Doing the Impossible, swallowing the sword, cutting through fear | Dan Meyer | TEDxMaastricht
-
0:08 - 0:10Asante
-
0:16 - 0:21Palikuwa na mfalme nchini India, Maharaja
na siku yake ya kuzaliwa ilitolewa amri -
0:21 - 0:24kwamba machifu wote walete
zawadi kwa mfalme. -
0:24 - 0:28Wengine wakaleta hariri bora,
wengine wakaleta panga maridadi, -
0:28 - 0:29wengine dhahabu
-
0:29 - 0:33mwisho wa mstari alikuja akitembea
mzee mdogo mwenye makunyanzi -
0:33 - 0:37ambaye alitembea kutoka kijijini kwake
kwa safari ya siku nyingi kando ya bahari. -
0:37 - 0:41alipokuwa akisogea mwana mfalme akauliza,
'Umemletea zawadi gani Mfalme?' -
0:41 - 0:45Na mzee yule taratibu sana
akakunjua mkono wake kuonyesha -
0:45 - 0:50kombe la baharini zuri sana, lenye makoa
ya zambarau na njano,nyekundu na bluu. -
0:50 - 0:51Na mwana Mfalme akasema,
-
0:51 - 0:54"Hiyo si zawadi kwa Mfalme!
Ni zawadi gani hiyo?" -
0:55 - 0:57Mzee yule akamwangalia taratibu
na kusema -
0:58 - 1:01"Kutembea mwendo mrefu.. ni sehemu
ya zawadi" -
1:01 - 1:03(Kicheko)
-
1:03 - 1:06Baada ya muda mfupi,
Nitawapa zawadi, -
1:06 - 1:08zawadi niaminiyo
ni zawadi inayostahili kuenezwa. -
1:08 - 1:10Ila kabla ya hayo, ngoja niwachukue
-
1:10 - 1:12kwenye mwendo wangu mrefu.
-
1:12 - 1:14Kama wengi wenu,
-
1:14 - 1:15Nilianza maisha kama mtoto mdogo.
-
1:15 - 1:17Wangapi kati yenu
mlianza maisha kama mtoto ? -
1:17 - 1:19Aliyezaliwa mchanga?
-
1:19 - 1:20Karibia nusu yenu.. Sawa
-
1:21 - 1:22(Kicheko)
-
1:22 - 1:25Na mliobakia, vipi?
Mlizaliwa mkiwa watu wazima? -
1:25 - 1:28Ama kweli, nataka kukutana na mama zenu!
-
1:28 - 1:29Ongelea yasiyowezekana!
-
1:31 - 1:35Nikiwa mtoto mdogo, siku zote nilipendezwa
kufanya mambo yasiyowezekana -
1:36 - 1:39Leo ni siku ambayo nimekuwa nikiitarajia
kwa miaka mingi, -
1:39 - 1:41kwa sababu leo ni siku ambayo
nitajaribu -
1:41 - 1:44kufanya yasiyowezekana
mbele ya macho yenu -
1:44 - 1:45Hapahapa TEDxMaastrich
-
1:46 - 1:48Nitaanza
-
1:49 - 1:51Kwa kuonyesha mwisho wake:
-
1:51 - 1:53Na nitawathibitishia kwamba
-
1:53 - 1:55yasiyowezekana siyo hayawezekani
-
1:55 - 1:58Na nitamalizia kwa kuwapa
zawadi yenye kustahili kuieneza: -
1:58 - 2:01Nitawaonyesha kwamba unaweza
kufanya yasiyowezekana maishani mwako. -
2:03 - 2:05katika kutafuta kufanya yasiyowezekana,
nimegundua kuna -
2:05 - 2:08mambo mawili yanayofanana
kati ya watu duniani. -
2:08 - 2:10Kila mtu ana hofu,
-
2:10 - 2:12na kila mtu ana ndoto.
-
2:13 - 2:18Katika kutafuta kufanya yasiyowezekana
nimegundua kuna vitu vitatu -
2:18 - 2:20ambavyo nimevifanya miaka mingi ambavyo
-
2:20 - 2:23vimenisababishia kufanya yasiyowezekana:
-
2:24 - 2:27Mchezo wa mpira wa kuchenga au "Trefball"
-
2:27 - 2:28Superman,
-
2:28 - 2:29na Mbu
-
2:29 - 2:31Hayo ni maneno yangu matatu makuu.
-
2:31 - 2:34Mmeshajua kwanini nafanya
yasiyowezekana maishani mwangu -
2:34 - 2:36Hivyo nitawachukua katika safari
yangu, ya mwendo mrefu -
2:36 - 2:39kutoka kwenye hofu hadi ndoto
-
2:39 - 2:41kutoka kwenye maneno hadi panga,
-
2:41 - 2:43Kutoka Mpira wa kuchenga
-
2:43 - 2:44hadi Superman
-
2:44 - 2:45hadi kwa Mbu
-
2:46 - 2:47Na ninatumaini kuwaonyesha
-
2:47 - 2:50unawezaje kufanya yasiyo
wezekana maishani mwako -
2:52 - 2:55Oktoba 4, mwaka 2007.
-
2:56 - 2:58Moyo wangu ulienda mbio,
magoti yangu yalitetema -
2:58 - 2:59nilipokuwa napanda jukwaani
-
2:59 - 3:01kwenye ukumbi wa Sanders
-
3:01 - 3:03Chuo cha Harvard kupokea
-
3:03 - 3:06Tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu
-
3:06 - 3:09kwa kushiriki kuandika ikisiri
ya utafiti wa kitabibu -
3:09 - 3:10ulioitwa "Kumeza Upanga...
