0:00:01.760,0:00:04.656 Napenda kujifunza lugha za kigeni. 0:00:04.680,0:00:08.736 napenda sana kiasi kwamba hujifunza lugha mpya kila baada ya miaka miwili, 0:00:08.760,0:00:10.856 sasa hivi najifunza lugha ya nane. 0:00:10.880,0:00:13.496 Pale watu wanapogundua kuhusu mimi, mara huniuliza, 0:00:13.520,0:00:15.616 "Unafanyaje hivyo? Siri yako ni ipi?" 0:00:15.640,0:00:18.656 Na niwe muwazi, kwa miaka mingi, jibu langu litakuwa, 0:00:18.680,0:00:21.000 "Sifahamu. Napenda tu kujifunza lugha." 0:00:21.720,0:00:23.976 Lakini watu hawakufurahishwa na jibu hilo. 0:00:24.000,0:00:27.976 Walitaka kufahamu kwanini wanatumia miaka kujaribu kuijfunza hata lugha moja, 0:00:28.000,0:00:29.536 kamwe hawafanikiwa unenaji, 0:00:29.560,0:00:32.616 na mimi natokea, nikijifunza lugha moja baada ya nyingine. 0:00:32.640,0:00:34.856 Walitaka kujua siri ya wanaisimu, 0:00:34.880,0:00:36.600 watu wanaoongea lugha nyingi. 0:00:37.400,0:00:38.816 Na hii ilinifanya kushangaa, pia, 0:00:38.840,0:00:41.136 wanaisimu wengine wanafanyaje? 0:00:41.160,0:00:42.656 Kitu gani tulichonacho? 0:00:42.680,0:00:44.616 Na kipi ambacho kinatuwezesha sisi 0:00:44.640,0:00:47.080 kujifunza lugha kwa haraka kuliko watu wengine? 0:00:47.880,0:00:50.720 Niliamua kukutana na watu wengine kama mimi ili kutambua. 0:00:51.760,0:00:53.816 Sehemu nzuri ya kuonana na wanaisimu wengi 0:00:53.840,0:00:56.136 ni katika hafla ambapo mamia ya wapenzi wa lugha 0:00:56.160,0:00:59.016 hukutana pamoja. 0:00:59.040,0:01:02.336 Kuna baadhi ya hafla za wanaisimu ambazo huandaliwa duniani kote, 0:01:02.360,0:01:03.736 na kwa hiyo niliamua kwenda huko 0:01:03.760,0:01:06.200 na kuwauliza wanaisimu kuhusu njia wanazotumia. 0:01:07.200,0:01:09.136 Nilikutana na Benny kutoka Ireland, 0:01:09.160,0:01:13.320 ambaye aliniambia kwamba njia yake ni kuanza kuongea kuanzia siku ya kwanza. 0:01:14.240,0:01:17.136 Hujifunza misemo michache kutoka katika kitabu cha misemo cha wasafiri 0:01:17.160,0:01:18.736 na huenda kukutana na wenyeji wa lugha husika 0:01:18.760,0:01:21.576 na kuanza maongezi nao moja kwa moja. 0:01:21.600,0:01:24.376 Hajali kukosea kuongea hata mara 200 kwa siku, 0:01:24.400,0:01:26.840 kwa sababu hivyo ndivyo anajifunza, ukilinganisha na mrejesho. 0:01:27.480,0:01:30.616 Na kilicho bora ni kwamba, haitaji kusafiri sana leo, 0:01:30.640,0:01:33.576 Sababu kwa urahisi unaweza fanya maongezi na wenyeji wa lugha 0:01:33.600,0:01:36.296 ukiwa umepumzika katika chumba chako, ukitumia tovuti. 0:01:36.320,0:01:38.096 Nilikutana pia na Lucas kutoka Brazil 0:01:38.120,0:01:40.600 ambaye alikuwa na njia ya kuvutia ya kujifunza Kirussia. 