0:00:08.380,0:00:09.561 Asante 0:00:16.270,0:00:21.200 Palikuwa na mfalme nchini India, Maharaja [br]na siku yake ya kuzaliwa ilitolewa amri 0:00:21.200,0:00:24.200 kwamba machifu wote walete[br]zawadi kwa mfalme. 0:00:24.400,0:00:28.370 Wengine wakaleta hariri bora,[br]wengine wakaleta panga maridadi, 0:00:28.370,0:00:29.490 wengine dhahabu 0:00:29.490,0:00:32.659 mwisho wa mstari alikuja akitembea[br]mzee mdogo mwenye makunyanzi 0:00:32.659,0:00:36.630 ambaye alitembea kutoka kijijini kwake[br]kwa safari ya siku nyingi kando ya bahari. 0:00:36.630,0:00:41.150 alipokuwa akisogea mwana mfalme akauliza,[br]'Umemletea zawadi gani Mfalme?' 0:00:41.457,0:00:44.750 Na mzee yule taratibu sana[br]akakunjua mkono wake kuonyesha 0:00:44.750,0:00:49.600 kombe la baharini zuri sana, lenye makoa[br]ya zambarau na njano,nyekundu na bluu. 0:00:50.160,0:00:51.380 Na mwana Mfalme akasema, 0:00:51.460,0:00:54.400 "Hiyo si zawadi kwa Mfalme![br]Ni zawadi gani hiyo?" 0:00:54.600,0:00:57.400 Mzee yule akamwangalia taratibu[br]na kusema 0:00:57.590,0:01:00.750 "Kutembea mwendo mrefu.. ni sehemu[br]ya zawadi" 0:01:01.060,0:01:02.560 (Kicheko) 0:01:02.900,0:01:05.970 Baada ya muda mfupi,[br]Nitawapa zawadi, 0:01:05.970,0:01:08.270 zawadi niaminiyo[br]ni zawadi inayostahili kuenezwa. 0:01:08.290,0:01:10.050 Ila kabla ya hayo, ngoja niwachukue 0:01:10.050,0:01:11.960 kwenye mwendo wangu mrefu. 0:01:12.160,0:01:13.740 Kama wengi wenu, 0:01:13.740,0:01:15.320 Nilianza maisha kama mtoto mdogo. 0:01:15.320,0:01:17.460 Wangapi kati yenu[br]mlianza maisha kama mtoto ? 0:01:17.460,0:01:18.510 Aliyezaliwa mchanga? 0:01:18.740,0:01:20.500 Karibia nusu yenu.. Sawa 0:01:20.570,0:01:21.590 (Kicheko) 0:01:21.820,0:01:24.910 Na mliobakia, vipi?[br]Mlizaliwa mkiwa watu wazima? 0:01:25.060,0:01:27.640 Ama kweli, nataka kukutana na mama zenu! 0:01:27.820,0:01:29.460 Ongelea yasiyowezekana! 0:01:30.560,0:01:34.740 Nikiwa mtoto mdogo, siku zote nilipendezwa[br]kufanya mambo yasiyowezekana 0:01:35.620,0:01:38.880 Leo ni siku ambayo nimekuwa nikiitarajia[br]kwa miaka mingi, 0:01:38.880,0:01:41.000 kwa sababu leo ni siku ambayo[br]nitajaribu 0:01:41.020,0:01:43.620 kufanya yasiyowezekana[br]mbele ya macho yenu 0:01:43.620,0:01:45.460 Hapahapa TEDxMaastrich 0:01:45.800,0:01:48.160 Nitaanza 0:01:48.760,0:01:50.880 Kwa kuonyesha mwisho wake: 0:01:51.220,0:01:52.640 Na nitawathibitishia kwamba 0:01:52.640,0:01:54.940 yasiyowezekana siyo hayawezekani 0:01:55.300,0:01:58.210 Na nitamalizia kwa kuwapa[br]zawadi yenye kustahili kuieneza: 0:01:58.210,0:02:01.350 Nitawaonyesha kwamba unaweza[br]kufanya yasiyowezekana maishani mwako. 0:02:02.660,0:02:05.420 katika kutafuta kufanya yasiyowezekana,[br]nimegundua kuna 0:02:05.420,0:02:08.229 mambo mawili yanayofanana[br]kati ya watu duniani. 0:02:08.229,0:02:09.870 Kila mtu ana hofu, 0:02:09.870,0:02:11.640 na kila mtu ana ndoto. 0:02:12.900,0:02:17.560 Katika kutafuta kufanya yasiyowezekana[br]nimegundua kuna vitu vitatu 0:02:17.560,0:02:20.100 ambavyo nimevifanya miaka mingi ambavyo 0:02:20.110,0:02:23.290 vimenisababishia kufanya yasiyowezekana: 0:02:24.200,0:02:26.900 Mchezo wa mpira wa kuchenga au "Trefball" 0:02:27.290,0:02:28.360 Superman, 0:02:28.460,0:02:29.460 na Mbu 0:02:29.460,0:02:30.810 Hayo ni maneno yangu matatu makuu. 0:02:30.810,0:02:33.500 Mmeshajua kwanini nafanya[br]yasiyowezekana maishani mwangu 0:02:33.610,0:02:36.220 Hivyo nitawachukua katika safari[br]yangu, ya mwendo mrefu 0:02:36.320,0:02:38.680 kutoka kwenye hofu hadi ndoto 0:02:38.740,0:02:40.980 kutoka kwenye maneno hadi panga, 0:02:41.160,0:02:42.740 Kutoka Mpira wa kuchenga 0:02:42.850,0:02:44.020 hadi Superman 0:02:44.020,0:02:45.340 hadi kwa Mbu 0:02:45.800,0:02:47.360 Na ninatumaini kuwaonyesha 0:02:47.360,0:02:49.900 unawezaje kufanya yasiyo[br]wezekana maishani mwako 0:02:52.480,0:02:54.934 Oktoba 4, mwaka 2007. 