52. Kwenye utafiti wangu, nimelenga kupeleleza
  kwenye jamii za bakteria
 53. ndani ya mwili wa binadamu.
 54. Inafanyaje kazi?
 55. Tunasampuli kutoka kwa mgonjwa.
 56. Inaweza kuwa ni sampuli ya damu au mate.
 57. Tunapiga elektroni ndani ya sampuli,
 58. elektroni zitaingilia na molekuli
  zozote za mazungumzo zilizopo,
 59. na huu muingiliano utatupa
  taarifa
 60. ya aina ya bakteria,
 61. aina ya mawasiliano
 62. na kiasi gani bakteria wanazungumza.
 63. Lakini inakuaje pale
  bakteria wakizungumza?

 64. Kabla sijaunda chombo cha kutafsiri,
 65. dhana yangu ya kwanza ilikua bakteria
  watakua na lugha ya halisi,
 66. kama vichanga ambao bado hawajaunda
  maneno na sentensi.
 67. Wanapocheka, wanafuraha;
  wanapolia, wanahuzuni.
 68. Rahisi kama hivyo.
 69. Lakini bakteria walionekana kutokuwa
  karibu na halisi kama nilivyodhani.
 70. Molekuli sio tu molekuli.
 71. Inaweza kumaanisha vitu tofauti
  kulingana na muktadha,
 72. kama tu vilio vya watoto
  vinavyomaanisha vitu tofauti:
 73. saa nyingine mtoto ana njaa,
 74. saa nyingine amelowa,
 75. saa nyingine ameumia au anaogopa.
 76. Wazazi wanajua jinsi ya kusoma hivi vilio.
 77. Na kua chombo kizuri cha kutafsiri,
 78. kinatakiwa kiwe na uwezo wa kusoma
  molekuli za ishara
 79. na kuzitafsiri
  kulingana na muktadha.
 80. Na nani anajua?
 81. Labda Tafsiri ya Google inaweza
  kuiptisha hii.
 82. (Kicheko)

 83. Hebu niwape mfano.

 84. Nimeleta baadhi ya taarifa za bakteria
  zinazoweza kuwa ngumu kuelewa
 85. kama hauna mafunzo,
 86. lakini jaribu kuangalia.
 87. (Kicheko)

 88. Hii ni familia ya bakteria yeye furaha
  ambayo imemshambulia mgonjwa.

 89. Wacha tuwaite familia ya Montague.
 90. Wanatumia wote rasilimali,
  wanazaliana, wanakua.
 91. Siku moja, wanapata mgeni mpya,
 92. familia ya bakteria Capulet.
 93. (Kicheko)

 94. Kila kitu ni sawa,
  alimradi wanafanya kazi kwa pamoja.

 95. Lakini kitu kisichopangwa kinatokea.
 96. Romeo wa Montague anakua na mahusiano
  na Juliet wa Capulet.
 97. (Kicheko)

 98. Na ndio, wanagawiana chembe za urithi.

 99. (Kicheko)

 100. Sasa, uhamisho wa kinasaba unaweza
  kuwa hatari kwa wakina Montague

 101. waliokuwa na matarajio ya kuwa familia
  pekee kwenye mgonjwa waliomshambulia,
 102. kugawana chembe za urithi
  kunachangia
 103. kwa wakina Capulet kutengeneza
  kinga kwa dawa.
 104. Hivyo wakina Montague wanaanza kuongea
  kwa ndani kuondoa hii familia nyingine
 105. kwa kutoa molekuli hii.
 106. (Kicheko)

 107. Na kwa maelezo:

 108. [Hebu turatibu shambulizi.]

 109. (Kicheko)

 110. Hebu turatibu shambulizi.

 111. Na kila mtu mara moja akaitikia
 112. kwa kutoa sumu
  itakayoua ile familia nyingine.
 113. [Ondoa!]

 114. (Kicheko)

 115. Wakina Capulet wakajibu kwa
  kuita shambulizi la kujibu.

 116. [Shambulia!]

