Return to Video

"Hatusongi mbele" kwenye maombolezo. Tunaendelea nayo mbele

  • 0:01 - 0:03
    Mwaka 2014 ulikua ,mkubwa kwangu.
  • 0:03 - 0:05
    Ulishawahi kuwa na hio,
  • 0:05 - 0:07
    kama tu mwaka mkubwa, kama mwaka bango?
  • 0:07 - 0:09
    Kwangu, ulienda hivi:
  • 0:09 - 0:12
    Oktoba 3, nilipoteza ujauzito wangu wa
    pili.
  • 0:12 - 0:15
    Halfu Oktoba 3, baba yangu alifariki kwa
    saratani.
  • 0:15 - 0:18
    Halafu tena Novemba 25,
    mme wangu Aaron alifariki
  • 0:18 - 0:21
    baada ya miaka mitatu
    ya hatua ya nne ya glioblastoma,
  • 0:21 - 0:23
    ambalo ni neno la mbwembwe
    la saratani ya ubongo.
  • 0:25 - 0:26
    Hivyo, nina vichekesho.
  • 0:27 - 0:28
    (Kicheko)
  • 0:28 - 0:32
    Watu wanapenda kunialika sehemu kila mara.
  • 0:32 - 0:33
    Maingiano kibao.
  • 0:33 - 0:36
    Kawaida, ninapoongelea
    hiki kipindi cha maisha yangu,
  • 0:36 - 0:40
    majibu ninayopata kimsingi ni:
  • 0:40 - 0:42
    (Mhemo)
  • 0:42 - 0:43
    "Siwezi -- siwezi kufikiria."
  • 0:45 - 0:47
    Lakini ninafikiri unaweza.
  • 0:48 - 0:49
    Ninafikiri unaweza.
  • 0:49 - 0:50
    Na ninafikiri kua unatakiwa
  • 0:50 - 0:53
    kwa sababu, siku moja,
    itakutokea wewe.
  • 0:53 - 0:58
    Labda sio hizi hasara kabisa
    kwenye namna hii maalum au kwa kazi hii,
  • 0:58 - 0:59
    ila nimesema, nina vichekesho
  • 0:59 - 1:03
    na utafiti nilioona
    utakushangaza:
  • 1:03 - 1:06
    kila mtu unaempenda ana
    nafasi asilimia 100 ya kufa.
  • 1:06 - 1:09
    (Kicheko)
  • 1:09 - 1:11
    Na ndio maana ukaja TED.
  • 1:11 - 1:13
    (Kicheko)
  • 1:13 - 1:16
    (Makofi)
  • 1:16 - 1:18
    Tangu hasara yote ilivyonitokea,
  • 1:18 - 1:22
    nimefanya kazi kuongelea kuhusu kifo na
    hasara,
  • 1:22 - 1:25
    sio yangu tu,
    kwa sababu ni rahisi kukumbuka,
  • 1:25 - 1:29
    lakini hasara na mikasa
    ambayo watu wengine wamepitia.
  • 1:29 - 1:31
    Ni sehemu, naweza kusema.
  • 1:31 - 1:33
    (Kicheko)
  • 1:33 - 1:36
    Ni sehemu ndogo, na natamani
    ningekua na hela nyingi, lakini ...
  • 1:36 - 1:37
    (Kicheko)
  • 1:37 - 1:41
    Nimeandika vitabu vya kuinua kweli,
  • 1:41 - 1:44
    nikaendesha podikasti ya kuinua sana,
    nikaanzaisha shirika lisilo la serikali.
  • 1:44 - 1:46
    Ninajaribu tu kufanya ninachoweza
  • 1:46 - 1:49
    kufanya watu wengi zaidi wafarijike
    kwenye hali zilizo ngumu,
  • 1:50 - 1:52
    na majonzi ni magumu sana.
  • 1:52 - 1:56
    Ni magumu sana, haswa
    kama ni majonzi ya mtu mwingine.
  • 1:57 - 2:02
    Basi sehemu ya hio kazi ni hili kundi
    nililoanzisha na rafiki yangu Moe,
  • 2:02 - 2:03
    ambae pia ni mjane;
  • 2:03 - 2:05
    tunaliita Chama cha Wajane Wadogo Wakali.
  • 2:05 - 2:07
    (Kicheko)
  • 2:07 - 2:09
    Na ni ukweli, tuna kadi za uwanachama
  • 2:09 - 2:11
    na tisheti.
  • 2:11 - 2:15
    Na pale mtu wako akifariki,
    mmeo, mke, mchumba,
  • 2:15 - 2:17
    hatujali kabisa kama ulikua kwenye ndoa,
  • 2:17 - 2:20
    marafiki zako na familia yako
    watakua tu wanaangalia
  • 2:20 - 2:22
    kwa marafiki wa marafiki
    wa marafiki wa marafiki
  • 2:22 - 2:25
    mpaka wapate mtu
    ambae amepitia hali inayofanana,
  • 2:25 - 2:27
    halafu watawasukuma
    mje pamoja
  • 2:27 - 2:32
    ili muongee miongoni mwenu na msiwe
    na masikitiko kwa watu wengine.
  • 2:32 - 2:34
    (Kicheko)
  • 2:34 - 2:35
    Basi ndicho tunachofanya.
  • 2:35 - 2:39
    Ni mfululizo tu wa makundi madogo,
  • 2:39 - 2:42
    ambapo wanaume, wanawake, mashoga, wa
    kawaida, wanandoa, wenye wenza,
  • 2:43 - 2:47
    wanaweza kuongelea kuhusu mtu wao
    aliyekufa,
  • 2:47 - 2:48
    na kusema vile vitu
  • 2:48 - 2:52
    ambavyo mtu mwingine kwenye maisha yao
    hayuko tayari kuvisikia bado.
  • 2:52 - 2:54
    Eneo kubwa la mazungumzo.
  • 2:54 - 2:56
    Kama, "Mme wangu alikufa wiki mbili
    zilizopita,
  • 2:56 - 2:58
    siwezi kuacha kufikiria kuhusu
    ngono, ni kawaida?"
  • 2:58 - 3:00
    Ndio.
  • 3:00 - 3:02
    "Je kama ni mmoja wa
    Property Brothers?"
  • 3:02 - 3:03
    Kawaida kidogo, ila nitaikubali.
  • 3:03 - 3:06
    (Kicheko)
  • 3:07 - 3:11
    Vitu kama, "Ona, nikiwa hadharani na
    nikaona wazee wanashikana mikono,
  • 3:11 - 3:13
    wenzi ambao ni wazi wamekua
    pamoja kwa miongo,
  • 3:13 - 3:16
    halafu ninawaangalia na kuwaza
  • 3:16 - 3:18
    vitu vyote ambavyo wamepitia
    pamoja,
  • 3:18 - 3:20
    vitu vizuri na vitu vibaya,
  • 3:20 - 3:23
    ugomvi waliokuanao
    kuhusu nani wa kutoa taka ...
  • 3:23 - 3:26
    nakuta tu moyo umejawa na hasira."
  • 3:26 - 3:27
    (Kicheko)
  • 3:27 - 3:29
    Na huo mfano ni wa pekee kwangu.
  • 3:30 - 3:33
    Mazungumzo mengi ambayo
    tunakuwa nayo kwenye kundi
  • 3:33 - 3:35
    yanaweza na yanakaa miongoni mwetu,
  • 3:35 - 3:37
    lakini kuna vitu tunavyoviongelea
  • 3:37 - 3:40
    ambavyo duniani --
    dunia ambayo iko karibu na majonzi
  • 3:40 - 3:42
    ila bado haijapigwa na majonzi
  • 3:42 - 3:44
    inaweza kweli kunufaika kusikia.
  • 3:44 - 3:45
    Na kama huwezi kusema,
  • 3:45 - 3:50
    ninavutiwa/uwezo tu wa
    masomo yabbsiyo ya kisayansi,
  • 3:50 - 3:52
    nilienda kwenye
    Chama cha Wajane Wadogo Wakali
  • 3:52 - 3:57
    na kusema, "Habari, marafiki, unakumbuka
    mtu wako alivyokufa?" Walikumbuka.
