JINSI YA KUSHINDA MAUDHI KATIKA MAHUSIANO!
-
0:00 - 0:05Jinsi ya Kushinda Maudhi
-
0:07 - 0:11Neema na amani iwe kwenu nyote
katika jina kuu la Yesu. -
0:11 - 0:19Karibuni nyote katika toleo lingine la 'Imani Ni Asili' hapa kwenye TV ya Moyo wa Mungu.
-
0:19 - 0:27Sasa, leo, nataka kushiriki nanyi nyote ujumbe wenye somo muhimu
-
0:27 - 0:35kuhusu jinsi ya kushinda maudhi
katika mahusiano yetu. -
0:35 - 0:41Maana nimeona mara nyingi sana
-
0:41 - 0:49jinsi mahusiano yanavyoweza kuharibika kwa urahisi kwa sababu ya maneno.
-
0:49 - 0:58Mahusiano mengi siku hizi yanaisha mapema kwa sababu ya maneno.
-
0:58 - 1:03Unaona ndoa zinaanguka kwenye talaka.
-
1:03 - 1:06Unaona familia zinavunjika.
-
1:06 - 1:18Unaona urafiki unafikia hatua ya kutengana kwa sababu ya maneno.
-
1:18 - 1:26Kwa njia hiyo hiyo, nimeona ni mara ngapi masuala madogo ambayo yangeweza
-
1:26 - 1:36kutatuliwa haraka, yanakuwa mbaya zaidi na kurefushwa kwa sababu ya maneno.
-
1:36 - 1:48Maneno ya bila kujali, maneno ya ovyo, maneno ya uchungu, maneno ya kichokozi, maneno yenye sumu.
-
1:48 - 1:54Lakini watu wa Mungu, ninawafafanulia leo
-
1:54 - 2:05kwamba si sumu ya maneno
bali ni uchafu wa mioyo -
2:05 - 2:12ambao hujenga maudhi
na kuvunja mahusiano, -
2:12 - 2:17wakati mwingine hata kupitailiza juu ya suluhu.
-
2:17 - 2:20Uchafuzi wa mioyo.
-
2:20 - 2:30Unaona, maneno yanaweza kusemwa katika wakati wa kutokuwa na hadhari, kutojali,
-
2:30 - 2:33uchochezi, maumivu au hasira.
-
2:33 - 2:45Lakini maneno hayo yanaweza kuwekwa moyoni kwa siku, wiki, miezi, hata miaka -
-
2:45 - 2:52muda mrefu baada ya hisia za wakati huo kufifia,
-
2:52 - 3:03muda mrefu baada ya hali zilizozunguka majibishano hayo kubadilika.
-
3:03 - 3:06Sasa, acha niseme wazi kabisa kwenu,
watu wa Mungu. -
3:06 - 3:12Siungi mkono kwa njia yoyote au kuunga mkono matumizi ya maneno yenye sumu.
-
3:12 - 3:14Hapana! Hapana kabisa.
-
3:14 - 3:20Kwa hakika, Bwana wetu Yesu Kristo alisema
katika Mathayo 12:36-37, -
3:20 - 3:28'Tutatoa hesabu kwa kila neno lisilo na maana linalosemwa.'
-
3:28 - 3:36Kama Wakristo, ni lazima tutoe sala hiyo ambayo Daudi alitoa katika Zaburi 141:3,
-
3:36 - 3:42'Ee Bwana, uweke mlinzi juu ya midomo yangu;
uweke mlinzi mlangoni pa kinywa changu’, -
3:42 - 3:44ili tuepuke matatizo ya ulimi.
-
3:44 - 3:51Kwa hivyo siungi mkono kwa njia yoyote matumizi ya maneno yenye sumu. Hapana!
-
3:51 - 3:57Lakini katika ujumbe wa leo,
Ninataka kuangazia mwitikio wetu -
3:57 - 4:03tunapokuwa kwenye upande wa kupokea.
-
4:03 - 4:11Unaona, suala si
kusikia maneno kama hayo. -
4:11 - 4:19Suala ni kuhifadhi maneno kama haya mioyoni mwetu.
-
4:19 - 4:27Uhifadhi wa sumu ndio unaoleta uchafuzi.
