-
Tangu 2007 - hadi sasa, ni kama miaka 17 -
nilikuwa nikiishi katika maumivu haya na mateso,
-
kwa kiwango ambacho nilianza
kuwa na mashaka kama kweli Mungu yupo.
-
Je, anaponya kama alivyosema katika Neno Lake?
-
Lakini sikupoteza tumaini kamwe.
Nilijua siku yangu itafika!
-
Sasa hivi, watu wa Mungu,
chochote kinachowaibia furaha yenu,
-
kunyang'anya amani yako, kuumiza afya yako - ugonjwa huo, maradhi, udhaifu -
-
kwa mamlaka katika jina la Yesu Kristo, natangaza uponyaji sasa hivi!
-
Upone kwa jina la Yesu! Urejeshwe!
-
Jina langu ni Lastone kutoka Zambia.
-
Sababu iliyonifanya nijiunganishe na God's Heart TV ilikuwa changamoto ya bawasiri (haemorrhoids),
-
ambayo nimekuwa nayo tangu 2007.
-
Kwa hiyo tatizo hili lilianza
nikiwa mdogo sana.
-
Iliendelea kutoka
na kurudi tena.
-
Nilipogundua hili linahitaji uangalizi,
nilitembelea zahanati na hospitali.
-
Niliambiwa nilihitaji kufanyiwa upasuaji au kuchukua dawa.
-
Nilianza kutumia baadhi ya dawa lakini bawasiri(haemorrhoids) haikuisha.
-
Ingetoka na kurudi - vivyo hivyo.
-
Tatizo hili lilinipa nyakati ngumu sana.
-
Nilianza kutokwa na damu.
-
Kila nilipotembelea choo,
niliona damu ikitoka.
-
Ile sehemu ya haja kubwa ilitoka
na nilikuwa naishi kwa maumivu.
-
Kama mwanaume, kulikuwa na
mambo fulani ambayo nililazimika kupunguza.
-
Sikuweza kuchangamana na watu au kushirikiana na watu wengi kwa sababu ya maumivu.
-
Wangekuuliza,
'Kwa nini umeketi hivyo?'
-
Kwa hivyo ningependelea kuwa mpweke, nibaki tu ndani au niwe na familia yangu.
-
Sikuweza kukaa juu ya kitu ambacho
kilikuwa yabisi au kigumu. Ilikuwa ngumu sana!
-
Kwa hivyo kutoka wakati huo, nilijaribu mimea.
-
Nilijaribu kupokea msaada kutoka kwa watu
ambao walisema wanaweza kuikata.
-
Walijaribu kufanya hivyo lakini tatizo
halikuisha - hadi mwaka huu, 2024.
-
Nilikutana na Ndugu Chris,
na ilinipa furaha kumuona tena.
-
Nilijiambia, 'Acha
nitume ombi la maombi.'
-
Tarehe 6 Julai, mwezi uliopita, nilijiunga na Huduma Ya Maombi Ya Pamoja kupitia TV ya Moyo wa Mungu.
-
Kwa mshangao wangu, nilipojaribu kuingiza barua pepe yangu, nenosiri langu halikupita.
-
Ilikuwa ikiniambia, 'Ni nenosiri lisilo sahihi'.
-
Nilichanganyikiwa na kufadhaika lakini
'nilijipoza' na kusema,
-
'Kuna sababu kwa nini haya
yanatokea - ni siku yangu!'
-
Kwa sababu, watu wa Mungu, nilikuwa na maumivu.
-
Hebu fikiria - huwezi kukaa vizuri
kwa sababu ya maumivu katika mkundu wako.
-
Kwa hivyo nikasema, 'Leo ni siku yangu. Ni siku yangu ya ukombozi, siku yangu ya mafanikio!'
-
Niliendelea kujiambia.
-
Kwa hivyo nilienda kwenye Facebook badala ya kupitia mwaliko wa Huduma Ya Maombi Ya Pamoja kupitia Zoom.
-
Nilienda Facebook na kujiambia,
'Leo ni siku yangu.'
-
Nilisikiliza shuhuda.
Niliendelea kujenga imani yangu na kuomba.
-
Na Ndugu Chris alihubiri
na kutuombea.
-
Nilijiungana na kujidhihirisha!
-
Nilihisi kitu kilikuwa kinatembea
tumboni mwangu.
-
Sehemu hii ya tumbo langu ilikuwa ikitetemeka.
-
Kuanzia hapo, nilijikuta tu
chini sakafuni.
-
Sala ilipokwisha jioni, nilienda chumbani kwangu kujiangalia.
-
Niligundua kuwa bawasiri (hemorrhoids)
ilikuwa imeanza kupungua.
-
Ilikuwa ndogo sana.
-
Basi nikampigia simu mke wangu aje kuona.
-
Kwa hivyo akaja na nikasema,
'Jambo hili linapungua'.
-
Kwa hivyo alijaribu kuangalia na tochi na akasema, 'Ndiyo, inapungua kweli.'
-
Kwa utukufu wa Mungu, wana wa Mungu,
niliponywa mara moja.
-
Bawasiri (hemorrhoid) hiyo ilikauka papo hapo.
-
Wiki hiyo ilipokwisha,
nilikuwa mzima kabisa!
-
Ninapozungumza nanyi wana wa Mungu,
mimi nipo huru. Nimepona kwa utukufu wa Mungu.
-
Sasa naweza kuketi kwa utukufu wa Mungu.
-
Kama unavyoona, sasa naweza kuketi.
-
Hiki ni kiti kigumu cha plastiki lakini sasa naweza kukikalia na hata kuruka hivi.
-
Hakuna maumivu. Niko huru!
-
Ninachoweza kusema ni, 'Asante, Yesu!'
-
Watoto wa Mungu, kama mlivyosikia, tangu 2007 - hadi sasa, ni kama miaka 17 -
-
Nilikuwa nikiishi katika maumivu haya na mateso,
-
kwa kiwango ambacho nilianza
kuwa na mashaka kama kweli Mungu yupo.
-
Je, anaponya kama alivyosema katika Neno Lake?
-
Lakini sikupoteza tumaini kamwe.
Nilijua siku yangu itafika!
-
Na Ndugu Chris 'akaingia' na
nimepona kwa utukufu wa Yesu!
-
Maumivu yote niliyokuwa nayasikia yamekwisha!
-
Ule moto niliouhisi kutokana na bawasiri (haemorrhoids) ile umetoweka!
-
Wana wa Mungu, kamwe usipoteze matumaini.
Endelea kuamini.
-
Kama unavyoona, sikujiunga na Maombi ya Pamoja kupitia Zoom
-
lakini niliomba kupitia Facebook;
NIlijiunga kupitia Facebook.
-
Nilijiambia, 'Leo ni siku yangu!'
Ni vivyo hivyo kwako.
-
Haijalishi changamoto unayokutana nayo au maumivu unayopitia,
-
ili mradi unaamini na umeunganishwa na Huduma hii ya Maombi ya Pamoja,
-
Mungu anakwenda kukugusa,
kukuponya na kukukomboa.
-
Unachohitaji ni kuamini.
-
Mwamini Bwana na Mungu
atakugusa na kukuponya. Amina!