POKEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU!!!
-
0:00 - 0:04Sasa hivi, naona moto wa Bwana ukianguka nyumbani kwako!
-
0:04 - 0:07Moto wa Bwana ukianguka juu ya moyo wako!
-
0:07 - 0:16Moto wa Bwana ukianguka sasa hivi - ukiteketeza maumivu hayo, ukiteketeza mateso hayo, ukiteketeza utumwa huo!
-
0:16 - 0:17Pokea moto!
-
0:19 - 0:30Mungu anabisha mlangoni mwa
moyo wako sasa hivi. -
0:30 - 0:33Lakini hatajilazimisha kuingia.
-
0:33 - 0:39Hapana. Hatajilazimisha
ndani ya moyo wako. -
0:39 - 0:45Lazima umruhusu aingie sasa hivi.
-
0:45 - 0:52Na tunapokaribia kuomba, nataka uzingatie jambo muhimu sana.
-
0:52 - 1:06Wengi wetu tunaojiunga na ibada hii leo tunamwomba Mungu atukomboe,
-
1:06 - 1:17lakini bado tunajilisha kitu kile kile ambacho kinachochea utumwa wetu.
-
1:17 - 1:21Tunamwomba Mungu atuponye siku ya leo
-
1:21 - 1:30lakini tunashikilia kitu kile kile ambacho kinazuia muujiza wetu.
-
1:30 - 1:35Tunamwomba Mungu uhuru,
Uhuru wa Kiungu leo, -
1:35 - 1:47bado wengi wetu tunashikilia kitu kile kile ambacho kinatuweka mateka.
-
1:47 - 1:50Kitu gani hicho?
-
1:50 - 2:01Kutosamehe, uchungu,
maudhi katika mioyo yetu. -
2:01 - 2:11Tunagaagaa katika sumu ya uchungu, lakini tunashangaa kwa nini bado tu wagonjwa kiroho.
-
2:11 - 2:15Watu wa Mungu, imetosha!
-
2:15 - 2:23Usingojee wakati unaofaa zaidi ili kufanya moyo wako utulie na Mungu.
-
2:23 - 2:30Usingojee wakati unaofaa zaidi ili kuachilia msamaha kwa mtu huyo
-
2:30 - 2:36aliyekudhulumu, aliyekudhuru, aliyekushitaki kwa uwongo, aliyekusingizia.
-
2:36 - 2:39Sasa ni wakati uliowekwa.
-
2:39 - 2:49Hivi sasa, kwa kila moyo uliofungwa na uchungu - nasema, ufunguliwe!
-
2:49 - 2:53Ufunguliwe, katika jina kuu
la Yesu Kristo! -
3:07 - 3:13Dawa pekee ya sumu ya dhambi ni Damu ya thamani ya Yesu Kristo.
-
3:13 - 3:22Hivi sasa, kwa kila moyo ulio na sumu ya kutosamehe, maumivu ya zamani, chuki -
-
3:22 - 3:30Utakaswe kwa Damu ya Yesu Kristo!
-
3:55 - 4:06Kizuizi hicho moyoni mwako -
kivunjwe kwa uwezo wa Mungu! -
4:17 - 4:21Kizuizi chochote cha kiroho
kwa muujiza wako leo, -
4:21 - 4:31Ninasema kwa imani katika jina la Yesu Kristo - ondolewa! Uondolewe sasa hivi!
-
4:45 - 4:50Ndiyo, watu wa Mungu!
Naweza kuona mioyo yenu iko tayari. -
4:50 - 4:54Ninaweza kuona mioyo yenu iko tayari
kupokea sasa hivi. -
4:54 - 5:05Biblia inasema katika 1 Yohana 1:5 Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza.
-
5:05 - 5:10Sasa hivi, kwa mamlaka
katika jina la Yesu Kristo - -
5:10 - 5:21Tengwa na giza!
-
5:35 - 5:42Popote zana hizo za giza zinazofanya kazi katika maisha yako -
-
5:42 - 5:49leo, kuwe na mwanga!
-
5:49 - 5:55Nuru nyumbani kwako! Nuru katika afya yako! Nuru katika kazi yako! Nuru katika familia yako!
-
5:55 - 5:59Pokea nuru ya Mungu sasa hivi!
-
6:20 - 6:25Kuwa huru kutoka katika madhihirisho yote
ya giza! -
6:25 - 6:28Ufunguliwe kutoka katika utumwa huo!
-
6:28 - 6:30Ufunguliwe kutoka katika mateso hayo!
-
6:30 - 6:33Ufunguliwe kutoka katika ndoto hiyo mbaya!
-
6:33 - 6:35Ufunguliwe kutoka katika uraibu huo!
-
6:35 - 6:39Ufunguliwe kutoka katika laana hiyo ya kizazi!
