Siri ya kujifunza lugha mpya
-
0:02 - 0:05Napenda kujifunza lugha za kigeni.
-
0:05 - 0:09napenda sana kiasi kwamba hujifunza lugha mpya kila baada ya miaka miwili,
-
0:09 - 0:11sasa hivi najifunza lugha ya nane.
-
0:11 - 0:13Pale watu wanapogundua kuhusu mimi, mara huniuliza,
-
0:14 - 0:16"Unafanyaje hivyo? Siri yako ni ipi?"
-
0:16 - 0:19Na niwe muwazi, kwa miaka mingi, jibu langu litakuwa,
-
0:19 - 0:21"Sifahamu. Napenda tu kujifunza lugha."
-
0:22 - 0:24Lakini watu hawakufurahishwa na jibu hilo.
-
0:24 - 0:28Walitaka kufahamu kwanini wanatumia miaka kujaribu kuijfunza hata lugha moja,
-
0:28 - 0:30kamwe hawafanikiwa unenaji,
-
0:30 - 0:33na mimi natokea, nikijifunza lugha moja baada ya nyingine.
-
0:33 - 0:35Walitaka kujua siri ya wanaisimu,
-
0:35 - 0:37watu wanaoongea lugha nyingi.
-
0:37 - 0:39Na hii ilinifanya kushangaa, pia,
-
0:39 - 0:41wanaisimu wengine wanafanyaje?
-
0:41 - 0:43Kitu gani tulichonacho?
-
0:43 - 0:45Na kipi ambacho kinatuwezesha sisi
-
0:45 - 0:47kujifunza lugha kwa haraka kuliko watu wengine?
-
0:48 - 0:51Niliamua kukutana na watu wengine kama mimi ili kutambua.
-
0:52 - 0:54Sehemu nzuri ya kuonana na wanaisimu wengi
-
0:54 - 0:56ni katika hafla ambapo mamia ya wapenzi wa lugha
-
0:56 - 0:59hukutana pamoja.
-
0:59 - 1:02Kuna baadhi ya hafla za wanaisimu ambazo huandaliwa duniani kote,
-
1:02 - 1:04na kwa hiyo niliamua kwenda huko
-
1:04 - 1:06na kuwauliza wanaisimu kuhusu njia wanazotumia.
-
1:07 - 1:09Nilikutana na Benny kutoka Ireland,
-
1:09 - 1:13ambaye aliniambia kwamba njia yake ni kuanza kuongea kuanzia siku ya kwanza.
-
1:14 - 1:17Hujifunza misemo michache kutoka katika kitabu cha misemo cha wasafiri
-
1:17 - 1:19na huenda kukutana na wenyeji wa lugha husika
-
1:19 - 1:22na kuanza maongezi nao moja kwa moja.
-
1:22 - 1:24Hajali kukosea kuongea hata mara 200 kwa siku,
-
1:24 - 1:27kwa sababu hivyo ndivyo anajifunza, ukilinganisha na mrejesho.
-
1:27 - 1:31Na kilicho bora ni kwamba, haitaji kusafiri sana leo,
-
1:31 - 1:34Sababu kwa urahisi unaweza fanya maongezi na wenyeji wa lugha
-
1:34 - 1:36ukiwa umepumzika katika chumba chako, ukitumia tovuti.
-
1:36 - 1:38Nilikutana pia na Lucas kutoka Brazil
-
1:38 - 1:41ambaye alikuwa na njia ya kuvutia ya kujifunza Kirussia.
-
1:41 - 1:47Kiurahisi aliwaalika waongeaji wa lugha ya Kirussia wapatao 100 kama marafiki katika mtandao wake wa Skype,
-
1:47 - 1:51na kisha alianza kupiga soga na mmoja wao
-
1:51 - 1:52na akaandika "Habari" kwa Kirussia.
-
1:53 - 1:56Yule mtu alijibu," Nzuri, hujambo?"
-
1:56 - 2:00Lucas alinakili haya maongezi na kuweka katika chumba cha maandishi alipoanza soga na mtu mwingine,
-
2:00 - 2:04na mtu alijibu. "Nipo salama, asante, na wewe hujambo?"
-
2:04 - 2:07Lucas alinakili tena na kuweka katika soga na mtu wa kwanza,
-
2:07 - 2:10na katika njia hii, aliwafanya watu wawili wasiojuana kuwa katika maongezi
-
2:10 - 2:12bila kufahamu hilo.
-
2:12 - 2:13(Kicheko)
-
2:13 - 2:15Si punde alianza kuchapa maneno mwenyewe,
-
2:15 - 2:17kwa sababu alikuwa na maongezi kama haya mengi
-
2:17 - 2:20kwamba aligundua jinsi gani maongezi ya Kirussia ambavyo kwa kawaida huanza.
-
2:20 - 2:22Njia yenye werevu sana, si ndiyo?
-
2:22 - 2:27Na kisha nilikutana na mwanaisimu ambaye muda wote huanza kwa kuigiza sauti za lugha,
-
2:27 - 2:31na wengine ambao amara zote hujifunza maneno 500 ya mara kwa mara katika lugha,
-
2:31 - 2:35na wengine ambao huanza kwa kusoma kitabu cha sarufi.
-
2:36 - 2:38Kama ningeuliza wanaisimu mbalimbali mia moja,
-
2:38 - 2:42Nilisikia namna mia moja mbalimbali za kujifunza lugha.
-
2:42 - 2:45Kila mtu alikuwa na njia tofauti ya kujifunza lugha,
-
2:45 - 2:49na wote mwishoni huja na matokeo sawa ya kuongea lugha baadhi kwa ufasaha.
-
2:50 - 2:54Na nilikuwa nawasikiliza wanaisimu hawa wakinieleza kuhusu njia zao,
-
2:54 - 2:57ghafla ikaniamsha:
-
2:57 - 3:00kitu kimoja ambacho wote tunacho
-
3:00 - 3:05ni kwamba tumeweza kutafuta namna ya kufurahia mchakato ya kujifunza lugha.
-
3:05 - 3:08Na hawa wanaisimu wote walikuwa wanaongelea kuhusu kujifunza lugha
-
3:08 - 3:10na ilikuwa inafurahisha sana.
-
3:10 - 3:11Ungewaona nyuso zao
-
3:11 - 3:14walipokuwa wakinionyesha chati za rangi zikielezea sarufi
-
3:14 - 3:16na kadi za maneno zilizotengenezwa kwa uangalifu,
-
3:16 - 3:19na takwimu zao kuhusu kujifunza maneno ya lugha kwa kutumia programu ya simu janja,
-
3:19 - 3:24au wanavyopenda kupika kutokana na maelezo ya upishi yaliyoandikwa katika lugha ya kigeni.
-
3:25 - 3:26Wote wanatumia njia mbalimbali,
-
3:26 - 3:30Lakini wanahakikisha ni kitu ambacho binafsi wanapendelea kufanya.
-
3:30 - 3:34Nimegundua kwamba hivi ndivyo mimi hujifunza lugha.
-
3:34 - 3:38Nilipokuwa najifunza Kispanyola, nilichoshwa na maandishi katika kitabu.
-
3:38 - 3:39Namaanisha, nani ambaye anataka kusoma kuhusu Jose
-
3:40 - 3:43akiuliza kuhusu uelekeo wa kwenda kituo gari moshi. Sawa?
-
3:43 - 3:45Nilitaka kusoma "Harry Porter" badala yake,
-
3:45 - 3:47kwa sababu ndicho kilikuwa kitabu nikipendacho sana nikiwa mdogo,
-
3:47 - 3:49na nimekisoma mara nyingi.
-
3:49 - 3:52Kwa hiyo nilipata tafsiri "Harry Porter" katika lugha ya Kispanyola na nikaanza kusoma,
-
3:53 - 3:56na kwa uhakika, sikuelewa chochote kile mwanzoni,
-
3:56 - 3:58lakini niliendelea kusoma kwa sababu nilikipenda kitabu,
-
3:58 - 4:02na mwishoni mwa kitabu, niliweza kukifatilia bila matatizo yoyote.
-
4:02 - 4:05Na jambo sawa lilitokea wakati nikijifunza Kijerumani.
-
4:05 - 4:08Niliamua kuangalia "Marafiki," ucheshi ninaopendelea, kwa Kijerumani,
-
4:08 - 4:11na tena, mwanzoni ilikuwa upuuzi tu.
