< Return to Video

Mgongano na Ujinga| Shafique Virani | TEDxUTSC

  • 0:14 - 0:16
    Kwa hiyo nimetua tu kwa ajili ya mkutano wa TED,
  • 0:16 - 0:18
    na wakati nilipokuwa nasubiria ndege uwanjani
  • 0:18 - 0:21
    Nilitokea kukutana na rafiki wa familia
    ambaye hatujaonana kwa muda mrefu.
  • 0:21 - 0:23
    Tunamwita mjomba Anwar
  • 0:23 - 0:27
    na anafanana sana Babar wa komedia maarufu ya Kikanada
  • 0:27 - 0:28
    Msikiti mdogo kwenye Praire.
  • 0:28 - 0:29
    (Vicheko)
  • 0:29 - 0:32
    Anapenda kuvaa nguo zake za kiasili za
    pajama za kurta,
  • 0:32 - 0:37
    anajitambia ndevu na lafudhi ya kupendeza ya Kipakistani.
  • 0:37 - 0:39
    Kwa hiyo alinikimbilia na kunikumbatia,
  • 0:39 - 0:43
    na kusema, "Unaendeleaje?
    Unafanya nini siku hizi? "
  • 0:43 - 0:46
    Kwa hiyo nikamwambia kuwa nimekuwa Profesa wa Mafunzo ya Kiislamu,
  • 0:46 - 0:50
    na najiweka bize nikisafiri na kutoa mafunzo
  • 0:50 - 0:52
    kusaidia watu kuuelewa Uislamu
    kidogo zaidi,
  • 0:52 - 0:55
    hasa baada ya 9/11.
  • 0:56 - 0:58
    Alinitazama machoni na kusema,
  • 0:58 - 1:01
    "Usizungumze na mimi kuhusu 9/11!
  • 1:01 - 1:06
    Kila ninapoenda, kila mtu ananiangalia
    kama ninawajibika kwa 9/11!
  • 1:06 - 1:10
    Mimi, nawajibika kwa 9/11?
  • 1:10 - 1:13
    Maduka ya 7-Eleven labda, lakini sio 9/11! "
  • 1:13 - 1:16
    (Vicheko) (Makofi)
  • 1:16 - 1:18
    Kama nilivyomwambia Uncle Anwar,
  • 1:18 - 1:21
    Nimekuwa nikisafiri sana
    na kutoa mazungumzo mengi,
  • 1:21 - 1:23
    na moja yao ilikuwa katika Kilabu ya Taifa ya Waandishi wa Habari.
  • 1:23 - 1:28
    Kipindi hicho, kemikali ya DHM ilikuwa ikizungumziwa sana.
  • 1:28 - 1:32
    Kiuhalisia, katika Idaho, asilimia 86 ya waliofanyiwa uchunguzi
  • 1:32 - 1:35
    walitaka kuipiga marufuku kemikali hii.
  • 1:35 - 1:39
    Ningependa kuwaambia mambo kadhaa muhimu kuhusu kemikali hii,
  • 1:39 - 1:41
    na kisha kuwauliza maoni yenu.
  • 1:41 - 1:43
    Mambo yote nitayowaambia
  • 1:43 - 1:47
    yamechapishwa katika fasihi zilizopitiwa na wanataaluma
  • 1:47 - 1:50
    na zimethibitishwa na wanasayansi mahiri
  • 1:50 - 1:53
    huko Harvard, MIT, Chuo Kikuu
    cha Toronto, na Oxford.
  • 1:54 - 1:59
    DHM haina rangi, harufu wala ladha.
  • 1:59 - 2:05
    Kuihema DHM kwa muda mrefu hudhuru sana mwili wa binadamu
  • 2:06 - 2:11
    Dalili za kumeza DHM
    ni pamoja na jasho jingi, kukojoa,
  • 2:11 - 2:17
    na kuhisi kujaa gesi, kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kukosa usawa wa elektrolaiti ya mwili.
  • 2:18 - 2:24
    DHM imekutwa katika wagonjwa wa kansa.
