< Return to Video

Mwalimu Apokea UPONYAJI WA MIUJIZA Kutokana na Maumivu ya Mgongo!

  • 0:00 - 0:06
    Maumivu yalikoma tu baada ya Ibada ya Kuingiliana ya Maombi na Ndugu Chris.
  • 0:06 - 0:14
    Baada ya sala hiyo, nilihisi amani ya ndani na nililala kama mtoto mchanga.
  • 0:17 - 0:24
    Kila uharibifu kwa mifupa yako, kila uharibifu wa tendons yako -
  • 0:24 - 0:31
    Ninasema, urejeshwe, katika jina kuu la Yesu Kristo!
  • 0:31 - 0:37
    Dada, nataka tu ugeuke. Geuka uso kwa mgongo wako.
  • 0:37 - 0:43
    Katika jina kuu la Yesu Kristo, popote pale maumivu yalipo,
  • 0:43 - 0:46
    upone kwa jina la Yesu.
  • 0:46 - 0:57
    Pokea uhuru, katika jina kuu la Yesu Kristo!
  • 0:57 - 1:03
    Asante, Yesu kwa mguso wako wa uponyaji.
  • 1:03 - 1:07
    Dada, geuka nyuma. Nataka ujichunguze.
  • 1:07 - 1:12
    Unaweza kujaribu kile ambacho hukuweza kufanya hapo awali. Inama chini na ujiangalie sasa hivi
  • 1:12 - 1:17
    kwa sababu Roho wa Mungu ameng'oa mzizi wa mateso hayo.
  • 1:19 - 1:25
    Jina langu ni Getrude. Ninatoka Zimbabwe.
  • 1:25 - 1:37
    Nilikuwa na tatizo kwenye mgongo wangu. Nilikuwa na maumivu makali ya mgongo tangu Novemba 2022.
  • 1:37 - 1:43
    Maumivu haya makali ya mgongo yaliniathiri sana kwa njia nyingi.
  • 1:43 - 1:48
    Mimi ni mwalimu kwa taaluma. Sikuweza kufanya kazi yangu ipasavyo.
  • 1:48 - 1:53
    Sikuweza kusimama mbele ya watoto kwa muda mrefu.
  • 1:53 - 1:58
    Sikuweza kufanya shughuli ambazo nilipaswa kufanya na wanafunzi wangu darasani.
  • 1:58 - 2:05
    Sikuweza kufanya shughuli za michezo. Nilisamehewa kuzifanya
  • 2:05 - 2:07
    kwa sababu ya maumivu makali ya mgongo.
  • 2:07 - 2:12
    Nyumbani, kama mama, sikuweza kufanya kazi za nyumbani kama vile
  • 2:12 - 2:17
    kufagia, kufua nguo, hata kuosha vyombo,
  • 2:17 - 2:21
    kwa sababu sikuweza kuinama kutokana na maumivu haya.
  • 2:21 - 2:24
    Sikuweza kulala vizuri pia.
  • 2:24 - 2:29
    Nilienda kumtembelea daktari na akanielekeza kwa tabibu,
  • 2:29 - 2:36
    ambapo nilikuwa na masaji ya matibabu, lakini hayakunisaidia kwa njia yoyote.
  • 2:36 - 2:38
    Niliendelea kuhisi maumivu.
  • 2:38 - 2:45
    Maumivu yalikoma tu baada ya Ibada ya Kuingiliana ya Maombi na Ndugu Chris.
  • 2:45 - 2:49
    Sikupata chochote kimwili kama kutapika,
  • 2:49 - 2:58
    lakini baada ya maombi, nilihisi amani ya ndani na nililala kama mtoto mchanga.
  • 2:58 - 3:02
    Hapo awali, ningekuwa na usiku usio na usingizi.
  • 3:02 - 3:07
    Sasa, ninaweza kufanya mambo yote ambayo sikuweza kufanya.
  • 3:07 - 3:13
    Hapo awali, nilikuwa nimevaa viatu vya gorofa tu. Sasa, ninavaa visigino vyangu tena.
  • 3:13 - 3:15
    Ninafanya kazi za nyumbani.
  • 3:15 - 3:20
    Sasa ninafanya shughuli za michezo na ninaweza kuinama.
  • 3:20 - 3:24
    Ilikuwa ngumu kwangu kuinama hivi.
  • 3:24 - 3:30
    Sikuweza kuvaa visigino kama ninavyofanya sasa.
  • 3:30 - 3:35
    Sasa nimevaa visigino kama unavyoona.
  • 3:35 - 3:38
    Nilikuwa nimevaa viatu vya gorofa tu.
  • 3:38 - 3:44
    Sasa naweza kuinama.
  • 3:44 - 3:52
    Hili lilikuwa jambo ambalo lilikuwa gumu sana kwangu kwa sababu ningesikia maumivu tu.
  • 3:52 - 3:56
    Lakini sasa, mimi ni mzima kabisa na ninataka kumshukuru Bwana kwa hili.
  • 3:56 - 4:00
    Kwa watazamaji kote ulimwenguni, ningependa tu kusema -
  • 4:00 - 4:05
    Yesu hakuwahi kuaga. Ni yeye yule jana, leo na hata milele.
  • 4:05 - 4:10
    Bado anaponya, hutoa na kubariki.
  • 4:10 - 4:14
    Na tunapaswa kumwamini daima, kumtumaini Yeye.
Title:
Mwalimu Apokea UPONYAJI WA MIUJIZA Kutokana na Maumivu ya Mgongo!
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
04:34

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions