-
Wanafunzi, karibuni kwenye ziara ya
UNESCO kuhusu 'haki ya elimu'.
-
"Subiri!" huenda mnafikiri.
-
"Haki ya elimu? Hilo linamaanisha nini?"
-
Sote tulio katika chumba hiki, elimu
ni kama jambo lingine tu la maisha.
-
Jambo rahisi, la kila siku.
-
♪ (muziki) ♪
-
Hata hivyo, elimu haipatikani kila wakati
-
na hili si jambo tu la zamani.
-
Katika sehemu nyingi duniani,
-
mamilioni ya watu,
hasa wasichana na wanawake,
-
hawajawahi kuingia darasani.
-
Fikiri tu kuhusu wanawake maishani mwako.
-
Fikiri akina mama,
dada zako, walimu, wanarika
-
wakishindwa kupata elimu
kwa sababu tu ni wanawake.
-
♪ (muziki) ♪
-
Tangazo la Jumla la Haki za Kibinadamu
-
na UNESCO zinafafanua elimu kama
haki ya msingi ya kila mwanaume, mwanamke
-
na mtoto. Kwa hivyo tunaposema kila mtu
-
ana haki ya kupata elimu
hatutaji tu ukweli wa kawaida,
-
kauli hii ni ya majivuno kutokana na
juhudi zilizofanywa miaka iliyopita
-
ili kuhakikisha kuwa elimu
inakuwa haki ya msingi ya binadamu
-
ili kuruhusu mtu yeyote na kila mtu
-
duniani kupata elimu.
-
Kuna sababu mbili kuu za umuhimu wa
haki ya kupata elimu.
-
Ya kwanza: elimu ni jambo moja
ambalo linainua hadhi yako ya
-
jamii na uchumi.
-
Haijalishi iwapo
ulizaliwa maskini au tajiri
-
kupata elimu kunaweza kukusaidia kufikia
-
malengo yako kamili.
-
Ya pili: kwa kutambua kuwa ni haki
-
elimu inakuwa jambo
tunaloweza kutetea na kuhakikisha.
-
Hii inamaanisha mashirika kama vile UNESCO
yanaweza kuweka viwango vya kimataifa
-
vya elimu na kufanya nchi
ziwajibikie kuhakikisha
-
kuwa haki ya elimu inatolewa kisheria.
-
Dunia ni mahali pakubwa
penye watu bilioni 7.6,
-
UNESCO huhakikisha vipi haki ya
-
elimu kwa watu bilioni 7.6 kwenye
kipimo cha ulimwengu?
-
Kwanza, tunafanya mikutano
ambako viongozi wanaweza kuja
-
pamoja ili kubuni makubaliano
-
kama vile makubaliano dhidi ya
ubaguzi katika elimu.
-
Desturi na viwango ili kuhakikisha
-
fursa sawa katika elimu,
kutetea haki za walimu, n.k...
-
Mikutano hii ni muhimu
ili nchi zote zikubali na kusema
-
hivi ndivyo elimu inafaa kuwa kwa wanadamu
-
bila kujali wanakotoka.
-
Tunafuatilia jinsi nchi zinatekeleza
-
haki ya elimu kwa kila mtu na
sheria na sera zinazotumika
-
kuhakikisha haki hii. Kila baada ya muda
UNESCO huwasiliana na nchi washirika
-
ikiziomba kushiriki maelezo
kuhusu jinsi wanahakikisha
-
haki ya elimu
-
na inatoa mapendekezo.
-
UNESCO pia inadumisha
ufuatiliaji mtandaoni
-
ili kutoa maelezo kuhusu hili.
-
Mwishowe, tunatetea haki ya elimu
-
kupitia utafiti wa masuala muhimu,
kama vile haki ya elimu kwa wakimbizi
-
au mifano ya jinsi sheria za elimu
katika nchi mahususi hutekelezwa.
-
Katika kiwango cha karibu tunaenda
na kuzipa nchi
-
zana zote wanazohitaji ili
kuimarisha mfumo wao wa elimu,
-
pia tunasaidia nchi kupanga
-
marekebisho yao ya elimu
na viwango vya kimataifa.
-
Kile hii inamaanisha ni tunahakikisha
mifumo yao ya sheria na sera
-
inaendana na viwango
-
ambavyo mashirika kama yetu yameweka.
-
Hii ni ili nchi zitoe mifumo
ya elimu iliyo thabiti na pana
-
kwa raia wake.
-
UNESCO ina mengi ya kufanya:
vijana na watoto milioni 263
-
hawawezi kufikia shule, chini ya nchi
1 kati ya 5 inaweza kutoa miaka 12
-
ya elimu bila malipo kwa raia wake.
-
Katika sehemu fulani za dunia
kwa mfano wasichana,
-
wakimbizi na watu walio na ulemavu
-
wana wakati mgumu kutumia haki yao
ya elimu,
-
vigezo vingi vinachangia hili kama vile
umaskini, mizozo na majanga asili.
-
Licha ya haya sisi UNESCO tunaendelea
kujitahidi kuhakikisha haki ya elimu
-
inaendelea kuwa kipaumbele cha kimataifa.
-
Ndiyo maana tuna maonyesho
kama haya ili kukumbuka
-
kilichofanywa na kinachohitaji kufanywa,
-
ili watu kote duniani waweze
kupata elimu na kutimiza ndoto zao.
-
Asante kwa kuja leo
na furahieni ziara iliyobaki.