  • 2:25 - 2:27
    Kuivuta DHM kwa bahati mbaya
  • 2:27 - 2:31
    ni chanzo kikuu cha tatu duniani cha kifo cha bila kunuia,
  • 2:31 - 2:34
    na kusababisha vifo karibu 400,000 kila mwaka,
  • 2:34 - 2:38
    kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani.
  • 2:39 - 2:41
    Kwa wale ambao watakuwa wategemezi,
  • 2:41 - 2:45
    Uondoaji wa DHM humaanisha namna fulani ya kifo.
  • 2:46 - 2:53
    Kutokana na habari hii, wangapi kati yenu mtaruhusu DHM kupatikana bure?
  • 2:55 - 2:57
    Karibia hamna yoyote.
  • 2:57 - 2:59
    Mmekubaliana kikamilifu na watu
  • 2:59 - 3:02
    niliyoongea nao katika Kilabu ya Taifa ya Waandishi wa Habari.
  • 3:02 - 3:04
    Napenda kuwaambia zaidi kidogo kuhusu hilo.
  • 3:04 - 3:07
    DHM ni Dioksidi ya Hidrojeni Monoksidi.
  • 3:07 - 3:11
    Pia inajulikana kama Hidrojeni Hydroksidi.
  • 3:11 - 3:14
    Lakini wengi wetu labda tunajua
    kwa jina lake la kawaida,
  • 3:14 - 3:16
    ambayo ni maji.
  • 3:18 - 3:22
    Kila nilichowaambia ni ukweli
  • 3:22 - 3:27
    uliothibitishwa na wanasayansi bora duniani kote.
  • 3:27 - 3:31
    Na bado, karibu kila mtu katika hadhira hapa
  • 3:31 - 3:35
    yuko tayari kupunguza upatikanaji wetu wa maji.
  • 3:36 - 3:40
    Tunapowasilishiwa kipengele fulani cha habari tu,
  • 3:40 - 3:45
    hujikuta tukifanya makosa katika ukadirifu wetu na maamuzi mabaya.
  • 3:46 - 3:49
    Hadithi ya DHM inadhihirisha mengi kuhusu
  • 3:49 - 3:52
    mada ambayo nataka
    kuzungumza nanyi,
  • 3:52 - 3:57
    aina nyingine ya DHM
    ambayo ni mbaya zaidi kuliko hii.
  • 3:57 - 4:01
    DHM ya kwanza ni
    Dioksidi ya Hidrojeni Monoksidi,
  • 4:01 - 4:05
    lakini ya pili ni kubagua utu wa Waislamu.
  • 4:06 - 4:07
    Media Tenor,
  • 4:07 - 4:11
    moja ya mashirika ya ulimwengu yanayoongoza katika maarifa na ufanisi wa vyombo vya habari,
  • 4:11 - 4:14
    ilipitia karibia nukuu milioni moja
    kuhusu Waislamu
  • 4:14 - 4:18
    katika vyombo vya habari vya Marekani na Ulaya.
  • 4:18 - 4:24
    asilimia 98 ya simulizi zilikuwa kuhusu ya wanamgambo wa Kiislam.
  • 4:24 - 4:31
    asilimia 2 tu zilikuwa kuhusu Waislamu wa kawaida bilioni 1.5,
  • 4:31 - 4:35
    robo ya wakazi wa dunia,
  • 4:35 - 4:37
    ambao tunaishi wote kwenye hii dunia.
  • 4:38 - 4:43
    Hii hali ni sawa na taarifa kuhusu niliyowapa kuhusu DHM.
  • 4:43 - 4:50
    Wakati habari zote tulizonazo ni kuhusu kipengele kimoja kisicho cha kawaida
  • 4:50 - 4:54
    sio tu tunashindwa kukielezea kipengele hicho,
  • 4:54 - 4:58
    lakini tunapata maana isiyo sahihi kabisa kuhusu suala hilo.
  • 4:58 - 5:03
    Tumechanganya vitendo
  • 5:03 - 5:08
    vya sehemu ndogo sana ya Waislamu duniani
  • 5:08 - 5:12
    na vya watu bilioni 1.5 duniani kote.