-
4:11 - 4:15Sikuelewa ni wapi neno moja limeishia na lingine lilipoanzia,
-
4:15 - 4:17lakini niliendelea kuangalia kila siku kwa sababu ilikuwa ni "Marafiki."
-
4:17 - 4:20Naweza kuangalia katika lugha yoyote. Napenda sana.
-
4:20 - 4:22Na baada sehemu ya pili au ya tatu,
-
4:22 - 4:24kiukweli, maongezi yalianza kuleta maana.
-
4:25 - 4:28Nilitambua hili baada ya kukutana na wanaisimu wengine.
-
4:28 - 4:30Sisi si wenye talanta
-
4:30 - 4:32na hatuna njia za kukatiza katika kujifunza lugha.
-
4:32 - 4:36Tumeweza kutafuta njia ya kufurahia mchakato,
-
4:36 - 4:39namna ya kubadili usomaji wa lugha kutoka kama somo la shule lisilofurahisha
-
4:39 - 4:43hadi katika shughuli ya kuvutia ambayo hutaona shida kuifanya kila siku.
-
4:44 - 4:46Kama hupendelei kuandika maneno kwenye karatasi,
-
4:46 - 4:47unaweza mara zote kuyachapa kwenye programu ya simu.
-
4:47 - 4:50Kama hupendelei kusikiliza vitabu vinavyochosha,
-
4:50 - 4:55tafuta video zinazovutia katika Youtube au katika vipindi vya lugha.
-
4:55 - 4:56Kama wewe ni mtu unayependelea upekee
-
4:56 - 4:59na hauwezi kuwaza ni namna gani utaweza ongea na wenyeji wa lugha moja kwa moja,
-
4:59 - 5:02unaweza kujifunza kujiongelesha mwenyewe.
-
5:02 - 5:04Unaweza kuongea na nafsi yako ukiwa katika chumba chako,
-
5:04 - 5:07ukieleza mipango yako ya mwisho wa wiki, siku yako ilikwendaje,
-
5:07 - 5:09au hata kupiga picha zisizo na mpangilio katika simu yako
-
5:09 - 5:13na kuelezea kuhusu picha hiyo kwa rafiki yako wa kufikirika.
-
5:13 - 5:16Hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha,
-
5:16 - 5:19na habari njema ni kwamba, inapatikana kwa mtu yoyote
-
5:19 - 5:21nani ambaye yuko tayari kujifunza katika mikono yake.
-
5:23 - 5:25Hivyo kukutana na wanaisimu wengine kulinisaidia kutambua
-
5:25 - 5:28kwamba ni muhimu sana kupata burudani
-
5:28 - 5:30katika mchakato wa kujifunza lugha,
-
5:30 - 5:33lakini pia furaha yenyewe pekee haitoshi.
-
5:34 - 5:36Kama unataka kuweza kufikia ufasaha katika lugha ya kigeni,
-
5:36 - 5:39utahitajika kutumia kanuni tatu zaidi.
-
5:40 - 5:42Kwanza, unahitaji njia zilizo bora.
-
5:43 - 5:47Ukijaribu kukumbuka listi ya maneno kwa ajili ya mtihani wa kesho,
-
5:47 - 5:49maneno yatahifadhiwa katika kumbukumbu yako ya muda mfupi
-
5:49 - 5:51na utayasahau baada ya siku chache.
-
5:51 - 5:54Kama, hata hivyo, unataka kukaa na maneno kwa muda mrefu,
-
5:54 - 5:57unahitaji kuyarudia katika kipindi cha siku chache
-
5:57 - 6:00ukifanya kitu kinachofahamika kama kurudia kwa nafasi.
-
6:00 - 6:04Unaweza kutumia programu za simu ambazo zinatumia mfumo huu kama vile Anki au Memrise,
-
6:04 - 6:07au unaweza kuandika orodha ya neno katika kijitabu ukitumia njia ya Goldlist,
-
6:07 - 6:10ambayo ni maarufu kwa wanaisimu wengi.
-
6:10 - 6:14Kama huna uhakika ni njia ipi inayofaa na kipi kinachopatikana,
-
6:14 - 6:17angalia chaneli za Youtube na tovuti za wanaisimu
-
6:17 - 6:18kupata hamasa kutoka kwao.
-
6:19 - 6:21Kama inawafaa wao, lazima itakufaa na wewe pia.
-
6:23 - 6:25Kanuni ya tatu ya kufuata
-
6:25 - 6:27ni kutengeneza mfumo katika kujifunza kwako.
-
6:28 - 6:32Wote tupo bize na hakuna aliye na muda wa kujifunza lugha mpya leo.
-
6:32 - 6:36Lakini tunaweza pata muda kama tukipanga mbele kidogo.
-
6:36 - 6:39Unaweza kuamka dakika kumi na tano mapema kabla ya muda wa kawaida wa kuamka?
-
6:39 - 6:42Huo utakuwa muda mzuri wa kuweza kupitia baadhi ya maneno.
-
6:43 - 6:46Unaweza sikiliza kipindi ukiwa unarudi nyumbani wakati unaendesha?
-
6:46 - 6:50Sasa, hiyo itakuwa nzuri kupata uzoefu wa kusikiliza.
-
6:50 - 6:53Kuna vitu vingi tunaweza fanya bila hata ya kupanga muda wa ziada,
-
6:53 - 6:56kama vile kusikiliza kipindi ukiwa unaelekea kazini,
-
6:56 - 6:58au wakati unafanya kazi za nyumbani.
-
6:58 - 7:01Kitu muhimu ni kutengeneza mpango katika kujifunza.
-
7:01 - 7:03"Nitajifunza kuongea kila Jumanne na Alhamisi
-
7:03 - 7:05na rafiki kwa dakika 20.
-
7:06 - 7:10Nitasikiliza video katika Youtube wakati nikipata kifungua kinywa."
-
7:10 - 7:12Kama utatengeneza mfumo katika kujifunza,
-
7:12 - 7:14huna haja ya kutafuta muda wa ziada,
-
7:14 - 7:16kwa sababu itakuwa namna ya maisha yako ya kila siku.
-
7:18 - 7:21Na mwisho, kama unataka kujifunza lugha kwa ufasaha,
-
7:21 - 7:24unahitaji kuwa na subira kidogo.
-
7:25 - 7:27Haiwezekani kujifunza lugha ndani ya miezi miwili,
-
7:27 - 7:31lakini inawezekana kabisa kufanya mabadiliko yanayoonekana katika miezi miwili,
-
7:31 - 7:35kama utajifunza katika kiasi kidogo kidogo kila siku katika namna ambayo unafurahia.
-
7:35 - 7:37Na hakuna kitu ambacho kinatuhamasisha zaidi
-
7:37 - 7:38ya mafanikio yetu.
-
7:39 - 7:41Nakumbuka vizuri wakati
-
7:41 - 7:45nilipoelewa utani wa kwanza kwa Kijerumani nilipokuwa naangalia "Marafiki."
-
7:45 - 7:47Nilifurahia sana na kuhamasika
-
7:47 - 7:50kwamba niliendelea kuangalia sehemu mbili zaidi siku hiyo,
-
7:50 - 7:52na nilivyoendelea kuangalia,
-
7:52 - 7:56Niliendelea kuelewa zaidi, ushindi huu mdogo,
-
7:56 - 8:00na hatua kwa hatua, nilifika katika hatua ambapo ningetumia lugha
-
8:00 - 8:03kwa uhuru na ufasaha kuweza kuelezea chochote.
-
8:03 - 8:04Hii ni hisia ya kusisimua.
-
8:05 - 8:06Siwezi tosheka na hisia hiyo,
-
8:07 - 8:09na ndiyo maana najifunza lugha mpya kila miaka miwili.
-
8:09 - 8:11Kwa hiyo ndiyo siri nzima ya mwanaisimu.
-
8:11 - 8:14Tafuta njia madhubuti ambayo unaweza kuitumia kwa mfumo
-
8:14 - 8:18katika kipindi cha muda fulani katika njia ambayo unafurahia,
-
8:18 - 8:22na hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha ndani ya miezi, na siyo miaka.
-
8:23 - 8:25Sasa, baadhi yenu mnaweza kuwaza,
-
8:25 - 8:27"Ni vizuri sana kufurahia kujifunza lugha,
-
8:27 - 8:30lakini si kwamba nyinyi wanaisimu
-
8:30 - 8:32mna talanta sana na wengi wetu hatuna hiyo talanta?"
-
8:33 - 8:36Hivyo, kuna kitu kimoja sijawaambia kuhusu Benny na Lucas.
-
8:37 - 8:43Benny alikuwa na miaka 11 ya kiselti cha Kiyalandi na miaka mitano ya lugha ya Kijerumani shuleni.
-
8:43 - 8:46Hakuweza kuongea baada ya kuhitimu masomo.
-
8:46 - 8:50Mpaka miaka 21, aliwaza kwamba hakuwa na jeni ya lugha
-
8:50 - 8:53na hakuweza kuongea lugha nyingine.
-
8:53 - 8:56Kisha akaanza kutafuta njia yake ya kujifunza lugha,
-
8:56 - 9:00ambapo ilikuwa ni kuongea na wenyeji wa lugha na kupata mrejesho kutoka kwao,
-
9:00 - 9:04na leo Benny anaweza kwa urahisi kufanya maongezi katika lugha 10.
-
9:05 - 9:08Lucas amejaribu kujifunza Kiingereza shuleni kwa miaka 10.
-
9:08 - 9:11Alikuwa ni moja ya wanafunzi wanaofanya vibaya darasani.
-
9:11 - 9:13Rafiki zake walikuwa wakimtania
-
9:13 - 9:15na kumpa kitabu cha Kirussia kama utani
-
9:15 - 9:19kwa sababu waliamini hawezi kamwe kujifunza lugha hiyo, au lugha yoyote.
-
9:19 - 9:21Na kisha Lucas akaanza kufanya majaribio na njia yake,
-
9:22 - 9:23akitafuta njia yake ya kujifunza,
-
9:25 - 9:29kwa mfano, kwa kupiga soga na watu asiowajua katika Skype.
-
9:29 - 9:31Na katika miaka 10,
-
9:31 - 9:34Lucas anaweza kuongea lugha 11 kwa ufasaha.
-
9:35 - 9:37Je hiyo inaonekana kama miujiza?
-
9:37 - 9:40Sasa, ninaona miujiza kama hii kila siku.
-
9:41 - 9:42Na kama mshauri wa lugha,
-
9:42 - 9:45Nasaidia watu kujifunza lugha wenyewe,
-
9:45 - 9:46na naona hili kila siku.
-
9:46 - 9:50Watu hupata shida kujifunza lugha kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini,
-
9:50 - 9:54na ghafla huchukua hatua ya kujifunza mikononi mwao,
-
9:54 - 9:57kuanza kutumia makala wanazofurahia, njia madhubuti zaidi,
-
9:57 - 9:59au wanaanza kufatilia kujifunza kwao
-
9:59 - 10:02kwamba wanaweza kuridhika na maendeleo yao,
-
10:02 - 10:04na hapo ndipo ghafla
-
10:04 - 10:08kwa maajabu wanatambua kipaji cha lugha ambacho walikuwa wanakosa maisha yao yote.
-
10:09 - 10:12Kwa hiyo kama umejaribu pia kujifunza lugha
-
10:12 - 10:14na ukakata tamaa,
-
10:14 - 10:16na kama huna kipaji cha lugha,
-
10:16 - 10:18jaribu tena.
-
10:18 - 10:21Labda upo karibu kidogo na njia moja ya kuburudika
-
10:21 - 10:23ili kujifunza lugha hiyo kwa ufasaha.
-
10:23 - 10:27Labda upo karibu kuja kuwa mwanaisimu.
-
10:27 - 10:28Asante.
-
10:28 - 10:32(Makofi)
- Title:
- Siri ya kujifunza lugha mpya
- Speaker:
- Lýdia Machová
- Description:
-
Unataka kujifunza lugha mpya lakini unaogopa au hauna uhakika wapi pa kuanzia? Hauhitaji kipaji chochote maalumu au "jeni ya lugha," anasema Lýdia Machová. Katika hotuba hii changamfu, yenye hamasa, anaeleza siri za wanaisimu(watu wanaoongea lugha nyingi) na anashirikisha kanuni nne za kusaidia kufungua kipaji chako kilichojificha cha lugha -- na kufurahia wakati ukifanya hivyo.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 10:45
Shang Li edited Swahili subtitles for The secrets to learning a new language | ||
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for The secrets to learning a new language | ||
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for The secrets to learning a new language | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for The secrets to learning a new language | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The secrets to learning a new language | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for The secrets to learning a new language |