< Return to Video

Mume wa Kiroho AMETOWESHWA! Miongo ya Uraibu IMEVUNJIKA!

  • 0:00 - 0:05
    Tangu wakati huo mnamo Machi, hadi sasa,
    maisha yangu hayajabaki kama ilivyokuwa.
  • 0:05 - 0:07
    Nimepona kabisa na nimekombolewa.
  • 0:07 - 0:09
    Hakuna shinikizo la damu tena.
  • 0:09 - 0:14
    Hakuna ugonjwa tena. Hakuna tena maumivu ya kichwa.
    Hakuna kizunguzungu tena.
  • 0:14 - 0:17
    Ndoto mbaya na mashambulizi -
    yote yamekoma!
  • 0:17 - 0:20
    Simwoni huyo mume wa kiroho tena.
  • 0:21 - 0:24
    Dada yetu wa Afrika Kusini tuombe.
  • 0:24 - 0:36
    Katika jina kuu la Yesu Kristo,
    toka sasa hivi!
  • 0:36 - 0:43
    Ewe pepo mchafu, chochote ulichoweka ndani yake, toka kwa jina la Yesu!
  • 0:43 - 0:47
    Roho nyuma ya uraibu huo -
    toka nje sasa hivi!
  • 0:47 - 0:59
    Toka sasa hivi,
    katika jina la Yesu Kristo!
  • 0:59 - 1:01
    Kitapike kwa jina la Yesu.
  • 1:01 - 1:06
    Chanzo cha mateso hayo, chanzo
    cha uraibu huo - toka sasa hivi!
  • 1:23 - 1:26
    Asante, Yesu.
  • 1:26 - 1:29
    Dada yetu, hongera. Uko huru!
  • 1:29 - 1:35
    Mpe Mungu utukufu kwa uhuru wako.
    Wewe uko huru. Asante, Yesu.
  • 1:37 - 1:40
    Jina langu ni Esther. Ninatoka Afrika Kusini.
  • 1:40 - 1:47
    Niliwasiliana na God's Heart TV nikiwa na
    tatizo la uraibu wa ugoro.
  • 1:47 - 1:53
    Uraibu huu ulianza nikiwa bado shuleni. Sasa nina karibu miaka 60.
  • 1:53 - 1:56
    Nilijaribu mara nyingi sana kuacha peke yangu.
  • 1:56 - 2:01
    Nilienda kwa waganga na dawa
    nilizopata kutoka kwa waganga
  • 2:01 - 2:07
    kukomesha au kuondoa hamu haikusaidia.
  • 2:07 - 2:11
    Na sijui kama kila mtu
    anajua kuhusu hili - ni tumbaku
  • 2:11 - 2:14
    na nikotini katika kitu hicho ni mbaya sana.
  • 2:14 - 2:18
    Inaendelea na kuendelea. Unaweza kuacha kwa leo na kesho utarudia tena.
  • 2:18 - 2:26
    Sikuweza kulala usiku. Ningepata
    mashambulizi mabaya, ndoto mbaya kila wakati.
  • 2:26 - 2:33
    Nilishambuliwa na mume wa kiroho
    na afya yangu haikuwa nzuri pia.
  • 2:33 - 2:40
    Nilienda kwa waganga kwa sababu nilikuwa na shinikizo la damu na vifundo vya miguu vilivyovimba.
  • 2:40 - 2:44
    Kwa hiyo, nilikuwa nimepewa dawa -
    lakini bila mafanikio.
  • 2:44 - 2:49
    Kazini, ningekuwa nikipigana na watu kwa sababu ya hasira iliyoniletea.
  • 2:49 - 2:52
    Na utendaji wangu kazini haukuwa mzuri.
  • 2:52 - 2:58
    Uchumi wangu ulikuwa mbaya sana kiasi kwamba
    sikuweza hata kulipa bili yoyote.
  • 2:58 - 3:03
    Kwa hivyo iliendelea hivyo hadi
    nikawasiliana na TV ya Moyo wa Mungu
  • 3:03 - 3:06
    kupata uingiliaji kati wa Mungu katika maisha yangu.
  • 3:06 - 3:12
    Ilikuwa mwanzoni mwa mwaka , mwezi Machi nilipopokea maombi kutoka kwa Ndugu Chris.
  • 3:12 - 3:20
    Nilihisi mkono wa Mungu ukinigusa kwa sababu nilitapika vitu vyenye sumu.
  • 3:20 - 3:28
