Ushuhuda wa Maombi ya MTANDAONI! | UPONYWAJI kutoka kwenye MIAKA 17 ya BAWASIRI (HAEMORRHOIDS)
-
0:00 - 0:10Tangu 2007 - hadi sasa, ni kama miaka 17 -
nilikuwa nikiishi katika maumivu haya na mateso, -
0:10 - 0:14kwa kiwango ambacho nilianza
kuwa na mashaka kama kweli Mungu yupo. -
0:14 - 0:16Je, anaponya kama alivyosema katika Neno Lake?
-
0:16 - 0:20Lakini sikupoteza tumaini kamwe.
Nilijua siku yangu itafika! -
0:22 - 0:31Sasa hivi, watu wa Mungu,
chochote kinachowaibia furaha yenu, -
0:31 - 0:43kunyang'anya amani yako, kuumiza afya yako - ugonjwa huo, maradhi, udhaifu -
-
0:43 - 0:49kwa mamlaka katika jina la Yesu Kristo, natangaza uponyaji sasa hivi!
-
0:49 - 0:57Upone kwa jina la Yesu! Urejeshwe!
-
0:59 - 1:02Jina langu ni Lastone kutoka Zambia.
-
1:02 - 1:10Sababu iliyonifanya nijiunganishe na God's Heart TV ilikuwa changamoto ya bawasiri (haemorrhoids),
-
1:10 - 1:14ambayo nimekuwa nayo tangu 2007.
-
1:14 - 1:18Kwa hiyo tatizo hili lilianza
nikiwa mdogo sana. -
1:18 - 1:24Iliendelea kutoka
na kurudi tena. -
1:24 - 1:30Nilipogundua hili linahitaji uangalizi,
nilitembelea zahanati na hospitali. -
1:30 - 1:36Niliambiwa nilihitaji kufanyiwa upasuaji au kuchukua dawa.
-
1:36 - 1:43Nilianza kutumia baadhi ya dawa lakini bawasiri(haemorrhoids) haikuisha.
-
1:43 - 1:46Ingetoka na kurudi - vivyo hivyo.
-
1:46 - 1:50Tatizo hili lilinipa nyakati ngumu sana.
-
1:50 - 1:52Nilianza kutokwa na damu.
-
1:52 - 1:57Kila nilipotembelea choo,
niliona damu ikitoka. -
1:57 - 2:04Ile sehemu ya haja kubwa ilitoka
na nilikuwa naishi kwa maumivu. -
2:04 - 2:11Kama mwanaume, kulikuwa na
mambo fulani ambayo nililazimika kupunguza. -
2:11 - 2:18Sikuweza kuchangamana na watu au kushirikiana na watu wengi kwa sababu ya maumivu.
-
2:18 - 2:20Wangekuuliza,
'Kwa nini umeketi hivyo?' -
2:20 - 2:26Kwa hivyo ningependelea kuwa mpweke, nibaki tu ndani au niwe na familia yangu.
-
2:26 - 2:32Sikuweza kukaa juu ya kitu ambacho
kilikuwa yabisi au kigumu. Ilikuwa ngumu sana! -
2:32 - 2:36Kwa hivyo kutoka wakati huo, nilijaribu mimea.
-
2:36 - 2:41Nilijaribu kupokea msaada kutoka kwa watu
ambao walisema wanaweza kuikata. -
2:41 - 2:49Walijaribu kufanya hivyo lakini tatizo
halikuisha - hadi mwaka huu, 2024. -
2:49 - 2:57Nilikutana na Ndugu Chris,
na ilinipa furaha kumuona tena. -
2:57 - 3:01Nilijiambia, 'Acha
nitume ombi la maombi.' -
3:01 - 3:11Tarehe 6 Julai, mwezi uliopita, nilijiunga na Huduma Ya Maombi Ya Pamoja kupitia TV ya Moyo wa Mungu.
-
3:11 - 3:18Kwa mshangao wangu, nilipojaribu kuingiza barua pepe yangu, nenosiri langu halikupita.
-
3:18 - 3:22Ilikuwa ikiniambia, 'Ni nenosiri lisilo sahihi'.
-
3:22 - 3:27Nilichanganyikiwa na kufadhaika lakini
'nilijipoza' na kusema, -
3:27 - 3:31'Kuna sababu kwa nini haya
yanatokea - ni siku yangu!' -
3:31 - 3:33Kwa sababu, watu wa Mungu, nilikuwa na maumivu.
-
3:33 - 3:39Hebu fikiria - huwezi kukaa vizuri
kwa sababu ya maumivu katika mkundu wako. -
3:39 - 3:46Kwa hivyo nikasema, 'Leo ni siku yangu. Ni siku yangu ya ukombozi, siku yangu ya mafanikio!'
-
3:46 - 3:47Niliendelea kujiambia.
-
3:47 - 3:53Kwa hivyo nilienda kwenye Facebook badala ya kupitia mwaliko wa Huduma Ya Maombi Ya Pamoja kupitia Zoom.
-
3:53 - 3:57Nilienda Facebook na kujiambia,
'Leo ni siku yangu.' -
3:57 - 4:02Nilisikiliza shuhuda.
Niliendelea kujenga imani yangu na kuomba. -
4:02 - 4:05Na Ndugu Chris alihubiri
na kutuombea. -
4:05 - 4:08Nilijiungana na kujidhihirisha!