  • 5:12 - 5:16
    Ni sawa kama tukichukulia matendo ya Ku Klux Klan,
  • 5:16 - 5:18
    kuchoma msalaba, na kusema,
  • 5:18 - 5:22
    "Hii ni uwakilishi
    wa Ukristo wote. "
  • 5:22 - 5:26
    Kwa bahati mbaya, aina hii ya mchanganyiko unazidi kuongezeka na kuwa wa kawaida,
  • 5:26 - 5:31
    kama tunavyoona katika ujumbe nyuma ya lori hilo, ambao unasema,
  • 5:31 - 5:36
    "Kila kitu nilicho wahi kuhitaji kujifunza kuhusu Uislamu nilijifunza 9/11. "
  • 5:38 - 5:41
    Naikumbuka 9/11 vizuri sana.
  • 5:41 - 5:44
    Nilikuwa nimeteuliwa katika kitivo cha Chuo Kikuu cha Harvard,
  • 5:44 - 5:48
    na nilipokuwa nikijiandaa na darasa langu la kwanza.
  • 5:48 - 5:50
    Nakumbuka darasa hilo.
  • 5:50 - 5:54
    Wanafunzi na mimi tulijitahidi kuelewa
  • 5:54 - 5:57
    uovu tuliokuwa tumeshuhudia.
  • 5:58 - 6:00
    Nilichokuta kinatia moyo
  • 6:00 - 6:07
    ilikuwa kwamba wote walikuwa wazi na wenye nia ya kujifunza na kuelewa.
  • 6:07 - 6:11
    Waligundua kuwa katika miaka yao yote ya kujifunza shuleni
  • 6:11 - 6:16
    hawakuwa na ukaribu na ulimwengu wa Kiislamu
  • 6:16 - 6:19
    na kwa hiyo, walitaka kuelewa.
  • 6:19 - 6:24
    Walitaka kuiona
    dunia hii katika uhalisia wake.
  • 6:24 - 6:29
    Tofauti kati ya ujumbe nyuma ya lori hii na hawa wanafunzi
  • 6:29 - 6:33
    inanikumbusha kifungu katika kitabu ambacho ninatafsiri
  • 6:33 - 6:38
    kilichotungwa na mwandishi maarufu
    kwa jina la Nasiruddin Tusi,
  • 6:38 - 6:40
    mmoja ya wanasayansi maarufu wa Kiislamu
  • 6:40 - 6:43
    na wanafalsafa kutoka zama za Kati.
  • 6:43 - 6:45
    Kifungu hiki kinasema,
  • 6:45 - 6:52
    "Yeye asiyejua na hajui
    kwamba hajui ni mpumbavu.
  • 6:52 - 6:54
    Muepuke.
  • 6:54 - 6:59
    Yeye asiyejua na anajua
    kwamba hajui ni mtafutaji.
  • 6:59 - 7:01
    Mfundishe.
  • 7:02 - 7:07
    Yeye anayejua na hajui
    kwamba anajua amelala.
  • 7:07 - 7:08
    Muamshe.
  • 7:09 - 7:15
    Na yeye anayejua na anajua kwamba anajua ni mwenye hekima.
  • 7:15 - 7:17
    Mfuate. "
  • 7:19 - 7:23
    Moja ya sababu 9/11 imewekwa kwenye kumbukumbu yangu,
  • 7:23 - 7:26
    labda kuliko watu wengine wengi
  • 7:28 - 7:30
    inaweza kusimuliwa na picha hii.
  • 7:31 - 7:35
    Huyu ni mjomba wangu, Salman Dhanani.
  • 7:35 - 7:39
    Alikuwa anajitolea katika jamii yake New York;
  • 7:39 - 7:45
    mpiganaji wa kweli wa haki za binadamu aliyekuwa daima akisaidia katika nchi zinazoendelea.
  • 7:47 - 7:51
    Alikuwa Makamu wa Rais
    wa kampuni ya bima inayoitwa Aon,
  • 7:51 - 7:54
    ambayo ilikuwa na ofisi zake kwenye sakafu ya 99
  • 7:54 - 7:58
    ya Mnara wa Kusini
    ya Kituo cha Biashara cha Dunia
  • 7:59 - 8:02
    Katika siku hiyo ya huzuni,
  • 8:02 - 8:05
    wakati ndege hizo
    ziliangukia ndani ya majengo hayo,
  • 8:05 - 8:09
    alikuwa na jukumu
    kwa kuwaokoa wafanyakazi wenzake.
