Ndugu Chris Akijibu Maswali ya PAPO KWA HAPO!
-
0:00 - 0:03Ikiwa uko kwenye uhusiano na mtu na moyo wako unafadhaika
-
0:03 - 0:07na unaendelea kusema, 'Sina hakika',
-
0:07 - 0:10Ningependekeza kwako, yeye sio 'yule' - yeye sio 'yule'.
-
0:14 - 0:20Hivi sasa, nataka kukupa fursa ya kuuliza maswali yoyote.
-
0:20 - 0:24Ikiwa una swali la kuuliza, onyesha tu kwa kuinua mkono wako.
-
0:24 - 0:29Ningependa kujua - tunapokuwa na karama na talanta nyingi,
-
0:29 - 0:33tunawezaje kujua kusudi letu mahususi ni nini?
-
0:33 - 0:44Sawa. Kwa hivyo kwako, kaka, tujizungumzie wenyewe. Ni talanta gani unayozungumzia?
-
0:44 - 0:48Muziki.
-
0:48 - 0:52Sawa. Muziki - ni mfano mzuri.
-
0:52 - 1:01Tunajua kutoka katika Biblia kwamba muziki ni zawadi kutoka kwa Mungu.
-
1:01 - 1:06Lakini angalia jamii leo.
-
1:06 - 1:19Watu wengi wanatumia zawadi wanayopokea kutoka kwa Mungu kumtukuza shetani.
-
1:19 - 1:23Ndugu, ikiwa Mungu amekupa kipawa katika eneo la muziki - vizuri ajabu!
-
1:23 - 1:27Fanya muziki kwa utukufu wa Mungu, sio kusherehekea ulimwengu,
-
1:27 - 1:35sio kusherehekea pesa, tamaa au mambo haya yote ya kipumbavu na ya bure. Kwa Mungu!
-
1:55 - 2:11Ikiwa unatumia karama yako kwa utukufu wa Mungu, Mungu ataendelea kuizidisha.
-
2:11 - 2:27Wala hatakupeleka mahali ambapo tabia yako haitastahimili kupamudu.
-
2:34 - 2:42Kwa sababu watu wengi leo - wanaweza kufikia mahali fulani na vipawa
-
2:42 - 2:47lakini wanaanguka haraka kwa sababu hawana tabia.
-
3:02 - 3:07Ikiwa umejaliwa kipawa
-
3:07 - 3:20na ukagundua kuwa haupo mahali unapotarajia kuwa na kipawa ulichonacho,
-
3:20 - 3:37pengine Mungu anakuhifadhi ili uifanyie kazi tabia yako.
-
3:37 - 3:51Zawadi huanza; tabia hukamilisha.
-
3:51 - 3:57Kwa hiyo, asante ndugu. Mungu akubariki! Ni swali zuri.
-
3:57 - 4:00Habari za mchana. Jina langu ni Dayron.
-
4:00 - 4:09Ukiwa kama kijana aliyekulia chini ya ulezi wa Nabii TB Joshua
-
4:09 - 4:15unaweza kutupa mifano ya jinsi ya kuwa na uhusiano wa ndani zaidi na Roho Mtakatifu,
-
4:15 - 4:22kufikia kiwango ambacho Mungu alikuwa akitenda kazi katika SCOAN?
-
4:22 - 4:27SAWA! Ni swali zuri.
-
4:27 - 4:38Nilisema kitu jana, kwamba safari yangu ni tofauti na yako.
-
4:38 - 4:47Na imani haijikiti katika kuiga.
-
4:47 - 5:05Inategemea Neno la Mungu mioyoni mwetu na usadikisho unaotokana na hilo.
-
5:05 - 5:15Kwa hiyo, naweza kukutajia leo baadhi ya mambo mahususi ambayo nilifanya.
-
5:15 - 5:21Lakini mimi si wewe na wewe si mimi.
-
5:21 - 5:28Unahitaji kujua, kupitia Neno la Mungu, kile anachotaka ufanye katika hali yako,
-
5:28 - 5:32kulingana na wito wako katika maisha.
-
5:45 - 5:53Lakini naweza kukupa baadhi ya kanuni
-
5:53 - 6:05ambazo inaweza kusaidia kila mtu, bila kujali Mungu anataka ufanye nini.