-
4:08 - 4:13Nilihisi kitu kilikuwa kinatembea
tumboni mwangu. -
4:13 - 4:17Sehemu hii ya tumbo langu ilikuwa ikitetemeka.
-
4:17 - 4:20Kuanzia hapo, nilijikuta tu
chini sakafuni. -
4:20 - 4:28Sala ilipokwisha jioni, nilienda chumbani kwangu kujiangalia.
-
4:28 - 4:32Niligundua kuwa bawasiri (hemorrhoids)
ilikuwa imeanza kupungua. -
4:32 - 4:34Ilikuwa ndogo sana.
-
4:34 - 4:38Basi nikampigia simu mke wangu aje kuona.
-
4:38 - 4:43Kwa hivyo akaja na nikasema,
'Jambo hili linapungua'. -
4:43 - 4:48Kwa hivyo alijaribu kuangalia na tochi na akasema, 'Ndiyo, inapungua kweli.'
-
4:48 - 4:53Kwa utukufu wa Mungu, wana wa Mungu,
niliponywa mara moja. -
4:53 - 4:56Bawasiri (hemorrhoid) hiyo ilikauka papo hapo.
-
4:56 - 5:03Wiki hiyo ilipokwisha,
nilikuwa mzima kabisa! -
5:03 - 5:10Ninapozungumza nanyi wana wa Mungu,
mimi nipo huru. Nimepona kwa utukufu wa Mungu. -
5:10 - 5:15Sasa naweza kuketi kwa utukufu wa Mungu.
-
5:15 - 5:18Kama unavyoona, sasa naweza kuketi.
-
5:18 - 5:27Hiki ni kiti kigumu cha plastiki lakini sasa naweza kukikalia na hata kuruka hivi.
-
5:27 - 5:32Hakuna maumivu. Niko huru!
-
5:32 - 5:35Ninachoweza kusema ni, 'Asante, Yesu!'
-
5:35 - 5:44Watoto wa Mungu, kama mlivyosikia, tangu 2007 - hadi sasa, ni kama miaka 17 -
-
5:44 - 5:49Nilikuwa nikiishi katika maumivu haya na mateso,
-
5:49 - 5:53kwa kiwango ambacho nilianza
kuwa na mashaka kama kweli Mungu yupo. -
5:53 - 5:56Je, anaponya kama alivyosema katika Neno Lake?
-
5:56 - 6:00Lakini sikupoteza tumaini kamwe.
Nilijua siku yangu itafika! -
6:00 - 6:05Na Ndugu Chris 'akaingia' na
nimepona kwa utukufu wa Yesu! -
6:05 - 6:08Maumivu yote niliyokuwa nayasikia yamekwisha!
-
6:08 - 6:13Ule moto niliouhisi kutokana na bawasiri (haemorrhoids) ile umetoweka!
-
6:13 - 6:18Wana wa Mungu, kamwe usipoteze matumaini.
Endelea kuamini. -
6:18 - 6:23Kama unavyoona, sikujiunga na Maombi ya Pamoja kupitia Zoom
-
6:23 - 6:27lakini niliomba kupitia Facebook;
NIlijiunga kupitia Facebook. -
6:27 - 6:32Nilijiambia, 'Leo ni siku yangu!'
Ni vivyo hivyo kwako. -
6:32 - 6:36Haijalishi changamoto unayokutana nayo au maumivu unayopitia,
-
6:36 - 6:44ili mradi unaamini na umeunganishwa na Huduma hii ya Maombi ya Pamoja,
-
6:44 - 6:48Mungu anakwenda kukugusa,
kukuponya na kukukomboa. -
6:48 - 6:50Unachohitaji ni kuamini.
-
6:50 - 6:54Mwamini Bwana na Mungu
atakugusa na kukuponya. Amina!
- Title:
- Ushuhuda wa Maombi ya MTANDAONI! | UPONYWAJI kutoka kwenye MIAKA 17 ya BAWASIRI (HAEMORRHOIDS)
- Description:
-
more » « less
Lastone kutoka Zambia alikuwa ameishi 'katika maumivu na mateso' kwa miaka kumi na saba kutokana na bawasiri (haemorrhoids). Lakini shida yake ilifikia tamati kwa njia ya kimuujiza baada ya kujiunga na mkondo wa moja kwa moja wa Ibada ya Pamoja ya Maombi na Ndugu Chris kupitia Facebook. Alipojiunga na maombi hayo kwa imani, nguvu za Mungu zilimpata na kujikuta yuko chini. Usiku huo huo, bawasiri (hemorrhoids) ilianza kupungua na kisha kukauka kwa namna ya kushangaza.
Je, ungependa kupokea maombi mtandaoni bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom? Tafadhali wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Saidia TV ya Moyo wa Mungu kifedha - https://godsheart.tv/financial/
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Mwingiliano - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 07:25
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for ONLINE Prayer Testimony! | HEALING from 17 YEARS of HAEMORRHOIDS | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for ONLINE Prayer Testimony! | HEALING from 17 YEARS of HAEMORRHOIDS | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for ONLINE Prayer Testimony! | HEALING from 17 YEARS of HAEMORRHOIDS | ||
| georgejbudeba edited Swahili subtitles for ONLINE Prayer Testimony! | HEALING from 17 YEARS of HAEMORRHOIDS |