  • 8:09 - 8:15
    Aliokoa maisha ya wenzake 80, na wakakimbia.
  • 8:16 - 8:20
    Lakini hadi walipotoka,
    alikuwa kachelewa.
  • 8:20 - 8:23
    Alikuwa amenaswa.
  • 8:23 - 8:28
    Na leo amezikwa chini ya saruji
  • 8:28 - 8:31
    ya lililowahi kuwa Kituo cha Biashara cha Dunia.
  • 8:31 - 8:33
    Alikuwa na miaka 63.
  • 8:35 - 8:39
    Picha hii imechukuliwa siku chache kabla ya kifo chake,
  • 8:39 - 8:41
    wakati baadhi ya watu katika familia yangu,
  • 8:41 - 8:47
    mjomba wangu Nizar, shangazi yangu Mumtaz
    na binamu yangu Fatima walimtembelea
  • 8:47 - 8:50
    na walipiga picha hii
    nje ya Umoja wa Mataifa.
  • 8:51 - 8:56
    Hawa ni Waislamu wa kawaida ambao hatusikii hadithi zao.
  • 8:58 - 9:01
    Utupu wa ufahamu ambao tunao
  • 9:01 - 9:04
    kuhusu ni robo ya binadamu
    katika ulimwengu wa Kiislamu.
  • 9:04 - 9:09
    Nadhani imedhihirishwa vyema na kura iliyotolewa mwezi uliopita,
  • 9:09 - 9:12
    na kati ya makampuni yanayoheshimika kwa upigaji kura dodoso nchini Marekani,
  • 9:12 - 9:14
    Upigaji kura kwa ajili ya Sera ya Umma.
  • 9:14 - 9:19
    Walihoji Wamarekani elfu moja, wa chama cha Democratic na cha Republican,
  • 9:19 - 9:22
    na matokeo yake, ninakuahidi
  • 9:22 - 9:26
    nisingeweza kufoji hata nikijaribu.
  • 9:26 - 9:30
    Robo moja ya Wamarekani
    wanafurahia kulipua Agrabah.
  • 9:30 - 9:32
    (Vicheko)
  • 9:32 - 9:36
    Sasa, kwa wale ambao hamjui,
    Agrabah ni ufalme wa kufikirika
  • 9:36 - 9:38
    kutoka hadithi maarufu ya Disney ya Aladdin.
  • 9:38 - 9:41
    (Vicheko) (Makofi)
  • 9:41 - 9:44
    Inashtua kwamba robo ya watu
  • 9:44 - 9:47
    walitaka kulipua ufalme wa kufikirika
  • 9:47 - 9:52
    labda kwa sababu itakuwa mahali fulani katika Mashariki ya Kati.
  • 9:52 - 9:57
    Lakini nadhani hilo, inaelezea tu kidogo, sivyo?
  • 9:57 - 10:04
    Kwa sababu picha tuliyo nayo
    ya watu wa kawaida
  • 10:04 - 10:09
    wanaoishi katika sehemu hiyo ya ulimwengu ni kama ya kufikirika, sivyo?
  • 10:10 - 10:15
    Na ni kitu ambacho nadhani
    kimekua kutokea vizazi kadhaa.
  • 10:15 - 10:18
    Hata hivyo, labda ni kama unabii
  • 10:18 - 10:21
    kwamba hii ilikuwa kuhusu ya kufikiria
    ufalme katika Aladdin,
  • 10:21 - 10:24
    kwa sababu hiyo ilikuwa kati ya filamu nilizopenda nikiwa mdogo.
  • 10:24 - 10:29
    Na ninakumbuka wimbo wa kwanza
    wa msimulizi.