  • 3:57 - 3:59
    "Unakumbuka vitu vyote watu
    walikuambia?"
  • 3:59 - 4:00
    "Ah, ndio."
  • 4:00 - 4:02
    "Ni vipi ulivyovichukia zaidi?"
  • 4:02 - 4:05
    Nilipata maoni mengi, majibu mengi,
    watu wanasema vitu vingi,
  • 4:05 - 4:08
    lakini viwili vilisimama juu haraka sana.
  • 4:09 - 4:10
    "Kusonga mbele."
  • 4:12 - 4:14
    Sasa, tangu 2014,
  • 4:14 - 4:18
    nitakuambia nilifunga ndoa tena na
    mwanaume mzuri kweli aitwae Matthew,
  • 4:18 - 4:21
    tuna watoto wanne
    kwenye familia yetu iliyochanganyika,
  • 4:21 - 4:25
    tuniashi kwenye viunga
    vya Minneapolis, Minnesota, Marekani.
  • 4:25 - 4:26
    Tuna mbwa aliyeokolewa.
  • 4:26 - 4:28
    (Kicheko)
  • 4:28 - 4:29
    ninaendesha gari la familia,
  • 4:29 - 4:32
    kama la aina ambayo milango inafunguka
    bila hata kuigusa.
  • 4:32 - 4:33
    (Kicheko)
  • 4:33 - 4:36
    Kama, "mezhure" yoyte, maisha ni mazuri.
  • 4:36 - 4:39
    Sijawahi pia kusema "mezhure,"
    sijawahi hata mara moja kuisema hivyo.
  • 4:39 - 4:45
    (Kicheko)
  • 4:45 - 4:46
    Sijui hata imetokea wapi.
  • 4:46 - 4:48
    (Kicheko)
  • 4:48 - 4:51
    Sijawahi kusikia mtu yeyote
    akiisema hivyo.
  • 4:51 - 4:53
    Inaonekana kama inapaswa kusemwa hivyo,
  • 4:53 - 4:55
    na ndio sababu lugha ya Kiingereza
    ni mbovu, basi ...
  • 4:55 - 4:56
    (Kicheko)
  • 4:56 - 4:58
    Ninavutiwa sana na mtu
    ambae anaiongea
  • 4:58 - 5:01
    kuongezea kwenye lugha
    inayoeleweka -- kazi nzuri.
  • 5:01 - 5:03
    (Kicheko)
  • 5:03 - 5:05
    Lakini, kwa vyovote vile ...
  • 5:05 - 5:06
    (Kicheko)
  • 5:06 - 5:11
    Kwa vyovyote vile, maisha ni mazuri
    sana sana, lakini "sijasonga mbele."
  • 5:12 - 5:15
    Sijasonga mbele,
    na siupendi kabisa huo msemo,
  • 5:15 - 5:17
    na ninaelewa kwanini wengine hawaupendi.
  • 5:17 - 5:18
    Kwa sababu unachosema
  • 5:18 - 5:23
    ni kua maisha na kifo cha Aaron
    na upendo ni wakati tu
  • 5:23 - 5:27
    ambao nauweza kuuacha nyuma yangu --
    na kua napaswa kufanya hivyo.
  • 5:27 - 5:31
    Na ninapoongelea kuhusu Aaron,
    ninaingia kirahisi kwenye hali halisi,
  • 5:31 - 5:33
    na nimewaza kweli kua hio inanifanya
    wa ajabu.
  • 5:33 - 5:36
    Halafu nikagundua kua kila mtu anafanya
    hivyo.
  • 5:37 - 5:41
    Na sio kwa sababu tuna kana
    au kwa sababu tunasahau,
  • 5:41 - 5:43
    ni kwa sababu watu
    tunaowapenda, tuliowapoteza,
  • 5:43 - 5:45
    bado ni halisi kwetu sisi.