0:02:55.840,0:02:58.120 Moyo wangu ulienda mbio,[br]magoti yangu yalitetema 0:02:58.120,0:02:59.340 nilipokuwa napanda jukwaani 0:02:59.340,0:03:00.930 kwenye ukumbi wa Sanders 0:03:01.040,0:03:03.240 Chuo cha Harvard kupokea 0:03:03.240,0:03:06.160 Tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu 0:03:06.160,0:03:08.660 kwa kushiriki kuandika ikisiri[br]ya utafiti wa kitabibu 0:03:08.660,0:03:10.270 ulioitwa "Kumeza Upanga... 0:03:10.420,0:03:11.740 ...na Athari zake" 0:03:11.870,0:03:13.275 (Kicheko) 0:03:13.840,0:03:17.880 Ilichapishwa kwenye jarida dogo[br]ambalo sikuwahi kulisoma kabla, 0:03:18.460,0:03:20.419 Jarida la Kitabibu la Uingereza. 0:03:21.360,0:03:24.740 Na kwangu, hiyo ilikuwa ndoto[br]isiyowezekana kuwa kweli, 0:03:24.900,0:03:28.120 ilikuwa ni mshangao usiotegemewa[br]kwa mtu kama mimi, 0:03:28.130,0:03:31.459 ilikuwa ni heshima ambayo sitaweza kusahau 0:03:31.459,0:03:34.539 Lakini haikuwa sehemu ya kubwa ya[br]kukumbuka maishani mwangu. 0:03:35.540,0:03:37.640 Mnamo Oktoba 4, mwaka 1967 0:03:38.020,0:03:40.260 kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 0:03:41.100,0:03:43.120 aliteseka na hofu kubwa kupita kiasi. 0:03:43.460,0:03:45.579 Alipojiandaa kupanda jukwaani, 0:03:45.579,0:03:47.234 moyo wake ulienda mbio, 0:03:47.500,0:03:49.162 magoti yake yalikuwa yakitetemeka. 0:03:49.780,0:03:52.120 Alikwenda kufungua kinywa chake kuongea, 0:03:56.490,0:03:58.130 maneno hayakuweza kutoka. 0:03:58.130,0:04:00.040 Alisimama akitetemeka na kutoa machozi. 0:04:00.630,0:04:02.360 Alipooza kwa mshtuko wa ghafla, 0:04:02.360,0:04:03.760 alipatwa fadhaa kwa hofu. 0:04:03.960,0:04:06.130 huyu kijana mwoga, mwenye aibu, mwembamba 0:04:06.130,0:04:08.142 alitesekana na hofu kubwa kupita kiasi. 0:04:08.649,0:04:10.330 Alikuwa na hofu ya giza, 0:04:10.520,0:04:11.640 hofu ya vimo virefu, 0:04:11.640,0:04:13.040 hofu ya buibui na nyoka ... 0:04:13.040,0:04:15.140 Kuna yeyote anayeogopa buibui na nyoka? 0:04:15.280,0:04:16.660 Naam, wachache wenu ... 0:04:16.660,0:04:19.079 Alikuwa na hofu ya maji na papa ... 0:04:19.079,0:04:21.939 Hofu ya madaktari na manesi na madaktari[br]wa meno, 0:04:21.939,0:04:24.680 na sindano na kutobolewa na vitu vya[br]ncha kali. 0:04:24.680,0:04:27.380 Lakini zaidi ya chochote,[br]alikuwa na hofu ya 0:04:27.470,0:04:28.470 watu 0:04:29.380,0:04:31.530 Huyo kijana mwoga,mwenye aibu na mwembamba 0:04:31.540,0:04:32.570 alikuwa mimi. 0:04:33.320,0:04:35.997 Nilikuwa na hofu ya kushindwa na [br]kukataliwa, 0:04:37.300,0:04:39.520 kutojithamini, kujiona duni, 0:04:39.520,0:04:42.840 na kitu ambacho hata hatukujua [br]unaweza kujiandikisha kwa siku hizo: 0:04:42.840,0:04:44.660 ugonjwa wa hofu ya ukaribu na watu. 0:04:44.955,0:04:48.610 Kwa sababu nilikuwa na hofu, waonevu[br]walinitania na kunipiga. 0:04:48.610,0:04:52.240 Walinicheka na kuniita majina,[br]Hawakuniruhusu kucheza nao 0:04:52.300,0:04:54.260 michezo ya aina yoyote. 0:04:55.020,0:04:58.056 Ah, kulikuwa na mchezo mmoja[br]walikuwa wakiruhusu kucheza kwenye ... 0:04:58.100,0:04:59.427 Mpira wa kuchenga - 0:04:59.500,0:05:01.443 na sikuwa mchengaji nzuri. 0:05:01.760,0:05:03.500 Waonevu waliita jina langu, 0:05:03.500,0:05:05.970 na nilipoangalia [br]niliona mipira myekundu ya kukwepa 0:05:05.970,0:05:08.200 ikivurumishwa usoni wangu kwa kasi kubwa 0:05:08.210,0:05:09.950 bam, bam, bam! 0:05:10.580,0:05:13.220 Ninakumbuka siku nyingi[br]nikirudi nyumbani kutoka shule, 0:05:13.300,0:05:18.180 uso wangu ulikuwa mwekundu ukichonyota,[br]masikio yangu yalikuwa mekundu yakivuma. 0:05:18.180,0:05:21.140 Macho yangu yalichoma kwa machozi, 0:05:21.180,0:05:23.515 na maneno yao yalichoma masikioni mwangu. 0:05:23.740,0:05:25.000 Na yeyote aliyesema, 0:05:25.020,0:05:28.660 "Fimbo na mawe vyaweza kunivunja mifupa,[br]bali maneno hayatoniumiza kamwe "... 0:05:28.880,0:05:30.131 Ni uongo. 0:05:30.310,0:05:31.980 Maneno huweza kukata kama kisu. 0:05:31.980,0:05:34.030 Maneno huweza kupenya kama upanga. 0:05:34.210,0:05:36.040 Maneno huwezafanya majeraha yenye kina 0:05:36.040,0:05:37.780 yasiweze kuonekana. 0:05:38.150,0:05:41.070 Hivyo nilikuwa na hofu.