-
3:10 - 3:12...na Athari zake"
-
3:12 - 3:13(Kicheko)
-
3:14 - 3:18Ilichapishwa kwenye jarida dogo
ambalo sikuwahi kulisoma kabla, -
3:18 - 3:20Jarida la Kitabibu la Uingereza.
-
3:21 - 3:25Na kwangu, hiyo ilikuwa ndoto
isiyowezekana kuwa kweli, -
3:25 - 3:28ilikuwa ni mshangao usiotegemewa
kwa mtu kama mimi, -
3:28 - 3:31ilikuwa ni heshima ambayo sitaweza kusahau
-
3:31 - 3:35Lakini haikuwa sehemu ya kubwa ya
kukumbuka maishani mwangu. -
3:36 - 3:38Mnamo Oktoba 4, mwaka 1967
-
3:38 - 3:40kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba
-
3:41 - 3:43aliteseka na hofu kubwa kupita kiasi.
-
3:43 - 3:46Alipojiandaa kupanda jukwaani,
-
3:46 - 3:47moyo wake ulienda mbio,
-
3:48 - 3:49magoti yake yalikuwa yakitetemeka.
-
3:50 - 3:52Alikwenda kufungua kinywa chake kuongea,
-
3:56 - 3:58maneno hayakuweza kutoka.
-
3:58 - 4:00Alisimama akitetemeka na kutoa machozi.
-
4:01 - 4:02Alipooza kwa mshtuko wa ghafla,
-
4:02 - 4:04alipatwa fadhaa kwa hofu.
-
4:04 - 4:06huyu kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba
-
4:06 - 4:08alitesekana na hofu kubwa kupita kiasi.
-
4:09 - 4:10Alikuwa na hofu ya giza,
-
4:11 - 4:12hofu ya vimo virefu,
-
4:12 - 4:13hofu ya buibui na nyoka ...
-
4:13 - 4:15Kuna yeyote anayeogopa buibui na nyoka?
-
4:15 - 4:17Naam, wachache wenu ...
-
4:17 - 4:19Alikuwa na hofu ya maji na papa ...
-
4:19 - 4:22Hofu ya madaktari na manesi na madaktari
wa meno, -
4:22 - 4:25na sindano na kutobolewa na vitu vya
ncha kali. -
4:25 - 4:27Lakini zaidi ya chochote,
alikuwa na hofu ya -
4:27 - 4:28watu
-
4:29 - 4:32Huyo kijana mwoga,mwenye aibu na mwembamba
-
4:32 - 4:33alikuwa mimi.
-
4:33 - 4:36Nilikuwa na hofu ya kushindwa na
kukataliwa, -
4:37 - 4:40kutojithamini, kujiona duni,
-
4:40 - 4:43na kitu ambacho hata hatukujua
unaweza kujiandikisha kwa siku hizo: -
4:43 - 4:45ugonjwa wa hofu ya ukaribu na watu.
-
4:45 - 4:49Kwa sababu nilikuwa na hofu, waonevu
walinitania na kunipiga. -
4:49 - 4:52Walinicheka na kuniita majina,
Hawakuniruhusu kucheza nao -
4:52 - 4:54michezo ya aina yoyote.
-
4:55 - 4:58Ah, kulikuwa na mchezo mmoja
walikuwa wakiruhusu kucheza kwenye ... -
4:58 - 4:59Mpira wa kuchenga -
-
5:00 - 5:01na sikuwa mchengaji nzuri.
-
5:02 - 5:04Waonevu waliita jina langu,
-
5:04 - 5:06na nilipoangalia
niliona mipira myekundu ya kukwepa -
5:06 - 5:08ikivurumishwa usoni wangu kwa kasi kubwa
-
5:08 - 5:10bam, bam, bam!
-
5:11 - 5:13Ninakumbuka siku nyingi
nikirudi nyumbani kutoka shule, -
5:13 - 5:18uso wangu ulikuwa mwekundu ukichonyota,
masikio yangu yalikuwa mekundu yakivuma. -
5:18 - 5:21Macho yangu yalichoma kwa machozi,
-
5:21 - 5:24na maneno yao yalichoma masikioni mwangu.
-
5:24 - 5:25Na yeyote aliyesema,
-
5:25 - 5:29"Fimbo na mawe vyaweza kunivunja mifupa,
bali maneno hayatoniumiza kamwe "... -
5:29 - 5:30Ni uongo.
-
5:30 - 5:32Maneno huweza kukata kama kisu.
-
5:32 - 5:34Maneno huweza kupenya kama upanga.
-
5:34 - 5:36Maneno huwezafanya majeraha yenye kina
-
5:36 - 5:38yasiweze kuonekana.
-
5:38 - 5:41Hivyo nilikuwa na hofu.
Na maneno yalikuwa adui yangu mkubwa. -
5:41 - 5:42Bado ni adui yangu.
-
5:43 - 5:45Lakini pia nilikuwa na ndoto.