  • 5:47 - 5:49
    Basi, ninaposema, "Oh, Aaron ni ..."
  • 5:50 - 5:53
    Ni kwa sababu Aaron bado yupo.
  • 5:54 - 5:56
    Na sio kwa namna
    alivyokua kabla.
  • 5:56 - 5:57
    iliyokua bora zaidi,
  • 5:57 - 6:01
    na sio namna ambayo watu wa kanisani
    wanavyojaribu kuniambia anavyokua.
  • 6:01 - 6:04
    ni kua tu amezimika,
  • 6:05 - 6:08
    na hivyo yupo sasa kwangu.
  • 6:09 - 6:10
    Hapa,
  • 6:10 - 6:12
    yupo hapa kwenye kazi ninayofanya,
  • 6:12 - 6:15
    kwenye mtoto tulionae pamoja,
  • 6:15 - 6:17
    kwenye hawa watoto wengine watatu
    ninaolea,
  • 6:17 - 6:20
    ambao hawajawahi kunuona,
    ambao hawana DNA yake,
  • 6:20 - 6:23
    lakini wapo kwenye maisha yangu tu
    kwa sababu nilikuwa na Aaron
  • 6:23 - 6:25
    na kwa sababu nilimpoteza Aaron.
  • 6:26 - 6:29
    Yupo nami kwenye ndoa yangu na Matthew,
  • 6:29 - 6:32
    kwa sababu maisha na upendo na kifo cha
    Aaron
  • 6:32 - 6:35
    vimenifanya kua mtu ambae
    Matthew angetaka kuoa.
  • 6:35 - 6:39
    Hivyo sijasonga mbele kutoka kwa Aaron,
  • 6:39 - 6:42
    nimesonga mbele na yeye.
  • 6:45 - 6:51
    (Makofi)
  • 6:51 - 6:56
    Tulisambaza majivu ya Aaron
    kwenye mto aupendao huko Minnesota,
  • 6:56 - 6:57
    na pale begi lilipokua tupu --
  • 6:57 - 7:02
    kwa sababu ukiwa umechomwa,
    unatoshea kwenye mfuko wa plastiki --
  • 7:02 - 7:05
    kulikua na majibu bado
    yamebaki kwenye vidole vyangu.
  • 7:05 - 7:08
    Na ningeingiza tu mikono yangu kwenye
    maji na kuisuuza,
  • 7:08 - 7:11
    lakini badala lake, nililamba mikono
    yangu,
  • 7:12 - 7:15
    kwa sababu niliogopa kupoteza zaidi
    ya nilichopoteza zaidi,
  • 7:15 - 7:19
    na nilitamani sana kuhakikisha kua
    atakua ni sehemu yangu daima.
  • 7:20 - 7:22
    Lakini bila shaka atakua.
  • 7:23 - 7:27
    Kwa sababu unapomuona mtu wako
    akijijaza na sumu kwa miaka mitatu,
  • 7:27 - 7:30
    ili tu aweze kuishi
    zaidi kidogo na wewe,
  • 7:30 - 7:32
    hilo linakaa na wewe.
  • 7:33 - 7:38
    Unapomuangalia akififia kutoka kwenye
    mtu mwenye afya siku mliokutana
  • 7:38 - 7:39
    kuwa sifuri, hiyo inakaa na wewe.
  • 7:39 - 7:42
    Unapomuangalia mwanao,
    amba hata bado hana miaka miwili,
  • 7:42 - 7:45
    akienda kitandani kwa baba yake
    siku ya mwisho ya maisha yake,
  • 7:45 - 7:47
    kama vile anajua kinachofuata
    masaa machache,
  • 7:47 - 7:52
    na kusema, "Nakupenda. Nimemaliza.
    Kwaheri."
  • 7:54 - 7:56
    Hiyo inakaa na wewe.
  • 7:57 - 8:02
    Kama tu unapopenda,
    hatimae, unapopenda kweli
  • 8:02 - 8:04
    mtu anaekuelewa na kukuona
  • 8:04 - 8:08
    na unaona pia, "Mungu wangu,
    nimekua nikikosea mda wote huu.