[br]Na maneno yalikuwa adui yangu mkubwa. 0:05:41.260,0:05:42.491 Bado ni adui yangu. 0:05:43.355,0:05:45.300 Lakini pia nilikuwa na ndoto. 0:05:45.300,0:05:47.980 Nilienda nyumbani[br]na kutorokea kwenye futuhi za Superman 0:05:47.980,0:05:49.774 na nilisoma futuhi za Superman 0:05:49.774,0:05:53.440 na niliota kutaka kuwa shujaa mkubwa[br]kama Superman. 0:05:53.480,0:05:56.240 Nilitaka kupigania kweli na haki, 0:05:56.240,0:05:58.680 Nilitaka kupambana dhidi ya[br]wahalifu na mahasimu, 0:05:58.680,0:06:02.895 Nilitaka kupaa duniani kote[br]kufanya vitendo vya ujasiri kuokoa maisha. 0:06:03.400,0:06:05.850 Nilikuwa pia navutiwa mno[br]na vitu vilivyokuwa kweli. 0:06:05.860,0:06:09.460 Nilisoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guiness[br]na kitabu cha Ripley kiitwacho Amini au Usiamini. 0:06:09.460,0:06:13.080 Yeyote kati yenu amewahi kusoma kitabu cha Rekodi za Dunia za Guinness au kitabu cha Ripley? 0:06:13.100,0:06:14.390 Navipenda vitabu hivi! 0:06:14.390,0:06:16.270 Niliona watu wafanyao ujasiri halisia. 0:06:16.270,0:06:17.790 Nikasema, Nataka kufanya hivyo. 0:06:17.790,0:06:19.330 Ikiwa waonevu hawataniruhusu 0:06:19.330,0:06:21.030 kucheza katika michezo yao yoyote, 0:06:21.030,0:06:23.335 Nataka kufanya maajabu, ujasiri halisi. 0:06:23.335,0:06:26.659 Nataka kufanya kitu cha kusifika[br]ambacho hao waonevu hawawezi kufanya. 0:06:26.659,0:06:28.609 Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, 0:06:28.609,0:06:30.729 Nataka kujua kuwa maisha yangu yana maana, 0:06:30.729,0:06:33.320 Nataka kufanya kitu cha kushangaza[br]kubadili ulimwengu; 0:06:33.320,0:06:36.960 Ninataka kuthibitisha[br]yasiyowezekana sio hayawezekani. 0:06:38.340,0:06:40.240 Kupeleka mbele miaka 10 - 0:06:40.240,0:06:42.706 Ilikuwa wiki kabla ya kutimiza miaka 21. 0:06:42.819,0:06:46.799 Mambo mawili yalitokea kwa siku moja[br]ambayo yangebadilisha maisha yangu milele. 0:06:47.040,0:06:49.391 Nilikuwa nikiishi Tamil Nadu, India Kusini 0:06:49.540,0:06:51.020 Nilikuwa mmishonari huko, 0:06:51.020,0:06:53.090 na mshauri wangu, rafiki yangu aliniuliza, 0:06:53.090,0:06:54.720 "Je, una Thromu, Daniel?" 0:06:54.720,0:06:57.440 Na nikasema, "Thromu?[br]Thromu ni nini? " 0:06:57.440,0:07:00.490 Alisema, "Thromu ni malengo makuu ya[br]maisha. 0:07:00.490,0:07:04.630 Ni muunganiko[br]wa ndoto na malengo, kama ungeweza 0:07:04.630,0:07:07.240 kufanya chochote unachotaka,[br]kwenda popote unapotaka 0:07:07.240,0:07:08.479 kuwa mtu yeyote unayetaka, 0:07:08.479,0:07:10.356 ungekwenda wapi?[br]Ungefanya nini? 0:07:10.356,0:07:11.280 Ungekuwa nani? 0:07:11.280,0:07:14.500 Nikasema, "Siwezi kufanya hivyo![br]Naogopa sana! Naogopa mengi mno! " 0:07:14.500,0:07:17.800 Usiku huo nilichukua mkeka wangu wa mchele[br]juu ya paa la ghorofa, 0:07:17.810,0:07:19.259 nikautandika chini ya nyota, 0:07:19.259,0:07:21.869 na kuangalia popo wakiwashambulia mbu. 0:07:21.869,0:07:26.200 Na yote niliyofikiria ilikuwa thromu,[br]na ndoto na malengo, 0:07:26.200,0:07:28.360 na wale washujaaji wenye mipira ya kuchenga. 0:07:28.760,0:07:30.730 Masaa machache baadaye niliamka. 0:07:31.220,0:07:33.940 Moyo wangu ulienda mbio,[br]magoti yangu yakitetemeka. 0:07:34.080,0:07:36.020 Safari hii haikuwa na hofu. 0:07:36.420,0:07:38.395 Mwili wangu wote ulitikisika. 0:07:38.500,0:07:40.180 Na kwa siku tano zilizofuata 0:07:40.330,0:07:44.199 Nilipoteza na kurudisha fahamu,[br]kitandani nikipigania maisha yangu. 0:07:44.199,0:07:48.239 Ubongo wangu ulikuwa unawaka[br]na homa ya malaria yenye jotoridi la 105. 0:07:48.390,0:07:51.600 Na kila fahamu ziliponirudia,[br]nilichowaza ilikuwa kuhusu thromu. 0:07:51.600,0:07:53.820 Niliwaza[br]"Nataka kufanya nini na maisha yangu?" 0:07:53.950,0:07:56.380 Hatimaye, usiku kabla[br]sijafikisha miaka 21, 0:07:56.380,0:07:58.030 katika wakati wa kuelewa, 0:07:58.030,0:07:59.639 Nilikuja kutambua: 0:07:59.639,0:08:02.100 Nilitambua kwamba yule mbu mdogo, 0:08:02.620,0:08:05.020 Anofelesi Stefensi, 0:08:05.280,0:08:06.610 yule mbu mdogo 0:08:06.610,0:08:08.390 aliye na uzito chini ya mikrogramu 5 0:08:08.390,0:08:09.810 chini ya punje ya chumvi, 0:08:09.810,0:08:12.780 anaweza kuangusha[br]mtu wa ratili 170, mtu wa kilo 80, 0:08:12.780,0:08:14.860 Niligundua kwamba alikuwa hasimu wangu. 