0:01:41.200,0:01:46.856 Kiurahisi aliwaalika waongeaji wa lugha ya Kirussia wapatao 100 kama marafiki katika mtandao wake wa Skype, 0:01:46.880,0:01:50.776 na kisha alianza kupiga soga na mmoja wao 0:01:50.800,0:01:52.240 na akaandika "Habari" kwa Kirussia. 0:01:53.000,0:01:55.576 Yule mtu alijibu," Nzuri, hujambo?" 0:01:55.600,0:02:00.056 Lucas alinakili haya maongezi na kuweka katika chumba cha maandishi alipoanza soga na mtu mwingine, 0:02:00.080,0:02:03.656 na mtu alijibu. "Nipo salama, asante, na wewe hujambo?" 0:02:03.680,0:02:06.656 Lucas alinakili tena na kuweka katika soga na mtu wa kwanza, 0:02:06.680,0:02:10.136 na katika njia hii, aliwafanya watu wawili wasiojuana kuwa katika maongezi 0:02:10.160,0:02:11.576 bila kufahamu hilo. 0:02:11.600,0:02:12.856 (Kicheko) 0:02:12.880,0:02:14.776 Si punde alianza kuchapa maneno mwenyewe, 0:02:14.800,0:02:16.936 kwa sababu alikuwa na maongezi kama haya mengi 0:02:16.960,0:02:19.976 kwamba aligundua jinsi gani maongezi ya Kirussia ambavyo kwa kawaida huanza. 0:02:20.000,0:02:22.336 Njia yenye werevu sana, si ndiyo? 0:02:22.360,0:02:26.856 Na kisha nilikutana na mwanaisimu ambaye muda wote huanza kwa kuigiza sauti za lugha, 0:02:26.880,0:02:31.296 na wengine ambao amara zote hujifunza maneno 500 ya mara kwa mara katika lugha, 0:02:31.320,0:02:34.720 na wengine ambao huanza kwa kusoma kitabu cha sarufi. 0:02:35.600,0:02:37.896 Kama ningeuliza wanaisimu mbalimbali mia moja, 0:02:37.920,0:02:41.536 Nilisikia namna mia moja mbalimbali za kujifunza lugha. 0:02:41.560,0:02:45.176 Kila mtu alikuwa na njia tofauti ya kujifunza lugha, 0:02:45.200,0:02:49.080 na wote mwishoni huja na matokeo sawa ya kuongea lugha baadhi kwa ufasaha. 0:02:50.120,0:02:54.416 Na nilikuwa nawasikiliza wanaisimu hawa wakinieleza kuhusu njia zao, 0:02:54.440,0:02:56.736 ghafla ikaniamsha: 0:02:56.760,0:02:59.896 kitu kimoja ambacho wote tunacho 0:02:59.920,0:03:05.456 ni kwamba tumeweza kutafuta namna ya kufurahia mchakato ya kujifunza lugha. 0:03:05.480,0:03:08.256 Na hawa wanaisimu wote walikuwa wanaongelea kuhusu kujifunza lugha 0:03:08.280,0:03:09.536 na ilikuwa inafurahisha sana. 0:03:09.560,0:03:11.136 Ungewaona nyuso zao 0:03:11.160,0:03:13.776 walipokuwa wakinionyesha chati za rangi zikielezea sarufi 0:03:13.800,0:03:16.296 na kadi za maneno zilizotengenezwa kwa uangalifu, 0:03:16.320,0:03:19.336 na takwimu zao kuhusu kujifunza maneno ya lugha kwa kutumia programu ya simu janja, 0:03:19.360,0:03:23.560 au wanavyopenda kupika kutokana na maelezo ya upishi yaliyoandikwa katika lugha ya kigeni. 0:03:24.680,0:03:26.416 Wote wanatumia njia mbalimbali, 0:03:26.440,0:03:30.216 Lakini wanahakikisha ni kitu ambacho binafsi wanapendelea kufanya. 