-
5:45 - 5:48Nilienda nyumbani
na kutorokea kwenye futuhi za Superman -
5:48 - 5:50na nilisoma futuhi za Superman
-
5:50 - 5:53na niliota kutaka kuwa shujaa mkubwa
kama Superman. -
5:53 - 5:56Nilitaka kupigania kweli na haki,
-
5:56 - 5:59Nilitaka kupambana dhidi ya
wahalifu na mahasimu, -
5:59 - 6:03Nilitaka kupaa duniani kote
kufanya vitendo vya ujasiri kuokoa maisha. -
6:03 - 6:06Nilikuwa pia navutiwa mno
na vitu vilivyokuwa kweli. -
6:06 - 6:09Nilisoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness
na kitabu cha Ripley kiitwacho Amini au Usiamini. -
6:09 - 6:13Yeyote kati yenu amewahi kusoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness au kitabu cha Ripley?
-
6:13 - 6:14Navipenda vitabu hivi!
-
6:14 - 6:16Niliona watu wafanyao ujasiri halisia.
-
6:16 - 6:18Nikasema, Nataka kufanya hivyo.
-
6:18 - 6:19Ikiwa waonevu hawataniruhusu
-
6:19 - 6:21kucheza katika michezo yao yoyote,
-
6:21 - 6:23Nataka kufanya maajabu, ujasiri halisi.
-
6:23 - 6:27Nataka kufanya kitu cha kusifika
ambacho hao waonevu hawawezi kufanya. -
6:27 - 6:29Nataka kupata kusudi langu na wito wangu,
-
6:29 - 6:31Nataka kujua kuwa maisha yangu yana maana,
-
6:31 - 6:33Nataka kufanya kitu cha kushangaza
kubadili ulimwengu; -
6:33 - 6:37Ninataka kuthibitisha
yasiyowezekana sio hayawezekani. -
6:38 - 6:40Kupeleka mbele miaka 10 -
-
6:40 - 6:43Ilikuwa wiki kabla ya kutimiza miaka 21.
-
6:43 - 6:47Mambo mawili yalitokea kwa siku moja
ambayo yangebadilisha maisha yangu milele. -
6:47 - 6:49Nilikuwa nikiishi Tamil Nadu, India Kusini
-
6:50 - 6:51Nilikuwa mmishonari huko,
-
6:51 - 6:53na mshauri wangu, rafiki yangu aliniuliza,
-
6:53 - 6:55"Je, una Thromu, Daniel?"
-
6:55 - 6:57Na nikasema, "Thromu?
Thromu ni nini? " -
6:57 - 7:00Alisema, "Thromu ni malengo makuu ya
maisha. -
7:00 - 7:05Ni muunganiko
wa ndoto na malengo, kama ungeweza -
7:05 - 7:07kufanya chochote unachotaka,
kwenda popote unapotaka -
7:07 - 7:08kuwa mtu yeyote unayetaka,
-
7:08 - 7:10ungekwenda wapi?
Ungefanya nini? -
7:10 - 7:11Ungekuwa nani?
-
7:11 - 7:14Nikasema, "Siwezi kufanya hivyo!
Naogopa sana! Naogopa mengi mno! " -
7:14 - 7:18Usiku huo nilichukua mkeka wangu wa mchele
juu ya paa la ghorofa, -
7:18 - 7:19nikautandika chini ya nyota,
-
7:19 - 7:22na kuangalia popo wakiwashambulia mbu.
-
7:22 - 7:26Na yote niliyofikiria ilikuwa thromu,
na ndoto na malengo, -
7:26 - 7:28na wale washujaaji wenye mipira ya kuchenga.
-
7:29 - 7:31Masaa machache baadaye niliamka.
-
7:31 - 7:34Moyo wangu ulienda mbio,
magoti yangu yakitetemeka. -
7:34 - 7:36Safari hii haikuwa na hofu.
-
7:36 - 7:38Mwili wangu wote ulitikisika.
-
7:38 - 7:40Na kwa siku tano zilizofuata
-
7:40 - 7:44Nilipoteza na kurudisha fahamu,
kitandani nikipigania maisha yangu. -
7:44 - 7:48Ubongo wangu ulikuwa unawaka
na homa ya malaria yenye jotoridi la 105. -
7:48 - 7:52Na kila fahamu ziliponirudia,
nilichowaza ilikuwa kuhusu thromu. -
7:52 - 7:54Niliwaza
"Nataka kufanya nini na maisha yangu?" -
7:54 - 7:56Hatimaye, usiku kabla
sijafikisha miaka 21, -
7:56 - 7:58katika wakati wa kuelewa,
-
7:58 - 8:00Nilikuja kutambua:
-
8:00 - 8:02Nilitambua kwamba yule mbu mdogo,
-
8:03 - 8:05Anofelesi Stefensi,
-
8:05 - 8:07yule mbu mdogo
-
8:07 - 8:08aliye na uzito chini ya mikrogramu 5
-
8:08 - 8:10chini ya punje ya chumvi,
-
8:10 - 8:13anaweza kuangusha
mtu wa ratili 170, mtu wa kilo 80, -
8:13 - 8:15Niligundua kwamba alikuwa hasimu wangu.
-
8:15 - 8:17Kisha nikagundua,
hapana, hapana, sio mbu, -
8:17 - 8:19Ni vimelea vidogo
ndani ya mbu, -
8:19 - 8:23Plasmodium Falciparum,
ambao huua zaidi ya watu milioni kwa mwaka -
8:24 - 8:26Kisha nikagundua
Hapana, hapana, tena ni ndogo zaidi, -
8:26 - 8:29lakini kwangu, ilionekana kubwa zaidi.