  • 10:29 - 10:33
    Waliimba, "Oh, nimetokea katika nchi,
    Kutoka mahali pa mbali,
  • 10:33 - 10:36
    Ambapo ngamia za wasafiri huzunguka,
  • 10:36 - 10:39
    Ambapo hukata sikio lako
    Ikiwa hawapendi uso wako,
  • 10:39 - 10:43
    haijastaarabika, lakini ati, ni nyumbani! "
  • 10:43 - 10:48
    Kutokea umri mdogo, watoto wanajifunza
  • 10:48 - 10:55
    kwamba watu wa ulimwengu huu wa Kiislam sio wastaarabu, wakatili.
  • 10:56 - 11:01
    Hakuna aliyefanya utafiti zaidi
    kuhusu hili kuliko Profesa Jack Shaheen.
  • 11:01 - 11:03
    Alipitia filamu karibu na elfu moja
  • 11:03 - 11:07
    zilizozalishwa zaidi ya kozi
    ya zaidi ya miaka mia kupitia Hollywood
  • 11:07 - 11:11
    na kupatikana kumi na mbili tu
  • 11:11 - 11:16
    ambayo ilionyesha Waislam au Waarabu
    kwa nuru nzuri.
  • 11:16 - 11:18
    Kwa kweli, alifikia hitimisho
  • 11:18 - 11:23
    kwamba kama kulikuwa na muigizaji wa kiume wa Kiislamu au wa Kiarabu katika filamu,
  • 11:23 - 11:26
    kutakuwa na nafasi ya 95%
    kwamba angeonyeshwa
  • 11:26 - 11:30
    kama mgomvi, mwenye tamaa au asiye muaminifu -
  • 11:30 - 11:33
    95%!
  • 11:36 - 11:40
    Watu kama Samuel Huntington
    wameelezea hali yetu ya sasa ya ulimwengu
  • 11:40 - 11:43
    kama "Mgongano wa Ustaarabu."
  • 11:44 - 11:45
    Zaidi kuwa wafikiriaji,
  • 11:45 - 11:50
    ambao tunatambua na kuelewa
    sehemu nyingine za dunia bora zaidi,
  • 11:50 - 11:55
    kutambua kwamba tunakabiliwa na "Mgongano wa Ujinga."
  • 11:56 - 11:59
    Tunawezaje kukabiliana na Mgongano wa Ujinga?
  • 11:59 - 12:02
    Naam, hili ni wazo
    ambalo nadhani ni muhimu kueneza.
  • 12:03 - 12:05
    Mimi kukaa kwenye bodi ya uongozi
  • 12:05 - 12:09
    ya Mpango wa Madrasa ya Watoto Afrika Mashariki,
  • 12:09 - 12:16
    ambayo hufikia zaidi
    maeneo duni ya mahali hapa,
  • 12:16 - 12:19
    kwa watoto ambao hawana uwezo wa kwenda shule.
  • 12:20 - 12:22
    Miaka thelathini iliyopita,
  • 12:22 - 12:25
    viongozi wa Kiislam kando ya pwani ya eneo hili
  • 12:25 - 12:27
    walionana na mtukufu Aga Khan,
  • 12:27 - 12:32
    ambaye babu yake alianzisha
    shule za kwanza za jamii ya mchanganyiko wa taifa
  • 12:32 - 12:33
    katika mkoa mzima,
  • 12:33 - 12:38
    kuuliza kama angeweza kuwasaidia kuwaelimisha watoto wadogo
  • 12:38 - 12:41
    katika jamii hizi zisizohitajika.
  • 12:42 - 12:46
    Kwa wakati huo, walianzisha mtaala wa ubunifu
  • 12:46 - 12:49
    ambao umesisitizwa
    kwenye CNN na BBC,
  • 12:49 - 12:53
    ambao unafundisha masomo yote
    kama inavyotegemewa kawaida,
  • 12:53 - 12:54
    lakini kwa kuongeza,
  • 12:54 - 12:57
    sehemu ya msingi ya mtaala
  • 12:57 - 13:00
    kwamba watoto wangu, unaowaona katika picha hii,
  • 13:00 - 13:03
    hujifunza kutoka katika umri mdogo
  • 13:04 - 13:09
    ni kwamba lazima wautambue wingi wa ulimwengu.
  • 13:09 - 13:11
    Wanapaswa kujifunza
    kuhusu vikundi vya lugha,
  • 13:11 - 13:15
    makabila,
    aina ya kabila na dini
  • 13:15 - 13:20
    wanaoshirikiana nao vijiji vyao, miji yao,
    nchi yao na dunia yetu.
  • 13:20 - 13:26
    Kwa maneno mengine, watoto hawa wadogo
    kukua na "maadili ya tamaduni nyingi."
  • 13:27 - 13:31
    Sasa, wengi wenu mnaweza kukumbuka,
    mwanzoni mwa mwaka 2008,
  • 13:31 - 13:35
    Kenya ilikuwa inakabiliwa na vurugu kali.
  • 13:35 - 13:38
    Vurugu za baada ya uchaguzi
    zilipotokea kote nchini,
  • 13:38 - 13:41
    kulikuwa na mauaji mabaya
  • 13:41 - 13:44
    pale wafuasi
    wa rais Mwai Kibaki
  • 13:44 - 13:47
    walipigana dhidi ya wafuasi
    wa mpinzani wake.
  • 13:48 - 13:52
    Kabila la Kikuyu, kabila la Luo, kabila la Kalenjin
    walikuwa wanauana.
  • 13:52 - 13:57
    Maelfu ya watu waliuawa;
    mamia ya maelfu walihamishwa.
  • 13:57 - 14:01
    Shule zetu zote sabini na tano
    Kenya zilifungwa.
  • 14:01 - 14:03
    Tulikuwa na wasiwasi.
  • 14:03 - 14:07
    Shule zetu zilipatikana
    katika maeneo maskini zaidi ya nchi,
  • 14:07 - 14:12
    maeneo ambayo yanawezekana zaidi
    kuathirika na vurugu hii.
  • 14:13 - 14:17
    Wakati bodi yetu ilipokuwa na mkutano wake,
  • 14:17 - 14:23
    Niliomba mara moja ripoti iwe tayari kutuambia,
  • 14:23 - 14:25
    "Ni nini kilichotokea kwa watoto wetu?"
  • 14:25 - 14:28
    "Ni nini kilichotokea kwa walimu wetu?"
  • 14:28 - 14:31
    "Je! Wazazi wanaojitolea
    katika shule zetu wapo salama? "
  • 14:31 - 14:34
    "Je, jamii zetu zipo salama?"
  • 14:34 - 14:36
    "Ni wangapi wamefariki?"
  • 14:37 - 14:41
    Ripoti hiyo iliporudi,
    tulishangazwa kwa kile tulichosoma.
  • 14:42 - 14:47
    Hakuna shule hata moja katika jumuiya zetu
  • 14:47 - 14:51
    ilikuwa imeathiriwa na vurugu.
  • 14:52 - 14:53
    Hata moja.
  • 14:54 - 15:00
    Na nina uhakika kwamba ni kwa sababu,
    kwa miaka thelathini iliyopita,
  • 15:00 - 15:04
    watoto hawa wamekua
    kujifunza kuhusu majirani zao,
  • 15:04 - 15:08
    kujifunza kuhusu makabila,
    na lugha, na nyimbo,
  • 15:08 - 15:13
    na dansi ya kila mtu
    katika mazingira yao,
  • 15:13 - 15:15
    na katika ulimwengu unaowazunguka.
  • 15:15 - 15:21
    Wamepewa chanjo ya kuepuka
    virusi vya chuki na uharibifu
  • 15:21 - 15:24
    kwamba mara nyingi watu wanavyojaribu kueneza.
  • 15:25 - 15:31
    Je! Unaweza kufikiri kama watoto
    kote ulimwenguni wangepaswa kufundishwa
  • 15:31 - 15:33
    kama watoto hawa walivyofundishwa?
  • 15:34 - 15:39
    Je! Tungeweza kuona unyanyasaji wa dini
    katika nchi za Iraq na Syria kama tunavyoona sasa?
  • 15:39 - 15:43
    Je! Matatizo ya ubaguzi wa rangi
    nchini Marekani yangekuwa kama yalivyo sasa?
  • 15:43 - 15:48
    Je! Unyanyapaa wa Uislamu ungekuwepo katika ulimwengu wa magharibi kama tunaoshuhudia sasa?
