< Return to Video

Number grid | Counting | Early Math | Khan Academy

  • 0:01 - 0:03
    Lengo la video hii ni kuandika,
  • 0:03 - 0:08
    namba zote kwa mpangilio
    kutoka sifuri mpaka 100.
  • 0:08 - 0:10
    Hivyo nitaandika kwa
    njia ya kuvutia zaidi, njia
  • 0:10 - 0:12
    ambayo labda itaruhusu
    sisi kuona baadhi ya chati
  • 0:12 - 0:14
    katika namba zenyewe.
  • 0:14 - 0:20
    Hebu tuanze, tunaanza na sifuri, moja, mbili,
  • 0:20 - 0:30
    tatu, nne, tano, sita,
    saba. nane, na tisa,
  • 0:30 - 0:32
    bila shaka tunajua
    namba inayofuata ni 10,
  • 0:32 - 0:35
    ambayo ninaweza kuiandika
    lakini badala ya kufanya hivyo,
  • 0:35 - 0:38
    nitakwenda kunakili na kuyaweka haya yote kama yalivyo.
  • 0:38 - 0:44
    Hivyo nanakili tuone nini kitatokea.
  • 0:44 - 0:47
    Hivyo kama nikifanya hivyo, hii itatusaidiaje?
  • 0:47 - 0:49
    Sawa tunajua namba inayofuatia ni 10,
  • 0:49 - 0:50
    ambayo njia moja ya kuifikiria.
  • 0:50 - 0:53
    Moja ikifuatiwa na sifuri.
  • 0:53 - 0:54
    Ni namba gani inafuata baada ya hiyo?
  • 0:54 - 0:57
    Vizuri ni 11, ambayo ni
    moja ikifuatiwa na moja.
  • 0:57 - 0:58
    Ni namba gani inafuatia baada ya hiyo?
  • 0:58 - 1:00
    Vizuri ni 12, ambayo ni
    moja ikifuatiwa na mbili,
  • 1:00 - 1:08
    na kisha 13, 14, 15, 16, 17, 18, na 19.
  • 1:08 - 1:10
    Vizuri hii inapendeza.
  • 1:10 - 1:13
    Huu mstari wa namba unaofuata kuanzia 10-19
  • 1:13 - 1:15
    unaonekana tu kama ule wa kwanza,
  • 1:15 - 1:17
    hivyo tarakimu ya 2 ni sawa katika njano,
  • 1:17 - 1:20
    lakini basi niliongeza namaba moja ya zambarau kwa mbele yake.
  • 1:20 - 1:23
    Na njia moja ya kufikiri juu yake ni, kila moja ya namba hizi,
  • 1:23 - 1:27
    namba moja ya zamabarau niliyoiongeza, iliwakilisha makumi.
  • 1:27 - 1:31
    Hivyo 11 inaweza kutazamwa kama 10 jumlisha moja,
  • 1:31 - 1:35
    12 inaweza kutazamwa kama 10 jumlisha mbili.
  • 1:35 - 1:38
    Hebu tuone kama hii inaendelea kufanya kazi.
  • 1:38 - 1:41
    Basi hebu tuchukue mstari mwingine wa namba.
  • 1:41 - 1:43
    Basi hebu tuchukue mstari mwingine, mstari wangu wa awali,
  • 1:43 - 1:46
    na je, napata nini baada ya 19?
  • 1:46 - 1:51
    Vizuri bila shaka baada ya 19 tunapata 20.
  • 1:51 - 2:04
    Hivyo 20, mbili na sifuri na kisha 21,
    22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29.
  • 2:04 - 2:06
    Nadhani unaweza kuanza
    kuona mfano hapa.
  • 2:06 - 2:08
    Je, tutafanya nini kwa mstari unaofuata?
  • 2:08 - 2:11
    Vizuri sasa tuko kwenye 30.
  • 2:11 - 2:15
    Hivyo namba ya kwanza 30 ni 30 jumlisha sifuri,
  • 2:15 - 2:19
    30 jumlisha moja, 30 jumlisha mbili,
    30 jumlisha tatu ambayo ni 33,
  • 2:19 - 2:26
    34, 35, 36, 37, 38, 39.
  • 2:26 - 2:29
    Kwa hiyo kwa kufanya hivyo tu nadhani tayari umeshaona mfano.
  • 2:29 - 2:33
    Tarakimu upande wa kulia zitaendelea kutoka sifuri, moja, mbili,
  • 2:33 - 2:34
    tatu, nne, tano, sita, saba,
  • 2:34 - 2:37
    nane, tisa, na kisha
    tarakimu upande wa kushoto,
  • 2:37 - 2:40
    kama uko kati ya 10 na 19,
    utakuwa na moja daima.
  • 2:40 - 2:42
    Kama uko kati ya 20 na 29,
    utakuwa na mbili daima.
  • 2:42 - 2:47
    Kama uko kati ya 30 na 39, utakuwa na tatu daima.
  • 2:47 - 2:48
    Sasa nawezaje kukamilisha hii
  • 2:48 - 2:51
    kwenda haraka mapaka 99?
  • 2:51 - 2:54
    Vizuri, hebu tufanye hivyo, kwa hiyo itakuwa 40 yangu,
  • 2:54 - 2:57
    Bado sijaiandika.
  • 2:57 - 3:02
    Hiyo itakuwa 50 yangu,
    hii itakuwa 60 yangu,
  • 3:04 - 3:13
    70, 80, na kisha nina
    90 hapa mbele yangu.
  • 3:13 - 3:19
    Na hivyo hii hapa tayari tulishasema
    hii itakwenda kuwa 40 yangu,
  • 3:19 - 3:24
    hii itakwenda kuwa 50 yangu, hii itakwenda kuwa,
  • 3:24 - 3:28
    Ninajaribu kuhakikisha kwamba
    ninatumia rangi zangu zote, 60 yangu,
  • 3:28 - 3:33
    hii inakwenda kuwa 70 yangu,
    na basi nina 80 yangu,
  • 3:33 - 3:39
    na kisha bila shaka nina,ngoja nitumie rangi ambayo,
  • 3:39 - 3:43
    Nitaitumia tena magenta, nitakuwa na 90 yangu.
  • 3:43 - 3:45
    Basi nini kitatokea kama nikiamua tu kuchukua hii,
  • 3:45 - 3:48
    hivyo basi acha tu kilichoko mbele yangu,
  • 3:48 - 3:50
    na kunakili kama ilivyo na kuiweka hapo.
  • 3:50 - 3:53
    Hivyo nakili kama ilivyo, na wacha niiweke hapo.
  • 3:53 - 3:58
    Hivyo sasa nina 41, 51, 61, 71, 81, na 91.
  • 3:58 - 4:03
    Sasa siwezi kufanya hivyo hapa,
    42, 52, 62, 72, 82, na 92.
  • 4:03 - 4:07
    Na ninaweza kufanya hivyo kwa kila moja ya hizi, kwa kila moja ya hizi sasa.
  • 4:07 - 4:12
    Ni hivyo , sasa, 44,
    54, 64, 74, 84, na 94.
  • 4:12 - 4:16
    Na hivyo wakati mimi nikifanya hivyo
    tunaona mfano kamili.
  • 4:16 - 4:20
    Tunaona mfano kamili
    na nimemaliza.
  • 4:20 - 4:29
    Nimemaliza kujaza
    namba zangu kutoka sifuri mpaka 99.
  • 4:29 - 4:34
    49, 59,69,79,89,99 na kama
    tunataka tu kujisikia vizuri,
  • 4:34 - 4:41
    tunaweza kuandika, tunaweza kuandika 100,
  • 4:41 - 4:45
    100 mbele yetu hapa.
  • 4:45 - 4:47
    Na utaona mfano
    bado unaweza kutumika, tulianzia kutoka moja
  • 4:47 - 4:50
    mbili, tatu, nne, tano,
    sita, saba, nane, tisa,
  • 4:50 - 4:55
    na sasa tuna 10 ikifuatiwa na sifuri.
  • 4:55 - 4:57
    Vizuri sana.
Title:
Number grid | Counting | Early Math | Khan Academy
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
Khan Academy
Duration:
04:58

Swahili subtitles

Revisions