-
8:29 - 8:30Niligundua,
-
8:30 - 8:31hofu ilikuwa hasimu yangu,
-
8:31 - 8:32vimelea yangu,
-
8:32 - 8:35vilivyonitia ulemavu
na kunipooza mimi maisha yangu yote. -
8:35 - 8:38Unajua, kuna tofauti
kati ya hatari na hofu. -
8:38 - 8:40Hatari ni halisi.
-
8:40 - 8:42Hofu ni hiari.
-
8:42 - 8:44Na nikagundua kuwa nina hiari:
-
8:44 - 8:48Aidha niishi kwa hofu,
na kufa katika kushindwa usiku ule, -
8:49 - 8:52au ningeweza kuua hofu yangu,
na ningeweza -
8:52 - 8:56kufikia ndoto zangu,
Ningeweza kuthubutu kuishi maisha. -
8:57 - 9:00Na unajua, kuna kitu kuhusu
kuwa kwenye kitanda cha mauti -
9:00 - 9:04na kukabiliwa na kifo ambacho haswa
kinakufanya utake kweli kuishi maisha. -
9:04 - 9:07Nikagundua kuwa kila mtu hufa,
si kila mtu huishi. -
9:08 - 9:10Ni katika kufa ndio sisi tunaishi.
-
9:10 - 9:12Unajua, wakati unapojifunza kufa,
-
9:12 - 9:13unajifunza kweli kuishi.
-
9:13 - 9:15Kwa hiyo nikaamua nitaenda kubadilisha
-
9:15 - 9:16hadithi yangu usiku huo.
-
9:17 - 9:18Sikutaka kufa.
-
9:18 - 9:20Hivyo nikafanya sala ndogo, nikasema,
-
9:20 - 9:22"Mungu, ukiniruhusu niishi
nifikishe miaka 21, -
9:22 - 9:25Sitaruhusu hofu
itawale maisha yangu tena. -
9:25 - 9:27Nitaziweka hofu zangu kifoni,
-
9:27 - 9:30Nitaenda kuzifikia ndoto zangu,
-
9:30 - 9:31Ninataka kubadilisha mtazamo wangu,
-
9:31 - 9:34Nataka kufanya kitu cha ajabu
na maisha yangu, -
9:34 - 9:36Nataka kupata kusudi langu na wito wangu,
-
9:36 - 9:39Ninataka kujua kuwa yasiyowezekana
si hayawezekani. " -
9:39 - 9:43Sitawaambia kama nilinusurika usiku ule;
Nitawaacha mfikirie. -
9:43 - 9:44(Kicheko)
-
9:44 - 9:47Lakini usiku huo niliandika orodha
ya Thromu zangu 10 za kwanza: -
9:47 - 9:50Niliamua nilitaka
kutembelea mabara makubwa -
9:50 - 9:52kutembelea Maajabu 7 ya Dunia
-
9:52 - 9:53kujifunza lugha nyingi,
-
9:53 - 9:55kuishi kwenye kisiwa kitupu,
-
9:55 - 9:56kuishi kwenye meli baharini,
-
9:56 - 9:59kuishi na kabila la Wahindi
katika Amazon, -
9:59 - 10:01kupanda hadi juu
ya mlima mrefu kuliko yote Sweden, -
10:01 - 10:03Nilitaka kuona mawio Mlima Everest,
-
10:03 - 10:05kufanya kazi na biashara ya muziki
Nashville, -
10:05 - 10:07Nilitaka kufanya kazi ya sarakasi,
-
10:07 - 10:09na nilitaka kuruka nje ya ndege.
-
10:09 - 10:12Zaidi ya miaka ishirini iliyofuata,
Nilitimiza thromu hizo kwa wingi. -
10:12 - 10:15Kila wakati niliondoa
thromu kwenye orodha yangu, -
10:15 - 10:18Niliongeza 5 au 10 zaidi kwenye orodha
na orodha yangu iliendelea kukua. -
10:19 - 10:23Kwa miaka saba iliyofuata, niliishi
kwenye kisiwa kidogo katika Bahamas -
10:23 - 10:25kwa karibu miaka saba
-
10:25 - 10:27katika kibanda cha makuti,
-
10:29 - 10:34nikiwinda papa na taa wa kula,
nikiwa mtu pekee kwenye kisiwa, -
10:34 - 10:36nikiwa nimevaa msuli,
-
10:37 - 10:39na nikajifunza kuogelea na papa.
-
10:39 - 10:41Na kutoka huko, nikahamia Mexico,
-
10:41 - 10:45na kisha nikasafiri
kwa bonde la Mto Amazon nchini Ecuador, -
10:45 - 10:48Pujo Pongo Ecuador,
niliishi na kabila moja huko, -
10:48 - 10:52na kidogo kidogo nilianza kuongeza
kujiamini kwa thromu zangu tu. -
10:52 - 10:55Nilihamia biashara ya muziki Nashville,
kisha Sweden, -
10:55 - 10:58nikahamia Stockholm,
kufanyakazi katika biashara ya muziki, -
10:58 - 11:02ambapo nilipanda kilele cha Ml. Kebnekaise
juu ya mzunguko wa Arctic. -
11:03 - 11:05Nilijifunza udamisi,
-
11:05 - 11:06na viinimacho,
-
11:06 - 11:07na kutembea kama ngongoti,
-
11:07 - 11:10kuendesha baiskeli kwa tairi moja,
kula moto, kula kioo. -
11:10 - 11:14Mwaka 1997 nilisikia kuna
wameza panga wasiozidi kumi na mbili -
11:14 - 11:15na nikasema, "Inabidi kufanya hivyo!"
-
11:15 - 11:18Nilikutana na mmeza panga,
na nikamwomba vidokezo. -
11:18 - 11:20Akasema, "Naam, nitakupa vidokezo 2:
-
11:20 - 11:22Namba 1: Ni hatari sana,
-
11:22 - 11:24Watu wamekufa wakifanya hivi.
-
11:24 - 11:25Namba 2:
-
11:25 - 11:26Usijaribu! "
-
11:26 - 11:28(Kicheko)
-
11:28 - 11:30Basi nikaiongeza kwenye orodha ya thromu.
-
11:30 - 11:33Na nikafanya mazoezi
mara 10 hadi 12 kwa siku, kila siku -
11:34 - 11:35kwa miaka minne.
-
11:35 - 11:37Sasa nilipigia hesabu hizo...
-
11:37 - 11:404 x 365 [x 12]
-
11:40 - 11:43Ilikuwa karibu 13,000
majaribio yasiyofanikiwa -
11:43 - 11:45kabla sijatia panga langu wa kwanza
chini koo mwaka 2001. -
11:46 - 11:48Wakati huo nikaweka thromu
-
11:48 - 11:51kuwa mtaalamu wa ulimwengu
kwa kumeza panga. -
11:51 - 11:54Basi nilitafuta kila kitabu,
gazeti, makala ya gazeti, -
11:54 - 11:58kila ripoti ya kitabibu,
Nilijifunza fiziolojia, anatomia, -
11:58 - 12:00Niliongea na madaktari na manesi,
-
12:00 - 12:02niliwakutanisha wameza panga wote
pamoja -
12:02 - 12:04kwenye Shirikisho la Wameza Panga
Kimataifa, -
12:04 - 12:06nikafanya ikisiri miaka 2
ya utafiti kitabibu -
12:06 - 12:09kuhusu Umezaji wa Panga na athari zake
-
12:09 - 12:11iliyochapishwa
katika Jarida la Kitabibu Uingereza. -
12:11 - 12:12(Kicheko)
-
12:12 - 12:13Asanteni.
-
12:13 - 12:18(Makofi)
-
12:18 - 12:22Na nilijifunza mambo ya kuvutia sana
kuhusu umezaji wa panga. -
12:22 - 12:25Vitu vingine ambavyo haujawahi kufikiria
kabla, hutasahau baada ya usiku huu. -
12:25 - 12:29Wakati utakapoenda nyumbani, na unakata
steki yako na kisu chako -
12:29 - 12:32au panga, au "bestek" zako,
utafikiri juu ya hili ... -
12:34 - 12:37Nilijifunza kwamba umezaji panga
ulianzia India - -
12:37 - 12:40mahali nilipona kwa mara ya kwanza
nikiwa kijana wa miaka 20 - -
12:40 - 12:42karibu miaka 4000 ya kale, karibu 2000 BC.
-
12:42 - 12:46Zaidi ya miaka 150 iliyopita,
wameza panga walitumika -
12:46 - 12:47katika medani za sayansi na kitabibu
-
12:47 - 12:51ili kusaidia kuunda
endoskopia imara mwaka 1868 -
12:51 - 12:54wakiwa na Dk. Adolf Kussmaul wa Freiburg, Ujerumani
-
12:54 - 12:57Mnamo 1906, elektrokadiogramu huko Wales,
-
12:57 - 13:00kujifunza matatizo ya kumeza,
na mmeng'enyo wa chakula, -
13:00 - 13:02aina ya bronkoskopia, .
-
13:02 - 13:04Lakini zaidi ya miaka 150 iliyopita,
-
13:04 - 13:08tunajua mamia ya madhara
na vifo kadhaa ... -
13:08 - 13:15Hii ni endoskopia imara
iliyoanzishwa na Dk. Adolph Kussmaul. -
13:15 - 13:19Lakini tuligundua kuwa kulikuwa na
Vifo 29 zaidi ya miaka 150 iliyopita. -
13:19 - 13:22pamoja na mmezaji panga huko London
aliyetoboa moyo wake kwa panga -
13:23 - 13:25Tulijifunza pia kuwa kuna kesi tatu hadi nane za
-
13:25 - 13:28madhara mkubwa ya umezaji panga
kila mwaka. -
13:28 - 13:30Najua kwa sababu mimi hupata simu.
-
13:30 - 13:31Nilikuwa na wawili,
-
13:31 - 13:34mmoja kutoka Sweden, na kutoka Orlando
wiki chache zilizopita, -
13:34 - 13:37wamezaji panga waliopo hospitalini
kutokana na madhara. -
13:37 - 13:39Kwa hiyo ni hatari sana.
-
13:39 - 13:42Jambo jingine nililojifunza ni kuwa
kumeza panga huchukua -
13:42 - 13:44miaka 2 hadi miaka 10
kujifunza jinsi ya kumeza panga -
13:44 - 13:46kwa watu wengi.
