< Return to Video

Volume of a rectangular prism: fractional dimensions | Geometry | 6th grade | Khan Academy

  • 0:00 - 0:01
  • 0:01 - 0:03
    Hebu tuone kama tunaweza kukokotoa ukubwa
  • 0:03 - 0:06
    wa huu mche mstatili, nadhani
  • 0:06 - 0:08
    unaufananisha na umbo la tofali
  • 0:08 - 0:10
    au tangisamaki.
  • 0:10 - 0:13
    Na kinachovutia hapa ni hivi vipimo
  • 0:13 - 0:16
    vilivyo kwenye sehemu, tuna upana.
  • 0:16 - 0:17
    Tunaweza kusema huu ni upana.
  • 0:17 - 0:20
    Upana wa hapa ni hatua 3/5.
  • 0:20 - 0:23
    Urefu wa hapa ni hatua 1 na 1/6,
  • 0:23 - 0:26
    na urefu wa hapa ni hatua 3/7.
  • 0:26 - 0:28
    Hivyo simamisha hii video,
  • 0:28 - 0:31
    na ujaribu kutafuta ukubwa wa umbo hili mwenyewe,
  • 0:31 - 0:34
    kabla ya kufanya pamoja.
  • 0:34 - 0:36
    Hivyo kuna njia mbalimbali za kufanya swali hili.
  • 0:36 - 0:39
    Njia moja wapo ya kufanya swali hili ni
  • 0:39 - 0:42
    kuweka hatua za ukubwa hapa,
  • 0:42 - 0:45
    na njia ya kutafuta hatua za ukubwa zitakazofaa
  • 0:45 - 0:50
    hapa ni kutafuta eneo la hiki kitako
  • 0:50 - 0:52
    hapa.
  • 0:52 - 0:53
    Hivyo muda mwingine unaweza kusema ukubwa ni
  • 0:53 - 0:59
    sawa na eneo la kitako mara urefu.
  • 0:59 - 1:02
    Huu hapa ni urefu,
  • 1:02 - 1:03
    ngoja niuelezee.
  • 1:03 - 1:05
    Hili ni eneo la kitako.
  • 1:05 - 1:08
    Eneo la kitako mara urefu.
  • 1:08 - 1:10
    Vizuri, eneo la kitako ni nini?
  • 1:10 - 1:12
    Eneo la kitako ni sawa
  • 1:12 - 1:15
    na urefu mara upana, hivyo huenda
  • 1:15 - 1:16
    umeona ikiandikwa kama hivi.
  • 1:16 - 1:19
    Huenda umeona ikiandikwa kama eneo la kitako,
  • 1:19 - 1:24
    litakuwa urefu mara upana.
  • 1:24 - 1:29
    Zidisha upana.
  • 1:29 - 1:34
    Urefu mara upana ni sawa na eneo la kitako chako,
  • 1:34 - 1:36
    hapa.
  • 1:36 - 1:39
    Na bila shaka, utazidisha mara urefu.
  • 1:39 - 1:40
    Au njia nyingine ni,
  • 1:40 - 1:42
    kuzidisha urefu uliopewa
  • 1:42 - 1:44
    mara upana mara urefu.
  • 1:44 - 1:47
    Utazidisha vipimo vitatu vya umbo hili,
  • 1:47 - 1:49
    ilikupata hatua za ukubwa
  • 1:49 - 1:52
    wa hili umbo.
  • 1:52 - 1:53
    Hivyo hebu tukokotoe.
  • 1:53 - 1:57
    Ukubwa utakuwa...urefu wetu ni ngapi?
  • 1:57 - 2:00
    Urefu wetu ni hatua 1 na 1/6.
  • 2:00 - 2:03
    Ninapozidisha sehemu,
  • 2:03 - 2:05
    Sipendelei kuzidisha namba mchanganyiko.
  • 2:05 - 2:08
    Huwa napendelea kuandika kwenye sehemu isiyo sahili.
  • 2:08 - 2:12
    Hivyo nabadili 1 na 1/6 kuwa sehemu isiyo sahili.
  • 2:12 - 2:14
    1 ni sawa na 6/6.
  • 2:14 - 2:16
    Jumlisha 1 ni 7/6.
  • 2:16 - 2:19
    Hivyo hii itakuwa 7/6.... huu ni
  • 2:19 - 2:27
    urefu --- mara 3/5--- huu ni urefu nilionao--
  • 2:27 - 2:29
    mara urefu, ambao ni 3/7.
  • 2:29 - 2:35
  • 2:35 - 2:37
    Na tunapozidisha sehemu,
  • 2:37 - 2:42
    tunazidisha viasi, hivyo itakuwa 7 mara
  • 2:42 - 2:47
    3 mara 3.
  • 2:47 - 2:50
    Na asili, tunazidisha asili.
  • 2:50 - 2:57
    Hivyo itakuwa 6 mara 5 mara 7.
  • 2:57 - 3:00
  • 3:00 - 3:01
    Sasa, tunazidisha hizi namba,
  • 3:01 - 3:07
    ilitupate jibu lililorahisiswa
  • 3:07 - 3:09
    hebu tuone.
  • 3:09 - 3:12
    Tuna 7 kwenye kiasi na 7 kwenye asili,
  • 3:12 - 3:15
    hivyo tugawe kiasi na asili kwa 7.
  • 3:15 - 3:19
  • 3:19 - 3:24
    Hivyo hii itakuwa 1, na hizi zote zitakuwa 1.
  • 3:24 - 3:27
    Pia tumeona kwenye kiasi na asili kuna 3.
  • 3:27 - 3:29
    Zote zinagawanyika kwa 3.
  • 3:29 - 3:30
    Tunaona 3 hapa juu.
  • 3:30 - 3:31
    Tunaona 3 hapa.
  • 3:31 - 3:32
    Hivyo tunagawanya kiasi
  • 3:32 - 3:35
    na asili kwa 3.
  • 3:35 - 3:36
    Hivyo tunagawanya kwa 3.
  • 3:36 - 3:38
    Gawanya kwa 3.
  • 3:38 - 3:40
    3 gawanya kwa 3 ni 1.
  • 3:40 - 3:45
    6 gawanya kwa 3 itakuwa sawa na 2.
  • 3:45 - 3:48
    Hivyo kwenye kiasi, tumebakiwa na ngapi?
  • 3:48 - 3:50
    Hii itakuwa sawa na kilichobakia,
  • 3:50 - 3:52
    kwenye hii 3.
  • 3:52 - 3:57
    Itakuwa sawa na 3 chini ya 2 mara 5.
  • 3:57 - 4:00
    2 mara 5 ni 10.
  • 4:00 - 4:01
    2 mara 5.
  • 4:01 - 4:06
    Hivyo ukubwa wa hapa ni hatua za ukubwa 3/10.
  • 4:06 - 4:10
    au tunaweza kujaza hatua za ukubwa 3/10 ndani ya hili tofali,
  • 4:10 - 4:15
    au hili tangisamaki, vyovyote utakavyoliita.
Title:
Volume of a rectangular prism: fractional dimensions | Geometry | 6th grade | Khan Academy
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
Khan Academy
Duration:
04:14

Swahili subtitles

Revisions