-
4:27 - 4:29Sasa, nataka kuwa wa vitendo.
-
4:29 - 4:33Hebu tutoe mfano wa vitendo wa hili.
-
4:33 - 4:38Hebu fikiria unakula, kunywa au kuchukua kitu kwenye mfumo wako
-
4:38 - 4:44na ni kitu cha ajabu na mwili wako unatambua kuwa ni sumu,
-
4:44 - 4:47kitu chenye sumu.
Je, mwitikio wako wa kwanza ni upi? -
4:47 - 4:49Unatema mate.
-
4:49 - 4:52Unakiondoa haraka iwezekanavyo.
-
4:52 - 4:56Mungu ameunda miili yetu
kwa njia ambayo sisi tunakikataa -
4:56 - 5:03na kutupilia mbali kile ambacho
tunatambua kuwa ni hatari. -
5:03 - 5:07Vivyo hivyo watu wa Mungu,
-
5:07 - 5:18kuwa na maneno yenye sumu
moyoni mwako ni hatari. -
5:18 - 5:31Kwa sababu kile unachoshikilia
kinaweza kukushika kwa urahisi. -
5:31 - 5:33Fikiria kuhusu hilo.
-
5:33 - 5:36Ngoja niseme tena.
-
5:36 - 5:46Kile ambacho moyo wako unakishikilia
kinaweza kukushika haraka. -
5:46 - 5:50Kwa hiyo, swali ni hili.
-
5:50 - 6:02Kwa nini basi ni jambo la kawaida sana leo kwetu kuweka kitu ambacho ni hatari sana?
-
6:02 - 6:05Ni swali.
-
6:05 - 6:10Na hii inanileta kwenye jambo kuu
Ninataka kusisitiza -
6:10 - 6:13katika ujumbe wa leo, watu wa Mungu.
-
6:13 - 6:23Ninaamini moja ya sababu kuu zinazochangia kosa hili katika mioyo yetu
-
6:23 - 6:31ni kwa sababu tunaandika maneno ya mwanadamu
mioyoni mwetu -
6:31 - 6:36kana kwamba ni Maneno ya Mungu.
-
6:36 - 6:38Namaanisha nini?
-
6:38 - 6:50Tunatoa kiwango sawa cha thamani, umuhimu, umuhimu kwa maneno ya kibinadamu,
-
6:50 - 6:54kana kwamba yalikuwa Neno la Mungu.
-
6:54 - 7:06Sasa, Yesu Kristo anasema katika Luka 6:45
kwamba mioyo yetu ni hazina. -
7:06 - 7:19Wengi leo wamepunguza au kushusha thamani ya hazina hii
-
7:19 - 7:22mpaka katika nafasi ya pipa la taka
-
7:22 - 7:28ambapo tunaruhusu kila aina ya uchafu,
kila aina ya takataka -
7:28 - 7:36kuongeza majeraha na kustawisha uongo
mioyoni mwetu. -
7:36 - 7:45Wengi wetu leo ni wepesi sana, wepesi sana wa kutoa mioyo yetu kwa bei nafuu
-
7:45 - 7:51kwa maneno yanayotoka
katika chanzo kisichoaminika. -
7:51 - 7:54Mfano wa kawaida, watu wa Mungu.
-
7:54 - 7:56Labda umegombana na mtu.
-
7:56 - 8:01Na katika mwenendo wa ugomvi huo, maneno hasi yametumika.
-
8:01 - 8:08Na usiku huo unapoenda kulala,
unaanza kugeuza maneno hayo hasi -
8:08 - 8:13tena na tena moyoni mwako.
-
8:13 - 8:21Unaanza kurudisha nyuma akilini mwako wakati maneno kama hayo yalisemwa.
-
8:21 - 8:29Kwa kweli, wengi wetu hata tunaendelea na mazungumzo ya kufikiria na mkosaji wetu.
-
8:29 - 8:32Nini kinaendelea?
-
8:32 - 8:39Tunashusha thamani ya moyo
-
8:39 - 8:46kwa sababu tunainua maneno ya mwanadamu.
