Hii si kwata.
Jina langu ni Greta Thunberg.
Tunaishi mwanzoni mwa uangamivu
mkubwa
Tabianchi yetu inakongoroka.
Watoto kama mimi wanaacha masomo yao ili waandamane.
Lakini bado tunaweza kurekebisha hili.
Bado unaweza kurekebisha hili.
Ili kuendelea kuishi, tuache kuchoma nishati ya visukuku, japo hili tu halitoshi.
Masuluhisho mengi yanatajwa, lakini vipi suluhisho lililo mbele
yetu?
Nimwachie rafiki yangu George aeleze.
Ipo mashine ya ajabu inayofyonza gesi ya ukaa hewani, ina gharama ndogo na inajijenga
yenyewe.
Inaitwa ... mti.
Mti ni mfano wa suluhisho la asili la tabianchi.
Mikoko, maeneo ya maozeo, mapori, maeneo chepechepe, sakafu za bahari, mwani, vinamasi, matumbawe, vina
chukua gesi ya ukaa hewani na kuifungia.
Maumbile asili ni zana ambayo tunaweza kutumia kurekebisha tabianchi yetu iliyokongoroka
Masuluhisho haya asili kwa tabianchi yanaweza kuleta tofauti kubwa.
Poa sana, sio?
Lakini kama tu tutaacha nishati za visukuku ardhini.
Na hii ndio balaa ... hivi sasa tunazipuuzia.
Tunatumia mara elfu zaidi kwa ruzuku kwenye nishati za visukuku duniani kuliko kwenye masuluhisho
ya asili.
Masuluhisho asili ya tabianchi hupata 2% tu
ya pesa zote zitumikazo kushughulikia kukongoroka kwa tabianchi.
Hii ni pesa yako, ni kodi zako na akiba zako.
Hata balaa zaidi, hivi sasa ambapo tunaihitaji asili zaidi
tunaiharibu haraka kuliko wakati wowote.
Hadi spishi 200 zinatoweka kila siku.
Sehemu kubwa ya barafu ya Aktiki imetoweka.
Wanyamapori wetu wengi wametoweka.
Udongo wetu mwingi umetoweka.
Sasa tufanye nini?
Utafanya nini?
Ni rahisi ... tunahitaji kulinda, kurejeza na kugharamia.
Linda.
Misitu ya tropiki inafyekwa
kwa kiwango cha viwanja 30 vya mpira kwa dakika.
Pale asili inatekeleza jambo muhimu, lazima tuilinde.
Rejeza.
Sehemu kubwa ya sayari yetu imeharibiwa.
Lakini asili inaweza kujirejeza
na tunaweza kusaidia mifumo ya ikolojia kurudi tena.
Gharamia.
Tunatakiwa kuacha kugharamia vitu vinavyoharibu asili
na kulipia vitu vinavyoisaidia.
Ni rahisi tu hivyo.
Linda, rejeza, gharamia.
Hili linaweza kufanyika kila mahali.
Watu wengi tayari wameanza kutumia masuluhisho asili kwa tabianchi.
Tunatakiwa kufanya hivyo kwa kiwango kikubwa.
Unaweza kuwa sehemu ya hili.
Pigia kura wale wanaolinda asili.
Shirikisha video hii.
Ongelea kuhusu hili.
Dunia kote kuna vikundi vya kushangaza vinavyopigania asili.
Ungana navyo!
Kila kitu ni muhimu.
Ufanyacho ni muhimu.