-
6:05 - 6:08nitakupa moja.
-
6:08 - 6:21Unapoamka asubuhi, mtu wa kwanza unayepaswa kumsalimia ni Mungu.
-
6:21 - 6:42Wengi wetu leo tukiamka asubuhi kitu cha kwanza kukisalimia ni simu zetu.
-
6:42 - 6:53Ikiwa unaweza kuanza siku yako kwa kupiga magoti katika maombi,
-
6:53 - 7:02unaanza siku kwenye msingi sahihi.
-
7:02 - 7:11Nabii TB Joshua aliishi maisha ya maombi.
-
7:11 - 7:23Hatuzungumzii juu ya maombi ya Jumapili au wakati wa ibada.
-
7:23 - 7:32Aliishi maisha ya maombi kila siku.
-
7:32 - 7:38Alisema, “Nilitunza kina cha uhusiano wangu na Mungu
-
7:38 - 7:42na Yesu alisimamia upana wa mafanikio yangu.”
-
7:57 - 8:10Kwa hivyo, watu wa Mungu, hakuna fomula maalum linapokuja suala la ukuaji wa kiroho.
-
8:10 - 8:21Ikiwa unataka kujenga uhusiano wako na Mungu, lazima uwe tayari kutoa wakati mzuri.
-
8:31 - 8:36Ni maisha ya kujitolea.
-
8:36 - 8:40Kwa sababu kutoa wakati huo,
-
8:40 - 8:48kuna maeneo mengine ya maisha yako utalazimika kuyatoa dhabihu.
-
8:48 - 8:54Lakini nawaambieni, chochote mtakachopoteza kwa ajili ya Mungu,
-
8:54 - 9:02utapata mara elfu.
-
9:02 - 9:13Kwa hiyo, asante, ndugu. Nimekupa moja tu lakini ni kitu cha wewe kujilisha.
-
9:13 - 9:17Ok, hebu sikia kutoka kwa ndugu yetu hapa.
-
9:17 - 9:21Jina langu ni Diolio na nina umri wa miaka 24.
-
9:21 - 9:27Swali langu ni - ungetoa ushauri gani kwako mwenyewe,
-
9:27 - 9:32pamoja na uzoefu wako katika Bwana, kama ungelikuwa na umri wa miaka 24.
-
9:32 - 9:42Mimi bado ni kijana; Mimi sio mzee hivyo!
-
9:42 - 9:47Nina umri wa miaka 35.
-
9:47 - 9:53Kwa hivyo, najiona bado ni kijana.
-
9:53 - 10:02Tuna vishawishi vingi sana vinavyotuzunguka.
-
10:02 - 10:09Lakini ushawishi bora ni Roho Mtakatifu.
-
10:09 - 10:13Ikiwa kuna kitu ningefanya tofauti,
-
10:13 - 10:20ingekuwa kutumia wakati mwingi zaidi kutafuta uhusiano wangu na Mungu -
-
10:20 - 10:24hata muda zaidi katika maombi, hata muda zaidi katika Neno,
-
10:24 - 10:32hata muda zaidi katika uwepo wa Mungu kwa sababu haya ni mambo ambayo thamani yake haipimiki.
-
10:53 - 11:08Ikiwa kitu kina thamani isiyopimika, unapaswa kuwa tayari kulipa gharama yoyote kwa hicho.
-
11:08 - 11:21Yesu alisema, 'Mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate.'
-
11:21 - 11:34Lipa gharama yoyote ili kuujenga uhusiano wako na Kristo.
-
11:34 - 11:40Sawa, tunataka kusikia kutoka kwa dada. Asante, dada.
-
11:40 - 11:44Baraka. Jina langu ni Yunet.
-
11:44 - 11:50Ninawezaje kubaki katika upendo na hofu ya Mungu?
-
11:50 - 11:54Kwa sababu imekuwa ngumu sana kwangu.
-
11:54 - 12:02Kwa hiyo, hebu tukuulize wewe, dada. Ukijichunguza, ni mambo gani hayo ambayo
-
12:02 - 12:06yanaathiri upendo wako kwa Mungu au hofu yako ya Mungu.
-
12:06 - 12:07Taja tu lolote kati ya mambo hayo.
-
12:17 - 12:22Tamaa na hasira.
-
12:22 - 12:31Kwa hiyo, jana, kwa neema ya Mungu, niliombea watu ukombozi.
-
12:31 - 12:35Ukombozi unamaanisha kung'oa kitu chochote cha kiroho
-
12:35 - 12:39ambacho kinakusukuma kufanya jambo kinyume na mapenzi yako.
-
12:52 - 13:07Sasa umekombolewa, una chaguo la kusema ndiyo au hapana.
-
13:07 - 13:12Usiwe na haraka sana kupiga makofi.
-
13:12 - 13:20Kwa sababu ukombozi hautaondoa majaribu.
-
13:20 - 13:29Na kwa kweli, ukombozi utaongeza majaribu.
-
13:29 - 13:35Kwa sababu shetani hataki uwe huru.
-
13:35 - 13:48Ndio maana lazima uwe umaanishe katika uhusiano wako na Mungu ili kudumisha kile unachopokea.
-
13:48 - 13:52Kwa hiyo, hebu tuzungumze kuhusu tamaa.
-
13:52 - 14:08Watu wengi leo wanamlaumu shetani kwa kuingia kwenye milango wanayoiacha wazi kwake.
-
14:08 - 14:19Wewe ndiye uliyemfungulia mlango na unashangaa anapoingia na kushambulia.
-
14:19 - 14:25Unamjaribu shetani ili akujaribu.
-
14:25 - 14:30'Mungu, niokoe kutoka kwenye roho ya tamaa' - lakini angalia simu yako.
-
14:30 - 14:33Picha nyingi kwenye simu yako, ikiwa utaniuliza niangalie -
-
14:33 - 14:34ungetaka kuzifuta.
-
14:53 - 15:02Kwa hivyo, ninachosema kwa dada yangu ni kwamba ikiwa unatambua maeneo ya maisha yako
-
15:02 - 15:06ambayo yanaathiri uhusiano wako na Mungu,
-
15:06 - 15:14kutambua maeneo hayo lazima sasa yakulete mahali pa kujitoa kwa kina zaidi kwa Mungu
-
15:14 - 15:16kuyashinda majaribu hayo.
-
15:36 - 15:43Tukijichunguza kwa dhati,
-
15:43 - 15:54sababu ya kutokuwa na mahusiano ya kudumu na Mungu
-
15:54 - 16:01haipo mbali sana na sisi wenyewe.
-
16:01 - 16:06Kwa hivyo, jibu liko mikononi mwako.
-
16:06 - 16:10Ukipokea ujumbe uliopokea katika mkutano huu,
-
16:10 - 16:25umeandaliwa kudumisha hofu ya Mungu.
-
16:25 - 16:28Asante.
-
16:28 - 16:31Jina langu ni Mario na nina umri wa miaka 27.
-
16:31 - 16:35Nina maswali mawili yanayohusiana.
-
16:35 - 16:49Kwanza, kuna mwelekeo wa kawaida wa kufikiri kwamba ili kufanikiwa, lazima uoe kwa gharama yoyote.
-
16:49 - 16:56Hata hivyo, tumeona katika maisha yako kwamba kulikuwa na mchakato
-
16:56 - 17:03na Mungu akiwa ni sehemu muhimu zaidi, kwa wakati ufaao, Alimleta mtu sahihi.
-
17:03 - 17:13Nini kinapaswa kuwa lengo letu kama vijana tukiwa na Mungu akiwa sehemu muhimu zaidi ya maisha yetu?
-
17:13 - 17:21kuwa na imani kuwa ni mtu sahihi anayekuja na mwenye nia sahihi?
-
17:21 - 17:29Pili, tunawezaje kujua kama wito wetu haujumuishi ndoa?
-
17:29 - 17:32Sawa. Asante kwa swali.
-
17:32 - 17:48Kwa hivyo, kwanza kabisa, wacha niseme kwa kila mtu - huyu ni mke wangu.
-
17:48 - 17:59Ninaweza kutoa ushauri juu ya suala hili kutokana na uzoefu wa vitendo sasa.
-
17:59 - 18:18Nilifikia wakati nilijiambia, 'Ikiwa sitaoa, nimeridhika.'
-
18:18 - 18:22Na nilipofika mahali pa kuridhika.