  • 15:49 - 15:53
    Unajua, ufafanuzi wetu
    ya mtu mwenye elimu nchi za Magharibi
  • 15:54 - 15:58
    ina maana kwamba wanapaswa kutuambia
    kitu kuhusu Sir Isaac Newton,
  • 15:58 - 16:01
    kuhusu Mozart, kuhusu Napoleon.
  • 16:02 - 16:05
    Lakini tungekuwa na wakati mgumu sana
  • 16:05 - 16:08
    kugundua hata wengi ya watu walioelimika katika ulimwengu wa Magharibi
  • 16:08 - 16:13
    ambao wanajua sawa na wale
    katika ulimwengu wa Kiislamu.
  • 16:14 - 16:15
    Hii ni ukweli pamoja na kwamba
  • 16:15 - 16:19
    kwamba maneno kama "algebra" na "algorithm" yametoka katika lugha ya Kiarabu;
  • 16:19 - 16:24
    kwamba baadhi ya majengo mahiri ya kisanifu duniani,
  • 16:24 - 16:29
    kama Taj Mahal,
    yametokea katika tamaduni za Kiislamu;
  • 16:29 - 16:33
    na kwamba "Kanuni ya Utabibu", na Ibn Sina,
  • 16:33 - 16:38
    ilikuwa ni kitabu kikuu cha utabibu Ulaya kwa miaka mingi.
  • 16:40 - 16:45
    Tunahitaji kutekeleza maono ya kimataifa katika mtaala wetu wa elimu
  • 16:45 - 16:48
    kutokea umri mdogo kabisa,
  • 16:48 - 16:53
    ili watoto wakue na ufahamu wa
    ulimwengu ambao tunaishi,
  • 16:53 - 16:55
    watu ambao ni sehemu ya jamii yetu.
  • 16:56 - 17:01
    Katika mlango wa Umoja wa Mataifa
    kumeandikwa shairi la Kiajemi
  • 17:01 - 17:06
    la Sa'di-yi Shirazi, mshairi wa Kiislamu wa karne ya 13, ambaye ameandika,
  • 17:07 - 17:10
    (Kiajemi) Watoto wa Adamu
    ni kama viungo vinavyotegemeana.
  • 17:10 - 17:15
    "Watoto wa Adamu
    ni kama viungo vya mmoja na mwingine
  • 17:15 - 17:18
    Kwa maana wote walikuwa wameumbwa kutoka kwa nafsi moja.
  • 17:19 - 17:23
    Pale misukosuko ya wakati
    huumiza mguu mmoja,
  • 17:23 - 17:28
    inawezekana vipi viungo vingine kuwa na amani?
  • 17:28 - 17:32
    Wewe usiyehisi maumivu ya wengine
  • 17:32 - 17:37
    Unawezaje kujiiita mwana wa Adamu?
  • 17:37 - 17:41
    Unawezaje kujiita binadamu? "
  • 17:41 - 17:43
    Ile hisia kwamba sisi ni familia moja ya binadamu
  • 17:43 - 17:50
    imepelekea baadhi ya hadithi za kusisimua zinazotia moyo katika siku za hivi karibuni.
  • 17:50 - 17:54
    Katika miezi michache iliyopita,
    kama matokeo ya mashambulizi ya kigaidi,
  • 17:54 - 17:57
    baadhi ya misimamo ya kikatili katika Magharibi
  • 17:57 - 17:59
    imegeuka dhidi ya Waislamu kati yao,
  • 17:59 - 18:03
    ambao hawakuwa na la kufanya
    na mashambulizi haya ya kigaidi.
  • 18:03 - 18:07
    Tumeona wanawake wakisukumizwa
    mbele ya mabasi yanayotembea,
  • 18:07 - 18:09
    misikiti ikichomwa moto,
  • 18:09 - 18:14
    na kichwa cha nguruwe
    kutupwa katika shule ya watoto.
