-
-
Tafuta ukubwa wa tufe lenye kipenyo cha sentimita 14.
-
Hivyo kama nina tufe-- hili si duara,
-
hili ni tufe.
-
Unaweza kuliona liko kama mviringo.
-
Nitatia kivuli kidogo
-
ili uweze kuona vizuri.
-
Tumepewa kipenyo.
-
Kwa hiyo kama tukitoka upande mmoja wa tufe
-
moja kwa moja kupitia katikati.
-
Tunaweza kuona kwenye tufe.
-
Na tumepita katikati,
-
huo umbali hapo ni sentimita 14.
-
Sasa, kutafuta ukubwa wa tufe,
-
na utaona uthibitisho baadae tutakapojifunza kalkulasi.
-
Lakini njia ya kutafuta ukubwa wa tufe
-
ni ukubwa ni sawa na 4/3 pai r kipeo cha tatu,
-
ambapo r ni nusukipenyo cha tufe.
-
Kwa hiyo tayari tuna kipenyo.
-
Na kama ilivyo kwa duara, nusukipenyo cha tufe
-
ni nusu ya kipenyo.
-
Kwa hiyo, nusukipenyo kitakuwa sentimita 7.
-
Na kwa hakika, tufe lenyewe ni
-
mpangilio wa vipimo vyote vitatu ambapo ni pamoja na
-
nusukipenyo.
-
Lakini kwa njia hii,
-
hebu tutumie nusukipenyo ambacho ni sentimita 7 katika
-
njia hii.
-
Kwa hiyo tutakuwa na ukubwa ni
-
sawa na 4/3 pai mara sentimita 7 kepeo cha tatu.
-
Nitaifanya hiyo kwa rangi ya waridi.
-
Hivyo mara sentimita 7 kipeo cha tatu.
-
Na kwa sababu inajumuisha pai,
-
tunaweza kutumia pai ambayo ni 3.14.
-
Watu wengine wanaweza kutumia 22/7.
-
Lakini tutatumia kikokotoo
-
ili kupata thamani sahihi ya huu ukubwa.
-
Kwa hiyo ukubwa utakuwa
-
ni 4 gawanya kwa 3.
-
Na siwezi kuweka pai pale,
-
kwa sababu inaweza kutafsiri kama 4 gawanya kwa 3 pai.
-
Hivyo 4 gawanya kwa 3 mara pai, mara 7 kipeo cha tatu.
-
Katika mpangilipo wa matendo ya kihisabati, nitaanza na namba kipeo
-
kabla ya kwenda kuzidisha,
-
hivyo ndivyo tutakavyofanya.
-
Na kizio kitakuwa katika sentimita za ukubwa.
-
-
Hivyo tunapata 1436.
-
Hatukuambiwa tuikaribishe kwa ngapi.
-
Hivyo nitaikaribisha katika makumi yaliyo karibu.
-
Kwa hiyo hii ni sawa na sentimita za ukubwa 1436.8.
-
Tumemaliza.