-
13:46 - 13:48Lakini ugunduzi unaovutia sana
Nilijifunza ilikuwa -
13:48 - 13:51jinsi wameza panga wanavyojifunza
kufanya yasiyowezekana. -
13:51 - 13:53Nami nitawapa siri ndogo:
-
13:54 - 13:58Usizingatie kwenye asilimia 99.9
kuwa haiwezekani. -
13:58 - 14:02Unazingatia hiyo 1% ambayo inawezekana,
na fikiria jinsi ya kufanya iwezeikane -
14:03 - 14:06Sasa napenda kukupeleka kwenye safari
ndani ya akili ya mmeza panga. -
14:06 - 14:09Ili kumeza panga,
inahitaji akili itafakari jambo, -
14:09 - 14:12uzingativu wa hali ya juu,
kuonyesha ufasaha ili -
14:12 - 14:16kutenganisha viungo vya ndani vya mwili
na kushinda vitendo hiari mwilini -
14:16 - 14:20kupitia njia ya ubongo iliyoimarishwa,
kupitia marido ya kumbukumbu ya misuli -
14:20 - 14:24kwa mazoezi ya makusudi
zaidi ya mara 10,000. -
14:24 - 14:28Sasa ngoja niwasafirishe kidogo
ndani ya mwili wa mmeza panga -
14:28 - 14:30Ili kumeza panga,
-
14:30 - 14:32Lazima niteleze panga juu ya ulimi wangu,
-
14:32 - 14:35nizuie kutaka kutapika
kwenye shingo ya umio, -
14:35 - 14:38zungusha mgeuko wa nyuzi 90
chini ya gegedu ya ulimi, -
14:38 - 14:41pitia kwenye msuli juu ya kilinda umio,
-
14:41 - 14:43zuia vitendohiari vya tumbo,
-
14:43 - 14:44telezea makali kwenye shimo la kifua
-
14:44 - 14:46kati ya mapafu.
-
14:46 - 14:48Katika hatua hii,
-
14:48 - 14:50Lazma kweli nisukume moyo wangu pembeni.
-
14:50 - 14:52Ikiwa utaangalia kwa makini,
-
14:52 - 14:54unawezaona moyo ukidunda kwa panga langu
-
14:54 - 14:56kwa sababu linaegemea moyo
-
14:56 - 14:59ikitenganishwa na karibu thumuni ya inchi
ya tishu ya umio. -
14:59 - 15:01Hicho sio kitu unaweza kudanganya.
-
15:01 - 15:03Kisha hutelezesha
kupita mfupa wa kifua, -
15:03 - 15:06kupita kilinda umio,
chini ndani ya tumbo, -
15:06 - 15:09zuia vitendohiari ndani ya tumbo
njia yote hadi kwenye mbuti. -
15:09 - 15:10Rahisi sana.
-
15:10 - 15:11(Kicheko)
-
15:11 - 15:13Kama ningetakiwa kwenda zaidi ya hapo,
-
15:13 - 15:18hadi kufikia mirija yangu ya mayai.
mirija ya mayai! (Kidachi) -
15:18 - 15:21Wanaume, mnaweza kuwauliza wake zenu
kuhusu hiyo baadaye ... -
15:22 - 15:24Watu huniuliza, wanasema,
-
15:24 - 15:27"lazima kuchukua ujasiri mwingi
ili kuhatarisha maisha yako, -
15:27 - 15:29kusogeza moyo wako,
na kumeza panga ... " -
15:29 - 15:30Hapana. Kinachofanya ujasiri halisi
-
15:30 - 15:33ni kwa yule kijana mwoga, mwenye aibu,
mwembamba -
15:33 - 15:36kwa kuhatarisha kushindwa na kukataliwa,
-
15:36 - 15:37kufungua moyo wake,
-
15:37 - 15:38na kumeza kiburi chake
-
15:38 - 15:41na kusimama hapa mbele
ya kundi la watu asiowafahamu kabisa -
15:41 - 15:44na kukuambia hadithi yake
kuhusu hofu na ndoto zake, -
15:44 - 15:48kwa hatarisha kumwaga habari zake,
vyote kihalisia na kitamathali. -
15:48 - 15:49Unaona - asante.
-
15:49 - 15:54(Makofi)
-
15:54 - 15:56Unaona, jambo la kustaajabisha sana ni
-
15:56 - 15:59Nimetaka kufanya mambo
ya kusifika maishani mwangu -
15:59 - 16:00na sasa nimesifika.
-
16:00 - 16:03Lakini jambo la kusifika haswa
sio kwamba ninaweza kumeza -
16:03 - 16:05panga 21 kwa mara moja,
-
16:08 - 16:10au futi 20 chini ya maji kwenye tanki
la papa 88 na taa -
16:10 - 16:12kwa kitabu cha Amini au Usiamini,
-
16:14 - 16:18au kuchowa hadi kuwa mwekundu nyuzi 1500
kwa Watu jasiri wa Stan Lee -
16:18 - 16:19kama "Mtu wa Chuma"
-
16:20 - 16:22na yule jamaa alikuwa moto!
-
16:22 - 16:25Au kuvuta gari kwa upanga kwa Ripley,
-
16:25 - 16:26au Guinness,
-
16:26 - 16:29au kufikia fainali za
shindano la vipaji Marekani, -
16:29 - 16:32au kushinda 2007
tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu. -
16:32 - 16:34La, hilo sio
jambo la kusifika sana. -
16:34 - 16:36Hivyo ndio watu wanafikiria.