  • 8:08 - 8:12
    Upendo sio mashindano au
    kipindi cha televisheni -- ni ukimya sana,
  • 8:12 - 8:16
    ni huu uzi usioonekana wa utulivu
    unatuunganisha wawili
  • 8:16 - 8:18
    hata kama kila kitu kina vurugu,
  • 8:18 - 8:21
    vitu vinapoenda vibaya,
    hata kama akiondoka."
  • 8:22 - 8:25
    Hio inakaa na wewe.
  • 8:27 - 8:28
    Tulikua tunafanya hivi --
  • 8:28 - 8:31
    mikono yangu ilikua na
    baridi na yeye ana joto,
  • 8:31 - 8:34
    nilichukua mikono yangu ya barafu
    na kuisukuma ndani ya shati lake ...
  • 8:35 - 8:37
    kuikandamiza kwenye mwili wake mkali.
  • 8:37 - 8:39
    (Kicheko)
  • 8:39 - 8:42
    Na alikua hapendi kabisa,
  • 8:42 - 8:43
    (Kicheko)
  • 8:43 - 8:44
    lakini alinipenda,
  • 8:44 - 8:49
    na alivyokufa,
    nililala kitandani na Aaron
  • 8:49 - 8:52
    na nikaweka mikono yangu chini yake
  • 8:53 - 8:56
    na nikahisi joto lake.
  • 8:58 - 9:02
    Na sikuweza hata kusema kama
    mikono yangu ilikua na baridi,
  • 9:02 - 9:03
    lakini ninaweza kuwaambia
  • 9:03 - 9:06
    kua nilijua ilikua mara ya mwisho
    ningeweza kufanya hivyo.
  • 9:08 - 9:11
    Na hio kumbukumbu
    itakua ya kusikitisha daima.
  • 9:12 - 9:14
    Hio kumbukumbu itauma daima.
  • 9:14 - 9:17
    Hata kama nikiwa na miaka 600
    na ni hologramu tu.
  • 9:17 - 9:19
    (Kicheko)
  • 9:20 - 9:26
    Kama tu kumbukumbu ya kukutana nae
    itanifanya nicheke daima.
  • 9:28 - 9:30
    Maombolezo hayatokei kwenye huu
    utupu,
  • 9:30 - 9:36
    yanatokea pamoja na na ikichanganyika
    na hisia zote hizi nyingine.
  • 9:38 - 9:43
    Hivyo, nikakutana na Matthew, mme wangu wa
    sasa --
  • 9:43 - 9:44
    ambae hapendi hicho cheo,
  • 9:44 - 9:48
    (Kicheko)
  • 9:49 - 9:50
    lakini ni sawa kabisa.
  • 9:50 - 9:53
    (Kicheko)
  • 9:54 - 9:56
    Nilikutana na Matthew, na ...
  • 9:58 - 10:01
    kulikua na hii pumzi ya wazi ya faraja
    kati ya watu wanaonipenda,
  • 10:01 - 10:03
    kama, "Imekwisha!
  • 10:05 - 10:06
    Ameweza.
  • 10:07 - 10:10
    Amepata mwisho mzuri,
    tunaweza kurudi nyumbani sasa.
  • 10:10 - 10:12
    Na tumefanya vizuri."
  • 10:12 - 10:15
    Na hio hadithi inafaa hata
    hata kwangu,
  • 10:15 - 10:18
    na nikawaza labda nimeipata
    hio pia, lakini haikua hivyo.
  • 10:18 - 10:21
    Nilipata sura nyingine.
  • 10:21 - 10:25
    Na ni sura nzuri sana --
    nakupenda, mpenzi --
  • 10:25 - 10:27
    ni sura nzuri sana.
  • 10:27 - 10:31
    Tena haswahaswa mwanzoni,
    ilikua kama ulimwengu mbadala,
  • 10:31 - 10:34
    au moja ya vile vitabu ya zamani vya
    "chagua shani yako" vya miaka ya 80
  • 10:34 - 10:36
    ambapo kuna mistari miwili sambamba.