0:03:30.240,0:03:34.136 Nimegundua kwamba hivi ndivyo mimi hujifunza lugha. 0:03:34.160,0:03:37.736 Nilipokuwa najifunza Kispanyola, nilichoshwa na maandishi katika kitabu. 0:03:37.760,0:03:39.496 Namaanisha, nani ambaye anataka kusoma kuhusu Jose 0:03:39.520,0:03:42.656 akiuliza kuhusu uelekeo wa kwenda kituo gari moshi. Sawa? 0:03:42.680,0:03:45.016 Nilitaka kusoma "Harry Porter" badala yake, 0:03:45.040,0:03:47.176 kwa sababu ndicho kilikuwa kitabu nikipendacho sana nikiwa mdogo, 0:03:47.200,0:03:48.856 na nimekisoma mara nyingi. 0:03:48.880,0:03:52.496 Kwa hiyo nilipata tafsiri "Harry Porter" katika lugha ya Kispanyola na nikaanza kusoma, 0:03:52.520,0:03:55.856 na kwa uhakika, sikuelewa chochote kile mwanzoni, 0:03:55.880,0:03:58.096 lakini niliendelea kusoma kwa sababu nilikipenda kitabu, 0:03:58.120,0:04:02.256 na mwishoni mwa kitabu, niliweza kukifatilia bila matatizo yoyote. 0:04:02.280,0:04:04.896 Na jambo sawa lilitokea wakati nikijifunza Kijerumani. 0:04:04.920,0:04:08.216 Niliamua kuangalia "Marafiki," ucheshi ninaopendelea, kwa Kijerumani, 0:04:08.240,0:04:11.336 na tena, mwanzoni ilikuwa upuuzi tu. 0:04:11.360,0:04:14.536 Sikuelewa ni wapi neno moja limeishia na lingine lilipoanzia, 0:04:14.560,0:04:17.216 lakini niliendelea kuangalia kila siku kwa sababu ilikuwa ni "Marafiki." 0:04:17.240,0:04:19.616 Naweza kuangalia katika lugha yoyote. Napenda sana. 0:04:19.640,0:04:21.656 Na baada sehemu ya pili au ya tatu, 0:04:21.680,0:04:24.040 kiukweli, maongezi yalianza kuleta maana. 0:04:25.080,0:04:28.136 Nilitambua hili baada ya kukutana na wanaisimu wengine. 0:04:28.160,0:04:29.736 Sisi si wenye talanta 0:04:29.760,0:04:32.176 na hatuna njia za kukatiza katika kujifunza lugha. 0:04:32.200,0:04:36.016 Tumeweza kutafuta njia ya kufurahia mchakato, 0:04:36.040,0:04:39.416 namna ya kubadili usomaji wa lugha kutoka kama somo la shule lisilofurahisha 0:04:39.440,0:04:42.640 hadi katika shughuli ya kuvutia ambayo hutaona shida kuifanya kila siku. 0:04:43.520,0:04:45.696 Kama hupendelei kuandika maneno kwenye karatasi, 0:04:45.720,0:04:47.416 unaweza mara zote kuyachapa kwenye programu ya simu. 0:04:47.440,0:04:50.256 Kama hupendelei kusikiliza vitabu vinavyochosha, 0:04:50.280,0:04:54.576 tafuta video zinazovutia katika Youtube au katika vipindi vya lugha. 0:04:54.600,0:04:56.296 Kama wewe ni mtu unayependelea upekee 0:04:56.320,0:04:59.336 na hauwezi kuwaza ni namna gani utaweza ongea na wenyeji wa lugha moja kwa moja, 0:04:59.360,0:05:01.696 unaweza kujifunza kujiongelesha mwenyewe. 0:05:01.720,0:05:04.296 Unaweza kuongea na nafsi yako ukiwa katika chumba chako, 0:05:04.320,0:05:07.216 ukieleza mipango yako ya mwisho wa wiki, siku yako ilikwendaje, 0:05:07.240,0:05:09.376 au hata kupiga picha zisizo na mpangilio katika simu yako 0:05:09.400,0:05:13.136 na kuelezea kuhusu picha hiyo kwa rafiki yako wa kufikirika. 0:05:13.160,0:05:15.656 Hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha, 0:05:15.680,0:05:18.536 na habari njema ni kwamba, inapatikana kwa mtu yoyote 0:05:18.560,0:05:21.240 nani ambaye yuko tayari kujifunza katika mikono yake. 0:05:22.520,0:05:24.616 Hivyo kukutana na wanaisimu wengine kulinisaidia kutambua 0:05:24.640,0:05:27.656 kwamba ni muhimu sana kupata burudani 0:05:27.680,0:05:29.776 katika mchakato wa kujifunza lugha, 0:05:29.800,0:05:32.840 lakini pia furaha yenyewe pekee haitoshi. 0:05:33.680,0:05:36.416 Kama unataka kuweza kufikia ufasaha katika lugha ya kigeni, 0:05:36.440,0:05:38.920 utahitajika kutumia kanuni tatu zaidi. 0:05:39.760,0:05:42.360 Kwanza, unahitaji njia zilizo bora. 0:05:43.160,0:05:46.576 Ukijaribu kukumbuka listi ya maneno kwa ajili ya mtihani wa kesho, 0:05:46.600,0:05:48.976 maneno yatahifadhiwa katika kumbukumbu yako ya muda mfupi 0:05:49.000,0:05:50.905 na utayasahau baada ya siku chache. 0:05:51.400,0:05:54.336 Kama, hata hivyo, unataka kukaa na maneno kwa muda mrefu, 0:05:54.360,0:05:57.296 unahitaji kuyarudia katika kipindi cha siku chache 0:05:57.320,0:05:59.536 ukifanya kitu kinachofahamika kama kurudia kwa nafasi. 0:05:59.560,0:06:03.816 Unaweza kutumia programu za simu ambazo zinatumia mfumo huu kama vile Anki au Memrise,[br] 0:06:03.840,0:06:07.176 au unaweza kuandika orodha ya neno katika kijitabu ukitumia njia ya Goldlist, 0:06:07.200,0:06:09.896 ambayo ni maarufu kwa wanaisimu wengi. 0:06:09.920,0:06:13.656 Kama huna uhakika ni njia ipi inayofaa na kipi kinachopatikana, 0:06:13.680,0:06:16.696 angalia chaneli za Youtube na tovuti za wanaisimu 0:06:16.720,0:06:18.496 kupata hamasa kutoka kwao. 0:06:18.520,0:06:21.440 Kama inawafaa wao, lazima itakufaa na wewe pia. 0:06:22.840,0:06:24.816 Kanuni ya tatu ya kufuata 0:06:24.840,0:06:27.000 ni kutengeneza mfumo katika kujifunza kwako. 0:06:27.720,0:06:31.936 Wote tupo bize na hakuna aliye na muda wa kujifunza lugha mpya leo. 0:06:31.960,0:06:35.736 Lakini tunaweza pata muda kama tukipanga mbele kidogo. 0:06:35.760,0:06:39.176 Unaweza kuamka dakika kumi na tano mapema kabla ya muda wa kawaida wa kuamka? 0:06:39.200,0:06:42.496 Huo utakuwa muda mzuri wa kuweza kupitia baadhi ya maneno. 0:06:42.520,0:06:46.256 Unaweza sikiliza kipindi ukiwa unarudi nyumbani wakati unaendesha? 0:06:46.280,0:06:49.736 Sasa, hiyo itakuwa nzuri kupata uzoefu wa kusikiliza. 