-
8:46 - 8:51Nini kinatokea kwa sababu hili,
watu wa Mungu? -
8:51 - 9:05Maudhi hukita mizizi kwa urahisi na
maneno kuwa majeraha. -
9:05 - 9:11Na ikiwa umakini hautachukuliwa, mioyo iliyoharibika itasababisha nyumba zilizoharibika.
-
9:11 - 9:16mahusiano yaliyoharibika,
fursa zilizoharibika. -
9:16 - 9:28Kwa sababu tumeyachukulia maneno ya mwanadamu kana kwamba ni Maneno ya Mungu.
-
9:28 - 9:33Watu wa Mungu, kushinda dhambi,
-
9:33 - 9:42lazima utambue kwamba moyo wako
ni wa thamani sana -
9:42 - 9:49kuweka maneno ambayo
hayahusiani na hatima yako. -
9:49 - 9:58Lazima utambue kwamba moyo wako ni wa thamani sana
-
9:58 - 10:05kuweka maneno ambayo
hayahusiani na hatima yako. -
10:05 - 10:12Watu wa Mungu, wacha niwaambie ukweli huu mkubwa, muhimu na unaobadilisha maisha!
-
10:12 - 10:19Maneno pekee yanayostahili mioyo yenu ni Maneno ya Mungu Aliye Hai!
-
10:19 - 10:25Maneno pekee ambayo ni ya kuaminika vya kutosha, ya kutegemewa vya kutosha,
-
10:25 - 10:31kutumainika vya kutosha, thabiti vya kutosha,
safi vya kutosha -
10:31 - 10:36kuyageuka tena na tena katika mioyo yetu
-
10:36 - 10:40ni Neno Hai la Mungu,
Neno la Roho Mtakatifu. -
10:40 - 10:52Kwa hiyo, watu wa Mungu, ni lazima tusitishe usajili wa matamko yasiyo halali!
-
10:52 - 10:54Namaanisha nini?
-
10:54 - 11:00Hata katika ulimwengu huu wa asili, tunatambua kwamba usajili ni kwa ajili ya kitu rasmi.
-
11:00 - 11:04Ni kwa ajili ya kitu ambacho
kimethibitishwa kuwa cha kweli. -
11:04 - 11:08Kwa hivyo, ni lazima tujiandikishe wakati wa kupiga kura ukifika.
-
11:08 - 11:11Lazima tujiandikishe ili kuhudhuria chuo kikuu.
-
11:11 - 11:15Ni lazima tujiandikishe tunapofunga ndoa.
-
11:15 - 11:21Mashirika ya serikali yanaweza kupokea maombi mengi lakini wanayachuja
-
11:21 - 11:28na kujiandikisha mara tu zikithibitishwa,
zikishathibitishwa. -
11:28 - 11:32Natumaini mnaona ninakoenda,
watu wa Mungu. -
11:32 - 11:40Akili zetu zinaweza kushughulikia mambo mengi bila moyo wetu kuyachukua,
-
11:40 - 11:43bila mioyo yetu kuyasajili.
-
11:43 - 11:48Usajili ni kwa vitu ambavyo vimethibitishwa kuwa kweli.
-
11:48 - 11:51Usajili sio kwa uwongo.
-
11:51 - 11:56Usajili si wa fantasia. Hapana!
-
11:56 - 12:04Acha kujiandikisha moyoni mwako
-
12:04 - 12:10matamko yasiyo rasmi juu ya maisha yako.
-
12:10 - 12:18Usijitoe moyo wako kwa maneno kama haya, watu wa Mungu.
-
12:18 - 12:23Matamko pekee ambayo
yanafaa kuzingatiwa -
12:23 - 12:30ni yale yalioidhinishwa na Maandiko, kwa kupatana na Maandiko, kulingana na Maandiko -
-
12:30 - 12:36mambo yapo safi, ya haki, ya adhimu, yaliyo bora, ya adili, ya kupendeza, yenye kusifiwa,
-
12:36 - 12:39kama Wafilipi 4:8 inavyosema.
-
12:39 - 12:42Hilo ndilo jambo pekee linalostahili.
-
12:42 - 12:48Maneno yasiyofaa hayastahili moyo wako.
-
12:48 - 12:53hayatafasiri thamani yako. Hapana!
-
12:53 - 12:56Mtu pekee anayestahili anayestahili ...
-
12:56 - 12:59Anastahili Mwana-Kondoo aketiye juu ya kiti cha enzi!
-
12:59 - 13:09Yule pekee anayestahili ndiye pekee aliye na uwezo wa kufafanua thamani yako,
-
13:09 - 13:11watu wa Mungu.
-
13:11 - 13:23Katika ulimwengu ambao kuna maoni na sauti nyingi zinazokinzana,
-
13:23 - 13:35maoni pekee ambayo ni muhimu sana,
maoni pekee yenye tija ni maoni ya Mungu. -
13:35 - 13:43Kwa hivyo, ikiwa mtu amezungumza
maneno mabaya juu ya maisha yako, -
13:43 - 13:47watu wa Mungu, msiyatie moyoni.
-
13:47 - 13:55Usimpe ibilisi nafasi,
kama Waefeso 4:27 inavyosema. -
13:55 - 14:00Yachunguze katika nuru safi ya
Neno la Mungu. -
14:00 - 14:04Unaweza kufikia hitimisho kwamba -
-
14:04 - 14:11Ninakataa kuchafuliwa na kile ambacho hakinifafanui.
-
14:11 - 14:16Ninakataa kuabudu maneno ambayo hayafanyi kazi.
-
14:16 - 14:23Ninakataa kupotoshwa na
habari za uwongo za shetani! -
14:23 - 14:26Ndiyo, yanaweza kunidhuru lakini
hayanishikilii. -
14:26 - 14:30Yanaweza kunidhulumu lakini
haYanimiliki. Hapana! -
14:30 - 14:34Ninaweza kujisikia vibaya lakini hisia zangu sio nahodha wa moyo wangu.
-
14:34 - 14:37Hisia zangu sio usukani wa roho yangu.
-
14:37 - 14:40Mimi si mtumwa wa hisia zangu.
-
14:40 - 14:45Naam, naweza kuitikia katika mwili
lakini sitawaliwi na mwili. -
14:45 - 14:47Asante, Yesu!
-
14:47 - 14:57Watu wa Mungu, Neno la Mungu linapokuwa mioyoni mwetu,
-
14:57 - 15:05tunaposhika Neno hilo,
huwa ngome yetu, -
15:05 - 15:07nanga yetu katika dhoruba,
-
15:07 - 15:16kimbilio letu kutokana na udanganyifu wa giza na mabadiliko ya hisia zetu.
-
15:16 - 15:18Basi ngoja nikueleze kwa namna hii leo.
-
15:18 - 15:25Jiulize swali hili.
-
15:25 - 15:33Je, kuna maneno mabaya ambayo yamesemwa juu ya maisha yako
-
15:33 - 15:42ambayo unayahifadhi moyoni mwako
wakati huu? -
15:42 - 15:45Zingatia kitu.
-
15:45 - 15:52Ili meli itie nanga bandarini, lazima
kuwe na nanga. -
15:52 - 16:01Unachohifadhi kinaonyesha
mahali unapotia nanga. -
16:01 - 16:04Kwa hivyo acha ujumbe huu wa leo ukutie moyo!
-
16:04 - 16:14Ruhusu ujumbe huu ukutie moyo kutia nanga maisha yako, tumaini lako, moyo wako
-
16:14 - 16:21juu ya mamlaka isiyobadilika ya Neno la Mungu lililo hai,
-
16:21 - 16:30si maneno ya mwanadamu yasiyo na nguvu na yanayobadilika.
-
16:30 - 16:37Mungu na abariki Neno Lake katikati
ya mioyo yetu, katika jina la Yesu. -
16:37 - 16:40Sasa hivi, tuombe pamoja.
-
16:42 - 16:46Wakati wa Maombi
-
16:47 - 16:55Kila uwongo wa shetani uliosajiliwa
moyoni mwako - -
16:55 - 17:00Ninasema, ubatilishwe!
-
17:00 - 17:05Ubatilishwe, katika jina kuu
la Yesu Kristo! -
17:05 - 17:11Kila tamko hasi
juu ya maisha yako - libatilishwe! -
17:11 - 17:15Ubatilishwe, katika jina la Yesu Kristo!
-
17:15 - 17:22Sumu yoyote ambayo imechafua moyo wako -
Natangaza utakaso sasa hivi! -
17:22 - 17:26Utakaswe!
-
17:26 - 17:32Usafishwe na
Damu ya Thamani ya Yesu Kristo! -
17:32 - 17:37Utakaswe na hiyo sumu ya uchungu!
-
17:37 - 17:41Utakaswe na sumu hiyo ya chuki!
-
17:41 - 17:51Utakaswe kutokana na sumu hiyo ya kosa,
katika jina kuu la Yesu Kristo. -
17:51 - 18:02Kumbuka, kushikilia maudhi kwa kweli ni onyesho la ukosefu wa usalama
-
18:02 - 18:07kuhusu utambulisho wetu katika Kristo.
-
18:07 - 18:17Wakati maneno yanakuwa majeraha, ni kiashiria cha jinsi tulivyoanguka
-
18:17 - 18:22kutoka kwenye ufahamu wa nafasi kuu ya Mungu.
-
18:22 - 18:30Hivi sasa, chochote kinachoshambulia hakikisho hilo la wewe ni nani katika Kristo -
-
18:30 - 18:34Ninasema, ondoshwa!
-
18:34 - 18:41Ondolewa, katika jina kuu
la Yesu Kristo! -
18:41 - 18:50Kataa sasa hivi kuwa dampo la uongo wa shetani.
-
18:50 - 18:57Kataa kuwa dampo la propaganda za shetani.
-
18:57 - 19:01Kwa imani katika jina la Yesu Kristo,
enenda katika nuru! -
19:01 - 19:02Zungumza kwenye nuru.
-
19:02 - 19:04Sogeza kwenye nuru.
-
19:04 - 19:07Tembea kwa uhuru. Tembea katika ukweli.
-
19:07 - 19:13Tembea katika nuru ya Neno lililo hai la Mungu na ushinde hisia,
-
19:13 - 19:18katika jina kuu la Yesu.
-
19:18 - 19:22Amina.
-
19:22 - 19:24Asante, Yesu.
- Title:
- JINSI YA KUSHINDA MAUDHI KATIKA MAHUSIANO!
- Description:
-
Unafanya nini pale maneno yanapokuwa majeraha? Jifunze kuzuia maneno yenye sumu yasichafue moyo wako katika ujumbe huu wa vitendo na Ndugu Chris unaoitwa, 'Jinsi ya Kushinda Maudhi'.
"Kile unachoshikilia kinaweza kukushika kwa urahisi." - Ndugu Chris
‘Imani Ni Asili’ ni kipindi kwenye TV ya Moyo Wa Mungu chenye maneno mafupi ya kutoa ari na kutia moyo katika maisha yako ya kila siku kutoka katika Neno Hai la Mungu – katika uzuri wa uumbaji Wake.
SURA:
00:00 - Utangulizi wa 'Imani ni Asili'
00:36 - Uharibifu unaoweza kuletwa na Maneno
01:55 - Suala si maneno yenye sumu bali ni moyo mchafu
04:03 - Shida sio kusikia lakini kuhifadhi
05:18 - Kile ambacho moyo wako unashikilia kinaweza kukushika si punde
06:17 - Sababu kuu inayochangia maudhi mioyoni mwetu
07:05 - Usiishushe hadhi ya hazina katika kiwango cha jalala.
09:30 - Jinsi ya kushinda kosa
10:41 - Komesha usajili wa matamko yasiyo halali
12:43 Maneno yasiyofaa hayastahili moyo wako
14:00 - Chunguza maneno katika nuru safi ya Neno la Mungu
15:53 - Unachohifadhi kinaonyesha mahali unapotia nanga
16:47 - Maombi kwa ajili ya watazamaji pamoja na Ndugu Chris#ImaniNiAsili
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Saidia TV ya Moyo wa Mungu kifedha - https://godsheart.tv/financial/
➡️ Habari kuhusu Maombi Shirikishi - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
- God's Heart TV
- Duration:
- 19:46
Stephenmigwi edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for HOW TO OVERCOME OFFENCE IN RELATIONSHIPS! |