  • 10:36 - 10:38
    Nikafungua moyo wangu kwa
    Matthew,
  • 10:38 - 10:42
    na ubongo wangu ukawa,
    "Ungependa kumfikiria Aaron?
  • 10:42 - 10:46
    Kama zamani, sasa, mbeleni,
    ingia tu huko," na nilifanya hivyo.
  • 10:47 - 10:50
    Na ghafla,
    hiyo mistari miwili ilifunguka kwa pamoja,
  • 10:50 - 10:54
    na kupendana na Matthew kumenisaidia
    sana kugundua ukubwa
  • 10:54 - 10:56
    wa nilichopoteza Aaron alivyofariki.
  • 10:58 - 10:59
    Na ilivyo muhimu,
  • 10:59 - 11:03
    ilinisaidia kugundua kua upendo wangu
    kwa Aaron
  • 11:03 - 11:05
    na maombolezo yangu kwa Aaron,
  • 11:05 - 11:09
    na upendo wangu kwa Matthew,
    sio nguvu za kupishana.
  • 11:11 - 11:13
    Ni sehemu tu za uzi mmoja
  • 11:14 - 11:16
    Ni vitu sawa sawa.
  • 11:18 - 11:21
    Wazazi wangu wangesemaje?
  • 11:21 - 11:23
    Mimi sio wa pekee.
  • 11:24 - 11:25
    (Kicheko)
  • 11:25 - 11:27
    Walikua na watoto wanne,
    walikua kama ... wa kweli.
  • 11:27 - 11:29
    (Kicheko)
  • 11:29 - 11:31
    Lakini mimi sio, mimi sio wa pekee.
  • 11:31 - 11:33
    Ninajua hilo, ninajua vizuri
  • 11:33 - 11:35
    kua siku nzima, kila siku
    duniani kote,
  • 11:35 - 11:37
    vitu vibaya vinatokea.
  • 11:37 - 11:38
    Kila mara.
  • 11:38 - 11:40
    Kama nilivyosema, mtu mcheshi.
  • 11:40 - 11:43
    Lakini vitu vibaya vinatokea,
  • 11:43 - 11:49
    watu wanapata hasara za kina na mbaya
    kila siku.
  • 11:49 - 11:52
    Na kama sehemu ya kazi yangu,
  • 11:52 - 11:53
    hii podikasti ya ajabu niliyonayo,
  • 11:53 - 11:55
    kuna mda ninaongea na watu
  • 11:55 - 11:58
    kuhusu kitu kibaya
    kilichowahi kuwatokea.
  • 11:58 - 12:01
    Na saa nyingine, hio ni
    kupotelewa na mpendwa,
  • 12:01 - 12:05
    mara nyingine siku, wiki miaka
    au miongo iliyopita.
  • 12:06 - 12:09
    Na hawa watu ninaowahoji,
  • 12:09 - 12:11
    hawajajifungia wenyewe
    kwenye hii hasara
  • 12:11 - 12:14
    na kuifanya sehemu kuu ya maisha yao.
  • 12:14 - 12:18
    Wameishi, dunia zao
    zimeendelea kuzunguka.
  • 12:19 - 12:23
    Lakini wanaongea na mimi,
    mgeni kabisa,
  • 12:23 - 12:25
    kuhusu mtu wanaempenda aliyekufa,
  • 12:25 - 12:28
    kwa sababu hivi ndivyo vitu tunavyopitia
  • 12:28 - 12:33
    vinavyotuonyesha na kutufanya
    kama tu wale wenye furaha.
  • 12:33 - 12:35
    Na kama ilivyo ya kudumu.
  • 12:37 - 12:39
    Baadae baada ya kupata kadi yako
    ya mwisho ya huruma
  • 12:39 - 12:41
    au pishi la moto la mwisho.
  • 12:42 - 12:44
    Kama, hatuangalii watu
    wanaotuzunguka
  • 12:44 - 12:48
    wakipitia furaha na maajabu ya maisha
    na kuwaambia "wasonge mbele", ndio?
