-
(Kuimba)
-
♪ (muziki) ♪
-
(Kuimba)
-
Hatari ya kusahau
ndiyo njia ya kutoweka kabisa.
-
Samaki wetu wa salmoni sasa ni spishi zinazohatarishwa.
-
Winnemem Wintu pia wangekuwa
kwenye orodha ya spishi zinazohatarishwa.
-
Samaki salmoni wanapopungua,
Winnemem Wintu pia wanapungua.
-
♪ (muziki) ♪
-
Nilikuja Bungeni
kuomba haki ya Kabila la Kalash,
-
linalohatarishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
-
Jamii hii ina miaka 6,000
na ina watu takriban 4,000 tu.
-
Jamii nzima iko katika hatari ya kufutika.
-
Kuheshimu ujuzi wa asili kuhusu mazingira,
-
kufungua fursa za kujifunza
-
kutoka kwa watu wanaoendelea
kuishi karibu na mazingira haya
-
ni fursa yetu sote
kukuza ujuzi wetu
-
kuhusu yanayotokea kwa sayari hii.
-
Ujuzi sio wa kitaaluma tu.
-
Ujuzi unaokuja
kupitia kukaa mahali pamoja
-
kwa muda mrefu, ni tofauti
-
na mtu anayejifunza
kwa miaka 5 au hata 20.
-
Ninawakilisha mamia ya miaka
ya ujuzi wa asili wa kienyeji.
-
Kwetu ni muhimu sana kuona
-
jinsi vizazi vijana
wanaweza kulinda mazingira zaidi.
-
Lakini pia jinsi ujuzi huu wote
unaweza kulindwa
-
kutulinda na kulinda
mustakabali wetu.
-
(Kihispania)
Sisi, watu wa asili wa dunia,
-
tunajua jinsi ya kuishi kwa maelewano
na Mama Dunia yetu.
-
Kwa sababu tunaiheshimu.
-
Kwa sababu tunaelewa kuwa ni muhimu
kudumisha usawa.
-
Usawa na uwiano.
-
♪ (muziki) ♪
-
Tukumbuke kwamba
kile ambacho hapo awali kilikuwa sauti ya waliodhulumiwa
-
sasa ni hotuba ya hekima ya mandhari.
-
Ninaamini kwa ajili ya kesho,
-
kwa wajukuu wetu
-
na vitukuu vyenu,
-
itakua ya kusisimua
-
kwa sababu tumejitoa
kuhakikisha hilo linatimia.
-
(akizungumza kwa Kihispania)
Ni muhimu kuleta mabadiliko sasa,
-
kwa sababu hatuna muda mwingi.
-
Tunapigania mabadiliko hayo.
-
Na dunia, IUCN, na wanachama wake,
-
wanahitaji kutambua
kwamba mabadiliko ni ya dharura.