Tunawezaje kupima umbali angani? - Yuan-Sen Ting
-
0:07 - 0:10Mwanga ndio kitu kilicho na kasi zaidi
tunalojua. -
0:10 - 0:13Lina kasi sana tunapima umbali mkubwa sana
-
0:13 - 0:16kutumia muda ambao mwanga hutumia
kuisafiri. -
0:16 - 0:20Kwa mwaka mmoja, mwanga husafiri takriban
maili bilioni sita, -
0:20 - 0:23umbali tunaoita mwaka mmoja wa mwanga.
-
0:23 - 0:25Kukupa wazo la umbali huu,
-
0:25 - 0:29mwezi, lililowachukua wanaanga wa Apollo
siku nne kuifikia, -
0:29 - 0:32ni sekundi moja tu la mwanga kutoka dunia.
-
0:32 - 0:37Wakati huo huo, nyota lililo karibu
kupita jua letu ni Proxima Centauri, -
0:37 - 0:40umbali wa miaka ya mwanga 4.24.
-
0:40 - 0:44Milky Way yetu iko kwenye mpango wa
miaka ya mwanga 100,000 toka upande mmoja. -
0:44 - 0:47Galaksi iliyo karibu sana na yetu,
Andromeda, -
0:47 - 0:50ni umbali wa takriban miaka ya mwanga
millioni 2.5 -
0:50 - 0:53Anga una upana mkubwa kushangaza.
-
0:53 - 0:57Lakini ngoja, tuanjuaje ubali wa nyota na
magalaksi? -
0:57 - 1:01Ata hivyo, tunapotazama anga,
tuna mtazamo wa mielekeo miwili. -
1:01 - 1:05Ukielekeza kidole chako kwa nyota moja,
huwezi kujua umbali wa nyota hio, -
1:05 - 1:09kwa hivyo wanaastrofysik wanajuaje?
-
1:09 - 1:11Kwa vitu vilivyo karibu sana,
-
1:11 - 1:15tunaweza kutumia dhana inayoitwa
"trigonometric parallax". -
1:15 - 1:17Wazo hili ni rahisi sana.
-
1:17 - 1:18Tufanye jaribio.
-
1:18 - 1:21Elekeza gumba lako na ufumbe jicho lako
la kushoto. -
1:21 - 1:25Sasa, fumbua jicho lako la kushoto na
ufumbe jicho lako la kulia. -
1:25 - 1:27Itaonekana ni kama gumba lako limesonga,
-
1:27 - 1:31wakati ambapo vitu vingine vilivyo mbali
kwenye usuli vimebaki pale pale. -
1:31 - 1:34Wazo hilo linatumika tunapotazama nyota,
-
1:34 - 1:38lakini nyota za mbali ziko na umbali
mkubwa sana kuliko mkono wako, -
1:38 - 1:40na dunia sio kubwa sana,
-
1:40 - 1:43kwa hivyo hata kama ungekuwa na darubini
tofauti kwenye ikweta, -
1:43 - 1:46huautaona mbadiliko mkubwa wa nafasi.
-
1:46 - 1:51Badala ya hivyo, tunatazama mabadiliko ya
msimamo wa nyota baada ya miezi sita, -
1:51 - 1:56msimamo nusu wa mzunguko mmoja wa dunia
kwa jua. -
1:56 - 1:59Tunapohesabu misimamo wa nyota kwenye
msimu wa kiangazi, -
1:59 - 2:03na tena kwenye msimu wa majira ya baridi,
ni kama kutazama na jicho lako jingine. -
2:03 - 2:05Nyota za karibu zinaonekana zimesongea
kwenye usuli -
2:05 - 2:08wa nyota na galaksi na nyota zilizo mbali.
-
2:08 - 2:13Lakini mbinu hii inatumika kwa vitu
vilivyo chini ya miaka ya mwanga elfu. -
2:13 - 2:16Kupita galaksi yetu,
umbali ni mkubwa sana -
2:16 - 2:21kiasi cha parallax ni ndogo sana
kuchunguza na vyombo vyetu vyovyote. -
2:21 - 2:24Kwa hivyo kwa wakati huu inabidi tutumie
mbinu nyingine -
2:24 - 2:27kutumia viashiria tunavyoita
mishumaa ya kiwangogezi. -
2:27 - 2:32mishumaa ya kiwangogezi ni vile vitu
ambavyo mwangaza wao -
2:32 - 2:34tunaujua vizuri sana.
-
2:34 - 2:37Kwa mfano, kama unaujua mwangaza wa
taa lako, -
2:37 - 2:41na umuulize rafiki yako alichukue hilo taa
na atembee mbali na wewe, -
2:41 - 2:44unajua kiasi cha mwangaza utakayopata
kutoka rafiki yako -
2:44 - 2:47itapungua na umbali.
-
2:47 - 2:50Kwa hivyo kufananisha kiasi cha
mwanga utakayopata -
2:50 - 2:52na mwangaza wa taa ile,
-
2:52 - 2:55unaweza kujua umbali wa rafiki yako.