    Na moyoni mwangu kulikuwa na furaha fulani niliyokuwa nayo - kwamba nimekombolewa. Mungu amenitendea!
  • 3:28 - 3:33
    Niko huru kutoka kwenye uraibu huu
    na Yesu ameniweka huru.
  • 3:33 - 3:40
    Na tangu wakati huo mnamo Machi, hadi sasa, maisha yangu hayabaki vile vile.
  • 3:40 - 3:42
    Nimepona kabisa na nimekombolewa.
  • 3:42 - 3:44
    Hakuna shinikizo la damu tena.
  • 3:44 - 3:47
    Hata dawa walizonipa
    nimeacha kuzitumia.
  • 3:47 - 3:52
    Hakuna ugonjwa tena. Hakuna tena maumivu ya kichwa.
    Hakuna kizunguzungu tena.
  • 3:52 - 3:58
    Asubuhi nilipoamka, nilikuwa nikihisi kizunguzungu na uzito ndani lakini sivyo tena.
  • 3:58 - 4:03
    Ndoto hizo zote, ndoto mbaya
    na mashambulizi - yote yamekoma!
  • 4:03 - 4:06
    Simwoni huyo mume wa kiroho tena.
  • 4:06 - 4:10
    Je, una hamu yoyote ya kutumia
    ugoro (tumbaku)?
  • 4:10 - 4:16
    Hapana. Kwa kweli nilijifunza kwamba
    katika Neno la Mungu linasema,
  • 4:16 - 4:23
    tunapopokea maombi ya wokovu,
    inatubidi kubadili namna tunavyofikiri.
  • 4:23 - 4:30
    Kwa hiyo, kubadili jinsi ninavyofikiri na kukaa katika Neno la Mungu kumenisaidia sana.
  • 4:30 - 4:33
    Kwa sababu ikiwa hautabadilisha
    jinsi unavyofikiri,
  • 4:33 - 4:37
    basi unaweza kurudi nyuma
    kwa kile ulichokuwa nacho.
  • 4:37 - 4:45
    Lakini kwa kubadilisha namna unavyofikiri na kumkubali Mungu katika Neno lake, inakuwa 'rahisi'.
  • 4:45 - 4:49
    Ninachotaka kushauri kwa yeyote
    aliye na hali kama hiyo -
  • 4:49 - 4:52
    usikae kimya juu yake;
    usiwe na aibu juu yake.
  • 4:52 - 4:57
    Kwa sababu Mungu haoni haya.
    Wala haendi kusema hapana.
  • 4:57 - 5:00
    Neno la Mungu linasema katika Zaburi 66:
  • 5:00 - 5:05
    'Kama singeungama dhambi yangu,
    Mungu asingenisikia.'
  • 5:05 - 5:08
    Huo ndio ushauri ninaotaka kukupa.
  • 5:08 - 5:13
    Inatubidi kusema hivyo kwa Mungu, kusema,
    'Mungu, nina hali fulani.'
  • 5:13 - 5:20
    Hatupaswi kuogopa au kuwa na haya kumwambia Mungu kuhusu shida tunayoikabili.
  • 5:20 - 5:21
    Na Mungu ni mwema.
Title:
Mume wa Kiroho AMETOWESHWA! Miongo ya Uraibu IMEVUNJIKA!
Description:

"Baada ya kujiunga na Maombi ya Pamoja, maisha yangu HAYAKUBAKI vile vile..." Esther kutoka Afrika Kusini alipokea ukombozi kutoka kwa miongo kadhaa ya uraibu wa ugoro (tumbaku), uhuru kutoka kwa mashambulizi mabaya ya kiroho na uponyaji kutokana na masuala mengi ya afya baada ya kujiunga na Huduma ya Maombi ya PAmoja na Ndugu Chris. Tunaamini ushuhuda wake wenye nguvu utahimiza imani yako katika Yesu Kristo!

Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, tafadhali wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Saidia TV ya Moyo wa Mungu kifedha - https://godsheart.tv/financial/
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
05:52

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions