Return to Video

Mkakati wa Kiulimwengu Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto

  • 0:00 - 0:04
    (Haya mazungumzo yana mambo pevu)
  • 0:05 - 0:07
    Kila wakati naulizwa unafanya kazi gani.
  • 0:08 - 0:09
    Na ninajibu,
  • 0:09 - 0:12
    "Ninafanya kazi kutokomeza ukatili
    dhidi ya watoto.
  • 0:12 - 0:16
    Ukatili wote dhidi ya watoto wote
    katika nchi zote."
  • 0:17 - 0:18
    Kawaida kunakuwa na ukimya.
  • 0:18 - 0:21
    Maranyingine, kulingana na mazingira,
  • 0:21 - 0:23
    "Oh, hiyo inaua mazungumzo."
  • 0:24 - 0:25
    Halafu maswali:
  • 0:25 - 0:28
    "Ukatili wa aina gani
    unaozungumzia?"
  • 0:28 - 0:29
    "Kuna ukatili kiasi gani?"
  • 0:29 - 0:32
    "Inatokea maeneo gani,
    inatokea hapa?"
  • 0:32 - 0:36
    Na ninapojibu hayo maswali,
    watu huwa wanashangazwa.
  • 0:36 - 0:38
    Wanashangazwa na ukubwa wa ukatili,
  • 0:38 - 0:40
    wanashangazwa na asili ya ukatili.
  • 0:40 - 0:42
    Lakini mara zote ninakuwa
    mwepesi kuhakikisha
  • 0:42 - 0:45
    Kuwa watu hawaachwi katika hali ya
    majonzi na huzuni.
  • 0:45 - 0:49
    Ninaamini tunayo fursa adimu
    ya kihistoria
  • 0:49 - 0:50
    katika kizazi hiki
  • 0:50 - 0:52
    kutokomeza ukatili dhidi ya watoto
  • 0:53 - 0:56
    Kuna harakati zinazokua kuhusiana na hili.
  • 0:56 - 0:59
    Serikali, serikali za kitaifa,
    serikali za majiji,
  • 0:59 - 1:01
    majimbo na wengine
    wanajiunga katika harakati hizo.
  • 1:01 - 1:04
    Na tutakapofanikiwa--
    na itatuhitaji sote--
  • 1:04 - 1:07
    tutabadilisha mwelekeo
    wa historia ya binadamu.
  • 1:08 - 1:10
    Ninamaanisha nini kwa
    ukatili dhidi ya watoto?
  • 1:10 - 1:12
    Ninamaanisha ukatili wote wa kimwili,
  • 1:12 - 1:15
    kingono, kihisia na
    ukatili wa kisaikolojia
  • 1:15 - 1:18
    unaotokea kwa watoto nyumbani,
  • 1:18 - 1:21
    shuleni, kwenye mitandao
    na katika jamii zao.
  • 1:22 - 1:24
    tunafanya kazi na washirika
    ulimwenguni kote
  • 1:24 - 1:27
    na kutoka kwa hao washirika,
    tunasikia hadithi mbaya
  • 1:27 - 1:28
    za mtoto mmoja mmoja.
  • 1:29 - 1:32
    Kwa mfano, Sarah, ana miaka 10.
  • 1:32 - 1:35
    Amebakwa mara kadhaa na baba yake wa kambo
  • 1:35 - 1:38
    na kutishiwa ukatili
    kama akimwambia mtu.
  • 1:38 - 1:42
    Faisal, alipigwa katika viganja vya mikono
    shuleni kwa waya,
  • 1:42 - 1:43
    kadhalilishwa na kuitwa punda
  • 1:43 - 1:47
    akasimamishwa nje kwenye baridi
    kwa kukosea kujibu swali.
  • 1:48 - 1:52
    Na kwa washirika tunaofanya nao kazi
    kufanya mitandao uwe salama kwa watoto
  • 1:52 - 1:55
    tunasikia hadithi kama za Angelika.
  • 1:55 - 1:57
    Miaka kumi na mbili,
  • 1:57 - 2:00
    akilazimishwa kufanya ngono
    na mjomba wake,
  • 2:01 - 2:04
    huku akirekodiwa na kuangaliwa na watu
    wazima wanaolipia
  • 2:06 - 2:10
    Mmoja kati ya wasichana 10 amepitia
    ukatili wa kingono kabla ya miaka 20.
  • 2:10 - 2:12
    Nusu ya watoto wanaishi kwenye nchi
  • 2:12 - 2:15
    ambazo hadhabu za viboko
    hazijapigwa marufuku.
  • 2:16 - 2:17
    na mwaka jana tu, Marekani,
  • 2:17 - 2:20
    taarifa milioni 45 zilitengenezwa
  • 2:20 - 2:24
    za picha na video za ukatili
    na unyanyaswaji wa watoto mitandaoni
  • 2:24 - 2:26
    Idadi hiyo ni mara mbili ya mwaka uliopita
  • 2:27 - 2:30
    sasa ukatili wa namna hii
    na ukatili wa namna nyingine
  • 2:30 - 2:33
    unajikusanya kuwa idadi kubwa
    ya kushangaza sana.
  • 2:33 - 2:35
    Watoto bilioni moja ulimwenguni kila mwaka
  • 2:35 - 2:37
    wanaopitia aina fulani ya ukatili.
  • 2:37 - 2:39
    Hiyo ni mtoto mmoja kwa kila wawili.
  • 2:39 - 2:41
    Hili ni tatizo la ulimwengu wote.
  • 2:43 - 2:44
    Hivyo ni nini kinachonipa matumaini?
  • 2:45 - 2:46
    Ngoja nizungumzie kuhusu Sweden na Uganda.
  • 2:46 - 2:49
    Labda ni nchi mbili zilizo tofauti sana
    kama unavyofikiri.
  • 2:50 - 2:51
    Ukizungumza na mchumi,
  • 2:51 - 2:54
    wanaweza kusema kuwa Sweden
    ina kipato cha wastani
  • 2:54 - 2:56
    wa takriban dola 50,000 kwa mwaka.
  • 2:56 - 2:58
    Na Uganda, ni dola 2,000.
  • 2:59 - 3:01
    Mwana historia atasema
  • 3:01 - 3:04
    Sweden haijawahi kuwa katika mgogoro wa
    wa kitaifa kwa miaka takriban 200.
  • 3:04 - 3:06
    Uganda bado inahangaika
    na migomo
  • 3:06 - 3:08
    kaskazini mwa nchi.
  • 3:09 - 3:11
    Mwanamuziki anaweza kusema
  • 3:11 - 3:15
    kuwa Uganda, wimbo wa taifa,
    "Oh Uganda, Ardhi ya Uzuri"
  • 3:15 - 3:17
    ni moja kati ya fupi sana ulimwenguni.
  • 3:17 - 3:20
    Fupi mno,
    Mara nyingi inachezwa zaidi ya mara moja.
  • 3:20 - 3:24
    Ninaamini Sweden hucheza yao
    na kuimba yao muda mrefu zaidi.
  • 3:25 - 3:27
    Lakini kwa kumaanisha zaidi,
  • 3:27 - 3:29
    Sweden na Uganda walifanya makubaliano,
  • 3:29 - 3:31
    wana muunganiko mmoja
    na kusudi moja,
  • 3:31 - 3:33
    makubaliano ya kutokomeza ukatili
    dhili ya watoto,
  • 3:33 - 3:36
    na wanachukua hatua kujaribu
    kufanya nchi zao kuingia
  • 3:36 - 3:40
    kwenye njia ya kutokomeza kabisa
    ukatili dhidi ya watoto ifikapo 2030.
  • 3:41 - 3:45
    Na nchi nyingine nyingi,
    majiji na majimbo yanaungana nao,
  • 3:45 - 3:46
    duniani kote.
  • 3:47 - 3:50
    Lakini inamaanisha nini haswa,
    inamaanisha nini kwa vitendo?