 117. Na wakawa na vita.

 118. Hii ni video ya bakteria wa ukweli
  wakipigana na viumbe kama upanga,

 119. ambapo wanajaribu kuuana
 120. kwa kuchomana kihalisi
  na kupasuana wenyewe.
 121. Familia ya yeyote atakayeshinda hii vita
  anakuwa bakteria mkuu.
 122. Hivyo ninachoweza kufanya ni kuchunguza
  mazungumzo ya bakteria

 123. yanayopelekea tabia
  tofauti za kwa pamoja
 124. kama ugomvi mliyouona.
 125. Na nilichofanya ni kupeleleza
  kwenye jamii za bakteria
 126. ndani ya mwili wa binadamu
 127. kwenye wagonjwa hospitalini.
 128. Nilifuatilia wagonjwa 62 kwenye jaribio,
 129. ambapo nilipima sampuli ya mgonjwa
  kwa aina moja ya shambulizi,
 130. bila kujua majibu ya
  vipimo vya kawaida.
 131. Basi, kwenye upimaji wa bakteria,

 132. sampuli inasambazwa kwenye kisahani,
 133. na kama bakteria watakua ndani ya siku
  tano,
 134. mgonjwa anagunduliwa kama ameathirika.
 135. Nilipomaliza utafiti na
  kulinganisha majibu ya chombo
 136. na vipimo vya kawaida
  na vipimo vya kuhakikisha,
 137. nilishtuka.
 138. Ilikua inashangaza zaidi
  kuliko nilivyowahi kutarajia.
 139. Ila kabla sijawaambia
  nini chombo kilionyesha,

 140. ningependa kuwaambia kuhusu
  mgonjwa mahsusi niliomfuatilia,
 141. binti mdogo.
 142. Alikua na cystic fibrosis,
 143. ugonjwa wa kurithi uliofanya mapafu yake
  kuathiriwa kirahisi na bakteria.
 144. Huyu binti hakua sehemu ya
  majaribio.
 145. Nilimfuatilia kwa sababu nilijua
  kutoka kwenye taarifa zake
 146. kua hakuwahi kupata mashambulizi
  kabla.
 147. Mara moja kwa mwezi, huyu binti
  alienda hospitali
 148. kuweka sampuli ya kohozi
  ambayo alitemea kwenye kikombe.
 149. Hii sampuli ilisafirishwa kwa
  uchunguzi wa bakteria
 150. huko maabara kuu
 151. ili madaktari watende haraka
  iwapi wangekuta shambulizi.
 152. Iliniruhusu mimi kupima chombo
  changu kwa sampuli zake pia.
 153. Miezi miwili ya mwanzo nilipima
  sampuli zake, hakukua na kitu.

 154. Lakini mwezi wa tatu,
 155. Niligundua mazungumzo ya
  bakteria kwenye sampuli yake.
 156. Bakteria walikua wanashirikiana
  kuharibu tishu ya pafu lake.
 157. Lakini vipimo vya kawaida
  havikuonyesha bakteria kabisa.
 158. Nilipima tena mwezi ujao,
 159. na niliona kua yale mazungumzo ya
  bakteria yamekua makali zaidi.
 160. Bado, vipimo vya kawaida
  havikuonyesha chochote.
 161. Utafiti wangu ukaisha, lakini nusu mwaka
  baadae, nikafuatilia hali yake
 162. kuona kama bakteria niliowajua
  pekee walipotea
 163. bila muingilio wa tiba.
 164. Hawakupotea.
 165. Yule binti sasa alikua amegundulika
  na mashambulio makali
 166. ya bakteria wabaya.
 167. Walikua ni wale wale bakteria
  chombo changu kiligundua kabla.
 168. Na licha ya ukali wa
  dawa za kutibu,
 169. ilikua inashindikana
  kuondoa mashambulizi.
 170. Madaktari waliona kua asingeweza
  kufikia miaka ya 20.
 171. Nilipopima kwenye sampuli ya binti huyu,