-
18:22 - 18:33suala la ndoa halikuwa mzigo tena.
-
18:33 - 18:54Na wakati haukuwa mzigo tena, Mungu alinipa mke wangu kutoka Mbinguni.
-
18:54 - 18:59Kwa nini nasema hivi?
-
18:59 - 19:08Ikiwa unatafuta ndoa kuliko Mungu,
-
19:08 - 19:19unaweza kuingia katika ndoa ambayo itaathiri uhusiano wako na Mungu.
-
19:19 - 19:30Kwa hiyo, suala la ndoa ni zaidi kuhusu ukomavu.
-
19:30 - 19:37Ikiwa umekomaa kiroho
-
19:37 - 19:47na wakati ulioamriwa na Mungu umefika wa wewe kuoa.
-
19:47 - 20:00kutakuwa na makubaliano ya moyo sambamba na kutafuta kusudi.
-
20:00 - 20:02Angalia, tunapozungumza juu ya makubaliano ya moyo,
-
20:02 - 20:06huhitaji mtu mwingine yeyote kukuthibitishia; unajua!
-
20:12 - 20:16Ikiwa uko kwenye uhusiano na mtu na moyo wako unafadhaika
-
20:16 - 20:20na unaendelea kusema, 'Sina hakika',
-
20:20 - 20:24Ningependekeza kwako, yeye sio 'yule' - yeye sio 'yule'.
-
20:36 - 20:40Mungu anazungumza na mioyo yetu.
-
20:40 - 20:53Hatakuongoza kwenye uhusiano ambao utaathiri maisha yako vibaya.
-
20:53 - 20:58Kwa hivyo, ikiwa uko mahali pazuri na Mungu,
-
20:58 - 21:02na wakati wa Mungu unawadia kwako kuoa,
-
21:02 - 21:14Roho wa Mungu atashuhudia pamoja na roho yako.
-
21:14 - 21:21Kwa haraka, nitawashikirisha hadithi fupi.
-
21:21 - 21:30Mungu alipoweka moyoni mwangu kuongea na Allison,
-
21:30 - 21:44ndani ya dakika tatu, nilitoka katika kusema hisia zilizokuwa moyoni mwangu
-
21:44 - 21:48hadi kusema, 'Je, utanioa?'
-
21:48 - 21:53Dakika tatu!
-
21:53 - 22:04Sasa, nataka kusisitiza kwamba sisemi kwamba namna ilivyotokea kwangu itakuwa sawa nanyi nyote.
-
22:04 - 22:13Ninachosema ni kwamba wakati Mungu anapozungumza na moyo wako, utajua.
-
22:13 - 22:23Kwa hivyo, wasiwasi wako unapaswa kuwa mahali sahihi na Mungu.
-
22:23 - 22:27Unapokuwa mahali sahihi na Mungu
-
22:27 - 22:37na wakati wake umefika wa wewe kuoa, itatokea kwa hiari yake.
-
22:37 - 22:42Na kwa kuzingatia swali la ndugu yetu, ikiwa si mapenzi ya Mungu uoe,
-
22:42 - 22:46utaendelea na safari yako kwa kuridhika, sio kuelemewa.
-
23:00 - 23:06Kwa hiyo, huo ni ushauri wangu kuhusu hilo.
-
23:06 - 23:17Siku hizi, wengi katika kanisa wameabudu familia kuliko Mungu
-
23:17 - 23:23na kuipa familia umakini mkubwa katika maisha yao.
-
23:23 - 23:27Lakini Biblia inasema wale walio tayari kumfuata Yesu
-
23:27 - 23:32lazima wawe tayari kutoa dhabihu familia, biashara, wakati wa ndoa.
-
23:32 - 23:35Kwa hivyo, bila kuondoa thamani ya familia,
-
23:35 - 23:38kuleta hoja ya Mungu tunayotamani hapa Cuba
-
23:38 - 23:41na kutanguliza uhusiano wetu na Mungu,
-
23:41 - 23:44tunapaswa kuwa tayari kwa kadiri gani kujidhabihu kwa namna hii?
-
23:44 - 23:58Kwa hiyo, hebu nikupeleke kwenye Kitabu cha Marko 3 kutoka mstari wa 31.