0:08:14.860,0:08:17.150 Kisha nikagundua,[br]hapana, hapana, sio mbu, 0:08:17.150,0:08:19.480 Ni vimelea vidogo[br]ndani ya mbu, 0:08:19.480,0:08:23.160 Plasmodium Falciparum,[br]ambao huua zaidi ya watu milioni kwa mwaka 0:08:23.509,0:08:25.999 Kisha nikagundua[br]Hapana, hapana, tena ni ndogo zaidi, 0:08:25.999,0:08:28.550 lakini kwangu, ilionekana kubwa zaidi. 0:08:28.550,0:08:29.640 Niligundua, 0:08:29.640,0:08:31.270 hofu ilikuwa hasimu yangu, 0:08:31.270,0:08:32.140 vimelea yangu, 0:08:32.140,0:08:34.990 vilivyonitia ulemavu[br]na kunipooza mimi maisha yangu yote. 0:08:35.200,0:08:38.080 Unajua, kuna tofauti[br]kati ya hatari na hofu. 0:08:38.109,0:08:39.698 Hatari ni halisi. 0:08:39.990,0:08:42.010 Hofu ni hiari. 0:08:42.080,0:08:44.309 Na nikagundua kuwa nina hiari: 0:08:44.309,0:08:48.180 Aidha niishi kwa hofu,[br]na kufa katika kushindwa usiku ule, 0:08:49.070,0:08:52.080 au ningeweza kuua hofu yangu,[br]na ningeweza 0:08:52.080,0:08:56.060 kufikia ndoto zangu,[br]Ningeweza kuthubutu kuishi maisha. 0:08:56.680,0:08:59.560 Na unajua, kuna kitu kuhusu[br]kuwa kwenye kitanda cha mauti 0:08:59.560,0:09:04.080 na kukabiliwa na kifo ambacho haswa[br]kinakufanya utake kweli kuishi maisha. 0:09:04.180,0:09:07.140 Nikagundua kuwa kila mtu hufa,[br]si kila mtu huishi. 0:09:08.040,0:09:09.890 Ni katika kufa ndio sisi tunaishi. 0:09:09.890,0:09:11.580 Unajua, wakati unapojifunza kufa, 0:09:11.580,0:09:13.070 unajifunza kweli kuishi. 0:09:13.070,0:09:15.140 Kwa hiyo nikaamua nitaenda kubadilisha 0:09:15.140,0:09:16.420 hadithi yangu usiku huo. 0:09:16.915,0:09:18.230 Sikutaka kufa. 0:09:18.230,0:09:20.010 Hivyo nikafanya sala ndogo, nikasema, 0:09:20.010,0:09:22.230 "Mungu, ukiniruhusu niishi[br]nifikishe miaka 21, 0:09:22.230,0:09:24.544 Sitaruhusu hofu[br]itawale maisha yangu tena. 0:09:24.670,0:09:26.520 Nitaziweka hofu zangu kifoni, 0:09:26.520,0:09:29.530 Nitaenda kuzifikia ndoto zangu, 0:09:29.530,0:09:31.270 Ninataka kubadilisha mtazamo wangu, 0:09:31.270,0:09:33.540 Nataka kufanya kitu cha ajabu[br]na maisha yangu, 0:09:33.540,0:09:35.550 Nataka kupata kusudi langu na wito wangu, 0:09:35.550,0:09:38.632 Ninataka kujua kuwa yasiyowezekana[br]si hayawezekani. " 0:09:38.780,0:09:42.820 Sitawaambia kama nilinusurika usiku ule;[br]Nitawaacha mfikirie. 0:09:42.850,0:09:43.978 (Kicheko) 0:09:43.978,0:09:47.100 Lakini usiku huo niliandika orodha[br]ya Thromu zangu 10 za kwanza: 0:09:47.100,0:09:50.210 Niliamua nilitaka[br]kutembelea mabara makubwa 0:09:50.210,0:09:51.820 kutembelea Maajabu 7 ya Dunia 0:09:51.820,0:09:53.410 kujifunza lugha nyingi, 0:09:53.410,0:09:54.940 kuishi kwenye kisiwa kitupu, 0:09:54.940,0:09:56.480 kuishi kwenye meli baharini, 0:09:56.480,0:09:58.650 kuishi na kabila la Wahindi[br]katika Amazon, 0:09:58.650,0:10:01.210 kupanda hadi juu[br]ya mlima mrefu kuliko yote Sweden, 0:10:01.210,0:10:03.180 Nilitaka kuona mawio Mlima Everest, 0:10:03.190,0:10:05.390 kufanya kazi na biashara ya muziki[br]Nashville, 0:10:05.400,0:10:07.060 Nilitaka kufanya kazi ya sarakasi, 0:10:07.080,0:10:09.120 na nilitaka kuruka nje ya ndege. 0:10:09.120,0:10:12.380 Zaidi ya miaka ishirini iliyofuata,[br]Nilitimiza thromu hizo kwa wingi. 0:10:12.410,0:10:14.650 Kila wakati niliondoa[br]thromu kwenye orodha yangu, 0:10:14.650,0:10:18.190 Niliongeza 5 au 10 zaidi kwenye orodha[br]na orodha yangu iliendelea kukua. 