-
6:57 - 7:03Katika 1 Wafalme 18:28, kisa cha Nabii Eliya na manabii wa Baali,
-
7:03 - 7:09Biblia inasema moto wa Bwana ukaanguka!
-
7:09 - 7:13Sasa hivi, naona moto wa Bwana ukianguka nyumbani kwako!
-
7:13 - 7:16Moto wa Bwana ukianguka juu ya moyo wako!
-
7:16 - 7:25Moto wa Bwana ukianguka sasa hivi - ukiteketeza maumivu hayo, mateso hayo, utumwa huo!
-
7:25 - 7:27Pokea moto!
-
7:49 - 7:54Ndiyo, pokea moto wa Roho Mtakatifu na upokee uponyaji wako!
-
7:54 - 7:59Pokea moto wa Roho Mtakatifu na kupokea ukombozi wako!
-
7:59 - 8:04Pokea moto wa Roho Mtakatifu na upokee mafanikio yako!
-
8:04 - 8:09Pokea moto wa Roho Mtakatifu na upokee uhuru wako leo!
-
8:26 - 8:36Hivi sasa, dhiki hiyo, ulevi ulioingia maishani mwako kupitia roho za mababu,
-
8:36 - 8:41laana za kizazi -
anza kuivunja sasa hivi! -
8:41 - 8:43Vunja minyororo ya mateso!
-
8:43 - 8:46Vunja minyororo ya uraibu! Ivunjwe!
-
9:08 - 9:14Uraibu huo wa pombe - uvunjwe,
katika jina la Yesu Kristo! -
9:14 - 9:20Uraibu huo wa sigara - uvunjwe,
katika jina la Yesu Kristo! -
9:20 - 9:28Uraibu huo wa ponografia na punyeto - uvunjwe sasa hivi!
-
9:46 - 9:49Ndiyo, watu wa Mungu,
pokea moto wa Roho Mtakatifu. -
9:49 - 9:57Weka mkono wako mahali ambapo umekuwa ukipata maumivu, magonjwa, mateso.
-
9:57 - 10:02Pokea moto wa Roho Mtakatifu
na upokee leo! -
10:19 - 10:30Ninazungumza na roho hiyo ya uchungu.
Sikiliza sauti ya Mungu. -
10:30 - 10:36Toka, kwa jina la Yesu Kristo!
-
10:36 - 10:42Maumivu hayo, mateso hayo, ugonjwa huo - toka nje!
-
10:58 - 11:06Chochote ambacho shetani ameweka kwenye mfumo wako na kusababisha maumivu, ugonjwa -
-
11:06 - 11:11Ninasema hivi sasa, Ondoshwa nje!
-
11:11 - 11:15Usafishwe kwa Damu
ya Yesu Kristo! -
11:15 - 11:17Tapika! Tapika huo uchungu!
-
11:17 - 11:21Tapika hiyo sumu!
Itapike sasa hivi! -
11:41 - 11:51Hiyo sumu ya kiroho inayochafua mwili wako, ikitesa mfumo wako, kuharibu viungo vyako -
-
11:51 - 11:55Nasema, fichuliwa!
-
11:55 - 12:00Itapike sasa hivi! Itapike,
katika jina la Yesu Kristo! -
12:00 - 12:07Tapika hiyo sumu, adha, ugonjwa! Upone!
-
12:24 - 12:35Ninazungumza na mateso hayo katika uwezo wako,
katika mfumo wako, katika viungo vyako. -
12:35 - 12:45Hilo shinikizo la damu, Hiyo high cholesterol, hicho kisukari - Uponywa!
-
12:45 - 12:48Upone sasa hivi!
-
13:08 - 13:19Ugumu huo wa kutembea, ugumu wa kula, ugumu wa kupumua - uponywe!
-
13:19 - 13:21Upone sasa hivi!
-
13:40 - 13:49Kwa mara nyingine tena, weka mkono wako, kama kitendo cha imani, mahali popote unapopata maumivu.
-
13:49 - 13:54Ikiwa una picha ya mpendwa, mtu wa familia ambaye ni mgonjwa,
-
13:54 - 13:56Shikilia picha hiyo kwa imani.
-
13:56 - 14:00Hebu tusihi Damu ya Yesu
juu ya hali hiyo. -
14:00 - 14:09Kumbuka, ni sala ya Kimaandiko inayoachilia nguvu za Mungu.
-
14:09 - 14:18Katika Isaya 53:5, inasema,
“Kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” -
14:18 - 14:25Sasa hivi, anza kusihi Damu ya Yesu juu ya hali yako,
-
14:25 - 14:29juu ya familia yako, juu ya afya yako,
juu ya kesi hiyo. -
14:29 - 14:35Omba kwa Damu ya Yesu sasa hivi.
