(Haya mazungumzo yana mambo pevu) Kila wakati naulizwa unafanya kazi gani. Na ninajibu, "Ninafanya kazi kutokomeza ukatili dhidi ya watoto. Ukatili wote dhidi ya watoto wote katika nchi zote." Kawaida kunakuwa na ukimya. Maranyingine, kulingana na mazingira, "Oh, hiyo inaua mazungumzo." Halafu maswali: "Ukatili wa aina gani unaozungumzia?" "Kuna ukatili kiasi gani?" "Inatokea maeneo gani, inatokea hapa?" Na ninapojibu hayo maswali, watu huwa wanashangazwa. Wanashangazwa na ukubwa wa ukatili, wanashangazwa na asili ya ukatili. Lakini mara zote ninakuwa mwepesi kuhakikisha Kuwa watu hawaachwi katika hali ya majonzi na huzuni. Ninaamini tunayo fursa adimu ya kihistoria katika kizazi hiki kutokomeza ukatili dhidi ya watoto Kuna harakati zinazokua kuhusiana na hili. Serikali, serikali za kitaifa, serikali za majiji, majimbo na wengine wanajiunga katika harakati hizo. Na tutakapofanikiwa-- na itatuhitaji sote-- tutabadilisha mwelekeo wa historia ya binadamu. Ninamaanisha nini kwa ukatili dhidi ya watoto? Ninamaanisha ukatili wote wa kimwili, kingono, kihisia na ukatili wa kisaikolojia unaotokea kwa watoto nyumbani, shuleni, kwenye mitandao na katika jamii zao. tunafanya kazi na washirika ulimwenguni kote na kutoka kwa hao washirika, tunasikia hadithi mbaya za mtoto mmoja mmoja. Kwa mfano, Sarah, ana miaka 10. Amebakwa mara kadhaa na baba yake wa kambo na kutishiwa ukatili kama akimwambia mtu. Faisal, alipigwa katika viganja vya mikono shuleni kwa waya, kadhalilishwa na kuitwa punda akasimamishwa nje kwenye baridi kwa kukosea kujibu swali. Na kwa washirika tunaofanya nao kazi kufanya mitandao uwe salama kwa watoto tunasikia hadithi kama za Angelika. Miaka kumi na mbili, akilazimishwa kufanya ngono na mjomba wake, huku akirekodiwa na kuangaliwa na watu wazima wanaolipia Mmoja kati ya wasichana 10 amepitia ukatili wa kingono kabla ya miaka 20. Nusu ya watoto wanaishi kwenye nchi ambazo hadhabu za viboko hazijapigwa marufuku. na mwaka jana tu, Marekani, taarifa milioni 45 zilitengenezwa za picha na video za ukatili na unyanyaswaji wa watoto mitandaoni Idadi hiyo ni mara mbili ya mwaka uliopita sasa ukatili wa namna hii na ukatili wa namna nyingine unajikusanya kuwa idadi kubwa ya kushangaza sana. Watoto bilioni moja ulimwenguni kila mwaka wanaopitia aina fulani ya ukatili. Hiyo ni mtoto mmoja kwa kila wawili. Hili ni tatizo la ulimwengu wote. Hivyo ni nini kinachonipa matumaini? Ngoja nizungumzie kuhusu Sweden na Uganda. Labda ni nchi mbili zilizo tofauti sana kama unavyofikiri. Ukizungumza na mchumi, wanaweza kusema kuwa Sweden ina kipato cha wastani wa takriban dola 50,000 kwa mwaka. Na Uganda, ni dola 2,000. Mwana historia atasema Sweden haijawahi kuwa katika mgogoro wa wa kitaifa kwa miaka takriban 200. Uganda bado inahangaika na migomo kaskazini mwa nchi. Mwanamuziki anaweza kusema kuwa Uganda, wimbo wa taifa, "Oh Uganda, Ardhi ya Uzuri" ni moja kati ya fupi sana ulimwenguni. Fupi mno, Mara nyingi inachezwa zaidi ya mara moja. Ninaamini Sweden hucheza yao na kuimba yao muda mrefu zaidi. Lakini kwa kumaanisha zaidi, Sweden na Uganda walifanya makubaliano, wana muunganiko mmoja na kusudi moja, makubaliano ya kutokomeza ukatili dhili ya watoto, na wanachukua hatua kujaribu kufanya nchi zao kuingia kwenye njia ya kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya watoto ifikapo 2030. Na nchi nyingine nyingi, majiji na majimbo yanaungana nao, duniani kote. Lakini inamaanisha nini haswa, inamaanisha nini kwa vitendo? Wanapofanya makubaliano hayo, wanafanya nini? Inamaanisha makubaliano ya hali ya juu kisiasa na kiuongozi. Kuweka na kutekeleza sheria. Na kuzindua mikakati, kubadilisha sera, Kuanzisha mazungumzo ya kitaifa ambayo yataanza kuamsha uelewa juu ya safari ya kubadili mitazamo na kufanya iwe haikubaliki kijamii kuwa na ukatili na unyanyasaji wa watoto katika nchi. Inamaanisha kutambua kuwa ukatili dhidi ya watoto upo katika nyanja zote, na hivyo mwitikio, na jibu, inabidi liwe na namna ya mfumo. Huwezi tu kufanya kipengele kimoja. Inahitaji wadau mbalimbali ndani na nje ya serikali. Inahitaji vikundi vya kidini, sekta binafsi na vyombo vya habari, wanazuoni, asasi za kiraia na wengine. Na inahitaji kuyachukua yale ambayo ni mambo mazuri na ushahidi mzuri wa kidunia unaotuelezea, lakini kwa kutumia taarifa za nchi kuweka mwanga juu ya simulizi zinazofichwa juu ya ukatili katika nchi fulani Na kutumia taarifa hiyo kuelekeza mwitikio wa kitaifa, lakini pia kutumia kupima na kufuatilia maendeleo. Na kushirikisha kile kinacholeta matokeo, kuwa wakweli pale ambapo mambo hayatokei. Na kushirikisha hamasa pale tunapoona mafanikio na ukatili ukipungua. Lakini je, tunaweza kufanya hili katika ngazi ya kiulimwengu? Watoto billioni moja kila mwaka wanapitia ukatili. Ninadhani kunaweza. Mwaka 2015, viongozi wa nchi 193 walikubali nchi zao kutokomeza ukatili, unyanyasaji na kutelekeza watoto ifikapo 2030. Ukatili dhidi ya watoto unaharibu yale yote tunayowekeza kwao: kwenye afya zao, elimu zao Mara nyingi kwa miaka wakati mwingine madhara na maambukizo ya maisha na vizazi. Lakini sio tu kuhusu makubaliano ya kimataifa na serikali Inajalisha sana. Lakini baadhi ya vitu pia vinabadilika kimsingi na sisi kama jamii ulimwenguni kote tunakataa tabia zisizokubalika ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikivumiliwa. Fikiri kuhusu harakati ya MIMI PIA namna ambavyo kitengo kwa kitengo tasnia kwa tasnia inawakamata wahalifu kuwaleta na kuwatia hatiani. Ni safari, lakini tumeianza. Angalia kilichotokea katika tasnia ya misaada. Baada ya matumizi mabaya ya madaraka, tasnia ya misaada sasa hivi inaangalia kwa makini sana Usalama wa watoto ulimwenguni kote. Lakini labda zaidi ya hivyo. Watoto na vijana wenyewe, kwa sehemu kwa msaada wa teknolojia, lakini kwa sasa wana sauti ambayo sidhani kama walikuwa nayo hapo awali. Na wanatumia sauti hiyo, Sio tu kuzungumzia hali inayowazunguka au kile wanachojua kinahitaji kuboreshwa, lakini kuwa sehemu ya suluhu ya mambo ambayo yanaelezea na kuathiri maisha yao. Fikiri kuhusu wanaharakati hawa wadogo ambao wanazungumza kupinga ukeketaji wa wanawake, ndoa za utotoni, uonevu wa kimtandao, shule salama, migogoro inayoumiza-- na listi inaendelea na kuendelea. Watoto hao ni wa muhimu sana. Hivyo tuna uongozi wa kisiasa, tuna wanaharakati wadogo, tuna suluhu zilizothibitishwa tuna uelewa wa jamii unaoongezeka-- tuko katika njia hiyo, tumeanza safari hiyo kutokomeza kabisa ifikapo 2030. Lakini suluhu hiso ni zipi? Miaka mitatu iliyopita, 2016, taasisi 10 za kiulimwengu zilikutana na kujipanga katika mpango ambao ni jumuishi, na mkakati wa hatua kwa hatua kutokomeza ukatili dhidi ya watoto. Unaoitwa INSPIRE. Uliangalia katika uhitaji wa sheria zinazoenda na wakati zinazogusia taratibu za kijamii, msaada wa wazazi na walezi, kutoa mwitikio kwa watoto waliopitia ukatili na unyanyaswaji. Na shule salama, ili watoto wawe katika mazingira ya kujifunza ambapo watanawiri. Kule Uganda, miaka minne iliyopita, msichana wa miaka nane angeweza kuolewa na mwanaume wa miaka 30. Hilo haliwezi kutokea tena. Mwaka 2016, Sheria ya mtoto ilifanya hilo kuwa kosa na kufanya umri wa chini kuolewa kuwa miaka 18. Hiyo ndiyo I ya INSPIRE: kupitisha na kutekeleza sheria. Cambodia inatoa msaada wa malezi, msaada kwa wazazi na walezi nchi nzima, hivyo wazazi wanapewa uwezo kulea watoto wao na kuweka nidhamu kwa namna isiyo ya kikatili nyumbani. hiyo ndiyo P ya INSPIRE, msaada kwa wazazi na walezi. Kule Uphilipino, Kuna vituo 100 vilivyowekwa kuwalinda wanawake na watoto nchi nzima. Wanawake na watoto ambao wako katika hatari kubwa ya ukatili na unyanyaswaji au waliopitia unyanyaswaji. Hiyo ndiyo R ya INSPIRE, huduma ya mwitikio na msaada. Na kule Uganda, zana ya shule salama imeshaanza kutumika kwa nusu ya walimu wa Uganda, ikiwawezesha kusimamia darasa kwa njia za kinidhamu zisizo za kikatili. Hiyo ndiyo E ya INSPIRE, elimu na stadi za maisha. Hiyo ni sehemu ndogo tu katika mpango wa INSPIRE. Lakini nchi nyingi zaidi zimekubali kuutekeleza, kuufanya uwe wa ndani, kuujaziliza kwa taarifa za wakati, na kuweka mpango pamoja, kufanya kazi kati ya vitengo, na kuanza ile safari ya kutokomeza. Canada, Mexico, Jamuhuri ya Kiarabu, Tanzania -- Nilishazitaja Sweden na Uganda -- Japan, Uphilipino, Indonesia, nchi nyingi zaidi, na sana miji, pia. Na hapa tulipo Scotland, Chuo cha Edinburgh kinatengeneza maabara ya kujifunzia ambayo itaenda kufuatilia safari kuwa miji ya Scotland na Uphilipino na Colombia inakwenda pamoja. Kuona kinachofanikiwa, kuchukua kile kilichotayarisha kutekelezwa katika nchi nzima na kuiweka chini kwa ngazi ya jiji, ambapo tunaamini kwamba tunaweza kufanya maendeleo ya haraka na ya kuonekana katika muda mfupi. Na tunapofanya hivyo, mafanikio hayo yatashirikishwa kupitia maabara ya mafunzo na zaidi katika Chuo kikuu cha Edinburgh. Kutokomeza ukatili ni jambo sahihi, ni uwekezaji makini, tunazo suluhu zilizothibitishwa, na tunao mwanzo wa safari. Lakini nini kitatokea Pale tutakapotokomeza ukatili dhidi ya watoto? Hebu tutafakari kwa muda. Kwanza, tafakari kuhusu watoto niliowataja. Sarah hatalala tena kitandani kwake usiku, akihofu juu ya sauti ya hatua za baba yake wa kambo akija juu kwenye ngazi. Faisal atakwenda shule na atanawiri. Hataogopa tena kuwa shuleni na kuonewa na kupigwa na kudhalilishwa na walimu. Na Angelika na wengine kama yeye hawatakuwa tena kama bidhaa inayoletwa mtandaoni kuwafurahisha watu wazima walioko maili nyingi mbali. Lakini kuzidisha manufaa ya kijamii, ya kiuchumi na kitamaduni ya hiyo. Kuzidisha hiyo kwa kila familia, kila jamii, kijiji, mji, jiji, nchi na ghafla, umepata utaratibu mpya umezaliwa. Kizazi kitachipua bila kupitia ukatili. Itatuhitaji sisi sote. Lakini tunayo fursa adimu ya kujaribu, na kuamini sisi pia, kama wazazi, tunajukumu la kufanya hivi. Halafu pale wote tunapoulizwa, "Unafanya kazi gani?" kila mmoja wetu anaweza kusema, " Ninabadilisha mwelekeo wa historia ya binadamu. Ninafanya kwa sehemu kutokomeza ukatili dhidi ya watoto." Hebu tufanye hili na tufanye sasa. Asanteni. (Makofi)