< Return to Video

CIVIX Explains: Forms of Misinformation

  • 0:00 - 0:04
    ♪ (muziki) ♪
  • 0:16 - 0:19
    Ili kukabili maelezo ya uongo na
    yanayopotosha
  • 0:19 - 0:22
    inaweza kuwa muhimu kutambua
    miundo yake tofauti.
  • 0:23 - 0:27
    Ifuatayo ni miundo tano ya kawaida ya
    maelezo ya kupotosha na ya uongo
  • 0:27 - 0:28
    unayopaswa kutafuta.
  • 0:29 - 0:30
    IMETUNGWA
  • 0:31 - 0:35
    Hadithi au dai lisilo la
    kweli linaitwa maudhui yaliyobuniwa.
  • 0:35 - 0:38
    Watu wanaweza kubuni hadithi
    kwa sababu za kisiasa
  • 0:38 - 0:40
    la lengo la kawaida zaidi ni pesa.
  • 0:40 - 0:43
    Mmiliki wa tovuti hunufaika kutokana
    na matangazo yanayoonekana
  • 0:43 - 0:45
    kando ya maudhui yake.
  • 0:45 - 0:48
    Kadri matangazo hayo yanapobofywa,
    ndivyo anapata pesa zaidi.
  • 0:49 - 0:50
    MLAGHAI
  • 0:51 - 0:55
    Tovuti za kulaghai hujaribu kuhadaa kwa
    kuiga mashirika yanayoaminika ya habari.
  • 0:56 - 1:00
    URL na nembo ya tovuti inayojulikana
    zaidi inaweza kubadilishwa tu kidogo
  • 1:00 - 1:02
    ili watu waamini
    wanaangalia tovuti halisi.
  • 1:02 - 1:03
    Lengo ni kuwapotosha watu
  • 1:03 - 1:06
    kuamini na kushiriki maelezo mabaya.
  • 1:08 - 1:10
    CHAMBO CHA KUBOFYA
  • 1:10 - 1:13
    Mada ya chambo cha kubofya hubuniwa
    kuchochea upekuzi wa kutosha
  • 1:13 - 1:16
    ambao watu hawawezi kujizuia kubofya
    ili kufahamu zaidi.
  • 1:16 - 1:19
    Chambo cha kubofya inaweza kuchochea
    mvuto kupitia kutia chumvi,
  • 1:20 - 1:21
    lugha yenye mhemuko,
  • 1:22 - 1:23
    au kubuni taharuki.
  • 1:24 - 1:27
    Sababu ya chambo cha kubofya
    ni kupata pesa kutokana na matangazo.
  • 1:29 - 1:30
    KUBADILISHWA
  • 1:30 - 1:34
    Maudhui yaliyobadilishwa ni maelezo
    halisi yanayoguezwa ili kubadilisha maana,
  • 1:34 - 1:37
    kama vile picha au video inayofanywa
    kuonyesha kitu
  • 1:37 - 1:38
    ambacho hakijaonyehwa kwenye halisi.
  • 1:39 - 1:43
    Picha ni moja kwa moja na huvutia
    zaidi hisia zetu kuliko maneno,
  • 1:43 - 1:46
    kwa hivyo ni njia rahisi ya
    kueneza maelezo ya kupotosha.
  • 1:48 - 1:49
    MUKTADHA USIO HALISI
  • 1:50 - 1:54
    Muktadha wa uongo ni wakati picha halisi
    inaunganishwa na hadithi isiyo sahihi.
  • 1:54 - 1:58
    Hii ni mojawapo ya miundo ya kawaida zaidi
    ya maelezo ya kupotosha na ya uongo.
  • 1:58 - 2:01
    Picha ambayo haijabadilishwa
    inaweza kupotosha kwa urahisi
  • 2:01 - 2:03
    ikiongezewa maelezo au mada ya uongo.
  • 2:05 - 2:07
    Kufahamu msamiati wa mchafuko wa maelezo
  • 2:07 - 2:10
    ni hatua muhimu katika kuwa
    watumiaji wa maelezo wenye ujuzi.
  • 2:11 - 2:13
    ♪ (muziki) ♪
Title:
CIVIX Explains: Forms of Misinformation
Description:

more » « less
Video Language:
English
Team:
Amplifying Voices
Project:
CIVIX
Duration:
02:26

Swahili subtitles

Revisions