-
23:58 - 24:12“Mama yake Yesu na ndugu zake wakaja, wakasimama nje wakatuma watu kwake kumwita.
-
24:12 - 24:18Umati wa watu ulikuwa umeketi kumzunguka;
-
24:18 - 24:28wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje wanakutafuta.
-
24:28 - 24:35Lakini Yesu akawajibu, "Mama yangu ni nani au ndugu zangu?"
-
24:35 - 24:39Akatazama pande zote, akawatazama walioketi wakimzunguka, akasema,
-
24:39 - 24:41Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu!
-
24:48 - 24:58Kwa maana yeyote anayefanya mapenzi ya Mungu ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.
-
24:58 - 25:10Sasa, Yesu hasemi hapa kwamba anaikana familia yake ya kibiolojia.
-
25:10 - 25:29Tunajua jukumu ambalo mama yake Yesu alitimiza katika huduma Yake na baadaye, ndugu zake pia.
-
25:29 - 25:40Kwa hiyo, Maandiko haya hayasemi, 'Sina mama, ndugu au jamaa.' Hapana!
-
25:40 - 26:02Yesu anachosema hapa ni kwamba Roho ni mzito kuliko damu.
-
26:02 - 26:14Yesu alikuwa huko kwa ajili ya jukumu kutoka kwa Mungu, akiwafundisha watu.
-
26:14 - 26:20Jukumu hilo la koroho lilikuwa muhimu zaidi wakati huo
-
26:20 - 26:24kuliko shinikizo la mama yake na ndugu zake kutaka kumwona.
-
26:36 - 26:40Kwa hivyo, suala la kusimamia familia yako, majukumu yako ya kibinadamu -
-
26:40 - 26:44lazima ufanye hivyo, ni vizuri, hakuna ubaya na hilo -
-
26:44 - 26:49lakini si katika gharama ya maisha yako ya kiroho.
-
27:04 - 27:12Ni suala la kuelewa vipaumbele vyako.
-
27:12 - 27:21Unawezaje kuwa baba, mama, kaka au dada mzuri anayeonyesha upendo
-
27:21 - 27:25na kusaidia familia yako ikiwa hauko mahali sahihi pamoja na Mungu?
-
27:41 - 27:54Njia kuu zaidi unayoweza kusaidia familia yako ni kutunza uhusiano wako na Mungu.
-
27:54 - 28:04Kwa sababu kufurika kwa uhusiano wako na Mungu kutawabariki wale wanaokuzunguka.
-
28:04 - 28:14Kwa hivyo, ikiwa sasa unakabiliwa na kudumaa kiroho kwa sababu unatoa
-
28:14 - 28:20muda mwingi, usikivu, kuzingatia, maslahi kwa familia yako - jiangalie mwenyewe.
-
28:35 - 28:41Familia ni muhimu sana.
-
28:41 - 28:48Lakini unaposimama mbele ya Yesu siku ya mwisho,
-
28:48 - 28:51mke wako hatakuwepo.
-
28:51 - 28:57Baba yako hatakuwepo; mama yako hatakuwepo.
-
28:57 - 29:01Ni wewe na Yesu.
-
29:01 - 29:06Asante.
-
29:08 - 29:13Baraka. Jina langu ni Carla; mimi nina miaka 23.
-
29:13 - 29:21Ikiwa una tamaa ya kumtumikia Mungu wakati wote, unajua ni wakati gani huo ndio wakati unaofaa?
-
29:21 - 29:24Nitajuaje kama mawazo yanayokubaliana na hili sio mawazo yangu tu
-
29:24 - 29:28na mawazo dhidi yake si mashambulizi kutoka kwa adui
-
29:28 - 29:33lakini ni kweli Mungu ananiambia anataka nifanye hivi, kwamba huu ndio wakati mwafaka?
-
29:33 - 29:46Kazi ya Mungu si suala la ustahili wa kibinadamu.
-
29:46 - 29:56Yesu alipomwagiza Petro katika Yohana 21,
-
29:56 - 30:10Hakumuuliza ikiwa alikuwa mwalimu wa Biblia anayestahili au msemaji mwenye kipawa.
-
30:10 - 30:17Alimuuliza swali, 'Je, wanipenda Mimi?'
-
30:17 - 30:29Ni upendo wetu kwa Kristo ambao ndio msingi wa huduma yenye ufanisi.
-
30:29 - 30:42Ikiwa unatunza uhusiano wako na Mungu na Yeye amekuita kwenye huduma,
-
30:42 - 30:54matukio yatatokea nje ya uwezo wako ambayo yatakusukuma kwenye wito wako.
-
30:54 - 30:59Haitakuwa swali la 'Sina hakika, ni mawazo yangu au ni mawazo ya Mungu?'
-
30:59 - 31:13Itakuwa ni ishara isiyoweza kufahamika na mwanadamu.
-
31:13 - 31:22Kwa hiyo, unachopaswa kukizingatia wewe ni - upendo wangu kwa Yesu.
-
31:22 - 31:27Hilo ndilo jambo muhimu zaidi.
-
31:27 - 31:39Ili kumfanyia Yesu mambo makuu, ni lazima uwe na upendo mkuu kwa Yesu.
-
31:39 - 31:44Asante.
-
31:44 - 31:49Kwa hiyo, ndugu yangu, endelea.
-
31:49 - 31:53Jina langu ni Fernando na nina umri wa miaka 18.
-
31:53 - 31:58Swali langu ni je vijana tufanye nini kwa ajili ya moto wa Mungu
-
31:58 - 32:02na hamu ya kumtumikia ili isizimishwe katika maisha yetu?
-
32:02 - 32:12Kwa hiyo, nikuulize ndugu. Unafikiri ni nini kinachozima moto wa Mungu?
-
32:12 - 32:15Dhambi.
-
32:15 - 32:18Sawa, umetoa jibu.
-
32:18 - 32:23Hakuna aliye mkamilifu hapa.
-
32:23 - 32:27Sisi sote hufanya makosa.
-
32:27 - 32:35Lakini kuna tofauti kati ya kufanya makosa katika kutafuta kusudi
-
32:35 - 32:39na kutenda dhambi kwa kutafuta kujiridhisha.
-
32:54 - 33:02Je, ni ushahidi gani kwamba Roho Mtakatifu anatawala mioyo yetu?
-
33:02 - 33:13Ni pale tunapofanya makosa na kuhukumiwa kuwa na dhambi.
-
33:13 - 33:22'Mungu, samahani! Sitaki kufanya lolote kuvunja uhusiano wangu na Wewe.'
-
33:22 - 33:32Unakimbilia kwa Mungu kwa toba - Na Yeye anakurejesha, na moto hauzimiki.
-
33:32 - 33:35Lakini jichinguze.
-
33:35 - 33:40Ikiwa utafanya vibaya na jibu lako la kwanza
-
33:40 - 33:46ni kutoa visingizio, kujihesabia haki,
-
33:46 - 33:54inaonyesha Roho wa Mungu hatawali moyo wako.
-
33:54 - 34:04Roho Mtakatifu husukuma dhamiri zetu kutubu.
-
34:04 - 34:20Lakini ikiwa unahalalisha kosa lako kwa ndani, unaondoa hitaji la toba.
-
34:20 - 34:26Wakati huo, moto unazimwa.
-
34:26 - 34:37Kwa sababu Roho wa Mungu hawezi kushiriki moyo unaotawaliwa na dhambi.
-
34:37 - 34:41Ninaweza tu kukupa mfano rahisi sana.
-
34:41 - 34:47Wengi wetu hapa huja kwenye tukio kama hili
-
34:47 - 34:55na kusema, Moto wa Roho Mtakatifu, unianguke!
-
34:55 - 35:04Lakini bado tunahifadhi kutokusamehe mtu fulani.
-
35:04 - 35:13Roho Mtakatifu hawezi kushiriki moyo wa kutosamehe.
-
35:13 - 35:21Kwa sababu, katika kesi ya kosa, ni kwa sababu mtu amekukosea,
-
35:21 - 35:27ni rahisi kwako kujisikia haki ya kukataa kusamehe.
-
35:43 - 35:56Unaweza kujisikia kuwa na haki mbele ya mwanadamu, lakini mbele za Mungu huna haki ya kushikilia kosa.
-
35:56 - 36:07Kwa sababu Yesu alikufa Msalabani na kusema, 'Baba, uwasamehe.'
-
36:07 - 36:11Ikiwa hakutunyima msamaha,
-
36:11 - 36:15sisi ni nani hata kumnyima mtu mwingine msamaha?
-
36:23 - 36:33Ninakupa mfano mmoja tu wa mambo yanayoweza kuzima moto wa Roho Mtakatifu.
-
36:33 - 36:37Moyo uliojaa maudhi.
-
36:37 - 36:42Kwa hiyo, asante kwa swali, ndugu.
-
36:42 - 36:48Habari za mchana. Baraka, kanisa! Jina langu ni Gema. Ninatoka Mayabeque.
-
36:48 - 36:50Hili ni swali langu.
-
36:50 - 36:58Umekuwa ukizungumza sana kuhusu tabia, Neno la Mungu na ushirika na Baba yetu.
-
36:58 - 37:11Tunawezaje kujua katika maisha yetu ikiwa tuna wito au karama ya kudhihirisha utukufu wa Mungu
-
37:11 - 37:20kutoa na kubadilisha maisha kwa kiwango kile kile tulichokuona ukifanya kati yetu jana?
-
37:20 - 37:29Neno la Mungu huakisi tabia yake.
-
37:29 - 37:36Linapokuja suala la tabia, hakuna njia za mkato.
-
37:36 - 37:44Maisha haya ni marathon, sio mbio.
-
37:44 - 38:00Nitamnukuu Nabii TB Joshua. Alisema, "Lazima tuthamini zaidi mchakato kuliko matokeo."
-
38:00 - 38:08Mchakato hujenga tabia.
-
38:08 - 38:24Badala ya kuzingatia moto, zingatia mafuta.
-
38:24 - 38:39Moto ni zawadi; mafuta ni tabia.
-
38:39 - 38:46Kwa hivyo, zingatia zaidi mafuta,
-
38:46 - 38:52ambayo yanahusiana na uhusiano wako na Mungu.
-
38:52 - 38:56Kwa sababu sio tu kufika mahali fulani au kufanikisha jambo fulani.
-
38:56 - 38:58Ni juu ya kutunza hadi mwisho.
-
39:05 - 39:21Ushahidi wa kuwa kweli ni uthabiti.
- Title:
- Ndugu Chris Akijibu Maswali ya PAPO KWA HAPO!
- Description:
-
Ndugu Chris anajibu maswali moja kwa moja kuhusu masuala kama vile ukomavu katika ndoa, kusimamia majukumu ya familia, kujua wito wako, masomo kutoka kwa Nabii T.B. Joshua, kutofautisha sauti ya Mungu, kutumia karama yako, ushauri wake kwake mwenyewe akiwa kijana, kudhibiti majaribu ya tamaa - na mengine mengi!
Unaweza kutazama video kamili kutoka kwenye Kongamano la Vijana la Cuba ambapo kipindi hiki cha Maswali na Majibu kilifanyika hapa - https://www.youtube.com/watch?v=XyAq6N2Mqd0
SURA:
00:00 - Muhtasari mfupi wa jibu juu ya ndoa
00:24 - Tunapokuwa na karama nyingi, tunawezaje kujua kusudi letu maalum?
03:58 - Ni masomo gani uliyojifunza kuhusu uhusiano wa kina na Roho Mtakatifu kutoka kwa Nabii T.B. Joshua?
09:17 - Ungempa ushauri gani mdogo wako?
11:40 - Ninawezaje kubaki katika upendo na hofu ya Mungu?
16:28 - Unawezaje kujua kwamba ni mtu anayefaa linapokuja suala la ndoa?
23:07 - Wengi wameabudu familia juu ya Mungu. Tunapaswa kuwa tayari kudhabihu nini juu ya swala la kusimamia madaraka ya familia?
29:07 - Unajuaje ikiwa umeitwa kumtumikia Mungu wakati wote?
31:49 Tufanye nini ili moto wa Mungu usizimike?
36:42 - Unawezaje kujua kama umeitwa katika huduma ya ukombozi?➡️ Pata Kutia Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Saidia TV ya Moyo wa Mungu kifedha - https://godsheart.tv/financial/
➡️ Habari kuhusu Maombi Shirikishi - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
- God's Heart TV
- Duration:
- 39:52
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Brother Chris Answers SPONTANEOUS Questions! |