-
2:55 - 2:58Kwa somo la falaki, taa lako linakua
aina spesheli ya nyota -
2:58 - 3:01inayoitwa "cepheid variable".
-
3:01 - 3:03Nyota hizi hazina msimamo wa kindani,
-
3:03 - 3:07kama baluni inayofutuka na kutoa hewa.
-
3:07 - 3:11Na kwa ajili kufutuka na kupoteza hewa
inarekebisha mwangaza wao, -
3:11 - 3:15tunaweza kuhesabu mwanga wao kwa kuhesabu
muda wa mzunguko huo, -
3:15 - 3:19na nyota zilizo na mwanga nyingi na
zinazobadilika polepole. -
3:19 - 3:22Kwa kufananisha mwangaza wa nyota hizi
-
3:22 - 3:24kwa mwangaza tuliohesabu kwa mbinu hii,
-
3:24 - 3:27tunagundua umbali wao.
-
3:27 - 3:30Kwa bahati mbaya, huu sio mwisho
wa hadithi. -
3:30 - 3:35Tunaweza kutazama nyota zilizo takriban
miaka milioni arubaini ya nyota pekee, -
3:35 - 3:38Baada ya hapo, hazionekani vizuri.
-
3:38 - 3:41Kwa bahati nzuri tunayo aina nyingine ya
mshumaa: -
3:41 - 3:44ya umaarufu aina ya "1a supernova".
-
3:44 - 3:50"Supernovae", milipuko mikubwa ndio moja
wa njia ambazo nyota hufa. -
3:50 - 3:52Milipuko hii ina mwangaza sana,
-
3:52 - 3:55inashinda mwangaza wa galaksi zilipo.
-
3:55 - 3:58Kwa hivyo tunaposhindwa kuona nyota
moja-moja ya galaksi, -
3:58 - 4:01bado tunaweza kuona "supernovae"
zinapotokea. -
4:01 - 4:05Na aina ya "type 1a supernovae" inaweza
kutumika kama mishumaa -
4:05 - 4:09kwa ajili zilizo na mwanga mkubwa sana
hufifia polepole kushinda zile dhaifu. -
4:09 - 4:11Kwa kuelewa uhusiano huu
-
4:11 - 4:13kati ya mwanga na kiwango cha kufifia,
-
4:13 - 4:16tunaweza kutumia "supernovae"kupata umbali
-
4:16 - 4:19wa bilioni kadhaa ya
miaka ya mwanga. -
4:19 - 4:24Lakini ni nini umuhumu wa kutazama vitu
vilivyo mbali nasi? -
4:24 - 4:27Basi kumbuka kasi ambao mwangaza husafiri.
-
4:27 - 4:31Kwa mfano, mwangaza wa jua unachukua
dakika nane kutufikia, -
4:31 - 4:37kumaanisha kuwa mwangaza tunaouona sasa
hivi ni picha ya jua dakika 8 zilizopita -
4:37 - 4:38Unapoiangalia "Big Dipper",
-
4:38 - 4:42unaangalia jinsi ilivyokuwa
miaka 80 iliyopita. -
4:42 - 4:43Na galaksi zisizoonekana
vyema? -
4:43 - 4:46Zina umbali wa mamilioni ya miaka
ya mwangaza . -
4:46 - 4:49Imezichukua mamilioni ya miaka kutufikia.
-
4:49 - 4:55Kwa hivyo ulimwengu wenyewe kwa njia, ina
mashine ya wakati. -
4:55 - 4:59Tunapotazama mbali zaidi,
tunagundua ulimwengu mchanga zaidi. -
4:59 - 5:02Wanaastrofysiks hujaribu kusoma historia
ya ulimwengu, -
5:02 - 5:06na kugundua lini na wapi tunapotoka.
-
5:06 - 5:11Ulimwengu unaendelea kututumia habari
kwa njia ya mwangaza. -
5:11 - 5:14Kilichobaki ni sisi kuisimbua.
- Title:
- Tunawezaje kupima umbali angani? - Yuan-Sen Ting
- Description:
-
Anagalia somo lote hapa: http://ed.ted.com/lessons/how-do-we-measure-distances-in-space-yuan-sen-ting
Tunapoangalia anga, tunaona muonekano wa usawa. Sasa je wanaanga wanajuaje umbali wa nyota kutoka duniani? Yuan-Sen Ting anatuonyesha jinsi vitu kama mishumaa vinavyoweza kusaidia kupima umbali wa vitu vilivyo mbali sana kutoka duniani.
Somo na Yuna-Sen Ting. Michoro na TED-Ed.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TED-Ed
- Duration:
- 05:30
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for How do we measure distances in space? - Yuan-Sen Ting | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for How do we measure distances in space? - Yuan-Sen Ting | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for How do we measure distances in space? - Yuan-Sen Ting | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for How do we measure distances in space? - Yuan-Sen Ting | |
![]() |
roina ochieng edited Swahili subtitles for How do we measure distances in space? - Yuan-Sen Ting | |
![]() |
roina ochieng edited Swahili subtitles for How do we measure distances in space? - Yuan-Sen Ting |