Mwanga ndio kitu kilicho na kasi zaidi tunalojua. Lina kasi sana tunapima umbali mkubwa sana kutumia muda ambao mwanga hutumia kuisafiri. Kwa mwaka mmoja, mwanga husafiri takriban maili bilioni sita, umbali tunaoita mwaka mmoja wa mwanga. Kukupa wazo la umbali huu, mwezi, lililowachukua wanaanga wa Apollo siku nne kuifikia, ni sekundi moja tu la mwanga kutoka dunia. Wakati huo huo, nyota lililo karibu kupita jua letu ni Proxima Centauri, umbali wa miaka ya mwanga 4.24. Milky Way yetu iko kwenye mpango wa miaka ya mwanga 100,000 toka upande mmoja. Galaksi iliyo karibu sana na yetu, Andromeda, ni umbali wa takriban miaka ya mwanga millioni 2.5 Anga una upana mkubwa kushangaza. Lakini ngoja, tuanjuaje ubali wa nyota na magalaksi? Ata hivyo, tunapotazama anga, tuna mtazamo wa mielekeo miwili. Ukielekeza kidole chako kwa nyota moja, huwezi kujua umbali wa nyota hio, kwa hivyo wanaastrofysik wanajuaje? Kwa vitu vilivyo karibu sana, tunaweza kutumia dhana inayoitwa "trigonometric parallax". Wazo hili ni rahisi sana. Tufanye jaribio. Elekeza gumba lako na ufumbe jicho lako la kushoto. Sasa, fumbua jicho lako la kushoto na ufumbe jicho lako la kulia. Itaonekana ni kama gumba lako limesonga, wakati ambapo vitu vingine vilivyo mbali kwenye usuli vimebaki pale pale. Wazo hilo linatumika tunapotazama nyota, lakini nyota za mbali ziko na umbali mkubwa sana kuliko mkono wako, na dunia sio kubwa sana, kwa hivyo hata kama ungekuwa na darubini tofauti kwenye ikweta, huautaona mbadiliko mkubwa wa nafasi. Badala ya hivyo, tunatazama mabadiliko ya msimamo wa nyota baada ya miezi sita, msimamo nusu wa mzunguko mmoja wa dunia kwa jua. Tunapohesabu misimamo wa nyota kwenye msimu wa kiangazi, na tena kwenye msimu wa majira ya baridi, ni kama kutazama na jicho lako jingine. Nyota za karibu zinaonekana zimesongea kwenye usuli wa nyota na galaksi na nyota zilizo mbali. Lakini mbinu hii inatumika kwa vitu vilivyo chini ya miaka ya mwanga elfu. Kupita galaksi yetu, umbali ni mkubwa sana kiasi cha parallax ni ndogo sana kuchunguza na vyombo vyetu vyovyote. Kwa hivyo kwa wakati huu inabidi tutumie mbinu nyingine kutumia viashiria tunavyoita mishumaa ya kiwangogezi. mishumaa ya kiwangogezi ni vile vitu ambavyo mwangaza wao tunaujua vizuri sana. Kwa mfano, kama unaujua mwangaza wa taa lako, na umuulize rafiki yako alichukue hilo taa na atembee mbali na wewe, unajua kiasi cha mwangaza utakayopata kutoka rafiki yako itapungua na umbali. Kwa hivyo kufananisha kiasi cha mwanga utakayopata na mwangaza wa taa ile, unaweza kujua umbali wa rafiki yako. Kwa somo la falaki, taa lako linakua aina spesheli ya nyota inayoitwa "cepheid variable". Nyota hizi hazina msimamo wa kindani, kama baluni inayofutuka na kutoa hewa. Na kwa ajili kufutuka na kupoteza hewa inarekebisha mwangaza wao, tunaweza kuhesabu mwanga wao kwa kuhesabu muda wa mzunguko huo, na nyota zilizo na mwanga nyingi na zinazobadilika polepole. Kwa kufananisha mwangaza wa nyota hizi kwa mwangaza tuliohesabu kwa mbinu hii, tunagundua umbali wao. Kwa bahati mbaya, huu sio mwisho wa hadithi. Tunaweza kutazama nyota zilizo takriban miaka milioni arubaini ya nyota pekee, Baada ya hapo, hazionekani vizuri. Kwa bahati nzuri tunayo aina nyingine ya mshumaa: ya umaarufu aina ya "1a supernova". "Supernovae", milipuko mikubwa ndio moja wa njia ambazo nyota hufa. Milipuko hii ina mwangaza sana, inashinda mwangaza wa galaksi zilipo. Kwa hivyo tunaposhindwa kuona nyota moja-moja ya galaksi, bado tunaweza kuona "supernovae" zinapotokea. Na aina ya "type 1a supernovae" inaweza kutumika kama mishumaa kwa ajili zilizo na mwanga mkubwa sana hufifia polepole kushinda zile dhaifu. Kwa kuelewa uhusiano huu kati ya mwanga na kiwango cha kufifia, tunaweza kutumia "supernovae"kupata umbali wa bilioni kadhaa ya miaka ya mwanga. Lakini ni nini umuhumu wa kutazama vitu vilivyo mbali nasi? Basi kumbuka kasi ambao mwangaza husafiri. Kwa mfano, mwangaza wa jua unachukua dakika nane kutufikia, kumaanisha kuwa mwangaza tunaouona sasa hivi ni picha ya jua dakika 8 zilizopita Unapoiangalia "Big Dipper", unaangalia jinsi ilivyokuwa miaka 80 iliyopita. Na galaksi zisizoonekana vyema? Zina umbali wa mamilioni ya miaka ya mwangaza . Imezichukua mamilioni ya miaka kutufikia. Kwa hivyo ulimwengu wenyewe kwa njia, ina mashine ya wakati. Tunapotazama mbali zaidi, tunagundua ulimwengu mchanga zaidi. Wanaastrofysiks hujaribu kusoma historia ya ulimwengu, na kugundua lini na wapi tunapotoka. Ulimwengu unaendelea kututumia habari kwa njia ya mwangaza. Kilichobaki ni sisi kuisimbua.