  • 3:50 - 3:52
    Wanapofanya makubaliano hayo,
    wanafanya nini?
  • 3:52 - 3:55
    Inamaanisha makubaliano ya hali ya juu
    kisiasa na kiuongozi.
  • 3:55 - 3:57
    Kuweka na kutekeleza sheria.
  • 3:58 - 4:00
    Na kuzindua mikakati,
    kubadilisha sera,
  • 4:00 - 4:02
    Kuanzisha mazungumzo ya kitaifa
  • 4:02 - 4:06
    ambayo yataanza kuamsha uelewa
    juu ya safari ya kubadili mitazamo
  • 4:06 - 4:07
    na kufanya iwe haikubaliki kijamii
  • 4:07 - 4:10
    kuwa na ukatili na unyanyasaji wa watoto
    katika nchi.
  • 4:11 - 4:14
    Inamaanisha kutambua kuwa
    ukatili dhidi ya watoto
  • 4:14 - 4:15
    upo katika nyanja zote,
  • 4:15 - 4:19
    na hivyo mwitikio, na jibu,
    inabidi liwe na namna ya mfumo.
  • 4:19 - 4:21
    Huwezi tu kufanya kipengele kimoja.
  • 4:21 - 4:24
    Inahitaji wadau mbalimbali ndani
    na nje ya serikali.
  • 4:24 - 4:26
    Inahitaji vikundi vya kidini,
    sekta binafsi na vyombo vya habari,
  • 4:27 - 4:30
    wanazuoni, asasi za kiraia
    na wengine.
  • 4:30 - 4:33
    Na inahitaji kuyachukua
    yale ambayo ni mambo mazuri
  • 4:33 - 4:35
    na ushahidi mzuri wa kidunia unaotuelezea,
  • 4:35 - 4:37
    lakini kwa kutumia taarifa za
    nchi
  • 4:37 - 4:42
    kuweka mwanga juu ya simulizi zinazofichwa
    juu ya ukatili katika nchi fulani
  • 4:42 - 4:45
    Na kutumia taarifa hiyo
    kuelekeza mwitikio wa kitaifa,
  • 4:45 - 4:48
    lakini pia kutumia kupima
    na kufuatilia maendeleo.
  • 4:48 - 4:50
    Na kushirikisha kile
    kinacholeta matokeo,
  • 4:50 - 4:52
    kuwa wakweli
    pale ambapo mambo hayatokei.
  • 4:53 - 4:54
    Na kushirikisha hamasa
  • 4:54 - 4:57
    pale tunapoona mafanikio
    na ukatili ukipungua.
  • 4:59 - 5:02
    Lakini je, tunaweza kufanya hili katika
    ngazi ya kiulimwengu?
  • 5:02 - 5:05
    Watoto billioni moja kila mwaka
    wanapitia ukatili.
  • 5:05 - 5:06
    Ninadhani kunaweza.
  • 5:06 - 5:11
    Mwaka 2015, viongozi wa nchi 193
    walikubali nchi zao
  • 5:11 - 5:14
    kutokomeza ukatili, unyanyasaji na
    kutelekeza watoto ifikapo 2030.
  • 5:14 - 5:16
    Ukatili dhidi ya watoto
  • 5:16 - 5:18
    unaharibu yale yote tunayowekeza
    kwao:
  • 5:18 - 5:20
    kwenye afya zao, elimu zao
  • 5:20 - 5:21
    Mara nyingi kwa miaka
  • 5:21 - 5:26
    wakati mwingine madhara na maambukizo ya
    maisha na vizazi.
  • 5:27 - 5:30
    Lakini sio tu kuhusu makubaliano ya
    kimataifa na serikali
  • 5:30 - 5:31
    Inajalisha sana.
  • 5:31 - 5:34
    Lakini baadhi ya vitu pia
    vinabadilika kimsingi
  • 5:34 - 5:36
    na sisi kama jamii ulimwenguni kote
  • 5:36 - 5:39
    tunakataa tabia
    zisizokubalika
  • 5:39 - 5:41
    ambazo kwa miaka mingi zimekuwa
    zikivumiliwa.
  • 5:41 - 5:43
    Fikiri kuhusu harakati ya
    MIMI PIA
  • 5:43 - 5:46
    namna ambavyo kitengo kwa kitengo
    tasnia kwa tasnia
  • 5:46 - 5:47
    inawakamata wahalifu
  • 5:47 - 5:49
    kuwaleta na kuwatia hatiani.
  • 5:49 - 5:52
    Ni safari,
    lakini tumeianza.
  • 5:52 - 5:54
    Angalia kilichotokea
    katika tasnia ya misaada.
  • 5:54 - 5:55
    Baada ya matumizi mabaya ya
    madaraka,
  • 5:55 - 5:58
    tasnia ya misaada
    sasa hivi inaangalia kwa makini sana
  • 5:58 - 6:01
    Usalama wa watoto
    ulimwenguni kote.
  • 6:03 - 6:05
    Lakini labda zaidi ya hivyo.
  • 6:05 - 6:08
    Watoto na vijana wenyewe,
  • 6:08 - 6:10
    kwa sehemu kwa msaada wa teknolojia,
  • 6:10 - 6:11
    lakini kwa sasa wana sauti
  • 6:11 - 6:13
    ambayo sidhani kama
    walikuwa nayo hapo awali.
  • 6:13 - 6:15
    Na wanatumia sauti hiyo,
  • 6:15 - 6:18
    Sio tu kuzungumzia hali
    inayowazunguka
  • 6:18 - 6:20
    au kile wanachojua kinahitaji kuboreshwa,
  • 6:20 - 6:22
    lakini kuwa sehemu ya suluhu ya mambo
  • 6:22 - 6:25
    ambayo yanaelezea
    na kuathiri maisha yao.
  • 6:26 - 6:28
    Fikiri kuhusu wanaharakati hawa wadogo
  • 6:28 - 6:30
    ambao wanazungumza kupinga
    ukeketaji wa wanawake,
  • 6:30 - 6:35
    ndoa za utotoni, uonevu wa kimtandao,
    shule salama, migogoro inayoumiza--
  • 6:35 - 6:36
    na listi inaendelea na kuendelea.
  • 6:37 - 6:39
    Watoto hao ni wa muhimu sana.
  • 6:40 - 6:42
    Hivyo tuna uongozi wa kisiasa,
  • 6:42 - 6:44
    tuna wanaharakati wadogo,
  • 6:44 - 6:46
    tuna suluhu zilizothibitishwa
  • 6:48 - 6:49
    tuna uelewa wa jamii unaoongezeka--
  • 6:49 - 6:50
    tuko katika njia hiyo,
  • 6:50 - 6:53
    tumeanza safari hiyo
    kutokomeza kabisa ifikapo 2030.
  • 6:53 - 6:55
    Lakini suluhu hiso ni zipi?
  • 6:56 - 6:58
    Miaka mitatu iliyopita, 2016,
  • 6:58 - 7:02
    taasisi 10 za kiulimwengu zilikutana
    na kujipanga katika mpango
  • 7:02 - 7:05
    ambao ni jumuishi,
    na mkakati wa hatua kwa hatua
  • 7:05 - 7:07
    kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.
  • 7:08 - 7:09
    Unaoitwa INSPIRE.
  • 7:09 - 7:12
    Uliangalia katika uhitaji wa
    sheria zinazoenda na wakati
  • 7:12 - 7:14
    zinazogusia taratibu za kijamii,
  • 7:14 - 7:16
    msaada wa wazazi na walezi,
  • 7:16 - 7:19
    kutoa mwitikio kwa watoto
    waliopitia ukatili na unyanyaswaji.
  • 7:19 - 7:21
    Na shule salama,
  • 7:21 - 7:24
    ili watoto wawe katika mazingira ya
    kujifunza ambapo watanawiri.
  • 7:25 - 7:27
    Kule Uganda, miaka minne iliyopita,
  • 7:27 - 7:30
    msichana wa miaka nane angeweza kuolewa
    na mwanaume wa miaka 30.
  • 7:31 - 7:32
    Hilo haliwezi kutokea tena.
  • 7:32 - 7:34
    Mwaka 2016, Sheria ya mtoto
    ilifanya hilo kuwa kosa
  • 7:34 - 7:37
    na kufanya umri wa chini kuolewa kuwa miaka 18.
  • 7:37 - 7:39
    Hiyo ndiyo I ya INSPIRE:
  • 7:39 - 7:42
    kupitisha na kutekeleza sheria.
  • 7:43 - 7:46
    Cambodia inatoa msaada wa malezi,
  • 7:46 - 7:48
    msaada kwa wazazi na walezi
    nchi nzima,
  • 7:48 - 7:51
    hivyo wazazi wanapewa uwezo
    kulea watoto wao
  • 7:51 - 7:55
    na kuweka nidhamu kwa namna
    isiyo ya kikatili nyumbani.
  • 7:55 - 7:57
    hiyo ndiyo P ya INSPIRE,
  • 7:57 - 7:59
    msaada kwa wazazi na walezi.
  • 7:59 - 8:00
    Kule Uphilipino,
  • 8:00 - 8:04
    Kuna vituo 100 vilivyowekwa
    kuwalinda wanawake na watoto nchi nzima.
  • 8:04 - 8:07
    Wanawake na watoto ambao wako katika
    hatari kubwa ya ukatili na unyanyaswaji
  • 8:07 - 8:09
    au waliopitia unyanyaswaji.
  • 8:09 - 8:12
    Hiyo ndiyo R ya INSPIRE,
    huduma ya mwitikio na msaada.
  • 8:12 - 8:17
    Na kule Uganda, zana ya
    shule salama imeshaanza kutumika
  • 8:17 - 8:19
    kwa nusu ya walimu wa Uganda,
  • 8:19 - 8:23
    ikiwawezesha kusimamia darasa
    kwa njia za kinidhamu zisizo za kikatili.
  • 8:24 - 8:27
    Hiyo ndiyo E ya INSPIRE,
    elimu na stadi za maisha.
  • 8:27 - 8:30
    Hiyo ni sehemu ndogo tu
    katika mpango wa INSPIRE.
  • 8:30 - 8:34
    Lakini nchi nyingi zaidi zimekubali
    kuutekeleza,
  • 8:34 - 8:35
    kuufanya uwe wa ndani,
  • 8:35 - 8:38
    kuujaziliza kwa taarifa za wakati,
    na kuweka mpango pamoja,
  • 8:38 - 8:39
    kufanya kazi kati ya vitengo,
  • 8:39 - 8:41
    na kuanza ile safari ya kutokomeza.
  • 8:41 - 8:45
    Canada, Mexico,
    Jamuhuri ya Kiarabu, Tanzania --
  • 8:45 - 8:47
    Nilishazitaja Sweden na Uganda --
  • 8:47 - 8:49
    Japan, Uphilipino, Indonesia,
  • 8:49 - 8:52
    nchi nyingi zaidi,
    na sana miji, pia.
  • 8:52 - 8:54
    Na hapa tulipo Scotland,
  • 8:54 - 8:57
    Chuo cha Edinburgh
    kinatengeneza maabara ya kujifunzia
  • 8:57 - 9:00
    ambayo itaenda kufuatilia safari
    kuwa miji ya Scotland
  • 9:00 - 9:05
    na Uphilipino
    na Colombia inakwenda pamoja.
  • 9:06 - 9:07
    Kuona kinachofanikiwa,
  • 9:07 - 9:10
    kuchukua kile kilichotayarisha
    kutekelezwa katika nchi nzima
  • 9:10 - 9:12
    na kuiweka chini kwa ngazi ya jiji,
  • 9:12 - 9:13
    ambapo tunaamini
  • 9:13 - 9:17
    kwamba tunaweza kufanya maendeleo
    ya haraka na ya kuonekana
  • 9:17 - 9:19
    katika muda mfupi.
  • 9:19 - 9:20
    Na tunapofanya hivyo,
  • 9:20 - 9:23
    mafanikio hayo yatashirikishwa
    kupitia maabara ya mafunzo na zaidi
  • 9:23 - 9:25
    katika Chuo kikuu cha Edinburgh.
  • 9:27 - 9:29
    Kutokomeza ukatili ni jambo sahihi,
  • 9:29 - 9:31
    ni uwekezaji makini,
  • 9:31 - 9:34
    tunazo suluhu zilizothibitishwa,
  • 9:34 - 9:36
    na tunao mwanzo wa safari.
  • 9:36 - 9:37
    Lakini nini kitatokea
  • 9:37 - 9:39
    Pale tutakapotokomeza
    ukatili dhidi ya watoto?
  • 9:39 - 9:40
    Hebu tutafakari kwa muda.
  • 9:42 - 9:45
    Kwanza, tafakari kuhusu
    watoto niliowataja.
  • 9:45 - 9:47
    Sarah hatalala tena kitandani
    kwake usiku,
  • 9:47 - 9:50
    akihofu juu ya sauti ya
    hatua za baba yake wa kambo
  • 9:50 - 9:51
    akija juu kwenye ngazi.
  • 9:52 - 9:54
    Faisal atakwenda shule
    na atanawiri.
  • 9:54 - 9:57
    Hataogopa tena kuwa shuleni
  • 9:57 - 10:00
    na kuonewa na kupigwa
    na kudhalilishwa na walimu.
  • 10:02 - 10:04
    Na Angelika na wengine kama yeye
  • 10:04 - 10:08
    hawatakuwa tena kama bidhaa
    inayoletwa mtandaoni
  • 10:08 - 10:11
    kuwafurahisha watu wazima
    walioko maili nyingi mbali.
  • 10:12 - 10:14
    Lakini kuzidisha manufaa ya kijamii,
  • 10:14 - 10:16
    ya kiuchumi na kitamaduni
    ya hiyo.
  • 10:16 - 10:19
    Kuzidisha hiyo kwa kila familia,
    kila jamii,
  • 10:19 - 10:21
    kijiji, mji, jiji, nchi
  • 10:21 - 10:24
    na ghafla, umepata
    utaratibu mpya umezaliwa.
  • 10:24 - 10:28
    Kizazi kitachipua
    bila kupitia ukatili.
  • 10:29 - 10:31
    Itatuhitaji sisi sote.
  • 10:31 - 10:34
    Lakini tunayo fursa adimu
    ya kujaribu,
  • 10:34 - 10:38
    na kuamini sisi pia, kama wazazi,
    tunajukumu la kufanya hivi.
  • 10:40 - 10:42
    Halafu pale wote tunapoulizwa,
  • 10:42 - 10:43
    "Unafanya kazi gani?"
  • 10:43 - 10:46
    kila mmoja wetu anaweza kusema,
  • 10:46 - 10:48
    " Ninabadilisha mwelekeo wa historia
    ya binadamu.
  • 10:49 - 10:52
    Ninafanya kwa sehemu kutokomeza
    ukatili dhidi ya watoto."
  • 10:53 - 10:55
    Hebu tufanye hili na tufanye sasa.
  • 10:55 - 10:56
    Asanteni.
  • 10:56 - 11:02
    (Makofi)
Title:
Mkakati wa Kiulimwengu Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto
Speaker:
Howard Taylor
Description:

Kila mwaka, watoto bilioni moja wanapitia ukatili majumbani, shuleni, kwenye mitandao au jamii zao, anazungumza wakili wa usalama wa watoto Howard Taylor. Tatizo ni la kijamii, kiuchumi, kisiasa -- na haraka. Katika mazungumzo ya kufungua macho, Taylor anaonyesha kwa nini tuna fursa adimu sasa hivi kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na kutengeneza hatma nzuri kwa kila mtoto.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
11:15

Swahili subtitles

Revisions