0:10:18.800,0:10:23.280 Kwa miaka saba iliyofuata, niliishi[br]kwenye kisiwa kidogo katika Bahamas 0:10:23.320,0:10:25.360 kwa karibu miaka saba 0:10:25.370,0:10:27.274 katika kibanda cha makuti, 0:10:29.480,0:10:33.820 nikiwinda papa na taa wa kula,[br]nikiwa mtu pekee kwenye kisiwa, 0:10:33.820,0:10:36.249 nikiwa nimevaa msuli, 0:10:36.680,0:10:39.160 na nikajifunza kuogelea na papa. 0:10:39.160,0:10:40.980 Na kutoka huko, nikahamia Mexico, 0:10:40.980,0:10:45.000 na kisha nikasafiri[br]kwa bonde la Mto Amazon nchini Ecuador, 0:10:45.241,0:10:48.100 Pujo Pongo Ecuador,[br]niliishi na kabila moja huko, 0:10:48.100,0:10:52.180 na kidogo kidogo nilianza kuongeza[br]kujiamini kwa thromu zangu tu. 0:10:52.180,0:10:55.100 Nilihamia biashara ya muziki Nashville,[br]kisha Sweden, 0:10:55.110,0:10:57.870 nikahamia Stockholm,[br]kufanyakazi katika biashara ya muziki, 0:10:57.870,0:11:01.920 ambapo nilipanda kilele cha Ml. Kebnekaise[br]juu ya mzunguko wa Arctic. 0:11:03.300,0:11:04.750 Nilijifunza udamisi, 0:11:04.750,0:11:05.860 na viinimacho, 0:11:05.860,0:11:07.480 na kutembea kama ngongoti, 0:11:07.480,0:11:10.440 kuendesha baiskeli kwa tairi moja,[br]kula moto, kula kioo. 0:11:10.450,0:11:13.620 Mwaka 1997 nilisikia kuna[br]wameza panga wasiozidi kumi na mbili 0:11:13.620,0:11:15.410 na nikasema, "Inabidi kufanya hivyo!" 0:11:15.420,0:11:18.290 Nilikutana na mmeza panga,[br]na nikamwomba vidokezo. 0:11:18.290,0:11:20.190 Akasema, "Naam, nitakupa vidokezo 2: 0:11:20.190,0:11:21.926 Namba 1: Ni hatari sana, 0:11:21.926,0:11:23.948 Watu wamekufa wakifanya hivi. 0:11:23.948,0:11:24.953 Namba 2: 0:11:24.953,0:11:26.206 Usijaribu! " 0:11:26.206,0:11:27.520 (Kicheko) 0:11:27.540,0:11:29.540 Basi nikaiongeza kwenye orodha ya thromu. 0:11:30.440,0:11:33.320 Na nikafanya mazoezi[br]mara 10 hadi 12 kwa siku, kila siku 0:11:33.660,0:11:35.160 kwa miaka minne. 0:11:35.209,0:11:36.709 Sasa nilipigia hesabu hizo... 0:11:36.709,0:11:40.020 4 x 365 [x 12] 0:11:40.020,0:11:42.660 Ilikuwa karibu 13,000[br]majaribio yasiyofanikiwa 0:11:42.660,0:11:45.420 kabla sijatia panga langu wa kwanza[br]chini koo mwaka 2001. 0:11:46.002,0:11:47.630 Wakati huo nikaweka thromu 0:11:47.630,0:11:50.940 kuwa mtaalamu wa ulimwengu[br]kwa kumeza panga. 0:11:50.970,0:11:53.820 Basi nilitafuta kila kitabu,[br]gazeti, makala ya gazeti, 0:11:53.820,0:11:57.670 kila ripoti ya kitabibu,[br]Nilijifunza fiziolojia, anatomia, 0:11:57.676,0:11:59.719 Niliongea na madaktari na manesi, 0:11:59.719,0:12:01.760 niliwakutanisha wameza panga wote[br]pamoja 0:12:01.760,0:12:04.250 kwenye Shirikisho la Wameza Panga[br]Kimataifa, 0:12:04.250,0:12:06.450 nikafanya ikisiri miaka 2[br]ya utafiti kitabibu 0:12:06.450,0:12:08.580 kuhusu Umezaji wa Panga na athari zake 0:12:08.580,0:12:10.980 iliyochapishwa[br]katika Jarida la Kitabibu Uingereza. 0:12:10.980,0:12:11.840 (Kicheko) 0:12:11.840,0:12:12.940 Asanteni. 0:12:12.960,0:12:17.748 (Makofi) 0:12:18.200,0:12:21.570 Na nilijifunza mambo ya kuvutia sana[br]kuhusu umezaji wa panga. 0:12:21.571,0:12:25.260 Vitu vingine ambavyo haujawahi kufikiria[br]kabla, hutasahau baada ya usiku huu. 0:12:25.260,0:12:28.550 Wakati utakapoenda nyumbani, na unakata[br]steki yako na kisu chako 0:12:28.550,0:12:31.759 au panga, au "bestek" zako,[br]utafikiri juu ya hili ... 0:12:34.257,0:12:36.589 Nilijifunza kwamba umezaji panga[br]ulianzia India - 0:12:36.589,0:12:39.889 mahali nilipona kwa mara ya kwanza[br]nikiwa kijana wa miaka 20 - 0:12:39.889,0:12:42.290 karibu miaka 4000 ya kale, karibu 2000 BC. 0:12:42.290,0:12:45.580 Zaidi ya miaka 150 iliyopita,[br]wameza panga walitumika 0:12:45.590,0:12:47.400 katika medani za sayansi na kitabibu 0:12:47.480,0:12:51.160 ili kusaidia kuunda[br]endoskopia imara mwaka 1868 0:12:51.160,0:12:53.820 wakiwa na Dk. Adolf Kussmaul wa Freiburg, Ujerumani 0:12:53.880,0:12:56.639 Mnamo 1906, elektrokadiogramu huko Wales, 0:12:56.639,0:13:00.240 kujifunza matatizo ya kumeza,[br]na mmeng'enyo wa chakula, 0:13:00.240,0:13:01.860 aina ya bronkoskopia, . 0:13:01.860,0:13:03.840 Lakini zaidi ya miaka 150 iliyopita, 0:13:03.840,0:13:07.860 tunajua mamia ya madhara[br]na vifo kadhaa ... 0:13:07.880,0:13:14.560 Hii ni endoskopia imara[br]iliyoanzishwa na Dk. Adolph Kussmaul. 0:13:14.740,0:13:18.679 Lakini tuligundua kuwa kulikuwa na[br]Vifo 29 zaidi ya miaka 150 iliyopita. 