 172. kifaa changu kilikua kwenye
  hatua za mwanzo.
 173. Sikujua hata
  kama njia yangu ilifanya kazi kabisa,
 174. hivyo nikawa na makubaliano
  na madaktari
 175. kutowaambia chombo changu
  kilichoonyesha
 176. ili kutokuharibu matibabu yao.
 177. Hivyo nilipoona haya majibu
  ambayo hata hayakuwa yamehakikishwa,
 178. sikudhubutu kusema
 179. ka sababu kutibu mgonjwa
  bila mashambulizi halisi
 180. pia ina matokeo mabaya
  kwa mgonjwa.
 181. Lakini sasa tunajua bora,
 182. na kuna wavulana na wasichana wadogo
  wengi bado wanaweza kuokolewa
 183. kwa sababu, bahati mbaya,
  hii hali inatokea mara nyingi.
 184. Wagonjwa wanaathirika,
 185. bakteria kwa namna flani hawaonekani
  kwenye vipimo vya kawaida,
 186. na ghafla, maambukizi yanatokea
  ndani ya mgojwa na dalili kali.
 187. Na kwenye mda huo, tayari tumechelewa.
 188. Majibu ya kushangaza ya
  wagonjwa 62 niliowafuatilia

 189. yalikua chombo changu kilishika
  mazungumzo ya bakteria
 190. kwa zaidi ya nusu ya sampuli za wagonjwa
 191. ambao walikua wamegundulika bila kitu
  kwa njia za upimaji za kawaida.
 192. Kwa maneno mengine, zaidi ya nusu ya
  hawa wagonjwa walirudi nyumbani wakiwaza
 193. kua wako huru na maambukizi,
 194. japokuwa kihalisi walibeba
  bakteria hatari.
 195. Ndani ya wagonjwa waliopimwa vibaya,
 196. bakteria walikuwa wanaandaa shambulizi
  la kuambatanishwa.
 197. Walikua wananong'onezana.
 198. Ninachoita "mnong'ono wa bakteria"
 199. ni bakteria ambao njia za kawaida
  za upimjai haziwezi kuona.
 200. Mpaka sasa, ni chombo cha kutafsiri tu
  kinachoweza kudaka hao wanong'onezaji.
 201. Ninaamini kua mda uliopo ambao
  bakteria bado wananong'onezana
 202. ni nafasi nzuri ya matibabu
  ya malengo.
 203. Kama yule binti angekua ametibiwwa
  kwenye kuu mda wenye nafasi,
 204. ingekua inawezekana kuua
  bakteria
 205. kwenye hatua yao ya mwanzo,
 206. kabla maambukizi kuwa nje ya uwezo.
 207. Nilichopitia na huyu binti mdogo
  kumenifanya niamue kufanya ninachoweza

 208. kusukuma hii teknolojia kwenye hospitali.
 209. Pamoja na madaktari,
 210. tayari ninafanya kazi kutumia
  hiki kifaa kwenye kliniki
 211. kutambua maambukizi ya kwanza.
 212. Japo bado haijajulikana jinsi
  madaktari watatibu wagonjwa

 213. kwenye kipindi cha mnong'ono,
 214. hiki kifaa kinaweza kusaidia madaktari
  kuwa makini na wagonjwa kwenye hatari.
 215. Kinaweza kuwasaidia kuhakikisha
  kama tiba imefanya kazi au la,
 216. na inaweza kusaidia kujibu maswali rahisi:
 217. Mgonjwa ana mashambulizi?
 218. Na bakteria wako wanapanga nini?
 219. Bakteria wanaongea,

 220. wanatengeneza mipango ya siri,
 221. na wanatumiana taarifa za siri.
 222. Lakini sio tu kuawaangalia wenyewe
  wakinong'onezana,
 223. sisi sote tunaweza kujifunza lugha ya siri
 224. na kua wenyewe wanong'onezi wa bakteria.
 225. Na, kama bakteria wangesema,
 226. "3-oxo-C12-aniline."
 227. (Kicheko)

 228. (Makofi)

 229. Asanteni.