0:06:49.760,0:06:53.216 Kuna vitu vingi tunaweza fanya bila hata ya kupanga muda wa ziada, 0:06:53.240,0:06:55.896 kama vile kusikiliza kipindi ukiwa unaelekea kazini, 0:06:55.920,0:06:57.576 au wakati unafanya kazi za nyumbani. 0:06:57.600,0:07:00.896 Kitu muhimu ni kutengeneza mpango katika kujifunza. 0:07:00.920,0:07:03.416 "Nitajifunza kuongea kila Jumanne na Alhamisi 0:07:03.440,0:07:05.496 na rafiki kwa dakika 20. 0:07:05.520,0:07:09.936 Nitasikiliza video katika Youtube wakati nikipata kifungua kinywa." 0:07:09.960,0:07:12.096 Kama utatengeneza mfumo katika kujifunza, 0:07:12.120,0:07:14.016 huna haja ya kutafuta muda wa ziada, 0:07:14.040,0:07:16.480 kwa sababu itakuwa namna ya maisha yako ya kila siku. 0:07:17.880,0:07:21.096 Na mwisho, kama unataka kujifunza lugha kwa ufasaha, 0:07:21.120,0:07:23.840 unahitaji kuwa na subira kidogo. 0:07:24.600,0:07:27.336 Haiwezekani kujifunza lugha ndani ya miezi miwili, 0:07:27.360,0:07:31.256 lakini inawezekana kabisa kufanya mabadiliko yanayoonekana katika miezi miwili, 0:07:31.280,0:07:35.016 kama utajifunza katika kiasi kidogo kidogo kila siku katika namna ambayo unafurahia. 0:07:35.040,0:07:37.176 Na hakuna kitu ambacho kinatuhamasisha zaidi 0:07:37.200,0:07:38.440 ya mafanikio yetu. 0:07:39.120,0:07:41.016 Nakumbuka vizuri wakati 0:07:41.040,0:07:44.720 nilipoelewa utani wa kwanza kwa Kijerumani nilipokuwa naangalia "Marafiki." 0:07:45.280,0:07:47.136 Nilifurahia sana na kuhamasika 0:07:47.160,0:07:50.176 kwamba niliendelea kuangalia sehemu mbili zaidi siku hiyo, 0:07:50.200,0:07:51.936 na nilivyoendelea kuangalia, 0:07:51.960,0:07:56.176 Niliendelea kuelewa zaidi, ushindi huu mdogo, 0:07:56.200,0:07:59.656 na hatua kwa hatua, nilifika katika hatua ambapo ningetumia lugha 0:07:59.680,0:08:02.536 kwa uhuru na ufasaha kuweza kuelezea chochote. 0:08:02.560,0:08:04.080 Hii ni hisia ya kusisimua. 0:08:04.800,0:08:06.496 Siwezi tosheka na hisia hiyo, 0:08:06.520,0:08:09.336 na ndiyo maana najifunza lugha mpya kila miaka miwili. 0:08:09.360,0:08:11.416 Kwa hiyo ndiyo siri nzima ya mwanaisimu. 0:08:11.440,0:08:14.296 Tafuta njia madhubuti ambayo unaweza kuitumia kwa mfumo 0:08:14.320,0:08:17.616 katika kipindi cha muda fulani katika njia ambayo unafurahia, 0:08:17.640,0:08:21.520 na hivi ndivyo wanaisimu hujifunza lugha ndani ya miezi, na siyo miaka. 0:08:23.160,0:08:24.776 Sasa, baadhi yenu mnaweza kuwaza, 0:08:24.800,0:08:27.136 "Ni vizuri sana kufurahia kujifunza lugha, 0:08:27.160,0:08:29.696 lakini si kwamba nyinyi wanaisimu 0:08:29.720,0:08:32.320 mna talanta sana na wengi wetu hatuna hiyo talanta?" 0:08:33.320,0:08:36.400 Hivyo, kuna kitu kimoja sijawaambia kuhusu Benny na Lucas. 