YouTube

Got a YouTube account?

Νέο: ενεργοποιείστε μεταφράσεις και λεζάντες που δημιουργήθηκαν από θεατές στο κανάλι σας στο YouTube!

Swahili υπότιτλους

← NatureNow: Greta Thunberg and George Monbiot make short film on the climate crisis

Πάρτε τον Κωδικό ενσωμάτωσης
64 Γλώσσες

Υπότιτλοι μεταφρασμένοι από Αγγλικά Showing Revision 1 created 12/15/2019 by Julian Picotto.

 1. Hii si kwata.
 2. Jina langu ni Greta Thunberg.
 3. Tunaishi mwanzoni mwa uangamivu
  mkubwa
 4. Tabianchi yetu inakongoroka.
 5. Watoto kama mimi wanaacha masomo yao ili waandamane.
 6. Lakini bado tunaweza kurekebisha hili.
 7. Bado unaweza kurekebisha hili.
 8. Ili kuendelea kuishi, tuache kuchoma nishati ya visukuku, japo hili tu halitoshi.
 9. Masuluhisho mengi yanatajwa, lakini vipi suluhisho lililo mbele
 10. yetu?
 11. Nimwachie rafiki yangu George aeleze.
 12. Ipo mashine ya ajabu inayofyonza gesi ya ukaa hewani, ina gharama ndogo na inajijenga
 13. yenyewe.
 14. Inaitwa ... mti.
 15. Mti ni mfano wa suluhisho la asili la tabianchi.
 16. Mikoko, maeneo ya maozeo, mapori, maeneo chepechepe, sakafu za bahari, mwani, vinamasi, matumbawe, vina
 17. chukua gesi ya ukaa hewani na kuifungia.
 18. Maumbile asili ni zana ambayo tunaweza kutumia kurekebisha tabianchi yetu iliyokongoroka
 19. Masuluhisho haya asili kwa tabianchi yanaweza kuleta tofauti kubwa.
 20. Poa sana, sio?
 21. Lakini kama tu tutaacha nishati za visukuku ardhini.
 22. Na hii ndio balaa ... hivi sasa tunazipuuzia.
 23. Tunatumia mara elfu zaidi kwa ruzuku kwenye nishati za visukuku duniani kuliko kwenye masuluhisho
 24. ya asili.
 25. Masuluhisho asili ya tabianchi hupata 2% tu
 26. ya pesa zote zitumikazo kushughulikia kukongoroka kwa tabianchi.
 27. Hii ni pesa yako, ni kodi zako na akiba zako.
 28. Hata balaa zaidi, hivi sasa ambapo tunaihitaji asili zaidi
 29. tunaiharibu haraka kuliko wakati wowote.
 30. Hadi spishi 200 zinatoweka kila siku.
 31. Sehemu kubwa ya barafu ya Aktiki imetoweka.
 32. Wanyamapori wetu wengi wametoweka.
 33. Udongo wetu mwingi umetoweka.
 34. Sasa tufanye nini?
 35. Utafanya nini?
 36. Ni rahisi ... tunahitaji kulinda, kurejeza na kugharamia.
 37. Linda.
 38. Misitu ya tropiki inafyekwa
 39. kwa kiwango cha viwanja 30 vya mpira kwa dakika.
 40. Pale asili inatekeleza jambo muhimu, lazima tuilinde.
 41. Rejeza.
 42. Sehemu kubwa ya sayari yetu imeharibiwa.
 43. Lakini asili inaweza kujirejeza
 44. na tunaweza kusaidia mifumo ya ikolojia kurudi tena.
 45. Gharamia.
 46. Tunatakiwa kuacha kugharamia vitu vinavyoharibu asili
 47. na kulipia vitu vinavyoisaidia.
 48. Ni rahisi tu hivyo.
 49. Linda, rejeza, gharamia.
 50. Hili linaweza kufanyika kila mahali.
 51. Watu wengi tayari wameanza kutumia masuluhisho asili kwa tabianchi.
 52. Tunatakiwa kufanya hivyo kwa kiwango kikubwa.
 53. Unaweza kuwa sehemu ya hili.
 54. Pigia kura wale wanaolinda asili.
 55. Shirikisha video hii.
 56. Ongelea kuhusu hili.
 57. Dunia kote kuna vikundi vya kushangaza vinavyopigania asili.
 58. Ungana navyo!
 59. Kila kitu ni muhimu.
 60. Ufanyacho ni muhimu.