0:13:18.679,0:13:22.462 pamoja na mmezaji panga huko London[br]aliyetoboa moyo wake kwa panga 0:13:23.142,0:13:25.340 Tulijifunza pia kuwa kuna kesi tatu hadi nane za 0:13:25.340,0:13:27.780 madhara mkubwa ya umezaji panga[br]kila mwaka. 0:13:27.780,0:13:29.880 Najua kwa sababu mimi hupata simu. 0:13:29.880,0:13:31.150 Nilikuwa na wawili, 0:13:31.150,0:13:34.320 mmoja kutoka Sweden, na kutoka Orlando[br]wiki chache zilizopita, 0:13:34.320,0:13:37.019 wamezaji panga waliopo hospitalini[br]kutokana na madhara. 0:13:37.019,0:13:38.769 Kwa hiyo ni hatari sana. 0:13:38.769,0:13:41.629 Jambo jingine nililojifunza ni kuwa[br]kumeza panga huchukua 0:13:41.629,0:13:44.320 miaka 2 hadi miaka 10[br]kujifunza jinsi ya kumeza panga 0:13:44.320,0:13:45.610 kwa watu wengi. 0:13:45.610,0:13:48.020 Lakini ugunduzi unaovutia sana[br]Nilijifunza ilikuwa 0:13:48.020,0:13:51.360 jinsi wameza panga wanavyojifunza[br]kufanya yasiyowezekana. 0:13:51.460,0:13:53.460 Nami nitawapa siri ndogo: 0:13:53.520,0:13:57.580 Usizingatie kwenye asilimia 99.9[br]kuwa haiwezekani. 0:13:57.580,0:14:02.030 Unazingatia hiyo 1% ambayo inawezekana,[br]na fikiria jinsi ya kufanya iwezeikane 0:14:02.817,0:14:06.140 Sasa napenda kukupeleka kwenye safari[br]ndani ya akili ya mmeza panga. 0:14:06.140,0:14:09.479 Ili kumeza panga,[br]inahitaji akili itafakari jambo, 0:14:09.479,0:14:12.270 uzingativu wa hali ya juu,[br]kuonyesha ufasaha ili 0:14:12.270,0:14:15.670 kutenganisha viungo vya ndani vya mwili[br]na kushinda vitendo hiari mwilini 0:14:15.710,0:14:20.370 kupitia njia ya ubongo iliyoimarishwa,[br]kupitia marido ya kumbukumbu ya misuli 0:14:20.450,0:14:23.720 kwa mazoezi ya makusudi[br]zaidi ya mara 10,000. 0:14:24.020,0:14:28.090 Sasa ngoja niwasafirishe kidogo[br]ndani ya mwili wa mmeza panga 0:14:28.310,0:14:30.130 Ili kumeza panga, 0:14:30.130,0:14:32.250 Lazima niteleze panga juu ya ulimi wangu, 0:14:32.250,0:14:34.780 nizuie kutaka kutapika[br]kwenye shingo ya umio, 0:14:34.780,0:14:37.740 zungusha mgeuko wa nyuzi 90[br]chini ya gegedu ya ulimi, 0:14:38.240,0:14:41.040 pitia kwenye msuli juu ya kilinda umio, 0:14:41.060,0:14:42.600 zuia vitendohiari vya tumbo, 0:14:42.600,0:14:44.380 telezea makali kwenye shimo la kifua 0:14:44.380,0:14:45.960 kati ya mapafu. 0:14:46.080,0:14:48.349 Katika hatua hii, 0:14:48.399,0:14:50.389 Lazma kweli nisukume moyo wangu pembeni. 0:14:50.389,0:14:51.720 Ikiwa utaangalia kwa makini, 0:14:51.720,0:14:53.860 unawezaona moyo ukidunda kwa panga langu 0:14:53.860,0:14:55.859 kwa sababu linaegemea moyo 0:14:55.859,0:14:58.809 ikitenganishwa na karibu thumuni ya inchi[br]ya tishu ya umio. 0:14:58.809,0:15:00.580 Hicho sio kitu unaweza kudanganya. 0:15:00.580,0:15:02.710 Kisha hutelezesha[br]kupita mfupa wa kifua, 0:15:02.710,0:15:05.540 kupita kilinda umio,[br]chini ndani ya tumbo, 0:15:05.540,0:15:09.020 zuia vitendohiari ndani ya tumbo[br]njia yote hadi kwenye mbuti. 0:15:09.020,0:15:09.750 Rahisi sana. 0:15:09.750,0:15:10.930 (Kicheko) 0:15:10.930,0:15:12.880 Kama ningetakiwa kwenda zaidi ya hapo, 0:15:12.880,0:15:17.720 hadi kufikia mirija yangu ya mayai.[br]mirija ya mayai! (Kidachi) 0:15:17.720,0:15:20.980 Wanaume, mnaweza kuwauliza wake zenu [br]kuhusu hiyo baadaye ... 0:15:22.160,0:15:23.900 Watu huniuliza, wanasema, 0:15:23.900,0:15:26.740 "lazima kuchukua ujasiri mwingi[br]ili kuhatarisha maisha yako, 0:15:26.740,0:15:28.800 kusogeza moyo wako,[br]na kumeza panga ... " 0:15:28.800,0:15:30.500 Hapana. Kinachofanya ujasiri halisi 0:15:30.500,0:15:33.020 ni kwa yule kijana mwoga, mwenye aibu,[br]mwembamba 0:15:33.080,0:15:35.620 kwa kuhatarisha kushindwa na kukataliwa, 0:15:35.620,0:15:37.040 kufungua moyo wake, 0:15:37.040,0:15:38.240 na kumeza kiburi chake 0:15:38.240,0:15:41.060 na kusimama hapa mbele[br]ya kundi la watu asiowafahamu kabisa 0:15:41.060,0:15:43.670 na kukuambia hadithi yake[br]kuhusu hofu na ndoto zake, 0:15:43.680,0:15:47.580 kwa hatarisha kumwaga habari zake,[br]vyote kihalisia na kitamathali. 0:15:48.280,0:15:49.450 Unaona - asante. 0:15:49.450,0:15:53.720 (Makofi) 0:15:53.850,0:15:56.250 Unaona, jambo la kustaajabisha sana ni 0:15:56.250,0:15:58.650 Nimetaka kufanya mambo[br]ya kusifika maishani mwangu 0:15:58.650,0:15:59.780 na sasa nimesifika. 0:15:59.780,0:16:02.880 Lakini jambo la kusifika haswa[br]sio kwamba ninaweza kumeza 0:16:02.880,0:16:05.170 panga 21 kwa mara moja, 0:16:07.640,0:16:10.500 au futi 20 chini ya maji kwenye tanki[br]la papa 88 na taa 0:16:10.500,0:16:12.307 kwa kitabu cha Amini au Usiamini, 0:16:13.840,0:16:17.600 au kuchowa hadi kuwa mwekundu nyuzi 1500[br]kwa Watu jasiri wa Stan Lee 0:16:17.610,0:16:19.470 kama "Mtu wa Chuma" 0:16:19.520,0:16:21.574 na yule jamaa alikuwa moto! 0:16:22.460,0:16:24.920 Au kuvuta gari kwa upanga kwa Ripley, 0:16:24.930,0:16:26.290 au Guinness, 0:16:26.290,0:16:28.760 au kufikia fainali za[br]shindano la vipaji Marekani, 0:16:28.820,0:16:31.540 au kushinda 2007[br]tuzo ya Ig Nobel katika Utabibu. 0:16:31.550,0:16:33.900 La, hilo sio[br]jambo la kusifika sana. 0:16:33.900,0:16:36.350 Hivyo ndio watu wanafikiria.[br]La, la, la. Sio hivyo. 0:16:36.350,0:16:37.800 Jambo la kusifika sana 0:16:37.800,0:16:40.660 ni Mungu angemchukua kijana,[br]mwoga, mwenye aibu mwembamba 0:16:40.660,0:16:42.200 aliyehofia vimo virefu, 0:16:42.200,0:16:43.890 aliyehofia ya maji na papa, 0:16:43.890,0:16:46.370 na madaktari na manesi[br]na sindano na vyenye ncha kali 0:16:46.370,0:16:47.640 na kuzungumza na watu 0:16:47.640,0:16:49.800 na sasa ananifanya[br]nipae duniani kote 0:16:49.800,0:16:51.320 katika kina cha futi 30,000 0:16:51.320,0:16:53.900 kumeza vitu vya ncha[br]chini ya maji ya tanki ya papa, 0:16:53.900,0:16:57.430 na kuzungumza na madaktari na wauguzi[br]na hadhira kama ninyi duniani 0:16:57.430,0:16:59.580 Hilo ni jambo la kustaajabu sana kwangu. 0:16:59.580,0:17:01.450 Nimetaka kufanya mambo yasiyowezekana - 0:17:01.450,0:17:02.380 Asante. 0:17:02.380,0:17:03.760 (Makofi) 0:17:03.760,0:17:05.220 Asante. 0:17:05.660,0:17:09.040 (Makofi) 0:17:09.700,0:17:12.569 Sikuzote nilitaka kufanya yasiyowezekana,[br]na sasa nimeweza. 0:17:12.569,0:17:15.858 Nilitaka kufanya kitu cha kusifika[br]maishani na kubadilisha ulimwengu, 0:17:15.858,0:17:16.898 na sasa nimeweza. 0:17:16.898,0:17:19.819 Siku zote nilitaka kupaa duniani kote[br]kufanya vitendo vigumu 0:17:19.819,0:17:21.378 na kuokoa maisha, sasa nimeweza. 0:17:21.378,0:17:22.720 Na unajua nini? 0:17:22.720,0:17:25.569 Bado kuna sehemu ndogo[br]ya ndoto kubwa ya yule mtoto mdogo 0:17:25.569,0:17:27.290 ndani kabisa. 0:17:30.320,0:17:36.197 (Kicheko) (Makofi) 0:17:37.000,0:17:40.240 Na unajua, sikuzote nilitaka kupata[br]kusudi langu na wito wangu, 0:17:40.270,0:17:41.530 na sasa nimepata. 0:17:41.540,0:17:42.920 Lakini nadhani nini? 0:17:42.920,0:17:46.230 Si kwa panga,[br]sio unavyofikiria, si kwa nguvu zangu. 0:17:46.230,0:17:48.510 Ni kwa udhaifu wangu, maneno yangu. 0:17:48.510,0:17:51.090 Kusudi langu na wito[br]ni kubadili ulimwengu 0:17:51.090,0:17:52.390 kwa kukata kupitia hofu, 0:17:52.390,0:17:54.910 upanga mmoja kwa wakati, neno moja [br]kwa wakati, 0:17:55.070,0:17:57.450 kisu moja kwa wakati, maisha kwa wakati, 0:17:57.540,0:17:59.700 kuhamasisha watu kuwa mashujaa 0:17:59.700,0:18:01.860 na kufanya yasiyowezekana maishani mwao. 0:18:02.060,0:18:04.680 Kusudi langu ni kusaidia wengine [br]kupata yao. 0:18:04.680,0:18:05.680 La kwako ni lipi? 0:18:05.680,0:18:06.960 Nini kusudi lako? 0:18:06.960,0:18:08.960 Uliwekwa kufanya nini hapa? 0:18:09.260,0:18:11.590 Naamini sisi wote[br]tumeitwa kuwa mashujaa. 0:18:12.160,0:18:14.260 Nguvu yako kubwa ni nini? 0:18:14.560,0:18:17.990 Kati ya idadi ya watu duniani[br]ya watu zaidi ya bilioni 7, 0:18:17.990,0:18:20.250 kuna wameza upanga[br]wachache sana 0:18:20.250,0:18:21.661 waliobakia duniani kote leo, 0:18:21.661,0:18:22.940 lakini kuna wewe mmoja. 0:18:22.940,0:18:24.070 Wewe ni wa pekee. 0:18:24.070,0:18:25.540 Hadithi yako ni nini? 0:18:25.540,0:18:27.760 Nini kinakufanya uwe tofauti? 0:18:27.760,0:18:29.180 Simulia hadithi yako, 0:18:29.180,0:18:31.721 hata kama sauti yako ni nyembamba [br]na inatetemeka. 0:18:31.900,0:18:33.340 Je, thromu zako ni nini? 0:18:33.340,0:18:35.850 kama ungefanya chochote,[br]kuwa yeyote, kwenda popote - 0:18:35.850,0:18:37.430 Ungefanya nini?[br]Ungekwenda wapi? 0:18:37.430,0:18:38.480 Ungefanya nini? 0:18:38.480,0:18:40.340 Unataka kufanya nini na maisha yako? 0:18:40.340,0:18:41.760 Nini ndoto zako kubwa? 0:18:41.760,0:18:44.450 Nini ndoto zako kubwa ulipokuwa mdogo?[br]Fikiria tena 0:18:44.450,0:18:46.240 Nina uhakika hii haikuwa hivyo, si ndiyo? 0:18:46.483,0:18:47.880 Nini zilikuwa ndoto zako [br]kuu 0:18:47.880,0:18:50.450 ulizofikiri zilikuwa ajabu sana[br]na zisizoeleweka? 0:18:50.450,0:18:54.040 Hakika hii inafanya ndoto zako zisionekane[br]za ajabu tena, sivyo? 0:18:55.370,0:18:57.050 Upanga wako ni nini? 0:18:57.050,0:18:58.650 Kila mmoja wenu ana upanga, 0:18:58.650,0:19:00.600 upanga wa pande mbili wa hofu na ndoto. 0:19:00.600,0:19:03.520 Meza upanga wako, chochote utachokuwa. 0:19:03.890,0:19:05.870 Fuata ndoto zako, mabibi na mabwana, 0:19:05.870,0:19:08.900 Hujachelewa sana kuwa[br]chochote unataka kuwa. 0:19:09.720,0:19:12.920 Kwa wale waonevu na mipira ya kukwepa, [br]wale watoto waliodhani 0:19:12.920,0:19:14.916 kuwa sitaweza kufanya yasiyowezekana, 0:19:15.060,0:19:17.645 Nina kitu kimoja tu cha kuwaambia: 0:19:17.645,0:19:18.841 Asanteni. 0:19:18.940,0:19:22.220 Kwa sababu kama si kwa wahalifu,[br]tusingekuwa kuwa na mashujaa. 0:19:23.020,0:19:27.237 Nipo hapa kuthibitisha[br]yasiyowezekana si hayawezekani. 0:19:28.300,0:19:32.310 Hii ni hatari sana,[br]Inaweza kuniua. 0:19:32.340,0:19:33.720 Natumaini mtafurahia. 0:19:33.720,0:19:35.260 (Kicheko) 0:19:36.350,0:19:38.700 Nitahitaji msaada wenu kwenye hili. 0:19:46.731,0:19:48.405 Hadhira:Mbili, tatu. 0:19:48.405,0:19:52.100 Dan Meyer:La, la, la. Nahitaji msaada wenu[br]kwenye kuhesabu, nyote, sawa? 0:19:52.100,0:19:53.210 (Vicheko) 0:19:53.210,0:19:55.840 Kama unajua maneno? Sawa?[br]Hesabu na mimi. Tayari? 0:19:55.870,0:19:56.964 Moja. 0:19:56.964,0:19:58.150 Mbili. 0:19:58.170,0:19:58.980 Tatu. 0:19:58.980,0:20:00.920 La, hiyo ni 2, lakini mmeelewa 0:20:06.760,0:20:07.780 Hadhira: Moja. 0:20:07.840,0:20:08.750 Mbili. 0:20:08.800,0:20:10.010 Tatu. 0:20:11.260,0:20:13.280 (Vuta pumzi) 0:20:14.360,0:20:15.940 (Makofi) 0:20:16.251,0:20:17.450 DM: Ndiyo! 0:20:17.450,0:20:23.100 (Makofi) (Kushangilia) 0:20:23.100,0:20:24.820 Asanteni sana. 0:20:25.450,0:20:28.800 Asante, asante, asante.[br]Asante kutoka kina cha moyo wangu 0:20:28.800,0:20:31.290 Kweli, asante[br]kutoka chini ya tumbo langu. 0:20:31.880,0:20:35.020 Niliwaambia nimekuja hapa kufanya[br]yasiyowezekana, na sasa nimeweza. 0:20:35.030,0:20:37.730 Ila hii haikuwa isiyowezekana.[br]Ninafanya hivi kila siku. 0:20:37.800,0:20:42.800 Kitu kisichowezekana ilikuwa yule mwoga, [br]mwenye aibu mwembamba kukabili hofu zake 0:20:42.840,0:20:44.600 kusimama hapa kwenye jukwaa la [TEDx], 0:20:44.600,0:20:47.100 na kubadilisha dunia,[br]neno moja kwa wakati, 0:20:47.100,0:20:49.080 upanga kwa wakati, maisha kwa wakati. 0:20:49.080,0:20:52.060 kama nimekufanya ufikiri kwa njia mpya,[br]kama nimekufanya uamini 0:20:52.060,0:20:54.460 yasiyowekana si hayawezekani, 0:20:54.460,0:20:57.960 ikiwa nimekufanya uelewe kuwa waweza[br]fanya yasiyowezekana maishani mwako, 0:20:58.120,0:21:01.020 basi kazi yangu imekwisha,[br]na yako ndiyo kwanza imeanza. 0:21:01.020,0:21:04.100 Usiache kuwa na ndoto. Usiache kuamini. 0:21:04.820,0:21:06.350 Asanteni kwa kuniamini 0:21:06.350,0:21:08.250 na asanteni kuwa sehemu [br]ya ndoto yangu. 0:21:08.250,0:21:09.550 Hii ni zawadi kwenu: 0:21:09.550,0:21:11.486 Yasiyowezekana si ... 0:21:11.486,0:21:12.920 Hadhira: Hayawezekani. 0:21:12.920,0:21:14.920 Mwendo mrefu ni sehemu ya zawadi. 0:21:15.100,0:21:19.560 (Makofi) 0:21:19.560,0:21:21.020 Asanteni. 0:21:21.060,0:21:25.360 (Makofi) 0:21:25.580,0:21:27.560 (Kushangilia) 0:21:27.750,0:21:30.570 Mwenyeji: Asante, Dan Meyer, wow!