-
14:35 - 14:39Sihi Damu ya Yesu Kristo.
-
15:02 - 15:06Kwa wale ambao wameunganishwa na familia yako,
-
15:06 - 15:08Nataka mje pamoja sasa hivi.
-
15:08 - 15:11Nataka nyinyi mje pamoja
na kuomba pamoja. -
15:11 - 15:13Tunakwenda kuziombea familia zetu.
-
15:13 - 15:23Ninaamuru kila roho ya kizuizi
Iiache familia yako! -
15:23 - 15:25Iachie familia yako leo!
-
15:38 - 15:48Ninaamuru kila roho ya vilio iiache familia yako sasa hivi!
-
16:01 - 16:12Ninaamuru kila roho inayosumbua ustawi wa familia yako iondoke sasa hivi!
-
16:12 - 16:14Ondoka, kwa jina la Yesu Kristo!
-
16:30 - 16:39Roho yoyote ya mpasuko ambayo inajaribu kugawanya familia yako -
-
16:39 - 16:46Namwambia huyo roho wa ajabu, ondoka!
Ondolewa sasa hivi! -
17:01 - 17:11Kila nguvu ya kiroho inayofanya kazi dhidi ya umoja wenu, umoja, amani kama familia -
-
17:11 - 17:16Ondolewa! Ondolewe sasa hivi!
-
17:35 - 17:43Katika familia yako, pokea moto wa
Roho Mtakatifu na acha furaha itawale! -
17:43 - 17:47Pokea moto wa Roho Mtakatifu na
amani itawale! -
17:47 - 17:53Pokea moto wa Roho Mtakatifu na
uache umoja utawale! -
17:53 - 17:57Pokea kwa imani katika jina la
Yesu Kristo! -
18:19 - 18:27Kila roho itendayo kazi
kinyume cha uthabiti wenu, -
18:27 - 18:34ambayo inasababisha kutofautiana katika kutembea kwako kiroho na Bwana -
-
18:34 - 18:43Namwambia huyo roho wa ajabu, toka nje!
Toka, katika jina la Yesu Kristo! -
19:03 - 19:12Najua kuna wengi wetu ambao tumekuwa tukipata msongo wa mawazo usio wa kawaida
-
19:12 - 19:25katika maeneo yetu ya kazi, kazi, familia, ndoa na fedha.
-
19:25 - 19:35Hivi sasa, kwa kila moyo uliounganishwa kwa wakati huu ambao unasumbuliwa na mafadhaiko yasiyo ya kawaida -
-
19:35 - 19:39Ninasema, pokea nguvu za Kimungu!
-
19:39 - 19:42Pokea nguvu isiyo ya kawaida!
-
19:42 - 19:45Pokea nguvu za kushinda!
-
19:45 - 19:50Pokea nguvu za kushinda,
katika jina la Yesu Kristo. -
20:08 - 20:19Kwa ule moyo uliolemewa na mitego na mahangaiko ya maisha haya - fanywa upya leo!
-
20:19 - 20:23Uwe huru, katika jina la Yesu Kristo!
-
20:44 - 20:53Ukombolewe na roho hiyo ya ulegevu.
-
20:53 - 20:57Ufanywe upya!
-
20:57 - 21:03Katika roho yako, ndani ya nafsi yako, katika mwili wako -
ufanywe upya leo! -
21:19 - 21:23Ufanywe upya ili uendelee kukazana!
-
21:23 - 21:25Fanywa upya ili uendelee!
-
21:25 - 21:28Fanywa upya ili uendelee kukua!
-
21:28 - 21:32Ufanywe upya ili uendelee kung’aa kwa furaha ya Bwana!
-
21:32 - 21:34Ifanywe upya sasa hivi!
-
21:50 - 21:59Sasa hivi, mwombe Mungu Mwenyezi
akusaidie kutenganisha -
21:59 - 22:05kutoka kwa chochote kinachojaribu kukutenganisha Naye.
-
22:05 - 22:06Muulize sasa hivi.
-
22:28 - 22:33Najua kuna wengi wetu tunapambana
na udhaifu. -
22:33 - 22:39Inaweza kuwa udhaifu wa kimwili, kihisia, kiakili au kiroho.
-
22:39 - 22:44Haijalishi udhaifu huo ni upi,
ahadi ya Mungu ni hiyo -
22:44 - 22:50Atadhihirisha nguvu zake
katika udhaifu huo. -
22:50 - 22:51Muulize sasa hivi.
-
22:51 - 22:55Mwombe Mungu aonyeshe nguvu zake
katika udhaifu wako. -
22:55 - 23:00Mwambie adhihirishe nguvu zake katika udhaifu wako sasa hivi.
-
23:27 - 23:31Kumbuka, ulikuwa ni udhaifu wa Daudi
-
23:31 - 23:39ambao kwa hakika ulionyesha nguvu za Mungu katika kukutana kwake na Goliathi.
-
23:39 - 23:44Mwambie Mungu sasa hivi adhihirishe nguvu zake katika udhaifu wako,
-
23:44 - 23:48ili utukufu wake uonekane katika maisha yako.
-
23:48 - 23:50Muulize sasa hivi.
-
24:22 - 24:27Katika jina kuu la Yesu Kristo tunaomba.
-
24:33 - 24:43Watu wa Mungu najua mmepatwa moto wa Roho Mtakatifu leo.
-
24:43 - 24:49Na nini kinatokea wakati roho yako inapounganishwa na Roho Wake?
-
24:49 - 24:51Uponyaji hufanyika.
-
24:51 - 24:52Ukombozi unafanyika.
-
24:52 - 24:55Uhuru unafanyika.
-
24:55 - 24:56Mafanikio hufanyika.
-
24:56 - 25:00Umeipokea katika Roho leo!
-
25:00 - 25:11Biblia inasema kwamba Mungu ametuita kutoka gizani na kutuingiza katika nuru yake ya ajabu!
-
25:11 - 25:18Leo, Mungu amekuita utoke katika magonjwa na uwe na afya njema.
-
25:18 - 25:22Amewaita kutoka katika utumwa
na kuingia katika uhuru. -
25:22 - 25:26Amekuita kutoja kwenye hofu na imani.
-
25:26 - 25:30Amekuita kwa uhuru wako leo.
-
25:30 - 25:33Kwa hivyo sasa hivi, anza kufurahi!
-
25:33 - 25:41Furahia uhuru wako, ukombozi, uponyaji, mafanikio!
-
25:41 - 25:48Hata kama bado haujaona udhihirisho huo kwa macho au kimwili, unaweza kufurahi!
-
25:48 - 25:51Unaweza kufurahi kama kitendo cha imani.
-
25:51 - 25:55Furahia sasa hivi!
-
25:55 - 26:03Na mnapofurahia watu wa Mungu ngoja niwakumbushe jambo la maana sana.
-
26:03 - 26:19Pale Mungu anapoingilia kati, huwezi kutenganisha suluhisho na wokovu.
-
26:19 - 26:27Kwa maneno mengine, chochote unachopokea kutoka kwa Yesu Kristo -
-
26:27 - 26:33kipo juu ya jukwaa la wokovu
wa nafsi yako. -
26:33 - 26:39Kwa hivyo, lazima uangalie ng'ambo ya muujiza uliopokea leo.
-
26:39 - 26:46tukio ulilokumbana nalo leo,
mguso uliohisi leo - angalia zaidi ya hapo. -
26:46 - 26:53Je, utaendeleaje na safari ya imani?
-
26:53 - 27:10Yesu Kristo alisema kwamba lazima tukeshe na kuomba (Mathayo 26:40-41).
-
27:10 - 27:21Jihadhari na ushawishi wowote katika ulimwengu huu ambao unajaribu kukudanganya
-
27:21 - 27:32kupunguza kiwango cha Neno la Mungu na kuifanya dhambi kuwa ya kawaida. Jihadharini.
-
27:32 - 27:38Weka moyo wako katika upatano na kweli ya Neno la Mungu.
-
27:38 - 27:44Fanya maisha yako yaendane na nuru yake
-
27:44 - 27:51na nuru hiyo iangaze ndani yako na kupitia kwako, katika jina la Yesu.
- Title:
- POKEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU!!!
- Description:
-
Shuhudia moto wa Roho Mtakatifu ukishuka kwa nguvu wakati uleule kote ulimwenguni wakati wa Ibada hii ya Maombi Shirikishi na Ndugu Chris - ukileta uponyaji, ukombozi na mafanikio ya ajabu! Maelfu ya waumini duniani kote huungana kupitia Zoom - katika mazingira ya imani - kuleta hali zao mbele za Mungu katika huduma hizi za mtandaoni za kila mwezi kwenye TV ya Moyo wa Mungu Nguvu za Mungu hazipitwi na wakati. Jiunge na maombi haya na ukamate moto wa Roho Mtakatifu, katika jina la Yesu!
Ili kujiunga na Ibada inayofuata ya Maombi Shirikishi na Ndugu Chris kupitia Zoom, tafadhali wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/interactive-prayer-form
#Maombi Shirikishi
➡️ Pats Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Saidia TV ya Moyo wa Mungu kifedha - https://godsheart.tv/financial/
➡️ Habari kuhusu Maombi Shirikishi - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
- God's Heart TV
- Duration:
- 28:22
Stephenmigwi edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for CATCH THE FIRE OF THE HOLY SPIRIT!!! � |