  • 12:48 - 12:52
    Hatutumi kadi ambazo zinasema
    "Hongera kwa mtoto mzuri,"
  • 12:52 - 12:55
    halafu, miaka mitano baadae, tunawaza,
    "Sherehe nyingine ya kuzaliwa? Acha hizo."
  • 12:55 - 12:57
    (Kicheko)
  • 12:57 - 12:59
    Ndio, tunaelewa, ana miaka mitano.
  • 12:59 - 13:00
    (Kicheko)
  • 13:00 - 13:01
    Wow.
  • 13:01 - 13:03
    (Kicheko)
  • 13:04 - 13:06
    Lakini maombolezo ni moja ya vile vitu,
  • 13:06 - 13:10
    kama kupenda au kuwa na mtoto
    au kuangalia "The Wire" kwenye HBO,
  • 13:10 - 13:14
    ambapo hauelewi
    mpaka upate, mpaka ufanye.
  • 13:15 - 13:21
    Na punde unavyofanya,
    punde ni mpenzi wako au mtoto wako,
  • 13:21 - 13:26
    punde ni maombolezo yako
    na uko mstari wa mbele kwenye msiba,
  • 13:26 - 13:27
    unaelewa.
  • 13:27 - 13:31
    Unaelewa unachopitia sio
    sehemu ya mda,
  • 13:31 - 13:33
    sio mfupa kua utajirudi,
  • 13:33 - 13:36
    lakini kua umeguswa na kitu kikali.
  • 13:37 - 13:38
    Kitu kisichotibika.
  • 13:38 - 13:41
    Hakiui, lakini saa nyingine
    yanakua kama yanaweza.
  • 13:43 - 13:47
    Na kama hatuwezi kuzuia miongoni mwetu,
  • 13:47 - 13:48
    nini tunaweza kufanya?
  • 13:51 - 13:55
    Nini tunaweza kufanya zaidi ya
    kukumbushiana
  • 13:55 - 13:58
    kua vitu vingine havirekebishiki,
  • 13:58 - 14:01
    na sio kila kidonda kinapaswa kupona.
  • 14:02 - 14:06
    Tunahitajiana kukumbuka,
  • 14:06 - 14:07
    kusaidiana kukumbuka,
  • 14:07 - 14:10
    kua maombolezo ni hisia ya mambo mengi.
  • 14:10 - 14:16
    Kua unaweza na utakua na huzuni, na
    furaha; utaomboleza na kupenda
  • 14:16 - 14:19
    kwenye mwaka au wiki au pumzi hio hio.
  • 14:21 - 14:27
    Tunahitaji kukumbuka kua mtu anaeomboleza
    ataenda kucheka na kutabasamu tena.
  • 14:27 - 14:31
    Wakibahatika,
    wanaweza hata kupenda tena.
  • 14:32 - 14:35
    Lakini ndio, hakika
    wataenda kusonga mbele.
  • 14:36 - 14:39
    Lakini hiyo haimaanishi kua
    wameendelea mbele.
  • 14:40 - 14:41
    Asanteni.
  • 14:41 - 14:48
    (Makofi)
Title:
"Hatusongi mbele" kwenye maombolezo. Tunaendelea nayo mbele
Speaker:
Nora Mclnerny
Description:

Kwenye maongezi ambayo yanapishana kwa kusikitisha na kuchekesha, mwandishi na mwanapodikasti Nora Mclnerny anashirikisha busara yake iliyopatikana kwa shida kuhusu maisha na kifo. Mtazamo wake wa wazi kwenye kitu ambacho, kwa kweli, kitatuathiri wote, ambacho ni huru na ni kigumu. Kwa nguvu zaidi, anatusisitizia kubadili jinsi tunavyoona maombolezo. "Mtu anaeomboleza ataenda kucheka na kutabasamu tena," anasema. "Wataenda kusonga mbele. Lakini haimaanishi wameendelea mbele."

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
15:05

Swahili subtitles

Revisions