0:08:37.159,0:08:42.976 Benny alikuwa na miaka 11 ya kiselti cha Kiyalandi na miaka mitano ya lugha ya Kijerumani shuleni. 0:08:43.000,0:08:46.216 Hakuweza kuongea baada ya kuhitimu masomo. 0:08:46.240,0:08:50.416 Mpaka miaka 21, aliwaza kwamba hakuwa na jeni ya lugha 0:08:50.440,0:08:52.856 na hakuweza kuongea lugha nyingine. 0:08:52.880,0:08:55.816 Kisha akaanza kutafuta njia yake ya kujifunza lugha, 0:08:55.840,0:08:59.696 ambapo ilikuwa ni kuongea na wenyeji wa lugha na kupata mrejesho kutoka kwao, 0:08:59.720,0:09:03.680 na leo Benny anaweza kwa urahisi kufanya maongezi katika lugha 10. 0:09:05.120,0:09:08.416 Lucas amejaribu kujifunza Kiingereza shuleni kwa miaka 10. 0:09:08.440,0:09:11.056 Alikuwa ni moja ya wanafunzi wanaofanya vibaya darasani. 0:09:11.080,0:09:12.696 Rafiki zake walikuwa wakimtania 0:09:12.720,0:09:15.336 na kumpa kitabu cha Kirussia kama utani 0:09:15.360,0:09:19.096 kwa sababu waliamini hawezi kamwe kujifunza lugha hiyo, au lugha yoyote. 0:09:19.120,0:09:21.496 Na kisha Lucas akaanza kufanya majaribio na njia yake, 0:09:21.520,0:09:23.320 akitafuta njia yake ya kujifunza, 0:09:24.520,0:09:28.696 kwa mfano, kwa kupiga soga na watu asiowajua katika Skype. 0:09:28.720,0:09:30.536 Na katika miaka 10, 0:09:30.560,0:09:33.880 Lucas anaweza kuongea lugha 11 kwa ufasaha. 0:09:35.000,0:09:36.560 Je hiyo inaonekana kama miujiza? 0:09:37.440,0:09:40.040 Sasa, ninaona miujiza kama hii kila siku. 0:09:40.760,0:09:42.096 Na kama mshauri wa lugha, 0:09:42.120,0:09:44.536 Nasaidia watu kujifunza lugha wenyewe, 0:09:44.560,0:09:45.856 na naona hili kila siku. 0:09:45.880,0:09:50.056 Watu hupata shida kujifunza lugha kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini, 0:09:50.080,0:09:53.936 na ghafla huchukua hatua ya kujifunza mikononi mwao, 0:09:53.960,0:09:57.256 kuanza kutumia makala wanazofurahia, njia madhubuti zaidi, 0:09:57.280,0:09:59.096 au wanaanza kufatilia kujifunza kwao 0:09:59.120,0:10:02.056 kwamba wanaweza kuridhika na maendeleo yao, 0:10:02.080,0:10:04.016 na hapo ndipo ghafla 0:10:04.040,0:10:08.240 kwa maajabu wanatambua kipaji cha lugha ambacho walikuwa wanakosa maisha yao yote. 0:10:09.480,0:10:11.656 Kwa hiyo kama umejaribu pia kujifunza lugha 0:10:11.680,0:10:14.096 na ukakata tamaa, 0:10:14.120,0:10:16.376 na kama huna kipaji cha lugha, 0:10:16.400,0:10:17.936 jaribu tena. 0:10:17.960,0:10:20.816 Labda upo karibu kidogo na njia moja ya kuburudika 0:10:20.840,0:10:22.602 ili kujifunza lugha hiyo kwa ufasaha. 0:10:22.960,0:10:26.896 Labda upo karibu kuja kuwa mwanaisimu. 0:10:26.920,0:10:28.136 Asante. 0:10:28.160,0:10:32.360 (Makofi)