La, la, la. Sio hivyo. -
16:36 - 16:38Jambo la kusifika sana
-
16:38 - 16:41ni Mungu angemchukua kijana,
mwoga, mwenye aibu mwembamba -
16:41 - 16:42aliyehofia vimo virefu,
-
16:42 - 16:44aliyehofia ya maji na papa,
-
16:44 - 16:46na madaktari na manesi
na sindano na vyenye ncha kali -
16:46 - 16:48na kuzungumza na watu
-
16:48 - 16:50na sasa ananifanya
nipae duniani kote -
16:50 - 16:51katika kina cha futi 30,000
-
16:51 - 16:54kumeza vitu vya ncha
chini ya maji ya tanki ya papa, -
16:54 - 16:57na kuzungumza na madaktari na wauguzi
na hadhira kama ninyi duniani -
16:57 - 17:00Hilo ni jambo la kustaajabu sana kwangu.
-
17:00 - 17:01Nimetaka kufanya mambo yasiyowezekana -
-
17:01 - 17:02Asante.
-
17:02 - 17:04(Makofi)
-
17:04 - 17:05Asante.
-
17:06 - 17:09(Makofi)
-
17:10 - 17:13Sikuzote nilitaka kufanya yasiyowezekana,
na sasa nimeweza. -
17:13 - 17:16Nilitaka kufanya kitu cha kusifika
maishani na kubadilisha ulimwengu, -
17:16 - 17:17na sasa nimeweza.
-
17:17 - 17:20Siku zote nilitaka kupaa duniani kote
kufanya vitendo vigumu -
17:20 - 17:21na kuokoa maisha, sasa nimeweza.
-
17:21 - 17:23Na unajua nini?
-
17:23 - 17:26Bado kuna sehemu ndogo
ya ndoto kubwa ya yule mtoto mdogo -
17:26 - 17:27ndani kabisa.
-
17:30 - 17:36(Kicheko) (Makofi)
-
17:37 - 17:40Na unajua, sikuzote nilitaka kupata
kusudi langu na wito wangu, -
17:40 - 17:42na sasa nimepata.
-
17:42 - 17:43Lakini nadhani nini?
-
17:43 - 17:46Si kwa panga,
sio unavyofikiria, si kwa nguvu zangu. -
17:46 - 17:49Ni kwa udhaifu wangu, maneno yangu.
-
17:49 - 17:51Kusudi langu na wito
ni kubadili ulimwengu -
17:51 - 17:52kwa kukata kupitia hofu,
-
17:52 - 17:55upanga mmoja kwa wakati, neno moja
kwa wakati, -
17:55 - 17:57kisu moja kwa wakati, maisha kwa wakati,
-
17:58 - 18:00kuhamasisha watu kuwa mashujaa
-
18:00 - 18:02na kufanya yasiyowezekana maishani mwao.
-
18:02 - 18:05Kusudi langu ni kusaidia wengine
kupata yao. -
18:05 - 18:06La kwako ni lipi?
-
18:06 - 18:07Nini kusudi lako?
-
18:07 - 18:09Uliwekwa kufanya nini hapa?
-
18:09 - 18:12Naamini sisi wote
tumeitwa kuwa mashujaa. -
18:12 - 18:14Nguvu yako kubwa ni nini?
-
18:15 - 18:18Kati ya idadi ya watu duniani
ya watu zaidi ya bilioni 7, -
18:18 - 18:20kuna wameza upanga
wachache sana -
18:20 - 18:22waliobakia duniani kote leo,
-
18:22 - 18:23lakini kuna wewe mmoja.
-
18:23 - 18:24Wewe ni wa pekee.
-
18:24 - 18:26Hadithi yako ni nini?
-
18:26 - 18:28Nini kinakufanya uwe tofauti?
-
18:28 - 18:29Simulia hadithi yako,
-
18:29 - 18:32hata kama sauti yako ni nyembamba
na inatetemeka. -
18:32 - 18:33Je, thromu zako ni nini?
-
18:33 - 18:36kama ungefanya chochote,
kuwa yeyote, kwenda popote - -
18:36 - 18:37Ungefanya nini?
Ungekwenda wapi? -
18:37 - 18:38Ungefanya nini?
-
18:38 - 18:40Unataka kufanya nini na maisha yako?
-
18:40 - 18:42Nini ndoto zako kubwa?
-
18:42 - 18:44Nini ndoto zako kubwa ulipokuwa mdogo?
Fikiria tena -
18:44 - 18:46Nina uhakika hii haikuwa hivyo, si ndiyo?
-
18:46 - 18:48Nini zilikuwa ndoto zako
kuu -
18:48 - 18:50ulizofikiri zilikuwa ajabu sana
na zisizoeleweka? -
18:50 - 18:54Hakika hii inafanya ndoto zako zisionekane
za ajabu tena, sivyo? -
18:55 - 18:57Upanga wako ni nini?
-
18:57 - 18:59Kila mmoja wenu ana upanga,
-
18:59 - 19:01upanga wa pande mbili wa hofu na ndoto.
-
19:01 - 19:04Meza upanga wako, chochote utachokuwa.
-
19:04 - 19:06Fuata ndoto zako, mabibi na mabwana,
-
19:06 - 19:09Hujachelewa sana kuwa
chochote unataka kuwa. -
19:10 - 19:13Kwa wale waonevu na mipira ya kukwepa,
wale watoto waliodhani -
19:13 - 19:15kuwa sitaweza kufanya yasiyowezekana,
-
19:15 - 19:18Nina kitu kimoja tu cha kuwaambia:
-
19:18 - 19:19Asanteni.
-
19:19 - 19:22Kwa sababu kama si kwa wahalifu,
tusingekuwa kuwa na mashujaa. -
19:23 - 19:27Nipo hapa kuthibitisha
yasiyowezekana si hayawezekani. -
19:28 - 19:32Hii ni hatari sana,
Inaweza kuniua. -
19:32 - 19:34Natumaini mtafurahia.
-
19:34 - 19:35(Kicheko)
-
19:36 - 19:39Nitahitaji msaada wenu kwenye hili.
-
19:47 - 19:48Hadhira:Mbili, tatu.
-
19:48 - 19:52Dan Meyer:La, la, la. Nahitaji msaada wenu
kwenye kuhesabu, nyote, sawa? -
19:52 - 19:53(Vicheko)
-
19:53 - 19:56Kama unajua maneno? Sawa?
Hesabu na mimi. Tayari? -
19:56 - 19:57Moja.
-
19:57 - 19:58Mbili.
-
19:58 - 19:59Tatu.
-
19:59 - 20:01La, hiyo ni 2, lakini mmeelewa
-
20:07 - 20:08Hadhira: Moja.
-
20:08 - 20:09Mbili.
-
20:09 - 20:10Tatu.
-
20:11 - 20:13(Vuta pumzi)
-
20:14 - 20:16(Makofi)
-
20:16 - 20:17DM: Ndiyo!
-
20:17 - 20:23(Makofi) (Kushangilia)
-
20:23 - 20:25Asanteni sana.
-
20:25 - 20:29Asante, asante, asante.
Asante kutoka kina cha moyo wangu -
20:29 - 20:31Kweli, asante
kutoka chini ya tumbo langu. -
20:32 - 20:35Niliwaambia nimekuja hapa kufanya
yasiyowezekana, na sasa nimeweza. -
20:35 - 20:38Ila hii haikuwa isiyowezekana.
Ninafanya hivi kila siku. -
20:38 - 20:43Kitu kisichowezekana ilikuwa yule mwoga,
mwenye aibu mwembamba kukabili hofu zake -
20:43 - 20:45kusimama hapa kwenye jukwaa la [TEDx],
-
20:45 - 20:47na kubadilisha dunia,
neno moja kwa wakati, -
20:47 - 20:49upanga kwa wakati, maisha kwa wakati.
-
20:49 - 20:52kama nimekufanya ufikiri kwa njia mpya,
kama nimekufanya uamini -
20:52 - 20:54yasiyowekana si hayawezekani,
-
20:54 - 20:58ikiwa nimekufanya uelewe kuwa waweza
fanya yasiyowezekana maishani mwako, -
20:58 - 21:01basi kazi yangu imekwisha,
na yako ndiyo kwanza imeanza. -
21:01 - 21:04Usiache kuwa na ndoto. Usiache kuamini.
-
21:05 - 21:06Asanteni kwa kuniamini
-
21:06 - 21:08na asanteni kuwa sehemu
ya ndoto yangu. -
21:08 - 21:10Hii ni zawadi kwenu:
-
21:10 - 21:11Yasiyowezekana si ...
-
21:11 - 21:13Hadhira: Hayawezekani.
-
21:13 - 21:15Mwendo mrefu ni sehemu ya zawadi.
-
21:15 - 21:20(Makofi)
-
21:20 - 21:21Asanteni.
-
21:21 - 21:25(Makofi)
-
21:26 - 21:28(Kushangilia)
-
21:28 - 21:31Mwenyeji: Asante, Dan Meyer, wow!
- Title:
- Doing the Impossible, swallowing the sword, cutting through fear | Dan Meyer | TEDxMaastricht
- Description:
-
Did you ever want to become a superhero, do the impossible and change the world?
As humans, we’re hard-wired for fear – to flee, fight or freeze in the face of danger. But can we learn to face our fears and overcome failure to do the impossible? Dan Meyer believes no matter how extreme our fears or how wild our dreams, we each have the potential to overcome our fears to become superheroes, do the impossible and change the world.
Director of a humanitarian aid agency in Kazakhstan, Meyer shares how he overcame a childhood of extreme fears, social anxiety disorder and bullying to do superhuman feats, become a finalist on America's Got Talent, win the 2007 Ig Nobel Prize in Medicine at Harvard, and become a 40x world record holder and world’s leading expert in one of the world's oldest and most dangerous arts - sword swallowing - and passionate about inspiring people to do the impossible in THEIR lives.
In this surprising and revealing TED talk, Meyer takes the audience on his journey from extreme fears to feats, wimp to world record holder, loser to Ig Nobel Prize winner and quitter to finalist on America's Got Talent. He reveals secrets behind the ancient art and science of sword swallowing, and describes his quest to cut through fear to overcome failure and the limitations of the human body to perform superhuman feats, do the impossible and change the world. He reveals tips on how YOU can do the impossible in YOUR life, and in a surprising ending, he attempts to do the impossible right before your eyes.
Dan Meyer @Halfdan
http://cuttingedgeinnertainment.comTEDxMaastricht:
http://tedxmaastricht.nlThis talk was given at a TEDx event using the TED conference format but independently organized by a local community. Learn more at http://ted.com/tedx
- Video Language:
- English
- Duration:
- 21:39