  • 18:14 - 18:16
    Wakati matukio haya yalianza kutokea
  • 18:16 - 18:20
    na Waislamu waliogopa
    kwenda nje katika jamii zao,
  • 18:20 - 18:24
    ndani ya masaa manne
    jumbe za Twitter 150,000 nchini Australia,
  • 18:24 - 18:28
    zenye lebo
    "Nitaendesha na wewe", ziliwekwa mtandaoni.
  • 18:28 - 18:30
    "Nitaendesha na wewe."
  • 18:30 - 18:33
    Tuko pamoja nawe.
    Wewe ni sehemu ya jumuiya yetu.
  • 18:33 - 18:36
    Huna chochote cha kuhofia.
  • 18:36 - 18:37
    Wiki chache zilizopita,
  • 18:37 - 18:42
    al-Shabab walishambulia basi
    njiani kwenda Mandera
  • 18:42 - 18:45
    kwenye mpaka wa Somalia na Kenya.
  • 18:45 - 18:47
    Walijaribu kuchukua Wakristo tu kutoka kwenye basi
  • 18:47 - 18:50
    kuwaua kinyama,
  • 18:50 - 18:52
    lakini Waislamu wailo kwenye basi hilo
  • 18:52 - 18:57
    walikataa kuruhusu ndugu zao wakristo wauawe.
  • 18:57 - 19:02
    Waliwaambia magaidi,
    "Huwezi kuchukua Wakristo hawa."
  • 19:02 - 19:06
    "Ikiwa unataka kuwaua,
    utatuua sisi sote. "
  • 19:06 - 19:11
    Wale magaidi waliogopa sana
    kwamba wakimbia.
  • 19:14 - 19:19
    Ikiwa tuna ufahamu kuhusu majirani zetu,
  • 19:19 - 19:22
    watu wanaounda ulimwengu wetu,
  • 19:22 - 19:26
    tutakuwa na silaha ya
    kusimama dhidi ya mtu yeyote
  • 19:26 - 19:31
    ambaye anatarajia kutoa utu wa wengine,
    ambaye anatarajia kutugawanya,
  • 19:32 - 19:38
    kwa sababu katika maneno ya Sa'di wa Shiraz,
    sisi wote ni watoto wa Adamu,
  • 19:38 - 19:42
    sisi ni familia moja ya binadamu.
  • 19:42 - 19:44
    Asante.
  • 19:44 - 19:46
    (Kushangilia)(Makofi)
Title:
Mgongano na Ujinga| Shafique Virani | TEDxUTSC
Description:

Akitoa ushahidi wa kustaajabisha, simulizi binafsi za kuvunja moyo, na ufahamu maridadi katika matukio ya ulimwengu, Dk. Shafique Virani anatuhimiza kukabiliana na mgongano na Ujinga kati ya Ulimwengu wa Magharibi na Uislamu, kuiondoa kuta za habari zisizo sahihi na kuweka madaraja ya ufahamu. Akitoa wito kwa uanadamu wetu, Dk. Virani anatoa njia ya maono, na huhamasisha matumaini kwa ajilli ya siku za mbeleni.

Profesa maarufu wa Mafunzo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Toronto, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha utamaduni wa Kusini mwa Asia, na Mwenyekiti wa awali wa Idara ya Mafunzo ya Historia, Dr Shafique Virani (PhD, Chuo Kikuu cha Harvard) ni mwandishi mwenye tuzo na kutambulika kimataifa kama msemaji wa umma aliyehutubia watu kutoka zaidi ya nchi 50 na wasikilizaji zaidi ya 15,000. Kitabu chake, Kina Ismaili katika zama za Kati: Historia ya uhimidi, Utafutaji wa Wokovu, inaaminika kuwa kitabu cha kwanza cha kitaaluma kutoka kwenye chuo kikuu kuu kuwa trailer yake cheyewe. Akitambulika kama”muonaji," Umoja wa Mataifa ulimtukuza kwa juhudi zake "katika kupanua mipaka ya ujuzi na ustawi wa wanadamu."

Majadiliano haya yalitolewa kwenye tukio la TEDx kwa kutumia muundo wa mkutano wa TED lakini kwa uhuru uliopangwa na jumuiya ya eneo. Jifunze zaidi katika http://ted.com/tedx

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDxTalks
Duration:
19:54

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions